Inasikitisha sana watu baada ya kufuturu wanaingiwa na uvivu wa kuswali swala ya faradhi ya isha,na hata tarawehee ambayo ni sunna muhimu sana miongoni mwa swala za usiku

Huu ni mwezi wa kuchuma sasa mbona hatuitumii hii fursa?
 
Wenzetu maswahaba walipokuwa wanaagana baada ya mazungumzo yao,walikuwa wanapeana nasaha kwa kusomeana suratil al asir ndio kisha wanaagana

Sura hii inazungumzia kwamba hakika wanadamu wote haijalishi waislamu au wasio waislamu,kuanzia baba yetu Adamu mpaka Mtume wa mwisho Muhammad swalla lahhu alaihy wa salaam, wote wapo katika hasara

Isipokuwa wale waliomwamini Allah kwa maana Mungu mmoja, kisha wakafanya mambo mema kwa maana matendo mema,kisha wakahusiana kuhusu mambo ya haki,kwa maana haki ya kumjua Allah, kukijua kitabu cha Allah na kujua mafundisho sahihi ya mtume Muhammad

Kisha wakahusiana juu ya kusubiri,hakika subira ni ibada kubwa sana,maana uwe na subira ya kuacha maovu uliyoyazoea na uwe na subira na kudumu kufanya mambo mema,maana hakika kudumu kufanya ibada za Allah ni mtihani mkubwa sana

Hawa ndio ambao hawapo katika hasara yani wamesamilika

Je sisi tupo upande upi? Tujitathimini na kufanya yale yenye kutupa mwisho mwema
 
Siku ya jana nikiwa pale mloganzila nimempeleka mzee wangu katika clinic yake,katika korido za pale hospitalini nikamsikia muislamu mwenzangu anaongea na simu huku akisema " tutamuoshea hapa hapa na kumswalia kabisa huku huku"

Naam huyo ni ndugu yetu katika imani ameondoka jana katika mgongo wa ardhi,na huenda yeye na wengine kama yeye waliazima kumaliza mfungo salama lkn hakika umri wao wa kuishi duniani umefikia mwisho


Je mimi na wewe ambao tupo hai hadi leo tunajitahidi vipi kuchuma zaidi ndani ya mwezi huu,je tutafanikiwa kumaliza salama mfungo au nasi huenda ikatufika safar ya kwenda kwa mola wetu?

Tutumie kila dakika na sekunde ya uhai wetu katika mwezi huu kuchuma thawabu nyingi zaidi kwani huenda,tusiimalize ramadhani hii au ama tusikutane na ramadhani nyengine

Tumche Allah sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…