Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Kwanini mnalazimisha nyumba isiuzwe?
Si mshakua watu wazima nyie?
Kwanini msipambane na wenzi wenu nao wawaachie urithi?

Hivi mama yenu mnamsumbua hivyo, vipi akifariki mkabaki peke yenu si mtachinjana?
Hakuna mtu yoyote aliyemsumbua anakaa kwake anakula kodi za nyumba 4 peke yake tatu za vijijini moja ya katikati ya mji zote zipo kwenye mirathi kilichotushtua ni kuita mdogo wake na kutaka kuuza nyumba ambayo kwanza imeandikwa kwenye mirathi, kaleta mpaka wateja bahati nzuri walinikuta nikawazuia kwa kuwaonyesha fomu ya mahakama inayoonyesha anayewauzia ni msimamizi wa mirathi siyo mmiliki wa mali. pili akishauza atatapeliwa mana sio mara ya kwanza kutapeliwa na huyo mdogo wake. Mara ya kwanza wakati baba akiwa hai alimshikia rafiki yake mdhamana kwa hati ya nyumba kwa bahati nzuri yule mtu alishinda kesi ila baba alikuwa anaugua sana mama akamtuma mdogo wake kufatilia hati iliyokuwa banka ma mdogo akafoji saini akachukulia mkopo baada ya baba kufariki miaka kama mi5 mbele nyumba ikauzwa na ma mdogo akamkana mama jlkama sio Mungu kusaidia nyumba ilikuwa iende moja kwa moja. Kilichosaidia ni barua za mama mdogo alizokuwa anamuandikia mama kumuomba avumilie atalioa deni huo ndio ushahidi pekee mama alioutumia mahakamani kushinda kesi na nyumba ikarudishwa. Tatu hata hivyo mali ya familia ikiuzwa ni vyema kukaa kikao na watoto ili iuzwe ili keaho kusiwe na manunguniko. Hata yeye ana mali nyingi tuu amerithi kwa wazazi wake mashamba mahekari kwa hekari hakuna aliyetaka kuziuza kwa hila. Najaribu kueleza ili mnielewe.
 
baba aliinunua ila aliandika jina la mama kwakuwa alishtakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi hivyo alifanya hivyo ili kuinusuru isitaifishwe, na kabla hajafariki aliandika mirathi msimamizi ni mama kuwa mali zote ni za watoto na zisiuzwe na alisema nyumba hiyo ni ya biashara hivyo chcht kitakachopatikana ni kwa ajili ya mama na wanae ila mama akiamua kuondoka kuolewa aache kila kitu aolewe.
Kipindi baba anayasema haya wewe ulikua na umri gani?
 
Tujikumbushe mali ni za baba na mama maana wa ndio waliozitafuta na sio za watoto.
Kwenye mali wengi wanafikiri ni za mwanaume tu na je kama hiyo nyumba alinunua mama yenu ndio ikaandikwa jina lake hamuoni mtakuwa mnamdhulumu mama yenu??
 
Ingekua mimi nisie baba wa hovyo,nisingeweza kuandika mirathi kwa mke,watoto watakua warithi ila mke asimamie ama kijana mkubwa
Hapo hamna chenu tena,mzee alishakosea kuandika mirathi kwa mpita njia
Hakuandika mirathi kwa mama aliandikia watoto ila msimamizi ni mama.
 
Sawa ila au bas
Tujikumbushe mali ni za baba na mama maana wa ndio waliozitafuta na sio za watoto.
Kwenye mali wengi wanafikiri ni za mwanaume tu na je kama hiyo nyumba alinunua mama yenu ndio ikaandikwa jina lake hamuoni mtakuwa mnamdhulumu mama yenu??
 
Watoto mpo sahihi sijajua kwa nini watu hawalioni hili.

Hiyo ndiyo asset inayosaidia huyo mama kujikimu,akiuza anaenda kuwa tegemezi kwa wanae.

