chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,002
20,662
Mbombo ngafu.....jidanganye kwamba maandamano yamekubaliwa!!!!
======

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limekutana na Viongozi wa CHADEMA na kuwahoji kuhusu maandamano waliyopanga kuyafanya January 24,2024 na wamekubaliana kuwa watawapa majibu kimaandishi kesho January 23,2024 kama maandamano yawepo au yasiwepo na kusisitiza kuwa hadi kufikia sasa Polisi hawajakubali wala kukataa uwepo wa maandamano hayo.

Akiongea na TBC, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema “Baada ya kuwaona Katibu Mkuu wa CHADEMA akitangaza kwa kutumia Vyombo mbalimbali kwamba tarehe 24 lazima atafanya maandamano suala hili tumelifuatilia kwa ukaribu na leo January 22,2024 tulimuita Katibu Mkuu wa Chama hicho lakini akatuma ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu akiwa na wenzake na tumefanya nao mahojiano mbalimbali kwa kina kulingana na suala walilotangaza”

“Mimi nikiwa na Maofisa wa Kamisheni mbalimbali baada ya kuwasikiliza kwa kina na sisi kufuatilia kwa kina dhamira yao na kwasababu walituletea taarifa yao kimaandishi sisi hatujakubali au kukataa maandamano yao, majibu yao tumekubaliana kwamba tutawaapa kimaandishi kesho January 23,2024”

“Hatujaawambia maandamano yapo au hayapo kwasababu walituandikia barua kwenye Himaya zao na sisi majibu watayapata kwenye Himaya walizoandika barua hizo ambapo utakuwa ndio mwongozo wa nini kinafanyika huku tukizingatia masuala ya kiusalama na Maslahi ya Taifa kwa ujumla, tumezingatia suala la amani na majibu yao watayapata kesho”

========For English Audience Only==========
The Tanzania Police Special Zone in Dar es Salaam has reported that they held discussions with leaders from the CHADEMA party concerning the planned demonstrations scheduled for January 24, 2024. According to the Police Commander, Jumanne Muliro, both parties reached an agreement to provide written responses on January 23, 2024, indicating whether the demonstrations will proceed or not. Notably, the police emphasized that, as of now, they neither approved nor disapproved of the proposed protests.

Speaking to TBC, Commander Muliro stated, "After seeing the Secretary-General of CHADEMA announcing through various media outlets that on the 24th, they must hold demonstrations, we closely followed this matter. Today, January 22, 2024, we summoned the Secretary-General of the party, who sent a message through the Deputy Secretary-General accompanied by others, and we conducted extensive interviews with them regarding the matter they had announced."

"Alongside officers from various commissions, after listening attentively and thoroughly investigating their intentions, and because they submitted their information to us in writing, we have neither accepted nor rejected their request for demonstrations. We have agreed that we will provide them with written responses on January 23, 2024."

"We have not informed them whether the demonstrations will happen or not because they wrote to us in their respective jurisdictions, and they will receive responses in those jurisdictions where they submitted their letters. This will guide them on what is happening, considering security issues and the overall national interest. We have prioritized peace, and they will receive their responses tomorrow."​

Pia Soma; Mbowe: Makubaliano na Jeshi la Polisi yamefikiwa kuwa maandamano yataendelea kama yalivyopangwa

Pia Soma; CHADEMA yatangaza Maandamano Kupinga Miswada ya Sheria za Uchaguzi iliyowasilishwa Bungeni
 
Hawajachukua nchi, wamejaa uongo uongo
CHADEMA ni matapeli sana .ndio huwa wanawafanyia hivyo wafuasi wao maana walishaona kuwa hawawezi kuhoji kitu wala kuuliza kitu.

Wanawaona wafuasi wao kama manyumbu wasio na akili ya utambuzi wala utashi wa aina yoyote ile.ndio maana wanaweza wabadilishia gia popote pale na wasihoji chochote kile zaidi ya kushangilia kama mazuzu na mahayawani.
 
Mbowe kaona hana jipya kaamua kutunga uongo eti polisi wemekubali bila hata kuwaonesha nyumbu kibali. Sasa watalalamika kwamba wamenyang'anywa kibali. Kumbe hakukuwa hata na mtu wa kuandamana.
 
CHADEMA ni matapeli sana .ndio huwa wanawafanyia hivyo wafuasi wao maana walishaona kuwa hawawezi kuhoji kitu wala kuuliza kitu.
Ni aibu kubwa kwa mtu wa umri wa Mbowe, miaka 70 ya kuzaliwa, kusema uongo hadharani.

Just imagine kadanganya mangapi kwa wanachadema tangu aingie kwenye siasa.
 
Rais Samia anatafuta matatizo ya nini, mbona aliwaachia kwenye mikutano na hapakuwa na shida?
 
eshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limekutana na Viongozi wa CHADEMA na kuwahoji kuhusu maandamano waliyopanga kuyafanya January 24,2024 na wamekubaliana kuwa watawapa majibu kimaandishi kesho January 23,2024 kama maandamano yawepo au yasiwepo na kusisitiza kuwa hadi kufikia sasa Polisi hawajakubali wala kukataa uwepo wa maandamano hayo.

Akiongea na TBC, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema “Baada ya kuwaona Katibu Mkuu wa CHADEMA akitangaza kwa kutumia Vyombo mbalimbali kwamba tarehe 24 lazima atafanya maandamano suala hili tumelifuatilia kwa ukaribu na leo January 22,2024 tulimuita Katibu Mkuu wa Chama hicho lakini akatuma ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu akiwa na wenzake na tumefanya nao mahojiano mbalimbali kwa kina kulingana na suala walilotangaza”

“Mimi nikiwa na Maofisa wa Kamisheni mbalimbali baada ya kuwasikiliza kwa kina na sisi kufuatilia kwa kina dhamira yao na kwasababu walituletea taarifa yao kimaandishi sisi hatujakubali au kukataa maandamano yao, majibu yao tumekubaliana kwamba tutawaapa kimaandishi kesho January 23,2024”

“Hatujaawambia maandamano yapo au hayapo kwasababu walituandikia barua kwenye Himaya zao na sisi majibu watayapata kwenye Himaya walizoandika barua hizo ambapo utakuwa ndio mwongozo wa nini kinafanyika huku tukizingatia masuala ya kiusalama na Maslahi ya Taifa kwa ujumla, tumezingatia suala la amani na majibu yao watayapata kesho”
 
Makubaliano na polisi juu ya nini? Polisi wanapewa taarifa ya uwepo wa maandamano na njia yatakakopita ili Kama Kuna haja ya kutoka ulinzi wafanye hivyo na siyo vinginevyo. Someni katiba ya jmt mkiwa timamu. Polisi wasijipe umuhimu kuzidi mipaka iliyowekwa kisheria.
Na hii mbinu ya mitandaoni ni ya kupunguza idadi ya waandamanaji ili cdm ionekane Kama haiungwi mkono, hakuna kingine!
 
Back
Top Bottom