Riwaya: From Isra to Isra (Kutoka Isra kwenda Isra)

SIMULIZI RIWAYA

JF-Expert Member
Feb 19, 2022
417
1,275
[MPYA 2024]

FROM ISRA TO ISRA.
Sehemu ya..............01
Mtunzi: Saul David
Simu: 0756862047
Email: saulstewarty@gmail.com


UTANGULIZI...

Ulikuwa ni mchana wa jua kali, Mwanaume mmoja alionekana akitembea katikati ya Jangwa moja kubwa, upepo mkali ulikuwa ukivuma kiasi cha kusababisha vumbe jingi kutanda hewani hali iliyosababisha mwanaume huyo kutembea kwa shida sana wakati huo mikononi mwaka alikuwa amembeba mtoto mchanga mwenye umri yapata wiki mbili hivi. Alijitahidi kumfunika mtoto huyo ili asipigwe na lile vumbi.
Hali ya mwanaume huyo aitwae David ilionekana kuwa mbaya sana, alitembea kwa kujikokota huku usoni akiwa na michilizi ya damu iliyokauka. Jangwa lilikuwa ni kubwa mno haukuonekana mwanzo wala mwisho wa jangwa hilo.
Baada ya kupiga hatua kadhaa David alisimama na kumtazama mtoto aliyekuwa amevalishwa kidani shingoni mwake, David alikifungua kidani hicho kilichokuwa na picha ya mwanamke mmoja mrembo sana, akawa anakitazama kisha akaachia tabasamu hafifu.
David aliinua macho yake na kutazama juu kisha akaongea....
"Duniani kuna mambo mengi sana, yapo tunayoyajua na kuyaona katika maisha yetu ya kila siku, lakini yapo yanayoendelea ambayo hatuyajui wala hatuamini Kama yapo. Mimi David nimefanikiwa kuyaona na kuyaishi yale ambayo sikuwahi kuwaza kama Kama yapo katika huu ulimwengu wetu. Haikuwa rahisi kuyakabiri maisha haya, lakini kwa msaada wa mwanamke niliempenda akanipenda SASHA nimeishi na nitaendelea kuishi nikiwa na kiumbe huyu mikononi mwangu, sitokufa, nitaishii.
Hii ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kukutana na SASHA...


FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya ........01.

Ilikuwa ni siku iliyojaa simanzi na majonzi kwa WATANZANIA wote hasa wale waliokuwa wamekusanyika siku hiyo katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam wakiuaga mwili wa aliye kuwa Rais wa Tanzania Dk John pombe magufuli.
Mwili wa shujaa huyo wa watanzania ulikuwa ukizungushwa uwanjani hapo kwa ajili ya kuagwa na maelfu ya watanzania waliokuwa wamekusanyika eneo Hilo.
Kilio cha watanzania kilisikika huku baadhi wakipunga mkono wa kwa heri kwa shujaa huyo wa aina yake kuwahi kutokea nchini Tanzania.
David alikuwa ni miongoni mwa watanzania waliofika kwenye uwanja wa uhuru kutoa heshima hizo za mwisho. uso wake ulionekana kujaa majonzi mno.

Wakati zoezi hilo likiendelea,
binti mmoja mrembo akiwa amevaa gauni jekundu refu linaloburuza mpaka chini alionekana akiwa anatembea tembea kule walipokuwa waombolezaji akiwa ameshikilia kichupa kidogo chenye rangi nyeupe mkono wa kulia na mkono wa kushoto aliishikilia boksi dogo lenye rangi nyeupe pia.
Binti huyo alikuwa akikinga matone ya machozi yaliyokuwa yakiwatoka waombolezaji hao kwa kutumia ile chupa yake.
Kila alipokuwa akimkaribia mtu yeyote anaelia alisubiri hadi tone la machozi litoke ndipo alikinga na tone hilo kuangukia ndani ya chupa yake, cha ajabu hakuna mtu yeyote aliyeweza kumuona binti huyo, aliendelea na shughuli yake kama kawaida pasipo kuonekana.

wimbo wa maombolezi ulibadirishwa na wimbo wa zuchu -Magufuli, ulianza kupigwa...

"Magufuli hai,
Hai!!
Hai hai hai!
Hai.....!!

Hapo watu wengi waliacha kulia na kuanza kuruka ruka ikiwa Kama sehemu ya kuenzi miongoni mwa nyimbo pendwa za rais magufuli.
Yule binti aliacha zoezi lake la kukusanya machozi akawa anasubiri nyakati za majonzi ili aendelee.
Alitazama chupa yake ilikuwa imefika katikati kwa ujazo wa machozi aliyokusanya.
Wakati akifanya hivyo mara kwa bahati mbaya kale kaboski kake keupe kalimponyoka na kuanguka chini, kakaporokoka kwenye ngazi katikati ya watu.
Yule binti alipatwa na mshituko mkubwa baada ya kuangusha lile boski kwani Sasa alikuwa anaonekana na kila mtu, ilionyesha kuwa lile akini boski ndilo lililokuwa likimfanya asionekane.
kwa bahati hakuna mtu aliyeshtuka binti huyo kuonekana ghafula kutokana na msongamano mkubwa wa watu.
***

David akiwa ni sehemu ya waombolezaji, mara aliona kuna kijiboksi kidogo cheupe kimedondokea miguuni pake.

Aliliangalia kwa sekunde kadhaa na taratibu akainama kutaka kuliokota.

"Achaa, usishikeee"
Sauti ya kike ilisikika kutoka nyuma yake, David aligeuka kutazama.
Akamuona binti mmoja mrembo sana amevaa gauni jekundu mkoni akiwa ameshikiria chupa nyeupe.

" Kwa hiyo unaona Mimi ni mwizi au" alisema David huku akiinama kuokota lile boksi.

"Achaaaaa"
Yule binti alipaza sauti kwa mara nyingine kumzuia David lakini haikusaidia kwani tayari David aliinama na kulichukua lile boksi, kisha akamtaka aje kulichukua.

Yule binti alibaki katika hali ya kuduwaa huku akiwa amemkodolea macho David.
David nae akiwa haelewi chochote kwa nia njema tu alitaka mkumsaidia yule binti lakini hakuja ni kwa nini Yule binti anamzuia kwa nguvu kubwa.

Wakati wakizidi kushangaana mara David alipigwa shoti ya ghafula kwenye ule mkono alokuwa ameshika lile boksi, akatetemeka na kuliachia likadondoka.
David alihisi mkono wake umekufa gazi, alimtazama Yule binti ambae nae alionekana kuduwazwa na tukio hilo.
Haraka yule binti aliinama na kuliokota boski lake akaanza kuondoka.

David akiwa bado ana maumivu kiasi, alimsindikiza yule binti aliyekuwa anaondoka kwa kasi akipotelea kwenye umati wa watu.
David hakuweza kusema lolote zaidi ya kubaki anashangaa tu, lakini jambo ambalo hakulielewa ni kwamba baada ya yule binti kulishika lile boski lake kwa mara nyingine ni yeye pekee ndiye aliyekuwa anamuona.
Watu wengine waliokuwa kwenye msiba huo hawakuwa wakimuona zaidi ya David pekee lakini yeye hakujua hilo....

ITAENDELEA....
Usikose kufuatilia SIMULIZI hii yenye mkasa wa kusisimua.Simulizi:


FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya................02
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047.

ILIPOISHIA....
Lakini jambo ambalo David hakulielewa ni kwamba baada ya yule binti kulishika lile boski lake kwa mara nyingine ni yeye pekee ndiye aliyekuwa anamuona.
Watu wengine wote waliokuwa kwenye msiba huo hawakuwa wakimuona yule binti isipokuwa David pekee...

SASA ENDELEA...
Baada ya yule binti kupotea machoni kwa David, Kijana huyu aliutazama mkono wake uliopigwa na shoti ya ajabu mara baada ya kulishika boksi lile akaona uko salama. Kichwani alibaki na maswali mengi akijiuliza msichana yule ni nani? Kwa nini alimzuia kuokota kile boksi kidogo? Kwa nini mara baada ya kuokota amepigwa na shoti ya ajabu. Bado David hakuwa na majibu ya maswali yake, mwisho aliamua kupotezea tukio lile akiamini pengine kulikuwa na vitu vyenye asili ya umeme ndani ya kile kijiboksi ndio sababu alimzuia. Hakutaka kulizingatia sana tukio lile ambalo kiasi lilikuwa na maajabu yake.


Dakika 45 baadae...
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julias Nyerere kundi kubwa la watu walionekana wakikimbia mara baada ya kuvunja geti, wakawa wanaelekea kwenda kushuhudia mwili wa Rais wao kipenzi ukiingizwa ndani ya ndege tayari kusafirishwa. Licha ya serikali kutoa siku mbili za kuuwaga mwili wa marehemu lakini hazikutusho kuwazuia maelfu wa Watanzania waliojitokeza hadi uwanja wa ndege kumsindikiza huku wakiimba na kulitaja jina la shujaa huyo.

Watu walifika uwanjani hapo walikuwa ni wengi mno, ikiacha idadi kubwa ya Watanzania waliojipanga pembeni ya barabara kutoka uwanja wa mpira wa uhuru hadi kufika uwanja wa ndege bado hawakufikia idada ya hawa waliofulika uwanjani hapo.
Licha ya kuwekwa utaratibu maalumu uwanjani hapo lakini ilikuwa ni ngumu kuwazuia Watanzania hao ambao baadae walivunja geti na kuanza kukimbia wakiingia ndani zaidi ya uwanja wa ndege. Hali hii ilipelekea wengine kuanguka na kuanza kukanyagana. Ilikuwa ni hatari sana hasa kwa wanawake na vijana wadogo walikuwa miongoni mwa waombolezaji hao.

David akiwa mmoja kati ya maelfu ya watu waliofika mahali hapo, alishuhudia kundi kubwa la watu likivunja geti na kuingia ndani ya uwanja wa ndege kwa kasi. David akiwa hatua kadhaa kutoka hapo, alijikuta akitabasamu na kuwaza moyoni.

"Huu ni upendo wa ajabu wanaouonyesha Watanzania kwa Rais wao, haijawahi tokea mahali popote Dunia, hakika walimpenda mno"
Aliwaza David na wakati akiwaza hayo ndipo alipoona tukio lingine la ajabu.

Katikati ya lile kundi kubwa la watu waliokuwa wakikimbia kwa mara nyingine tena alimuona yule binti mwenyewe gauni jekundu. David alitoa macho kwa mshangao baada ya kuona binti huyo akifanya mambo ya ajabu. Si kwamba alikuwa akikimbia kama wengine la hasha, yeye alikuwa bize akiwainua wale watu waliokuwa wakianguka chini kuwazuia wasikanyagwe. Alikuwa akiifanya kazi hiyo kwa kasi sana. Anaenda kushoto anamuinua huyu anarudi kulia, anakwenda mbele anarudi nyuma huku kasi yake ikionekana kutokuwa ya kawaida kabisa.
Yule binti aliendelea kuifanya kazi hiyo katikati ya ule umati mkubwa wa watu. Jambo la ajabu ni kwamba hakuna aliyekuwa akimuona zaidi ya David peke yake.
"Oo..oya mwanangu" Alisema David huku akimgusa begani mwanaume mmoja aliyekuwa amesimama pembeni karibu yake.
"Nambie" aliitika
"Unamuona yule msichana anachokifanya pale?"
"Msichana yupi?"
"Yule pale" David akanyoosha kidole katikati ya ule umati wa watu wanaokimbia
"Sasa watu wote wale nitajua ni mtu gani unamzungumzia" aliuliza yule mwanaume huku akimtazama David usoni kwa mshangao.
"Namaanisha yule Dada amevaa gauni jekundu kwani huoni anavyofanya katikati ya wale watu?"
"Eeh.. we jamaa mi sikuelewi bana" Alisema yule mwanaume huku akimuona David kama mwendawazimu, akazuga kama anapokea simu akaenda zake pembeni.

"Mbona anaonekana kwamba haoni nini pale?" David alijiuliza hukua akiamini kwa mtu mwenye macho yenye afya kamili kama yake asingeshindwa kumuona yule msichana mwenye gauni jekundu.

Wakati David akizidi kutazama mara ghafula akaona tukio lingine la ajabu. Kilishuka kitu cheusi kutoka juu angani kikaanguka chini katikati ya ule umati wa watu na baadae akasimama mtu mmoja aliyevalia mavazi meusi tii kuanzia juu hadi chini. Hata yeye alikuwa na ngozi nyeusi tii kama nguo zake. Alikuwa amevaa koti kubwa jeusi lenye kofia pana kichwani. Koti lake lilikuwa refu mno kiasi cha kugusa chini na kufanya miguu yake isionekane.
Mkononi alikuwa ameshikilia mkuki mrefu, akawa anatembea kumuelekea yule binti anayefanya kazi ya kuinua watu waliodondoka.
Yule mtu mwenye mavazi meusi naye alikuwa akipishana na watu pasipo kuonekana yaani alikuwa ni David pekee ndiye aliyekuwa akiwaona watu hao wa ajabu.
Yule mtu aliendelea kutembea akawa anamueleka yule binti, kwa bahati mbaya yule binti hakuwa amemuona kabisa na alipo mkaribia aliinua mkuki wake juu akiwa amedhamiria kuuzamisha kwenye mgongo wa yule binti aliyekuwa ameinama wakati huo.

David alishuhudia yote haya akiwa kwa mbali asielewe ni nini hasa kilikuwa kinaendelea. Alifumba macho kwa hofu asishuhudie tukio lile la kutisha. Kuna wakati alihisi kama yuko ndotoni lakini kila alipojaribu kuzinduka kutoka usingizini ndipo alipogundua kuwa haikuwa ni ndoto bali kila alichokiona na kukishuhudia kilikuwa ni kweli tupu.

Wakati yule mtu akiushusha kwa nguvu mkuki wake ghafula kufumba na kufumbua wakatokea wanawake wengine watano waliovaa mavazi mekundu sawa na alivyovaa yule binti. Mmoja kati yao akasimama mbele ya yule binti na wakati huo huo yule bwana mwenye mavazi meusi akausindilia mkuki wake kwenye mwili wa yule mwanamke aliyesimama mbele ya binti yule kumkinga, nikama mwanamke yule alikuwa amejitoa muhanga kuzuia mkuki usimpate yule binti na badala yake ukazama kwenye kifua chake na akatokea mgongoni.
David alipokuja kufumbua macho yake kuangalia kwa mara nyingine akakutana na tukio lingine la kutisha, aliona ule mkuki ukiwa umezama kwenye mwili wa mwanamke mwingine ambaye hakujua ametokea wapi huku wale wengine wanne wakiwa wamesimama imara kumzunguuka yule binti. David hakujua watu hawa wamefikaje fikaje mahali hapo na wametoka wapi. Kila alichokiona kilizidi kumchanganya na kumuacha mdomo wazi.
David alishuhudia yule mwanamke aliyechomwa mkuki akipukutika kama mchanga na baadae akawa moshi mweupe uliopotelea hewani. Wakati huo huo wale wanawake wanne waliosalia wakawa bado wamesimama kumzunguuka yule binti ambaye aliacha kufanya kile alichokuwa akikifanya sasa akawa anaelewa kuwa yuko hatarini kushambuliwa na yule mtu mwenye mavazi meusi.
Ajabu ni kwamba licha ya idada ya wale watu wa ajabu kuongezeka lakini bado ni David pekee ndiye aliyekuwa akiwaona. Watu wengine wote walikuwa bize na harakati za msiba wa Mheshimiwa Rais.

Yule binti alikuwa amesimama katikati huku akiwa amezinguukwa na wale wanawake wanne ambao kila mmoja alikuwa na kisu kidogo mkononi mwake kilichofungwa utepe mwekundu. Yule binti alipenya kati kati ya wale wanawake waliomzunguuka akapiga hatua kumsogelea yule mwanaume mwenye mavazi meusi.

"Tafadhali usimsogelee ni hatari" Aliongea mwanamke mmoja kati ya wale wanne.
"Acha niongee naye"
"Hapana Sasha anaweza kukudhuru" Yule mwanamke alisisitiza.
Naam, hilo ndilo jina halisi la binti huyo, aliitwa SASHA.
Wakati yote hayo yakiendelea David alikuwa kwa mbali akishuhudia. Alishangaa ni vipi anaona vitu ambavyo ama kwa hakika ni yeye pekee ndiye alikuwa na uwezo wa kuona lakini watu wengine hawakuelewa lolote. David hakujua ni vipi amepata uwezo huo, lakini mambo yalibadilika tangu pale alipoliokota lile boksi la SASHA akiwa ndani ya uwanja wa uhuru wakati ule wa kuuga mwili wa Mheshimiwa Rais.
ITAENDELEA...

FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........03
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Alishangaa ni vipi anaona vitu ambavyo ama kwa hakika ni yeye pekee ndiye alikuwa na uwezo wa kuona lakini watu wengine hawakuelewa lolote. David hakujua ni vipi amepata uwezo huo, lakini mambo yalibadilika tangu pale alipoliokota lile boksi la SASHA akiwa ndani ya uwanja wa uhuru wakati ule wa kuuga mwili wa Mheshimiwa Rais.

SASA ENDELEA...
"Tafadhali usimsogelee ni hatari" Aliongea mwanamke mmoja kati ya wale wanne waliomzunguuka Sasha
"Acha niongee naye"
"Hapana Sasha anaweza kukudhuru" Yule mwanamke alisisitiza.
"Hawezi" Sasha alijibu kwa kujiamini kisha akasogea na kusimama mbele ya yule mtu mwenye mavazi meusi, bado alikuwa na ule mkuki mkononi mwake.

"Unathubutuje kusimama mbele yangu tena ukiwa na silaha?" Sasha aliuliza akimtazama yule mwanaume kwa macho makali kiasi cha kuyafanya macho yake yang'ae sana.
Yule mwanaume alianza kutetemeka kwa hofu huku akipiga hatua kurudi nyuma,Sasha naye akazidi kumsogelea.
"Nakuuliza... Unapata wapi ujasiri wa kusimama mbele yangu na silaha!?" Sasha alifoka akiwa karibu kabisa na yule mwanaume ambaye alikosa kabisa ujasiri wa kumtazama Sasha usoni.
Wakati akiwa karibu kabisa kumfikia, yule mwanaume aliinua mkuki wake kwa mara nyingine tayari kumchoma Sasha lakini kabla hajafanya hivyo kufumba na kufumbua ghafula alitokea mwanamke mmoja tofuauti na hawa wanne waliosimama nyuma ya Sasha.
Mwanamke huyu alivaa mavazi yale yale sawa na aliyovaa Sasha na wale wanawake nyuma yake. Yule mwanamke aliushika ule mkuki kwa mkono wake wa kushoto kuuzuia, kisha mkono waka wa kulia alishika kisu kidogo ambacho alikisindilia kwa nguvu katikati ya shingo ya yule mwanaume mwenye mavazi meusi. Sekunde chache baadae yule mwanaume alipasuka vipande vipande mithiri ya puto kisha vile vipande vikaanguka ardhini na mwisho vikatoweka.

"Handan!??" Sasha aliita kwa mshangao ni kama hakutegemea kumuona mwanamke huyo mahali hapo. Ingawa gauni refu alilovaa mwanamke huyo lilikuwa na rangi nyekundu kama ilivyo kwa Sasha na wale wanawake wengine, lakini gauni mwanamke huyu lilikuwa na muundo tofauti huku kiunoni akiwa amevaa mkanda mpana uliochomekwa visu vingi kumzunguuka, aliitwa Handan.

"Hivi mnaelewa mnachokifanya!?" Handan aliongea kwa hasira akiwafokea wale wanawake wanne waliosimama nyuma ya Sasha kumlinda.

"Tulimzuia lakini hakutuelewa.." Alijibu mwanamke mmoja kwa unyenyekevu mkubwa huku wengine wote wakiwa wameinamisha vichwa vyao kuonyesha heshima kubwa kwa Handan ambaye sura yake haikuwa na hata chembe ya masihara.
"Sasha nimeagizwa nikurudishe nyumbani haraka" Alisema Handan.
"Hapana bado sijamaliza kazi yangu, angalia chupa yangu ya machozi bado haijajaa" Alisema Shasha huku akiitoa chupa yake kutoka kwenye mfuko wa gauni. Ilikuwa ni ile chupa aliyokuwa anaitumia kukusanya machozi wakati ule ndani ya uwanja wa uhuru.
Wakati huo wote bado David alikuwa akiwatazama watu hao wa ajabu kwa mbali.
"Eeh! Mungu wangu ni nini hiki nakishuhudia leo" David alijisemea mwenyewe kisha akajikuta anakosa nguvu na kukaa chini. Bado alihisi ni kama yuko ndotoni lakini hakika kila alichokiona kilikuwa ni kweli tupu. Jambo lililozidi kumuumiza kichwa ni kwamba wale watu wa ajabu aliwaona yeye peke yake lakini watu wengine waliokuwa maeneo hayo ya uwanja wa ndege hawakuona chochote. Kuna baadhi walipita hadi karibu kabisa na walipo akina Sasha lakini ni kweli hawakuona kitu.

Wakati David akiwa amekaa pale chini alitazama pembeni yake kisha akayarudisha tena macho yake kule walikokuwa wale watu wa ajabu. Lakini wakati David alipotazama pembeni ni kama kuna watu aliwaona miongoni mwa watu wengi waliokuwa maeneo hayo, akageuka tena kuwaangalia, aliwafahamu, walikuwa ni wanaume watatu.

"Ooh! Kumekuchaa..." Alisema David huku akiinuka taratibu na kuanza kuondoka. Alionyesha anawajua vizuri watu hao, na kitendo cha yeye kuinuka na kuanza kutembea haraka haraka kiliashilia wazi watu hawa si wema kwake. David aliendelea kutembea haraka haraka akikatisha katikati ya watu waliokuwa eneo hilo akawa anageuka nyuma mara kadhaa kuangalia akawaona wale watu bado wanamfuata, akiongeza mwendo nao wanaongeza. Mwisho David akaanza kukimbia, wale wanaume watatu nao wakaanza kumfuata wakimkimbiza.

Huku nyuma Sasha na Handan waliendelea na mazungumzo.

"Wameshajua kuwa umetoka nje ya ISRA ndio maana wamekufuata huku ni hatari Sasha naomba turudi nyumbani ISRA" Alisema Handan.
ISRA ilikuwa ni sehemu wanapotoka Sasha pamoja na watu hao wa ajabu.
"Handan hii ni kazi yangu ya kwanza kufanya nje ya Isra siwezi kurudi nyumbani nikiwa na chupa ambayo haijaja machozi, nitamueleza nini baba yangu ambaye ameniamini sana?" Alisema Sasha.
"Hata ukirudi na chupa iliyojaa machozi lakini tayari umeshakosea Sasha" Alisema Handan.
"Nimekosea nini tena!?"
"Leo hii kuna mwanadamu atakufa kwa ajili yako"
"Nani? Mwanadamu gani atakufa?"
"Yule kijana aliyeokota boksi lako la uono" Alisema Handan na hapo Sasha akamkumbuka kijana David aliyeokota boksi alilodondosha wakati ule akiwa anakusanya machozi uwanjani.

"Hapana, hawezi kufa, haiwezekani niwe sababu ya kifo chake" Alisema Sasha
"Huwezi kuzuia Sasha, mpaka sasa yule kijana anauwezo wa kutuona popote pale tutakapokuwa. Ni kinyume na sheria zetu, lazima auawe"
"Lakini kwa nini afe, hana kosa lolote"
"Sasha unatakiwa kuheshimu kanuni na taratibu zetu tofauti na hapo utakuwa unamuudhi baba yako na atakunyang'anya heshima yote aliyokupa, simama kwenye njia anayotaka baba yako, unajua ni kwa nini alikutuma huku peke yako bila walinzi? Alitaka kukujaribu lakini mpaka sasa umeshafanya makosa mawili unataka kuongeza la tatu kwa kumtetea huyo mwanadamu. Naomba usije ukafungua mdomo wako tena kujaribu kupinga, yule kijana ni lazima tumuue" Handan alieleza kwa kina huku sura yake ikionekana kutokuwa na hata chepe ya masihara.


Upande wa pili tayari wale wanaume watatu waliokuwa wakimkimbiza David walifanikiwa kumkata na sasa walikuwa naye ndani ya gari, mmoja akawa kulia mwingine kushoto huku David akiwa katikati yao. Dereva alikuwa akiendesha gari taratibu, David akawa ametulia akitafakari jambo. Akamtazama yule jamaa wa kushoto kisha akamgeukia yule wa kulia, akaongea...

"Jamani hebu subiri kwanza naombeni msinipeleke kwa yule mwanamke atanifanya kitu kibaya naombeni sana eeh! Jamani" David alikuwa akiomba na kukunja mikono yake, akatazama kulia na kushoto hakuna aliyemjali.

Mwisho gari lilifunga breki nje ya nyumba moja kubwa ya kifahari. Wale watu walimshusha David na kumbeba msobe msobe wakamuingiza ndani ya nyumba hiyo.

David alitupwa katikati ya sebule moja kubwa. Mbele yake ulionekana mwanamke mmoja amekaa kwenye kiti karibu na dirisha akiwa amewapa mgongo. Mara baada ya David kutupwa pale chini mwanamke huyo aligeuka taratibu akiwa ameweka pozi la haja.
David aliinua uso wake kwa hofu akatazamana na mwanamke huyo. Alikuwa ni mwanamke mmoja mrembo sana, mwenye uwezo wa kumvutia kila mwanaume atakayemtazama. Ukialichilia mbali mwanadada huyo kuwa na sura nzuri na umbo linalotuvia hata yeye pia alijua namna ya kujiongezea uzuri wake na kuonekana mrembo mara dufu.
Alikuwa amevaa kijisketi kifupi kilichoacha mapaja yake malaini wazi, huku juu alivaa kijinguo fulani chepesi sana kilichoziba chuchu zake zilizonona mithiri ya embe dodo lililoiva na kusubiri kuliwa, tumbo na kitovu lichokuwa na kipini vyote vilikuwa wazi, hakika alipendeza sana. Mwanadada huyu aliitwa Tesha, Naam ni Tesha Andrea Boniage.
Tesha na David waliatazamana kisha Tesha akaachia tabasamu mwanana lililozidi kuupamba uso wake, lakini tofauti na David yeye alimtazama Tesha huku uso wake ukionekana kujawa na mashaka na wasiwasi mwingi. Kwa dakika kadhaa David alikuwa amesahau kabisa habari za wale watu wa ajabu aliowaona uwanja wa ndege dakika chache zilizopita.

Je nini kitafuata?
Tesha ni nani hasa?
Vipi kuhusu mpango wa David kuuawa na wale watu wa ajabu?
Ungana nami katika simulizi hii iliyojaa Mikasa mingi ya kusisimua na kuburudisha. Vita, visasi,vichekesho,ushirikina,mauaji, miujiza bila kusahau love story nzuri sana ndani yake.
Ni mimi mwandishi wako mahiri SAUL DAVID.
WhatsApp: 0756862047

FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........04
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Lakini tofauti na David yeye alimtazama Tesha huku uso wake ukionekana kujawa na mashaka na wasiwasi mwingi. Kwa dakika kadhaa David alikuwa amesahau kabisa habari za wale watu wa ajabu aliowaona uwanja wa ndege dakika chache zilizopita.
SASA ENDELEA...

"Nitajaribu kuongea na baba, huenda akanielewa. Sitaki binadamu yeyote afe kwa ajili yangu" Sasha aliendelea kushikilia msimamo wako hakuwa tayari kabisa yeye kuwa ni sababu ya mwanadamu kufa.
"Sawa lakini huyo kijana lazima awe chini ya uangalizi kuanzia sasa, Zucc na Femi mtabaki mkimchunga huyu mtu sisi tunarudi nyumbani ISRA" Alisema Handan. Zucc na Femi walikuwa ni kati ya wale wanawake wanne waliosimama nyuma ya Sasha. Waliinamisha vichwa vyao chini kwa heshima kukubaliana na maagizo ya Handan.
"Tunaweza kuondoka sasa Sasha"
Alisema Handan na mwisho wakubaliana hivyo. Sasha Handan pamoja na wale wanawake wawili walishikana mikono na kuanza kupiga hatua kwenda mbele baada ya hapo walipaa juu kwa namna ya ajabu sana na mwisho wakatoweka ghafula.
Lakini kabla hawajatoweka Handan aligeuka nyuma akawapa ishara fulani Zucc na Femi ishara ambayo ilikuwa sio nzuri akiwa na maana kwamba walitakiwa kumuua David na si kumchunga kama alivyosema hapo awali. Zucc na Femi walitikisa vichwa vyao wakionyesha kuelewa ishara hiyo. Wakati Sasha na wenzake wanapaa na kutoweka, pia Ndege iliyoubeba mwili wa marehemu Mheshimiwa Rais nayo ndio ilikuwa inapaa na kuondoka.

Turudi nyumba aliyopelekwa David baada ya kukamatwa.
Tesha alitoa ishara fulani kwa wale vijana waliomleta David. Wote wakageuka taratibu na kuondoka, wakatoka nje ya nyumba, wakimuacha Tesha akiwa na David pekee ndani ya sebule ile kubwa.
Tesha alitembea kwa madaha huku akijibinua binua makalio yake makubwa akafika na kuchuchumaa mbele ya kijana David. Alipata shida kidogo kutokana na aina ya mavazi aliyoyavaa mwanamke huyo mrembo lakini alijitahidi kubana miguu yake vizuri kujisitili.
"Wewe" Tesha aliita huku akiuinua uso wa David kwa kutumia vidole vya mikono yake. David ambaye awali alikuwa ametazama chini aliinua uso wake taratibu akatazamana na Tesha usoni, bado alionekana mwenye hofu.
"Kwa nini unakuwa msanii! Eti wewe? Umetumia pesa zangu halafu hutaki kufanya kazi tuliyokubaliana kwa nini David" Aliuliza Tesha.
"Tesha ni kweli nilikuwa nahitaji pesa kwa ajili ya matibabu ya mdogo wangu lakini ukweli kazi yako siiwezi, nilichukua pesa zako ili tu niweze kumsaidia mdogo wangu kwa haraka. Kama kuna kazi nyingine unaweza kunipa lakini sio hiyo Tesha tafadhali" David alijaribu kujieleza.
"Sasa kwani hii kazi inaugumu gani David!?" Aliuliza Tesha lakini kabla hajajibiwa mara malango ulifunguliwa. Akaingia mwanaume mmoja aliyevalia suti nadhifu yenye rangi ya kijivu. Alionekana kuwa na haraka sana, lakini alipowaona David na Tesha pale sebuleni aliduwaa kidogo.
"Broo!" Tesha aliita
"What's going on"( nini kinaendelea?) Aliuliza yule mwanaume, aliitwa Godfrey kaka yake Tesha.
Tesha hakujibu kitu, Godfrey aliwapita pale walipo akaelekea chumba kingine huku akimuomba mdogo wake Tesha amfuate.
"Nakuja ole wako ukimbie tena" Tesha alimtisha David kisha akaondoka kuelekea chumbani akimfuata kaka yake
David alibaki amekaa pale chini sebuleni akiwa hajui afanye nini. Nguvu ya pesa aliyokuwa nayo msichana huyu ilikuwa ni ngumu kumkimbia.
"Au nihame Dar?" Aliwaza David lakini akakumbuka alikuwa akiishi na mama na mdogo wake mgonjwa ambao wote wanamtegemea yeye kwa kila kitu.
Wakati David akiwaza hayo ghafula kupitia kioo kikubwa cha dirisha kwa mara nyingine tena aliwaona wale wanawake wa ajabu waliovaa magauni mekundu wakiwa wamesimama nje ya nyumba hiyo wakimtazama. Safari hii walikuwa wawili tu yaani Zucc na Femi. David aliogopa sana, sasa alikosa uvumilivu wa kuendelea kuwatazama wanawake hao ambao awali aliwaona na kuhisi yuko ndotoni lakini sasa walimfuata kila anapokwenda. Na safari hii walikuwa wamekuja kuyaondoa maisha yake kama walivyoagizwa na Handan.

