I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,734
- 10,041
Kwa hiyo siku hizi hata uhuru wa matukio ya kidini tunaingiliwa?Naunga mkono hoja.
Sijui anahusiana nini na sherehe ya pasaka. Hapo hata umonitor tu wa malaika bado hajapata akipata itakuwaje?Hawa jamaa vipi? Kwa hiyo Jiwe ni wa maana kuliko kufufuka kwa Mwokozi wetu?
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Pasaka kama za kipindi cha nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Source: EATV news
Kwa hili serikali isipokuwa makini itajikuta inatengeneza chuki hadi kwa ule upande ambao ulikua unaikubali serikali na team jiweHamnazo hawa jeshi la police Yani tusisherekee kufufuka kwa nwokozi wetu kisa watu ambao hawako duniani?
Jeshi kuweni serious acheni kuingilia Imani zetu
Naona jeshi letu kama kawaida yao wametoa tamko katika siku yao aprili mosi.Agizo lolote linalotolewa katika hiki kipindi cha april fool ni la kulipuuza
Nchi hii tumeendekeza siasa mno. Kila kitu siasa hiyo ndio shida.Huu ni upuuzi mtu akishakufa na kuzikwa kuna nini cha ziada!
Ni hii katiba ya kipumbavu tuliyo nayo, hivi siku 21 watu wanaomboleza kipi labda cha maana? Tena ukute tunaye lazimishwa kumuomboleza kwa mujibu wa katiba alikuwa 'hopeless' enzi ya uhai wake.Nchi hii tumeendekeza siasa mno. Kila kitu siasa hiyo ndio shida.
Sidhani kama inahusu mambo ya kanisani, maana ibada ya pasaka ni ya kawaida haina shamrashamra. Alimaanisha starehe zenu huko mtaani...Kwa hiyo siku hizi hata uhuru wa matukio ya kidini tunaingiliwa?
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Pasaka kama za kipindi cha nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Source: EATV news