Hapana mkuu, AZAM kakaa mbaliii anacheki muvi, jamaa kaenda kuungana na kina SSEBO ndani ya Efm.
MTANGAZAJI mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar es salaam leo.
Kutokana na tafiti ya Ipsos ya mwaka 2013, inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha Radio One, ndiye mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM, Dickson Ponela, ameeleza kufurahishwa kwake kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.
Mpaka sasa Kitenge ameisha saini mkataba na kituo chetu na anatarajiwa kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM, alisema mkuregenzi huyo.
Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji waliobobea katika fani hiyo akiwemo Dizo One, Dennis Sebo, Sos B, Kanky Mwaigomole na Dj Majay.