Wakati huo Tesha na kaka yake Godfrey walikuwa ndani ya chumba cha kulia chakula wakifanya mazungumzo.
"Usiniambie kuhangaika kote huku ni kwa ajili ya yule mpuuzi wako Felix?" Aliuliza Godfrey huku akiwa amemtolea macho makali mdogo wake Tesha.
"Of course ni kwa ajili ya Felix kaka" Tesha alijibu
"Ooh! My Goodness, hivi wewe ni mara ngapi nakueleza kuwe Felix hakupendi tena! He's no longer in love with you, hakupendi hakutaki Tesha kwa nini huelewi lakini mdogo wangu" Godfrey alifoka.
"Sawa lakini mimi bado namhitaji kaka! Najua bado ananipenda kuna mahali tu nilimkosea ndio maana amekuwa mgumu kiasi hiki kaka! Can't you think. Ni mwanaume gani anaweza kukupa vitu vyote hivi na bado akawa hakupendi. Amenipa kila kitu nilichonacho sasa, utajiri wangu na wako vyote vimetoka kwake leo hii unadiliki vipi kusema Felix hanipendi" Tesha aliongea huku akirusharusha mikono yake.
"Ndio maana nakwambia mdogo wangu hivi vitu tulivyopata basi tuvitumie yeye si hakutaki basi huna budi kuachana naye, move on! Unamng'ang'ania wa nini? Mbona wanaume wengi tu, istoshe wewe ni mwanamke mwenye pesa zako, unaweza kuchagua mwanaume yeyote unayemtaka"
"Lakini kaka.."
"Kaka kitu gani Tesha"
"Nataka kujaribu njia ya mwisho kama nita prove kweli Felix hanitaki basi nitaachana naye i promise you"
Kimya kikatawala kwa muda...
"Nini unataka kufanya?" Godfrey akauliza
"Nataka nimtishie kuwa nataka kufunga ndoa na mwanaume mwingine, nataka tupige picha za uchumba mimi na David kisha picha hizo zisambae. Nihakikishe hata yeye huko Marekani alikoenda anaziona hizo picha kisha nitaona reaction yake atafanya nini" Alieleza Tesha
"So ndio maana umemleta David hapa?"
"Ndiyo na nilishamlipa tayari"
"Sasa kwa nini umemchagua David na sio mtu mwingine, nasikia umeenda kumteka kijana wa watu huko msibani Tesha why this?" Aliuliza Godfrey, Tesha akatabasamu.
"Unacheka!?"
"No kaka! Ni vile hujanielewa, namtaka David kwa sababu ni kijana mzuri, handsome. Namjua Felix vizuri anawivu sana, nikimtumia David atarudi hapa mkuku mkuku"
"Eee..."
"Yes bro"
"Basi umu..." Alisema Godfrey lakini kabla hajamalizia sentensi yake mara ghafula wanamuona David anakuja walipo huku anakimbia, akafika na kuanguka miguu mwao.

"Kuna watu...kuna watu wa ajabu hapo njee... Wanatisha..wa..wa ...." David aliongea kwa papara kiasi cha kuwafanya Godfrey na Tesha watazamane, wakawa hawamuelewi.


Upande wa pili Sasha Handan pamoja na wale wanawake wawili walionekana wakiibuka kutoka ndani ya maji ya bahari moja kubwa sana ambayo haikuonekana mwisho wake. Macho yao yalikuwa yakiwaka na kutoa mwanga mweupe kwa muda kisha yakarudi katika hali ya kawaida.

Walitembea hadi nchi kavu, walipo kanyaga tu ardhi mavazi yao wote yakabadilika kutoka rangi nyekundu na kuwa meupe tena yaling'aa sana.
Naam, sasa walikuwa ISRA mahali wanapotoka watu hawa wa ajabu.

Je, nini kitaendelea?
David atakuwa salama?
Sasha atafanya nini akigundua Handan kamgeuka?
Huyu Felix ni nani hasa?

ITAENDELEA....

FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........05
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Walitembea hadi nchi kavu, walipo kanyaga tu ardhi mavazi yao wote yakabadilika kutoka rangi nyekundu na kuwa meupe tena yaling'aa sana.
Naam, sasa walikuwa ISRA mahali wanapotoka watu hawa wa ajabu.

ILIPOISHIA...

"Kuna watu...kuna watu wa ajabu hapo njee... Wanatisha..wa..wa ...." David aliongea kwa papara kiasi cha kuwafanya Godfrey na Tesha watazamane, wakawa hawamuelewi.

Godfrey alipiga hatua akatembea kuelekea sebuleni huku Tesha akimfuata nyuma taratibu, David naye akawa anawafuata akiwa bado mwenye hofu kubwa. Wale watu wenye magauni mekundu walimtisha mno.
Baada ya Godfrey kufika pale sebuleni akaangaza macho yake huku na kule hakuona kitu. Akageuka na kumtazama mdogo wake kisha akamuonyesha ishara kuwa hakukuwa na kitu, hali ilikuwa shwari kabisa.

"Wewe unatuchezea akili sio?" Tesha aliuliza huku akigeuka na kumtazama David kwa macho makali.
"Hapana, nasema kweli Tesha niliona watu hapo dirishani"
"Wako wapi sasa mbona hawaonekani?"

David alipiga hatua akasimama sebuleni kuhakikisha kama ni kweli hakuna kilichoonekana, ajabu ni kwamba hakukuwa mtu tena pale dirishani, wale Zucc na Femi walipotea ghafula.
David aliduwaa kwa muda kisha taratibu akageuka na kumtazama Tesha.
"Unaniangalia nini? Wako wapi hao watu sasa? Acha kucheza na akili zetu David hizo janja janja zako nazijua tangu kitambo ila kaa ukijua kazi yangu utaifanya tu upende usipende kwa sababu pesa yangu umeshachukua" Alisema Tesha.
"Lakini Dada Tesha u..."
"Usiniite hivyo David, mimi sio dadako. Niite mchumba, mchumba wangu... Sawa David, unatakiwa kuzoea hivyo kuanzia sasa, unatakiwa uwe muigizaji mzuri. Sitaki mtu yeyote agundue kuwa uchumba wangu mimi na wewe ni wa kugushi sawa sawa!?"
"Sawa dada Tesha"
"Oh! My Goodness, unakichwa kigumu David..." Sasha alilalamika.
"Tesha...!" Mara Godfrey aliitaa
"Yes bro"
"Hebu angalia pale" Alisema Godfrey akinyoosha kidole chake kuelekea dirisha ambalo awali David ndipo alipowaona wale wanawake wa ajabu.
"Kuna nini?" Aliuliza Tesha akiwa hajaelewa ni nini kaka yake anamtaka atazame, akajitahidi kuangalia kwa makini.
"Kioo! Kioo kimevunjika" Alijibu Godfrey huku akitembea kusogea dirishani, Tesha naye akamfuata.
Ni kweli walipofika dirishani walishuhudia kioo kikiwa kimetengeneza mpasuko. Ilikuwa ni jambo la kushangaza sana kwani vioo hivyo vilikuwa ni vigumu na imara sana haikuwa rahisi hata kidogo kuvunjika kirahisi namna ile.
Godfrey na Tesha walitazamana wakiwa na maswali kichwani mwao yasiyo na majibu kisha wote kwa pamoja wakageuka na kumtazama David. Sasa kwa kiasi walianza kuyaamini maneno yake.
Godfrey akapiga hatua kutoka nje ya nyumba

"Unaenda wapi kaka?"
"Nataka niwaulize walinzi kama wameona lolote" Alijibu Godfrey huku akifungua mlango akatoka nje.


Upande wa pili tayari Sasha na walinzi wake walikuwa wameingia ndani ya mji wao, ISRA.
ISRA ulikuwa mji mkubwa sana huku watu kadhaa na makazi yao wakionekana kuishi ndani ya mji huo. Waliishi maisha yao kama ilivyo kwa binadamu wa kawaida, ingawa ISRA haikufanana na maisha ya Dunia hii ya sasa bali maisha yao yalionekana ni watu wanaoishi maisha ya zamani sana.
ISRA hakukuwa umeme wala maghorofa hakukuwa magari wala ndege, ni maisha ambayo yalionekana kama ni Dunia ya miaka elfu moja iliyopita. Hakukuwa Rais wa ISRA bali kiongozi mkuu wa mji huo ambaye aliitwa Gu Gamilo na huyu ndiye alikuwa baba mzazi wa Sasha.

Zilikuwa zimepita dakika kadhaa tangu Sasha na wenzake waingie ndani ya mji wa ISRA baada ya kuchomoza kutoka ndani ya maji ya bahari. Ajabu ni kwamba wakiwa ISRA hawakuwa na uwezo wa kupotea na kutokea mahali pengine kama iliyokuwa walipokuwa nje ya ISRA.
Sasa walionekana wakiwa wanakatiza katika ya mji wa ISRA kila mmoja akiwa juu ya farasi wake waliotembea taratibu sana. Alitangulia Handan akafuata Sasha na nyuma yake walifuata wale wanawake wawili. Walipita barabarani huku wakiwapungia mikono na baadhi ya watu ambao walikuwa wakiendelea na harakati mbalimbali za maisha ndani ya mji wa ISRA. Mavazi meupe ya kung'aa sana waliyovaa Sasha na wenzake yaliwafanya waonekane tofauti kabisa na watu wa mji wa ISRA. Ni kweli walikuwa ni watu wa tofauti kabisa kutokana na namna walivyokuwa wakisalimiwa kwa heshima na kila waliyekutana naye, watu waliokuwa barabarani walipisha na kusimama mbali wakiuacha msafara huo wa mwana wa Gu Gamilo upite.

"Mama kwani hawa ni akina nani?" Aliuliza mtoto mmoja wa kike yapata umri wa miaka minne hivi yeye na mama yake walitoka sokoni na ndipo hapo walipokutana na msafara wa Sasha, wakawa wanasubiri wapite ndipo nao wavuke barabara.

"Hawa wanaitwa WALINZI WA NAFSI mwanangu" Alijibu yule mama
"Mmh! walinzi? Wanalinda kitu gani?"
"Wanalinda NAFSI zilizopo ndani yaa miili yetu. Maisha yetu yapo mikononi mwao ni wao ndio wanaamua uishi au ufe"
"Kwa hiyo ni watu wabaya!?"
"Hapana mwanangu, hawa ni wazuri saana. Si unawaona jinsi wanavyong'aa hawana ubaya wowote. Bila wao kusingekuwa na AMANI ulimwenguni. Hawa watu wamesimama katikati ya WEMA na UBAYA, katikati ya MWANZO na MWISHO" alieleza yule mama huku akiwa ameachia tabasamu akijua kabisa maneno aliyokuwa akiongea ni magumu kueleweka kwa mtoto huyo mdogo mwenye umri wa miaka minne pekee.

ITAENDELEA...
ISRA kunanini?
Vipi kuhusu usalama wa David?
Hawa WALINZI WA NAFSI ni watu gani hasa?
TUKUTANE TENA KESHO.

FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........6-7
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Alieleza yule mama huku akiwa ameachia tabasamu akijua kabisa maneno aliyokuwa akiongea ni magumu kueleweka kwa mtoto huyo mdogo mwenye umri wa miaka minne pekee.

Je, nini kitaendelea...?

SONGA NAYO....
Sasha na msafara wake waliendelea kusonga mbele taratibu. Wakiwa na farasi zao, walitembea umbali mrefu wakiyaacha mbali sana makazi ya watu. Sasa wakawa wanafuata barabara moja iliyopita pembeni ya msitu mnene
"Mbona kuna ukimya sana eneo hili?" Aliuliza Sasha. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutoka nje ya ngome (ikulu) ya baba yake na nje ya ISRA pia, hivyo alikuwa hafahamu mambo mengi zaidi ya yale aliyosimuliwa tu.

"Huu msitu haruhusiwi mtu yeyote kusogea wala kuvuka zaidi ya wale wanye vibali vya kuingia Ikulu tu" Alieleza Handan.
"Vipi kuhusu hii barabara inaelekea wapi mbona kama inaingia ndani zaidi ya huu msitu?" Sasha aliuliza swali lingine huku akinyoosha kidole chake kukielekeza ilipo barabara nyingine iliyokuwa ikikatisha kuelekea ndani ya msitu huo wenye miti mirefu isivyo kawaida.

"Hii barabara ni yakuelekea kwa mtu mmoja maarufu sana hapa ISRA, mtu ambaye anajua mambo mengi kutuhusu sisi WALINZI WA NAFSI, mambo mazuri na mabaya" Handan alieleza kwa kifupi.
"Unamaanisha Bi Noha?"
"Ndiyo! Huyo huyo, kumbe unamfahamu?"
"Niliwahi kusimuliwa tu habari zake. Niliambiwa anaweza hata kukueleza hatima yako, yaani mambo yatakayotokea mbeleni?"
"Ndiyo inaaminika hivyo, lakini ni wachache sana ambao waliwahi kubahatika kukutana na Bi Noha, huwa haonekani kirahisi akienda unaweza kutembea msitu mzima na usimpate"
"Kwa nini sasa?"
"Inaaminika kuwa Bi Noha mwenyewe huwa anachagua watu wa kukutana nao na kwa sababu maalum si kila mtu anaweza kumuona, hata baba yako aliwahi kumuona mara moja tu kwa kipindi chote hiki... Na tangu siku baba yako alipoonana na Bi Noha ndipo waasi waliibuka ndani ya mji wa ISRA"
"Waasi gani?"
"Wapo wengi tu, mmoja wapo ni yule aliyetaka kukuchoma mkuki"
Maelezo haya kwa kiasi yalimshangaza Sasha, kwa miaka mingi sana amekuwa akisimuliwa habari za mtu huyo mwenye kuzijua siri nyingi za ISRA na watu wake. Alikuwa akitamani sana kuonana naye lakini kauli ya Handan ilimkatisha tamaa kwa asilimia fulani.

Wakati wakizidi kusonga mbele ghafula katikati hali ya kushangaza waliona vitu vyeusi mfano wa vimondo vikishuka kwa kasi kutoka angani na kufumba na kufumbua walijikuta wamezunguukwa na watu wengi mno walio valia mavazo meusi.
Watu hawa walifanana kabisa na yule mtu aliyetaka kumshambulia Sasha kwa kutumia mkuki wakati ule.
Walivaa makoti meusi yenye kofia kubwa kichwani huku mikononi mwao wakiwa wameshikilia mikuki.

"Nilijua tu hatuwezi kufika nyumbani bila kukutana na hawa jamaa" Alisema Handan huku akichomoa visu vyake na kuvishika sawa sawa, wale wanawake nyuma ya Sasha nao wakafanya hivyo kisha wakashuka kwenye farasi zao.

"Wewe usishuke baki hapo, tutapambana nao" Alisema Handan.
Mji huu wa ajabu ISRA si kwamba ulikuwa na amani siku zote la hasha, bado uongozi wa Gu Gamilo baba yake SASHA ulikuwa ukiingia kwenye vita ya mara kwa mara na viumbe hawa wa ajabu wanaovaa nguo nyeusi. Na hii ndio sababu pamoja na kwamba Sasha aliagizwa na baba yake kukusanya machozi ya watu akiwa peke yake lakini bado alikuwa akifuatiliwa na walinzi wake kwa siri.

Sekunde chache baadaye vita kali ilianza kati ya walinzi wa Sasha wakiongozwa na mlinzi mkuu Handan dhidi ya wale watu wa ajabu waliovalia makoti meusi. Haikuwasumbua sana kupambana nao kwani Handan na wale wanawake wawili walikuwa ni wajuzi wakubwa wa mapigano istoshe walionekana kuwa na nguvu za ajabu ndani yao. Kasi yao ilikuwa si ya kawaida, walitumia visu vidogo viwili lakini katika sekunde moja waliweza kuwaondosha maadui wawili au zaidi. Kila adui waliyemchoma kisu alipasuka vipande vipande kisha kuanguka ardhini na kupotea.

Wakati hayo yakiendelea taratibu Sasha alirudi nyuma na farasi wake akafika hadi pale inapoanzia ile barabara ya kuelekea kwa yule mtu wa ajabu Bi Noha.
Sasha aligeuka nyuma kutazama akaona Handan na wale wanawake walinzi wako bize kupambana na maadui. Haraka Sasha alivuta kamba za farasi wake ambaye alishika njia kuingia msituni kwa kasi sana. Tamaa ya Sasha ilikuwa ni kuonana na Bi Noha, alijua kama akimuomba mlinzi wake mkuu Handan waende wote kumtafuta angemkatalia hivyo aliona autumie mwanya huo kumtoroka.
Farasi wa Sasha alikimbia kwa kasi sana akipenya katikati ya msitu huo mnene. Lakini jambo la kushangaza huku nyuma anakotoka njia ilikuwa ikijifunga na kupote, Sasha hakujua hilo aliendelea kwenda mbele kwa kasi.


Upande wa pili nyumbani kwa mwanamke mrembo Tesha, wanajikuta wanaingia kwenye wimbi la hofu mara baada ya kuona kioo cha dirisha kimepasuka ghafula na wakilinganisha na maelezo ya David kuwa aliona watu wa ajabu pale dirishani, hofu iliwajaa.
Dakika chache baadae Godfrey kaka yake Tesha alirejea tena ndani.
"Walinzi wamesemaje..?" Aliuliza Tesha
"Hawajaona mtu yeyote nao pia wanashangaa kioo kimepasuka vipi ghafula hivi" Alieleza Godfrey kisha akageuka kumtazama David usoni, David akakwepesha macho yake.

"Wewe, unauhakika uliona watu hapa au ni wewe ulipasua hiki kioo ulikuwa unajaribu kutoroka?" Aliuliza Godfrey akiwa amemkazia macho David.
"Hapana mkuu, nimepasua na nini sasa si mngesikia sauti"
"Una uhakika? Hao watu uliowaona wakoje, ulishawahi kuwaona? au ukiwaona tena unaweza kuwakumbuka?"

"Aa..nd...hapana" David alijibu akisita, alijua kama akijibu ndiyo basi angeulizwa maswali mengi asiyo na majibu yake ingawa ni kweli ni kwa mara ya pili anawaona watu hao wa ajabu.

"Tesha si unaona mtu wako anavyo babaika kujibu, hiki kioo kavunja yeye" Alisema Godfrey kisha akaondoka na kuingia chumbani sekunde chache akatoka akiwa na briefcase mkononi akafungua mlango na kuondoka zake.
Tesha na David walibaki kimya wanatazamana kwa dakika kadhaa.
"It doesn't matter umevunja wewe au nani, cha muhimu kwa sasa tujadili namna utakavyoifanya kazi yangu sawa David"
Kimya..
"Unanisikia lakini Dav?"
"Nimekusikia Tesha lakini nikuulize kwanza swali, hivi ni kwa nini unataka tuwe wapenzi wa kuigiza why?" Aliuliza David.
Ni kweli kabisa David alikuwa hafahamu kiundani sababu za Tesha kufanya hivyo, hakuwa akielewa chochote kuwa Tesha anafanya hivyo ili tu kumpima aliyekuwa mpenzi wake yaani Felix ambaye ameonekana hamtaki tena licha ya kwamba amemuachia utajiri mkubwa sana. Tesha alikuwa ni mwanamitindo maarufu sana hapa nchini, alijua wazi kama atayaweka wazi mahusiano yake na David na kutangaza kuwa wanatarajia kufunga ndoa na mwanaume huyo hivi karibuni basi lazima taarifa hizi zingemfikia Felix huko Marekani.

"Nitakwambia sababu za kufanya hivi, ila kwanza kubali kuifanya kazi yangu David.. Au una mpenzi unaogopa atakuacha? it's okay twende tukaongee naye akitaka pesa pia nitampa muhimu akuruhusu na asitoe siri kama mahusiano yetu ni ya kuigiza"
"No,no,no sina mpenzi kwa sasa niko mwenyewe..."
Alisema David huku akiinua mikono yake kuonyesha msisitizo, alipomtazama Tesha akaona anamuangalia kwa macho fulani hivi yanayozungumza, ni kama hakutegemea kupata jibu kama hilo kutoka kwa David.
"Nini?" Aliuliza David baada ya kuona Tesha anamuangalia sana.
"Nothing, sasa kama uko single kwa nini inakuwa ngumu wewe kufanya kazi yangu....?" Aliuliza Tesha lakini kabla David hajajibu swali hilo mara simu yake iliita akaipokea haraka.

"Ndio mimi David...what....sawa nakuja" David aliongea kwa kifupi kisha akakata simu. Alionekana kuwa na huzuni, Tasha aliligundua hilo.
"Nini shida?"
"Mama anaumwa sana kapelekwa hospitali, natakiwa kwenda sasa hivi" Alisema David kisha akageuka tayari kuondoka.
"So unaondoka vipi kuhusu..... mmh! ...okay twende nikusindikize basi tutachukua gari yangu" Tesha aliongea na kubadilisha mada haraka.

Nje ya nyumba ya kifahari ya Tesha, walionekana wale wanawake wawili waliotumwa kumuua David ajabu ni kwamba walinzi waliokuwa wanazunguuka zunguuka eneo hilo wala hawakuwa wakiwaona. Mpaka sasa ni David pekee ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuwaona watu hao wa ajabu.
"Inakuwaje tumeshindwa kuingia ndani ya hii nyumba Zucc?" Aliuliza Femi
"Nashindwa kuelewa hii ni mara yangu ya kwanza inatokea kushindwa kuingia ndani ya nyumba ya binadamu, nahisi kuna kitu hakipo sawa" Alijibu Zucc.

Ni kweli kabisa wakati ule David amewaona wakiwa wamesimama dirishani walijaribu kupenya kuingia ndani wakitumia nguvu walizonazo lakini ajabu walishindwa kuingia ndani na mwisho wakajikuta wanaishia kupasua kioo.
"Kuna nguvu ya ziada ipo kwenye hii nyumba, tutauliza wakubwa zetu tukirudi ISRA. Tumsubiri tu huyu mwanadamu atoke tumuue akiwa nje."alieleza Femi. Wakakubaliana wamsubiri David mpaka atakapotoka.
Haukupita muda, mwisho wakawaona Tesha na David wakitoka nje ya nyumba hiyo wakiwa wameongozana wakaingia ndani ya gari moja kati ya magari saba ya kifahari yaliyoegeshwa pale nje, wakakaa siti za nyuma.
"Nawapeka wapi bosi?" Aliuliza Dereva wa Tesha. Tesha akageuka na kumtazama David yeye ndiye alikuwa na jibu la swali hilo, wakatazamana.

"Tupeleke hospitali ya Sanitas, pita barabara ya mwai kibaki" Alisema David.
"Jitahidi kwenda haraka tunawahi" Tesha alisisitiza kisha akageuka na kumtazama David, wakatazamana tena. Tesha akatazama pembeni haraka.
"Ee! Mungu wangu ujinga gani huu nawaza" Aliwaza tesha huku akiweka mkono wake juu ya kifua chake upande wa kushoto.
Wakati huo Dereva aliondosha gari kwa kasi mara baada ya kutoka nje ya geti akafuata barabara aliyoelekezwa. Wote hawakujua kuwa nyuma wanafuatiliwa na wale wanawake wa ajabu waliotumwa kumuua David, yaani Femi na Zucc.

Wakati gari waliyopanda David na Tesha ikizidi kwenda kwa kasi, upande wa pili Sasha akiwa juu ya farasi alionekana akiendelea kwenda mbele kwa kasi akipita katikati ya msitu ule mnene asijue huku nyuma alikotoka barabara ilikuwa ikijifunga.

Je, nini kitafuata?

ITAENDELEA...
(Ndugu msomaji bado tunatengeneza mizizi ya simulizi yetu bomba, jitahidi sana kuzingatia majina ya wahusika wakuu wa simulizi hii ili isikuchanganye...... (David, Tesha, Sasha, Felix, Gu Gumaro, Handan na wengine tutakao kutana nao mbele)
Endelea kufurahia SIMULIZI bomba ya SAUL DAVID... 0756862047.


FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........08
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...

Wakati gari waliyopanda David na Tesha ikizidi kwenda kwa kasi, upande wa pili Sasha akiwa juu ya farasi alionekana akiendelea kwenda mbele kwa kasi akipita katikati ya msitu ule mnene asijue huku nyuma alikotoka barabara ilikuwa ikijifunga.
Je nini kitafuata?

SASA ENDELEA....
Femi na Zucc wanawake waliotumwa na Handan kuhakikisha wanamuua David walionekana wakiwa wamesimama pembeni ya barabara. Tayari walikuwa wameshapanga ni namna gani watatekeleza mauaji ya kijana huyo ambaye amejikuta anaingia matatani tangu pale alipolishika boksi la Sasha kwa mikono yake.

"Wanakuja" Alisema Femi.
Zucc akiwa anatazama pembeni aligeuka kutazama upande wa pili wa barabara kwa mbali akaliona lile gari la Tesha ambalo kwa sasa David pia alikuwa ndani yake linakuja kwa kasi sana.
Femi na Zucc walikuwa wamepanga kusababisha ajali ambayo baadae itapelekea kifo cha David ili lengo lao litimie.

"Jitahidi kuwa makini Femi, ni NAFSI ya David pekee ndio tunaihitaji, hatakiwi kufa mtu mwingine tofauti na David"
"Usijali Zucc, ndani ya gari kuna watu wawili na watatu ni David, ni rahisi kuwalinda wengine na kumuua mmoja" Alisema Femi huku akisogea na kusimama katikati ya barabara.
Gari la Tesha likiwa limekaribia kufika pale walipo, Femi aliinua mkono wake wa kushoto akasogeza kiganja chake karibu na mdomo wake. Mara kuna moshi mweupe ukajitokeza juu ya kiganja cha mkono wake. Femi akavuta pumzi ndefu akiwa tayari kuupuliza ule moshi ambao ungekwenda moja kwa moja kwa dereva wa Tesha kisha kumchanganya na mwisho kusababisha ajali. Ajabu ni kwamba dereva wa Tesha hakuwa akimuona Femi pale katikati ya barabara.
David naye ambaye pengine angeweza kumuona hakuwa akitazama mbele, yeye alikuwa amejiinamia huku habari za mama yake kulazwa hospitali zikionekana kumchanganya sana.

"Femi achaaaa....!!" Mara Zucc alipiga kelele kumzuia mwezake.
Kwa kasi ya ajabu Femi aliruka na kusogea pembeni ya barabara tayari alishajua ni kwa nini mwenzake kamzuia asisababishe ajali ile waliyokusudia.
Kulikuwa na basi la abiria linakuja kutoka upande wa pili nyuma ya Femi, na endapo kama angelisababishia ajali gari la Tesha basi kulikuwa na hatari ya kutengeneza ajali nyingine ya basi hilo lililokuwa karibu kabisa.
Mwisho basi lile pamoja na gari la Tesha vilipishana salama salmini bila shida yoyote. Hii ikawa ni mara ya pili David ananusurika kuuawa.
"Huyu mtu inaonekana ana bahati ya pekee" Alisema Femi huku akionekana kukasilika mara baada ya kuipoteza nafasi ile.
"Tumfuate, safari hii tunamuondoa" Alijibu Zucc kisha wakashikana mikono wakapaa umbali wa mita kadhaa kisha wakapotea ghafula.

Upande wa pili katikati ya ule msitu mnene Sasha aliendelea kwenda kwa kasi akiwa juu ya farasi wake. Tayari alikuwa ameshaingia ndani sana ya msitu huo baada ya kwenda kwa zaidi ya dakika kumi.
Akiwa katika mwendo mara ghafula farasi akasimama. Ilikuwa ni hali iliyomshangaza Sasha kiasi, akajaribu kumpiga farasi wake asonge mbele lakini farasi akagoma kusogea, akajaribu tena na tena hali ikawa ni ile ile.
"Ooh! nini shida kipenzi changu" Alisema Sasha huku akimpapasa farasi wake lakini ghafula farasi alimrusha na kumtupa pembeni. Sasha alianguka chini akaumia mgongo, kabla hajafanya lolote farasi wake alikimbia huku akilia kwa sauti akatokomea kwenye msitu mnene.
Sasha akiwa pale chini ndipo aliposhtuka baada ya kugundua kuwa ile barabara aliyokuwa akiifuata imepotea ghafula, sasa alikuwa mwenyewe katikati ya msitu mnene.
Alijikongoja na kusimama kisha akawa anaangaza macho yake huko na kule. Hakuwa akiogopa hata kidogo mazingira kama hayo kwake yalikuwa ni ya kawaida, hayakumtisha.
Sasha alikuwa amedhamiria kwa dhati kuonana na Bi Noha kwa ghalama yoyote ile, alikuwa na shauku kubwa ya kuonana na mtu huyo.
Mara taratibu upepo ulianza kuvuma, upepo ambao ulikuwa ukiongezeka kadri muda unavyozidi kwenda. Sasha aliendelea kusimama imara huku akiangalia pande zote kwa ajili ya usalama wake. Hatimae upepo ukawa ni mkali sana kiasi cha kusababisha kimbuka kikubwa eneo lile.
Sasha alikimbia na kwenda kujificha nyuma ya mti mmoja mkubwa lakini hii haikutoshosha kimbunga kilikuwa ni kikali kiasi cha kuanza kung'oa miti iliyopa juu kama vipande vya karatasi, hali ilitisha mno. Sasha aliendelea kuushikilia ule mti lakini mwisho nao uling'oka na kupaa juu. Ajabu ni kwamba Sasha yeye hakubebwa na kile kimbunga, alibaki amejikunyata pale chini kwa zaidi ya dakika 5 mwisho hali ilianza kutulia na baadae kukawa na ukimya wa ajabu.

