Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Habarini ndugu.

Sisi tumezaliwa wa5 ke4 me1 na wote tuna miaka 40+, baba yetu alifariki 89 aliacha mali chache ikiwemo nyumba iliyopo katikati ya mji, nyumba hiyo baba aliinunua ila aliandika jina la mama kwakuwa alishtakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi hivyo alifanya hivyo ili kuinusuru isitaifishwe, na kabla hajafariki aliandika mirathi msimamizi ni mama kuwa mali zote ni za watoto na zisiuzwe na alisema nyumba hiyo ni ya biashara hivyo chcht kitakachopatikana ni kwa ajili ya mama na wanae ila mama akiamua kuondoka kuolewa aache kila kitu aolewe.

Tumekuwa na baadhi tuna miji yetu hatutegemei chochote kutoka ktk mali zilizoachwa na mzee, na baadhi tunafanya biasharea ktk nyumba hiyo na zaidi tunampa mama kodi km wapangaji ili aweze kupata mahitaji yake pasipo kututegemea sisi. Na tuliamua hivyo ili aishi kwa utulivu sababu umri wake ni mkubwa sana hana uwezo wa kufanya biashara yoyote tena. Ghafla mama ametaka kuuza nyumba tukamzuia, akaenda mahakamani tukaitwa hakimu akasema file la mirathi limepotea na nakala aliyopewa mama pia imepotea kwahy anampa mama haki ya kuuza nyumba na mama anasema wazi kuwa hakimu ni rafiki yake hivyo atamsaidia.

Sababu za mama kutaka kuuza nyumba ni ushawishi toka kwa mdogo wake ambaye alishaiba hati wakati baba anaumwa ilikuwa bank alimshikia rafiki yake mdhamana kwa kesi ya mauaji na alishinda kesi mama mdogo akachuku hati akaichukulia mkopo nyumba ikauzwa na bank ila baadae ilirudishwa baada ya kustakiana na mama yetu. sasa mama mdogo amerudi anamshawishi mama auze wafanye biashara ilhali mama hana uwezo huo, Naombeni msaada je file linaweza kupotea mahajamani?,na tutafanyaje tupate haki mana mirathi pekee ndio inathibitisha nyumba ilinunuliwa na baba.
tafuteni wakili haraka kama mnaweza pm
 
Kuna vitu vya kuzingatia;

1. Hiyo nyumba lazima kuna siku itauzwa, aidha atauza mama au itauzwa baadaye na warithi wengine. Hali hii inaweza kuwa moja ya msukumo unaomfanya mama atake kuuza sasa hivi. Kwa anavyoijua familia yake, anaweza kuwa na malengo mazuri ya kuepuka migogoro siku zijazo.

2. Kwavile mama aliandikishwa kwenye hati, nyumba hiyo ni yake yote. Sio sehemu ya mirathi ya baba yenu.

3. Kitu cha msingi ni kuhakikisha hali ya kipato endelevu cha mama. Kwahiyo, mnapoongea naye mjikite zaidi kwenye kujadili aina ya biashara anayotaka kufanya, ili muweze kusikilizana. Epukeni kumzuia kuuza nyumba.

4. Iwapo ataamua kuuza bila kufuata ushauri wenu. Inabidi mshirikiane naye kutafuta mteja wa bei ya soko. Asiuze kwa hasara. Kwa sababu mpaka mwisho nyinyi mtawajibika kumtunza.

5. Iwapo mama hataki hata kusaidiwa kupata bei ya soko na anamsikiliza mama mdogo na wateja wa bei za kutupa, inabidi kufanya maamuzi magumu sana. Mama auze atakavyo, lakini matunzo yake yanakuwa juu yake na mdogo wake. Hapo maana yake nyinyi msichukue mgao wowote iwapo mnaamini nyumba haijauzwa kwa bei ya soko. Baada ya hapo, mama mnaenda kumsalimia lakini jukumu la kumtunza kifedha sio lenu tena.

