Pumzika kwa amani mzee Mwinyi. Katika utawala wako ulitufanyia mengi katika taifa ikiwemo swala la kuifungua nchi, kutuepusha kuvaa midabwada, chakacha, kula ugali wa dona na mbilimbi, kuogea majani ya mpapai nk.

Mazishi yatafanyika kijijini kwao Mkuranga au Zanzibar?
 
Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi afariki dunia.

Taarifa hii imetolewa usiku huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

View attachment 2920484
Pole sana kwa familia na watanzania kwa ujumla kwa kumpoteza mpendwa wetu. Huyu ni rais ambaye wakati wa uongozi wake hakuwahi kuwa na kikundi cha watu wasiojulikana wanaopoteza roho za watu. Pumzika kwa amani mzee ruksa, umepigana vita vizuri mwnedo umeumaliza. Mwanga wa milele eeh Bwana umuangazie.
 
Ila tupo msibani sasa. Hayo mengine yanaweza kusubiri.
 
Duh! Kazi kwelikweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…