Mabadiliko haya yakipitishwa yatazuia raia wengine kufungua mashtaka kwa maslahi ya umma wanapohisi kuna uvunjifu wa Katiba.
Hutaruhisiwa kumtetea raia mwenzako hata kama hana uwezo wa kujitetea, hutaruhusiwa kutetea nchi yako kupitia mahakama isipokuwa pale tu unapokuwa umenyanyaswa moja kwa moja, na hutaweza kutoa mchango wako kuilinda KatibaYetu. Hii inaondoa uzalendo.
Kutoruhusu mtu au taasisi kufungua mashtaka bila kuathirika moja kwa moja inakulazimisha kujitegemea na kujitetea unapokutwa na unyimwaji wa haki zako unaohitaji mahakama kuingilia.
Mabadiliko haya yatawaathiri sana wasiokuwa na uwezo na ujasiri wa kujisimamia wenyewe kisheria kama vile walemavu, watoto, wajane na makundi mengine mengi ya kijamii ambayo yamekuwa yakisaidiwa na watetezi wa haki za binadamu kwa maslahi ya umma.