Historia ya muziki wa kizazi kipya na chimbuko la neno Bongo Fleva

Forest Hill

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
2,482
5,515
Disclaimer:imesimuliwa na Martin Izze

Chimbuko la muziki wa kizazi kipya tanzania na maana halisi neno Bongo Flava (SEHEMU YA KWANZA)

Moja kati ya mambo niyapendayo mno maishani ni muziki.Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa muziki si tu ule wa nje lakini kwa karibu ule wa nyumbani hasa muziki wa dansi na ule wenye umaarufu sana hivi sasa ujulikanao kama Bongo Flava (Muziki wa Kizazi Kipya). Katika mapenzi hayo imekuwa kama bahati kuwa mmoja wa vijana wengi tuliobahatika kuuona muziki huu wa kizazi kipya ukizaliwa na pengine bahati zaidi bila kusita kusema; kuwa mmoja kati ya wale tulioanzisha kusukuma gurudumu la muziki huu kufikia hapa ulipo na nafasi yake kutambulika si tu Afrika Mashariki bali pia kwa sasa duniani kwa ujumla.

Kama ilivyo kwa aina zingine za muziki Tanzania,mfano muziki wa dansi basi utakuwa mkosefu wa fadhila bila kujumuisha majina kama Patrick Balisidya,Mbaraka Mwaruka Mwinshehe, Salum Abdalah na hata Remmy Ongara. Hawa ni vinara na walifanya kila wawezalo kuja na ubunifu si tu kuvutia wateja wao bali kuutangaza muziki wao ndani na nje ya nchi na kuipa Tanzania kitambulisho chake kwenye jukwaa la sanaa ya muziki. Kazi za wanamuziki hawa zilifana sana kwa ushirikiano mkubwa na chombo ambacho kwa Tanzania ni muhimu sana katika kueneza au kutambulisha kitu kipya, RADIO.

Watangazaji kama Mzee Ibrahim Chimgege,Enock Ngombale,Timothy Pata,Abisai Stephen,Seif Salum Nkamba na Julius Nyaisangah chini ya ma-bwana mitambo mahiri kama akina James Mhilu na Crispin Lugongo wanastahili pongezi kwa kiasi kikubwa katika kurekodi na kusimamia mitambo wakati wanamuziki hawa wakitafuta majina na namna ya kujitambulisha kwa jamii itakayosikiliza muziki wao. Bahati mbaya huwasikii sana watu hawa katika zinazoitwa historia kwa sababu wengi ni rahisi kuwasahau lakini mchango wao ni mkubwa sana na unastahili heshima hasa unapoandika au kuizungumzia historia ya muziki wa dansi Tanzania.

Nimetoa mfano wa hali halisi kwa ufupi kuhusu muziki wa dansi ili kukupa nafasi ya kujua kwa undani kile ambacho kinakweza kichwa cha habari hapo juu.Nia yangu hasa ni kuandika yale niliyoyaona na uzoefu wangu katika muziki huu wa sasa maarufu kama Bongo Flava.Muziki huu umeshika kasi na unapendwa sana hivi sasa kila kona.Ni faraja kuona hata wale walio ughaibuni siku hizi si ajabu kumkuta mtu ana albamu jpya la mwanamuziki wa Bongo Flava akiicheza ndani ya nyumba yake au garini kwa fahari.Inafurahisha kuona mapenzi kwa muziki huu yamekuwa makubwa na hilo ndilo lengo kuu.

Pamoja na yote haya,kama ilivyo kwa kila jambo ni vyema historia yake ikawa nyoofu na si kama ilivyo sasa ambavyo imekuwa ikipindishwa pindishwa mno,sijui kama ni kwa makusudi au kwa wengi kutojua harakati na wanaharakati walioufikisha muziki huu hapa ulipo.Kwa kuandika kwa usahihi yale yaliojiri juu ya chimbuko la muziki huu tutakuwa tunawatunzia wanetu na wengineo haki ya kuuelewa na kuutukuza zaidi muziki huu na msimamo wake katika jamii ya leo na ijayo.Shukrani labda nizitoe kwa Kaka Bonny Makene na Uncle michuzi kwa kunisukuma kujaribu kuandika nikijuacho juu ya muziki huu.

Kama nilivyododosa hapo juu kuhusu muziki wa dansi basi sasa niingie kwenye muziki huu wa kizazi kipya.Muziki huu ni ule ambao unajumuisha mitindo mbali mbali ambayo zamani tulizoea kuona ikipigwa na watu wa nje ya Tanzania kuanzia Hip Hop,R&B,Zouk na hata Soul.

Katika Hip Hop ya Tanzania pia utakosa fadhila kama hutotaja vijana wa mwanzo kabisa ambao kuanzia mivao yao na kufoka foka kwao kulikuwa ni burudani na ushawishi tosha kwa watu kuanza kudadisi kuhusu maana halisi ya utamaduni huu hasa Tanzania.Kwa wakati huo ilionekana kama uhuni tena wa kupita kiasi.Nitawataja wachache ninaowakumbuka ambao kila kukicha ukigongana nao kwenye Night Clubs,Samora Avenue pale Salamander basi ulikuwa unachoka mwenyewe.Nakumbuka vijana kama John Simple,Dj Rusual,The BIG One,Babu Manju,David Nhigula,Abdulhakim Magomelo,Kessy,Ibony Moalim,Tom London,OPP (now Jay P) na Dj Ngomeley.

Tukiendelea hao niliowataja hapo juu walikuwa chachu katika uvaaji wa kihip-hop na katika kughani na sijui kama kuna mtu atasahau watu kama Fresh XE Mtui,BBG (alianza na Mr II),Adili kumbuka,KBC (Mbeya Tech),Saleh Jabir,Samia X,THE BIG,Rhymson,2Proud.Deplowmatz na wengineo wengi ambao walikuwepo na wakighani katka school parties au matamasha ya mtaani kabla hata ya kurekodi nyimbo zao studio.

Kwa mara ya kwanza pia promoters kama Joe Kusaga na Abdul hakim Magomelo walionekana kutobaki nyuma katika ukuzaji wa sanaa hii ambapo waliandaa matamasha mbali kama Yo! Rap Bonanza na Coco beach Bottle Parties kwa ajili ya kuwapa nafasi wale wenye uwezo wa kughani.Matokeo yake yalikuwa ya kufurahisha kwani kila mmoja alikuwa na shauku ya kuingia katika gemu.

Kwa vile sio watu wote walikuwa na uwezo wa kughani lakini pia kulikuwa na wale wenye kuimba kama wanamuziki wengi wa Marekani kwa kupitia matamasha mbali mbali kwenye Jumba la utamaduni la Urusi,Korea na mengineyo yalikuwa yakiandaliwa hasa na wanafunzi wa shule mbali mbali za sekondari jijini kama Forodhani pia matamasha yaliyokuwa yakifanyika kando kando ya ufukwe ambako wengi wenye kutaka kuimba walijitokeza.

Hapa tunakumbuka kundi kama la Mawingu na mwana dada Pamela,mwanadada Stara Thomas na Judith Wambura ambao uwezo wake wa kughani na kuimba kama Mc Lyte ulimpa tafu hasa alipofanya hivyo kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha DJ show ya Radio One,shukrani kwa Ipyana Malecela Mkwavi (RIP) kwa zawadi ya LP yenye instrumental (ala) tupu aliyonipatia kama zawadi aliporudi toka UK kwani instrumental ya single “Keep,Keeping on” ndiyo iliyomtambulisha Jay Dee wa leo Radioni kwa mara ya kwanza japokuwa kabla ya hapo alikuwa mwimbaji wa kwaya kanisani lakini mweye kusita kuingia kwenye muziki wa kidunia.Pia Kundi la R&B lililojulikana kama Four Krewz Flava pia Herbert Makange ambaye pia alikuwa akiimba.

Naweza nikawa nimesahahu majina machache hapo juu lakini kwa ufupi hao ni baadhi ya watu wa mwanzo kabisa kuuingiza masikioni mwa jamii muziki wa kizazi kipya pengine hata kabla ya chombo kilichoipaisha juu zaidi..RADIO.Na ninaposema Radio simaanishi Radio nyingine bali Radio One Stereo kama Radio pekee yenye kujivunia juu ya ukuaji wa muziki huu wa kizazi kipya kufikia hapa ulipo.

Lakini uko nako hakukuwa na mteremko,mambo yalikuwa mengi na mazito mpaka muziki kujipenyeza na kukubalika.Je nini kilichochea mapambano ya kuuchomeka muziki huu Radioni na kuupa nafasi ya kupigwa sambamba aina zingine za muziki kama ule wa dansi nk? nani alihusika katika harakati hizo na nini kilifuata? ugumu huo ulitokana na nini?

SEHEMU YA PILI

Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 1994 kituo cha Radio kilikuwa kimoja tu kinachomilikiwa na serikali na wanamuziki wengi wa awali Tanzania walitambulika kutokana na nyimbo zao kupigwa katika kituo hicho hasa kwenye vipindi mbali mbali hasa kipindi maarufu cha kilabu Raha Leo Show.Japokuwa hakukuwa na mfumo maalumu wa mahojiano na wanamuziki ndani ya Radio Tanzania lakini kipindi hiki kilionekana kumaliza karibu kila kitu katika utambulishi wao jkwaani na mpaka jina la mpiga ala au sauti wanazoimba kutoka safu ya mbele,kati hata nyuma.Mara nyingi onesho hili lilikuwa likifanyika LIVE.

Wanamuziki ninaowazungumzia ambao walipewa nafasi kwenye kipindi kama hiki ni wale waliokuwa wakipiga muziki wa dansi na pengine taarabu na kwaya japo hawa hawakuwa na nafasi sana wakati huo.

Mara baada ya serikali kulegeza masharti kidogo kwenye soko huria,hatimaye watu binafsi waliruhusiwa kuanzisha Radio binafsi na kwa kuanzia walipewa masafa mafupi kwanza kwa sababu za kiusalama na kupima uwezo wa kumiliki na kuendesha chombo hiki muhimu.

Moja kati ya Radio hizo za mwanzo kuanzishwa ni Radio One Stereo iliyokuwa ikipatikana katika Megahartz 99.6 FM na kuanzishwa kwa kituo hiki ama kwa hakika ilikuwa ni mwisho wa ukiritimba na ushindani ulianza rasmi.Baadhi ya watangazaji waanzilishi ambao waliombwa na mmiliki ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Mzee Reginald Abraham Mengi ni Mikidadi Mahamoud ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Utangazaji,Charles Hillary aliyekuwa Mtayarishaji Mkuu wa vipindi na baadaye Mratibu wa kituo na Julius Nyaisangah aliyesimamia vipindi vya burudani na usomaji habari.Hawa wote walitokea Radio Tanzania Dar Es salaam.

Mchango wao kwa watangazaji chipukizi ni mkubwa na haupimiki kwa wale ambao walipitia mikononi mwa hawa wakongwe bila shaka watakubaliana nami.Walihimiza kufanya kazi kitaaluma ,walitoa mafunzo na nidhamu ya hali ya juu tuwapo kazini juu ya utangazaji.Hakika walifunguaa ukurasa mpya kwenye kitabu cha utangazaji Tanzania.

Darasa la kwanza kuajiriwa mwaka 1994 lilikuwa na chipukizi kama Taji “Master T” Liundi,Deo “Best Friend” Mshigeni,Flora Nducha na Runkim Ramadhani Nyamka.Kila mtu alipewa angle/nafasi yake ya kujidai na kipindi anachoweza kumudu.Mfano Taji Liundi alikuwa katika vipindi vya muziki vyenye kutoa maudhui na elimu juu ya mitindo mbali mbali ya muziki na fashion,Taji alikuwa ni mchambuzi.Runkim “Zipompapompa” Nyamka yeye alikuwa mcheza muziki DJ fundi na alikabidhiwa vipindi vile vya ufundi wa kuchanganya muziki na mara nyingi wakati wa Weekend.

Radio lianza kukua kwa kasi huku Radio zingine zikianzishwa kukuza ushindani.Hivyo kituo kilihitaji darasa lingine kupambana na ushindani huo na darasa hilo lilikuja mwaka 1995 likinijumuisha mimi,Sunday Shomari na Peace Kwiyamba.Binafsi nilipewa jukumu la kusaidiana na Taji Liundi katika uchambuzi ndani ya vipindi mbali mbali,Sunday Simba Shomari alishirikiana na karibu kila kipindi kuleta mchangayiko na Peace alishirikiana kwa karibu na Deo “Best Friend” Mshigeni katika vipindi vya salamu na muziki wa taratibu.

Lakini mbali ya vipindi vya burudani uongozi wetu hapo baadaye uliona ni vyema baadhi yetu tukasoma taarifa za habari na kuripoti kupitia vipindi vya Current Affairs kama Nipashe n.k.Peace Kwiyamba na miye tulibahatika kuingia katika upande mwingine wa kituo na kuwa wasomaji kamili wa taarifa ya habari na maripota.Tulipata mafunzo yetu pale Radio Tanzania Dar Es Salaam chini ya wakufunzi kutoka chuo kikuu cha Whitwatersand kilichopo Afrika kusini.Mafunzo haya yalidhaminiwa na serikali kwa pamoja na mfuko wa Ebert Stiftung nchini Tanzania.

Taji “Master T” Liundi alikuwa ni kivutio cha aina yake si tu kwa uwezo wake wa kuchambua mambo mbali mbali,bali pia kwa mahojiano yenye ukina na wanamuziki mbali mbali,uwezo wake wa kuongea lugha zaidi ya tatu na kwa ubunifu.Ikumbukwe yeye ndiye mwanzilishi wa neno “Chombeza”,nenoalilolibuni kumaanisha kubembelezana kiaina kati ya wapendanao hasa nyakati za usiku alipokuwa akipiga kipindi maalumu cha nyimbo za taratibu.Neno hili sasa ni maarufu sana huko Tanzania.

Master T pia alikuwa na ushawishi mkubwa sana hasa kwa vijana ambao wengi walikuwa ni wasikilizaji wa vipindi alivyokuwa akiviendesha Radio One.Aliwalenga pia vijana waliokuwa na mwelekeo wa kuingia katika muziki wa kizazi kipya na hakusita kujitolea kuwashauri kwa ukaribu na hata kujichukulia muda wake wa ziada kushiriki kwenye mazoezi na wakati mwingine hata kuwalipia sehemu hizo za mazoezi.Kwa vile sasa tulikuwa timu moja Taji alinishirikisha sana katika mambo mbali mbali yahusuyo kazi na hata nje ya kazi.Tulikuwa bega kwa bega kwenye matamasha mbali mbali yaliyokuwa yakiandaliwa na vikundi vya utamaduni vya shule mbali mbali za sekondari jijini.

Kwa ukaribu huu mkubwa kati yangu na Taji nia hasa ilikuwa ni kubadilisha mtazamo wa muziki Tanzania kwani mpaka wakati huo ni nyimbo za Marekani na nchi zingine za Afrika ndizo zilizokuwa zikichukua nafasi katika Radio One’s Top Ten,Chaguo la msikilizaji na DJ Show vipindi ambavyo vilikuwa ni jahazi na vilibeba sura ya kituo.Vipindi hivi tuliviendesha kwa umahiri mkubwa huku tukipokezana na mwenzangu Master T.

Mabadiliko haya tuliyokuwa tukiyalenga ni yalikuwa hasa ni kujaribu kuupa nafasi muziki wetu hasa ule wa kizazi kipya katika show kubwa nilizozitaja hapo juu,lakini piajitihada zetu hazikuwa na mteremko hata kidogo bali vikwazo pia,vikwazo hivyo vilimweka Taji katika wakati mgumu zaidi na kufanya ajiulize mara mbili mbili kwamba yuko kwenye Radio yenye mabadiliko kwa manufaa ya nani zaidi kama si kizazi kipya?

Nitatoa aina mbili ya vikwazo tulivyokumbana navyo kati ya vingi ambavyo havikutaka kutoa nafasi kwa wanamuziki wetu wa kizazi kipya kuutangaza muziki wao.Na vikwazo hivi zilifanya yeyote aliyetaka kwenda kinyume aidha kupoteza kazi,kusimamishwa kazi au kupewa onyo kali kwa maandishi.

Mosi: Kutokana na mpangilio wa vipindi na kwa matakwa ya watayarishaji wakuu ilikuwa ni marufuku kupiga muziki wa ndani ya Tanzania zaidi ya ule wa dansi bila muziki huo kusikilizwa na mmoja kati ya watayarishaji na kuukubali.Zaidi ya hapo ni ruksa kupiga muziki wowote kutoka Afrika au Marekani mradi tu uwe ni clean version (toleo lisilo na lugha chafu).

Na Pili: Si ruksa kufanya mahojiano na mwanamuziki wa kizazi kipya au asiyefahamika bila mwanamuziki huyo kufanyiwa usaili na watayarishaji (nikiwa na maana wakongwe) niliowataja hapo juu.

Hayo ni machache tu,lakini yalituweka katika wakati mgumu sana.Kitu kimoja tulikubaliana na watayarishaji ni suala la kutopiga muziki weneye matusi na sote tulilipinga hilo lakini kwa haya mengineyo hatukuwa katika level sawa.Wengi tulionelea kuwa pengine tunarudishwa enzi ya Radio Tanzania bila kujua na tulipanga kupigania hilo kwa nguvu zote.

Mimi na Taji tulipata barua kadhaa za onyo na hata kuhamishwa vipindi wakati fulani.Lakini hilo halikutuzuia kuongea kwa sauti juu ya kile tulichoona si haki.Tulitaka uhuru zaidi kwenye vipindi tulivyokuwa tukiendesha ili kipindi maarufu kama Top Ten yetu ipambwe na muziki wa kizazi kipya na mchanganyiko wa miziki ya aina zingine.Hiyo ilikuwa ni ndoto yetu kila kukicha.

Kwa jitihada hizi za kupigania muziki huu wa kizazi kipya uende hewani sambamba na aina zingine za muziki bila ukiritimba au masharti uituweka katika nafasi mbaya kiasi sio kazini tu bali hata mitaani ambako baadhi walituona kama tunaiga sana u-Marekani na kwamba kwa kutaka kupiga nyimbo kama hizi za kizazi kipya basi sisi ni wahuni tu na labda lengo letu kuu lilikuwa ni kutaka kuwafurahisha watu wa makundi yetu tu,kwa mtazamo wao watu wa makazi ya hali ya juu kama Oysterbay,Masaki n.k bila kujua binafsi nilikuwa nikiishi (Mbagala Kwa Makuka) mbali kabisa na maeneo wanayoyasema.

Lakini lengo letu lilikuwa ni kutenda haki kwa kila mwanamuziki hata kama wa kizazi kipya bila kujali wasifu wa wanakotokea.Japokuwa mwanzo wao ulikuwa mgumu kwani mashairi katika nyimbo zao yalikuwa lege lege na kutokana na ufinyu wa viwango vya studio wakati huo midundo/mipigo ndani ya miziki yao ilionekana kutokuwa na mpangilio,lakini tulihoji kwa nini wasipewe nafasi tu kwanza halafu tuone jamii itawapokea vipi? ilikuwa si sahihi kukataa kuiga nyimbo zao na kufanaisha viwango vya urekodi na vile vya wanamuziki wengine wa kimataifa ambao nyimbo zao mpaka zilikuwa zikichosha.

Mambo yalikuwa magumu na yasiyotabirika kutokana na harakati hizi.Hatimaye Master T aliondoka Radio One na kwenda jijini Mwanza ambako Radio (Radio Free Africa) nyingine ilikuwa ikianzishwa.

Baada ya Master T kuondoka nilikabidhiwa vipindi vitatu mfululizo (DJ Show,Chaguo La Msikilizaji,na Top Ten) kuviendesha,kati ya hivyo DJ Show ilikuwa weekdays na vingine weekly,ilikuwa mshtuko na kwa kweli kazi ngumu lakini kwa vile nilipenda na bado naipenda sana kazi ya utangazaji sikusita kuendeleza kasi ile ile aliyoiacha Taji japokuwa siwezi kusema kuwa pengo lake lilizibika.Lakini tulikuwa bado tukibadilishana mawazo kila mara tukiongea kwenye simu akiwa Mwanza.Moja kati ya msisitizo katika kila mazungumzo yetu ilikuwa ni kukaza uzi na kamwe kutotetereka na yeye akianzisha mzimamo kama aliouacha huko Mwanza.

Mambo yalianza kubadilika na nadhani kwa sababu ya wakati pia.Makundi tuliyokuwa tukiyapigania ni makundi mawili makubwa na haya ni makundi ya mwanzo kabisa katika muziki wa kizazi kipya Tanzania ukiachilia mbali wale waliokuwa wakighani au kuimba bila kurekodi.

Kulikuwa na makundi ya Hip Hop kama Fresh XE Mtui,Kwanza Unit,Deplowmatz,Hard Blasters,Gangstar With Matatizo,Wagumu Weusi Asilia,Young Da’ Mob,II Proud,Saleh Jabir,Samia X,Bugz Malone,Sos B,Afro Reign na flava kama za akina Mohd Momella,4Kruz Flava,Stara Thomas, Pamela na Mawingu Band,Connie Francis,Jungle Crewz Posse,Kamakazi Soldiers(6-7 years old kids),Mac Mooger,E-Attack,Afro Reign (chini ya Seba Maganga),Bantu Pound,Hardcore Unit/immeditation Kingdom nk.

Pia kulikuwa na makundi ya Reagge kama Inno Nganyagwa,Pompidou,Kimbuteh & Roots Band,Justin Kalikawe,Innocent Galinoma (USA),Jontwa Jokeri,Makoya Man na wengineo.

Tusahahu kuwa hata muziki wa dansi uliingia katika kizazi kipya kwa kasi tofauti kabisa na kubadili mtazamo wa bendi kama Msondo na Sikinde.Nazungumzia band ya Diamond Sound,wana ikibinda Nkoi chini ya Eliston Angai.

Wakati pengine hawa makazi yao yalikuwa Dar Es salaam ambako pia studio nyingi zilikuwepo,tukumbuke pia mikoani kulikuwa na ma-rapa waliokuja juu ile mbaya.Kwa vile nilisoma mkoani mbeya namkumbuka Rapa aliyekuwa akiitwa BBG ambaye alikuwa kibwagizo tosha kwenye ma-disco mjini Mbeya kama RTC,Mount Livingstone,AA Cool Para wa Zanzibar,Comtish wa ZNZ,pia kundi la Bombastic nk.

Naweza kusema hawa ndio waliweza kufungua ukurasa mpya wa muziki wa kizazi kipya Tanzania na baadhi yao waliwahi kufanya mahojiano na Taji kabla hajaondoka kuelekea Mwanza na sio siri walikubalika japokuwa muziki wao ulianza kupigwa lakini sio sana kama ambavyo piganio letu lilitaka.

Japokuwa jitihada zilianza kuzaa matunda,kazi sasa ilikuwa kwa wanamuziki wenyewe kuhakikisha wanauweka ulimwengu wa Tanzania sawa na kwamba jitihada na harakati zetu za kuupigania muziki huu uende hewani haziangushwi na kushindwa kwao.Tuliwaasa kupiga muziki wa kueleweka wenye maadhi si ya ki-Marekani zaidi au nje zaidi bali muziki wenye mtazamo wa kitanzania.

