Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Naomba Msaada: Nyumba yetu inakaribia kuuzwa

Kisheria yote mawili yanawezekana, mama kufanikiwa kuuza nyumba yake na pia ninyi kufanikiwa kuzuia mama kuuza nyumba ya familia.

Nyumba kuwa ya mama ni kupitia mkataba wa mauziano au hati inayosoma jina lake.

Nyumba kuwa ya familia ni kupitia wosia na mirathi iliyofunguliwa ambapo mama alikubaliana nayo hapo awali akiwa anaomba usimamizi wa mirathi.

Sasa namna ya kupinga mauzo ni kukomaa kuwa nyumba ni ya familia. Mama hapaswi kubadili kauli sasa kuwa nyumba ni ya kwake binafsi ilhali alishakubali kuwa ni ya familia.

Nicheki kwa 0713368153 kwa msaada zaidi wa kisheria. Hiyo kesi yenu ipo mahakama ya mwanzo Kariakoo nini, maana ndio kuna michezo ya kupoteza mafaili?
Mkuu unawajua kumbee
Wanachofanyaga n kutafuta laana uwezi poteza faili kirahisi..

Ila sikuhixi bado wanadili na failing pekee
 
Kuna watu vichwa maji humu mkuu acha kabisa ila ndivyo Waafrika walivyo...

Inasikitisha sana kuona jukwaa au jf imevamiwa na watu waliokosa weledi kwenye mambo ya msingi na badala yake wanakimbilia kuzodoa....na hata kutukana........

Mimi najaribu kumuelewa mtoa mada katika angle nyingine kabisa!!

Jambo la wazi ambalo wengi hamlielewi ni kama vile huyo mama anakaribia kutapeliwa kwa mlango wa nyuma!!

Historia ya awali ya huyo mama mdogo ni kuwa alishawahi kufanya dhuruma lakini mahakama ikanusuru nyumba!!!

Achaneni na wajinga wajinga wa humu na nadhani ungejaribu kuwaona wataalamu wa sheria wakupe mwanga!!!!

Huyo mama kama akitapeliwa ni wazi kuwa atarudi kuwa mzigo wenu nyinyi watoto!!
 
Umetoa muongozo mzuri, mleta mada afuate ushauri huu kwa usaidizi...

1. Umiliki wa Nyumba

  • Ingawa jina lilisajiliwa kwa mama yenu kwa sababu ya mazingira ya kihistoria (kesi ya uhujumu uchumi), mali hii kiuhalisia ni mali ya baba yenu kwa kuwa ndiye aliyeinunua, na ushahidi ni mirathi aliyoiandika akabainisha mali ni ya watoto na si ya mama binafsi.
  • Kwa mujibu wa Sheria ya Mirathi (Probate and Administration of Estates Act, Cap 352 R.E 2002 – Tanzania), mali yoyote aliyokuwa akimiliki marehemu inapaswa kugawanywa kulingana na mirathi au kama hakuna, kwa urithi wa kisheria.

2. Kuhusu Mirathi na Faili la Mahakama

  • Faili la mirathi haliwezi kupotezwa kiholela, kwa sababu nyaraka za mirathi ni rekodi rasmi za Mahakama na huhifadhiwa kwenye Registry.
  • Ikiwa kweli jalada limepotea, unaweza kuomba upya Mahakama kutoa nakala ya uamuzi na hati za mirathi kupitia “certified copies” kwani kila jalada lina namba (probate file number).
  • Ikiwa mama alipewa nakala yake na inasemekana imepotea, bado Mahakama inabaki na wajibu wa kuhifadhi nakala. Kama hakuna, basi jambo hilo linaweza kufikishwa kwa Mahakama Kuu – Kitengo cha Ardhi au Mirathi kwa malalamiko ya upotevu wa faili.

3. Haki ya Mama Kuamua Kuuza

  • Kwa mujibu wa wasia, mama hakuwa mmiliki halisi bali msimamizi wa mali kwa ajili ya watoto.
  • Kwa hiyo, mama hana mamlaka ya kuuza mali kinyume na masharti ya mirathi (kwa mfano wasia kusema "mali zisiuzwe").
  • Kama atajaribu kuuza, hiyo ni kuzidisha mamlaka (breach of trust) na watoto wana haki ya kuzuia kwa kufungua shauri la kuzuia uuzaji (injunction).