Sasha aliinua uso wake taratibu kutazama, alishangaa kuona mazingira ya eneo hilo yamebadilika kabisa. Lilikuwa ni eneo jeupe sana kila mahali kulikuwa kweupe, sakafu juu na pembeni kote kulikuwa kweupe. Mbele yake aliona mlango wa mbao ukifunguka akatoka mwanamke mmoja aliyevaa gauni refu lenye rangi ya machungwa. Alimtazama Sasha kisha akaachia tabasamu pana.

"Haujachelewa Sasha" Alisema yule mwanamke huku akimuonyesha Sasha ishara kuwa asimame na kumfuata. Bila woga Sasha alifanya hivyo, akapiga hatua na kuingia ndani kupitia ule mlango, baada ya kuingia yule mwanamke akaufunga.

Upande wa pili tayari David na Tesha walifika hospitali mahali alipolazwa mama yake David kama alivyoelezwa kwenye simu.
David alishuka kwenye gari upesi akawa anaelekea ndani ya hospitali hiyo. Tesha naye alishuka sekunde chache baadae, akawa anaongea na simu huku akipiga hatua taratibu sana kuingia hospitali.
David akiwa mwenye haraka tayari alishapata maelekezo chumba alicholazwa mama yake akawa anapiga hatua ndefu ndefu kuelekea huko.
Ilikuwa ni wodi ya wagonjwa wa kike chumba namba saba. David alifika akasimama mlangoni, akavuta pumzi ndefu kisha akaitoa taratibu. Alinyonga kitasa cha mlango akafungua taratibu na kuingia.
Uso kwa uso David akagonganisha macho yake na macho ya mdogo wake wa kike, aitwae Tatu. Wakati huo akawaona madaktari zaidi ya watatu wakiwa wamesimama kukizunguuka kitanda alicholazwa mama yake.

Upande wa pili nako mara baada ya Sasha kuingia ndani kupitia ule mlango wa mbao, sasa alikuwa ndani ya chumba kimoja kipana sana, mbele yake aliona wanawake watatu wakiwa wamesimama kukizunguuka kitanda ambacho juu yake alilala bibi kizee moja aliyeonekana kuzeeka sana.
Mara baada ya Sasha kuingia wale watu waliosimama waligeuka kwa pamoja kumtazama. Mmoja kati yao alikimbia nakwenda kumkumbatia Sasha kwa nguvu.

Tatu mdogo wake David alipomuona kaka yake ameingia alikimbia na kwenda kumkumbatia kwa nguvu huku akilia machozi.

Yule mwanamke aliyemkumbatia Sasha naye alikuwa akilia machozi.

"Kaka" Tatu aliita
Wakati huo daktari mmoja akasogea pale walipo
"Wewe ndio David?"
"Ndio mimi Daktari"
"Mama yako alikuwa akikusuburi sana tunakuacha ufanye naye mazungumzo kisha uje ofisini" Alisema daktari

Upande wa pili...
"Sasha" Yule mwanamke aliyemkumbatia Sasha aliita.
"Abeee"
"Bi Noha, amekusuburi kwa zaidi ya miaka 10, aliamini lazima ipo siku utakuja kabla ya kifo chake, hatimaye leo umekuja, haujachelewa Sasha. Tunakuacha ufanye naye mazungumzo muhimu" Alisema yule mwanamke.

Je, nini kitafuata?

Ni nini kinaendelea kati ya matukio haya mawili ya sehemu mbili tofauti lakini yenye kufanana?
Nini maana yake?


FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........09
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Kaka" Tatu aliita
Wakati huo daktari mmoja akasogea pale walipo
"Wewe ndio David?"
"Ndio mimi Daktari"
"Mama yako alikuwa akikusuburi sana tunakuacha ufanye naye mazungumzo kisha uje ofisini" Alisema daktari


Madaktari wote walitoka nje wakamuacha David afanye mazungumzo na mama yake pale kitandani kama alivyoomba. Mwili wake ulionekana kudhoofika sana, wakati huo hakuwa na uwezo hata wa kijitikisa.

"Da..david mwanangu" Mama David aliongea kwa taabu kidogo
"Naam mama niko hapa, pole sana mama Mungu atakusaidia utapona"
"Asante, so..sogea karibu mwanangu"
David akakaa kitandani na kusogea karibu na mama yake.
"David"
"Naam mama"
"Naomba ufanye kitu kimoja mwanangu"
"Kipi mama? Nakusikiliza.."
"Oa mwanangu"
Ilikuwa ni kauli iliyomfanya David atoe macho kwa mshangao, hakuwa ametegemea kama mama yake ataongea kitu kama hicho.
"Umesema?" David Aliuliza akahisi labda amesikia vibaya
"Mama yako nakaribia kufa David, sina mda mrefu sana wakuishi. Natamani sana kukuona unaoa kabla sijafa moyo wangu uta...."
"Mama unaongea nini, huwezi kufa"
"David, najua unajua kabisa mimi sio wa kuishi muda mrefu, za...za...zawadi yangu ya pekee ninayotamani kuiona kutoka kwako ni kukuona ukioa mwanangu"
"Lakini mama mimi bado sijawa tayari kuishi na mwanamke kwa sasa napambana kuwahudumia wewe na mdogo wangu Tatu"
"Achana na mimi, ugonjwa wangu hautibiki hata hivyo umri wangu umeenda. Tafuta mwanamke atakaye saidiana na wewe kumtibu mdogo wako Tatu" Mama David aliongea kwa msisitizo.


Wakati maongezi haya yakiendelea bado Tesha alikuwa amesimama mbele ya mlango wa kuingia ndani ya hospitali hiyo akiwa anaongea na mtu kwenye simu, baadaye akamaliza maongezi na kukata. Punde wakatokea waandishi wa chombo kimoja cha habari.

"Mambo vipi Miss Tesha" Alisalimia yule dada mwandishi akionyesha uchangamfu wa hali ya juu huku mpiga picha akiwa makini na kazi yake.
"Poa poa mambo vipi" Tesha aliitika
"Tunaweza kufanya mahojiano kidogo please kama hutojali?"
"No no, hapa ni hospitali shoga, sio mahala pake"
"It's okay tupo kazini pia, kuna watu tumekuja kuchukua taarifa zao hapa walinusurika na ajali ya treni, just a minute Tesha.. tupe muda kidogo tu"
"Sawa dakika moja"
"Poa poa.."
"Siku hizi huonekani, wala hufanyi promo ya mitindo yako mipya kama tulivyo kuzoea... Shida ni nini au umepumzika? watu wameenda mbali na kusema Tesha ni mjamzito je, kuna ukweli wowote kuhusu taarifa hizi?"
"Hao ni watu sio mimi...Kila mmoja ana uhuru wa kuongea kila anachofikiri ni sahihi. Ukweli ni kwamba nilisimama kidogo na ishu za kikazi ila watu wangu bado waliendelea kuwajibika so hakuna kilicho haribika na habari njema ni kwamba wiki hii nimeingia ubia na kampuni kubwa ya mavazi na mitindo nchini Marekani GMK Fashion Group, kwa hiyo tegemeeni makubwa kutoka kwangu..."
"Na vipi kuhusu msimamo wa mahusiano yako kwa sasa, still upo single kama unavyosema siku zote?"
"Hahahah Nooo! Am not single... soon nitaenda kumuweka wazi mkalia ini wangu"
"Wow tutegemee lini miss Tesha..."
"Nimesema soon, so ni suala la kukaa na kusubiri, as you know mimi nikiongea kitu lazima nikitimize"
"Sawa Tesha, Hivi karibuni umekuwa uki...."
"Hapana jamani inatosha next time"
Alisema Tesha akikatisha mahojiano yale mara baada ya kumuona David anatoka kinyonge sana nje ya hospitali. Waandishi wa habari walimshukuru kwa ushirikiano wake na mwisho wakaondoka wakati huo David akafika pale alipo.
"Vipi David kwema?" Aliuliza Tesha, David akawa kimya
"Mama anaendeleaje?"
"Tunaweza kukaa mahali tuongee kidogo Tesha?" Badala ya kujibu swali David naye akauliza swali
Tesha alitulia kwa muda kisha akakubali ombi hilo. Walitoka na kuongozana hadi kwenye mgahawa mmoja karibu na hospitali hiyo, wakatafuta sehemu iliyotulia wakakaa tayari kwa mazungumzo.
"Nambie David" Tesha alianzisha mazungumzo baada ya kuona David amekaa kimya kwa muda mrefu. Wakati huo mhudumu alileta vinywaji walivyo agiza na kuondoka.

Wakati huo huo wale wanawake wawili wasioonekana machoni pa watu yaani Femi na Zucc walitokea ghafula kwenye kona moja ya mgahawa huo. Wakawa wanamtazama David akiwa kwenye mazungumzo muhimu na Tesha.

"Tesha" David aliita
"Nambie"
"Nimekubali kuifanya kazi yako ila na mimi nina sharti langu moja.."
"Woow! Mchumba si ndio huyu, haya niambie ni sharti gani? Au unataka nikuongezee pesa kwa ajili ya matibabu ya mama yako. Sio shida niambie tu ni kiasi gani wanahitaji"
"Hapana sio hivyo Tesha"
"Owk! Ni sharti gani hilo?"
"Badala ya kuishia kuigiza uchumba kama unavyotaka tunaweza kuigiza hadi ndoa pia, yaani tukaoana kabisa" Alisema David kauli iliyomfanya Tesha aliyekuwa anakunywa kinywaji apaliwe ghafula.
"Eti nini?"
"Ndiyo, tu-fake ndoa... Na harusi iwepo" David alisisitiza.
Tesha alimtazama David usoni akaona kabisa anamaanisha kile anachokisema.
"Mungu wangu" Aliwaza Tesha...
Awali Tesha alitaka kuigiza mahusiano na David kwa ajili tu ya kumnasa mwanaume wake Felix ili amrudie lakini sasa David naye anakuja na wazo jipya la ndoa akiwa na lengo la kumridhisha mama yake mzazi kama alivyomuomba.

Upande wa pili...
Wale wanawake waliokuwa wamekizunguuka kitanda alicholala yule bibi mzee sana walitoka wote na kumuacha Sasha pekee.
Sasha alimtazama yule bibi kwa sekunde kadhaa kisha akapiga hatua kumsogelea. Akiwa amekaribia kumfikia Sasha akasimama.

"Sogea binti yangu usiogope" Alisema yule bibi(Bi Noha) huku akiwa bado ameyafumba macho yake.
Sasha akasogea karibu zaidi, yule bibi akafungua macho yake.
"Nimekuwa nikikusubiri kwa miaka mingi sana mwanangu, nilijua ipo siku utakuja kabla sijafa"
"Bila shaka wewe ndio Bi Noha?"
"Ndio mimi mjukuu wangu, haya niambie kwa nini unataka uniona?" Aliuliza Bi Noha.
Sasha akawa kimya, ni kweli kwa kipindi kirefu alikuwa anashauku kubwa ya kuonana na Bi Noha lakini katu hakuwahi kuwaza ni kwa nini hasa anatamani kuonana na bibi huyo.
"Hahahah, hahahah hujui...umekuwa ukitamani tu kuniona na hujui kwa nini hahah" Bi Noha alicheka sana kiasi cha kumfanya Sasha aone ndani ya kinywa cha bibi huyo kilichokuwa na upungufu wa meno karibu yote.
"Ngoja nikusaidie kujibu mjukuu wangu... HATIMA.... Hatima ndio imekufanya uje hapa mjukuu wangu, ilikuwa ni lazima tu uje kuonana na mimi uyasikie maneno yangu. Ni Hatima yetu mimi na wewe kukutana ndio maana na mimi sijafa mpaka sasa"
"Unamaana gani kusema Hatima Bi Noha?"
"Kila kitu na kila mtu ataishi kulingana na Hatima yake Sasha umekuja kwa sababu ni hatima yako. Sasha mjukuu wangu kwa sasa ISRA ipo mikononi mwako pamoja na wanadamu ambao tunazilinda NAFSI zao"
Alisema Bi Noha, Sasha akawa hajamuelewa kabisa. Bi Noha akajikongoja akainuka na kuketi kitandani kisha akaendelea kuongea.

"Sasha mjukuu wangu, unakazi kubwa ya kufanya katika ISRA wewe na huyu kijana...Mnaweza kuamua kuharibu au kutengeneza" Alisema Bi Noha huku akinyoosha kidole chake kuelekea ukutani, Sasha akatazamana uelekeo wa kidole cha bi Noha. Ukutani ilijitokeza picha ya kijana mmoja ambaye sura yake haikuwa ngeni machoni kwa Sasha, alikuwa ni David. Picha mfano wa video ilionyesha wakati ule Sasha alipokutana na David pale uwanja wa uhuru wakati akikusanya machozi.
Naam, ni David huyu huyu ambaye kwa sasa anaomba kufungua ndoa ya kuigiza na mwanadada mrembo Tesha.

"Huyu mwanadamu hakikisha unamlinda kwa gharama yoyote ile, bila yeye ISRA itateketea na kupotea kabisa. Nitakwambia ni kwa nini..." Alisema Bi Noha.

ITAENDELEA...

FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........10
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Huyu mwanadamu hakikisha unamlinda kwa gharama yoyote ile, bila yeye ISRA itateketea na kupotea kabisa. Nitakwambia ni kwa nini..." Alisema Bi Noha.



Sasha aliitazama picha ya David pale ukutani ambayo ilitumia kama sekunde 30 mwisho ikatoweka, akageuka na kumtazama Bi Noha.

"Sijakuelewa Bi Noha, huyu mwanadamu anahusiana vipi na ISRA kuteketea?" Aliuliza Sasha.
Bi Noha alitulia kwa muda kisha akaongea..

"Inaonekana hujui chochote Sasha... Hebu nikuulize kwanza swali mjukuu wangu, unajua kazi ya hayo machozi uliyoagizwa na baba yako ukayakusanye kutoka kwa wanadamu?"

"Hapana, baba aliniambia atanieleza kila kitu pindi nitakaporudi"

"Hahah! Gu Gamilo hajahawi kubadilika... Sawa, nakuuliza swali lingine Sasha unajua ni kazi gani kubwa tunayoifanya sisi WALINZI WA NAFSI, kazi ambayo ilitufanya tukapewa nguvu zaidi ya wanadamu, kisha tukatengwa huku ISRA?"
Sasha alitulia kwa muda akionekana kufikiri jambo kisha akajibu...
"Tunalinda NAFSI za wanadamu"
"Nafsi zipi?"
"Zipi?"
"Ndiyo zipi? Si kila nafsi tunapaswa kuilinda.."
"Hapana hilo simfahamu Bi Noha"
"Ni sahihi lazima usijue kitu, baba yako amefanya makosa makubwa kukufungia Ikulu kwa kipindi chote hiki, bado unamengi sana ya kujifunza...hujui kitu. Sikiliza Sasha kwa miaka mingi sana nimekaa hapa nikisubiri siku kama ya leo ifike siku ambayo nitakutana na mtu ambaye ameibeba hatima ya ISRA"

"Kivipi bibi, naomba unielekeze tafadhali..."

"Nitakuhadithia simulizi moja ya miaka mingi iliyopita kabla hata hujazaliwa..." Alisema Bi Noha lakini kuna kitu cha tofauti Sasha alikigundua kutoka kwa Bi Noha.
Kadri muda unavyozidi kwenda ngozi ya Bi Noha ilizidi kuongezeka makunyazi na kubadilika rangi kuwa nyeupe. Hata sauti ya yake ilianza kukwaruza na kufifia taratibu sana. Sasa hakuwa na nguvu tena ya kuendelea kukaa, akalala kama alivyokuwa mwanzo. Kitu pekee ambacho aliendelea kufanya ni kuongea. Alisema...

"Hapo awali mji wa ISRA ulikuwa ukiongozwa na watu wawili, wa kwanza alikuwa ni baba yako Gu Gamilo wa pili alikuwa ni baba yako mkubwa yaani kaka yake na baba yako aliitwa MAGNUS. Kwa bahati mbaya Magnus aliingiwa na tamaa ya uongozi, akatamani kila kitu kiwe cha kwake.
Hakuwa kiongozi mzuri kama wengi walivyo tarajia, alivunja taratibu nyingi na miiko ya Walinzi wa nafsi kwa makusudi kabisa. Mwisho tamaa yake ikazidi kuwa kubwa akaupeleka utawala wake hadi kwa wanadamu ambao ni dhaifu sana kwetu. Magnus hakuishia hapo alitamani kuitawala ISRA akiwa yeye peke yake. Akatengeneza njama ya kufanya mapinduzi lakini kwa bahati nzuri baba yako aliweza kumzuia kabla hajaleta madhara makubwa ndani ya ISRA. Magnus alikamatwa akanyang'anywa kila kitu na baadae akatupwa nje ya ISRA. Magnus hakuwa na uwezo wa kurudi tena ISRA lakini tayari alikuwa ameshatengeneza jeshi kubwa na matabaka ndani ya ISRA. Wale waliokuwa wanamtii waligeuka na kuwa waasi, na huo ndio ukawa mwanzo wa uvunjifu wa amani na kuwepo kwa uasi ndani ya ISRA, ni hao ambao mpaka leo wanapambana na baba yako kila kukicha. Lakini si kwamba habari za Magnus ziliishia hapo la hasha, kwa miaka yote hii Magnus amejificha katikati ya wanadamu na anajipanga upya kuja kupambana kwa mara nyingine kuuludisha utawala wake. Magnus ni nyoka hatari ndani ya ISRA, huko aliko anaanda jeshi kubwa la kupambana na sisi lakini pia hata ndani ya ISRA pia analo jeshi kubwa ambalo linasubiri siku atakayolejea kwa mara nyingine"
Bi Noha alieleza mambo ambayo ama kwa hakika yaliibua maswali mengi kichwani kwa Sasha.

"Kwa hiyo Bi Noha ni lini Magnus amepanga kuja kuivamia ISRA? Kama amekuwa akijipanga kwa muda mrefu kwa nini mpaka leo hajawahi kuvamia?" Aliuliza Sasha

"Hana uwezo wa kuingia ISRA na mtu pekee ambaye anaweza kumzuia Magnus asirudi ISRA milele ni huyu mwanadamu niliyekuonyesha, ndio maana nimekwambia unatakiwa kumlinda huyu kijana kwa gharama yoyote ile" Alisema Bi Noha

"Lakini nawezaje kumlinda mwanadamu ikiwa mimi niko huku ISRA?"

"Sasha mjukuu wangu Hatima ndio itaamua kila kitu, kitu muhimu na cha pekee ambacho nataka kukukumbusha ni kwamba hautakiwi KUPENDANA na mwanadamu. Katu usije kuruhusu hisia zako zikampenda mwanadamu" Bi Noha aliongea kwa msisitizo na hapo ngozi yake ya mwili ikawa ni nyeupe sana na nyepesi kiasi cha kuanza kuchanika katika baadhi ya maeneo mwilini mwake. Lakini Bi Noha bado hakuacha kuongea, hapo ndipo Sasha alipogundua kuwa kadri bibi huyo anavyoongea ndivyo anavyozidi kuchoka na kunyong'onyea.

"Bi Noha usiendelee kuongea tafadhali" Alisema Sasha.
"Usijali mjukuu wangu, ni salama..."
Alisema Bi Noha kisha akaachama mdomo wake na kuuacha wazi.

"Amekufa" Ilisikika ya kike kutokea nyuma ya Sasha. Alipogeuka akawaona wale wanawake aliowakuta awali ndani ya chumba hicho wanarudi tena mkononi mwao wakiwa wamebeba jeneza. Ni kweli Bi Noha alikuwa amekufa.



Upande wa pili...
Bado maongezi kati ya David na Tesha yalikuwa yakiendelea.

"Badala ya kuishia kuigiza uchumba kama unavyotaka tunaweza kuigiza hadi ndoa pia, yaani tukaoana kabisa" Alisema David kauli iliyomfanya Tesha aliyekuwa anakunywa kinywaji apaliwe ghafula.
"Eti nini?"
"Ndiyo, tu-fake ndoa... Na harusi iwepo" David alisisitiza.

Tesha alimtazama David usoni akaona kabisa anamaanisha kile anachokisema.

"Mungu wangu" Aliwaza Tesha, kisha akauliza.

"Kwa nini, mbona ghafula hivyo?"

"Kama wewe ambavyo hujaniambia sababu ya kutaka tuigize mahusiano ya uchumba na mimi sitokuambia kwa nini nataka tuigize ndoa" Alijibu David.

"No! Lakini mimi jambo langu ni rahisi Uchumba huwezi kulinganisha na ndoa, ujue nitatakiwa kukwita mume wangu. Unaona ni rahisi?"

"Tesha unaogopa labda unahisi baadae nitasema tuachane alafu nitake nusu ya mali zako, hapana sio hivyo. Tunaweza kuingia mkataba kama ukitaka" Alieleza David, lakini bado ulikuwa ni mtihani mgumu kwa Tesha kuamua.

"Nahitaji muda wa kufikiri David hili jambo sio dogo, na wala sijui ni kwani nini wewe unalirahisisha namna hii" Alijibua Tesha.

Lakini wakati wakiendelea na mazungumzo haya kwa mbali alionekana mwanaume mmoja aliyevalia nguo nyeusi na kofia inayoziba uso wake akiwapiga picha Tesha na David kwa siri pale mgahawani.

Zucc na Femi nao pia walikuwa hawachezi mbali, bado waliendelea kurandaranda mle mgahawani kuangalia ni namna gani wanaweza kutengeneza tukio ambalo litapelekea kifo cha David.
Ajabu ni kwamba licha ya wao kuwa na nguvu zaidi ya binadamu wa kawaida lakini hawakuruhusiwa kuua moja kwa moja, hii ilikuwa ni kinyume kabisa na taratibu zao (walinzi wa nafsi). Sheria yao ni kwamba hawaruhusu kuua mwanadamu kwa mikono yao bali kutengeneza tukio ambalo litasababisha kifo cha mwanadamu.

"Basi ni heri tuwekane wazi tu kwa nini nataka uchumba na wewe kwa nini unataka ndoa ili twende sawa maa..." Alisema Tesha lakini mara simu yake iliyokuwa ndani ya mkoba wake mdogo ilianza kuita, wakati akitaka kuichukua kwa bahati mbaya akasukuma ule mkoba wake ukawa unadondoka chini. David aliwahi haraka kutaka kuudaka lakini tayari Tesha alishaushika David akaishia kuudaka mkono wa Tesha.
Walibaki wanatazamana kwa sekunde kadhaa huku mkono wa David ukiwa juu ya mkono wa Tesha. Taratibu Tesha akahisi mapigo yake ya moyo yanaanza kubadilika. Sasa ilikuwa ni mara ya pili kwa Tesha kupatwa na hali hii...

Je nini kitafuata?
Nini kinaendelea kati ya Tesha na David?
Ni nani anawapiga picha kwa siri?
Femi na Zucc watatengeneza tukio gani kumuua David?
Vipi kuhusu Sasha?
Je ni kweli Magnus yupo?
Na kama yupo ni nani na yuko wapi?

ITAENDELEA...

FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........11
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Walibaki wanatazamana kwa sekunde kadhaa huku mkono wa David ukiwa juu ya mkono wa Tesha. Taratibu Tesha akahisi mapigo yake ya moyo yanaanza kubadilika. Sasa ilikuwa ni mara ya pili kwa Tesha kupatwa na hali hii...
Je nini kitafuata?

SASA ENDELEA....
Haraka Tesha alitoa mkono wake kutoka kwenye mkono ya David huku akijikohoresha na kujifanya kama hakuna kitu kilichotokea.
"Mi naondoka..." Alisema Tesha
"Mbona ghafula?" Aliuliza David wakati huo tayari Tesha alishasimama.
"Ninadharula" Tesha alidanganya, kisha akachukua mkoba wake na kuanza kuondoka.
"Nitakupigia David tutaongea wakati mwingine..."
""Lakini hauna namba ya..." Alisema David, lakini alishindwa kumalizia sentesi yake kwani tayari Tesha alishafika mbali.

Tesha alitembea haraka haraka mara baada ya kutoka nje ya mgahawa huo alimpigia dereva wake simu akamataka asogeze gari. Sekunde chache baadae gari ilifika Tesha akafungua mlango na kuingia ndani. Baada ya kukaa kwenye kiti Tesha alivuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu, bado mapigo yake ya moyo yalikuwa hayajatulia kabisa.

"Vipi bosi uko sawa?"
"Eeh! Niko sawa kwani vipi?" Tesha alijibu huku akijaribu kuvunga kama hakuna kilichotokea lakini ukweli hakuwa sawa. Hata yeye alikuwa akijishangaa ni kwa nini anapatwa na hali hiyo mara zote anapotazamana na David usoni au hata akimgusa.

"No haiwezi kuwa hivyo...bado nampenda Felix wangu" Tesha alijisemea mwenyewe kwa sauti ya chini mara baada ya kuwaza kuwa pengine hisia zake zinataka kuhamia kwa David.
Aliamini haikuwa rahisi hata kidogo kwa 'super star' kama yeye kuzama penzini na kijana wa mtaani asiye na mbele wala nyuma. Licha ya kwamba tayari alishamsifia sana David kwa kaka yake kuwa ataweza kumfanya mpenzi wake Felix kupata wivu na kurudi haraka Tanzania.


David alibaki ndani ya mgahawa ule akiwa amekaa vile ile kama alivyoachwa na Tesha.
"Sasa shida yangu nini... Au nimekosea kumshika? Lakini mbona ilikuwa ni bahati mbaya tu?" Alijiuliza David huku akiutazama mkono wake aliotumia kumshika Tesha.
"Hivi ni kwamba mimi ni masikini sana hadi kuugusa mwili wake nakuwa nimekosea?" David aliendelea kujiuliza maswali.
Lakini wakati akiendelea kujiongelesha mwenyewe mara alipotazama chini aliona pochi ndogo sakafuni. Kumbe wakati ule Tesha amekaribia kuudondosha mkoba wake ile pochi ilichomoka kutoka kwenye mkoba huo ikadondoka chini, hakuna aliyeona.

"Ohoo!" Alisema David wakati akiangaza macho yake pande zote kuangalia kama kuna anayemuona ndani ya mgahawa ule kisha taratibu akaivuta ile pochi kwa mguu wake wa kulia, akainama na kuiokota.
Licha ya kwamba David alifahamu fika kuwa pochi hiyo ni ya Tesha lakini hakusita kuifungua na kuangalia vilivyomo ndani.

"Woow! Mambo ya dollar..." Alisema David huku akitabasamu mara baada ya kuona noti nyingi za kigeni(dollar) zikiwa zimepangwa vizuri ndani ya pochi hiyo, akaendelea kupekuwa.
Baadae aliichomoa picha moja ndogo iliyokuwa ndani ya pochi hiyo ya Tesha. Ilikuwa ni picha iliyokatwa upande mmoja, na upande uliobaki ulimuonyesha Tesha akiwa ameweka pozi moja mujarabu huku akiwa amevalia nguo nyepesi za beach. Alikuwa amevaa Chupi na sidiria pekee huku akiwa ameweka pozi la kujibinua kiasi, alipendeza sana na kufanana na wale wanawake wa Kibrazili pale Ipanema Beach.

"Ooh! Mashallah Mungu fundi jamani... Huyu dada ni mzuri hakuna mfano...eti anataka tuwe wachumba kwa kuigiza nitaweza kweli? hebu muangalie lips zake mmh! Au ni malaika na hatujui" David aliendelea kujiongelea mwenyewe huku akimalizia kinywaji kilichosalia katika glasi aliyotumia Tesha . Kwa muda mfupi alijikuta anasahau habari za mama yake kule hospitalini.
Akazidi kuipekuwa pochi ya Tesha, mara akakutana na kitu ambacho hakutegenea. Ilikuwa ni paketi mbili za mipira ya kiume(Condom).

"Huhuuu hahahaha Tesha Tesha.... hahahha" David alicheka sana.

Wakati huo Zucc na Femi walikuwa nyuma yake hatua kadhaa kutoka pale alipokuwa, wakawa wanamtazama huku Femi akionekana kifurahishwa sana na Tabia za David, akawa anatabasamu kila wakati. Tofauti na Zucc yeye alikuwa amevaa sura ya kazi, wakati wote alikuwa akimtazama David kwa macho makali huku akipiga hesabu ni namna gani atayaondoa maisha ya mwanadamu huyo ambaye mpaka sasa tayari walikuwa wamepoteza nafasi mbili za kumuua.

Mwisho David alirudisha kila kitu mahali pake ndani ya ile pochi, akawaza aihifadhi tu atampatia Tesha watakapoonana kwa mara nyingine. Akaiweka ile pochi mfukoni kisha akainuka tayari kwa kuondoka.

"Samahani kaka haujalipa?" Mara sauti ya mhudumu wa kike ilisikika kutokea nyuma yake. David akasimama na kumtazama dada huyo ambaye alipiga hatua na kusimama mbele yake.
"Mbo..mbona yule dada niliyekuwa naye alishalipa" David alijibu huku akijiumauma, ukweli hakuwa hata na senti tano mfukoni, aliogopa.
"Hapana hajalipa kaka yangu"
"Sasa kwa nini hamkumdai anapoondoka?" David alifoka huku akiangalia njia akiwaza pengine akimbie.
"Tuna mdai vipi wakati wewe upo na ulibaki hapa?"
"Aaaah! Sawaa.. umesema sijalipa eeh!" Alisema David huku safari hii akiachia tabasamu pana kiasi cha kumshanga yule dada, tayari alikumbuka kuwa mfukoni anayo pochi ya Tesha yenye pesa za kutosha.
Kwa mbwembwe sana akaingiza mkono mfukoni akatoa ile pochi na kuifungua, akachomoa noti moja na kumpatia yule.

