Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Wala changamoto sio kupambana na upinzani kama unavyofikiria wewe.

Mtu kama Gaguta alipelekwa Bukoka kwa sababu ni mwanajeshi, kuna maeneo mengi ya mazoezi yao ambayo wananchi walikuwa wanavamia na kuna wafugaji wa nchi jirani walikuwa wanaingia sana kwenye mapori kulisha mifugo na kuuwa wananchi.

Tangia apelekwe Bukoka ulisikia wafugaji wa kinyarwanda wameua mtu huko?
Natamani kujua kwanini mkoa wa Kagera wakuu wa mkoa huo mara nyingi wanapelekwa wanajeshi?
 
Mama ilimradi tu afanye lolote aongolewe kwa miaka watu walikuwa wanalalama kubadilisha badilisha wakuu wa mikoa na wilaya kunaondoa consistencies ndio maana Magufuli aliwaacha.

Hao watu kwa muda waliokaa wanafahamu changamoto za maeneo yao, plan zilizokuwepo na changamoto za watendaji wao.

Kingine Magufuli for once alijitahidi kuweka wakuu wa mikoa kutokana na maeneo wanayoyafahamu au skills zao ili watatue changamoto kutokana priority wanazozifahamu wao.
Magufuli kishakufa mkuu , jitahidi kwenda na Wakati .
 
Sky ebu nipe maon yako. Huyu Hapi na madhambi yote bado yumo. Samia nimeanza kumchukia sasa
Kusema ukweli Rais ni msikivu lakini kumbuka huko CCM wasafi ni wachache akiamua kuyafanyia kazi yote ghafla atakosa wakufanya nae kazi.
 
Nipate tabu ya nini, kubadilisha badilisha watu kunaondoa consistency.

Chukulia mtu kama Jokate ana plan zake kibao Kisarawe kesho umtoe umpleke sijui Rukwa si anaenda kuanza upya tena, huyo atakaenda huko ataendeleza legacy zake?

Kubadilisha badilisha watu vituo vya kazi ni mambo ya kishamba tu.
kwa hiyo viongozi wawe wa kudumu. Maana kutekeleza plans zako it takes years n years. Haipaswi iwe mtu anatekeleza hili na lile. Yapaswa system ndio iwekwe na ifuatwe ktk kutekeleza mopango ili mtu akifa afilie zake hatta wewe ukimrithi utaendeleza.
 
Back
Top Bottom