Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,251
- 35,591
Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua.
Watu wengi waliokuwa wanamuona Rais Samia kama rais bora wa mfano, kwa sasa (kupitia suala la bandari) wanamuona Rais wangu kama mtu mwenye upeo mdogo au mwenye tamaa kubwa za kifisadi kuliko mwanasiasa yoyote aliyewahi kutokea hapa Tanzania. Sakata la bandari limeondoa heshima yote ya Rais Samia.
Kwa nia njema kabisa, ningependa kumpa huu ushauri Rais wangu mama Samia ili kuepuka kikombe hichi cha mkataba ya kipuuzi wa Bandari kilichozika kabisa nyota yake ya kisiasa kuelekea 2025. Ni vyema mara moja akalikana bunge lililopitisha mkataba ule kwa kumtosa Spika Tulia (kufanya kama alichokifanya kwa Ndugai) na hapo hapo kumtosa waziri wako mkuu (Kassim Majaliwa) kwa kitendo cha 'kumshauri vibaya' na ikiwezekana kumpiga chini na Mwanasheria kwa kushindwa 'kuwajibika ipasavyo kisheria.' Narudia tena, kisiasa mama Samia ameshaanguka na namna pekee ya kujaribu kuinuka ni kuachana na hilo limkataba la DP world kwa style ya kuwatosa vilanja wake. Ushauri wangu huu ipo siku utakumbukwa!
ANGALIZO
Mimi ni miongoni wa watu humu JF ninayemkubali Rais Samia kwa upendo wake kwa watanzania wote na uungwana wake katika kufanya siasa. Ni kitu cha kipekee alichonacho (Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni). Upande wa pili mimi ni mkosoaji wa utendaji mbovu wa Rais Samia unaotokana na kivuli kichafu cha CCM kinachomfunika, uwezo wenye mashaka katika kuchanganua mambo makubwa na taswira ya kifisadi anayotengenezewa na watu fulani fulani waliomzunguka. Ukweli usemwe hata kama ni mchungu!