Mwaka 2013 nilikwenda kijijini ndani ndani uko kulikuwa na nyumba za udongo zilioezekwa nyasi lakini nililikuta kanisa la Roma likiwa na jengo kubwa la kanisa, hospital,shule ya msingi na sekondari na visima vya maji,kwa watu wote, Wakristo na Waislamu,Watanzania wote bila ubaguzi,usafiri pekee kutoka kijijini kwenda mjini ni lift ya Padre zaidi ya hapo utatembea kilomita kumi na nane ndio utakuta usafiri wa Lori au bus,huu ndio ukuu wa Kanisa la Roma,fuatana nami nikupe historia ya ushawishi wa kanisa la Roma duniani na Tanzania,tuanze na Roman Empire,yaani dola la Roma,dola la Roma lilikuwa milki kubwa lililoenea kwa karne kadhaa katika nchi zote zinazopakana na bahari ya Mediteranea,
Dola la Roma lilianza kwenye mji mkuu wa Roma na rasi ya Italia ikaendelea kuunganisha makabila na mataifa ya nchi nyingi kwenye mabara matatu ya Ulaya, Afrika na Asia,kuanzia karne ya 1 KK Watawala wa Dola wakaitwa makaisari:Kaisari wa kwanza alikuwa Augusto,nchi nyingi za sasa ziliwahi kuwa sehemu ya Dola la Roma kama vile Uingereza, Ufaransa,Hispania, Italia, Ugiriki na nchi za Balkani upande wa Ulaya, Moroko, Algeria,Tunisia, Libia na Misri upande wa Afrika, na Uturuki, Syria, Lebanon, Palestina, Jordan na hata Irak upande wa Asia,Upanuzi wa eneo la Roma kuanzia mwaka 510 KK hadi 480 BK;Dola la Roma lilipofikia kilele cha uenezi wake mwaka 117.
Katika kitabu chake Bw. Bergen kiitwacho Development and Religion in Tanzania,katika Ukurasa wake wa 98 mwandishi anasema "Catholic Missionaries came to East Africa to find not new churches, but new provinces of the Roman Church"kwa mujibu wa tafsiri yangu Wamishionari wa Kikatoliki hawakuja hapa Afrika ya Mashariki kwa minaajili ya kuasisi Makanisa mapya,bali walikuja kuunda majimbo mapya ya Kanisa la Roma,Ni kwamba,Tanzania (Tanganyika) ipo Afrika Mashariki, na kwa mujibu wa mwandishi Bergen,Tanzania nayo ni moja ya majimbo ya Kanisa la Roma,au kwa lugha nyepesi tuseme Tanzania ni koloni la Vatican! Je, ni kweli Tanzania (Tanganyika) ni Koloni la Vatican? Padri. Dk. Sivalon, naye katika kitabu chake Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania Bara (1953-1985) anaeleza bayana kuwa Mwalimu Julius Nyerere Rais wa Kwanza wa Tanzania alikuwa kiungo pekee kati ya Chama cha Mapinduzu (CCM),Serikali na Kanisa Katoliki,sijui mnanipata vizuri ndugu Watanzania!?
-Tanganyika kupewa Uhuru.
Baada ya mwarabu kufukuzwa na kina Karl Peters aka mkono wa damu na kwa kumlaghai Chifu Mangungo wa Msovelo kwa mkataba wa kilaghai uliotafsiriwa na Mkalimani Ramazan na baada ya "scramble and partition of Africa"Tanganyika ikawa chini ya Mjerumani,Wajerumani walikuwa na dini yao ya Kilutheri,ikumbukwe kuwa wakati wa ukoloni serikali ya kikoloni ilikuwa inatoa huduma zake za jamii hususani elimu kwa kuupendelea ukristo,kwa muislamu ili upate kusoma sharti ubatizwe na kuwa mkristo,waliobahatika kusoma bila kubatizwa ni watoto wa machifu,hivyo basi Waislamu waliotokana na Utawala wa Mwarabu walianza kupigania Uhuru Ili nao wapate Uhuru na kuabudu dini yao ya kiislamu,kwa hiyo Waislamu wengi walikuwa na vuguvugu la kuikomboa Tanganyika,kuelekea Tanganyika kupata Uhuru Muingereza akapewa Kuisimamia Tanganyika,
Taarifa za siri za CIA za miaka ya 1953 zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini kwamba baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka Tanganyika, mtu aliyepaswa kukabidhiwa nchi alikuwa ni kiongozi wa Wachaga Thomas Mariale,lakini katika nyaraka za shirika la Ujasusi la Uingereza la MI6 chini ya Fabian Society za mwaka 1944, zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini Chifu Kidaha alikuwa mtu sahihi wakukabidhiwa nchi baada ya Waingereza kuondoka.Nyaraka za shirika la Ujasusi la Kanisa Katoliki la Jeisuti za mwaka 1942 kupitia kwa Kasisi Arth Wills na Wash zinaonyesha kwamba wao waliamini Kambarage Burito Nyerere ndie alikuwa mtu sahihi wa kukabidhiwa nchi baada ya Uingereza kuondoka, tangu hapo walimbatiza pale Tabora na kumbadili jina na kuitwa Julius Kambarage Nyerere, hii ilikuja baada ya kifo cha Chifu Burito, awali kulikuwa na mwendo mrefu wa kumshawishi Chifu Burito akubali mtoto wake ajiunge nao lakini mzee yule alipinga, .