4. Hatari ya Ushawishi na Udanganyifu

  • Ushawishi kutoka kwa mdogo wake unaweza kupelekea undue influence – jambo ambalo Mahakama inaweza kuzuia endapo nyinyi mtawasilisha ushahidi.
  • Historia ya hati kuchukuliwa benki tayari ni dalili ya hatari, hivyo mnapaswa kuchukua hatua haraka kisheria.

5. Mambo ya Kufanya Hivi Sasa

  1. Nendeni Mahakama (ambapo mirathi ilifunguliwa) muombe namba ya jalada na nakala ya hukumu / hati ya mirathi (probate or letters of administration).
  2. Fungueni shauri jipya kama jalada limepotea, mkieleza kuwa kuna jaribio la mama kuhamisha mali kinyume na mirathi.
  3. Ombeni amri ya Mahakama ya kuzuia uuzaji (injunction) mpaka suala la umiliki na mirathi liamuliwe upya.
  4. Kama hamna uaminifu na hakimu wa eneo, pelekeni suala Mahakama Kuu – Probate and Administration Registry ili lisimamiwe juu.
  5. Hifadhi ushahidi wote (nakala za wasia, ushahidi kuwa baba ndiye alinunua nyumba, na ushahidi wa ulaghai wa hati huko nyuma).
 
Nie watoto inaonekana hamna maelewano na mama. Hata hivo, acha kutegemea mali ya urithi, huwa inaleta migogoro, laana na vifo visivotarajiwa. Mwacheni mama afanye anavotaka, tofauti na hapo tegemea ugonvi na mama
Hapana urithi ni haki sio hisani
 
Sasa hivi ndio wanamlea hivyo kwa kuzuia nyumba isiuzwe, bibi kutaka kuuza nyumba ni akili za kitoto kwa hiyo analelewa kwa kukatazwa.
Kwahiyo asingekuwa na nyumba wasingemlea mama yao?
 
😹😹😹 Mwenzao kajitesa kumshawishi dingi yao mpk kampa mjengo, km rahisi nao si wahongwe..!!
Unataka kusema bibi mkubwa aliruka sarakasi za kutosha kwa bed mpaka mdingi akameza funguo.
 
Kuna wamama wengine wanazingua sana,kama mmsha jua tatizo ni Mama yenu mdogo-why msitatute njia ya kumu handle.
Mkishindwa kabisa,tafuteni njia ya kumuondoa huyo Mama yenu mdogo-mnakaaje kizembe zembe hivyo yani mwanamke moja anawashinda.
 
Mimi sijata

Ka mali wala sijawah kuenda mahakamani nimeitwa zaidi ya mara 3 sikuona sbb ya kwenda, kilichonifanya niombe msada ni hali ya mama ya afya ya akili na mwili, na ni baada ya kutaka kuuza nyumba ya zaid ya mil 250 kwa mil 80, na umri wake ni mkubwa hawezi kufanya biashara wala chcht nyumba hy ndio msaada kwake, na mshauri wake mkuu ni mdogo wake wa kike ambaye alishawah kufoji signatir akachukua mkopo wa nyumba hy hy ikaja kuuzwa na bank. Lengo sio kumdhulumu wala kugombea msli ila ni kuhakikishs hakuna utapeli unafanyika dhidi yake na familia kwa ujumla mana mirathi yeye ni msimamizi na mmiliki pia.
hapo kumrudisha nyuma ni ngumu sana kifupi haiwezekani

yawezekana hakimu ana maslai yake hapo ama kasha hakikishiwa kupewa mgao

mshaurini kama anataka kuuza basi atafutwe mteja wa bei ya juu sio hiyo anayo taka iuza

sema yote ni kuzunguka njia rahisi mpotezeni ma mdg wenu iwe kwa uchawi ama kwa wasiojulikana (natania ila ndo njia rahisi)
 
Mimi sijata

Ka mali wala sijawah kuenda mahakamani nimeitwa zaidi ya mara 3 sikuona sbb ya kwenda, kilichonifanya niombe msada ni hali ya mama ya afya ya akili na mwili, na ni baada ya kutaka kuuza nyumba ya zaid ya mil 250 kwa mil 80, na umri wake ni mkubwa hawezi kufanya biashara wala chcht nyumba hy ndio msaada kwake, na mshauri wake mkuu ni mdogo wake wa kike ambaye alishawah kufoji signatir akachukua mkopo wa nyumba hy hy ikaja kuuzwa na bank. Lengo sio kumdhulumu wala kugombea msli ila ni kuhakikishs hakuna utapeli unafanyika dhidi yake na familia kwa ujumla mana mirathi yeye ni msimamizi na mmiliki pia.
Mfungulieni mashtaka mama mdogo, huyo ndo adui yenu.
 
