Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,053
- 24,446
Kufuatia Chadema kutangaza kufanya maandamano ya amani Jan 24, 2023 jijini Dar es salaam , hadi kufikia hivi Sasa Polisi ambao ndio wanaopaswa kuhakikisha maandamano hayo yanafanyika Kwa amani hawajatoa tamko lolote la kuruhusu ama kupinga maandamano hayo, japo tayari Chadema ilishawapa taarifa Kwa maandishi Kama inavyotakiwa!
Ikumbukwe mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alitoa agizo Kwa jeshi la wananchi kuitumia siku hiyo ya maandamano kufanya usafi jijini Dar es salaam, jambo ambalo inajulikana wazi ni namna ya kujaribu kuyazuia maandamano hayo!
Za ndani ni kuwa kutokana na ukimya wa muda mrefu wa jeshi la polisi tokea wapokee taarifa ya kuandamana, ni kuwa siku mbili kabla ya tarehe ya maandamano jeshi la polisi litajitokeza na kuyapiga marufuku Kwa kutoka sababu ambazo mara nyingi zimekuwa zikizoeleka!
Wito Kwa jeshi la polisi!
Ni vyema hiyo azma ya kuyazuia hayo maandamano mkaifuta mara Moja, kwani hayo si maandamano ya vurugu wala kuvunja amani!
Hayo maandamano ni haki ya kikatiba Kwa wananchi wote, maana hakuna Sheria ambayo Chadema itakuwa imevunja Kwa kuyafanya!
Waacheni waandamane wakimaliza watarudi nyumbani Kwa amani, kile ambacho mamlaka inataka kukifanya hasa kwenye miswada ya Sheria inayopigiwa kelele kuipitisha ni rahisi tu!
Dawa ya mbwa anayebweka ni kumrushia pande la nyama!