Mkuu naona unaendelea kupigilia msumari pale pale ..single mother sio chaguo sahihi
Wanawake wanazingua mzee. Me kuna mwanamke nimezaa nae watoto wawili, na bado namuona singo maza. Hata akiwa amebaki pekeake hapa duniani simuoi abadani
 
Maisha hayapo hivyo bwashee , wewe ukishindwa kumlea mke wako na mtoto kuna wataalam wa mambo tutawamudu vizuri tu, na maisha yataenda vizuri sana

Sasa kama ni hivyo mbona mnalalamika tukiongea na Wake zetu mnaoishi nao? Inafikia mpaka mnawapiga. Yaani nyie ni wajinga Sana. Yaani umpige mwanamke kwa kuongea na Mzazi mwenzake?πŸ€“πŸ€“ Ambaye ulimkuta na walizaa.
Kweli dunia haiishi vituko
 
Kwenye usabato ndoa ni ya mke mmoja tu, watu kuzaa sio ndoa, hata mke wako wa ndani ya ndoa anaweza kuzaa na mwanaume mwingine nje ya ndoa.
 
Mkuu, point ipo, nimeipenda sana tusiwe wepesi wa kuweka watu wote kwenye kapu moja. Binadamu wanatofautiana sana kulingana na tabia, malezi, mazingira na maamuzi yao binafsi. Ndiyo maana ni vizuri kumuangalia mtu kama yeye, si kwa label aliyonayo.

Kwenye mahusiano kanuni yako haifanyi kazi hata kwa asilimia 10% kwa sababu mahusiano ili yawepo yenye tija kuna mambo lazima yawepo.

1. Maslahi
2. Mahitaji
3. maono.
4. Tabia.

Hizo pointi 1&2 ndio msingi mkuu wa mahusiano yoyote unayoyaona Duniani.

Chukua mwanamke mwenye Tabia njema, lakini kama utaathiri maslahi na mahitaji yake nakuhakikishia asilimia Mia moja hilo husiano linakufa.

Unapomuoa Single mother lazima ujue mbali na hitaji la upendo na mahitaji yake ya kimwili, pia mtoto wake kumhudumia sio hiyari kwani ni hitaji lake la msingi.

Unaposhindwa kufanya hivyo automatically utaona negative effects ambazo zitatikisa misingi ya mahusiano yenu. Na nikuambie tuu.

Wanaume wengi hufeli kwenye mahusiano kwa sababu ya kushindwa kuyajua ni yapi maslahi na mahitaji ya msingi ya mwanamke aliyemuoa
 
Kwenye usabato ndoa ni ya mke mmoja tu, watu kuzaa sio ndoa, hata mke wako wa ndani ya ndoa anaweza kuzaa na mwanaume mwingine nje ya ndoa.

Lete Aya ya Biblia inayotoka kwenye Amri za Mungu. Kisha tutaendelea kupeana masomo hapa mpaka kichwa yako ielewe.
 
🀣🀣🀣Hao mm nawaitaga vihelehele wa kuingilia yasiyo wahusu ila mwisho wao hua ni maumivu makali na majuto
Wala hakuna mkuu tatizo mnataka muwaache wanawake halafu wasipate watu , mkiwakuta tumewaweka ndani na kuwatunza wakapendeza mnapata pressure
 
Mama wa mtoto wangu naongea nae vizuri tu , na mume wake ni muelewa , busara tu za kiutu uzima zinatumika bwashee
 
Vijana mna mioyo miepesi sana.Sembuse single maza, wazee wa wazamani walikuwa wanalea watoto waliozaliwa na mke nje ya ndoa huku akiwa ndani ya ndoa.
 
Leta Aya ya biblia kwenye amri kumi inayokataza kula nguruwe au kambale.
Biblia haina amri kumi. Unasoma Biblia ipi?



Mungu alimpa Musa amri zaidi ya Mia sita.

Kuna amri za mahusiano ya mtu na mungu na watu.



Kuna amri ya vyakula

Kuna amri ya mipaka

Kuna amri ya afya na usafi wa mwili

Kuna amri za vita

Kuna amri za Waajiri na waajiriwa

Kuna amri za talaka na mirathi

Kuna amri za kilimo na mifugo.

Zipo nyingi Sana. Na hiy
o ndio huitwa torati.
 
Vijana mna mioyo miepesi sana.Sembuse single maza, wazee wa wazamani walikuwa wanalea watoto waliozaliwa na mke nje ya ndoa huku akiwa ndani ya ndoa.

Sheria za zamani unazijua lakini?

Unapoongea Jambo liangalie kwa upana wake.

Unajua zamani kisheria mtoto yoyote anayezaliwa kwenye nyumba yako ni wako?
Mtoto yeyote anayezaliwa hata na mtumwa wako ni wako?

Unajua zamani wanawake waliuzwa kwa kitu kinachoitwa Mahari?
Na ukimnunua mwanamke Hana haki ya kuondoka kwao wala kuvunja ndoa. Mwenye mamlaka hayo ni mwanaume aliyemnunua?

Sasa hivi hayo mambo hayapo. Hata umnunue mwanamke Leo (utoe mahari) Kesho anaweza kukukimbia na usifanye chochote.

Bado usione gap lililopo
 
Sasa wafundisheni na vijana wengine hii Tabia. Waache wivu.
Wakubali mke kuolewa na mwanaume zaidi ya mmojaa
Ili kuoa single maza au kuishi nae inabidi uwe umepevuka kiakili sana , wanaume wengi wanakwepa sana kuishi na wanawake wenye akili timamu
 
Kuoa mtu mwenye mtoto kuna complexity:
β€” Kuna mawasiliano na mzazi mwingine, lazime uyaachilie.
β€” Kuna responsibility za ziada.
β€” Kuna hofu ya kumkanya mtoto.

Hizo ni facts, Siweki ubishi.

Lakini hii ni thinking error inaitwa overgeneralization.

Reality ni kwamba:
β€” Si kila single mother ni mbaya.
β€” Si kila mwanamke ambaye hana mtoto itakuwa rahisi kuishi naye.
β€” Kuna wanawake wazuri, kuna wanawake wabaya
Kama ilivyo kwa wanaume pia.

Kwa kiasi kikubwa kwenye huu uzi naiona fear of loss, fear of competition na fear ya kukosa full control over her.

My take:
β€” Chagua mtu based on character.
β€” Evaluate, siyo tu kuogopa kundi lote bila informations sahihi.

Siyo kila single mother ni matokeo ya ujinga au malezi mabaya:
β€” Wengine kifo cha mwenza,
β€” Wengine walitafutiwa tu visababu vya kuachwa sababu ya kukwepa majukumu,
β€” Wengine kubakwa,
β€” Wengine mimba za utotoni kipindi akili haijakomaa,
β€” Wengine walitelekezwa,
β€” Wengine shinikizo la kifamilia/kijamii.

Usioe mwanamke ambaye,
β€” Hana heshima wala hajiheshimu,
β€” Asiye muadilifu,
β€” Asiye wajibika,
β€” Asiyejua mipaka, na
β€” Asiye tayari kujifunza au kuelekezwa anapokosea,
Haijalishi ni single mother au la.

Hizo sifa mara zote zinatoka kwenye malezi aliyolelewa na siyo personal experience pekee.
 
Miaka ya mwishoni mwa 90 nimeshuhudia jamaa akiondoka kwenye familia aliyozaliwa na kuhamia kwa ukoo wa baba halisi bila mgogoro.

Kwa hiyo wazee na ukoo wake walikuwa wanajua kuwa kuna watoto sio wao na ndio maana watoto wakihama ilikuwa haileti mgogoro.
Kiukweli wazee walikuwa na uvumilivu wa mambo ya mahusiano, mambo ambayo vijana wa leo wanachomana visu na mkaa.
 

Zamani Sheria zake zilikuwa tofauti na sasa
 

Tatizo la ChatGpt ndio hili. Muandiko haujifichi labda uhariri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…