Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Pale alipohitaji kitu chochote tunekuwa tukimpa kwa wakati, achilia mbali kipato anachopata ktkt nyumba, na sehemu nyingine
Nyie mama yenu ukiachana na kodi je mlikuwa mnamtunza na kumuhudumia vizuri .??
 
Kwa hesabu za haraka mama yenu ana miaka 58+ cz kama wote mna 40+18 ya usichana wa mama jumla inafika 58.

Huyu ni mzee anahitaji kushauriwa vyema.
Adui wa kwa sasa ni mama mdogo,Mama mdogo hana mume? Kaeni na mumewe au ndugu zake wengine.
Urithi wa babà usipotee.

Mkiweza mvunjeni mguu mama mdogo ajue anacheza na moto😂,mama yenu akili itamkaa sawa
Dah hili la kumvunja mguu nimelipokea😂
Mama ana 74 mkuu
 
Kisheria yote mawili yanawezekana, mama kufanikiwa kuuza nyumba yake na pia ninyi kufanikiwa kuzuia mama kuuza nyumba ya familia.

Nyumba kuwa ya mama ni kupitia mkataba wa mauziano au hati inayosoma jina lake.

Nyumba kuwa ya familia ni kupitia wosia na mirathi iliyofunguliwa ambapo mama alikubaliana nayo hapo awali akiwa anaomba usimamizi wa mirathi.

Sasa namna ya kupinga mauzo ni kukomaa kuwa nyumba ni ya familia. Mama hapaswi kubadili kauli sasa kuwa nyumba ni ya kwake binafsi ilhali alishakubali kuwa ni ya familia.

Nicheki kwa 0713368153 kwa msaada zaidi wa kisheria. Hiyo kesi yenu ipo mahakama ya mwanzo Kariakoo nini, maana ndio kuna michezo ya kupoteza mafaili?
Asante mkuu, nitakuchek mapema sana
 
Habarini ndugu.

Sisi tumezaliwa wa5 ke4 me1 na wote tuna miaka 40+, baba yetu alifariki 89 aliacha mali chache ikiwemo nyumba iliyopo katikati ya mji, nyumba hiyo baba aliinunua ila aliandika jina la mama kwakuwa alishtakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi hivyo alifanya hivyo ili kuinusuru isitaifishwe, na kabla hajafariki aliandika mirathi msimamizi ni mama kuwa mali zote ni za watoto na zisiuzwe na alisema nyumba hiyo ni ya biashara hivyo chcht kitakachopatikana ni kwa ajili ya mama na wanae ila mama akiamua kuondoka kuolewa aache kila kitu aolewe.

Tumekuwa na baadhi tuna miji yetu hatutegemei chochote kutoka ktk mali zilizoachwa na mzee, na baadhi tunafanya biasharea ktk nyumba hiyo na zaidi tunampa mama kodi km wapangaji ili aweze kupata mahitaji yake pasipo kututegemea sisi. Na tuliamua hivyo ili aishi kwa utulivu sababu umri wake ni mkubwa sana hana uwezo wa kufanya biashara yoyote tena. Ghafla mama ametaka kuuza nyumba tukamzuia, akaenda mahakamani tukaitwa hakimu akasema file la mirathi limepotea na nakala aliyopewa mama pia imepotea kwahy anampa mama haki ya kuuza nyumba na mama anasema wazi kuwa hakimu ni rafiki yake hivyo atamsaidia.

Sababu za mama kutaka kuuza nyumba ni ushawishi toka kwa mdogo wake ambaye alishaiba hati wakati baba anaumwa ilikuwa bank alimshikia rafiki yake mdhamana kwa kesi ya mauaji na alishinda kesi mama mdogo akachuku hati akaichukulia mkopo nyumba ikauzwa na bank ila baadae ilirudishwa baada ya kustakiana na mama yetu. sasa mama mdogo amerudi anamshawishi mama auze wafanye biashara ilhali mama hana uwezo huo, Naombeni msaada je file linaweza kupotea mahajamani?,na tutafanyaje tupate haki mana mirathi pekee ndio inathibitisha nyumba ilinunuliwa na baba.
Nchi imeoza kila mtu amekuwa mhuni. Yaani mama watoto anataka kudhurumu watoto wake mwenyewe. Mahakama nazo zimekuwa sehemu ya kuhalalisha uhuni! Hivi tunaelekea wapi kama taifa?
 
Pale alipohitaji kitu chochote tunekuwa tukimpa kwa wakati, achilia mbali kipato anachopata ktkt nyumba, na sehemu nyingine
Shortcut mfanyieni umafia mama mdogo maana ni tapeli huwezi fanya biashara na kibibi wa miaka 74 kwanza anaweza kuwa mchawi
 
No, ndugu upande wa mama wapo imara sana kuharibu watoto kimalezi kwasababu sio ukoo wao .
Takwimu nyingi zinaonyesha, upande wa mama huwa kuna huruma zaidi, kuthibitisha hili, wazazi wako wote wafariki (baba & mama), utaona ni upande upi utakaojishughulisha zaidi.​
 
Hapana. Wosia ambao ni mirathi iliweka bayana kwamba mama ni msimamizi tu wa mirathi lakini nyumba isiuzwe kwa namna yoyote zaidi ya kufanyia biashara pekee.

