Rais Samia nakushauri watose sasa Spika (Tulia) na PM (Majaliwa), sakata la bandari limekumaliza kisiasa!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,153
Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua.

Watu wengi waliokuwa wanamuona Rais Samia kama rais bora wa mfano, kwa sasa (kupitia suala la bandari) wanamuona Rais wangu kama mtu mwenye upeo mdogo au mwenye tamaa kubwa za kifisadi kuliko mwanasiasa yoyote aliyewahi kutokea hapa Tanzania. Sakata la bandari limeondoa heshima yote ya Rais Samia.

Kwa nia njema kabisa, ningependa kumpa huu ushauri Rais wangu mama Samia ili kuepuka kikombe hichi cha mkataba ya kipuuzi wa Bandari kilichozika kabisa nyota yake ya kisiasa kuelekea 2025. Ni vyema mara moja akalikana bunge lililopitisha mkataba ule kwa kumtosa Spika Tulia (kufanya kama alichokifanya kwa Ndugai) na hapo hapo kumtosa waziri wako mkuu (Kassim Majaliwa) kwa kitendo cha 'kumshauri vibaya' na ikiwezekana kumpiga chini na Mwanasheria kwa kushindwa 'kuwajibika ipasavyo kisheria.' Narudia tena, kisiasa mama Samia ameshaanguka na namna pekee ya kujaribu kuinuka ni kuachana na hilo limkataba la DP world kwa style ya kuwatosa vilanja wake. Ushauri wangu huu ipo siku utakumbukwa!

ANGALIZO
Mimi ni miongoni wa watu humu JF ninayemkubali Rais Samia kwa upendo wake kwa watanzania wote na uungwana wake katika kufanya siasa. Ni kitu cha kipekee alichonacho (Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni). Upande wa pili mimi ni mkosoaji wa utendaji mbovu wa Rais Samia unaotokana na kivuli kichafu cha CCM kinachomfunika, uwezo wenye mashaka katika kuchanganua mambo makubwa na taswira ya kifisadi anayotengenezewa na watu fulani fulani waliomzunguka. Ukweli usemwe hata kama ni mchungu!
 
Mimi naamim katika nafasi ya pili naamini amejifinza pakubwa, mi naona huu udhaifu unatoka na katiba dhaifu tuliyonayo ambayo wenye maamuzi wengi wanategema fadhila ya rais ilinkuenddelea kuwa na nafasi walizonanzo kwa hiyo Kila wakati hujaribu kusoma gesture ya rais na kufanya anavyotaka au wanavyohisi anataka matokeo yake hamna anayetoa ushauri WA kweli Bali wakumfurahisha rais.

Karibu mpya ingeamdress hayo mambo muhimu na kuzipa taasisi uwezo WA kufanya maamuzi sahihi pasipo kuingiliwa sana.

Kama kweli sheria za nchi zinaweza kurekebishwa ili zikidhi matwakwa ya kampuni Moja basi hiyo ni hatari it's narrow thinking kwa kweli.
 
Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua...
Suala la Bandari lina shida gani?
 
Ukiangalia kwa jicho la umakini hili suala utagundua kwamba waliomuingiza chaka huyu mama ni wabunge wanaoongozwa na njaa kali na ulafi kushindwa kupingana wao kwa wao sababu sasa hivi mle ndani wapo wao tu so wanaona wakienda tofauti na wengine raisi atawaona wasaliti na atakuwa hawabebi awamu ijayo kumbe sometimes yeye rais alitegemea challenges watakazopeana kwenye mjadala wa hili jambo ndizo zimuongoze lakini wao wakaishia kugonga gonga meza kwamba kila kitu kipo safi yeye akaona amalize kazi kumbe halikuwa jambo bora.

Na hii yote ni kutokana na wanajua hawapendwi na wananchi wao kwa sababu kugombea kwao ubunge haikuwa ili wakawasemee shida zao bali ilikuwa ni chance ya kupata ukwasi
 
Wa kutoswa kama kuna mtu wa kutoswa, ni yeye mwenyewe Mama Samia.

Hili dili kwa habari zinazotufikia ,limetengenezwa ndani ya familia yake.

Mwalimu alisema, Ikulu si mahali pa kufanya biashara, na ndugu walielewe hilo.

Spika na Majaliwa hawajiamini, wanajua nguvu ya Rais na lililompata Ndugai.

Mama akiwa fair, abebe mzigo wake.

Mimi vile vile nilikuwa namkubali sana mama Samia,lakini katika hili la Bandari, NO!
 
kuna wengine maprofesa wanatolewa kamasi huko mahakamani hadi mmoja anasema hakusoma documents alikua anaumwa hahahahhaha wale ndio wanyongwe kabisa
Mruma asingejitambulisha Kama profesa mbele ya vile vitoto vya kizungu. Angesema from foo alipata div foo Kama waziri Fulani aliyepata F ya uraia, F ya hesabu na F ya kiingereza.

Kujitambulisha Kama Prof kumewavua nguo maprof wengi wa kitanzania.

Mruma na dada Joy hawachekani japo mruma anajua ung'eng'e kiasi.
 
kuna wengine maprofesa wanatolewa kamasi huko mahakamani hadi mmoja anasema hakusoma documents alikua anaumwa hahahahhaha wale ndio wanyongwe kabisa
Tena document ambayo alitumia kunukuu katika utetezi wake😂😂😂
 
Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua...
Hakuna mtu atampinga sababu ya kilichotokea kwa ndugai. Yeye ndio katengeneza watu wamuunge mkono kuliko kumwambia ukweli
 
Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua...
Angejitosa na yeye mwenyewea, aiache Tanganyika yetu

Yeye ndiye Alfa na Omega wa low mind 'akili ndogo' na elimu yake ya kuungaunga 'QT'
 
Haihitaji kubishana kwa chochote, suala la Bandari limefifisha kabisa nyota ya kisiasa ya Rais Samia, kwa hali ilivyo sasa Rais Samia akisema akagombee hata udiwani katika kata yoyote ile Tanganyika huenda akaangukia pua...
Watajuana wenyewe
 
Hao wote uliowataja hawana hatia hata kidogo, yeye kaamua kukumbatia genge hatari la msoga wazee wa mjini akija kugundua atakuwa hana hamu nao.

Kwenye hili la bandari msoga ndio washauri wake hao wengine akina Tulia,Majaliwa, Mpango nk wapowapo tu na ukweli wanaujua.

Tatizo la nchi yetu ni njaa na kutokujiamini ulitegemea Majaliwa aseme mkataba ni mbaya au mwanasheria mkuu wa serikali aseme mkataba ni mbaya? Genge la Msoga liko jikoni mengi yatakuja
 
Ifahamike pasi na shaka, Uwaziri mkuu au Uspika hauna hati miliki. Moja kwa moja kwenye hoja.

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa, bila aibu na bila kupepesa macho, ametoa kauli za uongo na zenye kulenga kuchangamya wananchi juu ya mkataba wa uendelezaji bandari, hali kadhalika hili kimefanywa na Spika wa Bunge, Tulia Ackson.

Ni aibu hata kuweka clip zao kwa sasa, maana wamejidhalilisha na wako UCHI!

Namna pekee ya kumrudishia nguo Rais wetu Samiah Suluhu Hassan ni kuwafyeka shingo hawa waongo wawili, aibu gani hii?!!!
 
Hivi twaweza hawajaja na zile polls zao za record low approval rating. Ngoja nimuulize Fatma karume approval rating ya Biggie inasimamaje "record low" au high.
 
Back
Top Bottom