Blender

JF-Expert Member
Mar 5, 2022
3,421
5,277
Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb), Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Rais, Mipango Na Uwekezaji, akiwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2024/2025 amesema Kiwango cha wananchi wanaopata maji safi na salama kimeongezeka hadi kufikia asilimia 88.6 mijini na asilimia 78 vijijini.

Pia ameongeza kuwa idadi ya watalii imeongezeka mara mbili zaidi ya ilivyokuwa mwanzo.

"Idadi ya watalii imeongezeka kutoka watalii 1,711,625 mwaka 2021 na kufikia watalii 3,818,080 mwaka 2022, ikilinganishwa na lengo la kufikia watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025/2026.

Hii imesababisha kuongezeka kwa mapato ya utalii kutoka Dola za Kimarekani bilioni 1.31 mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Kimarekani bilioni 2.53 mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 93.1."

#KutokaBungeni

Prof. anazungumzia vijiji gani, vya Ulaya?

20231106_140730.jpg
 
Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb), Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Rais, Mipango Na Uwekezaji, akiwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2024/2025 amesema Kiwango...
Profesa Kitila Mkumbo Na Juma Aweso Waziri wa maji.

Tunaomba mfike Kata ya Matundasi Wilaya ya Chunya na mkoa anaotoka Spika wa bunge.

Kata nzima Hakuna maji na matokeo yake wananchi hawana vyoo wanajisaidua vichajani na mvua zikinyesha wanakunywa maji yaliyotokea kwenye vichaka wananchi wanakojisaidia
 
Back
Top Bottom