Pongezi kwenu Single Mothers

Pongezi kwenu Single Mothers

Mkuu naona unaendelea kupigilia msumari pale pale ..single mother sio chaguo sahihi
Wanawake wanazingua mzee. Me kuna mwanamke nimezaa nae watoto wawili, na bado namuona singo maza. Hata akiwa amebaki pekeake hapa duniani simuoi abadani
 
Maisha hayapo hivyo bwashee , wewe ukishindwa kumlea mke wako na mtoto kuna wataalam wa mambo tutawamudu vizuri tu, na maisha yataenda vizuri sana

Sasa kama ni hivyo mbona mnalalamika tukiongea na Wake zetu mnaoishi nao? Inafikia mpaka mnawapiga. Yaani nyie ni wajinga Sana. Yaani umpige mwanamke kwa kuongea na Mzazi mwenzake?🤓🤓 Ambaye ulimkuta na walizaa.
Kweli dunia haiishi vituko
 
Sasa kama ni hivyo mbona mnalalamika tukiongea na Wake zetu mnaoishi nao? Inafikia mpaka mnawapiga. Yaani nyie ni wajinga Sana. Yaani umpige mwanamke kwa kuongea na Mzazi mwenzake?🤓🤓 Ambaye ulimkuta na walizaa.
Kweli dunia haiishi vituko
Kwenye usabato ndoa ni ya mke mmoja tu, watu kuzaa sio ndoa, hata mke wako wa ndani ya ndoa anaweza kuzaa na mwanaume mwingine nje ya ndoa.
 
Mkuu, point ipo, nimeipenda sana tusiwe wepesi wa kuweka watu wote kwenye kapu moja. Binadamu wanatofautiana sana kulingana na tabia, malezi, mazingira na maamuzi yao binafsi. Ndiyo maana ni vizuri kumuangalia mtu kama yeye, si kwa label aliyonayo.

Kwenye mahusiano kanuni yako haifanyi kazi hata kwa asilimia 10% kwa sababu mahusiano ili yawepo yenye tija kuna mambo lazima yawepo.

1. Maslahi
2. Mahitaji
3. maono.
4. Tabia.

Hizo pointi 1&2 ndio msingi mkuu wa mahusiano yoyote unayoyaona Duniani.

Chukua mwanamke mwenye Tabia njema, lakini kama utaathiri maslahi na mahitaji yake nakuhakikishia asilimia Mia moja hilo husiano linakufa.

Unapomuoa Single mother lazima ujue mbali na hitaji la upendo na mahitaji yake ya kimwili, pia mtoto wake kumhudumia sio hiyari kwani ni hitaji lake la msingi.

Unaposhindwa kufanya hivyo automatically utaona negative effects ambazo zitatikisa misingi ya mahusiano yenu. Na nikuambie tuu.

Wanaume wengi hufeli kwenye mahusiano kwa sababu ya kushindwa kuyajua ni yapi maslahi na mahitaji ya msingi ya mwanamke aliyemuoa
 
Kwenye usabato ndoa ni ya mke mmoja tu, watu kuzaa sio ndoa, hata mke wako wa ndani ya ndoa anaweza kuzaa na mwanaume mwingine nje ya ndoa.

Lete Aya ya Biblia inayotoka kwenye Amri za Mungu. Kisha tutaendelea kupeana masomo hapa mpaka kichwa yako ielewe.
 
🤣🤣🤣Hao mm nawaitaga vihelehele wa kuingilia yasiyo wahusu ila mwisho wao hua ni maumivu makali na majuto
Wala hakuna mkuu tatizo mnataka muwaache wanawake halafu wasipate watu , mkiwakuta tumewaweka ndani na kuwatunza wakapendeza mnapata pressure
 
Sasa kama ni hivyo mbona mnalalamika tukiongea na Wake zetu mnaoishi nao? Inafikia mpaka mnawapiga. Yaani nyie ni wajinga Sana. Yaani umpige mwanamke kwa kuongea na Mzazi mwenzake?🤓🤓 Ambaye ulimkuta na walizaa.
Kweli dunia haiishi vituko
Mama wa mtoto wangu naongea nae vizuri tu , na mume wake ni muelewa , busara tu za kiutu uzima zinatumika bwashee
 
Leta Aya ya biblia kwenye amri kumi inayokataza kula nguruwe au kambale.
Biblia haina amri kumi. Unasoma Biblia ipi?