2025 -43 = 1982
Baba alifariki 1989
Mzee alimwachia mama watoto 5 wakiwa wadogo sana, amepambana mpaka nyie kufikia kuwa na miji yenu.

Ameona hiyo pesa mnayompatia ya kudunduliza kila mwezi haimtoshelezi, na umri umesogea sana.

Mwacheni afaidi mali zake akiumalizia uzee wake.
Kuna kitu gani anafaidi na pesa katika umri huo,mtu mwenye umri huo kitu chenye thamani kwake kwa sasa ni care_apewe huduma zote na hakuna mtu wa kumpa zaidi ya hao hai watoto wake hasa hao wa kike.
 
2025 -43 = 1982
Baba alifariki 1989
Mzee alimwachia mama watoto 5 wakiwa wadogo sana, amepambana mpaka nyie kufikia kuwa na miji yenu.

Ameona hiyo pesa mnayompatia ya kudunduliza kila mwezi haimtoshelezi, na umri umesogea sana.

Mwacheni afaidi mali zake akiumalizia uzee wake.
 
Habarini ndugu.

Sisi tumezaliwa wa5 ke4 me1 na wote tuna miaka 40+, baba yetu alifariki 89 aliacha mali chache ikiwemo nyumba iliyopo katikati ya mji, nyumba hiyo baba aliinunua ila aliandika jina la mama kwakuwa alishtakiwa kwa kesi ya uhujumu uchumi hivyo alifanya hivyo ili kuinusuru isitaifishwe, na kabla hajafariki aliandika mirathi msimamizi ni mama kuwa mali zote ni za watoto na zisiuzwe na alisema nyumba hiyo ni ya biashara hivyo chcht kitakachopatikana ni kwa ajili ya mama na wanae ila mama akiamua kuondoka kuolewa aache kila kitu aolewe.

Tumekuwa na baadhi tuna miji yetu hatutegemei chochote kutoka ktk mali zilizoachwa na mzee, na baadhi tunafanya biasharea ktk nyumba hiyo na zaidi tunampa mama kodi km wapangaji ili aweze kupata mahitaji yake pasipo kututegemea sisi. Na tuliamua hivyo ili aishi kwa utulivu sababu umri wake ni mkubwa sana hana uwezo wa kufanya biashara yoyote tena. Ghafla mama ametaka kuuza nyumba tukamzuia, akaenda mahakamani tukaitwa hakimu akasema file la mirathi limepotea na nakala aliyopewa mama pia imepotea kwahy anampa mama haki ya kuuza nyumba na mama anasema wazi kuwa hakimu ni rafiki yake hivyo atamsaidia.

Sababu za mama kutaka kuuza nyumba ni ushawishi toka kwa mdogo wake ambaye alishaiba hati wakati baba anaumwa ilikuwa bank alimshikia rafiki yake mdhamana kwa kesi ya mauaji na alishinda kesi mama mdogo akachuku hati akaichukulia mkopo nyumba ikauzwa na bank ila baadae ilirudishwa baada ya kustakiana na mama yetu. sasa mama mdogo amerudi anamshawishi mama auze wafanye biashara ilhali mama hana uwezo huo, Naombeni msaada je file linaweza kupotea mahajamani?,na tutafanyaje tupate haki mana mirathi pekee ndio inathibitisha nyumba ilinunuliwa na baba.
Na wamama nao wanaingia tamaa ya kudhulumu watoto...aisee dunia nyoko
 
Kuna kitu gani anafaidi na pesa katika umri huo,mtu mwenye umri huo kitu chenye thamani kwake kwa sasa ni care_apewe huduma zote na hakuna mtu wa kumpa zaidi ya hao hai watoto wake hasa hao wa kike.
Labda care inasua sua mkuu.
 
Kwahiyo asingekuwa na nyumba wasingemlea mama yao?
Kwanza watoto kulea wazazi ni tatizo lakini mzazi kuuza mali zake halafu alelewe na watoto ni tatizo kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom