Bilioni 7.2 Kupeleka Maji Safi na Salama Vijiji 8 Halmashauri ya Wilaya ya Momba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,906
945

BILIONI 7.2 KUPELEKA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI 8 HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA

MBUNGE wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe (CCM) amesema matamanio yake ni kuona Vijiji vyote 72 vya Halmashauri ya Wilaya ya Momba vinafikiwa na huduma ya Maji Safi na Salama.

Mheshimiwa Sichalwe ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Msangano, wakati wa zoezi la kukabidhi mradi wa Maji wenye thamani ya Tsh. bilioni 7.2 kwa Mkandarasi wa Kampuni ya JUPTER ya Jijini Dar es salaam.

"Kwa takwimu nilizonazo ni kwamba upatikanaji wa maji kwenye jimbo langu ni asilimia 30 tu, maana kati ya vijiji 72 ni vijiji 20 tu ndivyo vinapata maji safi na salama, vilivyobaki vyote bado havina maji" - Mhe. Condester Sichalwe

Mradi ambao umesainiwa utatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi 3, na Vijiji vitakavyo nufaika na mradi huo ni Msangano, Ntinga, Ipata, Chindi, Nkala, Makamba, Naming'ongo na Yala.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-05-29 at 14.18.27.mp4
    20.1 MB
  • WhatsApp Image 2023-05-29 at 14.16.53.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-29 at 14.16.53.jpeg
    76.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-05-29 at 14.16.54.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-29 at 14.16.54.jpeg
    96.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom