Hapa hutapata ubishi toka kwangu. Mimi pia ningependa kupata ufumbuzi wa huu uhalifu unaotokea.Kama CHADEMA wanataka watu na Jeshi la polisi linashindwa kuwakamata basi tuna Jeshi la hovyo.
Pili, Serikali iombe msaada nje ukweli ujulikane kwa sababu mpaka sasa Jeshi la polisi halijakamata hata mtu mmoja.
Lakini Serikali hii haitaki kuomba msaada nje.
Pia hawa wanaokamatwa na kutekwa wanasema wameshafatwa na polisi na watu wa usalama kwamba waache kuiponda Serikali.
Leo hii jeshi la polisi, na resources zote walizonazo, wamefikia wapi na uchunguzi wa Lissu, Azory, Roma, Ben Saanane?
Siamini kama serikali ndiyo inayofanya huu uhalifu, watu wanaichukia, lakini wanaendelea kufanya hivyo hivyo.
Na mwisho, sidhani kama suluhu ya haya matatizo ni kuipindua serikali ya Magufuli.
Tusubiri 2020.