Mama amezeeka anataka kwenda kuwekeza wapi ktk umri huo, kama siyo ushauri mbaya wa mama yenu wadogo.
Nyumba katikati ya mjini ni mali kubwa na nyumba na kiwanja chake ni asset / mtaji endelevu inayoongezeka thamani na kutoa fursa kwa watoto na wajukuu kuingia katika mikataba minono na matajiri au mabenki huku mkiingiza kipato endelevu, makazi ghorofani ya kukodisha, kuishi n.k ikiwa mtaingia mikataba sahihi.
Mama kuuza nyumba mjini kati kisha kwenda kujenga majoring ktk uzee huo ni kosa kubwa dhidi ya legacy ya mtaji aliyowawekea nyie na mama yenu na watoto wenu.
Mstueni mama yenu, endeleeni kumtunza katika umri wake mkubwa hadi mwisho wa maisha yake ili asisikilize maneno ya nduguze ambao ni wazee pia kiumri.
Tutalalamika kuhusu familia za kina Dewji, Gulamali, Mengi n.k zenye utajiri. Utajiri huongezeka pale mali kama hizo zinapotunzwa zirithishwe kwa watoto ili legacy iendelee ya utajiri endelevu.
Kwanini siku zote waswahili haturithishi vizazi, tunadai kila kizazi kianze moja ktk kutafuta utajiri ?