Hapa nadhani kuna factions(vigroup vya kisiasa)mbali mbali za wakoloni wakiingereza ambapo kila faction ilikuwa na mtu wake ambaye wangetaka awe Rais wa Tanganyika (baada ya kuona vugu vugu la uhuru kwenye nchi za Afrika haliwezi kuzuilika).Unaweza kuona kwamba Julius aliandaliwa na faction fulani (including yule padre wake) na Oscar aliandaliwa na faction fulani (including huyo askofu wake wa kianglikana). Pia kuna faction nyingine zilikua zinataka chifu huyu au yule awe Rais.Kidhehebu Muingereza aliwapendelea Anglicans kwanza, then Presbyterians, then Lutherans. Muingereza hakupenda wakatoliki. Walutheri alikuwa na wasi wasi nao kidogo kwamba wangependa wajerumani zaidi ya waingereza.
Moja wapo ya Dilemma ya waingereza kidini ni kwamba mjerumani alishakuja Tanganyika. Since ulutheri ndio ilikua dini ya watawala wa Ujerumani (Bismark na Kaiser), Wakoloni wa kijerumani walichagua maeneo mazuri sana ya TZ (Kilimanjaro, Usambara, Arusha, Mbeya, Iringa na Kagera) na kuyafanya maeneo ya walutheri. Of course wakatoliki wakijerumani walipewa pia sehemu ya maeneo hayo. Muingereza kuja akabidi aeneze uanglikana kwenye maeneo ambayo sio mazuri sana (Dodoma etc). Ingawa aliweka makanisa pia kwenye maeneo yale ya walutheri.
Baada ya Waingereza kuzidiwa na Jesuit Father's kupitia Padre Arth Wills wa kanisa la Roma ambao bila kupepesa walimtaka Julius Nyerere kuwa Kiongozi wa Tanganyika baada ya Uhuru baada ya kumfuatilia kwa miaka 20, Waingereza wakaamua kutumia Format ya double agent ‘rafiki’ wao namba moja (Julius) na ‘rafiki’ wao namba mbili (Oscar), ili rafiki yao namba moja asipofanya wanachotaka basi rafiki yao namba mbili anamuondoa huyo namba moja na kuwa kiongozi. Mara nyingi wanapenda rafiki yao namba moja awe boya na rafiki wao namba mbili ndo awe na madaraka ya kweli. Waingerea vile vile wameweza kuweka marais waislamu marafiki zao kwenye nchi za kiafrika e.g. magenerali wakiislamu wa Nigeria,saa nyingine wanaangalia maslahi yao na sio dini.
Tukubali tukatae, Kanisa Katoliki lina upper hand kwenye siasa za dunia, si wengi wanajua kuwa kila rais katika Dunia hii lazima aungwe mkono na Vatican yaani Roma lazima itoe baraka zake,hapa Tanzania tumeona kila rais anapokuwa ni Mkristo ni lazima awe Mkatoliki!,Julius Nyerere alikuwa Mkatoliki, Benjamin Mkapa Mkatoliki na John Magufuli Mkatoliki,na atakaye mfuatia Mama Samia baada muda wake, ni lazima awe Mkatoliki!,hii ni indorsement toka Roma,kama hawakutaki utaondoka na kama wanakutaka utakaa,huu ni mfumo uliojichimbia mizizi toka enzi za Roman Empire,ni sawa na Marekani sasa na baada ya miaka mia ijayo,kuna nguvu itaendelea kuwa nazo,
Now,the winds of change is blowing across Tanzania,uprotestanti umepata nguvu tena Tanzania (especially wapentekoste na walutheri) wengine wametokea Kanisa Katoliki nadhani around 1/3 to 40% ya watanzania kwa sasa ni waprotestanti wa madhehebu mbali mbali,kuna dalili kwamba baada ya miaka 70 ya uhuru (2031) waprotestanti ndo wataiongoza Tanzania,lakini pia Waislamu wamepata nguvu, lakini tukumbuke Roman Katoliki lilipita katikati ya yote CIA waliomtaka Chifu Thomas Marealle na kati kati ya M16 waliomtaka Chifu Kidaha na wao wakahitimisha kumleta Julius Nyerere kama Kiongozi ajae wa Tanganyika baada ya vetting za miaka 20.
Nimalizie kwa kusema Julius Nyerere hakuwaangusha Roman Katoliki waliomchagua wala Watanzania tulionufaika nae,nadhani kutokana na political maneuverings alizopitia Julius Nyerere katika mazingira magumu na hatarishi anastahili kuwa mwenye heri wa kanisa lake la Roma,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliaminiwa na aka-deliver na kwenda extra miles kuifanya Tanzania kuwa Mama wa ukombozi katika bara la Afrika,nathubutu kusema bila ya yeye kanisa la Roma lingepata shida na Tanganyika ingepata shida,sijui kama leo tungekuwa na Tanzania.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
-Bachelor of business administration in International business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.