"Keep change" Alisema David,
Kauli hii ilimnyima uhuru Femi akajikuta nacheka kwa sauti, hakika David alionekana kumfurahisha sana.
Sauti hii ya kicheko ilipenya vizuri kwenye masikio ya David akageuka haraka kutazama. Mara hiyo Zucc na Femi wakapotea ghafula.
David aliangaza macho yake huku na kule hakuona mtu, kulia kushoto mbele nyuma kote hakukuwa mtu.
"Wewe ndio umecheka?" David alimuuliza yule dada muhudumu ambaye aliikunja sura yake akionekana ushangazwa na swali la David. Yeye hakuwa ameisikia sauti hiyo ya kicheko, kama ilivyokuwa kwamba ni David pekee ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuwaona watu hao wa ajabu vivyo hivyo hata sauti zao aliweza kuzisikia yeye peke yake.
"Kwa hiyo haujacheka si ndiyo...!!" David alijijibu swali lake mara baada ya kuona yule dada ameonyesha hajui kitu.

Baada ya Zucc na Femi kupotea ghafula walitokea pembeni ya mlangoni nje ya mgahawa.
"Unakuwa kichaa sasa Femi, ni kipi kimekuchekesha?"
"Nisamehe bure Zucc huyu mwanadamu anavituko sana, kanifurahisha..."
"Yaani badala ya kuumiza kichwa kufikiria tunamuua vipi wewe unacheka kweli Femi?"
"Nimesema samahani Zucc, vipi umeshapata jibu tunamuua vipi?"
"Hapana, nimewaza tumuue moja kwa moja bila kutafuta sababu za kibinadamu la sivyo tutachelewa kurudi ISRA"
"Nini? Unataka tumuue moja kwa moja, hapana hatutakiwi kufanya hivyo Zucc tunavunja sheria" Alisema Femi wakati huo David alionekana akitoka mgahawani akawa anaondoka zake. Hakuwaona Zucc na Femi pale pembeni ya mlango.

Zucc alichomoa kile kisu chake kidogo akawa anapiga hatua kumfuata David kwa nyuma.
"Zucc usifanye hivyo tafadhali.." Aliongea Femi akijaribu kumzuia mwenzake, lakini Zucc hakumjali.

Je nini kitafuata?
David atakuwa salama?
Vipi kuhusu Sasha kule kwa Bi Noha?
Ni nani aliwapiga picha David na Tesha pale mgahawani?

ITAENDELEA....

FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........12
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Zucc alichomoa kile kisu chake kidogo akawa anapiga hatua kumfuata David kwa nyuma.
"Zucc usifanye hivyo tafadhali.." Aliongea Femi akijaribu kumzuia mwenzake, lakini Zucc hakumjali.

SASA ENDELEA...

Upande wa pili, msituni alipo Sasha....
"Amekufa" Ilisikika sauti ya kike kutokea nyuma ya Sasha. Alipogeuka akawaona wale wanawake aliowakuta awali ndani ya chumba hicho wanarudi tena mkononi mwao wakiwa wamebeba jeneza. Ni kweli Bi Noha alikuwa amekufa.
Wale wanawake waliweka jeneza chini kisha wakaubebe mwili wa bibi kizee(Bi Noha) na kuuweka ndani ya jeneza lile baada ya hapo wakaliinua jeneza na kuingia nalo ndani ya chumba cha pili.

Sasha alibaki katika hali ya kuduwaa asijue afanye nini, kila kitu kilichokuwa kinatokea kilikuwa ni kigeni kwake. Kwanza kabisa alikuwa akiyatafakari maelezo ya Bi Noha ambaye kwa sasa ni marehemu. Ni maelezo yaliyokuwa na mafumbo makubwa kiasi cha kumfanya Sasha atamani kujua zaidi lakini ndio hivyo Bi Noha hakuwepo tena.

Bado hakujua ni namna gani ataweza kutekeleza jukumu alilopewa la kuhakikisha anamlinda kijana David ambaye ni mwanadamu wa kawaida tofauti kabisa na yeye.

Wakati akiwa bado amesimama mara kikasikika kishindo kikubwa kikiambatana na mtikisiko mnene wa ardhi. Wale wanawake wakatoka haraka hadi pale alipo Sasha, walionekana kuwa kwenye hali ya mshtuko kama ilivyo kwa Sasha. Wakampita na kutoka nje kabisa ya chumba kile.

"Msitu wetu umefikia kikomo chake...!!" Alisikika mmoja kati ya wale wanawake akiongea. Wakawa wanatazama juu.
Hali ya hewa ilikuwa inabadikika taratibu, ule mwanga mweupe ulitoweka, huku mawingu yakionekana kwenda kasi sana angani. Upepo nao ukazidi kuongezeka kiasi cha kuyafanya magauni marefu waliyovaa wale wanawake yapepe mithiri ya bendera kwenye mlingoti wake.
"Tumtoe Sasha hapa haraka..." Mwanamke mwingine akadakia. Wakati huo tayari Sasha naye alikuwa ametoka nje. Alistaajabu kuona hali ya hewa ilivyobadilika ghafula.

"Sasha..!" Mwanamke mmoja kati ya wale wanne aliita na kumsogelea Sasha, akamshika mikono yake yote miwili kisha akaongea kwa hisia sana.

"Sasha, mwisho wetu umefika...tayari Bi Noha ameikamilisha kazi yake. Hakikisha unayafuata na kuyatimiza yale yote aliyokwambia bila kukosea. Umepewa jukumu zito ambalo kuna wakati utaona kama linakuelemea, usikate tamaa endelea kupambana kwa ajili ya ISRA. Kuna mambo mengi makubwa na magumu utakutana nayo kuanzia dakika hii ukiwa ISRA na hata utakapotoka nje ya ISRA. Utakutana na vita ya kila aina kutoka kwa ndugu zako pamoja na Wanadamu. Wewe ni MLINZI WA NAFSI Hatima ya walinzi wa nafsi wote wa ISRA umeibeba wewe..."
Aliongea yule mwanamke huku maelezo yake yakikatishwa na mtikisiko mkubwa wa ardhi ulioanza taratibu na kuongezeka kadri muda ulivyozidi kwenda

"Muondoe hapa haraka, muondoeeee......" Wale wanawake wengine walipiga kelele kali mno kwa pamoja, kelele zilizopasua anga na kusikika upande wa pili nje kabisa ya msitu huo.


Handan mwanamke mahiri aliyepewa jukumu la kulinda usalama wa Sasha mtoto wa mkuu wa ISRA Gu Gamilo alionekana pembeni ya msitu alioingia Sasha. Uso wa Handan pamoja wa na wale wanawake wawili alioambatana nao ulionyesha kuwa na wasiwasi mwingi.
Tayari walishamaliza kupambana na wale viumbe wa ajabu ndipo wanapogundua kuwa Sasha hayupo amewatoroka.
Baada ya kufuatilia nyayo za farasi wakagundua kuwa Sasha aliingia msituni jambo ambalo hakuruhusiwa kabisa kufanya.
Handan alikuwa akiogopa sana kwani alimjua Mkuu wa ISRA ni mtu asiye na masihara hata kidogo endapo akigundua kuwa Handan amefanya uzembe na kumuacha Sasha akaingia ndani ya msitu huo basi kifo kilikuwa ni halali yao.

"Sasha huyu mtoto!!" Handan alilaani huku akipiga hatua kwenda mbele na kurudi nyuma, alikuwa amechanganyikiwa si kidogo.
"Tutanyaje Handan" Aliuliza mmoja kati ya wale wanawake wawili
"Tufanyaje sasa! Tutamsubiri atoke, na iwe kheri tu atoke salama la sivyo Mkuu atatuua wote..." Alijibu Handan.
"Kwa nini tusijaribu kumfuata tukamtafute kuliko kuendelea kusubiri hapa"
"Nini?" Handan Aliuliza huku akimtazama yule mwanamke kwa macho makali
"Aa.. na..naogopa anaweza kupatwa na jambo baya wakati tuna nafasi ya kuingia msituni kumsaidia"
"Kwani huzijui sheria za ISRA? Tangu lini ikaruhusu kuingia kwenye huu msitu bila ruksa, hata Mkuu Gu Gamilo mwenyewe akitaka kuingia ni lazima atoe taarifa kwa viongozi wote ISRA. Iweje sisi tuingie? Na usije thubutu kuufungua mdomo wako kuongea mbele za watu kuwambia kama Sasha aliingia kweye huu msitu. Itakuwa ni kesi kubwa ambayo hata Gu Gamilo mwenyewe hawezi kuibeba" Handan aliongea kwa msisitizo, akatulia kwa muda kisha akaendelea...

"Unajua adhabu atakayopata Sasha kama ikifahamika kuwa ameingia kwenye huu msitu? Unajua? Hujui... Ni kifo, watamuua... Sasa unahisi baba ataweza kumuhukumu mtoto wake kifo? Na kama akishindwa unajua nini kitatokea? Viongozi maadui wa Gu Gamilo wataleta shinikizo la Sasha kuuawa kitakachofuata ni vita. Alafu kwanza unaongea ongea tu tumfutate tumfutate, tunamfuata kupitia njia gani wakati njia haipo imepotea" Handan alizidi kufoka.
Ni kweli maelezo yake yalikuwa sahihi kabisa, kama utakumbuka wakati Sasha akikimbia na farasi wake kuingia msituni njia ilikuwa ikijifunga. Na hii ndio ilikuwa alama pekee kuashilia kama kuna mtu kaingia ndani ya msitu huo wa ajabu.

Wakati Handan na wenzake wanahangaika wasijue cha kufanya ghafula unatokea msafara wa watu karibu ishirini wakiwa na farasi wakija kwa kasi.

"Ooh! Mambo yameharibika sasa" Alisema Handan mara baada ya kuuona msafara huo.
"Ni akina nani kwani?" Aliuliza mmoja kati ya wale wanawake aliokuwa pamoja nao.
"Ni DUMAYO mjomba wake Sasha. Huyu mwanaume ni nuksi tupu, ni moja kati ya watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa sana hapa ISRA" Alijibu Handan wakati huo msafara wa Dumayo ukawa karibu kuwafikia, wakapunguza kasi za farasi wao.

"Hakikisha mahuonyeshi wasiwasi wowote, Dumayo hatakiwi kujua kama Sasha kaingia ndani ya huu msitu" Alisema Handan na mwisho Dumayo na msafara wake wakafika walipo, wakasimama.
Handan na wale wanawake wawili waliinamisha vichwa vyao chini kwa heshima.
Dumayo akiwa katikati ya msafara huo aliwatazama Handan na wenzake mmoja baada ya mwingine huku uso wake ukionekana kujawa na dharau ya kiwango cha juu.

"Handan mwanamke shujaa mlinzi wa Sasha... Ni wapi mnatoka wakati huu? Usiniambie leo hii kwa mara ya kwanza Sasha karuhusiwa kutoka nje ya Ikulu?" Aliuliza Dumayo
Handan akainua uso wake na kumtazama Dumayo usoni, alionyesha kuwa na chuki kali dhidi ya mtu huyu. Ukiacha yule Magnus aliyekuwa na tamaa ya uongozi na baadae kufanya uasi lakini akaishia kufukuzwa na kutupwa nje ya ISRA, Dumayo naye alikuwa mmoja kati ya watu waliokuwa na tamaa ile ile kama Magnus.

"Si nje ya Ikulu tu, ametoka hadi nje ya ISRA..." Alijibu Handan kauli iliyomshtua kiasi Dumayo. Alibinua midomo yake kisha akatoa ishara fulani akiwataka watu wake wasonge mbele, nao walikuwa wakielekea Ikulu vilevile.
Waliendelea na safari lakini baada ya kupiga hatua kadhaa Dumayo akasimamisha farasi wake tena, ni kama vile aliona kitu kisicho cha kawaida. Akageuka na kuanza kurudi pale walipo akina Handan.

Kabla hajawafikia Dumayo akawa anaangaza macho yake kuelekea msituni, ni kama kuna jambo alikuwa anahakikisha. Mwisho akawafikia akina Handan

"Iko wapi njia ya kuelekea kwa Bi Noha? Kunamtu kaingia msituni? Ni nani? Sasha?" Dumayo aliuliza maswali mfululizo, Handan na wenzake wakainamisha vichwa vyao chini, hakuna aliyejibu.
Tayari Dumayo alikuwa na jibu sahihi. Aliamini kwa vyovyote vile lazima kuna mtu kaingia msituni na lazima atakuwa ni Sasha. Na huo ndio ulikuwa ukweli wenyewe. Dumayo akatabasamu na kuwaza...

"Hii ni nafasi nyingine ya kumnasa Gu Gamilo, kwisha habari yake...Anampenda sana Sasha hawezi kuchomoka kwenye hili.... Sasa ni yeye au Sasha mmoja wao ni lazima afukuzwe nje ya ISRA kama walivyomfanya Magnus. Nitahakikisha nashikilia hili suala mpaka kieleweke..." Aliwaza Dumayo

Mara ghafula wote walihisi miguu yao ikitetemeka, farasi wakaanza kupiga kelele na kurudi nyuma. Ilikuwa ni tetemeko la ardhi lililoanza ghafula.
Kufumba na kufumbua waliona kimbunga cha ajabu kikichomoza na kupanda juu kutokea katikati ya msitu ule, kimbunga hicho kiliambatana na mtikisiko mkubwa wa ardhi kiasi cha kusababisha ardhi kuanza kutengeneza mpasuko na kutitia chini katikati ya msitu ule.
Hali ilikuwa inatisha sana. Si Handan si Dumayo wala wafuasi wake, wote walipanda farasi na kukimbia mbali kabisa na msitu huo ambao sasa ulikuwa kwenye majanga makubwa. Miti ilikuwa iking'orewa na kurushwa juu huku mingine ikititia na kuzama ardhi. Msitu wa Bi Noha ukawa unatoweka kwa namna ya ajabu mno.

"Maskini Sasha! Nini kimetokea huko...? Ooh! Jamni naogopa mimi... Tafadhali toka ukiwa salama we binti" Aliwaza Handan.
Tukio hili liliutikisa mji wa ISRA, ndani ya dakika tano tu tayari ISRA yote ilikuwa na taarifa za kile kinachoendelea katika msitu wa Bi Noha.
Mkuu wa ISRA Gu Gamilo baba yake Sasha alionekana akiingia haraka haraka katika mkokoteni wake maalumu unaovutwa na farasi wanne wenye rangi nyeupe tayari kwenda kushuhudia tukio hilo la ki historia ndani ya mji wa ISRA.

Turudi upande wa pili...
Wakati dereva wa gari la Tesha akizidi kukanyaga mafuta kumrudisha bosi wake nyumbani mara Tesha alimtaka asimame ghafula.
"Nini tena bosi?"
"Nimedondosha pochi yangu pale mgahawani..."
"Mmh! Kwa hiyo turudi au? Si atakutunzia yule jamaa wako David sijui" Alisema Dereva
Tesha hakujali sana kuhusu pesa zake, lakini alipokumbuka vitu vingine vilivyomo kwenye pochi yaani ile picha ya utupu na ile mipira ya kiume(condom) akaona asimpe David nafasi ya kuikagua pochi yake, ni aibu.
"Hapana turudi" Alisema Tesha na mara hiyo dereva akageuza gari na kuanza kurudi.
Hakuna aliyejua kuhusu majanga mazito yanayokaribia kumkuta David ambaye yuko njiani kuuliwa na wale wanawake wa ajabu kutoka ISRA Zucc na Femi.
Je nini kitafuata?
Sasha atakuwa salama?
Dumayo atafanya nini?
Magnus ni nani na yuko wapi?
Nini Hatima ya David, Tesha na Sasha?

ITAENDELEA....

FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........13
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Hapana turudi" Alisema Tesha na mara hiyo dereva akageuza gari na kuanza kurudi.
Hakuna aliyejua kuhusu majanga mazito yanayokaribia kumkuta David ambaye yuko njiani kuuliwa na wale wanawake wa ajabu kutoka ISRA Zucc na Femi.
SASA ENDELEA...
David alionekana akitembea mara baada ya kutoka nje ya mgahawa akawa analielekea geti dogo linalounganisha uzio wa kuta mbili zinazouzunguuka mgahawa huo.

Sura ya David ilionekana kuwa na tabasamu angavu, bado alikuwa akikumbuka vile vitu alivyoviona ndani ya pochi ya mwanamitindo maarufu Tesha, akaishia kutabasamu mwenyewe.
Akiwa amebakiza hatua kadhaa kulifikia geti mara ghafula alishtushwa na mlio mkali wa vyuma vikigongana nyuma yake karibu kabisa na shingo yake.
David aligeuka haraka kutazama ndipo hapo anapokutana na tukio la ajabu ambalo hakuwa kulishuhudia tangu kuzaliwa kwake.
Wale wanawake wa ajabu waliokuwa wanamfuatilia tangu awali sasa walikuwa nyuma yake yaani Zucc na Femi. Mikononi mwao kila mmoja alikuwa ameshikilia visu vidogo viwili.
Kisu kimoja cha Zucc kilikuwa karibu kabisa na shingo ya David. Ilionekana wazi Zucc alikusudia kumuua David lakini alizuiliwa na kisu cha Femi ambaye alifika haraka kabla Zucc hajakizamisha kisu chake katika shingo ya David.
Wakiwa katika hali hiyo, Zucc na Femi walitazama kwa macho makali huku kila mmoja akionekana kutofurahishwa kabisa na uamuzi wa mwenzake.
David alibaki amesimama huku akiwa ametoa macho kwa mshangao mkubwa. Mwili wake wote ulikuwa ukitetemeka kwa hofu kubwa aliyokuwa nayo. Haja ndogo ilikuwa karibu kumtoka.

"Unaelewa unachokifanya Femi..?" Zucc aliongea kwa jazba sana.
"Siwezi kukuruhusu uvunje sheria yetu Zucc, ninyi ndio mnasababisha majanga hayaishi kutuandama katika mji wa ISRA kwa sababu ya kuzidharau sheria muhimu kama hizi" Femi aliongea huku naye akiwa ameikunja sura yake.
"Femi potea kwenye macho yangu mara moja kabla sijakuumiza..."
"Siwezi kukuacha umuue huyu mwanadamu Zucc, labda uniue mimi kwanza.."
Femi alijibu kisha akageuka na kumtazama David ambaye tayari alishadondoka chini kutokana na hofu kubwa aliyokuwa nayo.

"David, inuka kimbiaa...." Alisema Femi kauli iliyopenya vizuri kwenye masikio ya David.
David akajizoazoa pale chini kujaribu kusimama lakini akajikuta anaanguka tena kwa mara nyingine, hofu ilikuwa imemjaa kiasi cha kumfanya akose nguvu kabisa.
Kufumba na kufumbua ugomvi mkubwa ulianza kati ya Femi na Zucc. Wanawake hawa wa ajabu walianza kupigana kwa kasi sana huku kila mmoja akionekana yupo vizuri katika matumizi ya visu vile vidogo.
Kasi yao ilikuwa ya ajabu sana, kunawakati waliruka juu umbali wa mita kadhaa kutoka ardhini wakakutana hewani na kuendelea kupigana huku wakishuka chini kwa kasi na kutua tena ardhini.
Wakati hayo yakiendelea yule dada muhudumu wa mgahawa alikuwa akishuhudia kila kitu, kupitia kioo cha dirisha la mgahawa huo. Ajabu ni kwamba yeye alikuwa akimuona David pekee lakini hakuwa akiwaona Zucc na Femi. Aliona wakati David akianguka na kujaribu kusimama huku akionekana mwenye hofu. Yule dada muhudumu aliamua kumpotezea akiamini kuna namna David alikuwa na upungufu wa akili kwani hata alipokuwa mle mgahawani alikuwa akionyesha tabia za ajabu ajabu.
Lakini kadri muda ulivyokwenda yule dada muhudumu akaanza kuhisi kitu cha tofauti wakati anaendelea kumtazamaza David.

"Au unamajini huyu kaka..." Alisema yule dada muhudumu huku akiitazama ile noti ya dollar aliyopewa na David akaogopa na kuiweka pembeni ya meza huku akiendelea kutazama nje.
Hadi dakika tatu zinakwisha katika purukushani nzito ya Femi na Zucc hakuna aliyefanikiwa kumgusa mwenzake zaidi ya kuchaniana yale magauni yao marefu. Vipande vya nguo vilivyodondoka chini vilitoweka kwa namna ya ajabu na kupotea.

Hatimae David alifanikiwa kusimama akakimbia kulielekea lile geti dogo lakini kabla hajafika kufumba na kufumbua Zucc alikuwa amesimama mbele yake huku akihema kwa nguvu.

Kwa mara nyingine tena Zucc aliinua kisu chake tayari kumchoma David ambaye hakuwa na namna yoyote ya kujitetea mbele ya mwanamke huyo wa ajabu.
Femi aliyekuwa ameanguka chini mara baada ya kuzidiwa nguvu na Zucc aliinuka tena na kuiona hatari iliyokuwa karibu kumkuta David.
Kwa ustadi wa hali ya juu Femi alivirusha visu vyake vyote viwili kwa pamoja kumuelekea Zucc huku vikimpita David pasipo kumgusa.
Zucc aliyekuwa tayari kumchoma David alijikuta anasitisha zoezi hilo akainama haraka kuvikwepa vile visu viwili vilivyorushwa na Femi. Alipokuja kuinuka tayari Femi alishafika na kusimama mbele ya David kumlinda.
Zucc aliinua mkono wake wa kushoto wenye kisu akaurusha kwa nguvu kumuelekea Femi ambaye alikizuia kisu kile kwa mkono wake kikamtoboa na kumsababishia jeraha kubwa.
Damu yenye rangi ya kijani ikawa inamtoka mkononi lakini bado aliendelea kusimama kidete, kwa mara nyingine akamzoa Zucc na kuanguka naye chini. Purukushani ya aina yake ikaendelea kwa kasi ile ile kama mwanzo.

David akapata wasaa mwingine wa kukimbia kuyatetea maisha yake akafanikiwa kulifikia geti, lakini ile anakanyaga tu getini mara alisukumwa kwa nguvu na watu waliokuwa wanaingia kupitia geti hilo dogo.
David alirushwa kama karatasi iliyopulizwa na upepo, akaanguka chini na kupigiza kichwa chake, aliumia vibaya mno.
Akiwa na hali ya mawenge mawenge pale chini aliinua uso wake kutazama akaona wanaume wanne wakiwa na rungu mkono wa kulia na mkono wa kushoto kila mmoja alishikilia ngao iliyokuwa na maandishi yaliyosomeka M.A.G.N.U.S
Kichwani walivaa vitu kama helmet zilizokuwa na vioo vyenye rangi nyekundu.
David alimuona mmoja kati ya wanaume hao akiweka ardhini kitu kama spika ya redio, akakiwasha. Mara sauti kama mlio wa gari la wagonjwa (Ambulance) ulianza kusikika.
Wakati hayo yakiendelea yule dada muhudumu wa mgahawa alikuwa akishuhudia. Alishtushwa sana na namna watu hao walivyoingia na kumsukuma David. Kwa namna walivyoonekana akaamini kabisa hawa ni majambazi. Yule dada akawa anahangaika kuitafuta simu yake ili awapigie polisi.
Mwili wake ulikuwa ukitetemeka kwa hofu, mara aliona tukio lingine la ajabu tukio lililomfanya yule dada ashindwe kistahimiri, akaanguka chini kama mzigo na kupoteza fahamu.
Wakati mlio ule wa king'ora ukisikika kutoka kwenye kile kifaa, Zucc na Femi walishtushwa na kuacha kupigana walipogeuka kutazama tayari walikuwa wamechelewa. Ule mlio ulikuwa ni kero kubwa kwao, mlio ambao uliwafanya Femi na Zucc kuanza kukosa nguvu wakaanza kuyumba yumba huku wakijitahidi kuziba masikio yao, bado haikusaidia. Yule jamaa mwenye kile kifaa akawa anaongeza sauti zaidi huku wale wengine watatu wakiwasogelea Zucc na Femi taratibu na kwa tahadhali kubwa ngao zao wakiwa wameziweka mbele.

Mwisho Zucc na Femi walijikuta wanakosa nguvu kabisa wakaanguka chini wote wawili. Mara tu baada ya kuanguka sasa wakawa wanaonekana kwa macho ya kibinadamu na hii ndio sababu iliyomfanya yule dada mhudumu wa mgahawa azimie mara baada ya kuona watu wa ajabu wametokea kusikojulikana.
David alishuhudia yote haya akiwa pale chini ardhini, hakujua wanaume hawa wanne ni watu gani, wametoka wapi, kazi yao ni ipi, ni binadamu au nao ni viumbe wa ajabu kama walivyo Zucc na Femi.
Wakati akiwaza hayo mara ghafula anamuona mwanadada mrembo sana Tesha akiingia akupitia lile geti dogo.
Dada huyu ambaye ni super star' mwanamitindo maarufu nchini alikuwa amerudi kwa mara nyingine kuifuata pochi yake aliyoidondosha. Laiti kama angejua asingethubutu kukanyaga tena mgahawani hapo.

Upande wa pili- ISRA
Msitu wa Bi Noha ulikuwa kwenye majanga makubwa. Kimbunga kilikuwa ni kikali mno huku tetemeko la ardhi nalo likizidi kushika kasi. Miti ilikuwa iking'orewa na kurushwa juu huku mingine ikititia na kuzama ardhi. Msitu wa Bi Noha ukawa unatoweka kwa namna ya ajabu mno. Handan, Dumayo na watu wao walionekana wamesimama umbali wa hatua kadhaa kutoka ulipo msitu huo wakawa wanashuhudia kwa macho mambo yanayoendelea.

"Maskini Sasha! Nini kimetokea huko...? Ooh! Jamani naogopa mimi... Tafadhali toka ukiwa salama we binti" Aliwaza Handan huku akionekana kuwa na wasiwasi mwingi.

Katika hali wasiyotegemea, mara wanamuona Sasha anachomoza kutoka katika ya kimbunga kile cha ajabu. Alikuwa juu ya farasi wake anaekimbia kwa kasi sana. Nyuma yake hali ilikuwa ni tete ardhi ilikuwa ikititia huku kimbunga nacho kikimfuata kwa kasi. Sasha alimkimbiza farasi wake kwa kasi sana, laiti kama ingekua ni gari tungesema yuko spidi ya 180.
Hali ilitisha sana kulikuwa na kila dalili kuwa Sasha hataweza kutoka akiwa salama badala yake atamezwa pamoja na msitu huo.
Je nini kitafuata?
Sasha atasalimika?
Vipi kuhusu David na Tesha?
Watu hawa wenye ngao zenye maandishi yanayosomeka M.A.G.N.U.S ni akina nani hasa?

ITAENDELEA....

FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........14
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Hali ilitisha sana kulikuwa na kila dalili kuwa Sasha hataweza kutoka akiwa salama badala yake atamezwa pamoja na msitu huo.

SASA ENDELEA...

Sasha alijitahidi kumkimbiza farasi kwa nguvu zake zote lakini bado hali ilikuwa si shwari. Kila farasi alipopiga hatua na kuacha ardhi basi nyuma yake ardhi hio ilititia kwenda chini.
Handan mlinzi mkuu wa Sasha alipiga hesabu za haraka haraka ni jinsi gani ya kumsaidia Sasha, haraka akaruka na kumdandia farasi wake kisha akaanzaa kumuendesha kuelekea kule anakotokea Sasha.

Ulikuwa ni uamzi wa kikakamavu uliomuacha kinywa wazi Dumayo pamoja na watu wake, hakuna aliyetegema kama Handan angekubali kujitosa kuelekea kwenye hatari ile.

Sasa ikawa wakutane katikati, Handan anakuja kwa kasi na farasi wake huku upande wa pili Sasha naye akija kwa kasi akilikimbia balaa lile nyuma yake.
Kwa bahati mbaya farasi wa Handan akasimama ghafula. Handan akajitahidi kuvuta kamba ili farasi asonge mbele lakini wapi farasi akagoma katakata huku akiwa anarudi nyuma kupingana na Handan.

Wakati huo Sasha alikuwa amebakiza kama hatua ishirini hivi kumfikia Handan hatimae kasi ya kimbunga na ule mtitio wa ardhi vikamzidi farasi wake kasi.
Sasha na farasi wake wakajikuta wanamezwa na kimbunga kile huku wakienda chini kuelekea kwenye shimo kubwa lililotengenezwa na ardhi iliyokuwa ikititia, tayari msitu wote ulikuwa umezama kwenye shimo.

"Sashaaaaaaaaaa.......!!" Handan aliita na kuweka mikono yake kichwani akiwa juu ya farasi. Lilikuwa ni tukio la kutisha na kuumiza mno.

Tofauti na ilivyokuwa kwa wengine, Dumayo mjomba wake Sasha yeye akawa anatabasamu.

Lakini bado Handan hakutaka kukubali kirahisi namna ile kumpoteza binti wa Mkuu wa ISRA Gu Gamilo. Katika hali ambayo hakuna aliyetegemea, Handan alichukua kamba moja ndefu mno iliyokuwa kwenye shingo ya farasi wake, haraka akajifunga kiunoni kisha upande mwingine wa kamba ile akamfunga farasi wake mguuni kisha akampiga na kumuacha aende, yule farasi akawa anakimbia kurudi alikotoka wakati Handan naye akawa anakimbia kuelekea kwenye shimo lile kubwa.
Bila kusita Handan alifika na kuruka akajitosa moja kwa moja na kuanza kushuka chini kwa kasi huku ile kamba ikiwa kiunoni kwake.

Kitendo hicho kiliwaacha vinywa wazi Dumayo na watu wake. Hatimae yule farasi wa Handan akiwa amefungwa kamba mguuni alifika pale walipo. Lakini bado kamba iliendelea kufunguka kwa kasi kuelekea shimoni kule aliporukia Handan.
Haraka mwanamke mmoja kati ya wale wawili (walinzi wa Sasha) alipanda juu ya farasi wa Handan mwenye kamba mguuni akaanza kukimbia naye kusonga mbele zaidi. Mara kamba ikakaza ikiwa ni ishara kuwa sasa imefika kikomo kati ya Handan shimoni na farasi juu ya ardhi.
Kilichotakiwa sasa ni farasi kuanza kuvuta kamba ile ili kumtoka Handan.

Yule mwanamke wa pili naye alisogeza farasi wake wakaunganisha ile kamba kwenye miguu ya farasi wote wawili kisha wakaanza kuwapeleka mbele huku ile kamba ikizidi kusogezwa na kumvuta Handan.
Mchezo wote huo ulikuwa ukishuhudiwa na Dumayo pamoja na watu wake.
Dumayo aligeuka na kumtazama mlinzi wake mkuu aliyekuwa mkono wa kulia.

"Unajua ni kwa nini siku zote shemeji Gu Gamilo anatuzidi nguvu!?" Aliuliza Dumayo, yule mlinzi akatikisa kichwa akiashiria hajui.

