Matukio ya kutengenezwa ya kujiteka

Matukio ya kutengenezwa ya kujiteka

Intelejensia yenu haijui kwa mjomba? Si mkawachukue muwadhalilishe hadharani?

Mapanga na mifuko ya sandarusi baharini ndiye mjomba?

Au unazungumzia mjomba magu?
 
Na kama matukio haya yanaandaliwa na wasikamatwe wanao yaandaaa ni ufala
 
.Nimepata Taarifa ya mshangao mkubwa jioni ya leo punde tu nilivyowasili nyumbani kwangu Mafinga jioni ya leo baada ya kuona kwenye mitandao ya kijamii na kusikiliza kwenye vyombo vya Habari sasa nakaa natafakari ni aina gani ya vijana tuliokuwa nao

Mapema leo asubuhi muda wa saa 12:00 asubuhi nilipanda gari aina ya NEW FORCE yenye namba ya usajili ya T 226 DJQ nakukaa siti yenye namba G3 ambapo jirani wangu aliyekuwa amejivika shuka la kimasai alikuwa amekaa siti namba G4 ambaye alionekana kuwa na hofu wakati wote na kutumia simu yake kwa kutuma jumbe tofauti kila mara

Wakati tupo njiani kijana yule nilitaka kujenga urafiki walau Tupige hata stori mbili tatu lakini ilishindikana ila tulipofika Morogoro ndipo alianza kunisemesha kwa kuhitaji nimsaidie kununua maji kwa kuwa nilikuwa upande wa dirishani nikafanya hivyo nikiwa na dhamira ya kumsaidia ndipo tulipoanza kupiga stori mbili tatu

Lakini nilisikia tukiwa njiani anawasiliana na mtu mmoja mwenye sauti ya kike na kumtaka aandae mazingira ya hapo wanapokutani.

Wakati wote namuaangalia kijana huyu ambaye awali nilikuwa simfahamu vizuri nilimbaini kwa sura nikamjua na hakutaka kuongea na mimi zaidii ya kujifichaficha

Sasa nimefika nyumbani Naanda kusikiliza radio nasikia kuna kijana wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kutekwa nilipoingia Facebook ndo nikaona picha yake nikamwambia mke wangu ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Kuwa kijana huyu nimependa naye basi moja kutoka Dar es Salaam na mke wangu hakuamini

Nipende kuambia ndugu watanzania wenzangu kijana huyu HAJATEKWA WALA NINI MAANA NILIKUWA NAYE MWANZO WA SAFARI YOTE NA KAMA KATEKWA LABDA NI KWENYE NDOTO

HIVYO TAARIFA ZOTE ZA UTEKWAJI WAKE NI ZA KUPUUZWA MAANA ANATAKA KUTAFUTA UMAARUFU WA AJABU KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO YA KIJAMII

*JONATHANA KWEPE*
Peleka huko propaganda zako za kishamba. Mnataka kuitumbukiza Nchi yetu kwenye matatizo kwa sababu ya njaa zenu za madaraka. Au wewe ndie mtekaji mwenyewe? Acheni kutufanya watanzania hatuna akili kama mlivyo nyinyi! Zero brain kabisa!
 
Lolote lawezekana aisee.

Na kusema ukweli Magufuli ana maadui kila kona.

Hata ndani ya CCM wapo. CHADEMA ndo wamejaa hadi pomoni.

Hivyo sitashangaa kabisa kama kuna mipango ya hujuma dhidi yake na wahusika wakawa ni kutoka CHADEMA na CCM wakifanya kazi kwa ushirikiano.
Hapana Mkuu, nakataa nakataa...awamu hii vitengo wamejazana kila kona , hakuna kitu utafanya serikali isijue....hakuna.

Yani kama kuna mbinu chafu zozote watajua tu...refer ishu ya ndege kukamatwa Canada
 
Hv kwa hali ilivyo sasa no ajira uchumi mbovu Maisha magumu watu wafukuzwa kazi watu wanauawa hovyo maiti zinaokotwa watu wanapigwa risasi bila hatia hv mtu unaanzaje kumshabikia magufuri au mtoa uzi unaishi magogoni..
Acheni kujiteka na kutengeneza scenario za kufikirika hapa na chapeni kazi kama Watanzania wenzenu. Wewe umeona au umeokota maiti ngapi mkuu au unaimba tu!
 
Human memory sucks. Hivyo hayo maneno unadhani yalisemwa lakini huna uhakika. Kwasababu hoja zako zimejengwa kwa maneno ya kudhani na si ukweli, hoja zote ulizoleta haziwezi kukubalika.

Swali langu hukujibu mkuu.