Mungu alimpa Musa amri zaidi ya Mia sita.

Kuna amri za mahusiano ya mtu na mungu na watu.



Kuna amri ya vyakula

Kuna amri ya mipaka

Kuna amri ya afya na usafi wa mwili

Kuna amri za vita

Kuna amri za Waajiri na waajiriwa

Kuna amri za talaka na mirathi

Kuna amri za kilimo na mifugo.

Zipo nyingi Sana. Na hiy
o ndio huitwa torati.
 
Vijana mna mioyo miepesi sana.Sembuse single maza, wazee wa wazamani walikuwa wanalea watoto waliozaliwa na mke nje ya ndoa huku akiwa ndani ya ndoa.

Sheria za zamani unazijua lakini?

Unapoongea Jambo liangalie kwa upana wake.

Unajua zamani kisheria mtoto yoyote anayezaliwa kwenye nyumba yako ni wako?
Mtoto yeyote anayezaliwa hata na mtumwa wako ni wako?

Unajua zamani wanawake waliuzwa kwa kitu kinachoitwa Mahari?
Na ukimnunua mwanamke Hana haki ya kuondoka kwao wala kuvunja ndoa. Mwenye mamlaka hayo ni mwanaume aliyemnunua?

Sasa hivi hayo mambo hayapo. Hata umnunue mwanamke Leo (utoe mahari) Kesho anaweza kukukimbia na usifanye chochote.

Bado usione gap lililopo
 
Sasa wafundisheni na vijana wengine hii Tabia. Waache wivu.
Wakubali mke kuolewa na mwanaume zaidi ya mmojaa
Ili kuoa single maza au kuishi nae inabidi uwe umepevuka kiakili sana , wanaume wengi wanakwepa sana kuishi na wanawake wenye akili timamu
 
KIJANA USIWE WENYE ILE NOTION YA "SIO KILA SINGLE MOTHER NI MBAYA" WENGI WAMEPOTEA. MASHAKA NDIO AKILI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Kila Siku nitawapa darasa mpaka liwaingie. Maana kuna watu vichwa ngumu.

2. Kanuni za ulinzi na usalama sio tuu kama majeshi ya nchi. Bali hata katika maisha yako.

3. Unapoenda Sokoni jioni ukakuta tunda au bidhaa nzuri sana ambayo ilikuwepo tangu asubuhi. Usikurupe. Usiende kichwakichwa kiboya. Utapigwa. Lazima ujiulize kwa nini hii bidhaa ni nzuri lakini mpaka jioni hii haijachukuliwa? Hilo ni swali la watu wanaotumia akili zao sawasawa.

4. Usijifanye unamacho kuliko wengine. Kunaitwa kukurupuka.

5. Umeenda porini ni mchana au jioni. Ukakuta juu ya mti kuna tunda zuri limeiva. Kwa sababu umjinga hujiulizi kwa nini tunda hii mpaka sasa halijachumwa,halijaliwa na ndege au wadudu. Unakurupuka.

6. Kwenye maisha yako usiweke uaminifu kwenye hamna. Kwanza kanuni ya Kwanza ya usalama inasema trust no one. Suspect everything and everyone. Hiyo ndio njia ya kuishi kwa Amani kuliko kujizima data.

7. Oooh! Taikon sio Kila mwanamke single mother anakipengele na anadrama. Usiseme kama watu wajinga.
Hiyo kauli yako inaonyesha tayari upo kwenye hatari.

8. Kwenye maisha, usipende kuishi kwa exceptional. Kwamba Exceptional ndio maisha. Yaani usipende kuishi kwa kukamaria/kubet katika mambo nyeti.

9. Kila Jambo linamuda wake. Umri wa kuolewa ni miaka 16-25 hapo. Akichelewa sana miaka 30.
Mtu asiyejua kufanya mambo kwa wakati, hajui wakati sahihi wa kufanya mambo yake. Hajui vipaombele muhimu vinavyodhibitiwa na Muda. Huyo mtilie mashaka.

14. Umri wa kijana kuoa ni miaka 20-40.
Sio mwanaume anakuja anamiaka 45 mara 50+ anataka kukuoa binti Mdogo.

15. Mbaya zaidi anakuambia sikuwahi kuwa na mke. Binti mwenye akili hawezi kukubali kuolewa na mtu asiyejua kutumia wakati vizuri.

16. Ooh! Nilikuwa natafuta pesa. Sijui blah blah blah! Kutafuta pesa ni muhimu lakini hakufanyi mambo mengine ya muhimu kusimama.

17. Unaposema Kuwa sio Kila single mothers anakipengele lazima ujue kuwa vipengele vya wanaawake vinatokana na mahitaji yao kwa sehemu kubwa ambayo Yana shape tabia zao.

18. Sio hiyari. Mtoto wa single mother lazima umfurahishe ili single mother asikuletee kipengele. Hilo lipo hivyo. Huwezi badili. Kama hutaki ukweli huu achana na single mother. Utawatesa bure tuu.

19. Pili, mtoto wako na mtoto wasingle mother lazima uwachukulie wote ni Wako na uwahudumie sawa. Kama hutaki kipengele.

20. Tatu, kumhudumia mtoto wa single mother hakuondoi ukweli kuwa huyo sio mtoto wako na hauna mamlaka naye yoyote Yale kushinda Babake Mzazi.

21. Kuoa single mothers ni competition ya hiyari kushindana na Mzazi mwenza wa single mother. Lazima ulinganishwe karibu kwa Kila kitu.
Omba Mungu mzazi mwenzie asifanikiwe. Akifanikiwa mwanamke yupo proudly na mwanaume mshindi sio wewe uliyefeli maisha hata kama anaishi na wewe.

22. Mara nyingi single mother hawatakusumbua watoto wakiwa wadogo. Subiri wajitegemee yaani wakishaanza kuwa na familia zao.
Kumbuka mwanamke anapoteza kukutii kadiri umri wako unavyopanda.
Utii wake atauhamishia kwa watoto na wanaume wenye nguvu sio Wewe.

23. Lazima ujue ukweli huu. Wanawake wengi pamoja na kuumizwa na waliowazalisha ila hao wanaume ndio walikuwa wanaume wa ndoto zao. Sio wewe.

24. Wanawake wengi watakushangaa na kukudharau kwa kuoa single mother au mwanamke Mzee ilhali wanawake wabichi wapo. Wengi wao watakuona kama wewe ni mwanaume mwenye thamani ndogo.
Ndio maana Wafalme na makuhani huoa Wanawake bikira au wadogo ili kulinda heshima yakifalme na kikuhani.

25. Elewa ukifanya mambo ambayo wanawake wangekuwa wanaume wasingefanya. Basi wanawake wanakudharau. Ni kwamba hujitambui.

26. Kumbuka wanawake ni viumbe wanaojua vitu vizuri na kujua thamani. Hivyo huheshimu wanaume wanaojua vitu vizuri na wenye kujiheshimu thamani zao.

27. Wewe ni Mjinga kama utaoa single mother alafu umzuie asiongee na Mzazi mwenzake. Kwa nini wasiongee wakati wanamtoto? Huyo mtoto ni wako?
Wao ndio walimzaa. Ni mtoto wao.

28. Unaposema mkeo ambaye ni single mother anaongea na Mzazi mwenzake sio kwamba unamfanya huyo mwanamke aonekane hajitambui. Wewe ndio unaelezea watu kwamba hujitambui. Hillo Jambo ungepaswa kuliona mapema kabla hujamuoa.

29. Sio dhambi wala kosa Mkeo uliyemkuta single mother kuongea na Mzazi mwenzake. Huo ni wajibu. Wanamtoto pamoja. Lazima wajadiliane kuhusu mtoto wao. Ulitaka nani ajadiliane naye wakati babaake yupo?

30. Kama ulikuwa hutaki hayo ungeoa asiye na mtoto/watoto.

31. Single mothers sio kwa wanaume wenye mapenzi Yale makali, wenye visheria Sheria uchwara. Wewe ndio unaleta vipengele single mother hana kipengele.

32. Elewa, kisaikolojia mtoto hufurahi kuona Mama na Baba yake wakikaa pamoja. Wakishiriki pamoja kuhusu kumlea.
Wakienda pamoja out, wakishitiki sherehe ya mtoto pamoja.

33. Sio wewe Step father. Kamwe huwezi ziba pengo la Baba Mzazi wamtoto.

34. Ukioa single mother lazima umruhusu mkeo amualike Baba Mzazi kwenye sherehe kama birthday za mtoto wao. Mahafali,, sijui shule, sijui sikukuu kutoka mara mojamoja waache waende. Ni kwaajili ya mtoto.

35. Mtoto hujifunza upendo halisi kwa wazazi wake sio watu Back

36. Yatima hata umpe upendo vipi ule atauhesabu tuu kama Msaada na sio upendo.
Upendo mtu anajifunza na anaupata kwa Baba na Mama yake, na unaingia moyoni.

37. Upendo mtu anaupata kwa mkewe au Mumewe. Na sio zaidi ya hapo.
Upendo wowote nje ya watu hao huonekana kama Deni.

38. Upendo MTU ataupata nyumbani. Sehemu yoyote ambayo sio nyumbani hata waonyeshe upendo kiasi gani bado utakuwa na wasiwasi, hofu na hutakuwa na furaha na Raha ya kweli.

39. Ndio maana kukaa kwa ndugu ni KAZI kwa sababu hata wawe wema na waonyeshe upendo kiasi gani. Bado kuna gap hawawezi kuliziba.
Au ukiishi na ndugu hapo kwako, hata umfanyie nini ambacho kwao hafanyiwi bado kuna gap huwezi kuliziba.

40. Usiishi kwa notions ambayo ni exceptional cases

41. Kama kinajulikana ni kibaya nawe hesabu ni kibaya na hiyo haimaanishi kwamba hakuna exceptional yaani wachache ambao ni Wema, wazuri

42. Uzuri wa vitu vinavyosemwa vibaya usiyokane na mtazamo wako. Bali kitu au mtu huyo akuonyeshe na uone mwenyewe bila mihemko.

Mimi nimemaliza.

Taikonmaster
Kwa Sasa, Sababei, Dar es salaam
Kuoa mtu mwenye mtoto kuna complexity:
— Kuna mawasiliano na mzazi mwingine, lazime uyaachilie.
— Kuna responsibility za ziada.
— Kuna hofu ya kumkanya mtoto.

Hizo ni facts, Siweki ubishi.

Lakini hii ni thinking error inaitwa overgeneralization.

Reality ni kwamba:
— Si kila single mother ni mbaya.
— Si kila mwanamke ambaye hana mtoto itakuwa rahisi kuishi naye.
— Kuna wanawake wazuri, kuna wanawake wabaya
Kama ilivyo kwa wanaume pia.

Kwa kiasi kikubwa kwenye huu uzi naiona fear of loss, fear of competition na fear ya kukosa full control over her.

My take:
— Chagua mtu based on character.
— Evaluate, siyo tu kuogopa kundi lote bila informations sahihi.

Siyo kila single mother ni matokeo ya ujinga au malezi mabaya:
— Wengine kifo cha mwenza,
— Wengine walitafutiwa tu visababu vya kuachwa sababu ya kukwepa majukumu,
— Wengine kubakwa,
— Wengine mimba za utotoni kipindi akili haijakomaa,
— Wengine walitelekezwa,
— Wengine shinikizo la kifamilia/kijamii.