"Angalia wanachokifanya hawa wanawake, hivi ndivyo walivyo watu wake wote wanaomzunguuka Gu Gamilo. Wako tayari kufa kwa ajili yake. Nataka na ninyi muwe hivyo, mpambane kufa na kupona la sivyo hatuwezi kumdhibiti Gu Gamilo" Alifoka Dumayo mjomba wa Sasha, huku zoezi la kumchomoa Handan likizidi kushika kasi .


Upande wa pili...
Turudi nyuma wakati Tesha akiwa njiani kurudi alikotoka mara baada ya kubaini kuwa aliidondosha pochi yake kule mgahawani.
Njiani Tesha alijikuta akimuwaza sana David. Ni kwa muda mfupi sana alikuwa amekaa na mwanaume huyo lakini alijikuta anamzoea ghafula na taratibu David akaanza kuitawala akili yake.

Alijikuta anatamani kuongozana naye wakati wote. Ali-miss uwepo wake, ongea yake vituko vyake na hata tabasamu lake.
Kila alipoyafumba macho yake aliiona taswira ya David ikiwa imeutawala ufahamu wake.
Tesha alikumbuka kwa mara ya kwanza alipokutana na David


,,,,,,, Ilikuwa ni siku ya mwisho ya juma(weekend) aliingia uwanja wa mpira kuangalia mechi ya mpira wa miguu wa wanawake kati ya simba queen na yanga princess . Alifika uwanjani hapo kama mmoja kati ya wahamasishaji wa kampeni ya kitaifa ya Mwanamke jasiri, lakini pia alikuwa katika harakati za kutangaza mtindo mpya kutoka katika kampuni yake ya mitindo maarufu kama Tesha Fashion. Siku hiyo David naye aliingia kama mfanya biashara ndogo ndogo akiuza vinywaji baridi.

Alipopita karibu na Tesha waliangaliana huku Tesha akionekana kuvutiwa na muonekano wa David. Na hapo ndipo alipopata wazo la kumtumia David kwa ajili ya kumrusha roho mpenzi wake Felix aliyekuwa amemtelekeza na kwenda zake Marekani.
Wazo hilo lilipita kwenye ufahamu wa Tesha akaona linafaa. Alimtegeshea David hadi alipopita mara nyingine akamwita na kununua maji. Kisha kwa siri sana wakati Tesha akilipa pesa aliunganisha na kadi ya mawasiliano.

" Kuna namba za simu hapo utanicheki, nina shida na wewe" Alisema Tesha huku akiwa makini asije akanaswa na kamera.
David aliduwaa kidogo akiwa hajategemea kabisa kitu kama hicho kutoka kwa mwanadada huyo maarufu.

Usiku wa siku hiyo David akiwa na shauku kubwa ya kujua ni jambo gani hasa lilimfanya mlimbwende Tesha akampatia mawasiliano ya simu, alipiga simu mara kadhaa na baadae ilipokelewa akajitambulisha na mwisho wakaweka miadi ya kukutana kesho yake asubuhi .
Asubuhi ya siku iliyofuata David na Tesha walikutana na ndipo Tesha alipoweka wazi nia yake ya kutaka kuigiza uchumba na mwanaume huyo na kuahidi kumlipa pesa nyingi.
Ilikuwa ni ngumu sana kwa David kumuamini Tesha kwani hakuona sababu ya msingi kwa Tesha kufanya hivyo lakini Tesha alimvutia kwa kumpa kiasi kikubwa cha pesa . David alizipokea pesa hizo bila hiyana huku wakikubaliana kukutana kwa wakati mwingine kwa ajili ya maelezo zaidi
Lakini tangu siku hiyo David akawa ni mtu wa kumzunguusha Tesha akiogopa pengine atajiingiza kwenye matatizo makubwa kama atakubali kufanya kama anavyotaka super star' huyo.

Mwisho David akajikuta anaanza kuandamwa na vijana walioagizwa na Tesha kumfuatilia kijana huyo kwani tayari alishakula pesa zake.


Kumbukumbu hizi za Tesha zilikatishwa na breki kali ya gari.
"Tumefika Madam" Alisema Dereva.
Tesha hakujibu kitu akafungua mlango wa gari na kushuka. Pembeni aliona gari nyingine aina ya Noah nyeusi iliyokuwa imesimama pembeni ya barabara huku milango yote ikiwa imefunguliwa na kuachwa wazi.
Tesha alipiga jicho kutazama ndani hakukuwa na mtu. Akaendelea na safari yake huku akiwaza pengine anaweza asimkute David mle mgahawani.

"Kama hayupo basi atakuwa hospitali kwa mama yake" Aliwaza Tesha.
Wakati akikaribia geti dogo la kuingilia ndani ya mgahawa huo alisikia sauti kali ya king'ora mfano wa gari la ambulance, sauti hiyo ilikuwa ikitoka ndani mahali anapokwenda.
Tesha hakujali sana akaamini pembeni kuna shughuli ilikuwa ikiendelea mle ndani.

Mwisho alifika getini tayari kuingia ndani, hapo ndipo Tesha alipojikuta anapatwa na mshtuko wa ajabu mara baada ya kushuhudia mambo yaliyokuwa yakiendelea mle ndani.
Aliona wanaume wanne wakiwa na helmet zenye vioo vyekundu, mkononi wakiwa na ngao na marungu makubwa.
Alipotazama pembeni Tesha akagonganisha macho yake na macho ya David aliyekuwa amelala chini ardhini akiwa hoi taabani.
Tesha alibaki katika hali ya mshangao mkubwa asijue cha kufanya, mwili wake ulikuwa umepigwa na ganzi ya ghafula hakuweza kurudi nyuma wala kusonga mbele, bado wale watu wenye helmet walikuwa hawajamuona.
Mara ghafula pasipo kutegemea Tesha alivutwa nje na mtu mmoja ambaye hakumuona sura yake, mtu huyo alimvuta kwa nguvu na kumbana pembeni ya ukuta huku akiwa ameuziba mdomo wa Tesha kwa kiganja chake cha mkono.

"Shiiiiiiiiiiiiii...." Alisema mtu huyo ikiwa ni ishara kwa Tesha kwamba anyamaze kimya.

Je ni nani huyo?
Katoka wapi?
Kwanini yuko hapa?
Vipi kuhusu Handan na Sasha?

ITAENDELEA...

FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........15
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Shiiiiiiiiiiiiii...." Alisema mtu huyo ikiwa ni ishara kwa Tesha kwamba anyamaze kimya.

SASA ENDELEA...
"Kaka...!!" Tesha aliita kwa mshangao mara baada ya kuutoa mkono wa mtu huyo mdomoni kwake na kumtazama.
"Tuondoke hapa sasa hivi" Alisema yule mtu, alikuwa ni Godfrey kaka yake Tesha
"Umefikaje hapa?" Tesha aliuliza
"Huu sio wakati wake tuondoke kwanza hapa" Godfrey alisisitiza huku akiushika mkono wa Tesha akaanza kumvuta kuelekea kwenye gari lake, wakafika na kuingia ndani. Wakati huo ile sauti ya king'ora kutoka ndani ya mgahawa iliacha kusikika kukawa kimya.
"Vipi jamani kwema?" Aliuliza Dereva wa Tesha mara baada ya kuona mtu na kaka yake wameingia mkukumkuku ndani ya gari.
"Kaka God nini kinaendelea mbona sielewi, wale watu mle ndani ni akina nani?" Tesha naye akaongeza swali lingine huku akimtazama kaka yake kwa macho ya kuuliza. Ni kweli Tesha hakuwa akielewa chochote hadi dakika hiyo. Mambo aliyoyaona mle mgahawani na baadae kaka yake Godfrey anatokea ghafula kumtoa yalizidi kumshangaza.

"Endesha gari bro, tuondoke hapa haraka"Alisema Godfrey, Dereva akatii na kuwasha gari tayari kuondoka.
"Hebu subiri kwanza, usiondoke" Mara Godfrey alimzuia tena dereva huku akiwa ametoa macho kutazama kwenye 'site mirror'
"Pandisha vioo vya gari haraka" Alisema Godfrey, dereva akafanya kama anavyoagizwa.
Godfrey, Tesha na dereva wake waligeuka kutazama kule mgahawani wakawaona wale wanaume waliovaa helmet wanatoka getini mmoja baada ya mwingine huku wakiwa wamewabeba wale wanawake wa ajabu yaani Zucc na Femi ambao walikuwa wamepoteza fahamu wakati huo.
Mwanaume wa mwisho kutoka naye alikuwa amembeba kijana David begani kwake. David naye hakuwa akijilewa alikuwa amepoteza fahamu vilevile.

"David...!" Tesha aliita kwa sauti ya chini akajaribu kufungua mlango wa gari ili atoke lakini Godfrey akamzuia.
"Unafanya nini Tesha hebu jitulize kwanza!"
"Ni David wamemteka David.."
"Sawa, lakini ni hatari kama utatoka. Unataka na wewe uingie kwenye matatizo au?"
"Basi tupige simu Polisi haraka" Alisema Tesha kisha akachukua mkoba wake akatoa simu na kubinya namba 111.

"Acha usipige..." Alisema Godfrey
"Kwa nini kaka, mbona sikuelewi lakini..."
Alisima Tesha, Godfrey hakujibu kitu, akachukua simu yake akawa anawapiga picha wale wanaume wanne ambao waliingia kwenye gari wakiwa wamewabeba watu watatu yaani Femi, Zucc na David. Wakawasha gari lao na kuondoka kwa kasi eneo hilo.

Godfrey aliacha zoezi lake la kupiga picha, akavuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu, alionekana mtu mwenye mawazo na wasiwasi mwingi. Akageuka na kumtazama mdogo wake Tesha.

"Nenda nyumbani Tesha nitakuja then tutaongea vizuri.."
"No tuonge hapa hapa, watu wametekwa mbele ya macho yetu alafu wewe kirahisi tu unanizuia nisipige simu polisi kwa nini ani! Istoshe aliyetekwa ni David mwanaume wangu"
"Mwanaume wako how!?" Aliuliza Godfrey huku akimtazama Tesha usoni, Tesha akatazama pembeni kwa aibu ni kama neno hilo lilimtoka kwa bahati mbaya.

"Yes he's my Man, kwani sikukwambia nina kazi naye? alafu kaka Godfrey hebu kuwa serious basi niambie ni nini kinaendelea..."
"Tesha nenda nyumbani kwanza kwa sasa sina muda wa kukueleza ila nakuahidi baada ya saa moja nitakuwa home tutaongea vizuri na kuhusu usalama wa huyo mwanaume wako niachie mimi" Alieleza Godfrey kisha akapokea simu yake iliyokuwa ikiita.
Tesha alipiga jicho la kuibia kutaza jina la mpigaji akalisoma
'Brandina-usalama'

"Hallo..." Godfrey alianzisha mazungumzo.
"Ndio nimefika hapa mbona sikuoni" Ilisikika sauti ya kike simuni.
"Nipo ndani ya hii gari mbele yako, nimeshakuona nakuja" Alijibu Godfrey kisha akakata simu. Nyuma yao aliliona gari dogo aina ya Toyota IST likifunga breki.
"Tesha nikukute nyumbani, just one hour okay" Alisema Godfrey. Kishingo upande Tesha akatikisa kichwa kukubali. Godfrey alishuka garini akapiga hatua na kuingia kwenye ile Toyota, wakati huo dereva wa Tesha naye aliwasha gari wakaondoka eneo hilo.

"Pole" Brandina mwanamke mmoja mweusi na mrembo aliyekuwa ndani ya gari alianzisha mazungumzo mara tu baada ya Godfrey kuingia na kuketi pembeni yake.
"Asante lakini sijafanikiwa kuwafuatilia"alijibu Godfrey
"Kwa nini?" Aliuliza Brandina huku akivua miwani yake
"Mdogo wangu alikuwa hapa, ikabidi nimtoe kwanza, ndiye aliyenichelewesha"
"Mdogo wako yupi Tesha?"
"Ndiyo"
"Tesha huyu super star'.."
"Yap"
"Sasa alikuwa anafanya nini kwenye huu mgahawa wa hadhi ya chini"
"Nafikiri kuna mtu alikuwa anakutana naye na hakutaka kuonekana, ni kijana mmoja anaitwa David naye kachukuliwa na hao majamaa tunao wafuatilia"
"Wamewachukua watu wangapi leo?"
"Watatu, nimeona wanawake wawili na huyu jamaa David ni watatu"
"Oops! Hawa jamaa wanatuumiza akili sana ni kheri serikali itangaze tu jambo hili na kuliweka wazi kuliko kufanya siri na watu wanaendelea kutoweka kila kukicha"
"Sasa kwa nini haitangazi, unajua siwaelewi kabisa?"
"Hawataki kutengeneza taharuki kwa raia, unajua hawa jamaa ni kama wana nguvu flani ambazo sio za kawaida yani ni kama wanatumia nguvu za giza hivi hata sielewi, huwezi kuamini ni miaka mitatu sasa tunaendelea kuwasaka kimya kimya lakini hakuna kitu tumewahi kupata hadi leo zaidi ya kukumbana na matukio ya ajabu ajabu yenye miujiza kibao"
"Lakini mbona kama hawa wanawake waliowateka leo sio wa kawaida yaani kwa kuwatazama tu wanamuonekano tofauti kabisa"
"Ndio maana nakwambia hili suala sio jepesi Godfrey. Kuna wakati hawa jamaa wenye helmet huwa wanaviteka viumbe vya ajabu kama hivyo unavyosema na kuna wakati huwa wanawateka binadamu wa kawaida kama walivyomteka mpenzi wako Dayana mwaka jana"
"Mmh! Sasa ni akina nani hawa?"
"Hatuelewi kabisa, vipi umepiga picha hata moja"
"Yap! Kuna hizi picha nimefanikiwa kuwapiga"
"Okay Good" Aliesema Brandina huku akiipokea simu ya David
Akawa anatazama picha zile moja baada ya nyingine.
"Si unaona hawa wanawake waliowabeba.. wamevaa magauni ya ajabu alafu yanafanana. Kwa Dunia yetu hii ni nani anaweza kuvaa kama hivi na akatoka mtaani kutembea"
"Ni ajabu sana, angalia hata gari la hawa jamaa halina plete number. Ni ngumu kuwapata" Godfrey aliongezea.
Baada ya hapo walishuka na kuingia mgahawani wakakagua mazingira na baadae walifanikiwa kumuona yule dada muhudumu aliyeanguka na kupoteza fahamu.
Brandina alipiga simu kutoa taarifa na punde gari ya wagonjwa ikafika na kumchukua.
"Huyu binti akiamka asizungumze na mtu yeyote hadi nifike mimi sawa" Brandina alitoa maelezo kwa mmoja kati ya watoa huduma wa afya waliofika mahali hapo.
"Sawa afande"
"God naomba unikutanishe na Tesha anaweza kuwa aliona chochote cha kutusaidia"
"Hapana, mdogo wangu hajaona chochote"
"Usijali sitamuingiza kwenye hii kesi isipokuwa nataka maelezo yake kidogo tu" Brandina alimtoa wasiwasi Godfrey.


ISRA...
Jitihada za kumvuta Handan kutoka shimoni ziliendelea, farasi walizidi kusogea mbele huku kamba ya Handan nayo ikizidi kusogea juu taratibu kutoka shimoni. Wakati huo hali ya hewa ilikuwa shwari kabisa kile kimbunga na tetemeko la ardhi vilitoweka ghafula mara tu baada ya Sasha kuzama shimoni akiwa na farasi wake.
Baada ya jitihada kubwa za wale wanawake walinzi wa Sasha kufanyika mwisho kamba ilifika ukomo, watu hawakuamini macho yao mara baada ya kumuona Handan akichomoza kutoka shimoni huku akiwa amemkumbatia Sasha kifuani mwake.
Handan na Sasha walitoka nje ya shimo, wale wanawake wawili walinzi walikimbia na kwenda kuwapokea kwa furaha.
Miili ya Sasha na Handan ilikuwa imejeruhiwa vibaya mno kutokana na misukosuko waliyokutana nayo shimoni. Damu yenye rangi ya kijani ilikuwa ikiwatoka katika maeneo mbalimbali waliyojeruhiwa.

"Asante Handan..." Alisema Sasha huku akimtazama Handan usoni mlinzi wake namba moja aliyejitoa kuyaokoa maisha yake.
"Usijali, lakini kwa nini ukafanya hivyo Sasha? Uliingia kufanya nini msituni?" Aliuliza Handan wote wakawa makini kusikiliza Sasha atajibu nini. Sasha naye akawa anawaza ni jibu gani sahihi la kuwapa kwani tayari alishaelezwa kuwa kila alichoongea na Bi Noha kilikuwa ni siri kubwa. Hakutakiwa kabisa kuufungua mdomo wake kuzungumza kuhusu jukumu zito alilopewa la kumlinda mwanadamu David.
Akiwa anawaza nini ajibu mara watu zaidi ya kumi na tano walifika na kuwazunguuka huku wakiwa wamenyoosha panga zao mbele. Walikuwa ni wale watu kutoka msafara wa Dumayo mjomba wa Sasha.
"Kuna nini? Mnataka nini?" Aliuliza Sasha huku akiwatazama watu hao kwa macho makali.
"Hawajui kitu hawa, mtu wa kumuuliza ni mjomba wako" Handan aliongea kwa sauti ya chini huku akiwapa ishara wale wanawake wengine walinzi wa Sasha wasijaribu kufanya lolote.
Sekunde chache baada Dumayo mjomba wa Sasha naye akasogea karibu akiwa juu ya farasi wake.

"Tunawakamata kwa kosa la kuingia ndani ya msitu bila ruhusa, mmesababisha majanga makubwa sana ndani ya ISRA, kutoweka kwa msitu wa Bi Noha ni laana kubwa ndani ya ISRA, ni lazima muwajibike kwa hili" Alisema Dumayo.
Je nini kitafuata?
David kapelekwa wapi?
Ni akina nani wamemchukua?
Kwa nini?

ITAENDELEA...


FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........16
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Mmesababisha majanga makubwa sana ndani ya ISRA, kutoweka kwa msitu wa Bi Noha ni laana kubwa ndani ya ISRA, ni lazima muwajibike kwa hili" Alisema Dumayo.

Je nini kitafuata?

SASA ENDELEA...
ISRA ...
Mkuu wa ISRA Gu Gamilo pamoja na askari na baadhi ya wafanyakazi wengine ndani ya Ikulu ya ISRA walionekana pembeni ya shimo kubwa mahali palipokuwepo msitu mkubwa maarufu kama msitu wa Bi Noha.
Walikuwa wakitazama maafa makubwa yaliyotokea kiasi cha kusababisha msitu huo kutoweka wote kwa namna ya ajabu sana. Ilikuwa ni hali iliyomshangaza kila mmoja. Hakuna aliyekuwa na jibu sahihi ni kipi hasa kimepelekea msitu huo kupatwa na majanga na mwisho kuzama wote ardhini.
Gu Gamilo baba yake Sasha alitazama kwa umakini huku uso wake ukionekana kujawa na wasiwasi mwingi.
Gu Gamilo alikuwa ni mzee kiasi sura yake iliyokunjamana wakati wote, ilikuwa ni adimu kuliona tabasamu la mzee huyo. Nywele zake ndefu na nyeupe alizozifunga kwa juu, huku kidevu chake kikiwa kimefunikwa na ndevu zenye rangi nyeupe vilevile vilimfanya mzee huyo kuwa na muonekano wa pekee katika ISRA.

Mpaka dakika hiyo hakuna aliyejua sekeseke lilotokea upande wa pili wa shimo hilo kule walipo Dumayo Sasha na akina Handan.

Tukio la kutoweka kwa msitu huo lilionekana kumtisha sana Gu Gamilo kiasi cha mkumfanya akumbuke kwa mara ya mwisho alivyoingia ndani ya msitu huo akafanikiwa kuonana na Bi Noha ambaye kwa sasa ni marehemu. Gu Gamilo aliyakumbuka vizuri maneno mazito aliyowahi kuelezwa na bibi kizee huyu, alisema...

...... Umefanya kosa kubwa bila kufikiria kwa makini Gu Gamilo, kumfukuza Kaka yako MAGNUS nje ya ISRA bado hujamaliza tatizo, kwa kosa alilofanya alistahili adhabu kubwa zaidi ya hiyo. Ipo siku utayakumbuka maneno yangu Siku ambayo Magnus atarudi tena ISRA na kuitikisa kwa mara nyingine. Haijarishi itachukua miaka mingapi lakini jua kwamba Magnus ni lazima atarudi tena akiwa amejipanga vilivyo. Atakushambulia kutoka pande zote, mashariki magharibi kaskazini na kusini. Itakuwa ni siku ambayo utakosa kwa kukimbilia hata msitu wangu ambao pengine ungeweza kujificha hautokuwepo tena, litakuwepo shimo kubwa lisilo na mwisho Gu Gamilo..........
Haya yalikuwa ni maelezo ya Bi Noha ambaye ni kama alijua siku moja msitu wake utatoweka na kubaki shimo.

........Bi Noha, nifanyaje sasa kuzuia hili lisitokee tafadhali nisaidie, nawezaje kumzuia kaka Magnus...........

........Hakuna mtu yeyote ISRA atakae weza kumzuia Magnus, isipokuwa yupo Mwanadamu mmoja ambaye ataweza kupambana naye na kumzuia Magnus asirudi tena ISRA, mwanadamu huyo anahitaji ulinzi. Kama atakufa basi ISRA itakuwa kwenye wakati mgumu, kama akiwa hai basi ISRA itaendelea kusimama...........

........Ni mwanadamu gani huyo Bi Noha, unaweza kuniambia tafadhali.........

.........Mtafute, na hakikisha unamlinda kabla Magnus hajamtambua........


Hizi zilikuwa ni kumbukumbu za Mkuu wa ISRA Gu Gamilo. Baada ya hapo aliondoka kinyonge yeye na watu wake huku kila mmoja akisubiri kwa hamu Gu Gamilo atasema nini baada ya tukio hilo ambalo wengi waliliona kama ishara mbaya kwa ISRA.
Hatimae Gu Gamilo alilejea Ikulu ya ISRA yeye na msafara wake, wakati anaingia lango kuu la Ikulu alipokelewa kwa shauku na mkewe kipenzi Malkia Hella(Mama yake Sasha). Alikuwa akimsubiri Mumewe kwa hamu ili amueleze ni nini hasa kimetokea maana kila mtu alionekana kuogopa.
Alipoiona Sura ya huzuni kwa mumewe Gu Gamilo ilikuwa ni tafsiri tosha kuwa mambo hayakuwa mazuri kabisa.

"Ni nini kinaendelea huko nje Gu Gamilo..." Aliuliza Malkia Hella
"Umetoweka.." Gu Gamilo alijibu kinyonge
"Nini? Nini kimetoweka!?"
"Msitu wa Bi Noha" Ilikuwa ni kauli iliyo muacha kinywa wazi Malkia Hella.
Akiwa katika hali hiyo ya mshangao mara wakasikia mlio wa farasi langoni. Gu Gamilo na mkewe wakageuka taratibu kutazama.
Uso kwa uso wakamuona Dumayo anaingia taratibu na msafara wake. Gu Gamilo aliikunja sura yake akionyesha wazi ni jinsi gani alikuwa anamchukia shemeji yake huyo. Lakini tofauti na Malkia Hella yeye alitabasamu mara baada ya kumuona kaka yake Dumayo anaingia.

Katika hali ya kushangaza nyuma ya msafara wa Dumayo walionekana wanawake wanne wakiwa wamefungwa kamba mikokoni huku wakivutwa na watu wa Dumayo waliokuwa juu ya farasi. Wanawake hawa walikuwa ni Sasha, Handan pamoja na wale walinzi wengine wawili.
Gu Gamilo alitoa macho kwa mshangao asiamini anachokiona.
"Sasha" Gu Gamilo aliita kwa sauti ya chini.
Wakati huo Dumayo yeye awaka anatabasamu tu kama kawaida yake.


Upande wa pili......
David alifumbua macho yake taratibu fahamu zikiwa zimemrejea. Hali akiwa na maumivu makali ya kichwa, alitazama mahali alipo. Alikuwa ndani ya chumba kimoja kipana huku mikono na miguu yake ikiwa imefungwa na vyuma maalumu vilivyokuwa ukutani. Alikuwa ametanuliwa mikono yake na kusimamishwa kama vile yupo msalabani.
Alipotazama mbele akawaona wale jamaa wenye helmet zenye vioo vyekundu wakimalizia kuwafunga watu wengine watatu ukutani kama vile walivyomfunga yeye baada ya hapo wakafungua mlango wa chumba hicho wakatoka na kuondoka. David alitazama kushoto na kulia kwake ndipo akagundua kuwa karibu kuta zote nne za chumba hicho kulikuwa na watu wamefungwa kama yeye na wengi wao walikuwa wamepoteza fahamu hawajitambui. Kwa Haraka haraka aliwahesabu walifika kumi na mbili. David aliogopa sana, hakuelewa ni wapi yupo na amefikaje. Bado kumbukumbu zake zilikuwa hazijakaa sawasawa.

"Oya nyie, nifungueni, njooni mnifungue....mnajua mimi ni nani!??" David alianza kupiga kelele huku akifoka.
"NYIE JAMAAAAAAA..."
David alizidi kupiga kelele.
"Kelele zako hazito saidia kitu, unamaliza nguvu zako bure..."
Mara sauti hii ya kike ilisikika kutoka pembeni yake upande wa kushoto. Haraka David akageuka kutazama ni nani aliyemuongelesha.
Uso kwa uso akagonganisha macho yake na mmoja kati ya wale wanawake waliokuwa wakimfuatilia tangu awali. Alikuwa ni Femi, naye alikuwa amefungwa vilevile kama yeye.

David aliogopa sana alipomuona lakini alipogundua naye amefungwa kama yeye aliduwaa huku kumbukumbu za matukio kadhaa yaliyotokea tangu alipoanza kuwaona wanawake hao wa ajabu zikijirudia kichwani kwake kama filamu.

"We..we. ni nani?"
"Naitwa Femi..." Alijibu Femi huku akitema mate chini, mate yaliyochanganyikana na damu ya kijani.
David alitazama yale mate pale chini kisha akageuka tena na kumtazama yule mwanamke akiwa katika hali ya mshangao mkubwa.

"Fe..femi wa wapi? Kwa nini mlikuwa mnanifuatilia?"
"Kwa sababu tunataka kukuua" Femi alieleza bila kusita
"Bado unaendeleza ukichaa wako Femi si ndiyo?" Mara sauti ya Zucc kutoka upande wa kulia kwa David ilisikika. David alishtuka na kugeuka kumtazama.
"Na wewe pia ulikuwa ukinifuatilia..!" Alisema David lakini bado alionekana kuogopa.
"Achana naye huyo!" Alisema Femi akimtaka David asiendelee kuzungumza na Zucc, David akageuka tena upande wake wa kushoto alipo Femi.

"Mnataka kuniua nimewakosa nini kwani?"
"Tumeagizwa tukuue..." Alijibu Femi lakini kabla hajaendelea zaidi Zucc akamkatisha kwa sauti kali iliyojaa hasira, hakupendezwa kabisa na anachokifanya mwenzake.
"Femi nimesema acha ujingaaaa ..." Alifoka
"Zucc hakuna tulichobakiza kwani hata nikimwambia ukweli kuna ubaya gani? Unafikiri tutapona na tayari tumeshafanya uzembe wenyewe mwisho tumeingia kwenye mikono ya MAGNUS" Alieleza Femi.
"Ma..ma.. Magnus ndio na..nani kwani?" Aliuliza David akiwa ndio kwa mara yake ya kwanza analisikia jina la mtu huyo MAGNUS , mtu ambaye kwa mujibu wa maelezo ya marehemu Bi Noha anatakiwa kupambana naye siku za usoni.
Kabla David hajajibiwa swali lake mara wakasikia mtikisiko mkubwa na baadae wakahisi kama wanasogea mbele.
Kumbe chumba hicho kilikuwa ni moja kati ya vyumba vingi ndani ya Meli moja kubwa ambayo sasa iling'oa nanga na kuanza kukata mawimbi taratibu kuelekea kusiko julikana.

ITAENDELEA...



SIMULIZI HII INAPATIKANA YOTE KWA WHATSAPP NAMBA 0756862047 KARIBU
 
FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya..........17
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Kumbe chumba hicho kilikuwa ni moja kati ya vyumba vingi ndani ya Meli moja kubwa ambayo sasa iling'oa nanga na kuanza kukata mawimbi taratibu kuelekea kusiko julikana...

SASA ENDELEA...

Zilikuwa zimepita dakika 55 tangu Tesha alipolejea kutoka kule mgahawani. Sasa alikuwa ndani ya sebule moja kubwa nyumbani kwake.

Tesha hakuwa ametulia kabisa, bado alikuwa akilitafakari lile tukio la kutekwa kwa David na watu wasiojulikana. Alikuwa akimsubiri kaka yake Godfrey kwa hamu kubwa ili aje ampatie maelezo kwa kina kwani alionyesha wazi anajua kila kinachoendelea ndio sababu alimzuia kupiga simu polisi.

Tesha alikosa amani kabisa, tangu afike nyumbani kwake hakupata muda wa kukaa, wakati wote alikuwa amesimama wima akizunguuka zunguuka sebuleni huku akili yake ikiwa imetawaliwa na taswira ya Mwanaume David. Akazidi kumuomba Mungu wake amuepushe na kila aina ya ubaya ambao David anaweza kufanyiwa na watu wale wenye helmet kichwani.

Dakika chache baadae Tesha alisikia muungurumo wa gari nje ya nyumba yake haraka akakimbia dirishani kwenda kuchungulia. Baada ya kufunua pazia aliona gari mbili zikiwa zimeongozana kuingia ndani. Moja aliifahamu ni gari ya kaka yake Godfrey lakini nyingine hakujua ni ya nani.
Alirudi na kukaa juu ya sofa akawa anamsubiri kaka yake kwa hamu ambaye punde aliingia akiwa ameongozana na mwanamke mmoja mweusi na mnene aliyevalia suti ya damu ya mzee na miwani ya jua myeusi, alikuwa ni Brandina.
Baada ya salama Godfrey akafanya utambulisho.

"Aaa.. karibu sana nyumbani kwetu Brandina, huyu ni mdogo wangu anaitwa Tesha, Tesha huyu ni Askari mpelelezi anaitwa Brandina. Ni rafiki yangu pia" Alieleza Godfrey kisha Tesha akamkaribisha Brandina kwa mara nyingine.

