Jitihada za Rais Samia kusambaza maji safi na salama

Jitihada za Rais Samia kusambaza maji safi na salama

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,441
Reaction score
1,050
Chini ya Rais Samia Suluhu, kila familia itapata maji safi na salama. Jitihada za kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata maji safi na salama ni jitihada za kupongezwa sana kwani zimekuwa na muendelezo chanya tangu Rais Samia Suluhu aingie madarakani.

Kwa mujibu wa ripoti ya tathmini ya ukuaji wa uchumi katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 kati ya Januari - Machi 2022. Kiwango cha ujazo wa maji yanayosambazwa kwa Wananchi kimeendelea kuimarika zaidi ukilinganisha na kiwango cha robo ya kwanza ya mwaka 2021.

Shughuli hii inajumisha uchimbaji wa visima, kutibu maji magumu kuwa maji malaini kwa ajili ya matumizi ya binadamu na kilimo, uchimbaji wa visima binafsi na uvunaji wa maji mvua.

Takwimu kutoka NBS zinaonesha kwamba kiwango kimeongezeka kutoka cubic meter milioni 76.8% mwaka 2021 katika robo ya kwanza mwaka huo, hadi kufikia cubic meter milioni 86.9% katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

Hii sawa na ongezeko la asilimia 11.9 kutoka asilimia 9.0 ya robo ya kwanza ya mwaka 2021. Kuimarika kwa sekta hii kumetokana na jitihada zilivyofanywa na serikali ya Rais Samia Suluhu kuwa kuboresha miundombinu ya maji mijini na vijijini
 
Screenshot_20220814-193150.png
Kabla ya mwaka 2030,Rais Samia atakuwa amefuta kabisa tatizo la maji hapa Tanzania na kuwatua wakina mama ndioe kichwani..

Dar tayari 👇
 
Mbona huku kuanzia ubungo mpaka mbezi tatizo maji ni kubwa Sana tangu mama Samia aingie madarakani na sijui kwa maeneo mengine kukoje
 
Mbona huku kuanzia ubungo mpaka mbezi tatizo maji ni kubwa Sana tangu mama Samia aingie madarakani na sijui kwa maeneo mengine kukoje
Mama ameahidi kupeleka maji kila sehemu hata uko mai yatafika endelea kusubiri Rais Samia hana propaganda yeye anafanya utekelezaji
 
Kwa upande wa Lindi, nilikopita hivi karibuni lina ukweli hili kwani nimekuta maji yanapelekwa Mchinga sasa kutokea Ng'apa......kazi inaenda kwa kasi. Sijajua kuhusu upatikanaji haswa wa maji yenyewe lkn miundombinu tu inaonekana!
 
Kufika 2025,tatizo la maji Tanzania litakuwa limefutwa kwa zaidi ya 90% ,Mjini na Vijijini.👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220815-163443.png
    Screenshot_20220815-163443.png
    93.3 KB · Views: 8
Kwa upande wa Lindi, nilikopita hivi karibuni lina ukweli hili kwani nimekuta maji yanapelekwa Mchinga sasa kutokea Ng'apa......kazi inaenda kwa kasi. Sijajua kuhusu upatikanaji haswa wa maji yenyewe lkn miundombinu tu inaonekana!
Ungefatilia ungeona Rais Samia anataka kuifungua kila sehemu ya Tanzania itapata huduma zote muhimu hasa maji, elimu na afya
 
Back
Top Bottom