Mtu akiandika mirathi/wosia akiwa na akili zake timamu basi hakuna namna mtu mwingine anaweza ku challenge.
Hati inasoma jina la mama yupo hai alafu Kuna wosio.
Hapo mahakama itasema mtoa wosia ametoa wosia kwenye mali isiyo yake au hata iseme chumo la pamoja sasa hapo automatically aliyebaki ndiye anakuwa mmiliki.
Kuzuia isiuzwe ni kipengere
Hapo nyie inabidi muiombe mahakama ilinde haki yenu ya mgao wa Mali ya chumo la baba yenu na yeye mama hapate chake mmalizane.
 
Nyumba ina jina la mama na ilinunuliwa mwaka 85 baba alikuwa na kesi mbaya sana ya uhujumu uchumi hivyo kwa maelezo ya mama mwenyewe siku za nyuma kabla hajabadilika alisema baba alimpa hela akanunua kwa jina lake ili asifilisiwe na serikali. Ila kwenye mirathi ya baba imetajwa hiyo nyumba ila mirathi ndio imefichwa
Kisheria hiyo nyumba ni ya mama yenu kwani hati zinasoma jina lake

Hata kama kuna usia wa baba yenu unaosema hiyo nyumba ni ya watoto usia huo unakua BATILI kwasababu kisheria nyumba sio ya marehemu ni ya Mama…… kinacho tambulisha mmiliki wa nyumba ni HATI

Hapo mnatakiwa kama watoto mkae kitako na mama yenu muyajenge kiungwana tu kwamba kama ni LAZIMA kuiuza basi mumsaidie kupata mteja wa bei nzuri na awaangali mgao kama watoto wake

Njia pekee ya kuzuia labda awe na matatizo ya kiakili yanayothibitika kwamba hana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kuna watu wanatumia advantage hiyo kutaka kunufaika wao

Lakini kama ana akili timamu hataka kama kuna mtu anamuhadaa hakuna namna mtamtaweza kufanya kwani ni mali yake kihalali

Inaonekana mnamaugonvi sana kwenye familia yenu…. Yajengeni kwanza
 
watu wengi hawajui msimamizi wa mirathi sio lazima awe mrithi. Kama marehemu baba yako aliacha usia ni bora ufatwe usia na hoja karatasi au jalada vilipotea siyo sababu ya yeye kutaka kuuza nyumba. kuna watu wanasema hiyo mali ni ya mama yenu lakini wanasahau nyumba ilijengwa na baba na kwenye mirathi pamoja na mali alizoacha marehemu ni pamoja na watoto.
kama nyumba ikiuzwa na mama yenu akatapanya pesa mzigo wa kumtunza utabaki kwenu.
tafuteni wakili mzuri pia huyo hakimu mlipotini kwenye tume ya mahakama wana kamati zao za kimaadili na hizo nyaraka fatilieni zimepotelea wapi kama mahakamani, kama mahakamani fatilieni mahakama za juu.
usisikilize ushauri wa wanasheria wa mtaani.
 
Kwanza kabla ya kuzuia kuuza nyumba mnapaswa mumuulize vitu 3 muhimu sn.
-kwann anauza nyumba.
- mgao wenu kama watoto amepangaje.
-baada ya kuuza na kuwapa mgao wenu kama watoto je yeye ana mipango gn na pesa zilizobaki.


Kama hana majibu yanayoeleweka nendeni mahakamani mkapinge kuuzwa Kwa nyumba..
Kama nyumba ilinunuliwa na baba yenu na maandishi yapo maana yake nyumba ni ya family hawezi akauza bila kuwashirikisha,au kuwapa mgao wenu kama watoto.
Mkuu sheria ya mirathi unaielewa vizuri?

'Mgao' wa watoto hao siuoni hapo maana wamezidi umri wa tegemezi na siyo warithi wa moja kwa moja wa mali hiyo.

Mama yao huyo angelifariki tungejadili vinginevyo.

Lakini kwa sasa mmiliki halali ni mama yao.
 
Mkuu sheria ya mirathi unaielewa vizuri?

'Mgao' wa watoto hao siuoni hapo maana wamezidi umri wa tegemezi na siyo warithi wa moja kwa moja wa mali hiyo.

Mama yao huyo angelifariki tungejadili vinginevyo.

Lakini kwa sasa mmiliki halali ni mama yao.
Mke hana urthi kwa mumewe,wanaorithi ni watoto tu


Mke ana asilimia fulani ya mali kama wamechuma wote na sio kurithi mali.
Mtoto anarithi mali ya baba au mama yake automatically.
Umeshajiuliza kwann mke akifiwa na mume na bado akawa anaishi nyumba ya mumewe.
Kama akitaka kuolewa tena na mwanaume mwingine ni marufuku kuishi mle ndani ya nyumba ya marehemu mumewe? especially kama akiwa na watoto wa marehemu?
 
Mke hana urthi kwa mumewe,wanaorithi ni watoto tu


Mke ana asilimia fulani ya mali kama wamechuma wote na sio kurithi mali.
Mtoto anarithi mali ya baba au mama yake automatically.
Umeshajiuliza kwann mke akifiwa na mume na bado akawa anaishi nyumba ya mumewe.
Kama akitaka kuolewa tena na mwanaume mwingine ni marufuku kuishi mle ndani ya nyumba ya marehemu mumewe? especially kama akiwa na watoto wa marehemu?
Inamaana mume akifa mke wa ndoa hana mgao katika mirathi ya mume waliyechuma hiyo mali pamoja?

Kama hana haki, kwa nini ikitokea wanandoa kupeana talaka, mke agawiwe mali walochuma na mumewe kisheria na si watoto?

Anaway hili sijakubaliana na wewe ngoja nilitreave makabrasha!
 
Back
Top Bottom