Isitoshe, sheria ni msumeno. Kumbe huyo Jaji ana uwezo wa kusamehe tu wavunja sheria kama anavyosamehe CCM kwa makosa kibao wanayofanya kisheria?
You are absolutely right, HUMAN MEMORY SUCKS.

Lakini hii clip ipo YouTube. Usitake kubishana na mimi. Ni kiasi cha kuitafuta hotuba ya Mbowe na Mdee jioni ya tarehe 16 February, 2018 ili uone nimepotosha kiasi gani.

CDM wamefanya civil & criminal disobedience kama mkakati wao wa kufanya siasa za kiharakati kwa muda mrefu sana.

I will admit, mbinu zao ndizo zilizoipa CDM umaarufu mkubwa mpaka kukaribia kuing'oa CCM.

Lakini hizi mbinu zao mara nying zilivuka mipaka. Kuna vyama vingi vya kisiasa duniani vilivyofungiwa kwa makosa madogo kuliko yao.

Awamu za nyuma za serikali ya TZ hazikutaka kufanya hivyo kwa sababu ingeleta picha mbaya duniani kuwa chama kikuu cha upinzani TZ kufungiwa.

Pengine utakumbuka katika awamu ya 4. CDM waliivuruga serikali bila kukaripiwa mpaka wakamuita Rais Kikwete DHAIFU.

Unaikumbuka hii?
 
Naanza kupatwa na mashaka kuwa huenda kuna watu wanaunda matukio flani flani ili kutimiza azma zao za kisiasa dhidi ya rais Magufuli.

Mtu anaenda kujificha kwa mjomba wake huko halafu wenzake wanasema kapotea au katekwa halafu lawama anaanza kupewa rais Magufuli.

Haya matukio ya kupotea potea watu inabidi tuyaangalie kwa jicho la tatu na si kumeza kila kitu tukisikiacho.

Msidanganyike kirahisi. Stukeni.
Ile trilioni 300 ilishalipwa???
 
Serikali isifanyie mzaha hawa watu wanaotafuta kiki kwa kuichafua serikali. Lazima uchunguzi wa ndani ufanyike kujua huyu anadai alitekwa kama maelezo yake ni ya kweli
Kwa hiyo na Roma alijiteka? Na wale mashehe walijiteka? Peleka huko porojo zako za kishamba! Msidhani watanzania ni wajinga kama nyinyi mlivyo!
 
Hakuna Shaka yoyote kuwa wanaweza kuhusika Katika Hilo.
 
Wengine walikuwa wanahusika miaka hiyo ila walikuwa wanazuga kwa kulaani yanayotokea ila awamu hii ni tofauti, baba mwenye nyumba hajawahi kulaani au kukemea tukio lolote la mauaji au upoteaji wa watu, ukiondoa lile la Kibiti ambapo makada wa chama ndo walikuwa wanauawa, naamini nimesaidia katika dodoso lako!
 
Naanza kupatwa na mashaka kuwa huenda kuna watu wanaunda matukio flani flani ili kutimiza azma zao za kisiasa dhidi ya rais Magufuli.

Mtu anaenda kujificha kwa mjomba wake huko halafu wenzake wanasema kapotea au katekwa halafu lawama anaanza kupewa rais Magufuli.

Haya matukio ya kupotea potea watu inabidi tuyaangalie kwa jicho la tatu na si kumeza kila kitu tukisikiacho.

Msidanganyike kirahisi. Stukeni.

HATA MIMI NAHISI HIVYO HIVYO, HAYA YOTE NI YA KUPIKA ILI SERIKALI IJIONDOE NA LAWAMA

IRUHUSU WACHUNGUZI WA KIMATAIFA KWA HAYO MATUKIO YOTE ILI TUKATE MZIZI WA FITINA TUENDELEE KUJENGA NCHI YA VIWANDA SIO NCHI YA HISIA HASI KILA SIKU
 
Kuna tetesi kuwa Nondo hakupotea bali amejipoteza mwenyewe maksudi.

Sijui ukweli hapa upo wapi kwa sababu hapo nyuma watu walipotea kikweli.

Ninachotaka kukielezea hapa chini ni dhana ya kuwa watu wanafanya maigizo au MIKAKATI ili ulimwengu uione serikali ya Magufuli kwa mtizamo m-baya.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Kinachofuatia ni dhana ambayo inawezekana haina ukweli wowote. Work with me here:

FEBRUARY 16, 2018
Katika hitimisho la kampeni ya ile chaguzi ndogo ya Kinondoni:

HALIMA MDEE alisema (paraphrase):
Tufanye vurugu kama Libya, Syria au Iraq.
This is significant, nifuatilie.

FREEMAN MBOWE alisema (paraphrase)
Tunahitaji kuikabili serikali mpaka wauwawe watu 100 au 200.
This is also significant.

