Mamaake ni Single Mother lakini kamkataza asioe Single Mother

Mamaake ni Single Mother lakini kamkataza asioe Single Mother

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
38,858
Reaction score
90,342
MAMAAKE NI SINGLE MOTHER LAKINI KAMKATAZA ASIOE SINGLE MOTHER.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Rafiki Yangu wa shule(A'Level) na chuo kikuu amenipigia akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa.

2. Kitabia ni Mpole, sio mtu wa maneno mengi. Mtu wa Amani, asiyetaka vuruguvurugu. Sio mtu wa Principles na makanuni kanuni kama Mimi.
Wengi humuita mtu piece. Kwa Sisi wataalam tunamtambua kama Niceman.

3. Wakati tukiwa chuo alikuwa anadhulumiwa kutokana na huruma zake. Boom likitoka washkaji wanamkopesha kwa ahadi ya kumrejeshea. Lakini hakuna aliyewahi kurudisha.
Basi jamaa Kila mara alikuwa akinilalamikia. Nikamwambia wakikutaka wakikope walete kwangu.

4. Basi tukiwa vimbwetani tulikuwa tunataniani na bahati nzuri unavyojitambulisha ndivyo unavyochukuliwa. Fikiria MTU akukope laki moja, asirudishe, alafu aje tena miezi kadhaa mbele akukope elfu hamsini, asirudishe, achukue PC yako aseme imeibiwa ubaki umeng'aa. Basi ndivyo tabia ya Rafiki Yangu hiyo.

5. Mwenyewe nilipomuuliza why yupo hivyo. Anasema hapendi migogoro, Sijui vurugu. Lakini niligundua anatabia ya Uoga, kutojiamini na MTU wakuigulia ndani kwa ndani.

6. Miaka zaidi ya kumi imepita tangu tumalize chuo kikuu. Hatujaonana zaidi ya mitandaoni huko na mara mojamoja kuwasiliana kwenye WhatsApp

7. Hivi karibuni alinipa wito tuonane. Tukaonana maeneo ya Shoppers pale Mbezi Beach.

8. Baada ya kuzungumzia kuhusu mambo mengine y maisha hasa tukikumbushia Stori za chuoni. Tukafika kwenye lengo la kukutana Siku Ile.

9. Alikuwa anamabadiliko kiasi, kidevu na mashavu vikiwa vimefunikwa na ndevu tofauti na alivyokuwa chuo. Kitambia kiasi. Mambo yake hayakuonekana kwamba ni mabaya. Hata yeye mwenyewe alikiri hela ya kubadilisha mboga haimsumbui.

10. Akaniambia, anataka kuoa. Sasa nikajua anataka niwe bestman wake. Akamsifia Sana huyo mchumba wake. Huku akitumia simu kunionyesha picha za huyo mwanamke.

11. Ni mwanamke mzuri. Mweupe. Mwenye uso mzuri kutokana na macho na pua mchongoko aliyonayo.
Shape yake size ya kati. Nikamsifu huku nikimhakikishia binti ni chombo kwelikweli.

12. Hakuishia hapo, kusindilia CV, akasema mwanamke wake ni Mfamasia katika Moja ya hospital za private hapa jijini Dar es salaam. Nikamwambia hiyo kwako ni bahati Mzee huku tukicheka wote.

13. Uso wake ulikuwa na furaha Sana aliponisikia nikimpongeza. Ni kama alikuwa akiniamini hivi au kunikubali kwa namna Fulani. Na nili meet mahitaji yake.

14. Nikamuuliza kwa hiyo ndoa lini? Au ndio Ile ya kusogea tuishi? Kabla hajajibu nikamwambia yeye ni MTU wa kufuata protocol na mambo ya Mila na taratibu.

15. Hapo akatulia. Ni kama alikuwa amesafirisha mawazo Yake sehemu. Nami nikamuacha kwa sekunde huku nikimtazama.

16. Akaniambia, Lakini anamtoto.

17. Aliongea hivyo huku akiniangalia kama MTU aliyehisi neno baya limemponyoka mbele ya Mtu anayeheshima. So macho yake ni kama yalikuwa yanategemea kuona mshtuko, au badiliko hasi, au namna yoyote mbaya.

18. Nikamwambia Mtoto sio tatizo.
19. Akaniambia lakini nasomaga Makala zako. Unasemaga vijana wasioe Single Mother.

20. Nikatabasamu. Nikasema vijana ambao hawajaamua, vijana ambao hawana upendo wote. Vijana wasiojiweza na wanaojitafuta kiuchumi wasioe single mother. Lakini haimaanishi single mother wote wanamatatizo. Ila asilimia kubwa wanashida kubwa.