"Tesha najua unamaswali mengi ya kuniuliza juu ya tukio uliloliona masaa machache yaliyopita pale mgahawani, nimekuja hapa na Brandina kwa makusudi kwa sababu yeye ndiye atakueleza japo kwa ufupi kila kilichotokea, atakuwa na maswali machache ya kukuuliza na mwisho atatupa ufafanuzi nini kifanyike, karibu Madam Brandina"
"Asante sana God...Tesha"

"Abeeh!"

"Kwanza kabisa pole, najua utakuwa na wasiwasi mwingi ila nikutoe hofu kwamba utakuwa salama wala hakuna shida kubwa"

"Kuwa salama mimi sio tatizo afande, vipi kuhusu David,?"Aliuliza Tesha, Brandina akasita kujibu akageuka na kutazamana na Godfrey.

"Aah.. ukweli tunajaribu kupambana kuhakikisha David pamoja na wengine wote waliotekwa na watu hawa wanapatikana haraka iwezekanavyo"
"Ina maana kuna watu wengine wengi wametekwa?"
"Ndiyo, serikali inajaribu kulifuatilia suala hili kimya kimya ili kuepuka kuzua taharuki kwa Raia. Ni miaka minne sasa imepita tangu matukio kama haya yaanze kutokea hapa nchini" Alieleza Brandina, akatulia kwa muda kisha akaendelea...

"Nimeanza kufuatilia suala hili miaka mitatu iliyopita kabla sijakutana na kaka yako Godfrey ambaye naye alipotelewa na mpenzi wake Dayana mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha kama hivi leo. Tangu siku hiyo nimekuwa nikishirikiana na kaka yako Godfrey ambaye sio siri amekuwa akinisaidia sana sana kuwafuatilia hawa watekaji"

"So ni akina nani wanafanya huu utekaji na huwa wanawapeleka wapi watu wanaowateka?" Aliuliza Tesha

"Hatujui, nachoweza kusema watu hawa wamekuwa wakifanya matukio ya utekaji kwa kujirudia rudia na huwa tunashindwa kuwakamata kwa sababu kuna mambo ya ajabu kidogo huwa yanaambatana na matukio haya, ni kama kuna nguvu zisizo za kawaida huwa zinatumika"

"Una maana gani?"

"Anamaanisha uchawi, yaani nguvu za giza" Godfrey akadakia.

"Mmh!" Tesha akaguna

"Tesha.." Aliita Brandina

"Abeeh"

"Ni kitu gani ulikiona mara baada ya kuingia mle mgahawani kabla kaka yako hajaja kukutoa?"

"Aaa! ukweli niliona tu wanaume wanne wale wenye helmet wakiwa wamesimama mbele ya wanawake wawili waliovaa magauni mekundu wakiwa wamelala chini pembeni yao nlimuona pia David akiwa amelala chini. Aliweza kufumbua macho na kunitazama ghafula ndio kaka akatokea na kunitoa pale" Alieleza Tesha

"Sawa pole sana, vipi kabla ya hapo David aliwahi kukueleza jambo lolote ambalo uliona sio la kawaida au unahisi linaweza kuhusiana kwa namna yoyote na huu utekaji?"

"Mmh! Hapana sina mazoea ya mda mrefu na David, nina mda mfupi sana tangu nijuane naye....aah! Kuna kitu Nimekumbuka... Leo hii kabla hatujatoka humu ndani David alikuwa hapa sebuleni mimi na kaka tulikuwa chumbani ghafula alikuja akikimbia akasema ameona watu wa ajabu hapa dirishani"

"Enhe! Ikawaje? Godfrey ulikuwepo pia?"
"Yes madam nilikuwepo"
"Sasa mbona hujanieleza kitu muhimu kama hiki, ni watu gani aliwaona?"

"Nilipitiwa tu, ila ni kweli David alidai ameona watu wa ajabu hapo dirishani na tulipokuja kutazama ni kweli kioo kilikuwa kimepasuka ajabu ni kwamba tulipo wauliza walinzi wakadai hawajaona mtu yeyote nje"

"Ni dirisha lipi?"
"Hilo hapo mbele yako"

Brandina alisimama akapiga hatua hadi pale dirishani akawa anachunguza kwa makini. Macho yake yalitua kwenye picha moja kubwa ukutani, ilikuwa ni picha ya mwanaume mmoja mtanashati akiwa amepiga picha hiyo pamoja na Tesha nje ya kampuni yake ya mitindo Tesha Fashion.
Brandina alionyesha mshtuko mkubwa sana mara tu baada ya kuitazama picha hiyo, lakini akajitahidi kuficha mshtuko wake.

"Huyu mwanaume ni nani?" Aliuliza Brandina.
Kabla ya kujibu Tesha na Godfrey wakatazamana.

"Anaitwa Felix ni mchumba wa Tesha" Alijibu Godfrey.

"Mchumba!? And David who is he?"

"David ni rafiki tu wa kawaida, kwani vipi afande?" Alijibu Tesha akionekana kukerwa na maswali ya Brandina.

"Nothing special" Alijibu Brandina, akarudi kwenye kiti na kuendelea na mazungumzo.

Mwisho kabisa Brandina alishukuru akaaga na kuondoka huku akiahidi kurudi kwa mara nyingine kama itabidi.

Brandina alitoka nje ya jengo hilo la kifahari, akaingia kweye gari yake kisha akachukua faili moja na kulipekua haraka haraka. Alifunua mahali penye picha za watu kadhaa zilizobandikwa juu ya karatasi. Brandina alikaza macho yake kutazama picha moja kati ya zile zote huku akivua miwani.
Amini usiamini picha anayoitazama Brandina ilikuwa ni picha ya Felix mpenzi wa Tesha. Katika picha hiyo Felix alionekana akiwa amesimama pembeni ya Noah nyeusi na mkononi mwake ameshikilia helmet yenye kioo chekundu kama ile waliyovaa watekaji wa David.
Chini ya picha hiyo kulikuwa na maelezo yaliyoandikwa kwa kalamu ya wino yaliyosomeka

'2019-tukio namba 11'

Brandina alivuta pumzi ndefu na kuitoa taratibu kisha akainua macho yake kulitazama jengo hilo la kifahari.
"Anaitwa Felix" Alisema Brandina kisha akatabasamu.


Upande wa pili.......ISRA.
Gu Gamilo alitoa macho kwa mshangao asiamini anachokiona.
"Sasha" Gu Gamilo aliita kwa sauti ya chini.
Wakati huo Dumayo yeye awaka anatabasamu tu kama kawaida yake.

Punde wakaingia viongozi wengine wenye nyazifa za juu ndani ya mji wa ISRA, tayari Dumayo alishasambaza uvumi kabla ya kufika Ikulu kuwa Sasha mtoto wa Gu Gamilo ameingia ndani ya msitu wa Bi Noha bila ruhusa na kisha kusababisha msitu huo kupotea. Viongozi wengi walifika ili kuja kuthibitisha taarifa hizo.

"Sasha ameingia ndani ya msitu bila ruhusa, kinyume na sheria na taratibu zetu za ISRA. Amesababisha msitu pamoja na Bi Noha kutoweka na kuacha shimo la mauti, hii ni laana kubwa ndani ya ISRA laana kubwa mno, ni lazima kifanyike kitu kuondoa laana iliyosababishwa na mtoto wa Gu Gamilo" Dumayo aliongea kwa nguvu huku akinyoosha mkono wake wenye upanga kumuelekea Sasha. Watu wote waliokuwepo mahali hapo waliguna kwa mshangao na kushika midomo yao, zilikuwa ni taarifa mbaya sana kuwahi kutokea ISRA.

Maneno haya ya Dumayo yalipenya kama msumali wa moto kwenye moyo wa Gu Gamilo, aligeuka taratibu na kumtazama binti yake Sasha, Wakatazamana. Sasha akainamisha kichwa chake chini. Hii ilikuwa ni ishara tosha kwa Gu Gamilo kuwa tuhuma alizozitoa shemeji yake Dumayo ni kweli tupu.

Gu Gamilo alifumba macho yake akiwa na uchungu mkubwa, hakika alikuwa na mtihani mkubwa sana mbele yake hakujua ni jinsi gani ataweza kumtoa binti yake kipenzi Sasha kwenye balaa kubwa lililoko mbele yake.


Katikati ya Bahari Meli iliyowabeba David, Zucc, Femi pamoja na mateka wengine iliendelea kuchana mawimbi ikizidi kusonga mbele. Hakuna aliyeelewa ni wapi wanapelekwa...

ITAENDELEA....
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
 
FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya............18
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Brandina Askari mpelelezi anayo picha ya Felix mchumba wa Tesha katika faili lake la kazi. Wakati huo meli iliyowabeba mateka David akiwa mmoja wapo inaendelea kusonga mbele kuelekea kusiko julikana.
Upande wa pili Dumayo anatangaza hadharani kosa kubwa alilolifanya Sasha.

ITAENDELEA...
ISRA.
Gu Gamilo alifumba macho yake akiwa na uchungu mkubwa, hakika alikuwa na mtihani mkubwa sana mbele yake hakujua ni jinsi gani ataweza kumtoa binti yake kipenzi Sasha kwenye balaa kubwa lililoko mbele yake.

"Mchukueni Sasha na wenzake wawekeni gerezani" Hatimae Mkuu wa ISRA Gu Gamilo alitoa amri kwa Askari ambao walitii na kuwabeba Sasha, Handan pamoja na wale wanawake wawili wakawakokota kuwapeleka gerezani kama walivyoagizwa.

"Unafanya nini Gu Gamilo?" Aliuliza mkewe (Malkia Hella) kwa sauti ya chini ambayo ni mumewe pekee ndiye aliyeweza kusikia.
"Unahisi nitafanya nini!? Inabidi kila kitu kiende kama sheria inavyosema... Sasha ataadhibiwa" Alisema Gu Gamilo akionyesha msimamo wake kama Mkuu wa ISRA lakini ukweli ukawa pale pale hata yeye mwenyewe alikuwa akiumia mno ila hakuwa na namna.
Malkia Hella alionekana kufedheheshwa mno na maneno hayo ya Gu Gamilo lakini alipotazamana na kaka yake Dumayo wakatabasamu na kukonyezana kwa siri.

Gu Gamilo akiwa ameweka mikono yake nyuma akapiga hatua kusogea hadi karibu na viongozi wa ISRA ambao walifika punde mara baada ya kusikia uvumi wa taarifa za Sasha binti wa Gu Gamilo kukamatwa.

"Tukutane kesho asubuhi kwa ajili ya kujadili hukumu ya Sasha" Alisema Gu Gamilo huku akiwatazama wale viongozi kwa macho makali.
"Mkuu sizani kama kuna sababu ya kusubiri hadi asubuhi ya kesho, hili suala ni kubwa mno. Angalia tayari msitu wa Bi Noha umetoweka haupo tena, hili sio suala la kulisubirisha hata kidogo. Aliyekosa aadhibiwe haraka iwezekanavyo kuepuka laana ndani ya ISRA" Aliongea kiongozi mmoja huku wengine wakitikisa vichwa vyao kukubaliana na maelezo yake.

"Kwa hiyo mnanifundisha cha kufanya si ndiyo, kwani mimi sijui kama hili nikosa kubwa linastahiri adhabu? Nawauliza mimi sijuiii?" Gu Gamilo alifoka huku midomo yake ikitetemeka kwa hasira.
Mara Dumayo akadakia...
"Mkuu amekwisha wapa maelezo mfike kesho asubuhi haraka ya nini. Muhimu mshtakiwa yupo mikononi mwake hakuna kitakacho haribika" Alisema Dumayo kauli iliyojaa unafiki mwingi ndani yake. Akageuka kumtazama shemeji yake Gu Gamilo, wakatazamana.
Mwsho wale viongozi waliondoka, Dumayo yeye akabaki hapo kama mgeni ndani ya Ikulu ya ISRA.
Wakati huo jua lilikuwa linakaribia kuzama.


Kabla ya jua kuzama tayari meli iliyowabeba akina David na wale wanawake wa ajabu kutoka ISRA (Zucc na Femi) ilitia nanga katika fukwe ya kisiwa kimoja kidogo.
Tayari kulikuwa na watu zaidi ya kumi ambao walikuwa wamesimama kwenye fukwe hiyo wakiisubiri meli hiyo kwa hamu. Walivalia nguo sawa kabisa na wale jamaa wenye helmet waliofanya utekaji wa watu waliopo melini.
Mara tu baada ya meli kusimama mateka walianza kushushwa mmoja baada ya mwingine, wakapokelewa na watu waliokuwa ufukweni kisha wakapakizwa kama magunia ndani ya gari linalofanana na lile gari la wakandarasi ambalo hubeba mchanga (tipper).
Wakati huo wale mateka waliokuwa wamepoteza fahamu tayari wote walikuwa wamerejewa na fahamu zao, wakawa wanaogopa na kupiga kelele kwa hofu lakini hakuna aliyeonyesha kuwajali.
Kulikuwa na mlima mkubwa katika kisiwa hicho, mara baada ya kumaliza kuwashuka mateka kutoka kwenye meli na kuwapakiza katika gari, safari ilianza huku gari hilo likifuata barabara moja iliyojengwa kwa namna ya ajabu sana.
Barabara hiyo ilikuwa ikikatiza chini ya ardhi katikati ya mlima na kutokea upande wa pili.
Dakika saba pekee zilitosha gari hilo kutokea upande wa pili wa mlima ambako huko kulikuwa na uwazi mkubwa na majengo kadha wa kadha yaliyozunguushiwa ukuta mrefu na mpana sana.
Kulikuwa na ulinzi mkubwa sana eneo hilo. Walinzi kadhaa wenye siraha mkononi walionekana wakirandaranda ndani na nje ya ngome hiyo huku wengine wakionekana wako juu kabisa mlimani.

David pamoja na mateka wengine walipokelewa na watu wengine tofauti ambao walifanya kazi ya kuwavua nguo zote wakawaacha na nguo za ndani pekee. Isipokuwa Zucc na Femi wao hawakuvuliwa yale magauni yao badala yake walitenganishwa na mateka wengine wao wakabebwa kuelekea katika jengo moja kubwa la ghorofa.

David pamoja na mateka wengine wakiwa na nguo za ndani pekee waliamrishwa waingie tena ndani ya lile gari lililowaleta, wakafanya hivyo. Baada ya hapo lile gari lilianza kurudi nyuma hadi mahali fulani ambapo Dereva alibinya kitufe fulani lile bodi la nyuma waliko David na wenzake likaanza kubinuka kama vile linamwaga mchanga.
David na wenzake walipiga kelele za kuomba msaada huku wakijaribu kujizuia wasidondoke lakini hakuna aliyewaonea huruma mwisho walijikuta wakimwagwa wote katika bonde moja kubwa ambako huko walipokelewa na watu wengine wengi waliokuwa wamevuliwa nguo na kuachwa na nguo za ndani tu kama wao.

David alianguka katika bonde hilo na kuumia vibaya sana, kichwa na mguu wake wa kushoto.
Akiwa amelala pale chini alishuhudia watu wengi karibu mia moja na kidogo wakiwa katika bonde hilo. Walikuwa wamechakaa sana kutokana na mazingira na maisha magumu wanayopitia wakiwa katika bonde hilo.
David alijikuta akikata tamaa ya maisha, hakujua ameletwa hapo kwa ajili gani na kwa nini. Hali ilitisha mno.
Wakati akiwa pale chini asijue cha kufanya. Mara aliona wale watu wakitimua mbio kuelekea kwenye kona moja ya bonde hilo. Walikuwa wakikimbia kwa kasi huku wakisukumana na wengine kuanguka chini.
David alipoinua macho yake kutazama juu zaidi aliona gari kama lile lililowaleta likimwaga chakula amacho ni mikate na maji. Wale watu walianza kugombaniana kila mmoja akipambana apate angalau maji au mkate. Hali ilikuwa ni tete, hadi dakika tano zinakatika bado mapambano hayo yalikuwa yakiendelea na kila aliyepata angalau maji au mkate alikimbia Kwenye kona yake na kuanza kukifakamia kile alichopata kwa kasi sana, walionekana ni watu wenye njaa kali sana.
David na wenzake wageni walipigwa na butwaa wasielewe A wala B.


Muda ukazidi kwenda jua likazama na sasa giza likaingia.
Sasha alionekana akiwa amekaa na kujiinamia ndani ya chumba kimoja kichafu chenye kitanda cha nyasi. Chumba kingine kinachofuata alionekana mlinzi wake namba moja Handan kisha vyumba vingine walikuwepo wale wanawake wengine walinzi wa Sasha. Lilikuwa ni gereza mahali walipofungiwa kama alivyoagiza baba yake Gu Gamilo.

Sasha alikuwa amezama kwenye dimbwi la mawazo asielewe nini hatima yake. Hakujua ni hukumu gani ingetolewa asubuhi ya siku inayofuata.
Lakini pamoja na yote hayo bado Sasha hakuacha kuyakumbuka maelezo aliyopewa na marehemu Bi Noha kuhusu jukumu kubwa la kumlinda mwanadamu aitwae David ili tu kuiokoa ISRA isiingie mikononi mwa mtu mbaya aitwae Magnus ambaye ni baba yake mkubwa.


Upande wa piliii...
David akiwa ndani ya bonde lile la ajabu alikaa na kujikunyata mahali huku akiwa ameegemea ukuta wa bonde hilo. Kulikuwa na baridi kali sana mahali hapo, lakini hakuna aliyejali labda kuwapa mashuka ya kujifunika, la hasha hakuwepo mtu wa aina hiyo.
Kijana David alikuwa akitafakari namna mambo yalivyobadirika ghafula na kujikuta ameingia kwenye maisha ya ajabu sana.
Anakumbuka kwa mara ya mwisho alipokuwa katika msiba wa hayati Mheshimiwa Rais JPM ndipo mambo yalibadilika ghafula baada ya kukutana na yule msichana mwenye gauni jekundu (Sasha).

David akiwa katika dimbwi la mawazo mara alisikia vishindo na mwisho kuna mtu akawa amesimama mbele yake.
Aliinua uso wake taratibu sana kumtazama kuanzia chini, akaona miguu na mapaja akagundua alikuwa ni mwanamke, akaona chupi yake yenye rangi ya bluu, hips, tumbo, matiti yaliyofunikwa na sidiria iliyochakaa sana kisha akaitazama sura nzuri ya mwanamke huyo lakini ilikuwa imefubaa kutokana na aina ya maisha wanayoishi kule bondeni.
Yule mwanamke akanyoosha mkono wake uliokuwa na kipande cha mkate na maji akawa anampatia David.

David alimtazama kwanza kwa sekunde kadhaa kisha akapokea. Yule mwanamke akakaa pembeni yake.

"Asante" David alishukuru kinyonge.
Kimya kikatawala kwa sekunde kadhaa kisha yule mwanamke akaongea.

"Naitwa Dayana, nilitekwa na kuletwa hapa kama wewe, ni mwaka mmoja sasa umepita, niko hapa" Alieleza Dayana...
"Mwaka?" David aliuliza kwa mshangao.
Naam huyu ni Dayana yule yule ambaye Godfrey kaka yake Tesha alidai amempoteza mwaka mmoja uliopita.

0756862047

Je, nini kitafuata?
Ni wapi hapa wameletwa mateka hawa?
Zucc na Femi wamepelekwa wapi?
Sasha atapewa adhabu gani?
Vipi kuhusu Brandina na ile picha ya Felix?

Mambo ni mengi, Endelea kuungana nami katika mfululizo wa simulizi hii MARIDHAWA
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
 
FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya............19
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Naitwa Dayana, nilitekwa na kuletwa hapa kama wewe, ni mwaka mmoja sasa umepita, niko hapa" Alielaza Dayana...
"Mwaka?" David aliuliza kwa mshangao.
Naam huyu ni Dayana yule yule ambaye Godfrey kaka yake Tesha alidai amempoteza mwaka mmoja uliopita.

SASA ENDELEA....

"Ndio nina mwaka na mwezi mmoja tangu nimetupwa ndani ya hili bonde" Alijibu Dayana.

David alitulia kwa sekunde kadhaa akijaribu kulitafakari jibu hilo kutoka kwa Dayana. Aligeuka kumtazama mwanamke huyo ambaye wala hakuwa na hata chembe ya aibu kwa namna alivyokuwa amevaa, asilimia kubwa ya mwili wake ulikuwa wazi, chupi na sidiria aliyovaa ndio angalau vilimsitiri sehemu zake nyeti lakini bado hata sidiria yake ilikuwa imechanika upande hivyo kufanya nusu ya matiti yake madogo kuwa wazi.

"Kwa hiyo mkiwa humu huwa mnafanya nini? Kuna kazi mnafanya kama watumwa?" Mwisho David akauliza.

"Wala tunaishi tu kama unavyotuona. Mimi pia wakati nimefika nilihisi labda tumeletwa kama watumwa tutafanyishwa kazi usiku na mchana lakini hapa mambo ni tofauti kabisa tunaamka tunakula tunalala tunaamka tunakula tunalala hayo ndio maisha yetu. Isipokuwa chakula ni cha shida sana. Kama ulivyoona, tunaishi kwa kugombaniana chakula mwenye nguvu ndio ataishi. Wapo watu waliofia humu kwa sababu ya kukosa chakula na maji"
Maelezo haya kutoka kwa Dayana yalizidi kumtisha David. Akatamani kujua zaidi.

"Kwa hiyo sababu ya hawa watu kutuleta hapa ni nini?"

"Sijui, kwa kweli sijui kabisa! Huwa mwanatuita sisi wote ni FUNGUO, funguo ya mkuu wa eneo hili anaitwa MAGNUS" Kwa mara ya pili Sasa David analisikia jina la mtu huyu aitwae Magnus. Mara ya kwanza alilisikia kutoka kwa Femi wakati ule wakiwa ndani ya meli.

"Funguo?"

"Ndiyo SISI NI FUNGUO"

"Funguzo za nini?"

"Funguo za Magnus"

"Kufungua nini?"

"Sielewi, inaonekana alishafungwa mahali kwa hiyo sisi ni kama funguo zake. Huwa anakuja kutusalimia mara moja moja, akisimama pale juu utasikia anapaza sauti anasema HABARI ZA LEO FUNGUO ZANGU.... Huwa simpendi yule mzee, anatisha hana utu ndani yake, anakera hata kumtazama" Alieleza Dayana.
Kimya kikatawala tena kwa muda

"Kwa hiyo hakuna namna yoyote ya kutoka humu? Hakuna aliyewahi kutoroka akafanikiwa?" Aliuliza David

"Hahahah! Utatoroka uende wapi, utatokaje kwenye hili bonde? Kila aliyejaribu kutoroka aliishia kufa. Kifupi hakuna namna yoyote ya kutoroka.."

"Ipo namna! ipo sema ni uwoga wako tu..." Mara sauti ya kiume ilisikika ikipingana na maelezo ya Dayana. Akatokea jamaa mmoja mwembamba na mrefu, akafika na kukaa pembeni ya David, alikuwa ni mmoja wao ndani ya bonde lile.

"Zungu..!!" Dayana aliita kwa mshangao.

"Nini!? Naona umepata boyfriend mpya umeamua kunikimbia"

"Acha masihara yako bwana huyu ni mgeni nimekuja kumriwadha kidogo..."

"Upo kamati ya mapokezi humu bondeni au? halafu mbona wamekuja wageni kibao mbona umewaacha umekuja kwa huyu mwamba hapa, umeshampenda tayari?" Aliuliza Zungu huku akichukua mkate ambao Dayana alimpa David akaanza kula.

"Unaitwa nani jamaa?" Aliuliza Zungu, David akawa kimya.
"Huna jina?"

"David.."

"David wow! Napendaga watu wenye majina ya Biblia kidogo huwa wanakuwa waelewa, sasa sikia David usimsikilize huyu Dayana ni muoga, kutoroka hapa inawezekana kabisa kama tukiamua mtu wangu, sema tawile" Alieleza Zungu

"Muongo usimsikilize anataka akufanye chambo, utakufa David" Dayana akadakia

"Kausha basi na wewe... Tangu lini nikaongopa au unafikiri mimi muongo muongo kama wewe!?"

"Kwani mimi niliwahi kukudanganya nini?"

"Hujui au?"

"Nini...!!"

"Unasikia David huyu demu alipofika kwenye hili bonde kwa mara ya kwanza wahuni walitaka kupita naye, walitaka kumbaka, mimi ndio nikamtetea. Mpaka leo hajawahi kunipa chochote anazingua"

"Kwa hiyo ulitaka nikupe nini!?"

"Kwani wewe hujui au?"

"Sijui, nitakupa nini sasa"

"Wewe ni mwanamke alafu hujui cha kunipa..."

"Kwa hiyo umesema kutoroka inawezekana?" David akaingilia kati mazungumzo ya Dayana na Zungu.

"Yes! Wewe uko safi sana, subiri watu walale nitakupeleka mahali, kila siku mimi huwa nafanya utafiti namna ya kutoroka tayari nazijua njia nyingi zinazotoka hadi nje kabisa ya hili bonde ishu ni kuvuka huo mlima hadi upande wa pili kule ufukweni" Alieleza Zungu


ISRA
Mkuu wa ISRA Gu Gamilo alionekana akiwa amekaa meza moja na shemeji yake Dumayo. Ilikuwa ni muda mfupi umepita tangu awatawanye wale viongozi wa ISRA na kuwaambia wafike asubuhi ya siku inayofuata kujadili hukumu ya SASHA.

"Unajua huwa siamini kabisa mtu ambaye tulishirikiana naye bega kwa bega hadi tukafanikiwa kumuondoa MAGNUS hapa ISRA leo hii amegeuka na kuwa msaliti kama vile Magnus mwenyewe" Alisema Gu Gamilo huku akimtazama Dumayo usoni.

"Ah! Tatizo Shemeji unashindwa kunielewa, mimi siku zote huwa nasimama upande wenye haki. Ndio maana nilipambana kufa na kupona hadi tukamshinda na kumuondoa Magnus" Alieleza Dumayo. Gu Gamilo akawa anamtazama akijua kabisa Dumayo hakuwa anamaanisha anachokisema hata kidogo bali moyo wake umejaa chuki na wivu mkubwa.

"Kwa hiyo ulishindwa kumstiri binti yangu? kulikuwa na ulazima gani wa kumdharirisha Sasha namna ile, huoni kama umenichafua hata mimi?''

"Sasha kavunja sheria na kusababisha balaa kubwa ndani ya ISRA shemeji. Lazima aadhibiwe, Nilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo unavyotaka lakini unajua kwa nini sijafanya?"

"Kwa nini?"

"Kwa sababu siku zote umekuwa ukimpendelea Sasha kuliko watoto wako wengine? Kuna kila dalili kuwa hata kiti chako cha uongozi siku moja utamrithisha Sasha na sio mtu mwingine ndio maana nataka nimfutilie mbali huyu binti"
"Kwanini, unahisi Sasha hastahiri kuwa mkuu wa ISRA hapo baadae?"

"Gu Gamilo, unajua kabisa Sasha sio familia yako! Sasha sio damu yako Sasha sio mtoto wenu wala sio...." Alisema Dumayo lakini kabla hajamalizia sentensi yake tayari upanga wa Gu Gamilo ulikuwa kwenye shingo yake.

"Katu! Nisije sikia kwa mara nyingine unaongea huo upuunzi mbele yangu wala mbele ya mtu yeyote yule Dumayo ni marufuku. Siku nikikusikia tena nitakukata shingo yako bila huruma.... Sasha ni mwanangu...ni binti yangu" Gu Gamilo aliongea kwa msisitizo akionekana mwenye jazba sana kisha akatupa upanga chini, akainuka na kuondoka.

"Ahahah! Nimekugusa pabaya... Hata hivyo huna utakalo fanya tayari Sasha ameshavuruga mambo..." Dumayo alijisemea mwenyewe. Wakati huo mdogo wake yaani Malkia Hella akajitokeza mahali alipokuwa amejificha akifuatilia maongezi ya mumewe na kaka yake.

"Sijui ni mdudu gani alishamuingia huyu mwanaume huwa hataki kabisa kusikia mtu akisema Sasha sio mtoto wetu" Alisema Malkia Hella huku akisogea na kukaa pale alipokuwa amekaa Gu Gamilo kabla hajaondoka.

"Usijali dada tayari tumeshapata njia ya kumtoa Sasha hapa Ikulu na ikiwezekana atanyang'anywa nguvu zake na kufukuzwa kabisa hadi nje ya ISRA kama vile alivyofanyiwa Magnus" alisema Dumayo

"Mmh! Kwa kweli sidhani, kwa namna anavyompenda Sasha sijui kama ataweza kuruhusu hili litoke"

"Ataruhusu tu apende asipende, halafu ni kwa nini anakapenda sana haka ka binti"

"Hata sielewi kaka yangu! Niliwahi kumpeleleza siku moja akadai kuwa aliambiwa na mtabiri mmoja kuwa Sasha ndiye atakuja kuiokoa ISRA hapo baadae kama ikiingia kwenye matatizo"

"Hahahahah hahahahah! Mtabiri gani huyo.. ni Bi Noha au?" Dumayo alicheka sana na kuuliza.
"Hapana sio Bi Noha"
Dumayo akazidi kucheka tena na tena.


Baada ya Gu Gamilo kuondoka, alienda ndani ya chumba kimoja cha siri akaagiza askari wake mashuhuri sana ISRA aitwe.

Baada ya muda askari huyo alifika na kumsalimia mkuu wa ISRA Gu Gamilo kwa heshima kubwa.

"Dojin" Gu Gamilo aliita

"Ndiyo Mheshimiwa"

"Nimekwita hapa nataka nikupe kazi moja ngumu ambayo itakuwa ni kubwa pengine kuliko kazi zote nilizowahi kukupa hapo kabla"

"Niko tayari kufanya kazi yoyote utakayonipa Mheshimiwa"

"Dojin.." Gu Gamilo aliita tena

"Ndiyo mkuu"

"Siku zote tumekuwa tukipambana kuiweka ISRA kwenye mikono salama, tumepigana vita nyingi na ngumu tukiwa pamoja. Vita hivyo bado havijafika mwisho Dojin. Unakumbuka kuna mtoto tuliwahi kumuokota wakati ule tukipigana vita na Magnus miaka mingi iliyopita?"

"Nakumbuka mkuu wangu"

"Unakumbuka nini kilitokea siku hiyo baada ya kumuokota huyo mtoto mchanga?"

"Nakumbuka kila kitu Mheshimiwa, alitokea bibi kizee mmoja wa ajabu akasema tumlee na kumlinda huyo mtoto kwa sababu ameibeba hatima ya ISRA hapo baadae"

"Vizuri kumbe unakumbuka, basi hayo maneno hata Bi Noha alishawahi kuniambia pia siku nilipo kutana naye. Unajua huyo mtoto mchanga tuliyemuokota ni nani?"
"Hapana sijui Mheshimiwa!?"

"Ni Sasha... Huyu binti yangu ambaye natakiwa kuitoa hukumu yake kesho" Alisema Gu Gamilo kauli iliyomshtua na kumuacha kinywa wazi Dojin. Siku zote alikuwa anaamini Sasha ni mtoto halisi wa Gu Gamilo kama wengine wanavyoamini. Hakuwa akijua kama yule mtoto waliyemuokota wakati ule alilelewa na Mkuu wa ISRA na ndio Sasha mwenyewe, hii ilikuwa ni siri kubwa.

"Nakata umtoroshe Sasha, kimbia nenda naye mbali hakikisha anakuwa salama, ikiwezakana toka naye hadi nje ya ISRA usirudi mpaka pale nitakapo kutaarifu" Alisema Gu Gamilo kauli iliyomfanya Dojin atoe macho kwa mshangao.

Je nini kitafuta?

Ni shillingi elf 1 tu 0756862047

Tayari tumeifahamu historia ya SASHA kwa ufupi...

Sasha ataweza kutoshoshwa?

Vipi kuhusu David naye ataweza kutoroka kutoka kwenye lile Bonde?

ITAENDELEA....
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
 
FROM ISRA TO ISRA
Sehemu ya............19
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Naitwa Dayana, nilitekwa na kuletwa hapa kama wewe, ni mwaka mmoja sasa umepita, niko hapa" Alielaza Dayana...
"Mwaka?" David aliuliza kwa mshangao.
Naam huyu ni Dayana yule yule ambaye Godfrey kaka yake Tesha alidai amempoteza mwaka mmoja uliopita.

SASA ENDELEA....

"Ndio nina mwaka na mwezi mmoja tangu nimetupwa ndani ya hili bonde" Alijibu Dayana.

David alitulia kwa sekunde kadhaa akijaribu kulitafakari jibu hilo kutoka kwa Dayana. Aligeuka kumtazama mwanamke huyo ambaye wala hakuwa na hata chembe ya aibu kwa namna alivyokuwa amevaa, asilimia kubwa ya mwili wake ulikuwa wazi, chupi na sidiria aliyovaa ndio angalau vilimsitiri sehemu zake nyeti lakini bado hata sidiria yake ilikuwa imechanika upande hivyo kufanya nusu ya matiti yake madogo kuwa wazi.

"Kwa hiyo mkiwa humu huwa mnafanya nini? Kuna kazi mnafanya kama watumwa?" Mwisho David akauliza.

"Wala tunaishi tu kama unavyotuona. Mimi pia wakati nimefika nilihisi labda tumeletwa kama watumwa tutafanyishwa kazi usiku na mchana lakini hapa mambo ni tofauti kabisa tunaamka tunakula tunalala tunaamka tunakula tunalala hayo ndio maisha yetu. Isipokuwa chakula ni cha shida sana. Kama ulivyoona, tunaishi kwa kugombaniana chakula mwenye nguvu ndio ataishi. Wapo watu waliofia humu kwa sababu ya kukosa chakula na maji"
Maelezo haya kutoka kwa Dayana yalizidi kumtisha David. Akatamani kujua zaidi.

"Kwa hiyo sababu ya hawa watu kutuleta hapa ni nini?"

"Sijui, kwa kweli sijui kabisa! Huwa mwanatuita sisi wote ni FUNGUO, funguo ya mkuu wa eneo hili anaitwa MAGNUS" Kwa mara ya pili Sasa David analisikia jina la mtu huyu aitwae Magnus. Mara ya kwanza alilisikia kutoka kwa Femi wakati ule wakiwa ndani ya meli.

"Funguo?"

"Ndiyo SISI NI FUNGUO"

"Funguzo za nini?"

"Funguo za Magnus"

"Kufungua nini?"

"Sielewi, inaonekana alishafungwa mahali kwa hiyo sisi ni kama funguo zake. Huwa anakuja kutusalimia mara moja moja, akisimama pale juu utasikia anapaza sauti anasema HABARI ZA LEO FUNGUO ZANGU.... Huwa simpendi yule mzee, anatisha hana utu ndani yake, anakera hata kumtazama" Alieleza Dayana.
Kimya kikatawala tena kwa muda

"Kwa hiyo hakuna namna yoyote ya kutoka humu? Hakuna aliyewahi kutoroka akafanikiwa?" Aliuliza David

"Hahahah! Utatoroka uende wapi, utatokaje kwenye hili bonde? Kila aliyejaribu kutoroka aliishia kufa. Kifupi hakuna namna yoyote ya kutoroka.."

"Ipo namna! ipo sema ni uwoga wako tu..." Mara sauti ya kiume ilisikika ikipingana na maelezo ya Dayana. Akatokea jamaa mmoja mwembamba na mrefu, akafika na kukaa pembeni ya David, alikuwa ni mmoja wao ndani ya bonde lile.

"Zungu..!!" Dayana aliita kwa mshangao.

"Nini!? Naona umepata boyfriend mpya umeamua kunikimbia"

"Acha masihara yako bwana huyu ni mgeni nimekuja kumriwadha kidogo..."

"Upo kamati ya mapokezi humu bondeni au? halafu mbona wamekuja wageni kibao mbona umewaacha umekuja kwa huyu mwamba hapa, umeshampenda tayari?" Aliuliza Zungu huku akichukua mkate ambao Dayana alimpa David akaanza kula.

"Unaitwa nani jamaa?" Aliuliza Zungu, David akawa kimya.
"Huna jina?"

"David.."

"David wow! Napendaga watu wenye majina ya Biblia kidogo huwa wanakuwa waelewa, sasa sikia David usimsikilize huyu Dayana ni muoga, kutoroka hapa inawezekana kabisa kama tukiamua mtu wangu, sema tawile" Alieleza Zungu

"Muongo usimsikilize anataka akufanye chambo, utakufa David" Dayana akadakia

"Kausha basi na wewe... Tangu lini nikaongopa au unafikiri mimi muongo muongo kama wewe!?"

"Kwani mimi niliwahi kukudanganya nini?"

"Hujui au?"

"Nini...!!"

"Unasikia David huyu demu alipofika kwenye hili bonde kwa mara ya kwanza wahuni walitaka kupita naye, walitaka kumbaka, mimi ndio nikamtetea. Mpaka leo hajawahi kunipa chochote anazingua"

"Kwa hiyo ulitaka nikupe nini!?"

"Kwani wewe hujui au?"

"Sijui, nitakupa nini sasa"

"Wewe ni mwanamke alafu hujui cha kunipa..."

"Kwa hiyo umesema kutoroka inawezekana?" David akaingilia kati mazungumzo ya Dayana na Zungu.

"Yes! Wewe uko safi sana, subiri watu walale nitakupeleka mahali, kila siku mimi huwa nafanya utafiti namna ya kutoroka tayari nazijua njia nyingi zinazotoka hadi nje kabisa ya hili bonde ishu ni kuvuka huo mlima hadi upande wa pili kule ufukweni" Alieleza Zungu


ISRA
Mkuu wa ISRA Gu Gamilo alionekana akiwa amekaa meza moja na shemeji yake Dumayo. Ilikuwa ni muda mfupi umepita tangu awatawanye wale viongozi wa ISRA na kuwaambia wafike asubuhi ya siku inayofuata kujadili hukumu ya SASHA.

"Unajua huwa siamini kabisa mtu ambaye tulishirikiana naye bega kwa bega hadi tukafanikiwa kumuondoa MAGNUS hapa ISRA leo hii amegeuka na kuwa msaliti kama vile Magnus mwenyewe" Alisema Gu Gamilo huku akimtazama Dumayo usoni.

"Ah! Tatizo Shemeji unashindwa kunielewa, mimi siku zote huwa nasimama upande wenye haki. Ndio maana nilipambana kufa na kupona hadi tukamshinda na kumuondoa Magnus" Alieleza Dumayo. Gu Gamilo akawa anamtazama akijua kabisa Dumayo hakuwa anamaanisha anachokisema hata kidogo bali moyo wake umejaa chuki na wivu mkubwa.

"Kwa hiyo ulishindwa kumstiri binti yangu? kulikuwa na ulazima gani wa kumdharirisha Sasha namna ile, huoni kama umenichafua hata mimi?''

"Sasha kavunja sheria na kusababisha balaa kubwa ndani ya ISRA shemeji. Lazima aadhibiwe, Nilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo unavyotaka lakini unajua kwa nini sijafanya?"

"Kwa nini?"

"Kwa sababu siku zote umekuwa ukimpendelea Sasha kuliko watoto wako wengine? Kuna kila dalili kuwa hata kiti chako cha uongozi siku moja utamrithisha Sasha na sio mtu mwingine ndio maana nataka nimfutilie mbali huyu binti"
"Kwanini, unahisi Sasha hastahiri kuwa mkuu wa ISRA hapo baadae?"

"Gu Gamilo, unajua kabisa Sasha sio familia yako! Sasha sio damu yako Sasha sio mtoto wenu wala sio...." Alisema Dumayo lakini kabla hajamalizia sentensi yake tayari upanga wa Gu Gamilo ulikuwa kwenye shingo yake.

"Katu! Nisije sikia kwa mara nyingine unaongea huo upuunzi mbele yangu wala mbele ya mtu yeyote yule Dumayo ni marufuku. Siku nikikusikia tena nitakukata shingo yako bila huruma.... Sasha ni mwanangu...ni binti yangu" Gu Gamilo aliongea kwa msisitizo akionekana mwenye jazba sana kisha akatupa upanga chini, akainuka na kuondoka.

"Ahahah! Nimekugusa pabaya... Hata hivyo huna utakalo fanya tayari Sasha ameshavuruga mambo..." Dumayo alijisemea mwenyewe. Wakati huo mdogo wake yaani Malkia Hella akajitokeza mahali alipokuwa amejificha akifuatilia maongezi ya mumewe na kaka yake.

"Sijui ni mdudu gani alishamuingia huyu mwanaume huwa hataki kabisa kusikia mtu akisema Sasha sio mtoto wetu" Alisema Malkia Hella huku akisogea na kukaa pale alipokuwa amekaa Gu Gamilo kabla hajaondoka.

"Usijali dada tayari tumeshapata njia ya kumtoa Sasha hapa Ikulu na ikiwezekana atanyang'anywa nguvu zake na kufukuzwa kabisa hadi nje ya ISRA kama vile alivyofanyiwa Magnus" alisema Dumayo

"Mmh! Kwa kweli sidhani, kwa namna anavyompenda Sasha sijui kama ataweza kuruhusu hili litoke"

"Ataruhusu tu apende asipende, halafu ni kwa nini anakapenda sana haka ka binti"

"Hata sielewi kaka yangu! Niliwahi kumpeleleza siku moja akadai kuwa aliambiwa na mtabiri mmoja kuwa Sasha ndiye atakuja kuiokoa ISRA hapo baadae kama ikiingia kwenye matatizo"

"Hahahahah hahahahah! Mtabiri gani huyo.. ni Bi Noha au?" Dumayo alicheka sana na kuuliza.
"Hapana sio Bi Noha"
Dumayo akazidi kucheka tena na tena.


Baada ya Gu Gamilo kuondoka, alienda ndani ya chumba kimoja cha siri akaagiza askari wake mashuhuri sana ISRA aitwe.

Baada ya muda askari huyo alifika na kumsalimia mkuu wa ISRA Gu Gamilo kwa heshima kubwa.

"Dojin" Gu Gamilo aliita

"Ndiyo Mheshimiwa"

"Nimekwita hapa nataka nikupe kazi moja ngumu ambayo itakuwa ni kubwa pengine kuliko kazi zote nilizowahi kukupa hapo kabla"

"Niko tayari kufanya kazi yoyote utakayonipa Mheshimiwa"

"Dojin.." Gu Gamilo aliita tena

"Ndiyo mkuu"

"Siku zote tumekuwa tukipambana kuiweka ISRA kwenye mikono salama, tumepigana vita nyingi na ngumu tukiwa pamoja. Vita hivyo bado havijafika mwisho Dojin. Unakumbuka kuna mtoto tuliwahi kumuokota wakati ule tukipigana vita na Magnus miaka mingi iliyopita?"

"Nakumbuka mkuu wangu"

"Unakumbuka nini kilitokea siku hiyo baada ya kumuokota huyo mtoto mchanga?"

"Nakumbuka kila kitu Mheshimiwa, alitokea bibi kizee mmoja wa ajabu akasema tumlee na kumlinda huyo mtoto kwa sababu ameibeba hatima ya ISRA hapo baadae"

"Vizuri kumbe unakumbuka, basi hayo maneno hata Bi Noha alishawahi kuniambia pia siku nilipo kutana naye. Unajua huyo mtoto mchanga tuliyemuokota ni nani?"
"Hapana sijui Mheshimiwa!?"

"Ni Sasha... Huyu binti yangu ambaye natakiwa kuitoa hukumu yake kesho" Alisema Gu Gamilo kauli iliyomshtua na kumuacha kinywa wazi Dojin. Siku zote alikuwa anaamini Sasha ni mtoto halisi wa Gu Gamilo kama wengine wanavyoamini. Hakuwa akijua kama yule mtoto waliyemuokota wakati ule alilelewa na Mkuu wa ISRA na ndio Sasha mwenyewe, hii ilikuwa ni siri kubwa.

"Nakata umtoroshe Sasha, kimbia nenda naye mbali hakikisha anakuwa salama, ikiwezakana toka naye hadi nje ya ISRA usirudi mpaka pale nitakapo kutaarifu" Alisema Gu Gamilo kauli iliyomfanya Dojin atoe macho kwa mshangao.

Je nini kitafuta?

Ni shillingi elf 1 tu 0756862047

Tayari tumeifahamu historia ya SASHA kwa ufupi...

Sasha ataweza kutoshoshwa?

Vipi kuhusu David naye ataweza kutoroka kutoka kwenye lile Bonde?

ITAENDELEA....
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
 
FORM ISRA TO ISRA
Sehemu ya............20
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...

"Nakata umtoroshe Sasha, kimbia nenda naye mbali hakikisha anakuwa salama, ikiwezakana toka naye hadi nje ya ISRA usirudi mpaka pale nitakapo kutaarifu" Alisema Gu Gamilo kauli iliyomfanya Dojin atoe macho kwa mshangao.

SASA ENDELEA...

"Siko tayari kumuona binti yangu anapewa adhabu ya kifo au hata kufukuzwa ISRA, kama atanyang'anywa nguvu zake na kufukuzwa sito isamehe nafsi yangu milele. Kumbuka tuliagizwa kumlinda tangu akiwa ni mtoto mchanga, nimefanya hivyo mpaka sasa ana umri wa miaka 23. Siwezi kukubali kumpoteza Sasha kirahisi namna hii" Gu Gamilo alitoa maelezo ambayo kwa kiasi yalimuingia askari wake mashuhuri Dojin. Lakini bado jukumu analopewa kumtorosha Sasha lilikuwa ni gumu mno.

Dakika chache baadae Gu Gamilo akiongozana na Dojin waliingia hadi gerezani kule alipofungiwa Sasha na wenzake.
Ulinzi ulikuwa ni mkali sana eneo hilo lakini kwa kuwa ni Mkuu wa ISRA basi aliachwa apite pasipo pingamizi lolote.

"Babaaa.." Sasha aliita hali akionekana kuwa na uchungu mkubwa mara tu baada ya kumuona baba yake Gu Gamilo akija pale alipo.

"Nisubiri hapa.." Gu Gamilo alimwambia Dojin naye akatii, hakutaka askari huyo asikilize maongezi kati yake na binti yake Sasha.
Gu Gamilo alipiga hatua akasimama nyuma ya uzio wa nondo za chuma ambao uliwatenganisha yeye na binti yake aliyepo ndani ya gereza hilo.

"Mwanangu..." Aliita Gu Gamilo huku akikumbatiana na binti yake kwa taabu sana wakipitisha mikono yao katikati ya zile nondo. Gu Gamilo akambusu Sasha katika paji la uso.

"Nisamehe baba, nisamehe sana"

"Usijali Sasha naelewa, ni kosa langu mimi.... Kwa mara ya kwanza nilikuacha utoke nje ya Ikulu lakini sikukupa maelezo ya kutosha nini ufanye na nini usifanye. Nisamehe mimi mwanangu" Gu Gamilo aliongea kwa uchungu mkubwa.
Wakazidi kukumbatiana na mwanae ambaye alilia kwa uchungu sana.

"Yako wapi machozi uliyokusanya?" Aliuliza Gu Gamilo, Sasha akaingiza mkono wake ndani ya mfuko wa gauni lake akatoa ile chupa aliyokuwa akiitumia kukusanya machozi akamkabithi baba yake.

"Sikufanikiwa kujaza machozi, nisamehe baba yangu"

"Usijali ni mara yako ya kwanza, hata hivyo umejitahidi sana"
Kimya kilitawala kwa sekunde kadhaa..

"Sasha" Gu Gamilo aliita.

"Abee..."

"Najua ni kweli uliingia kwenye ule msitu! Niambie ni nini uliona? Je ulifanikiwa kukutana na Bi Noha?" Gu Gamilo aliuliza maswali mfululizo kwa sauti ya chini na tulivu huku akionekana kuwa na shauku ya kujua.

Sasha akawa kimya hakujibu kitu.

"Nambie tu mwanangu usiogope.. Bi Noha alikwambia nini?"

Sasha aliendelea kuwa kimya, alikumbuka vizuri katazo alilopewa kuwa kila alichoambiwa na Bi Noha kinatakiwa kubaki siri, hakutakiwa kumweleza mtu yeyote yule kuhusu jukumu zito la kumlinda mwanadamu aitwae David.

"Sikumbuki kitu baba, sikumbuki kabisa, kumbukumbu zangu zimepotea" Sasha alidanganya.
Gu Gamilo alimtazama usoni akajua wazi binti yake hayuko radhi kueleza ukweli.

"Sawa mwanangu, basi nisikilize kwa makini, sitaki kesho uadhibiwe tayari kuna mtu nimemuandaa atakutorosha usiku wa leo, mtakimbia na kwenda mbali mahali ambapo hawawezi kuwapata"

"Hapana! Hapana baba huwezi kufanya hivyo"

"Nisikilize mimi baba yako Sasha! Unatakiwa kuondoka ISRA haraka iwezekanavyo"

"Hapana! Siwezi baba... Tayari nimekuweka kwenye matatizo, sitaki niendelee kuwa mzigo kwako. Acha waniadhibu vile wanavyotaka wao wewe baki kama Mkuu wa ISRA simama kwenye sheria za ISRA"

"Sasha...!" Gu Gamilo alifoka.

"Baba siwezi. Hata nikitoroka kila mtu atajua kuwa wewe ndio umenitorosha. Ya nini hayo yote, acha tu baba usihangaike na mimi"

"Sijali hayo yote mwanangu! Ni lazima uwe hai ni lazima uishi Sasha, wewe ni muhimu kuliko unavyofikiri"

"Ni muhimu kwako baba lakini sio muhimu kuliko sheria za ISRA" Sasha aliendelea kushikilia msimamo wake.
Kimya kilitawala tena kwa muda...

"Hii ni amri, sio ombi tena. Mimi kama mkuu wa ISRA nataka uishi, usiku wa leo ni lazima utoroshwe na Dojin" Aliongea Gu Gamilo kwa sauti iliyojaa mamlaka.

"Ni kheri nife kuliko kufanya hivyo baba..." Alisema Sasha kisha taratibu akaanza kufungua kamba za gauni lake.
Hii ilikuwa na maana kwamba, kwa sheria za ISRA mwanamke yeyote ambaye ataonyesha mwili wake mbele ya mwanaume asiye mume wake basi hastahiri kuishi. Hata sehemu ya mabega yake ikiwa wazi tayari anakuwa amevunja sheria hiyo ya ISRA. Baada ya kulazimishwa sana na baba yake Sasha aliona ni heri ajitengenezee adhabu hiyo ya kifo kwa kuivunja sheria hiyo ya ISRA kwani tayari mbele yake kulikuwa na wanaume wawili, Dojin na Gu Gamilo baba yake. Aliona ni heri kufa kuliko kuendelea kuwa mzigo kwa baba yake.

"Sasha achaaa...." Alisema Gu Gamilo huku akitazama pembeni na kuondoka haraka, Dojin naye aliziba macho yake akageuka na kumfuata Gu Gamilo nyuma, wakaondoka upesi huku Gu Gamilo alionekana mwenye hasira sana.

Hali machozi yakimtoka Sasha alisitisha kufanya kile alichokusudia kufanya, akafunga tena kamba za gauni lake akaegemeza kichwa chake ukutani huku machozi yakimbubujika kama maji.

Wakati haya yakiendelea kulikuwa na askri mmoja mpambe wa karibu wa Dumayo, alikuwa akifuatilia kwa karibu nyendo zote za Gu Gamilo. Mara baada ya kuondoka askari huyu alikimbia kupeleka habari kwa Dumayo juu ya kila alichokiona na kusikia. Alifika akaingia ndani ya chumba alichoandaliwa Dumayo kama mgeni katika Ikulu ya ISRA, akawa anamnong'oneza.

Dumayo alitabasamu mara baada ya kusikiliza maelezo ya askari huyo.

"Kwa hiyo Sasha amekataa kutoroshwa?" Aliuliza Dumayo.
"Ndiyo, kagoma kabisa..."

"Pumbaaafu, angejichanganya kidogo tu basi ndio ulikuwa mwisho wake yeye na baba yake" Alisema Dumayo, kisha akamgeukia askari wake.

"Endelea kuwafuatilia, ukiona kitu chochote cha tofauti njoo haraka unipe taarifa"

"Sawa Mheshimiwa" Alijibu yule askari kisha akaondoka. Dumayo naye akaingia chumbani na kujitupa kitandani.


Ulikuwa ni usiku mzito mno. Usiku mzito kwa Dumayo, Gu Gamilo, Malkia Hella na Sasha. Usiku mzito pia kwa Tesha, Brandina na David.

Dumayo yeye alikuwa akiisubiri kwa hamu asubuhi ya siku inayofuata ili kujua ni hukumu gani itapitishwa na Mkuu wa ISRA Gu Gamilo.

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Gu Gamilo mwenyewe. Usiku huo akiwa kitandani alitazama juu ya paa huku akili yake ikiwaza nini afanye, tayari binti yake Sasha amekataa katakata kutoroshwa na ameona ni heri kufa kuliko kuzidisha matatizo kwa baba yake. Kichwa kikazidi kumuuma Gu Gamilo, muda ulizidi kusonga bado hakuwa na jibu nini afanye.
Pembeni yake alilala mkewe Malkia Hella, naye hakuwa na usingizi, alikuwa akiisubiri kwa hamu asubuhi ya siku inayofuata ili ashuhudie mtoto wake wa kumlea ambaye ni kipenzi cha mumewe akipewa adhabu ambayo aliamini lazima itamfurasha.

Hali ilikuwa hivyo kwa Sasha pia kule gerezani, tayari alishakata tamaa ya kila kitu. Hakujua hatima yake itakuwa ni ipi itakapofika asubuhi. Lakini kila alipokumbuka maelezo aliyopewa na marehemu Bi Noha kule msituni, moyoni akapata tumaini.
"Sitokufa" Sasha alijisemea mwenyewe.


Upande wa pili kwa mwanamke mrembo kupindukia na mwanamitindo maarufu nchini Tanzania Tesha, naye hakupata hata repe la usingizi. Wakati wote alikuwa akimfikiria David. Ni mwanaume aliyemzoea kwa muda mfupi sana lakini anashangaa kuona moyo wake unatamani kuendelea kuwa karibu naye. Hakujua kama yuko salama au laa! yuko hai au wamemuua.
Kwa muda mfupi Tesha alijikuta anamsahau kabisa mpenzi wake Felix ambaye kwa sasa amemtelekeza na kwenda zake Marekani.

Usiku huo pia polisi mpelelezi Brandina naye hakuwa amelala. Alikuwa nyumbani kwake ndani ya chumba kimoja kidogo. Ukutani kulikuwa na ubao wenye picha nyingi zikiwemo zile picha alizopiga Godfrey kaka yake Tesha wakati wa tukio la kutekwa kwa David pale mgahawani.
Brandina alikuwa akiichimba kwa undani kesi ya utekaji wa watu katika maeneo mbalimbali nchini.
Ni muda mrefu tangu Brandina na askari wenzake wameanza kuipeleleza kesi hii lakini mpaka sasa hawakuwa na majibu kamili ni wapi wanapelekwa mateka hao? Ni nani kiongozi wa oparesheni hiyo ya utekaji? Ni nini sababu ya kufanya utekaji huo?, Hakuna aliyejua.
Lakini moja kati ya picha zilizokuwa katika ubao ule ilikuwa ni picha ya Felix mpenzi wa Tesha. Ilionekana wazi Brandina anamjua Felix vizuri na ni mmoja kati ya watu anaowafuatilia.


Upande mwingine usiku ulikuwa ni mrefu pia kwa kijana David akiwa ndani ya lile bonde la ajabu.
Tayari maisha yake yamebadilika ghafula na kujikuta ni mmoja kati ya mateka wanaoshinda wakiwa wamevaa nguo za ndani pekee, si wanaume si wanawake. Wote walikuwa ni mateka wa mtu wanayemuita Magnus.
Huyu alikuwa ni Magnus yule yule kutoka ISRA kaka yake Gu Gamilo na baba mkubwa wa Sasha. Alifukuzwa ISRA miaka mingi iliyopita mara baada ya kufanya uasi mkubwa, tangu siku hiyo hakuwahi kurudi tena ISRA.

David alikuwa amekaa na kuegemea ukuta wa bonde hilo huku yule mwanamke Dayana akiwa amelala usingizi miguuni pake.
David alikuwa akisubiri wakati ufike ambao Zungu alimuahidi atamuonyesha njia za kutoka katika bonde hilo.

Je nini hatima ya MKASA huu?
Endelea kuwa nami Katika sehemu zinazofuata.

ITAENDELEA....

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047
 
TUNAENDELEA KESHO
FB_IMG_1704734287293.jpg
 
KUTOKA ISRA KWENDA ISRA
Sehemu ya............21
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

MAREKANI
Ni Katika hoteli moja ya kifahari na maarufu nchini Marekani - LUXOR LAS VEGAS ndani ya mji wa Nevada. Mwanaume mmoja wa ki-afrika anaonekana akiwa ndani ya bwawa la kuogelea 'swimming pool' alikuwa amejilaza juu ya boya lililomfanya aelee juu ya maji huku akiwa ameitanua mikono na miguu yake.
Kijana huyu anaeonekana kuwa na pesa ndefu aliyafumba macho yake na kutulia. Alionekana mtu mwenye mawazo sana.

Mara simu yake iliyokuwa juu ya meza pembeni ya bwawa hilo ilitoa muungurumo 'vibration'.
Mwanaume huyu alifumbua macho yake kisha akajivuta hadi pembeni ya bwawa akajifunga taulo lake na kuifuata simu yake.
Kulikuwa na jumbe sita zilizoingia mfululizo kwenye programu ya WhatsApp akazifungua. Akaona ujumbe wa maandishi ulioambatana na picha nne pamoja na video moja.
Mwanaume huyo alifungua na kuzitazama kwanza zile picha.
Zilikuwa ni picha zilizomuonyesha mwanamitindo maarufu nchini Tanzania Tesha akiwa kwenye mazungumzo nyeti na kijana mmoja aitwae David mgahawani.
Kama utakumbuka wakati ule Tesha na David walipokuwa mgahawani wakifanya mazungumzo kuna mtu alionekana anawapiga picha kwa siri.

Mwanaume huyo alionyesha mshtuko kiasi mara baada ya kuziona picha zile, haraka akausoma ujumbe wa maandishi kabla ya kuicheza ile video. Ujumbe ulisomeka hivi...

,,,,,,Bro Felix huyu ndio jamaa anaonekana kuwa karibu sana na Shem Tesha siku za hivi karibuni na hii ni video ya majibu aliyoyatoa leo kuhusu uhalisia wa mahusiano yake wakati akihojiwa na waandishi wa habari,,,,,,

Alimaliza kuusoma ujumbe huo taratibu mapigo yake ya moyo yakaanza kumuenda mbio
Ndiyo, Mwanaume huyu alikuwa ni Felix yule mpenzi wa Tesha ambaye amekuwa akitajwa mara nyingi kuwa ameondoka na kumtelekeza Tesha akaja Marekani. Bado haikujulikana sababu hasa ya Felix kufanya hivyo lakini pamoja na hayo yote Felix alimuajili mtu nchini Tanzania ambaye alikuwa akimfuatilia Tesha kwa ukaribu na kumpa habari kwa kila anachokifanya. Hii ni ishara tosha kwamba bado Felix anamuhitaji Tesha.

Ujumbe huo ulimfanya Felix kuingiwa na ubaridi wa hofu, haraka bila kupoteza muda akaicheza ile video. Ilikuwa ni kipande kifupi cha video kilichomuonyesha Tesha akifanya mahojiano na waandishi wa habari wakati ule pale hospitali alipomsindikiza David kumuona mama yake.

" Na vipi kuhusu msimamo wa mahusiano yako kwa sasa , still upo single kama unavyosema siku zote ?" Aliuliza mwandishi wa habari

"Hahahah Nooo! Am not single ... soon nitaenda kumuweka wazi mkalia ini wangu "

" Wow tutegemee lini miss Tesha ..."
" Nimesema soon, so ni suala la kukaa na kusubiri, as you know mimi nikiongea kitu lazima nikitimize "
" Sawa Tesha, Hivi karibuni umekuwa uki ...."
" Hapana jamani inatosha next time "


Video iliishia hapo lakini tayari ilitosha kumfanya Felix awe katika hali ya kupaniki.

Felix akatembea haraka kuelekea chumbani kwake lakini kabla hajafika njiani anakutana na msaidizi wake wa karibu ambaye alitoka kidogo wakati bosi wake akiogelea, aliitwa Haron.

"Bosi vipi kwema!?" Aliuliza Haron

"Sio kwema hata kidogo" alijibu Felix akapiga hatua na kuingia ndani ya chumba chake akakaa kindani.

"Nini shida tena Mkuu?"
Felix hakujibu alitulia kimya akiwa amejiinamia kwa sekunde kadhaa kisha akainua uso wake na kumtazama Haron usoni.

"Hivi ni kwa nini mnaninyima uhuru wangu? Kwa nini wewe na baba mnataka niishi vile mnavyotaka ninyi na sio ninavyotaka mimi?" Felix aliuliza huku akimtazama Haron kwa macho makali, alionekana kuwa na jazba.