ANALYSIS
- Kama utakumbuka katika nchi alizozitaja MDEE, watu walikufa kwa mikono ya serikali.

Wakati "mataifa makubwa" walipotaka kuing'oa serikali walisema: He is out of control and HE KILLS HIS OWN PEOPLE.

Huu usemi kuwa "ANAUA WATU WAKE" ndiyo uliokua unasemwa kabla ya uvamizi na kupinduliwa kwa serikali husika na mataifa makubwa.

Alichokisema MBOWE haikua kuteleza kwa ulimi. Nadhani huu ndio mkakati mzima wa upinzani, hasa CDM, kuleta vurugu na kuwashambulia polisi mpaka polisi wawaue watu wengi.

Nadhani "handlers" wao waliwaambia kuwa kama watu 100 au 200 wakiuawa na polisi basi itayafanya mataifa makubwa watoe tamko kuwa:

Magufuli hafai, ANAWAUA WATU WAKE.
He is out of control, he is KILLING HIS OWN PEOPLE.

DHAMIRA
Kwa shinikizo hili la kuwa Magufuli ni kiongozi mbaya na sasa ANAUA RAIA WAKE MWENYEWE itakuwa rahisi kwa Security Council ya Umoja wa mataifa kuingilia kati.

Sote tunajua, kama UN Security Council italeta majeshi ya kuuingilia kati utawala wa Magufuli, ni nani hasa atakaeletwa.

NONDO
Je ni kweli kuwa, kama huu utekaji wa NONDO ni fekero, basi huu ni muendelezo tu wa haka kamchezo kachafu kanakochezwa na upinzani?
Mbona unajihami, mmeshamteka mtoto wa watu, cjuui kama yupo hai
 
Haya uliyoyaandika ni dhahiri sasa hawa wenzetu wanazidi kujipambanua kuwa na muelekeo ovu dhidi yaTaifa hili.

Nami pia nikuunge mkono kwa kukumbushia yale ambayo tulishayaandika huko nyuma

Kupotosha Umma kwa kuwatia hofu wananchi waichukie Serikali halali

Wanachokitengeneza CHADEMA ni siasa za "Appeal to Fear"

Kutafuta huruma za Kisiasa kwa kuichafua Nchi

Pinga pinga na timu yao iliyoshindwa mitandaoni
 
Lolote lawezekana aisee.

Na kusema ukweli Magufuli ana maadui kila kona.

Hata ndani ya CCM wapo. CHADEMA ndo wamejaa hadi pomoni.

Hivyo sitashangaa kabisa kama kuna mipango ya hujuma dhidi yake na wahusika wakawa ni kutoka CHADEMA na CCM wakifanya kazi kwa ushirikiano.
Muulizeni jamaa yenu sababu yakumiliki Maadui wengi badala ya marafiki
 
Nieleweshe kitu hapa:

Mwanzo umesema ulitamani kupiga nae story, ukashindwa ila baada ya kukuomba umnunulie maji NDIPO MKAANZA KUPIGA STORY MBILI TATU. (That means alivua shuka lake mkaanza kupiga hizo story mbili tatu)

Baadae tena ukasema huyo kijana hakutaka kuongea na wewe zaidi ya kujifichaficha.

Hilo shuka la kimasai alikuw amejifunika uso mzima au shingoni tu ila uso upo wazi...??

Alifanya nn kilichokuonesha kwamba ana hofu wakati wote...?? ( ieleweke kwamba kutuma msg kwa simu sio kigezo cha kuwa na hofu)

TCRA na makampuni ya simu pia yapo, yanaweza kuchunguza jumbe zake.

Unadhani kama kuna watu walipanga kumtumia huyo dogo kutimiza dhamira hyo, WALISHINDWA KUTUMIA GARI BINAFSI MPK AJICHANGANYE KWENYE NEW FORCE, ilhali wakijua kwamba kuna siku picha yake itaonekana kwny media..??

What a coincidence uwe wewe, mwenye access na JF, ukae nae siti moja, utake urafiki na mtu usiyemjua, ugundue ana hofu etc.
 
Naanza kupatwa na mashaka kuwa huenda kuna watu wanaunda matukio flani flani ili kutimiza azma zao za kisiasa dhidi ya rais Magufuli.

Mtu anaenda kujificha kwa mjomba wake huko halafu wenzake wanasema kapotea au katekwa halafu lawama anaanza kupewa rais Magufuli.

Haya matukio ya kupotea potea watu inabidi tuyaangalie kwa jicho la tatu na si kumeza kila kitu tukisikiacho.

Msidanganyike kirahisi. Stukeni.
Kweli Nyani Ngabu na akili yako na exposure yako ndio unaandika hayo?

Watu wanakufa na kupotea n.a. kuumia. Wewe unafanya utani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom