Kuruhusu maandamano ya amani ya Chadema, je Rais Samia ameshawachoka wahafidhina wa CCM wasiotaka mabadiliko nchini?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Kwa kweli leo tarehe 24, inabidi iingie katika historia kwa nchi hii, kwa kuwa ni kwa mara ya kwanza, tokea tupate uhuru kwa serikali yetu kuruhusu maandamano ya amani ya chama cha upinzani!

Ingawa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) na 18(2) inaruhusu maandamano hayo ya amani, lakini wakati wote vyama vya upinzani, vilipokuwa vikiomba vibali hivyo kwa Jeshi la Polisi, jibu limekuwa kukataliwa kwa visingizio vya kuwa maandamano hayo, yataleta uvunjifu wa amani nchini!

Lakini wakati wote chama tawala cha CCM, kimekuwa kikifanya maandamano hayo, bila vikwazo vyovyote!

Wakati wao CCM wamekuwa wakilyatumia majeshi yetu, ili kutuogopesha sisi vyama vya upinzani ili tusiandamane!

Hata katika maandamano haya yaliyofanyika leo, alijitokeza Mkuu wa Mkoa wa Dar, kueleza kuwa wanajeshi wapatao 8,000 na Polisi wapatao 5,000 watashiriki kwenye yaafi, siku hiyohiyo iliyopangwa kwa maandamano hayo ya amani, yaliyotangazwa na Mwenekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Nimetafakari kwa umakini na kujiuliza, hivi inawezekanaje hawahawa CCM, ambao kwa miaka yote, wamekuwa hawataki kabisa kuruhusu maandamano yoyote ya amani ya vyama vya upinzani, leo hii wakubali ",kiulaini" kabisa maandamano ya Chadema??

Ndiyo nikapata jibu kuwa huenda hata Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ameshawachoka hao wahafidhina wake, ndani ya CCM, wasiotaka mabadiliko yoyote ndani ya nchi na wakiamoni pia wao CCM, ndiyo wamepewa "hatimiliki" ya kutawala nchi hii, milele na milele!

Nikapata jibu kuwa, yeye Rais Samia, ambaye pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ametoa baraka, maandamano hayo yafanyike, kwa kuwa ameshawachoka wahafidhina ndani ya chama chake na wale wanaojiita chawa wa Mama!

Mungu ibariki Tanzania
 
Hoja kuu ingekua katiba mpya ningeelewa walau!!

Ugum wa maisha plus chaguzi plus ubadhirifu vingetibiwa vyema Kwa katiba mpya tu!!

Uchaguzi mkuu wa 2025 usifanyike bila katiba mpya!!

Nataka kuona viongozi wanaowajibika kivitendo Kwa wananchi na Sio kama punching bag ya kisiasa!!

Ngoja nione hii show inafuatiwa na Nini nyuma ya pazia!

Lazima Kuna move inahalalishwa kutokea!

Kama sio serikali mseto au nusu mkate tutajua mbeleni!!
 
Ingawa katika Katiba ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) na 18(2) inaruhusu maandamano hayo ya amani, lakini wakati wote vyama vya upinzani, vilipokuwa vikiomba vibali hivyo kwa Jeshi la Polisi, jibu limekuwa kukataliwa kwa visingizio vya kuwa maandamano hayo, yataleta uvunjifu wa amani nchini!

Nikapata jibu kuwa, yeye Rais Samia, ambaye pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ametoa baraka, maandamano hayo yafanyike!

Mungu ibariki Tanzania
Na mimi nakuunga mkono. Kuna kitu kimetokea. Siwezi kujua exactly ni kitu gani lakini kuna kitu. Kumbe yule bweha aliyesema kuna usafi alijikurupukia tu.
 
Na uzuri hakuna hata mende alieuwawa
Hakika..........

Tumeuthibitishia Ulimwengu kuwa sisi vyama vya upinzani ni watu wa amani kwelikweli!

Lakini kuukweli ni wao CCM ambao wataleta umwagijaji damu hapa nchini, kutokana na tabia yao ya kung'ang'ania madarakani na kutotaka kuyaachia madaraka hayo na hivyo kufanya hila nyingi, za kuhakikisha wanabaki madarakani "for hooks andi crooks"
 
Hoja kuu ingekua katiba mpya ningeelewa walau!!