6. Ushauri wangu, hiyo nakala ya mirathi wala msiitafute kwa sababu haiwezi kubadili matokeo. Kisheria, nyumba hiyo yote ni ya mama.

7. Kujibu swali lako, YES, nakala za kesi za zamani zinaweza kupotea. Tangu mwaka 1989 alipofariki mzee wenu, kumeshakuwa na mabadiliko mengi ya mifumo ya mahakama. Kimantiki, nakala zikipotea kesi inasikilizwa upya. Kwahiyo, mirathi hiyo inaweza kufunguliwa upya, lakini haitakuwa kuhusu nyumba tu, mitathi yote itafunguliwa upya. Kama mkitaka kuhusu nyumba peke yake, hiyo inakuwa ni kesi tofauti ya nyumba sio mirathi. Mirathi haiwezi kuwa ya mali moja tu.
 
Muacheni auze ila akimaliza pesa na maisha yakianza kumnyoosha msimsaidie, muacheni ateseke.
 
Kama wote wa4 mna miaka zaidi ya 40 mama atakua ana miaka zaidi ya 60. Sasa na uzee huo anahangaika nini? Mkamateni mama yenu mdogo na mumkemee
 
Okay pole Sana

Naomba umcheki Mwansheria akupe muongozo mzuri Kama upo DSM mtafute Jebra Kambole. Au pascall Mayalla wakupe ushauri wa kisheria .

Then nachona hapo mgepata mshauri mzuri wa Ku-Solve huo mgogoro bila kufika mahakamani


Mfano Kama kaka yenu yupo financially broke , mnaweza kumtafuta mkaongea nae friendly mkaona namna gani mnaweza kumpiga tafu pasipo kuuza Nyumba.

Ila usitumie Ubabe tumia akili sana sio nguvu .

Shida kubwa ya nyie wanawake mnapanic na mnatumia ubabe Sana

So ni vizuri utafute Mwnaume MTU mzima amabaye yupo smart aingilie kati mshauriane namna ya kumtulizamama yenu na huyo kaka yenu .


So Ukiona hizo njia za kidiplomasia zimefeli ndo utumie ubabe
Pascal Mayalla sio mwanasheria wa mahakamani, ni wapa JF tu.
 
Mmkuu uneandika kwa
M NDIO MANAA BAADHI YA MALIZANGU NILIWEKA JINA LA MAMA WOII

SIO HAWA
Herufi kubwa na bold kabisa,
Ila hata mimi nimejifunza sana, kwa hili kilicho changu naandika majina ya watoto sitaki mambo mengi. Siku nikilala watoto wataendeleza km wana akili.
 
Na hapo ndo panapokuaga pagumu, ndugu, jamaa, marafiki na jamii yote itawalaumu kwa kushindwa kumtunza mzazi wenu. Mkikomaa asiuze anawaambia msimpangie matumizi ya mali yake. Kazii kweli kweli 🤔
Kumuacha tu auze ila warning apewe mdogo wake ambaye wanashirikiana kuuza. Ikiwa nyumba itauzwa awajibike kumlea ndugu yake hata hela itapoisha.

Mi nyumba ya mzee huwa nawaza ibakie kwa wajukuu zake tu ambao ni watoto wangu na wa dada yangu japo wale wa dada yangu wako unyamwezini ila itakuwa sehemu ya kufikia wakija kutembea bongo. Kama watakuja kuiuza shauri yao ila iwe tu alama ya chimbuko lao.

So far, niko natengeneza mji wangu kwa sasa ambapo utakuwa urithi wa wanangu ila ni pembezoni kidogo mwa mji.
 
Kwa hesabu za haraka mama yenu ana miaka 58+ cz kama wote mna 40+18 ya usichana wa mama jumla inafika 58.

Huyu ni mzee anahitaji kushauriwa vyema.
Adui wa kwa sasa ni mama mdogo,Mama mdogo hana mume? Kaeni na mumewe au ndugu zake wengine.
Urithi wa babà usipotee.