21. Akaniambia ananielewa ninamaanisha nini. Nikamwambia sasa tatizo nini. Kama vigezo vingine vimekaa vizuri na amethibitisha anampenda, na yupo tayari kukabiliana na changamoto zozote why not.

22. Akapumua. Akawa kama anapitisha mawazo yake mbele ya kioo huku akiyaangalia. Nikameambia OA. Hata hivyo wewe sio mtu wa Principles ngumu. Utaweza na mtafurahia.

23. Akaongea polepole, tatizo Bi.mkubwa akimaanisha Mamaake. Anasema Mamaake anamzuia asimuoe huyo mwanamke. Kisa na mkasa huyo mwanamke anamtoto.

24. Amejaribu kumshawishi mamaake lakini bi. Mkubwa amegoma. Anasema kama yeye sio mtoto wake amuoe huyo mfamasia.

25. Hivyo amekuja kwangu kuomba ushauri akitegemea Mimi nitampa suluhu Bora kabisa katika mtihani wake huo.

26. Wewe ungekuwa Mimi ungemshauri vipi?

27. Hataki kugombana na Mama Yake kwani anampenda.
28. Hataki kumpoteza mfamasia kwani naye anampenda na anamuona kama mkewe mtarajiwa.

29. Mshikaji anasema, Mamaake mwenyewe aliolewa akiwa tayari na mtoto. Ingawaje baada ya miaka kupita Mzee wao alifariki. Ananiambia kuna Siku mamaake alimrushia maneno yasiyofaa kidogo amjibu kwamba mbona yeye aliolewa akiwa single mother. Lakini alijikuta akijizuia.

30. Binafsi nilimwambia Kwanza asitishe wazo la harusi ya hivi karibuni huku akiendelea na mahusiano na huyo mfamasia.

31. Ajipe muda zaidi, huku mamaake akiona mchango na faida ya mfamasia kwa kijana wake. Akigundua tabia za Mkamwana wake.
Tabia njema na upendo huyeyusha mitazamo potofu na chuki zisizo na sababu.

32. Then baadaye anaweza kumuoa. Lengo ni kutomuudhi Mama lakini pia kupima subira, uvumilivu na usikivu wa mwanamke, Mfamasia.

33. Mshikaji ananiambia mwanamke anahitaji hiyo ndoa kwa haraka kwa udi na uvumba. Kwamba umri kidogo umesogea kwani anamiaka 29. Mshikaji miaka 35.

34. Nikamwambia uamuzi wote uko mikononi mwake. Mimi ushauri wangu ndio huo.
Nilimuambia kama anania ya kumuoa huyo binti lazima ajue anatakiwa kuoa mwanamke ambaye aanasubira, mvumilivu na anayemsikiliza(mwamini).

Kama anahisi utampotezea muda huyo hakuamini. Hiyo ni red flag.

35. Nikamwambia, mambo mazuri kama ndoa hayahitaji haraka. Kuuziwa mbuzi kwenye gunia ni dakika.

36. Nikamwambia, ndoa ni halalalisho la kisheria lakini halizuii nyie kuendelea na mahusiano yenu.

37. Nikamwambia, Mamaake kuna hoja anazo na hatakiwi kuzipuuza. Jukumu lake ni kuzifuatilia kwa kujipa muda.

38. Nikamwambia, usifanye jambo hili kumridhisha au kumthibitishia yeyote unampenda. Bali Fanya. Jambo hili kwa kuonyesha wewe umekua mwanaume na unajua kufanya maamuzi sahihi.
Kwa kulinda heshima ya Kila mmoja wao bila kuathiri yake.

39. Basi tukamaliza. Alinishukuru lakini bado aliniambia amechanganyikiwa.

Je wewe ungemshauri Jambo gani?

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
kama bado anasubiri kila mtu aridhike… basi hata akioa leo, bado hatakuwa ameoa ,ataendelea kuidhinishwa kila hatua ya maisha yake.

Mama hayupo kundi la Kila mtu.
Ni mhusika nyeti Sana katika maisha ya watu wengi. Hasa walioleleewa na Mama.

So jamaa hoja anayo.
Ingawaje maisha ni yake.
 
Mwanaume hapaswi kutumia emotions wala feelings kwenye maamuzi ya mambo makubwa kama kuoa, ambapo ni ungamo litakaloathiri vizazi vyake vijavyo. Yani ni decision ambayo ni "Multi-Generations" to come.

Mimi nimeoa, nina watoto kadhaa. Lakini ikitokea leo hii nimeachana na mke wangu na nikataka kuoa tena, sitaoa mwanamke aliyekwisha kuzaa!

Ni decision ambayo unapaswa kutanguliza logic mbele na siyo hidia.
 
