Wadau, kichwa cha habari chajieleza. Mtangazaji Maulidi Kitenge hajaondoka Wasafi FM Radio bali amefurushwa kwa sababu ya safari zake za mara kwa mara nje ya nchi, hususan nchini Marekani.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani kutoka Wasafi FM, Maulidi Kitenge amekuwa akienda nchini Marekani kwa mwaka mara nne jambo ambalo limekuwa likimkera CEO wa Wasafi, Nasibu Abdul 'Diamond'.
"Mfano, Novemba mwaka jana alikwenda Marekani. Januari mwaka huu, wakati Rais Joe Biden anaapishwa akaenda. Machi akaenda tena, mwezi Julai pia akaenda, mpaka unaingia Agosti yuko kule. Diamond akaona jamaa anakuwa nje ya kituo cha kazi muda mwingi, akaamua kumtimua," kilisema chanzo hicho.
"Amekuwa akitumia nguvu kubwa kutuma matangazo yake Wasafi akiwa kule, kama kusoma Magazeti (Kurasa za Magazeti, Chumvi na Ndimu) na Michezo (Sports Arena) ili aoneshe kuwa, hakuna pengo la kazi zake, lakini ukweli ni kwamba, Diamond amekuwa akikereka sana, akashindwa kumvumilia, akamtumia barua ya kumwachisha kazi," kiliongeza chanzo hicho.