UTEUZI: Abdul-Razaq Badru Mkurugenzi Mkuu mpya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Rais amefanya teuzi zifuatazo:

1. Dkt. Thomas Nestory Bwana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI)

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Bwana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Mazingira (Biodiversity Conservation) Ofisi ya Makamu wa Rais. Anachukua nafasi ya Dkt. Geofrey Mkamilo ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzo huu umeanza 3 Februari, 2024

2. Amemteua Abdul-Razak Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Kabla ya uteuzi huu Bw. Badru alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB). Aidha aliyeluwa Mkurugenzi wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba atapangiwa kazi nyingine.

3. Amemteua Dkt. Bill Kiwia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)

Dkt. Kiwia anachukua nafasi ya Bw. Badru ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF)

Uteuzi huu unaanza tarehe 6 Februari, 2024

IMG_8998.jpeg
 
Huyu ni mtu wa Bara ndani ndani huko hana tatizo ni mwadilifu naona anenda kuondoa kikokotoo kile kinaliza watu.
Watanzania mnanunulika kwa gharama ndogo sana especially ninyi mnaohesabu siku ili mshike ujira wenu,tena kama ni walimu ndiyo kabisa huwa hawaelewi mipaka ya kuwaamini wanasiasa.

Kudhani fulani alishindwa kuondoa kitu fulani kwa sababu ya uwepo wake na kwamba atakayechukua nafasi yake atakiondoa huo ni moja ya ujinga kwa sababu hayo mashirika siyo ya mtu mmoja ni taasisi iliyo ndani ya serikali so hawezi tu mtu akapitisha sheria serikali ikamwangalia tu hata hiyo serikali huwa ndani ya hiyo michezo as long as ndiyo msimamizi mkuu wa taasisi.
 
Na hiki ndio anacho weza kukifanya sana pale magogoni kuteua na kutengua TU.

Kashindwa
1.sukari
2.Umeme

Vitu vya maana Kwa watanganyika wa chini kabisa. Pia kasahau kua aliwaidi watanganyika mwishoni mwa January kua angewasha geneleta Moja kutoka kwenye bwawa la Nyerere. Kimya
 
Kumuondoa Kashimba (PsssF) wamemshauri vibaya. Kashimba ameliongoza hilo shirika vizuri sana kwani lilikuwa hoi leo mnamuondoa mnampa mtu wenu aliyeshindwa kusimamia mikopo ya wanafunzi!
Kashimba mtu wa hovyo sana, shirika liliuzia watu viwanja kigamboni kimbiji, na kwingine nchini, maafisa wake hawataki kutoa mikataba ya ununuzi kwa wateja wa hivyo viwanja, na wala hawataki kutoa hati. Hovyo kabisa. Bora aje mwingine afumue baadhi ya idara kama hiyo niliyoitaja, afukuze kabisa wakawe maafisa tarafa huko.
 
Na hiki ndio anacho weza kukifanya sana pale magogoni kuteua na kutengua TU.

Kashindwa
1.sukari
2.Umeme

Vitu vya maana Kwa watanganyika wa chini kabisa. Pia kasahau kua aliwaidi watanganyika mwishoni mwa January kua angewasha geneleta Moja kutoka kwenye bwawa la Nyerere. Kimya
Wanaona/tunaona anakotupeleka watanganyika.. Wasaliti akina Mwigulu na makamba kuna siku watalipa usaliti
 
Watanzania mnanunulika kwa gharama ndogo sana especially ninyi mnaohesabu siku ili mshike ujira wenu,tena kama ni walimu ndiyo kabisa huwa hawaelewi mipaka ya kuwaamini wanasiasa.

Kudhani fulani alishindwa kuondoa kitu fulani kwa sababu ya uwepo wake na kwamba atakayechukua nafasi yake atakiondoa huo ni moja ya ujinga kwa sababu hayo mashirika siyo ya mtu mmoja ni taasisi iliyo ndani ya serikali so hawezi tu mtu akapitisha sheria serikali ikamwangalia tu hata hiyo serikali huwa ndani ya hiyo michezo as long as ndiyo msimamizi mkuu wa taasisi.
Ninakupata sana.
 
Back
Top Bottom