Maulidi Kitenge aacha kazi ITV/Radio one

Maulidi Kitenge aacha kazi ITV/Radio one

Taarifa zilizopo ni kuwa kiko Dodoma.
Hapa ndio yale yale ya 'simba na yanga', na mara nyingi mwisho wake ni fulfillment ya tamaa za muda mfupi lakini haya mambo ya kuhamia hamia vituo vya huko Dar es Salaa hakuchangii lolote fani ya habari. Anyway, yote maisha.
DU7C9302.JPG
Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akisaini Mkataba wa kazi na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam.​

Mazungumzo ya kitenge na mkurugenzi wa EFM wakati wa kusaini huo mkataba .

Kitenge:Haka ndo katakuwa "ka mshahara" kangu.??? Ohhh...waooo.
Mkurugenzi EFM:Ahahaa..kadogo sana bw. kitenge tafadhali hebu ongezea japo sifuri mbili mbele.
Kitenge: Mbona kubwa sana mkuu, mpaka inatoka kwenye kibox cha kujaza
Mkurugenzi EFM:Kawaida kitenge kwani ile barua yako nimeiona , ikanisikitisha sana kwani gharama za maisha ziko juu sana.
Kitenge:Asante sana mkuu, najuta sana kuchelewa kujiunga nanyi, kwani kule koo lilikuwa lishaanza kukauka na ngozi kunywea kama mtu aliyekula chumvi nyingi.
Mkurugenzi EFM:Ahahaahhhaa .... Usijali sana kitenge hesabu kuanzia sasa utaanza kung'aa kama zile enzi zako kwani umekuja kwenye maziwa na asali.
Kitenge :Lazima niende kwa mzee wa upako nikatoe ushuhuda juu ya
mambo haya makubwa.
Mkurugenzi:Haya piga sahihi yako kwanza hapo juu ya jina lako na usisahau kuhakiki tarehe ya kusaini mkataba kama iko sahihi.
 
Kung'atuka kwa kingereza ni kustep down, sasa turudi kwenye hoja ya msingi

Kitenge ameresign au amestep down?

Matola, nimeshakwambia mimi kizungu sijui. Sikatai, yawezekana kwa kizungu ni sahihi, sikatai. Ila kwa kiswahili kuna maana tofauti kati ya kujiuzulu na kuacha kazi. Maulid kaacha kazi,hajajiuzulu.Narudia tena. yawezekana kwa kizungu ni sahihi. Wanyamwezi tunasema 'me and you are in the same pool but in a different pond', mbona sioni tunapopishana?
 
Last edited by a moderator:
ni uamuzi mzuri,walk away from trouble if you can....
 
Kuajiriwa siku zote ni KUTUMIKA, believe it or not, TULIOAJIRIWA WOTE TUNATUMIKA! Tena tunatumika kisawa sawa! Asiyetumika ni yule tu ALIYEJIARIRI! Nampa HONGERA kama amejikomboa na kuamua 'kutotumika' hivyo amejijengea misingi ya kujiajiri! Lakini kama anaenda kuajiriwa kwingine na bado anasema ametumika IPP basi ataendelea kutumika kama alivyotumika mwanzo (akiwa IPP), there will be no any difference!

Hilo nalo neno mkuu, point taken wc high credibility .
 
Nikiangalia huyu mtangazaji anavyo andika naishia kucheka tuu!
Kuna mambo najiuliza kwanini ameamua kutangaza ameondoka? kulikuwa kuna ulazima wa kusema hayo yote?

Ni wazi MTU akisoma alivyo andika atajua fika huyu mtu analengo Fulani na anataka watu wamuone mwajiri wake mbaya au kumuaribia biashara.

Pamoja na umahiri wa kitenge kwenye utangazaji wa habari za michezo kwa sisi wasikilizaji wa radio one na watazamaji wa ITV bado kumebaki watangazaji wazuri kama Amri masali,Katanga hi yo sikweli patapwaya!

Hivi kumbe busara aliyonayo Millard Ayo imewashinda wengi kiasi hiki? Hivi ukiondoka kimya kama ulivyo ajiriwa kimya kuna kosa? IPP media naona ndio kiwanda cha kuzalisha watangazaji Tanzania na ni ngumu kuwalipa kila mtu kulingana na matakwa yake!

Hivi kuondoka kwa matangazo ni busara?hadi Leo pamoja na Allan laki,Adrian stepp kuondoka kwa kuutangazia umma sikuwai kuona mapengo yao mpaka Leo, kuondoka kwa matangazo mengi kunachukuliwa kama njia ya kutaka kuharibu.
 
Kaacha kazi siyo kujiuzulu kwani aliajiliwa na Umma?huko ni kuacha kazi wala haina haja ya sisi kujua.

Ukiona mtu anaondoka kwa matangazo ujue hana busara na anataka muajiri wake aonekane mbaya na anataka kumharibia biashara.
Kijana Millard Ayo ana busara sana.
 
Matola, nimeshakwambia mimi kizungu sijui. Sikatai, yawezekana kwa kizungu ni sahihi, sikatai. Ila kwa kiswahili kuna maana tofauti kati ya kujiuzulu na kuacha kazi. Maulid kaacha kazi,hajajiuzulu.Narudia tena. yawezekana kwa kizungu ni sahihi. Wanyamwezi tunasema 'me and you are in the same pool but in a different pond', mbona sioni tunapopishana?
Na wewe tulia sasa upewe darasa, hakuna tafsiri ya kingereza kuja kwenye kiswahili yenye maneno kuacha kazi.

Kwa kingereza sahihi na kupata tafsiri sahihi ya kiswahili basi madeiwaka watumie neno Terminate = kusitisha pale wanapoandika barua za kuacha kazi.
 
Last edited by a moderator:
Hata kama yupo kijasiliamali zaidi si inatakiwa awahudumie unyumba sawasawa kama dini inavoagiza? Sasa anaweza kweli wake wanne du kuna siku tutapata habari za kugutusha kama kweli anawahudumia sawasawa yaani haki zawa kwa wote

Mtu unaoa wake wanne halafu unategemea ulipwe sh ngapi ikutoshe?
 
Kumbe katimkia E FM dooh homa ya jiji ila kusema ukweli hizi radio zinazoishia magomeni zinaua fame zao ambazo nazo kwa kiasi zingewasaidia au zina wasaidia katika kuongeza kipato.
 
Ukimtoa Ayo wengi wanaoondoka ITV/EATV na kwenda kwenye Media Nyingine Umaarufu Unakwisha ! ( Maono yangu Binafsi ) 😛eace:

Hivi issue ni umaarufu ama nini kinaingia mfukoni mwisho wa siku watoto Wapate kwenda chooni? Think Big ww..
 
Ukiona mtu anaondoka kwa matangazo ujue hana busara na anataka muajiri wake aonekane mbaya na anataka kumharibia biashara.
Kijana Millard Ayo ana busara sana.
Hiyo picha ya Kitenge kama isingekuwa na maelezo mimi ningejuwa anasaini fomu za kuichezea Yanga.

Hata huko BBC sijaona ulimbukeni huu wa kusaini mkataba wa kazi mbele ya media, haya mambo yanawahusu wacheza mpira tu ili kudraw attention ya mashabiki.

Hivi hiyo redio frequence zake ni ngapi maana nasikia makele yake tu sijawahiwhata kuisikiliza.
 
Hahaaaa halafu bora wangekuwa wembemba ..ana wake wanne wote mitinginya hataree

Wake wanne? Mimi nilisikia ni wawili. Nampongeza kwa kuwa na wake wawili. Kuwa na mke mmoja na michepuko kibao ni gharama kuliko wake wawili wanaotambulika
 
Nikiangalia huyu mtangazaji anavyo andika naishia kucheka tuu!
Luna mambo back najiuliza kwanini ameamua kutangaza ameondoka ?kulikuwa Luna ulazima was kusema hayo yote?

Ni wazi MTU akisoma alivyo andika atajua fika huyu mtu analengo Fulani na anataka watu wamuone mwajiri wake mbaya au kumuaribia biashara.

Pamoja name umahiri was kitenge kwenye utangazaji was habari za michezo kwa sisi wasikilizaji wa radio one na watazamaji wa ITV bado kumebaki watangazaji wazuri kama Amri masali,Katanga hi yo sikweli patapwaya!

Hivi kumbe busara aliyonayo Millard Ayo imewashinda wengi kiasi hiki? Hivi ukiondoka kimya kama ulivyo ajiriwa kimya kuna kosa? IPP media naona ndio kiwanda cha kuzalisha watangazaji Tanzania na ni ngumu kuwalipa kila mtu kulingana na matakwa yake!

Hivi kuondoka kwa matangazo ni busara?hadi Leo pamoja na Allan laki,Adrian stepp kuondoka kwa kuutangazia umma sikuwai kuona mapengo yao mpaka Leo, kuondoka kwa matangazo mengi kunachukuliwa kama njia ya kutaka kuharibu.

Mkuu edit habari yako kama unajifunza kuandika!!!
 
Kwa taarifa nilizopata kwa kupitia masafa ya Ungo ni kwamba.
Maulidi Baraka wa Kitenge anafanya kama ya Juma Nkamia.
Yaani alitoka utanganzaji akasepa ungune leo Waziri.
Sasa Maulidi Kitenge anatarajia kugombea Ubunge,sasa ameamua kutoka mapema ili ajipange.
Atakuwa mgombea wa chama cha wakulima TPP
 
Back
Top Bottom