Ugum wa maisha plus chaguzi plus ubadhirifu vingetibiwa vyema Kwa katiba mpya tu!!

Uchaguzi mkuu wa 2025 usifanyike bila katiba mpya!!

Nataka kuona viongozi wanaowajibika kivitendo Kwa wananchi na Sio kama punching bag ya kisiasa!!

Ngoja nione hii show inafuatiwa na Nini nyuma ya pazia!

Lazima Kuna move inahalalishwa kutokea!

Kama sio serikali mseto au nusu mkate tutajua mbeleni!!
Treni ni kubwa, huanza safari polepole. Leo umekuwa ni mwanzo mzuri. Nasema hivyo kwa sababu sikumbuki siku ambayo maandamano ya kuipinga serikali yaliwahi kufana hivi ukitilia maanani kuwa wananchi bado wamejaa woga. BTW haya maandamno yamejumuisha na katiba mpya.
 
Kwa kweli leo tarehe 24, inabidi iingie katika historia kwa nchi hii, kwa kuwa ni kwa mara ya kwanza, tokea tupate uhuru kwa serikali yetu kuruhusu maandamano ya amani ya chama cha upinzani!

Ingawa katika Katiba ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) na 18(2) inaruhusu maandamano hayo ya amani, lakini wakati wote vyama vya upinzani, vilipokuwa vikiomba vibali hivyo kwa Jeshi la Polisi, jibu limekuwa kukataliwa kwa visingizio vya kuwa maandamano hayo, yataleta uvunjifu wa amani nchini!

Lakini wakati wote chama tawala cha CCM, kimekuwa kikifanya maandamano hayo, bila vikwazo vyovyote!

Wakati wao CCM wamekuwa wakilyatumia majeshi yetu, ili kutuogopesha sisi vyama vya upinzani ili tusiandamane!

Hata katika maandamano haya yaliyofanyika leo, alijitokeza Mkuu wa Mkoa wa Dar, kueleza kuwa wanajeshi wapatao 8,000 na Polisi wapatao 5,000 watashiriki kwenye yaafi, siku hiyohiyo iliyopangwa kwa maandamano hayo ya amani, yaliyotangazwa na Mwenekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Nimetafakari kwa umakini na kujiuliza, hivi inawezekanaje hawahawa CCM, ambao kwa miaka yote, wamekuwa hawataki kabisa kuruhusu maandamano yoyote ya amani ya vyama vya upinzani, leo hii wakubali ",kiulaini" kabisa maandamano ya Chadema??

Ndiyo nikapata jibu kuwa huenda hata Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ameshawachoka hao wahafidhina wake, ndani ya CCM, wasiotaka mabadiliko yoyote ndani ya nchi na wakiamoni pia wao CCM, ndiyo wamepewa "hatimiliki" ya kutawala nchi hii, milele na milele!

Nikapata jibu kuwa, yeye Rais Samia, ambaye pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ametoa baraka, maandamano hayo yafanyike, kwa kuwa ameshawachoka wahafidhina ndani ya chama chake na wale wanaojiita chawa wa Mama!

Mungu ibariki Tanzania

..Chadema wamemtegeshea maandamano wakati ana safari kwenda nje.

..Samia angezuia maandamano na kuumiza watu angepata mapokezi mabaya huko nje kama kiongozi mkatili dhidi ya watu wake.
 
CCM ni baba wa siasa za nchi hii. Polepole mmeshaanza kumsifu mwenyekiti wa CCM.. Inapendeza. Njia nyeupe kwa mama 2025
 
Yule RC si wa kumtilia maanani.

Yule cheo kinachomfaa ni kuitwa chief of comedians hapa nchini!
Role ya huyo jamaa ni kubwa Dana kufanikisha maandamano haya !SEMA ni vile tuna one way traffic ya fikra!!

Zile kauli huwenda ndio jeshi likaingilia kati wananchi waruhusiwe kuandamana who knows!!

Hapa Kuna wanasiasa matajiri watakaangwa na maandamano haya nani anajua!!?

Kama namuona kikwete Kwa mbaali sijui kwanini!!!

Wito wa kwenda Vatican sasa utafana Kwa bi tozo kasafishiwa njia nadhani!!