Usioe mwanamke ambaye,
— Hana heshima wala hajiheshimu,
— Asiye muadilifu,
— Asiye wajibika,
— Asiyejua mipaka, na
— Asiye tayari kujifunza au kuelekezwa anapokosea,
Haijalishi ni single mother au la.

Hizo sifa mara zote zinatoka kwenye malezi aliyolelewa na siyo personal experience pekee.
 
Sheria za zamani unazijua lakini?

Unapoongea Jambo liangalie kwa upana wake.

Unajua zamani kisheria mtoto yoyote anayezaliwa kwenye nyumba yako ni wako?
Mtoto yeyote anayezaliwa hata na mtumwa wako ni wako?

Unajua zamani wanawake waliuzwa kwa kitu kinachoitwa Mahari?
Na ukimnunua mwanamke Hana haki ya kuondoka kwao wala kuvunja ndoa. Mwenye mamlaka hayo ni mwanaume aliyemnunua?

Sasa hivi hayo mambo hayapo. Hata umnunue mwanamke Leo (utoe mahari) Kesho anaweza kukukimbia na usifanye chochote.

Bado usione gap lililopo
Miaka ya mwishoni mwa 90 nimeshuhudia jamaa akiondoka kwenye familia aliyozaliwa na kuhamia kwa ukoo wa baba halisi bila mgogoro.

Kwa hiyo wazee na ukoo wake walikuwa wanajua kuwa kuna watoto sio wao na ndio maana watoto wakihama ilikuwa haileti mgogoro.
Kiukweli wazee walikuwa na uvumilivu wa mambo ya mahusiano, mambo ambayo vijana wa leo wanachomana visu na mkaa.
 
Miaka ya mwishoni mwa 90 nimeshuhudia jamaa akiondoka kwenye familia aliyozaliwa na kuhamia kwa ukoo wa baba halisi bila mgogoro.

Kwa hiyo wazee na ukoo wake walikuwa wanajua kuwa kuna watoto sio wao na ndio maana watoto wakihama ilikuwa haileti mgogoro.
Kiukweli wazee walikuwa na uvumilivu wa mambo ya mahusiano, mambo ambayo vijana wa leo wanachomana visu na mkaa.

Zamani Sheria zake zilikuwa tofauti na sasa
 
Kuoa mtu mwenye mtoto kuna complexity:
— Kuna mawasiliano na mzazi mwingine, lazime uyaachilie.
— Kuna responsibility za ziada.
— Kuna hofu ya kumkanya mtoto.

Hizo ni facts, Siweki ubishi.

Lakini hii ni thinking error inaitwa overgeneralization.

Reality ni kwamba:
— Si kila single mother ni mbaya.
— Si kila mwanamke ambaye hana mtoto itakuwa rahisi kuishi naye.
— Kuna wanawake wazuri, kuna wanawake wabaya
Kama ilivyo kwa wanaume pia.

Kwa kiasi kikubwa kwenye huu uzi naiona fear of loss, fear of competition na fear ya kukosa full control over her.

My take:
— Chagua mtu based on character.
— Evaluate, siyo tu kuogopa kundi lote bila informations sahihi.

Siyo kila single mother ni matokeo ya ujinga au malezi mabaya:
— Wengine kifo cha mwenza,
— Wengine walitafutiwa tu visababu vya kuachwa sababu ya kukwepa majukumu,
— Wengine kubakwa,
— Wengine mimba za utotoni kipindi akili haijakomaa,
— Wengine walitelekezwa,
— Wengine shinikizo la kifamilia/kijamii.

Usioe mwanamke ambaye,
— Hana heshima wala hajiheshimu,
— Asiye muadilifu,
— Asiye wajibika,
— Asiyejua mipaka, na
— Asiye tayari kujifunza au kuelekezwa anapokosea,
Haijalishi ni single mother au la.

Hizo sifa mara zote zinatoka kwenye malezi aliyolelewa na siyo personal experience pekee.

Tatizo la ChatGpt ndio hili. Muandiko haujifichi labda uhariri sana
 
Back
Top Bottom