Maulidi Kitenge aacha kazi ITV/Radio one

Maulidi Kitenge aacha kazi ITV/Radio one

Ukimtoa Ayo wengi wanaoondoka ITV/EATV na kwenda kwenye Media Nyingine Umaarufu Unakwisha ! ( Maono yangu Binafsi ) 😛eace:
 
Mkuu abdalah majura anakituo cha radio? Kinaitwaje? Maana kuna ck nlikutana nae kwenye mizinguko ya mjin, yupo kawaida sana tena kwa miguu!

Nifahamishe hicho kituo cha radio plz

Akili za kijinga hizi ulitaka kila kona umuone na gari? anamiliki radio station Dodoma.
 
uandishi wake wa barua hauna tofauti na Pasco mate wake wa TSJ, hiko chuo walishindwa hata kumualika Asha Mtwangi awafundishe kuandika barua wanafunzi wake.
Mkuu So Notorious, asante kwa kumtambulisha Kitenge kama mate wangu TSJ, kiukweli sio mate wangu TSJ bali colleague kwenye fani!. Mimi ni wa TSJ ile ya Tanzania School of Journalism sasa (IJMC) na Kitenge ni wa TSJ hii ya sasa ya Time School of Journalism. Mimi na Maulid tuna gap ya kama miaka 10!, ila tunachofana ni idadi ya wake na tofouti ya watoto, yeye watoto ni wawili, mimi 7!.
Pasco
 
Anayekimbia bila taarifa ndio sio muungwana lkn huyo kaacha kazi na barua kaandiks mshahara karudisha na shukrani ametoa kwa mwajili wake.unataka awe mstaarabu wa aina ipi tena

Ngoja siku mfanyakazi wako wa ndani akupe 24 hr notice ndo utajua.

Imagine mfanyakazi wako wa dukani akwambie kesho naacha kazi, utajua.

cc Husninyo
The Boss
 
Last edited by a moderator:
Hio Message yake amekosea ama ?

Sababu anasema baada ya kutumika kwa miaka 14... hii inatoa maana nyingine kabisa ukilinganisha na kutumikia

Hapo kwenye red color nami pamenipa ukakasi kidogo. Naomba labda wajuzi wa lugh watuwekee sawa maana yake kimantiki.

kutumika?
kutumikia?
Kuajiriwa siku zote ni KUTUMIKA, believe it or not, TULIOAJIRIWA WOTE TUNATUMIKA! Tena tunatumika kisawa sawa! Asiyetumika ni yule tu ALIYEJIARIRI! Nampa HONGERA kama amejikomboa na kuamua 'kutotumika' hivyo amejijengea misingi ya kujiajiri! Lakini kama anaenda kuajiriwa kwingine na bado anasema ametumika IPP basi ataendelea kutumika kama alivyotumika mwanzo (akiwa IPP), there will be no any difference!
 
Watangazaji wana umuhimu gani si kila mtu anaweza kuwa mtangazaji? Ukiona kada ambayo kila mtu anaweza akaifanya tu vizuri awe amesoma ama hajasoma jua kazi hiyo siyo ya mhimu mfano polisi, watangazaji si watu mhimu kihivo maana leo hii hata wewe unaweza ukawa mtangazaji hata kama si kwa viwango vya kiutangazaji ila ukitangaza watu watakusikia tu

Mkuu ni kweli, kila mtu anaweza kuongea au kutangaza, kuimba au kucheza na hata kuendesha gari bila Leseni. Lakini kama ulivyo umuhimu wa leseni katika uendeshaji wa gari, ni muhimu pia kwa watangazaji kupitia darasani ili angalau tu wajue maadili ya utangazaji na mila na desturi zetu katika fani hiyo. Kimsingi wajue kanuni tulizo kubaliana katika fani hiyo kwa maslahi ya nchi yetu.
 
Ameshasaini Mkataba Redio EFM 93.7 See below akimwaga wino!

Kitenge.jpg
 

Attachments

  • Maulidi.jpg
    Maulidi.jpg
    48.6 KB · Views: 121
Wabongo bwana nani kakwambia ameondoka sababu ya kulipwa kidogo lakini mbona kilakitu ameweka wazi katika barua yake , lazima muwe waelewa na sio kupamba mambo amewaambia anakwenda kufanya kazi zake binafsi!!
 
Swahiba na wewe upo chama cha waajili? hivi mkifukuzaga watu huwa mnawapa muda wa kupata replacement job?

Mimi enzi za utumwa wa kuajiliwa niliacha kazi effectively same day kutokana na personal reason ila kwa kuwa muajili tuna historia naye fulani aliniita ofisini kwake akaniuliza tatizo hasa ni nini nilimweleza mimi na mtoto wake wa kiume ambae alikuwa acting General Manager hatuelewani kabisa na nilitaka kumpa kichapo ila nilitunza heshima ya chairman wa group of companies.

Basi yule Chairman akamuuru niandikiwe certificante of service nzuri na nilipwe haki zote anazolipwa mtu aliyeachishwa kazi.

mimi sipo chama cha waajiri ila napinga kumuita muungwana mtu anaeacha kazi ndani ya 24hrs. kwa maslahi binafsi sawa, unasepa tu hata kimya kimya ila wote tunajua kama kitendo hicho si cha kiuungwana.
 
mimi sipo chama cha waajiri ila napinga kumuita muungwana mtu anaeacha kazi ndani ya 24hrs. kwa maslahi binafsi sawa, unasepa tu hata kimya kimya ila wote tunajua kama kitendo hicho si cha kiuungwana.

Kwenye kumwagana hakuna uungwana labda iwe unaenda kusoma ndio utatoa taarifa hata miezi mitatu kabla.

Waswahili tuna roho mbaya unaweza kutoa taarifa mapema kwa nia njema kumbe wenzio wakatumia muda huo kukumaliza.
 
Inaonekana IPP inawalipa kidogo sana wafanyakazi wake.
Pia wengi wanamlalamikia mtu mmoja wanayemwita kwa jina la utani la 'm'bichwa' kuwa hawatendei haki.

Pale Radio One/ITV hakuna mtu mnafiki kama Deo Rweyunga...nafikiri ndio huyo unayemtaja kama m'bichwa
 
Kwenye kumwagana hakuna uungwana labda iwe unaenda kusoma ndio utatoa taarifa hata miezi mitatu kabla.

Waswahili tuna roho mbaya unaweza kutoa taarifa mapema kwa nia njema kumbe wenzio wakatumia muda huo kukumaliza.

hapo umenena shem
 
ukiacha makosa yake mengine mnayoyataja hapa swala la wake wengi ni kumuonea wivu tu, yeye wake zake kawatambulisha, wengine humu dini inaruhusu mke mmoja ila wanao watano wa siri, acheni unafiki nyie bana,
 
Ngoja siku mfanyakazi wako wa ndani akupe 24 hr notice ndo utajua.

Imagine mfanyakazi wako wa dukani akwambie kesho naacha kazi, utajua.

cc Husninyo
The Boss

yaani, hapo ndio ataisoma namba. halafu awe na mtoto mchanga sasa na dada wa kazi ndio kashaaga kesho anasepa.
 
Chezea E fm ni hatari wanachukua kila mtangazaji mzuri jijini hpa!
 
Back
Top Bottom