Tulishauri kuwa ili muziki uwe na nafsi basi ni vyema tukaweka vionjo vya kwetu zaidi kama wenzetu wa Afrika ya Kusini na mtindo wao Kwaito.Hata huko Marekani kulikuwa na mtindo tofauti kidogo wenye mahadhi ya hip hop ulioanzishwa na mkongwe Teddy Riley unaoitwa “New Jack Swing” ambao ulibaki kam Hip Hop ila yenye vionjo tofauti na ladha ya New York.Nilitoa mifano hii makusudi kwenye kipindi maarufu nilichokuwa nikiendesha cha DJ Show kwa sababu walengwa na wadau wengi wa muziki Tanzania walikuwa wasikilizaji wakubwa wa kipindi hiki.DJ show ndio ilikuwa kilabu Raha Leo Show yao na nilisisitiza sana kwenye mapinduzi ya kuwa na mtindo wetu mpya wenye ladha yetu wenyewe.

SEHEMU YA TATU

Kwa vile kwa namna moja au nyingine harakati zilionekana kuanza kuzaa matunda,nami niliona ni vyema nikauchukua mwanya huu kuzaa kile ambacho mwenzangu Master T alikuwa mstari wa mbele kukingia kifua ili kufanikisha azma ya kuwaweka vijana wa Tanzania na muziki wao wa kizazi kipya mbele ya watanzania lakini huku kukiwa na msisitizo wa “cha kwetu”.
Nilibahatika kufanya mazungumzo na mmoja wa wana Hip Hop mahiri nchini anayetokea kwenye kundi la Kwanza Unit Kibacha “KBC” Singo ambaye tulikuwa tukifahamiana kwa muda mrefu toka mkoani Mbeya ambako sote tulikuwa tukisoma miaka ya mwanzoni ya tisini.KBC alikuwa ni msomaji mzuri na muelewa wa mambo mengi ya Hip Hop.

Nilimweleza azma yangu ya kujaribu kuuingiza muziki huu hewani lakini kwa ushauri wa nini kifanyike ili tusichekwe kwa kuonekana tunaiga sana umarekani.KBC alicheka lakini alikubaliana nami na kusema hatuwezi kuibadilisha Hip Hop kufuata midundo yetu lakini tunaweza kuibadilisha kulingana na lugha pia vionjo vya kwetu.Lakini kwanza KBC alisema si kila mtu anaweza kufanya Hip Hop na lazima anayetaka kuingia katika game lazima ajue misingi ya muziki wenyewe.Nilikubali maoni ya KBC na niliuomba uongozi wa Radio one kugawa saa nzima,kuanzia saa 12 mpaka saa moja jioni katika siku moja ya wiki ili kutimiza haja hiyo,hasa hasa kuutenga muda huo kwa muziki wa Rap/Hip Hop tu na si kitu kingine ili kuupa muziki huu nafasi zaidi ya kusikika na kutambulika tofauti kabisa na ule wa kutoka The Bronx,Dirty Dirty South au South Central L.A.

Niliomba kwa uongozi ili KBC aongoze kipindi hicho lakini uongozi kwa sababu za kueleweka ulikataa na kunitaka niendeshe kipindi hicho mimi mwenyewe na KBC awe mgeni maalumu au mtoa mada katika kipindi hicho wakati wowote akiwa na nafasi.Kipindi kilikwenda hewani kwa mara ya kwanza na KBC alikuwa regular.

Matokeo yalikuwa mazuri kwani vijana wengi walikipokea kwa mikono miwili na kushukuru mchango wa KBC katika kipindi hiki.

Hip Hop ya Tanzania ilianza kubadilika na kuanza kuwa na sura na mwelekeo wa Tanzania kama tulivyotarajia kwani kwa mara ya kwanza mkali mwingine wa Hip Hop Ramadhani “Chief Rhymson” Mponjika alitoa single yake kwa kumshirikisha mkongwe wa miondoko ya dansi aitwaye Hassan Seyvunde na kibao ambacho kilitamba sana sio kwenye Radio tu hata kwenye TV kutokana na maudhui yake.Pia kundi lao la Kwanza Unit walikubali mwito na kuibuka na kibao kiitwacho Msafiri ambapo rekodi ilikuwa na kiitikio kilichodurufu rekodi ya mkongwe wa muziki wa dansi Tanzania al maarufu kama Mzee Mzima King Kikii Mwanza Mpango.King Kikii naye alijumuika na familia ya Kwanza Unit katika matamasha mbali mbali kuwapiga tafu na mara wimbo huo ulipopigwa katika matamasha hayo mapokeo yalikuwa ni ya kuridhisha na huo ndio ukawa mwanzo wa Hip Hop ya Tanzania kupanda chati na kukubalika zaidi.

Wakati haya yote yanatokea mkongwe mwingine kwa jina la 2Proud (sasa Sugu) naye hakuwa nyuma alitoa nyimbo ambazo zilikuwa gumzo na zenye ujumbe wa moja kwa moja kwa viongozi wa siasa Tanzania mpaka aliyekuwa Mratibu wa vipindi wa Radio One Charles Hillary alianza kukubali kazi za wasanii wa kizazi kipya na kuamua kuvunja baadhi ya masharti ambayo hapo mwanzo yalikuwa ni kikwazo.CharlesHillary kwa mara ya kwanza alikubali kupiga wimbo wa msanii wa huyu IIProud uitwao “Ni Mimi” katika moja ya vipindi ambavyo alikuwa akiviendesha.

Huu ulikuwa ni mwanzo mzuri na upanuzi mkubwa kwa muziki wa Hip Hop Tanzania ambao sasa ulianza kushamiri kila kona na kwa kasi kubwa.

Lakini changamoto haikuwa kwenye Hip Hop ya Tanzania tu bali hata muziki wa dansi nao ulianza kubadilika kutokana na wakati.Kama ilivyo kwa KBC na mchanganuo wake wa mawazo kwenye kipindi changu cha Rap time ambacho sio siri kiliwafungua macho vijana wengi waliotaka kuingia katika muizki katika miaka ya 90 ukiachilia wale wakongwe,basi katika dansi nako kulikuwa na mapinduzi yake.

Sote tunakumbuka bendi kama Diamond Sound ambayo ilikuwa ikipiga nyimbo nyingi za Congo na zikiimbwa kwa lugha ya kilingala.Niliwahi kumwalika kiongozi wa band hiyo Elliston Angai katika kipindi cha DJ Show na rapa wake mashuhuri Allan Mulumba Nkashama na kufanya nao mazungumzo ni namna gani wanaweza kushirikisha vionjo vya Tanzania zaidi katika nyimbo zao na Rap zao.Bila kusita walikaribisha wazo hilo na kama ilikuwa ni mgongano wa mawazo kumbe nao walikuwa wanatafakari namna ya kutawala soko la muziki wao kwa kuuza CD ambazo muziki wake utakuwa na mtazamo na ladha ya Tanzania.

Allain Mulumba kutokana na ubunifu wake alikuja na rap yake ya kwanza kabisa baada ya changamoto hiyo kwenye DJ Show ambayo alitumia tangazo la sabuni kuonesha muonjo huo.Tangazo lile lilikuwa na maneno kama “Omari mbona unajikuna sana,sio siri mamaa! ninawashwa sana ngwarariii ngwararaaa”.

Ndipo sote tulipokubali maapokezi ya muziki na kwa kutumia lugha yetu kumbe unalipa.Ukumbi wa Silent Inn ulilipuka kwa furaha ya Rap hiyo ambayo kwa mara ya kwanza ilipigwa usiku huo na kutambulishwa rasmi,mashuhuda wenzangu katika mapinduzi haya usiku huo pale Silent Inn walikuwa waandishi wenzangu Sebastian Maganga (Radio One),Farouq Karim (ITV Zanzibar),John Ngahyoma (ITV Dar) na Chacha Maginga (sasa TBC1) .Baada ya hapo tulishuhudia band nyingi zikiiga sana mtindo huu na kuibuka na rap za kiswahili kwenye miziki waliyokuwa wakipiga ambayo ina asili ya Congo.Tunakumbuka bendi kama FM Musica na zingine ambazo zilifuata nyayo.

Nanyambulisha haya kwa makusudi ili kuweka kumbukumbu sawa na kwa vile kuna kusahahulika kwa matukio muhimu kama haya hasa inapofika wakati wa watu aidha wasiojua kumbukumbu hizi au kwa makusudi ya kukidhiana wanaandika zinazoitwa historia juu ya mabadiliko ya muziki wa kizazi kipya Tanzania bila ya kutaja mambo muhimu kama haya.

Na nikiri wazi kuwa pamoja na kuwepo kwa kipindi cha DJ Show ambacho ni cha kwanza kutambulisha muziki huu wa kizazi kipya hewani na kuwa kipindi pekee chenye heshima hiyo kabla ya kingine chochote,hivi leo husikii wengi wakikipa heshima yake na pengine kukisahau kabisa katika kumbukumbu za muziki huu tunaousheherekea hivi leo.Waulize wanamuziki wakongwe katika anga za muziki huu watakwambia ukweli huu.Pia kumekuwa na kusahaulika kwa waandishi wa kwanza kabisa kuandika habari za wanamuziki hawa kwenye makala na hata kuwafanyia mahojiano kwa mara ya kwanza.Waandishi kama Angetileh Osiah,Tom Kirumbi,Albert Memba ,Ibra Poza,Issa Michuzi au Juma Pinto.

Tukirudi kwenye Radio lazima nikubali baadaye pia kulikuwa na upinzani na vituo vingine ambavyo navyo viliendeleza muziki huu wa kizazi kipya kwa kasi kubwa sana.Pia watayarishaji wa muziki kama Enrique “Rick” Figueredo wa Sound Crafters pale Temeke,Joakim “Master Jay” Kimario wa MMJ Production,Boniphas “Bonny Luv” Kilosa wa Mawingu Studios,Paul “P” Funk wa Bongo Records (alianzisha kundi la vijna wa miaka saba lililopiga HipHop),Marlon Linje wa Don Bosco studio.Shukurani kwa kipindi cha Dr Beat chini ya KBC na Dj Bonny “Luv” Kilosa na Othman “OJ” Njaidi ambao waliendeleza libeneke katika mtindo ule ule wa ushindani lakini tukiwa marafiki wa karibu na kubadilishana mawazo mara kwa mara kwani sote lengo letu lilikuwa moja.Dr Beat ilikuwa chini ya Clouds FM.

Pia wadhamini na mapromota ambao walikuwa na moyo wa dhati katika kuendeleza sana hii ya muziki wa kizazi kipya.Na upozungumzia muziki huu basi huwezi kumsahahu Joseph ‘Joe” Kussaga na Abdulhakim Magomelo.

Lakini mimi binafsi mbali ya mkongwe Taji Liundi ambaye alifungua njia ya mapambano na harakati ili kuupa muziki huu nafasi yake kama ilivyo dansi na aina nyengine ya muziki,kamwe sitomsahahukijana mwenye akili “Genius” Dj Sebastian Maganga ambaye alipokea kwa dhati mikoba ya DJ SHOW baada ya miye kuachia ngazi.Sebastian ana nafasi ya pekee sana katika muziki huu tangu alipojiunga na Radio One toka Radio Tumaini,ikumbukwe pia Sebastian ni mwana HipHop aliyetoka na kundi la Afro Reign toka miaka hiyoo.Sebastian ni mbunifu na ndio yeye aliyenisukuma zaidi katika kuibadili DJ Show moja kwa moja na kuachana na nyimbo nyingi za Marekani katika kipindi cha DJ SHOW na pole pole tuliweza kufanikiwa kwa kushirikiana na DJ Jumanne kutoka Holland ambaye alitutengenezea promo nyingi za kipindi na kubadili usikivu wa kipindi hiki kutoka muziki wa Snoopy Dogg/Dr Dre mpaka ule wa akina Mr II/Kwanza Unit.

Na katika kufanikisha hilo kwa vile DJ Show ilikuwa inapiga muziki mchanganyiko lakini wa kileo.Siku moja tukiwa kwenye kipindi Sebastian aligusia mfumo wa kutenga muziki katika dakika 30 kila genre,kama tunapiga Reggae basi alishauri iwe dakika 30,kama R&B ya Tanzania basi tutenge dakika 30 nk.Nilikubaliana na wazo hilo kwani lingetufanya tutoe nafasi sawa kwa kila aina ya mtindo na sio upendeleo wa kupiga Hip Hop au R&B tu masaa yote mawili ya kipindi.

Ilipofika dakika 30 za muziki wa R & B,siku hiyo nilikuwa kwenye usukani na kwa mbwembwe nilicheza nyimbo ya kundi la R&B lililoitwa 4Krewz Flava na baadaye kuiunganisha na nyimbo nyingine ya Unique Sistaz.Kwa vile midundo,mpangilio,lugha na utaalamu wa muziki wenyewe kamwe huwezi kuufananisha na ule wa Soul 4 Real au SWV kutoka Marekani,tulipenda tutofautishe kidogo kati ya aina hizi mbili na ndipo session hii niliibatiza jina ambalo lingetofautisha R&B ya Marekani na ile ya kwetu….niliipa session hii jina la BONGO FLAVA.

Hii ilikuwa mwaka 1996 na ndio ulikuwa mwanzo wa neno BONGO FLAVA likiwa na maana muziki wenye mahadhi ya nje lakini wenye vionjo na ladha ya Tanzania na si vinginevyo lengo kuu ni kuitofautisha na muziki ule wa Marekani.Hip Hop ya Tanzania ilibaki na itabaki vile vile kama ilivyo,ila muziki wowote ule wa nje,mbali ya Hip Hop na DANSI ya Tanzania niliuita na kuufahamishakwa umma wa watanzania kama BONGO FLAVA ndani ya kipindi cha DJ SHOW cha Radio One.

Nikifikia tamati ya mtazamo wangu na jinsi nilivyoshuhudia muziki huu ukikua pengine kumekuwa na ubishi ambao kwa maana halisi nimeonelea nao niudodose kidogo hii leo.Nilipokuwa nyumbani Tanzania nilipata bahati ya kutembelea Clouds FM ambako mwenzangu Sebastian Maganga sasa ni Mkuu wa Vipindi na aligusia suala hili la chimbuko zima la muziki huu na neno BONGO FLAVA.Niliweka haya unayoyasoma wewe hapa bloguni kama yalivyo na niliomba yeyote mwenye kuona tofauti na ninauona ukweli kujitokeza lakini hakutokea mtu kupinga.

Nasema hivi kwa vile huko nyuma kuna waliodiriki kujitokeza/kujitangaza hapo mwanzo na kudai kuwa neno hili BONGO FLAVA ni jina lililotokana au kutungwa na wao,kitu ambacho mimi na mwenzangu Sebastian Maganga tunakipinga kwa sababu tunajua ukweli uko wapi.Watu hawa (tunafahamiana fika) waliombwa kuja studio za Clouds FM siku hiyo katika mahojiano maalum na kuuthibitishia umma juu ya dai lao lakini hakuna aliyetokea.

Ni kweli kila mtu na mtazamo wake katika kila jambo kutokana na alivyolishuhudia lakini ni vyema tukawa wakweli kidogo bila kupindisha mambo pale tunapotaka kuuhabarisha umma juu ya yale tunayotaka wayafahamu.Katika mnyambulisho huu hapa juu sio lengo wala nia yangu kumsuta mtu na inawezekana kabisa kama binadamu wa kawaida kuna mambo nimeyasahau,kama ndivyo basi ni vyema tukasahihishana ili kurekebisha mambo na sio kudanganya kwa kudhani ukweli kamwe hautojulikana na ndio maana nimeamua kuandika haya ili kuweka yale ninayoyajua wazi kwa faida ya kizazi kijacho na hata cha sasa ambacho kimekuwa kikipotoshwa na wachache.

Na kwa kufanya hivi sina nia hata kidogo ya kutaka au kuuukwa umaarufu,kwani nimekuwa maarufu toka nina miaka 19 na sihitaji wala silazimishi kuwa maarufu hivi leo.

Ieleweke kuwa haya yote ni katika kutoa elimu kama shuhuda wa mapinduzi ya muziki huu Tanzania kwani kumekuwa dhahiri na upotoshaji wa makusudi au wa kutojijua inapokuja katika mambo muhimu yanaohusu muziki wa kizazi kipya Tanzania.
Kwa mfano neno hili la BONGO FLAVA lilizaliwa na kutokea katika kipindi cha DJ Show na si vinginevyo kama ambavyo imekuwa ikidaiwa katika zinazoitwa historia za muziki huu wa kizazi kipya kutoka vianzio mbali mbali.

Mfano mwingine hai ni ule kuwa kuna kuna wanaosema TANZANIA MUSIC AWARDS imeanzishwa na mwanamuziki James Dandu (ambaye alikuwa ni rafiki yangu mkubwa) lakini watu wanasahau kuwa TANZANIA MUSIC AWARDS ilianzishwa na mwanamuziki wa zamani wa bendi ya Mawenzi/Prodyuza John Kagaruki chini ya kampuni yake ya Serengeti Production kwa kushirikiana na BASATA mwaka 1997 na sherehe za kwanza kabisa ambazo zilirushwa live na kituo cha ITV zilifanyika pale Whitesand Hotel.

Ni kweli mwaka uliofuata sherehe hizi hazikufanyika tena na zilipwaya.Lakini tusisahau kuwa mwaka 2000 kampuni ya Look Promotion kwa kushirikiana na Clouds FM walifanya tena onesho hili ikiwa ni mara ya pili kufanyika Tanzania.Na mwaka uliofuata bia ya Kilimanjaro kwa kushirikiana na mwanamuziki James “CJ MASSIVE” Dandu na kampuni yake ya Dandu Planet walizindua upya sherehe hizi ambazo zimekuwa zikifanyika kila mwaka toka wakati huo.

Mifano kama hii na mingineyo mingi tu inaleta mushkeri hasa inavyopotoshwa kwa makusudi ilhali mashuhuda wake tupo tena tukiwa hai.

SEHEMU YA MWISHO
Kufikia hatua hii basi labda niseme tu kuwa imefika wakati wanamuziki wa Hip Hop na Bongo Flava leo hii wana nafasi yao katika jamii ya Tanzania na wanapaswa kuenziwa,kukumbukwa na kuheshimika bila kuchanganya aina hizi mbili za muziki kwani ni vitu viwili tofauti kabisa lakini lengo likiwa moja.Kuna mambo mawili ambayo nadhani yakifanyika basi angalau kumbukumbu ya wale wakongwe walioanzisha harakati na mapinduzi katika muziki huu watadumishwa na wale wapya watajifunza kutokana na kuwaenzi wakongwe hawa.

Hapa tusisahau pia wakongwe waliokuwa wakipiga ianyoitwa Hard Core HipHop kama Fresh XE ambaye sidhani kama alibahatika kurekodi,Samia X,GWM,E-Attack,Underground Soul,Hasheem,KU Crew,Nigga One,D-Rob au II Proud na wengineo ambao walikuwapo hata kabla ya kipindi cha DJ SHOW au Radio One kuanza lakini hawakuwa na sehemu ya kuutangaza muziki wao.Hawa kamwe hawatasahaulika na wana heshima kubwa sana kwenye muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.

Bila kutegemea “Awards” ambazo zinaonekana kuwa na dosari kila zinapofanyika kila mwaka kwa tuhuma za upendeleo nadhani imefika wakati mwafaka kwa muziki huu na wanamuziki wake kuwa na tuzo zake maalum zitakazofanyika kila mwaka na kuzitofautisha kabisa na zile tulizozioea za muziki mchanganyiko.

Kuwepo na utaratibu wa kujumuisha wiki ya tuzo hizo na usaidiaji wa jamii kwa wakongwe watakotumikiwa tuzo hizo kutembelea baadhi ya shule za msingi au sekondari na kutoa changamoto ya maisha na elimu juu ya muziki huu kwa ujumla kwa kizazi hiki kijacho.Pia hata kushiriki nao katika shughuli za usafi wa mazingira kwa siku hiyo.Huu ni mchango tosha na ishara kuwa muziki huu si uhuni ni sehemu ya maisha kwa kizazi kipya.

Vile vile sehemu ya mapato na udhamini wa onesho hili iende kusaidia shule masikini au ya watoto wasiobahatika na wenye ulemavu wa namna moja au nyingine.

Kwa kufanya haya na mengineyo mengi muziki huu sio tu utakuwa ni wenye kujijengea heshima bali kuweka kumbukumbu kubwa ya mapinduzi kwenye ulimwengu wa muziki Tanzania na hadhi yake kuwa ni ile isiyofutika kwa urahisi machoni na akilini mwa kizazi cha sasa na hata kile kijacho kwa muda mrefu
 
ahsante kwa kumbukumbu mujarabu

Madogo wa dotcom wapitie hapa
 
Aisee shikamoo
Kwa haya uliyoandika unahitaji kuandika kitabu
Na filamu kabisa, ila hasa kitabu kwasababu filamu huwa zinafeli kubeba details ndogo dogo za muhimu

Andika kitabu mzee, simulizi hii inavutia sana. Ni urithi wa kihistoria, miaka ijayo hakutakuwapo wengine wa kuisimulia hii historia vizuri zaidi ya kitabu ambacho kimeandikwa na watu walioshuhudia haya first hand, tena jambo zuri wengi iliowataja bado wazima, kusanyikeni pamoja na mtaalamu wa uandishi uandike kitabu
 
Kuna mtu umemtaja anaitwa Mac mooger, hivi huyo ni yule yule aliye kuja I'm wa na ali Kiba ama ni coincidence tu?
 
Kinachofurahisha na kusisimua juu ya historia uliyoweka hapa ni
Kwanza umeishi sehemu ya historia hiyo hivyo unaelezea kiundani,
Pia ni simulizi ya kizalendo, kusisitiza kuwa mlifight hiphop iwe ya kitz zaidi ni jambo la kizalendo
 
maelezo ya nani haya?

Sent from my CPH2083 using JamiiForums mobile app
 
Maneno meeeeengi.

Mwanzilishi wa Bongo Fleva ni jamaa mmoja anaitwa SALEHE JABIR.

Huyu ndo mtu wa kwanza duniani kurekodi rap kwa Kiswahili.

Albamu yake aliita SWAHILI RAP. Ilitoka mwanzoni mwanzoni mwa miaka ya 1990. Mie nakumbuka niliinunua mwaka 1992.

Hiyo albamu ilisambaa sana na ilipigwa sana kwa vijana ndo ikawafungua watu macho kuwa kumbe inawezekana kurap kwa Kiswahili na nyimbo zikaswihi.

Baada ya hapo ndo rap za Kiswahili za kila aina zikaanza kutoka na fani ikakua ikazaa neno la Bongo Fleva.

Huu hapa ni moja ya nyimbo zilizokuwepo kwenye albamu ya Swahili Rap (na hiyo picha ndo ilikuwa kwenye ganda la hiyo albamu, ambayo iliuzwa katika kanda):

uko vizuri
 
Kuna mtu umemtaja anaitwa Mac mooger, hivi huyo ni yule yule aliye kuja I'm wa na ali Kiba ama ni coincidence tu?
Mac Muga story ya kweli, jamaa bonge la Mnyamwezi. Alisoma Tambaza akakipa South Africa nafikiri kabla hajamaliza Form Four.

Story imeandika mengi sana na kunikumbusha vijundi vingi vya zamani, DJ Shiw na enzi za kumpelekea Taji Liundi chrome tapes.

Respect to Hard Blasterz na "Funga Kazi".

RIP DJ Hakim "Kim" Mgomelo. Yo! Rap Bonanza uliturusha.
 
Mwamba Mike Mhagama na sauti lake kuuubwa.Vp hujamuelezea vizuri Rankeem Ramadhan a k a Mzee Nyamka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom