Polisi watoa kibali cha maandamano kwa CHADEMA. Wawasisitiza viongozi kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
1706024890811.png

SIASA: Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limetoa kibali kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya Maandamano yaliyotangazwa kufanyika Januari 24, 2024 katika baadhi ya Mitaa ya Jiji la Dar

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Kariakoo, Jeshi la Polisi limesema Maandamano hayo hayatazuiwa na Polisi iwapo tu hayataleta uvunjifu wa amani au kusababisha vitendo vya kihalifu

Jeshi la Polisi limeitaka CHADEMA kuhakikisha inazuia lugha za uchochezi na kejeli zinazoweza kusababisha uvunjifu wa Sheria. Pia, limeagiza kufuatwa kwa taratibu katika maeneo yote ambayo chama hicho kimetoa taarifa za kufanya maandamano
---
BARUA YA POLISI
Kumb.Na. GB.795/1054/01/03 23/01/2024
CHAMA CHA DF.MOKRAS1A NA MAENDELEO
PO BOX31191
UFIPA STREET KINONDONI
DAR ES SALAAM

FAX / TEL NO (0222668866)

email :info@chadema.or.lz
websiteiwww.chadema.or.tz

YAH: TAARIFA YA MAAMDAMANO

Tafadhali husika na soino tajwa hapo juu na rejea barua yako yenyc Kumb: Na.C/ADM/MS/l 1/59 ya tarehe 16/01/2024.

Kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu zinazohusu ’'taarifa za MAANDAMANO, hayatazuiwa na Jeshi la Polisi iwapo Maandamano hayo hayataleta uvunjifu wa amani, au kusababisha kutendeka kwa vitendo vya kihalifu.

Kwa barua hii viongozi wa CDM na wanachama mnalojukumu la kuzuia lugha za uchochczi, kcjeli zinazowcza kupclekea kutendcka kwa vitendo vya uvunjaji wa shcria. Mtalaztmika kufuata utaratibu wa kisheria katika macneo yotc kwa kadri mtakavyoclekezwa na wasimamizi wa shcria Polisi w .kiwa ni kiongozi
katika eneo bilo mlilolitolca taarifa.

Maandamano hayo yasisababishe uvunjivu wa amani/watu kuibiwa au kuporwa na yawe kwenyc njia zilizokubaliwa.Taarifa ycnu pia izingatie muda wa kilichoelezwa kwenye barua ycnu ikiwa ni pamoja na kutoanzishwa mambo mengine ambayo hayamo kwenyc taarifa iliyotol'ewa Polisi.

5. Aidha ukiukwaji wowote wa masharti hayo utalilazimisha Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria bila kusita ili kuzuia madhara ya kuvunjika kwa amani.

6. Naamini msingi wa taarifa yenu utabaki kuwa ni kudumishwa kwa amani na utulivu uliopo nchini

MKUU WA POLISI (W) KARIAJ^QO,uXi
DARES SALAAM^a ya KA^Ak..

NAKALA
Mkuu wa Wilaya ya Ilala - Kwa taarifa tafadhali.
Kamanda wa Polisi (M) Ilala - Kwa taarifa tafadhali.

PIA SOMA:
- Jeshi la Polisi: Hatujakubali au kukataa maandamano, tutawapa majibu tarehe 23

- Kama Jeshi litafanya usafi tarehe 23-24, basi CHADEMA ifanye maandamano tarehe 25 wapite njia zikiwa safi

- CHADEMA yatangaza Maandamano Kupinga Miswada ya Sheria za Uchaguzi iliyowasilishwa Bungeni

- Mbowe: Makubaliano na Jeshi la Polisi yamefikiwa kuwa maandamano yataendelea kama yalivyopangwa

1706022122645.png

1706022201431.png
 

Attachments

  • CamScanner 01-23-2024 17.00.pdf
    483.5 KB · Views: 3
Ifahamike kwamba Polisi kikatiba hawana uwezo wa kuzuia maandamano ya kisiasa , hii si kazi yao , wanachoweza kufanya ni kama wana majukumu mengine watasema hawana askari wa kutosha

Screenshot_2024-01-23-17-54-29-1.png
Screenshot_2024-01-23-17-54-39-1.png


Tunawashukuru kwa kutupatia Ulinzi

CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE
 
Back
Top Bottom