BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,517
8,454
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mara nyingi anapokwenda nje ya Nchi huwa anafuatana na jopo la Wafanyabiashara lakini kwa sasa anataka kugeuka kidogo na atakuwa anasafiri pia na Wasanii ili kuwapa nafasi ya kujifunza zaidi kutoka nje ya Nchi na kutanua wigo wa kazi zao.

Rais Samia amesema hayo usiku huu wa leo May 25,2024 wakati akishiriki uzinduzi wa album mpya ya Msanii Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambapo amesema “Tunapofungua Nchi Wageni wanakuja kwetu na sisi tunakwenda kwao na mara nyingi ninapokwenda kwao huwa nafuatana na jopo la Wafanyabiashara, sasa nataka kugeuka kidogo nataka sasa niwe nachukua Wasanii”

“Nataka nifuatane na Wasanii inategemea ratiba yangu kule nakokwenda lakini kila ninapokwenda kukiwa na matamasha ya utamaduni nitabeba Wasaniii lakini zaidi nitakuwa na safari keshokutwa na moja ya kazi ninayokwenda kuifanya ni kutafuta nafasi za mafunzo kwa Wasanii wetu hasa Waigizaji”

“Tunakwenda Korea na mnawajua ni Wazuri sana kwa kuigiza, michezo yao naona inatambatamba kwenye TV zetu, kwahiyo tunaenda kutafuta nafasi za mafunzo na nadhani tutafanikiwa”
 
Sipendi mtu mwenye mamlaka kubwa kama raisi anapokuwa siti ya mbele kushadadia vitu soft soft tu!
Hii nchi ina matatizo chungu nzima, yenye kuhitaji kushughulikiwa, inauma sana viongozi ambao tumewapa dhamana wanahangaika na mambo yasiyokuwa ya msingi ili apate kwenda na upepo uliopo.
Sikukuu kama ya wafanyakazi tulitarajia rais angekuwepo na walau basi atoe neno, lakini hakutokea,
Anaacha mambo ya msingi anaenda kuzindua albamu ya Hamonaizi!
Nchi yangu Tanzania
 
Back
Top Bottom