Huyo kijana anaekatazwa na mama yake mambo ya kuoa bado ni kiazi kwa jinsi single maza walivyo wajanja bora akatafute wa kufanana nae huko kihurio.

Wewe Mamaako akikukataza kitu hupati shida?
Hujiulizi bi mkubwa anaona nini nisichokiona?

Au unasema tuu Bi.mkubwa ana mitazamo potofu bila kufuatilia na kuchunguza hoja zake?
 
Mwanaume hapaswi kutumia emotions wala feelings kwenye maamuzi ya mambo makubwa kama kuoa, ambapo ni ungamo litakaloathiri vizazi vyake vijavyo. Yani ni decision ambayo ni "Multi-Generations" to come.

Mimi nimeoa, nina watoto kadhaa. Lakini ikitokea leo hii nimeachana na mke wangu na nikataka kuoa tena, sitaoa mwanamke aliyekwisha kuzaa!

Ni decision ambayo unapaswa kutanguliza logic mbele na siyo hidia.

Upo sahihi.
Lakini uamuzi wako mara nyingi ni ule wa wanaume wenye principles tata
 
Wewe Mamaako akikukataza kitu hupati shida?
Hujiulizi bi mkubwa anaona nini nisichokiona?

Au unasema tuu Bi.mkubwa ana mitazamo potofu bila kufuatilia na kuchunguza hoja zake?
Mimi mama yangu ndio namkataza vitu , ndio maana huwa nasema bado nyie ni vijana wadogo na bado mna mitazamo ya kivulana
 
Mimi mama yangu ndio namkataza vitu , ndio maana huwa nasema bado nyie ni vijana wadogo na bado mna mitazamo ya kivulana

😂😂
Unamuonea kisa unampa pesa.
Acha unyanyasaji kwa mamaako..

Huna uwezo wa kumkataza Mamaako Jambo lolote😄😄
Yeye anakuchora tuu. Kuna mambo yakupasa ujifunze kuhusu Wanawake, akiwemo Mamaako.
 
Upo sahihi.
Lakini uamuzi wako mara nyingi ni ule wa wanaume wenye principles tata
Kazini leo kaja kuhudumiwa mtoto wa miaka 3, ana malezi mabovu mpaka anamuambia mama yale "Mommy I hate you". Baba mtu naye anasema "mimi ngoja niondoke hapa maana akiniona ndiyo atasumbua sana".

Sasa, mwanaume ili uwe na familia iliyonyooka, hauna budi kusimama katika upande wa "Principles Tata" ili uje uwe na kizazi productive.
 
Kama bi mkubwa wake hataki, bac atafute mke mwengne na kama bi mkubwa wake alikuw single mother bac anajua changamoto zao

Hapana. Anaweza kununua muda. Wengi wamefanya hivi wakafanikiwa. Na wanaishi vizuri baina na wake zao na mama anafurahia.

Akimuacha kwa sababu ya Mama. Siku akioa mwingine alafu aliyemuoa akawa kipengele ugomvi na mamaake utazuka upya na atamkumbuka mfamasia. Huku mfamasia akisema aliacha laana hata kama ni uongo.

Awe na subira kwani wanaharakia wapi?
 
Kazini leo kaja kuhudumiwa mtoto wa miaka 3, ana malezi mabovu mpaka anamuambia mama yale "Mommy I hate you". Baba mtu naye anasema "mimi ngoja niondoke hapa maana akiniona ndiyo atasumbua sana".

Sasa, mwanaume ili uwe na familia iliyonyooka, hauna budi kusimama katika upande wa "Principles Tata" ili uje uwe na kizazi productive.

Ukiwa mkoloni miaka hii dunia inakuzomea ingawaje matatizo mengi yanakuwa hayakukuti hasa haya matatizo ya mahusiano
 
Kwanamna ulivyo elezea tabia na kariba ya rafiki yako, ingekua ni mimi ningemshauri asioe kwanza na amsikilize mama yake sababu mama yake ni single mama na anafaham pengine mitihani na maumivu aliyo yapitia kutokana na kuolewa akiwa tayari anamtoto.
Na kwanamna huyo mchumba wake anavyo itaka ndoa kwa uharaka, sioni kama anaweza akawa mtu sahihi kwasababu analazimisha ndoa kwakua umri umeenda na sio kwakua yupo tayari kuingia kwenye ndoa.
 
Kwanamna ulivyo elezea tabia na kariba ya rafiki yako, ingekua ni mimi ningemshauri asioe kwanza na amsikilize mama yake sababu mama yake ni single mama na anafaham pengine mitihani na maumivu aliyo yapitia kutokana na kuolewa akiwa tayari anamtoto.

Jamaa anaonekana anampenda Sana Mfamasia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom