Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Mimi sijata

Ka mali wala sijawah kuenda mahakamani nimeitwa zaidi ya mara 3 sikuona sbb ya kwenda, kilichonifanya niombe msada ni hali ya mama ya afya ya akili na mwili, na ni baada ya kutaka kuuza nyumba ya zaid ya mil 250 kwa mil 80, na umri wake ni mkubwa hawezi kufanya biashara wala chcht nyumba hy ndio msaada kwake, na mshauri wake mkuu ni mdogo wake wa kike ambaye alishawah kufoji signatir akachukua mkopo wa nyumba hy hy ikaja kuuzwa na bank. Lengo sio kumdhulumu wala kugombea msli ila ni kuhakikishs hakuna utapeli unafanyika dhidi yake na familia kwa ujumla mana mirathi yeye ni msimamizi na mmiliki pia.
Nafikiri kwa umri wake na historia ya mdogo wake, na inaonekana urithi mlipewa wote na mama yenu, nafikiri mna haki na judge yeyote anayetumia akili atawapa haki, wazee wanaibiwa sana maana uwezo wa akili umepungua kiasi, piganeni
 
Habarini ndugu.

Sisi tumezaliwa wa5 ke4 me1 na wote tuna miaka 40+, baba yetu alifariki 89 aliacha mali chache ikiwemo nyumba iliyopo katikati ya mji, nyumba hiyo baba aliinunua ila aliandika jina la mama kwakuwa alishtakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi hivyo alifanya hivyo ili kuinusuru isitaifishwe, na kabla hajafariki aliandika mirathi msimamizi ni mama kuwa mali zote ni za watoto na zisiuzwe na alisema nyumba hiyo ni ya biashara hivyo chcht kitakachopatikana ni kwa ajili ya mama na wanae ila mama akiamua kuondoka kuolewa aache kila kitu aolewe.

Tumekuwa na baadhi tuna miji yetu hatutegemei chochote kutoka ktk mali zilizoachwa na mzee, na baadhi tunafanya biasharea ktk nyumba hiyo na zaidi tunampa mama kodi km wapangaji ili aweze kupata mahitaji yake pasipo kututegemea sisi. Na tuliamua hivyo ili aishi kwa utulivu sababu umri wake ni mkubwa sana hana uwezo wa kufanya biashara yoyote tena. Ghafla mama ametaka kuuza nyumba tukamzuia, akaenda mahakamani tukaitwa hakimu akasema file la mirathi limepotea na nakala aliyopewa mama pia imepotea kwahy anampa mama haki ya kuuza nyumba na mama anasema wazi kuwa hakimu ni rafiki yake hivyo atamsaidia.

Sababu za mama kutaka kuuza nyumba ni ushawishi toka kwa mdogo wake ambaye alishaiba hati wakati baba anaumwa ilikuwa bank alimshikia rafiki yake mdhamana kwa kesi ya mauaji na alishinda kesi mama mdogo akachuku hati akaichukulia mkopo nyumba ikauzwa na bank ila baadae ilirudishwa baada ya kustakiana na mama yetu. sasa mama mdogo amerudi anamshawishi mama auze wafanye biashara ilhali mama hana uwezo huo, Naombeni msaada je file linaweza kupotea mahajamani?,na tutafanyaje tupate haki mana mirathi pekee ndio inathibitisha nyumba ilinunuliwa na baba.
Mtoa mada tupatie update ya yalioendelea nyumba imeuzwa au?
 
Inamaana mume akifa mke wa ndoa hana mgao katika mirathi ya mume waliyechuma hiyo mali pamoja?

Kama hana haki, kwa nini ikitokea wanandoa kupeana talaka, mke agawiwe mali walochuma na mumewe kisheria na si watoto?

Anaway hili sijakubaliana na wewe ngoja nilitreave makabrasha!
Elewa neno kurithi na kupata mgao,
Hivi ni vitu 2 tofauti.
Mke ana mgao lakini sio urithi anayerithi ni mtoto.

Urithi unapata kwa wazazi wako na sio kwa mume.
 
Muacheni auze hela ikiisha hamna kumpokelea simu kmmk
 
Habarini ndugu.

Sisi tumezaliwa wa5 ke4 me1 na wote tuna miaka 40+, baba yetu alifariki 89 aliacha mali chache ikiwemo nyumba iliyopo katikati ya mji, nyumba hiyo baba aliinunua ila aliandika jina la mama kwakuwa alishtakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi hivyo alifanya hivyo ili kuinusuru isitaifishwe, na kabla hajafariki aliandika mirathi msimamizi ni mama kuwa mali zote ni za watoto na zisiuzwe na alisema nyumba hiyo ni ya biashara hivyo chcht kitakachopatikana ni kwa ajili ya mama na wanae ila mama akiamua kuondoka kuolewa aache kila kitu aolewe.

Tumekuwa na baadhi tuna miji yetu hatutegemei chochote kutoka ktk mali zilizoachwa na mzee, na baadhi tunafanya biasharea ktk nyumba hiyo na zaidi tunampa mama kodi km wapangaji ili aweze kupata mahitaji yake pasipo kututegemea sisi. Na tuliamua hivyo ili aishi kwa utulivu sababu umri wake ni mkubwa sana hana uwezo wa kufanya biashara yoyote tena.

Ghafla mama ametaka kuuza nyumba tukamzuia, akaenda mahakamani tukaitwa hakimu akasema file la mirathi limepotea na nakala aliyopewa mama pia imepotea kwahy anampa mama haki ya kuuza nyumba na mama anasema wazi kuwa hakimu ni rafiki yake hivyo atamsaidia.

Sababu za mama kutaka kuuza nyumba ni ushawishi toka kwa mdogo wake ambaye alishaiba hati wakati baba anaumwa; ilikuwa bank alimshikia rafiki yake mdhamana kwa kesi ya mauaji na alishinda kesi mama mdogo akachukua hati akaichukulia mkopo nyumba ikauzwa na bank ila baadae ilirudishwa baada ya kushtakiana na mama yetu.

Sasa mama mdogo amerudi anamshawishi mama auze wafanye biashara ilhali mama hana uwezo huo.

Naombeni msaada je file linaweza kupotea mahakamani? Na tutafanyaje tupate haki? Maana mirathi pekee ndio inathibitisha nyumba ilinunuliwa na baba.
Nenda kalipie consultation fee Kwa wakili upate ushaur wa kisheria ,,huo ushaur watu walisomea kabsa class
 
Mirathi kwa dini ya kiislamu inatatua hili tatizo sekunde
 
Back
Top Bottom