Mkiweza mvunjeni mguu mama mdogo ajue anacheza na moto😂,mama yenu akili itamkaa sawa
 
Ni kweli tuna mali zetu lakini hii nyumba ni mali ya famili n sio nyumba tuh kuna na mshamba ambayo bab aliacha alitaka kuyauza kinyemel ila ndugu wa bba wakakataa.
Kisheria yote mawili yanawezekana, mama kufanikiwa kuuza nyumba yake na pia ninyi kufanikiwa kuzuia mama kuuza nyumba ya familia.

Nyumba kuwa ya mama ni kupitia mkataba wa mauziano au hati inayosoma jina lake.

Nyumba kuwa ya familia ni kupitia wosia na mirathi iliyofunguliwa ambapo mama alikubaliana nayo hapo awali akiwa anaomba usimamizi wa mirathi.

Sasa namna ya kupinga mauzo ni kukomaa kuwa nyumba ni ya familia. Mama hapaswi kubadili kauli sasa kuwa nyumba ni ya kwake binafsi ilhali alishakubali kuwa ni ya familia.

Nicheki kwa 0713368153 kwa msaada zaidi wa kisheria. Hiyo kesi yenu ipo mahakama ya mwanzo Kariakoo nini, maana ndio kuna michezo ya kupoteza mafaili?
 
Kama Mna maisha yenu na mna Mali zenu, muache huyo mama afanye anachohisi ni sahihi .

Sifikirii Kama ni sahihi kugombana kisa hizo takatakata ambazo ni useless.

We tengeneza Maisha yako yasimame Mali kitu gani
Tatizo huwa unatoa ushauri kihisia! Mama akiuza hiyo hela haitakaa hata mwezi na ataanza wasumbua watoto na kudai wamemtelekeza! Kisekibaha usisikilize ushauri wa watu kama hawa. Komaa isiuzwe
 
Mkuu, kama Mali ni ya baba, Je nani alimteua mama kuwa msimamizi wa mirathi?
Kama hakuna aliyemteua basi mama haruhusiwi kuuza hiyo nyumba, mpaka kikao cha ndugu kitakapompitisha yeye na mirathi hiyo kusajiliwa mahakamani.
Kama hati ya nyumba inamtaja yeye kama ndo mwenye kiwanja basi kuzuia mauzo ya hiyo nyumba utahitajika kuithibitishia mahakama kuwa mama Hana sound mind hivo maamuzi yake sio sahihi
"Unsound mind" tembeeni na hii gap mahakamani tafuteni ushahidi wa kitaalamu hadithi imeisha
 
Hapana. Wosia ambao ni mirathi iliweka bayana kwamba mama ni msimamizi tu wa mirathi lakini nyumba isiuzwe kwa namna yoyote zaidi ya kufanyia biashara pekee.

Mtu akiandika mirathi/wosia akiwa na akili zake timamu basi hakuna namna mtu mwingine anaweza ku challenge.
Apoo usiwe na shaka iyo aiwez kuuzwa bila kuwa na signature zenu wote yan watoto kuwa na aman tu
 
lakini nyumba isiuzwe kwa namna yoyote zaidi ya kufanyia biashara pekee.

Mtu akiandika mirathi/wosia akiwa na akili zake timamu basi hakuna namna mtu mwingine anaweza ku challenge.
Kisheria, huu wosia ulikuwa na makosa. Ungeweza kupingwa wakati ule wa kuomba usimamizi wa mirathi.
1. Wosia uligawa mali isiyo ya marehemu
2. Unazuia warithi kufurahia mali kikamilifu, huwezi mpa mtu kitu halafu umzuie asikiuze, unless aseme kuwa kulikuwa na trust fund au wakfu, ambapo katika maelezo haya vinaonekana havikuwepo.
 
Ana haki ya kuuza . Kama una itaka sana tafuta pesa kwa kiasi anachotaka kuuza nunua wewe. Hata baba yako angekuwa hai akaamua kuiuza msingemzuia kwani ni mali yake.
 
Back
Top Bottom