DOKEZO Ester Noah Mwanyilu, Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya Pandahill Mbeya amepotea

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Kajeba

JF-Expert Member
Oct 15, 2020
827
1,966
Kwa kweli inasikitisha mno, Mwanafunzi

Naomba wana JF muisikilize audio hii kwa umakini pia vyombo vya serkali vinavyohusika vichukue hatua.

==========

UPDATES...
Ester Noah Mwanyilu, Mwanafunzi wa kidato cha tano mchepuo wa PCB, Shule ya Secondari Pandahill hajulikani alipo baada ya kudaiwa kukimbia na kupotea zaidi ya mwezi mmoja uliopita wakati akikimbia adhabu kutoka shuleni hapo.

Sauti inayodaiwa ni mzazi wa Mwanafunzi mtoto huyo inaeleza kuwa maelezo hayo yametolewa na shule husika licha ya kuwa kuna mazingira tatanishi pia inadaiwa kabla ya kupotea Ester aliandika baru ambayo ndani yake aliandika “Naomba Mwalimu Jimmy aache kuwafanya Wanafunzi kuwa na maisha magumu kama alivyonifanyia mimi.”

IMG-20230621-WA0008.jpg

======
Tamko la Afisa Elimu kuhusu kupotea kwa Mwanafunzi Ester
JamiiForums imewasiliana na Afisa Elimu Mbeya (Sekondari), Ernest Hinju ambaye amekiri kutokea kwa tukio hilo na kasema lipo katika ufatiliaji chini ya Jeshi la Polisi.

"Ni tukio la kweli lilitokea katika shule hiyo zaidi ya mwezi mmoja uliopita, kwa sasa suala lipo chini ya Jeshi la Polisi'.

“Polisi ndio wenye mamlaka ya kuelezea wapi walipofikia, lakini hakuna rekodi ya matukio ya aina hiyo kutokea shuleni hapo huko nyuma.”

JamiiForums imemtafuta RPC wa Mbeya bila mafanikio
Katika kufatilia taarifa za kupotea kwa Mwanafunzi Ester JamiiForums ilimtafuta RPC wa Mbeya ambaye Simu yake haikupokelewa, Pia JamiiForums tuliwasiliana na Msaidizi wake ambaye alisema yupo nje ya Mkoa kikazi na akatoa taarifa kuwa RPC yupo likizo. Jamii Forums itaendelea kumtafuta RPC tukimpata tutaleta mrejesho.

JamiiForums imemtafuta Mkuu wa Shule ya Pandahill
JamiiForums tumewasiliana na Mkuu wa Shule ya Pandahili, ndugu Zephaniah James ambaye amesema wao walichofanya ni kutoa taarifa Polisi. Walienda kutoa taarifa Polisi ya Mwanafunzi kupotea Tarehe 19/05/2023. Hadi sasa Polisi wanaendelea kumtafuta.

Mwanafunzi hakumaliza mitihani hivyo ripoti ya Mitihani aliyofanya waliambiwa Wazazi wakachukue Shuleni hadi sasa hivi hawajaenda kuchukua mitihani hiyo.

Kuhusu vitu vya mwanafunzi(nguo, Mabegi, Madaftari) bado Vipo Bwenini alipokua analala. Polisi walisema wakabidhiwe wazazi kwa Maandishi lakini hadi sasa hivi hawajaenda kuchukua. Wazazi walisema wataenda kuvichukua na Polisi ila ndo wanasubiriwa.

Tamko la Waziri Mkuu juu ya kupotea kwa binti Ester Noah Mwanyiru
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameamuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na Kamati ya Usalama ya Mkoa huo wafanye uchunguzi zaidi na kwa haraka kuhusiana na tukio la kupotea kwa binti Esther Noah Mwanyiru ambaye alikuwa akisoma shule ya sekondari ya Panda Hill mkoani humo.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Alhamisi, Juni 22, 2023 baada ya kupokea ‘clip’ yenye maelezo ya mzazi wa binti huyo ambaye alikuwa akisoma kidato cha tano, tahsusi ya PCB kwenye shule hiyo.

Katika ‘clip’ hiyo, Mama yake Esther anadai kwamba yeye na mume wake waliitwa na uongozi wa shule hiyo na kujulishwa kwamba Esther hajaonekana tangu asubuhi ya tarehe 18 Mei, 2023.

Amesema, hadi sasa zimepita siku zaidi ya 20 wamekuwa wakimtafuta binti yao kila mahali bila mafanikio na hakuna dalili za kumpata.

IMG-20230622-WA0018.jpg
Mama Esther anadai kuwa Esther aliacha ujumbe wa maandishi akiwaaga rafiki zake na kuomba Mwalimu Jimmy aache kuwafanyia wanafunzi wengine kitendo alichomfayia yeye kwani kimesababisha maisha yake kuwa magumu.

“Naomba umfikishie salamu Mwalimu Jimmy, mwambie ameyafanya maisha yangu kuwa magumu sana hapa shuleni…..; ” Asiendelee kuwafanyia wanafunzi wengine kama alivyoyafanya maisha yangu mimi kuwa magumu.” alisema mama yake Esther akisoma sehemu ya ujumbe huo.

1687504767431.png


JamiiForums tumefanikiwa kuzungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema alikuwa likizo na ndio amerudi kazini, amesema kuhusiana na Ester kupotea walianza kufanyia kazi tangu tarehe 19, 06, 2023.

Anasema tukio liliripotiwa kituo cha polisi Mbarizi ufuatiliaji ulianza na waliandika maelezo ya watu wote shuleni, walimu, mwalimu wa zamu(uongozi mzima wa shule), anasema kipindi hicho kilikuwa ni kipindi cha mitihani, Kidato cha sita walikuwa wanamaliza mitihani na wao kidato cha tano walikuwa wanafanya mitihani ya muhula, ivyo anahisi ulinzi haukuwa mkali sana getini kwa watu kutoka nje kwa kuwa wanafunzi wengine walikuwa wamemaliza mitihani na walikuwa wanaruhusiwa kutoka nje ya geti.

Amesema kuwa ufatiliaji ulifanyika na baada ya kuona hapatikani kweli walimu walihojiwa na hata yule mwalimu aliyetajwa kwenye ule ujumbe unadaiwa kuachwa na Ester, Mwalimu Jimmy pia alihojiwa. Kama ilivyo taratibu za kipolisi tukipata taarifa ufatiliaji unaanza tulianza kufatilia, vikosi vyetu vyote vya upelelezi pamoja na intelijensia viliingia kazini vikaendelea kufatilia tukihusisha na taasisi nyingine na majirani zake na yule mama au mazazi na marafiki zake na yule mwanafunzi pamoja na yule mama, na pia kufatilia kama kuna mawasiliano na mtu alikuwa akiwasiliana kupitia simu, (Mama yake alisema likuwa na simu anatumia wakati wa likizo)

Amesema bado mpaka sasa wanaendelea kufatilia na wanaona shule wanajukumu la kusema maana mtoto walikuwa naye wao kwenye shule yao, walikabidhiwa na wanasema hawajui ivyo wana jukumula kusema, ikkabidi tuseme shauri liende kwenye ofisi za mashataka ili shule waweze kushtakiwa, kwa hiyo tukiwa tunaendela kusubiri maamuzi ya ofisi za mashtaka wasome huo ushadidi tumekusanya nasi bado tunaendelea kufatilia, maana ofisi ya mashtaka ndio wanajua kama ushahidi unafaa, na kama unafaa watapelekwa mahakamani na kama wataona bado haufai wataturudishia ili tuendelee kukusanya ushahidi zaidi.

Kamanda amesema Mkuu wa Mkoa wa Mbeya anatarajia kufanya mazungumzo na familia ya Mtoto Ester na kisha atazungumza na vyombo vya habari juu ya tukio zima, Kamanda ameongeza Mkuu wa Mkoa pamoja na Waziri Mkuu wametoa tamko la kuongezwa nguvu zaidi katika kufatilia tukio hili ili waweze kupata ufumbuzi wa wapi alipo mtoto huyo nao wamepokea maagizo na wanayafanyi akazi.

Lakini pia anadai zipo taarifa kuwa watu wanadai anaonekana, ila wakienda wanakuta haikuwa taarifa sahihi, lakini kila taarifa wanayopata wanaifanyia kazi, ameongeza kuwa wanaongeza nguvu zaidi na pia watamuita mazazi wa Ester ili wamuhoji zaidi juu ya wapi mtoto huyo alikuwa anapendelea kwenda maana wamezunguka maeneo yote na hawajamuona wala kuona mwili wa mtoto huyo.

Pia soma: Mkuu wa Mkoa Mbeya, Juma Homera: Kama kuna mtu yupo na mwanafunzi wa shule ya Pandahill, Ester Noah Mwanyilu ni vyema akamuachia
 
Sio kweli, shule inatoa ushirikiano mkubwa sana...Ukiangalia platforms zote za shule zinatoa taarifa juu ya upotevu wa mwanafunzi huyu. Kuanzia waalimu, viongozi na wafanyakazi wengine wasiokua walimu wanatoa taarifa.

Mpaka wanafunzi walioruhusiwa na wazazi wao kuwa na simu nyumbani huku wanasambaza taarifa hizi. Kwenye groups nyingi za Whatsapp wamesambaza pia hiyo taarifa..Kwa Polisi sijui Bado. Pengine labda mzazi anahitaji mtoto apatikane Kwa haraka, ndo inapelekea yeye kusema hivo..Well mengine Mungu anajua zaidi.
 
Sio kweli, shule inatoa ushirikiano mkubwa sana. Ukiangalia platforms zote za shule zinatoa taarifa juu ya upotevu wa mwanafunzi huyu. Kuanzia waalimu, viongozi na wafanyakazi wengine wasiokua walimu wanatoa taarifa.

Mpaka wanafunzi walioruhusiwa na wazazi wao kuwa na simu nyumbani huku wanasambaza taarifa hizi. Kwenye groups nyingi za Whatsapp wamesambaza pia hiyo taarifa..Kwa Polisi sijui Bado. Pengine labda mzazi anahitaji mtoto apatikane Kwa haraka, ndo inapelekea yeye kusema hivo. Well mengine Mungu anajua zaidi.
Huo ushirikiano wanautolea wapi?

Shule inamfumo mzuri wa usalama, electric fence na cctv camera
Kwanin hawaelezi mtoto alitokaje nje ya gate?
Video za cctv ziko wapi?
Mitihani aliyokuwa amefanya kabla ya kupotea iko wapi?
 
Huyu mama amejieleza vizuri sana tena precisely kwa hoja zenye mashiko, sasa na hao wenye shule nao wajitokeze wajibu maswali ya huyo mzazi, ila kiukweli walimu timizeni wajibu wenu kama walezi wa watoto wa wenzenu nanyi mtakuja kulipwa kipimo sawia na hicho mnachowapimia watoto wa wenzenu
 
Huyu mama amejieleza vizuri sana tena precisely kwa hoja zenye mashiko, sasa na hao wenye shule nao wajitokeze wajibu maswali ya huyo mzazi, ila kiukweli walimu timizeni wajibu wenu kama walezi wa watoto wa wenzenu nanyi mtakuja kulipwa kipimo sawia na hicho mnachowapimia watoto wa wenzenu
Hilo ni jukumu la vyombo vya ulinzi na usalama mkuu..wao ndo waishurutishe hyo shule katika mchakato wa upelelezi.
 
Huo ushirikiano wanautolea wapi?

Shule inamfumo mzuri wa usalama, electric fence na cctv camera
Kwanin hawaelezi mtoto alitokaje nje ya gate?
Video za cctv ziko wapi?
Mitihani aliyokuwa amefanya kabla ya kupotea iko wapi?
Sasa ndugu unataka wakuonyeshe CCTV video ww? Ndio maana wakakuambia issue Iko mikononi mwa polisi wao wakiziitaji hizo video za CCTV watapewa na sio ww
 
Sio kweli, shule inatoa ushirikiano mkubwa sana...Ukiangalia platforms zote za shule zinatoa taarifa juu ya upotevu wa mwanafunzi huyu. Kuanzia waalimu, viongozi na wafanyakazi wengine wasiokua walimu wanatoa taarifa.

Mpaka wanafunzi walioruhusiwa na wazazi wao kuwa na simu nyumbani huku wanasambaza taarifa hizi. Kwenye groups nyingi za Whatsapp wamesambaza pia hiyo taarifa..Kwa Polisi sijui Bado. Pengine labda mzazi anahitaji mtoto apatikane Kwa haraka, ndo inapelekea yeye kusema hivo..Well mengine Mungu anajua zaidi.
Mi sijapata tangazo kwenye MAGRUPU yangu ya Wasap Wala sijaliona FB

Hayo magup yenu yanaishia UYOLE😡😡😡😡
 
Inategemeana una-associate na ma group Gani mkuu, ukiwa eneo sahihi utapata taarifa hizo...kama ulivopata humu lakini umepata in negative way..
Habari hizi husaambaa sana hasa huyu mwezi unaisha na taarifa mmeshindwa hata kumtumia Askofu (Mwanakondoo Ameshinda) jina limenitoka
 
Nimesikia sauti iliyorekodiwa ambayo imesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwa inalalamika kuwa Shule ya Pandahili Mbeya haitoi ushirikiano kwa wazazi wa mwanafunzi ambaye alikuwa akisoma kwenye shule hiyo aliyetajwa kwa jina la Ester Noa Mwanyiru kupotea.


Sauti husika

1687368101356.png

Picha ya Mwanafunzi Ester Noa Mwanyiru
 
Back
Top Bottom