"Ni kuhusu Tesha tena au?" Aliuliza Haron

"Ndiyo ni kuhusu mwanamke ninaempenda Tesha, hivi Haron unajua nini kinataka kutokea? Tesha amechoka kusubiri sasa anataka kuniacha kwa sababu ya sheria zenu za ajabu nisizozi....."

"Kaa kimya Felix" Haron alimkatisha Felix aliyekuwa akilalamika huku akitupa mikono yake kama mwendawazimu.

Haron akapiga hatua akasogea karibu kabisa na Felix, sasa wakawa wanatazamana

"Hivi ni mara ngapi tukueleze kwamba hutakiwi kumpenda mwanadamu, Felix wewe sio kama wao. Hapa sio kwenu, inabidi akili yako ipambane kufikiria ni jinsi gani tunamsaidia baba yako MAGNUS kurudi nyumbani kwetu ISRA huna cha....."

"Mimi ni Binadamu Haron, sina tofauti na wao, nina haki ya kupenda kama wengine wanavyopenda. Nampenda Tesha na niko tayari hata kufa kwa ajili yake. Hakuna mtu anaweza kunizuia narudia tena HAKUNAAA" Felix alifoka

"Huna unachokijua Felix, wakati baba na mama yako wanafukuzwa ISRA ulikuwa mtoto mdogo sana, huelewi chochote kwa hiyo sio kosa lako. Ila kaa ukijua hapa sio kwetu na hutakiwi kumpenda mwanadamu yeyote, hizi ni sheria za nyumbani kwetu ISRA unatakiwa kuziheshimu kwa sababu wewe pia umezaliwa huko. Hii ndio sababu baba yako amekuleta Marekani ili kukuweka mbali na yule mwanamke Tesha. Sasa kama utalazimisha basi utamuweka hatarini hata huyo Tesha mwenyewe, Magnus baba yako atamuua"

"Eeh! Atamuua eti eeh! Kwa hiyo mnajaribu kunitishia si ndio?... Sawa, tutaona"
Alisema Felix kisha akainuka pale kitandani, akasogea mbele akachukua wembe uliokuwa mezani, bila kusita akajikata kidogo kwenye mshipa wa damu mkono wake wa kulia.

Haron alitoa macho kumshangaa Felix asijue nini maana yake.

Damu yenye rangi ya kijani ikawa inamtoka Felix mahali alipojijeruhi.

"Unaona hii damu, i swear one day I'll bleed red... Siku moja nitavuja damu nyekundu. Siku ambayo nitajitenga na ninyi, nitaanza maisha yangu nikiwa huru kama watu wengine. Nakwambia wewe na baba pia nitamwambia" Felix aliongea akimaanisha, akachukua simu yake tena na kutazama zile picha alizotumiwa.

"Oda tiketi mbili za ndege kesho asubuhi na mapema tunaanza safari kurudi Tanzania" Alisema Felix

"Nini?"

"Kama hutaki acha nitapiga simu mwenyewe" Alijibu Felix kisha akaondoka na kuingia bafuni.

"Nilijua tu haitokuwa rahisi kukuongoza, ngoja nimtaarifu baba yako tuone, sitaki shida mimi" Haron alijisemea mwenyewe huku akichukua simu yake akapiga namba alizokuwa amezihifadhi kwa jina la 'ISRA KING' ni namba za Magnus.


Upande wa pili simu iliita kwa muda mwisho ikapokelewa.

"Mheshimiwa Felix mwanao anataka kurudi nyumbani, kuna taarifa amezipata hukusu yule mpenzi wake. Sasa analazimisha kurudi nyumbani"

"Naingia darasani kwa sasa, fanya vile anavyotaka. Muache arudi" Sauti nzito na yenye kukwaruza ilijibu kwa ufupi kutoka upande wa pili wa simu kisha ikakatwa.

Katika moja ya majengo makubwa ndani ya kile kisiwa walichopelekwa mateka David na wengine, alionekana Mzee mmoja mwenye umri kama miaka 67 hivi. Alikuwa na uso mweusi wenye sura ngumu iliyokomaa Nywele zake ndefu na nyeupe sana zinazofika mabegani mwake, hata ndevu zake nyingi zilikuwa na rangi nyeupe pia. Macho yake yalikuwa ni mekundu sana, kila alipotembea aliongozana na wanawake wanne ambao mikononi mwao walishikilia visahani vidogo vilivyokuwa na mizizi fulani iliyochomwa na kutoa moshi mwingi mweupe. Harufu ya Moshi huo ilikuwa ni burudani tosha kwa mzee huyo ambaye wakati huu alikuwa amevalia kanzu nzito nyeusi inayoburuza chini pale anapotembea.
Naam huyu si mwingine bali ndiye MAGNUS mwenyewe kutoka ISRA, kaka yake Gu Gamilo na baba mkubwa wa Sasha lakini pia ni baba mzazi wa kijana Felix.
Magnus alitembea taratibu sana huku mikono yake ikiwa nyuma. Kila alipopita askari wake walinzi waliinamisha vichwa vyao chini kwa heshima kubwa.
Mwisho Magnus aliingia katika chumba kimoja kikubwa mithiri wa hekaru. Ndani alikuta kuna watu karibu thelathini wamekaa wanasubiri. Wengi wao walikuwa ni wanawake waliovalia magauni mekundu. Wanaume ambao idadi yao ilikuwa ni watu sita pekee wao walivaa kanzu ndefu zenye rangi nyekundu pia.
Hawa waliitwa wanafunzi wa Magnus. Jambo la kushangaza miongoni mwa wanafunzi hao alikuwepo Zucc na Femi wale wanawake wawili kutoka ISRA waliotumwa kumuua kijana David lakini wakashindwa na mwisho wakajikuta wanatekwa na kuletwa katika kisiwa hicho cha Magnus. Hivi ndivyo Magnus alivyofanya wakati wote. Mateka wote kutoka ISRA aliwageuza wanafunzi wake huku akiwafundisha mambo mengi kiasi cha kuweza kuwashawishi na kuwafanya watu wake waaminifu. Lakini mateka ambao ni binadamu aliwapeleka kule kwenye lile bonde la ajabu kama alivyofanya kwa David na wenzake huku akiwabatiza jina na kuwaita 'Funguo'.

Chumba hicho hakikuwa na taa, badala yake kulikuwa na mishumaa mikubwa iliyowekwa juu ukutani kukizunguuka chumba chote. Pia ukutani kulichorwa michoro mingi inayoonyesha picha na maadhari ya mji wa ISRA.

Magnus alifika na kusimama mbele ya darasa lake, wale wanawake alioongozana nao waliweka vile visahani vinavyotoa moshi mezani kisha wakaondoka na kutoka nje ya darasa hilo.

Magnus akiwa pale mbele aliwatazama wanafunzi wake kwa zamu mmoja baada ya mwingine kisha akaongea kwa sauti kubwa na nzito inayokoroma iliyojaa kitetemeshi.

"Mapinduzi yafanyikeeeee......!!!"

"Kwa ajili ya maisha bora ya ISRA na watu wake"
Wanafunzi wa Magnus waliitikia isipokuwa Zucc na Femi, hii ndiyo ilikuwa kauli mbiu ya Magnus na wanafunzi wake.
Akarudia tena huku safari hii akikunja ngumi mkono wake wa kulia na kuinua.

"MAPINDUZI YAFANYIKEEEEEEE....."

"KWA AJILI YA MAISHA BORA YA ISRA NA WATU WAKE...." Waliitika

Kelele hizo zilisikika mpaka kule bondeni aliko David na wenzake.
David aliinua macho yake kutazama juu ya bonde zinakotokea kelele hizo. Akawa haelewi ni nini kinaendelea.

"Kila siku huwa wanafanya hivyo..." Sauti ya Dayana iliyojaa usingizi ilisikika akiwa amelala pale miguuni pake.

"Kumbe haujalala?" Aliuliza David, huku akimtazama Dayana kwa macho yaliyojaa huruma. Ni mmoja kati ya wanawake wanaopitia mateso wakiishi nusu uchi ndani ya bonde hilo.

"Wameniamsha hao washezi na kelele zao, ujue najisikia vizuri sana kulala hapa miguuni pako David" Alisema Dayana huku akifumbua macho yake yaliyoregea akawa anamtazama David usoni.

ITAENDELEA...
Simulizi hii inapatikana yote hadi episode ya 125 kwa Tsh 1500/= tu lipa kwa namba M-PESA ~ 0756862047
AIRTEL MONEY~ 0788967317
JINA-SAUL MWANAWIMA
UKILIPIA TUMA SCREENSHOT AU SMS YA MALIPO kwa namba hizo hizo WhatsApp au kawaida
 
KUTOKA ISRA KWENDA ISRA
Sehemu ya............22
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Wameniamsha hao washezi na kelele zao, ujue najisikia vizuri sana kulala hapa miguuni pako David" Alisema Dayana huku akifumbua macho yake yaliyoregea akawa anamtazama David usoni.

Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA...

Usiku ulikuwa umesogea sana lakini mwanga wa mwezi ulisaidia kuwaangazia katika bonde lile kubwa na la ajabu.

"Kwa hiyo hivi ndivyo huwa unalala siku zote?" Aliuliza David


"Kivipi, kulala kwenye miguu ya watu au?" Dayana naye akajibu kwa swali huku akionekana kukelwa na kauli ya David.


"Hapana namaanisha hakuna sehemu za kulala! Baridi kali namna hii mnaweza kuishi hivi tena bila nguo alafu bado kuna vitu vingi sivielewi elewi Dayana"
Dayana alinyanyua kichwa chake kutoka miguuni kwa David kisha akakaa.


"Hivi kumbe nilivyokwambia awali watu wanakufa humu hukunielewa?"


"Sawa nakumbuka, lakini mbona wewe unaishi na umeniambia umemaliza mwaka mzima kwenye hili bonde, hii inawezekanaje? Kuna mahitaji muhimu ya kibinadamu humu bondeni hamna"


"Mfano nini David? Kama ni chakula umeona wanatupa mikate na maji kila siku asubuhi mchana na jioni, mahitaji gani mengine unataka? Humu ni kama kambi ya jeshi"


"Sawa lakini vipi kuhusu kulala, kuoga, kujisaidia, kujikinga na maradhi, hali ya hewa na mambo mengine mengi"
Aliuliza David, Dayana akacheka sana.


"Wewe ni last-born kwenu eeh! Mbona unadeka hivyo. Anyway David kila mtu humu anaishi kwa kujiongeza. Sio siri maisha ni magumu mno kama unavyosema. Kuna muda hadi unaweza kutamani kufa lakini ndio hivyo bado tunapenda kuendelea kuishi tunaamini siku moja ipo tutaokolewa kutoka kwenye hili bonde la mauti. Kuhusu kuoga sijui nini, kuna mto na chemchem za maji huko mbele nitakupeleka kesho ukaone. Kama ni baridi inazuilika ndio maana unaona watu wamekaa kimakundi makundi wamewasha moto wanaota. Hivyo maisha yanasonga. Wapo wanaojaribu kujenga vibanda humu humu bondeni. Usinione hivi nilikuwa mnene sana na mwili wangu ulionawili lakini sasa nimekonda hatari na bado naendelea kukonda"
Alieleza Dayana.


"Kwa hiyo hapo ndio umekonda?" Aliuliza David huku akiukagua mwili wa Dayana juu hadi chini. Tayari David alianza kuizoea hali ya kukaa nusu uchi wala hakuwa na haya tena ya kumtazama Dayana.

Mara Zungu akatokea akiwa amebeba rundo la kuni na nyasi kiasi. Begani mwake alikuwa na nguo ya ndani (taiti).


"Ooh! Mrembo wangu umeamkaa? Au wamekuamsha hao jamaa wa Mapinduzi Yafanyikeee...Kwa ajili ya maisha bora ya ISRA na watu wake" Alisema Zungu na kuirudia ile kauli mbiu ya Magnus na wanafunzi wake, alikuwa akiisikia kila siku usiku wakati wa darasa la Magnus hivyo aliikalili.


"Huko ISRA wanakotaka maisha bora ndio wapi kwani?" Aliuliza David


"Hakuna mtu anayejua, sisi wenyewe tunaishia kusikia kama wewe. Labda hapa ndio ISRA yenyewe utajuaje" Alisema Zungu huku akiutua ule mzigo wa kuni akauweka chini kisha akachukua ile nguo ya ndani ya kike 'taiti' akamrushia Dayana.

"Umeiba wapi tena? Hata haijakauka maskini umeanua nguo ya watu Zungu" Alisema Dayana akiikagua nguo hiyo.


"Huitaki niirudishe au?"


"Aah! Hapana sijasema hivyo, asante Zungu kama Zungu, tena ngoja niivae sasa hivi" Alisema Dayana, akainuka na kuanza kuelekea kwenye kona moja ya bonde hilo.


"Sasa si uvalie hapa hapa" Alisema Zungu huku akitabasamu.
"Achana na mimi wewe..."


Dayana aliondoka kubadilisha nguo ya ndani aliyoletewa na Zungu. Wakati huo David akawa anamtazama Zungu namna anavyo hangaika kuwasha moto kwa kutumia mawe. Alikuwa akiyagonganisha mawe hayo yaliyotoa cheche za moto.

"Mbona unaniangalia sana mshikaji wangu, haya ndio maisha yetu. Tunapambana"


"Hiyo nguo uliyompa Dayana umetoa wapi kwani?"


"Nmetoa huko mtoni nilipoenda kukusanya kuni, kuna maza alikuwa kaanika alafu akapitiwa na usingizi hapo hapo, nikapita nayo"


"Kwa hiyo akiamka atavaa nini, atabaki uchi?"


"Atajua mwenyewe, mara nyingi huwa tunachukua nguo kutoka kwa watu waliokufa yaani maiti, mtu akifa ukiwahi unachukua nguo zake, angalau unakuwa hata na nguo mbili au tatu za kubadilisha. Mfano hii pensi ya jeans niliyovaa nilichukua kwa mwamba mmoja aliamua kujiua mwenyewe baada ya kuona maisha yamekuwa magumu humu bondeni, alizoea maisha ya kishua huko kwao. Alipoletwa tukamwambia watu tuna miaka humu bondeni akaona bora atembee na mia, akajipiga kitanzi" Alieleza Zungu na mara hiyo Dayana akawa amerejea akiwa amevaa ile taiti ya rangi ya pink.

"Woow! Umependeza mamaa kama Mobeto au Tesha kabisa" Alisema Zungu huku akimtazama Dayana kwa macho yaliyojaa tamaa za kiume.

David alijikuta anakumbuka mbali mara baada ya Zungu kumtaja staa Tesha, akawa amekaza macho yake kumtazama Dayana lakini alikuwa mbali kimawazo.

"Aah! Mwanangu macho hayo, demu wa watu huyu" Alisema Zungu kisha wote wakacheka kwa sauti.

Waliendelea kupiga stori mbili tatu David akionekana kutaka kujua mengi kuhusiana na uhalisia wa maisha ya mateka katika bonde la Magnus.

Mwisho ulifika ule mda ambao Zungu aliahidi angeenda kumuonyesha David njia za kutoka katika bonde hilo la ajabu. Wakainuka tayari kuondoka, Dayana naye akasimama.

"Na wewe vipi!?" Aliuliza Zungu

"Naenda pia, sikuamini kabisa Zungu unaweza ukamfanya chambo mkaka wa watu wakamuua bure."

"Aah! Hapana Dayana, mimi binafsi namuamini Zungu hawezi kunifanyia kitu kibaya, acha tuungane kuangalia ni namna gani ya kutoka kwenye hili bonde na hiki kisiwa. Binafsi siko tayari kumaliza mwaka kama ninyi, nitapambana na tutatoka kurudi nyumbani" David aliongea kwa sauti ya upole yenye kumaanisha, Dayana akatabasamu.

"Naam! Mwamba huyu hapa! Ujue siku zote nimekuwa natamani kushirikiana na mtu mwenye ujasiri kama wako David, sema nini kama anataka kutufuata acha twende naye" Alisema Zungu, mwisho wakakubaliana kuondoka kwa pamoja.

Walitembea kwa tahadhali sana wasije kushtukiwa na wenzao pamoja na askari walinzi ambao walikuwa wakirandaranda juu kabisa ya bonde hilo.

"Mmh! Hili bonde ni kubwa sana eeh!" Aliuliza David baada ya mwendo wa kama dakika tano hivi.

"Saana! Limekaa kama bakuli flani hivi, ni duara, ukuta umetuzunguuka pande zote. Na kila kona kuna walinzi, huwezi kutoka kirahisi mpaka uwe na master mind kama mimi" Alieleza Zungu na kujisifia kama kawaida yake.

Wakatembea tena kwa dakika mbili zaidi mara ghafula Zungu akasimama.

"Sasa sikieni, bakini kwanza kwenye hii kona mimi nikasome ramani hapo mbele. Huwa kunakuwa na walinzi wengi sana hapa tukishavuka tu huko mbele ni kuteleza, acha nicheki kwanza kama dakika 10 nitarudi" Alieleza Zungu kisha wakakubaliana hivyo akaondoka akiwaacha David na Dayana wanamsubiri.

David alisimama akiwa ameegemea ukuta wa bonde hilo, akayafumba macho yake akionekana kutafakari jambo. Kuna wakati alihisi labda yuko kwenye usingizi mzito wenye ndoto ya ajabu ataamka kama kawaida na kuendelea na maisha yake, lakini la hasha, kila kilichokuwa kinatokea kilikuwa ni kweli tupu.

Mara ghafula David alihisi kuna mtu amesimama mbele yake, haraka akafungua macho yake kutazama. Ni kweli kulikuwa na mtu.

"Dayana?" David aliita kwa mshangao

"David please!?" Alisema Dayana kwa sauti ndogo iliyolegea huku akizidi kumsogelea David akamkumbatia.

"Nini tena Dayana...!"

"Nisaidie mwenzio, ni mda sasa sijananlii.."

"Nanlii nini hebu sogea basi Zungu atatukuta hapa"

"Kasema anarudi baada ya dakika 10, Davii..zinatosha sana please nisaidie mwenzio nateseka" Alisema Dayana huku akianza kuushika shika mwili wa David. Ilikuwa ni rahisi kwa sababu pia wote walivaa nguo za ndani pekee

"Da...ya...naaa!!" David aliita kwa taabu kidogo lakini Dayana hakuacha, alidhamiria.



Upande wa pili Godfrey anashtuka ghafula kutoka usingizini, katikati ya usiku mnene huku akiliita jina la mpenzi wake aliyepotea miezi 13 iliyopita, Dayana.

"Dayana.. Dayana uko wapi mama" Alijisemea Godfrey huku akionekana kuhema kwa nguvu, alikuwa ameota ndoto mbaya sana kumhusu mpenzi wake huyo waliyependana sana.

Godfrey aliinuka pale kitandani akawa anaelekea sebuleni angalau apate chochote kutuliza akili.
Akiwa sebureni anamkuta mdogo wake Tesha akiwa bado hajalala.

"Tesha?" Godfrey aliita kwa mshangao, Tesha hakujibu.

"Mbona hujalala mpaka sasa?"

"Sina usingizi kabisa kaka, kila nikifikiria mambo yaliyotokea leo nakosa amani. Sijui David yuko wapi, yuko salama au laa!" Alijibu Tesha kisha akanywa glasi moja ya bia iliyokuwa mezani.

Godfrey alimtazama mdogo wake usoni kwa masikitiko makubwa akaona kabisa ni kweli suala la David lilikuwa likimtesa si kidogo. Alikumbuka hata yeye pia anapitia katika hali kama hiyo tangu siku alipompoteza Dayana katika mazingira ya ajabu sana.
Hakuna aliyejua kuwa usiku huu Dayana na David wako pamoja ndani ya bonde moja la ajabu katika kisiwa alichojichimbia Magnus baada ya kufukuzwa ISRA.

"Tesha.."

"Nambie bro"

"Unampenda?"

"Na..nani?"

"I mean David, do you love him?"
Aliuliza Godfrey huku akimtazama mdogo wake kwa macho ya udadisi

Je, nini kitafuata?

David atafanya nini mbele ya Dayana?
Vipi kuhusu Felix kule Marekani?
Ni ipi itakuwa adhabu ya Sasha asubuhi?
ITAENDELEA...
Simulizi hii inapatikana yote hadi episode ya 125 kwa Tsh 1500/= tu lipa kwa namba M-PESA ~ 0756862047
AIRTEL MONEY~ 0788967317
JINA-SAUL MWANAWIMA
UKILIPIA TUMA SCREENSHOT AU SMS YA MALIPO kwa namba hizo hizo WhatsApp au kawaida
 
KUTOKA ISRA KWENDA ISRA
Sehemu ya............23
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
"Tesha.."
"Nambie bro"
"Unampenda?"
"Na..nani?"
"I mean David, do you love him?"
Aliuliza Godfrey huku akimtazama mdogo wake kwa macho ya udadisi

SASA ENDELEA...
"You're not serious bro! Yaani mimi naongelea habari za kijana wa watu kutekwa wewe unaanza kuleta habari za mahusiano. Mimi kweli naweza ku-date na yule mwanaume kaka unanivunjia heshima jamani" Alisema Tesha.

"Naona kabisa unachokiongea na kilichopo moyoni mwako ni vitu viwili tofauti, Tesha kataa au kubali unampenda David, nililiona hilo tangu siku uliyoanza kutuma watu wamfuatilie. Sema unajua nini ni bora kumpenda David ambaye wewe unaona sio type yako kuliko kumpenda Felix mwanaume ambaye hakupendi kakukimbia na kwenda zake Marekani"

"Una mambo ya hovyo sana kaka, hivi wewe leo ni wa kuanza kunichagulia mwanaume wa ku-date naye, like serious? Mbona wewe sikuchagulii wanawake zake"

"Wewe ni mdogo wangu Tesha, ndugu tuliobaki tuko wawili tu mimi na wewe, lazima nikushauri nikiona unapita njia sio. Hata kama uta mind ila mimi sitoacha kukwambia Felix sio mwanaume. Mtu gani kwanza hataki kujulikana, hataki umuweke wazi mahusiano yenu, hataki mpige picha za pamoja, hataki kuongea na waandishi wa habari yani yupo yupo tu kama jambazi bana, asee!!"

"Hiyo ni lifestyle yake aliyochagua kwanini umuingilie, hapendi mambo ya social media. Mbona huongelei kuhusu pesa zake unazotumia kila siku"

"Lifestyle kitu gani mdogo wangu unapigwa hebu amka usingizini. haya mme-date miaka mingapi, siku ile nilikushauri umwambie angalau kama hataki mahusiano yenu yawe wazi basi akupeleke hata nyumbani kwao alikujibu nini?"
Aliuliza Godfrey, Tesha akawa kimya.

"Unajisahaurisha eti! Basi nakukumbusha alisema hana ndugu. Haya mtu gani huyo hana ndugu? Inaingia akilini kweli hiyo? Tesha mdogo wangu utakuja kudate na majini ohoo!" Alisema Godfrey kisha akachukua chupa ya bia aliyokuwa anatumia Tesha akaondoka nayo kurudi chumbani kwake.

"Sasa bia yangu unapeleka wapi?"

"Kalale bana, hii ni saa saba usiku. Kama wewe unamuwaza David hata mimi namuwaza Dayana" Alisema Godfrey huku akifunga mlango wa chumba chake.

"Huna lolote, unajishaua tu hapo" Tesha alijisemea mwenyewe kwa sauti ya chini. Akainuka kuelekea chumbani kwake kulala. Kabla hajafuata korido inayoelekea ulipo mlango wa chumba chake Tesha aliinua macho kutazama juu ukutani mahali ilipokuwepo picha ya Felix akasimama kwa sekunde kadhaa kuitazama.

"Eti hana ndugu, ila kaka ni kama kaongea ukweli flani hivi" Alisema Tesha kisha akaondoka zake, kwa kiasi maneno ya kaka yake yalimuingia.


Upande wa pili nyumbani kwa afisa upelelezi wa jeshi la polisi Brandina naye alikuwa bado hajalala. Huyu ni mmoja kati ya askari waliokuwa wakiifuatilia kwa siri kesi ya utekajinyara ulioanza miaka kadhaa iliyopita.

Tayari kuna jambo jipya Brandina alikuwa amelipata katika harakati zake za upelelezi. Ni kuhusu picha ya Felix aliyoiona nyumbani kwa mwadada mrembo na maarufu nchini Tanzania Tesha. Picha hii ndiyo iliyokuwa ikimnyima usingizi Brandina akawa macho mpaka mda huu.

Mara ghafula alisikia mlango wa nyumba yake unagongwa kwa nguvu. Brandina alitahamaki akatazama saa yake ya mkononi akaoni ni saa saba na nusu za usiku. Haraka alifungua droo ya meza kubwa iliyokuwa mbele yake kulikuwa na bastola akaichukua kisha akatoka hadi sebuleni akaelekea mlangoni.
Mlango ulikuwa bado unagongwa kwa nguvu sana.

"Nani?"Brandina akauliza

"Aah! We mwanamke, uniite mwenyewe alafu bado unauliza nani" Sauti ya kiume ilisikika kutoka nje ya nyumba.

"Mmh! Umewahi sana, sijategemea kama ungefika haraka kiasi hiki" alisema Brandina huku akifungua mlango. Akaingia mwanaume mmoja mnene na mrefu aliyevaa koti kubwa jeusi, mkononi alishika tochi yenye mwanga mkali pamoja na begi dogo jeusi.

"Kwa hiyo umekuja kwa mguu?"

"Ndiyo gari yangu haiwaki kabisa, nikaona nisichelewe simu yako ilikuwa ya muhimu sana. Haya niambie kuna nini usiku huu Brandina?" Alieleza mwanaume huyo na mwisho akauliza swali.

"Umekuja na ile CD ya CCTV kamera"

"Kama kawaida, nimeleta kila kitu ulichoniagiza Inspekta"

"Haya twende" Alisema Brandina, kisha akaongozana na yule mwanaume ambaye yeye pia ni afisa upelelezi wa jeshi la polisi anayeshirikiana na Brandina kuifuatilia kesi hii ya utekaji, anaitwa Inspekta Masoud.

Waliongozana na kuingia kwenye kile chumba alichokuwa Brandina awali.

"Woow! Uko Smart sana Inspekta Brandina, kumbe hadi nyumbani unaofisi pia" Alisema Inspekta Masoud huku akitazama maadhari ya chumba kile.

"Unafikiri kuitwa mfanyakazi bora huwa inakuja kirahisi rahisi tu, kazi inakuwa imefanyika kweli, naomba hiyo CD"

"Eeh! Hata mimi naona hakuna kulala, CD hii hapa"

Brandina aliipokea CD Kutoka kwa Masoud kisha akaiweka kwenye kompyuta yake ndogo, akaicheza video iliyokuwa ndani ya CD hiyo.

Ilikuwa ni video iliyerekodiwa na kamera za CCTV nje ya Supermarket moja kubwa jijini Dar es salaam, ilikuwa ni usiku wa tarehe 21/07/2019 siku ya Jumapili, siku ambayo wanaume watatu walevi walitekwa na watu wasiojulikana nje ya Supermarket hiyo.
Kama kawaida watekaji walikuwa ni walewale wanaovaa helmet zenye vioo vya rangi nyekundu. Lakini kwa bahati nzuri mmoja kati ya wale watekaji alivua helmet yake kabla ya kuingia ndani ya gari bila kujua mahali hapo palikuwa na kamera za CCTV, zikamnasa.

Ilipofika wakati ule mtu huyo anavua helmet Brandina akasimamisha video hiyo.

"Unamuona huyu jamaa" Alisema Brandina

"Eeh! Nilishamuona kitambo sana, huyu tumemfuatilia tangu mwaka 2019 mpaka leo hatujajua ni nani, katoka wapi anafanya nini.." Alijibu Inspekta Masoud.

"Sasa mimi leo nimempata huyu mtu"

"Acha utani wako Brandina, unajua hili jambo sio la kutia masihara hata kidogo"

"Amini hivyo Inspekta Masoud, huyu mtu anaitwa Felix ni mpenzi wa Tesha huyu dada maarufu mwanamitindo"

"Tesha? Tesha huyu huyu super star?"

"Ndiyo"

"Acha hizo bwana, enhe! hebu nielekeze vizuri imekuwaje"

Brandina alieleza kila kitu tangu mwanzo alipopigiwa simu na Godfrey wakati wa tukio lingine la utekaji pale mgahawani kisha wakaenda hadi nyumbani kwa Tesha kuongea naye na baadae ndipo alipoiona picha ya Felix ikiwa ukutani.

"Kwa maelezo yao wanadai kwa sasa Felix yupo nchini Marekani, sina kingine nachokijua" Brandina Alimaliza kutoa maelezo.

" Sawa, kazi nzuri, hongera sana Brandina hii ni hatua moja kubwa mno. So tunafanyaje, huyu jamaa lazima tumpate"

"Kabisa, na sijui kwa nini Tesha hajaweka wazi mahusiano yao, nimekagua karibu picha zake zote kwenye mitandao ya kijamii Instagram Twitter Facebook kote sijamuona Felix"

"Kama anafanya hizi kazi hawezi kujiweka wazi mtandaoni" Alieleza Inspekta Masoud.

"Sahihi kabisa"

"Kwa hiyo tumvizie mpaka atakaporudi au tunafanyaje"

"Hatuna mda wa kupoteza Inspekta, huyu tunaanza kumsaka kimya kimya huko huko Marekani, tutafuatilia tangu alipotoka hapa Tanzania, alitumia ndege gani alifikia wapi akaenda wapi. Kila kitu lazima tukijue, inabidi tuombe msaada kitengo cha UJASUSI nchini, wao pia watawasiliana na shirika la Ujasusi nchini Marekani CIA, wote tuungane kuhakikisha tunampata Felix" Brandina alitoa wazo.

"Yes! Uko sahihi"

Naam, sasa nguvu kubwa inakwenda kutumika kumtia nguvuni Felix mtoto wa Magnus kutoka ISRA.
Je, watafanikiwa?
Vipi kuhusu hukumu ya Sasha kule ISRA?
Nini kinaendelea kati ya David na Dayana kule bondeni?

ITAENDELEA.....

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

.Simulizi hii inapatikana yote hadi episode ya 125 kwa Tsh 1500/= tu lipa kwa namba M-PESA ~ 0756862047
AIRTEL MONEY~ 0788967317
JINA-SAUL MWANAWIMA
UKILIPIA TUMA SCREENSHOT AU SMS YA MALIPO kwa namba hizo hizo WhatsApp au kawaida
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom