BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lumbira iliyopo Kata ya Luanda Wilaya ya Mbozi mkoani hapa, Jafari Mwashitete (16) amekutwa amefariki shuleni akidaiwa kujinyoga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe ACP Theopista Mallya amethibitisha kutokea kwa tukio la kujinyonga kwa mwanafunzi huyo.

ACP Mallya amedai kuwa walipokea taarifa ya kujinyonga kwa mwanafunzi huyo jana Jumatatu Julai 3, 2023 saa 10 jioni na kwamba ilikutwa karatasi mfukoni kwa mtoto huyo yenye ujumbe unaoeleza kutokutaka kusoma shule ya Lumbira badala yake anataka kusoma katika shule ya Myovizi.

"Ujumbe huo unaeleza kwamba marehemu alitaka kusoma Myovizi lakini wazazi wake walimhamisha na kumpeleka Shule ya Sekondari Lumbila jambo ambalo hakulitaka," amesema Mallya.

Aidha ametoa wito kwa wazazi kuwa wanapaswa kuwasikiliza watoto wao na kujua mawazo yao ili kuepusha matukio ya aina hiyo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lumbira, Kawawa Mwashilindi amesema alipata taarifa za tukio na kuwa mwanafunzi huyo alijinyonga katika jengo la maabara lililopo shuleni hapo.

Amesema Jafari alikuwa akisoma kidato cha tatu ambapo alihamia shuleni hapo akitokea Shule ya Sekondari Myovizi na kwamba mpaka umauti unamkuta alikuwa eneo la shule akiwa amevaa sare za shule.

MWANANCHI
 
Mbeya again!

Sipendi kukubaliana na report za awali ambazo hata hazijafanyiwa uchunguzi. Kisa tu kukuta ujumbe mfukoni tayari polisi wanahitimisha kajinyonga?

Je kama alinyongwa na kuwekewa ujumbe mfukoni?


Fanyeni Investigation acheni uzembe.
 
Marehem atakuwa msambaa huyu.
Pumzika kwa Amani Dogo.

Japo ataulizwa mbona umekuja kabla ya siku Yako?. Hizi roho za kujinyonga zinapaswa kuharibiwa kwa damu ya YESU.
Ukijinyonga uendi kuzimu Wala mbinguni hata shetani achukui vibudu Thus wazee wa utajiri wa punje wengi ujiua mkataba ukiisha kukwepa mateso ya shetani kuzimu
 
Huo wito wa kuwasikiliza watoto si itakuwa tabu kwenye nyumba zetu,hivi kweli mwanao anakwambia Baba nipeleka Shule ya Feza,ada mil.9 kwa mwaka wakati uwezo wako ni shule ya mil.1,utamkubalia tu ili umridhishe wakati hujui hata hiyo mil.1 utaiotoa wapi?tuombe tu Mungu atuepushe na haya mabalaa kwa kweli...
 
Shuleni kwangu Kuna mwanafunzi aliwahi kuhamishwa siku nimekutana nae alikuwa analia kwa kuhamishwa ilinichukua mda sana kumwambia Nia nzuri ya wazazi wake
Pale uhamisho inapokuwa mgumu mzazi shirikiana na Mwl kumjenga mtoto kisaikolojia
 
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lumbira Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe, Jafari Mwashitete mwenye umri wa miaka 16 amejinyonga kwa kutumia tai huku akiacha ujumbe wa kupinga kuhamishwa Shuke.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amesema mwili wa Mwanafunzi huyo umekutwa ukiwa umening'inia kwenye kenchi za maabara iliyokuwa inajengwa kwenye Shule hiyo.

Kamanda Mallya amesema "Ni kweli taarifa hizo tunazo na alijinyonga kwenye kenchi ya maabara iliyokuwa inajengwa kwenye shule hiyo kwa kutumia tai, kwenye mfuko wa Mtoto huyo aliacha ujumbe kuwa hataki kusoma kwenye Shule aliyohamishiwa na Wazazi wake ya Lumbira alitaka kuendelea kwenye Shule aliyosoma kidato cha kwanza na cha pili ya Myovizi"

Kamanda Mallya amesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
 
Huko Myovizi inawezekana kijana alishakuwa na ka manzi,na anaona kabisa anawaachia masela,inauma,u know
 
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lumbira Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe, Jafari Mwashitete mwenye umri wa miaka 16 amejinyonga kwa kutumia tai huku akiacha ujumbe wa kupinga kuhamishwa Shuke.

Akiongea na Ayo TV kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amesema mwili wa Mwanafunzi huyo umekutwa ukiwa umening'inia kwenye kenchi za maabara iliyokuwa inajengwa kwenye Shule hiyo.

Kamanda Mallya amesema "Ni kweli taarifa hizo tunazo na alijinyonga kwenye kenchi ya maabara iliyokuwa inajengwa kwenye shule hiyo kwa kutumia tai, kwenye mfuko wa Mtoto huyo aliacha ujumbe kuwa hataki kusoma kwenye Shule aliyohamishiwa na Wazazi wake ya Lumbira alitaka kuendelea kwenye Shule aliyosoma kidato cha kwanza na cha pili ya Myovizi"

Kamanda Mallya amesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
 
Hivi ni tai gani inayoweza kunyongaa tena alifunga kwa kenchi?? Mmmmh kuna walakini hapaa, shule ihojiwe vizuri.
 
Wanyiha hao washatoana kafara, kujinyonga na tai ufe mchezo?!!!
 
Back
Top Bottom