Kuna picha inachezwa tutaiona hivinkaribuni!!

JE DKT SAMIAH NDIO ABDU JUMBE WA LEO!!?NILIWAHI ANDIKA NGOJA TUONE!!
 
Asante kwa matembezi ya hisani. Hakuna maandamano pale.
Njaa inakusumbua wewe chukua kitoweo hicho ukale na wanao
FB_IMG_1704538063091.jpg
 
Hoja kuu ingekua katiba mpya ningeelewa walau!!

Ugum wa maisha plus chaguzi plus ubadhirifu vingetibiwa vyema Kwa katiba mpya tu!!

Uchaguzi mkuu wa 2025 usifanyike bila katiba mpya!!

Nataka kuona viongozi wanaowajibika kivitendo Kwa wananchi na Sio kama punching bag ya kisiasa!!

Ngoja nione hii show inafuatiwa na Nini nyuma ya pazia!

Lazima Kuna move inahalalishwa kutokea!

Kama sio serikali mseto au nusu mkate tutajua mbeleni!!
Mkuu maandamano ya katiba mpya hakuna mwenye tatizo nayo, unaweza hata ww kuyaitisha, sisi tutakuwa tayari kukuunga mkono. Labda useme ww ni wale mnaotoa maneno matupu lakini hamna uthubutu.
 
Niliwahi sema ..Mama kizimkazi anaweza ondoka na kijiji aidha 2024 au 2030 kwamba anaruhusu katiba mpya anajikataa then kimbembe anawaachia Green kucheza uwanja wa ugenini.
 
..Chadema wamemtegeshea maandamano wakati ana safari kwenda nje.

..Samia angezuia maandamano na kuumiza watu angepata mapokezi mabaya huko nje kama kiongozi mkatili dhidi ya watu wake.
Hata angekuwepo hapa nchini, maandamano hayo yalikuwa yafanyike
 
Kwa kweli leo tarehe 24, inabidi iingie katika historia kwa nchi hii, kwa kuwa ni kwa mara ya kwanza, tokea tupate uhuru kwa serikali yetu kuruhusu maandamano ya amani ya chama cha upinzani!

Ingawa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) na 18(2) inaruhusu maandamano hayo ya amani, lakini wakati wote vyama vya upinzani, vilipokuwa vikiomba vibali hivyo kwa Jeshi la Polisi, jibu limekuwa kukataliwa kwa visingizio vya kuwa maandamano hayo, yataleta uvunjifu wa amani nchini!

Lakini wakati wote chama tawala cha CCM, kimekuwa kikifanya maandamano hayo, bila vikwazo vyovyote!

Wakati wao CCM wamekuwa wakilyatumia majeshi yetu, ili kutuogopesha sisi vyama vya upinzani ili tusiandamane!

Hata katika maandamano haya yaliyofanyika leo, alijitokeza Mkuu wa Mkoa wa Dar, kueleza kuwa wanajeshi wapatao 8,000 na Polisi wapatao 5,000 watashiriki kwenye yaafi, siku hiyohiyo iliyopangwa kwa maandamano hayo ya amani, yaliyotangazwa na Mwenekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Nimetafakari kwa umakini na kujiuliza, hivi inawezekanaje hawahawa CCM, ambao kwa miaka yote, wamekuwa hawataki kabisa kuruhusu maandamano yoyote ya amani ya vyama vya upinzani, leo hii wakubali ",kiulaini" kabisa maandamano ya Chadema??

Ndiyo nikapata jibu kuwa huenda hata Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ameshawachoka hao wahafidhina wake, ndani ya CCM, wasiotaka mabadiliko yoyote ndani ya nchi na wakiamoni pia wao CCM, ndiyo wamepewa "hatimiliki" ya kutawala nchi hii, milele na milele!

Nikapata jibu kuwa, yeye Rais Samia, ambaye pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu, ametoa baraka, maandamano hayo yafanyike, kwa kuwa ameshawachoka wahafidhina ndani ya chama chake na wale wanaojiita chawa wa Mama!

Mungu ibariki Tanzania

Anafuata sheria. Maandamano kisheria hayatakiwi kuzuiliwa na kuyazuia haina maana watu wanakupenda
 
Back
Top Bottom