Biashara kwa wazee tunaona wastaafu wanavyoishia kunufaisha wasimamizi na kufa kwa stress.

Japo uhusiano na mama yenu unatia shaka labda kwa vile tumepata taarifa ya upande mmoja.
 
Muacheni auze si mali yake walitafuta na mumewe..!!
Na nyie jitahidini wanaume zenu wawape urithi.
Huo kutafuta na mmewe futa sema iliotafutwa na mmewe ,nyie wnwake wajanjajanja sana mali atafute mwanaume useme ni zenu apo apn asee
 
Habarini ndugu.

Sisi tumezaliwa wa5 ke4 me1 na wote tuna miaka 40+, baba yetu alifariki 89 aliacha mali chache ikiwemo nyumba iliyopo katikati ya mji, nyumba hiyo baba aliinunua ila aliandika jina la mama kwakuwa alishtakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi hivyo alifanya hivyo ili kuinusuru isitaifishwe, na kabla hajafariki aliandika mirathi msimamizi ni mama kuwa mali zote ni za watoto na zisiuzwe na alisema nyumba hiyo ni ya biashara hivyo chcht kitakachopatikana ni kwa ajili ya mama na wanae ila mama akiamua kuondoka kuolewa aache kila kitu aolewe.

Tumekuwa na baadhi tuna miji yetu hatutegemei chochote kutoka ktk mali zilizoachwa na mzee, na baadhi tunafanya biasharea ktk nyumba hiyo na zaidi tunampa mama kodi km wapangaji ili aweze kupata mahitaji yake pasipo kututegemea sisi. Na tuliamua hivyo ili aishi kwa utulivu sababu umri wake ni mkubwa sana hana uwezo wa kufanya biashara yoyote tena. Ghafla mama ametaka kuuza nyumba tukamzuia, akaenda mahakamani tukaitwa hakimu akasema file la mirathi limepotea na nakala aliyopewa mama pia imepotea kwahy anampa mama haki ya kuuza nyumba na mama anasema wazi kuwa hakimu ni rafiki yake hivyo atamsaidia.

Sababu za mama kutaka kuuza nyumba ni ushawishi toka kwa mdogo wake ambaye alishaiba hati wakati baba anaumwa ilikuwa bank alimshikia rafiki yake mdhamana kwa kesi ya mauaji na alishinda kesi mama mdogo akachuku hati akaichukulia mkopo nyumba ikauzwa na bank ila baadae ilirudishwa baada ya kustakiana na mama yetu. sasa mama mdogo amerudi anamshawishi mama auze wafanye biashara ilhali mama hana uwezo huo, Naombeni msaada je file linaweza kupotea mahajamani?,na tutafanyaje tupate haki mana mirathi pekee ndio inathibitisha nyumba ilinunuliwa na baba.
Kwanza poleni kwa changamoto za mirathi, kusema kweli issues za mirathi ni pasua kichwa!.
  1. Kitu cha kwanza cha kuelewa ni hiyo nyumba ni ya mama yenu baada ya kuachiwa na mume wake ambaye ni baba yenu, na baba aliacha wosia isiuzwe ili iwafaidie watoto, suppose angeitwa ikiwa under 18 years. Sasa maadam nyote ni over 18 na mna miji yenu, mnatakiwa kumsaidia mama yenu aishi vizuri siku zake zilizobakia, akiitwa, then ndipo inaingia kwenye miliki ya nyinyi watoto.
  2. Ili nyumba isiuzwe na mama, Baba alipaswa kuanzisha trust , ambayo inge i manage nyumba na kumtunza mama na watoto. Kwa vile nyumba iko mikononi mwa mama, akiona kipato cha kodi anachopata ni kidogo mno kum sustain comfortably, anapaswa ashauriane na nyinyi mkubali kuuza nyumba na kufanya investment nyingine itakayo ms sustain mama yenu kuishi maisha comfortable
  3. Document muhimu sana ni document ya kikao cha familia kuhusu msimamizi wa mirathi baada ya kifo cha baba yenu, kila mtoto alipaswa apate copy, ambapo ndio imefungulia mirathi.
  4. Mirathi ikiisha amuliwa na mahakama, sio jukumu la mahakama kuwatunzia, ni jukumu lenu kutunza uamuzi wa mirathi, ila mahakama inatunza nakala, tena siku hizi ni nakala mtandao, wewe tunza tuu kumbukumbu ya case number na tarehe ya uamuzi, hiyo mirathi inaibuliwa online!.
  5. Mnatakiwa msimzuei mama kuuza nyumba, ila mnawajibika kumsaidia asije kuuza kwa kutapeliwa halafu agageuka mzigo kwenu!.
  6. Mali ni na mama na mume wake, nyinyi watoto kila mtu atafute zake na jukumu la kumtunza mama, yenu liko pale pale!.
P
 
M NDIO MANAA BAADHI YA MALIZANGU NILIWEKA JINA LA MAMA WOII

SIO HAWA
 
Asante sana

Ndugu paskal,
Naomba kujua kama baba aliacha wosia kwa kutaja mali zote ikiwemo na nyumba hiyo kuwaa ni mali za watoto na zisiuzwe na kusema mama ni msimamizi tuu watoto waakikuwa wapewe je mama anahaki ya kuuza hiyo nyumba?? Mirayhi iliandikwa naa kufikishwa mahakamani na ni kweeli ghata mimi binafsi niliwah kuulizia hy mirayhi nikaonyeshwa kwenye kumbukumbu za mafile kuwaa ipo na. Sasa kama mali za baba ni za mama kwanini kjlikuwa na mirathi aliyoandika baba na kututaja watoto wake kama wamiliki na mama msimamizi?? Tena aliandik ikiwa mama atataka kuolewa aolewe ila aache mali zote kamazilivyo. Samahani lakininaomba unisaidie kunielewesha
 
Kwanza kabla ya kuzuia kuuza nyumba mnapaswa mumuulize vitu 3 muhuni sn.
-kwann anauza nyumba.
- mgao wenu kama watoto amepangaje.
-baada ya kuuza na kuwapa mgao wenu kama watoto je yeye ana mipango gn na pesa zilizobaki.

Kama hana majibu yanayoeleweka nendeni mahakamani mkapinge kuuzwa Kwa nyumba..
Kama nyumba ilinunuliwa na baba yenu na maandishi yapo maana yake nyumba ni ya family hawezi akauza bila kuwashirikisha,au kuwapa mgao wenu kama watoto.
Hapa nimeelewa
 
Kwanini mnalazimisha nyumba isiuzwe?
Si mshakua watu wazima nyie?
Kwanini msipambane na wenzi wenu nao wawaachie urithi?

Hivi mama yenu mnamsumbua hivyo, vipi akifariki mkabaki peke yenu si mtachinjana?
Kwahiyo trump hakuachiwa uruthi Wacha wenge mkuu
 
Yaani umeolewa unataka mali ya mama yako alioachiwa na mme wake na akawalea yeye kiwa single mother hadi mkaolewa na wewe uza nyumba ya mmeo dadeki kitoto vya Kinondoni kijinga sana

USSR
Jamani eeeeh! Huyu dada asisakamwe! Amesema mama anataka kuuza nyumba kutokana na ushawishi wa mdogo wake ambaye ni mamake mdogo na mleta mada. Huyo mbibi anataka kudhulumiwa nyumba na huyo mdogo wake. Hapa ndipo sheria mkononi huwa inafanya kazi! Naweza kukuelekeza kwa wataalam wa kupiga mapanga huyu mdogo mtu anyofolewe bichwa!
 
Asante sana kwa kunielewa.
 
Back
Top Bottom