Ramadhan Special Thread
IJUE SWAUM YAKO 1⃣8⃣
📚 سؤال وجواب في أحكام الصيام.

📜 AMESUKUTUWA MAJI KINYWANI KISHA YAKAPITILIZA TUMBONI, JE ATAKUWA AMEFUNGUA MTU HUYU.?

Swali:
Je, ikiwa mfungaji amesukutuwa maji kinywani au ameyavuta maji puani, kisha yakapitiliza mpaka tumboni, atakuwa amefungua?

Jawabu:
Ikiwa mfungaji atasukutuwa maji kinywani au kuyavuta maji puani, kisha yakapitiliza na kuingia tumboni atakuwa hajafungua, kwa sababu hakukusudia.

Na Allaah Ta’alaa anasema:
“Wala hapana lawama juu yenu kwa yake mliyokosea. Lakini ipo lawama kwa yale ambayo nyoyo zenu imeyafanya kwa makusudi”. [Al-Ahzaab/5].

✍️ فضيلة الشيخ محمد العثيمين رحمه الله
Tarjama; Ustadh Abu Halima Arafat حفظه الله تعالى ورعاه
 
IJUE SWAUM YAKO 1⃣6⃣
📚 سؤال وجواب في أحكام الصيام.

📜 JE KUONJA CHAKULA KUNAHARIBU SWAUM.?

Swali:
Je, kuonja chakula kunaharibu funga ya mtu

Jawabu:
kuonja chakula hakuharibu funga ya mtu, endapo hatomeza, lakini mtu asifanye hivyo mpaka awe anahitajia.

✍️ فضيلة الشيخ محمد العثيمين رحمه الله
Tarjama; Ustadh Abu Halima Arafat حفظه الله تعالى ورعاه

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
🌱 جزى الله خيرًا من قرأها وعمل بها وساعدنا على نشرها..
فَالدَّالُّ عَلَى الْخَيْرِ كَفَاعِلِه
 
IJUE SWAUM YAKO 1⃣1⃣
📚 سؤال وجواب في أحكام الصيام.

📜 KWA SHARTI HILI ITAFAA KUPIGA MSWAKI NA DAWA YA MENO KWA ALIYEFUNGA, MCHANA WA RAMADHAN.

Swali:
Ni ipi hukumu ya kupiga mswaki kwa kutumia dawa ya meno wakati wa mchana kwa mtu aliyefunga?

Jawabu:
Kupiga mswaki kwa kutumia dawa ya meno wakati wa mchana kwa mtu aliyefunga, ni sawa iwe katika mwezi wa Ramadhani au miezi mingine, hakuna tatizo endapo haikupita kwenye koo na kuingia tumboni.

Lakini iliyo bora ni kuacha kutumia, kwa sababu inapenya kwa haraka (kuingia tumboni), kwa hiyo huenda ikapita na kuingia tumboni hali ya kuwa mtu hajui.

✍️ فضيلة الشيخ محمد العثيمين رحمه الله
Tarjama; Ustadh Abu Halima Arafat حفظه الله تعالى ورعاه

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
🌱 جزى الله خيرًا من قرأها وعمل بها وساعدنا على نشرها..
فَالدَّالُّ عَلَى الْخَيْرِ كَفَاعِلِه
 
IJUE SWAUM YAKO 0⃣1⃣
📚سؤال وجواب في أحكام الصيام.
✍️ لفضيلة الشيخ محمد العثيمين رحمه الله

📜 JE NIA YA SIKU YA KWANZA YA RAMADHANI INATOSHA KWA MWEZI MZIMA❓

SWALI 01;
Je, kunuwia siku ya kwanza katika mwezi wa Ramadhani kunatosheleza kuwa ndio Nia ya mwezi mzima?

JAWABU;
Nia ya siku ya kwanza ya Ramadhani inatosheleza, wala si mwenye kuhitajia kuifanya upya Nia yake kila siku.
Isipokuwa ikipatikana sababu ambayo ameruhusiwa yeye kula mchana (wa Ramadhani) atakula, na akitaka kuendelea tena na saumu atanuwia upya.

Tarjama; Ustadh Abu Halima Arafat حفظه الله تعالى ورعاه

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
🌱 جزى الله خيرًا من قرأها وعمل بها وساعدنا على نشرها..
فَالدَّالُّ عَلَى الْخَيْرِ كَفَاعِلِه
 
b49c0f541160424db2f217d1972b2507.jpg
 
Mmekua wachoyo mno siku hizi..zamani daah tulifaidi aiseee....uji..mara chapati kdg tambi...
Yani siku hzi mnajifungia manyumbani kwenu sio tena vibarazani...
Aaaaaghhhh
 
Mmekua wachoyo mno siku hizi..zamani daah tulifaidi aiseee....uji..mara chapati kdg tambi...
Yani siku hzi mnajifungia manyumbani kwenu sio tena vibarazani...
Aaaaaghhhh
Hii kweli! Zamani wslikua wanakula nje kwenye mkeka ukipita unaitwa au wanapitisha nyumba hadi nyumba.
 
Mmekua wachoyo mno siku hizi..zamani daah tulifaidi aiseee....uji..mara chapati kdg tambi...
Yani siku hzi mnajifungia manyumbani kwenu sio tena vibarazani...
Aaaaaghhhh
njoo kwetu huo utaratibu bado upo na wifi yako kaondoka fika bila kukosa
 
Mmekua wachoyo mno siku hizi..zamani daah tulifaidi aiseee....uji..mara chapati kdg tambi...
Yani siku hzi mnajifungia manyumbani kwenu sio tena vibarazani...
Aaaaaghhhh
Ukute hayo majumba hata watu hawamo tena. Na kama wamo basi sio wale wale mnaowajua nyie hao mnaowaita wa 'zamani'
Binafsi Ramadhan karibu yote nafutaria ofisini, huyo jirani nampelekea nini! Maisha yamebadilika sio tena km yale tuliotoka zama hizo.
Ila nafkiri kuna baadhi ya sehemu bado watu wanaendeleza huo utaratibu. Sema ukute na wewe jirani hata nyumbani hukai kwa mihangaiko ya kutwa. Unarudi nyumbani kulala tu kama umepanga room hotel
 
Back
Top Bottom