Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

singanojr

JF-Expert Member
Sep 24, 2020
1,525
8,542
IBILISI RUDISHA FAHAMU ZETU(MIMI NA MKE WANGU).


BY ISSAI SINGANO .
(Singano jr).

DIBAJI
Saa saba mchana Frida alionekana akiingiza gari ndani ya hospitali na taasisi ya kitafiti ya Neuroscience inayopatikana Kibaha , kilomita kadhaa kutoka ilipo hospitali ya Tumbi.

Ilikuwa ni hospitali kubwa mno na ya kisasa yenye jengo moja lililoenda hewani kwa ghorofa kumi kumi na nane hivi na kufanya kuwa jengo refu zaidi ndani ya mkoa wote wa Pwani.

Hospitali hio ilijengwa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia shirika la taasisi isiokuwa ya kiserikali ifahamikayo kama Haliz Neuroscience Foundation(HNF).

Taasisi ya Haliz ilisifika dunia nzima kwa kujikita zaidi katika kuutafiti ubongo na maswala ya neva kwa ujumla wake, sera ya taasisi hio ilikuwa ni kuwezesha mataifa mengi kujifunza namna mfumo wa ubongo na neva unavyofanya kazi na hii imechangia sana kufungua matawi yake mengi karibia nchi nyingi duniani.

Mashirika ya Afya ya umoja wa kimataifa yalikuwa yakiunga mkono kazi kubwa ambayo ilikuwa ikifanywa na taasisi hii kubwa ya kimarekanni isiokuwa ya faida(Non-profit organisation).

Katika miaka ya hivi karibuni maendeleo ya sayansi ya neva na ubongo yalikuwa yamepiga hatua kubwa sana , wale wagonjwa ambao walikuwa wamepoteza kumbukumbu ilikuwa rahisi kurejeshewa kumbukummbu zao ndani ya muda mfupi tu chini ya taasisi hii ya Haliz.

Haikuwa wagonjwa waliopoteza kumbukummbu tu , watu wengi ambao walionekana kusahau mambo muhimu katika maisha yao , iwe ni kubukumbu za utotini au za ukubwani taasisi ya Haliz ilikuwa na teknolojia ya tiba ya kurahisisha hayo yote.

Licha ya taasisi hio kufanikiwa lakini bado utafiti wa kuujua ubongo wa binadamu ulikuwa ukiendelea zaidi , kwani wanasayansi wanaamini ubongo uwezo wake ni mkubwa kuliko ile ambavyo inadhaniwa , hivyo wanaamini kuuwezesha ubongo kufikia uwezo wake kamili kimatumizi italeta maendeleo makubwa.

Frida alitembea kwa kujiamini kabisa ndani ya hospitali hio huku akipokelewa na harufu ya taasisi hio yenye kuzoeleka katika pua zake, kwa namna baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hio walivyokuwa wakimsalimia kwa kutingisha vichwa ilionekana alikuwa ni mfanyakazi mwenye cheo.

Aliishia kutoa tabasamu huku akitingisha kichwa kwa kuonyesha tabasamu kwa baadhi ya watu aliopishana nao ndani na ndani ya dakika kadhaa aliweza kuzifikia lift na kuingia ndani, lakini kabla hata ya mlango wa lift haujajifunga mwanaume mzungu wa makamo alievalia koti la kimaabara aliweza kuzuia lift hio na kuingia ndani.

Alikuwa ni mtanashati kweli aliependezeshwa na miwani ya macho , huku akiwa amepambwa na tabasamu.
“Well!. Fancy meeting you here, Frida”Aliongea yule mzungu na kumfanya Frida kutoa tabasamu.

“Una ajenda gani kukimbilia lift Blake, huu si muda wako wa kufanya Demostrations na wanafunzi?”Aliuliza Frida na kumfana Blake kutoa kicheko kama anakohoa.

“Ndio nimemaliza, kulikuwa na mabadilishano na Dr John , Vipi wewe ndio umekuja kutubariki na utaalamu wako?,nilidhani upo likizo?”

“Nipo likizo ndio , lakini haimaanishi sipaswi kufika hapa , nina biashara katika floor ya kumi na saba”

“Wow!, Wow! , Floor ya wabobevu, sina neno la kuongezea, See you Frida”Aliongea Dr Blake na ni muda uleule Lift ilisimama katika floor ya kumi na bwana huyo mzungu alitoka akimuacha Frida kuendelea na safari yake.

Frida aliishia kutoa tabasamu tu huku akiangalia namna ambavyo Blake anapotelea kwenye macho yake wakati lift ikijifunga.
Haikuwa kama ambavyo amesema Frida kwani mara baada ya lift kufika katika foor ya kumi na saba alitoka katika lift na kuingia katika floor hio ambayo ilikuwa na utulivu wa hali ya juu , ilikuwa ni ubaridi tu na harufu ya kuvutia , huku rangi ya taa zisizokuwa na mwanga mkali zikipendezesha eneo hilo.

Frida hakuingia ndani ya Foor hio bali alizunguka upande wa kushoto kwake na kuanza kupandisha ngazi kuelekea juu na ndani ya dakika chache tu aliweza kutokezea juu kabisa ya jengo hilo.

Licha ya kwamba alionekana kutembea kwa haraka, lakini kwa namna ambavyo alikuwa na spidi hakuonyesha hata kuchoka, alionekana kama aina ya wanawake ambao walikuwa na mazoezi makali.

Baada ya kutoka katika paa kabisa ya jengo hilo refu na kumfanya kuona mazingira ya mji wa Kibaha na baadhi ya maeneo ya Dar es salaam na Bagamoyo alivuta pumzi na kisha aliendelea kupiga hatua kusogea mbele.

Hali ya hewa haikuwa ya jua kali ,ilikuwa ni kama vile mvua ingenyesha muda wowote.

Mbele yake Frida alikuwa amesimama mwanaume alievalia suti ya rangi ya bluu akiangalia upande wa maeneo ya Dar es salaam kwa umakini mkubwa kana kwamba kuna kitu alichokuwa akitafuta.

Alikuwa ni mzungu kwa muonekao wa nywele tu na kadri Frida ambavyo alikuwa akitembea hatua zake zilionyesha hali ya kuwa dhaifu kiasi.

Kama ilivyo mwanaume yule alivyosimama ndio namna ambavyo Frida alienda kusimama katika ukingo wa jengo hilo na kuendela kuangalia upande wa mbele yake, ilikuwa ni kama vile anamwigizia yule mtu , na upande wa yule mtu hakugeuka kabisa ni kama alijua nani amefika hapo na kusimama pembeni yake.

“Any progress on KF-Target?”Aliongea yule mzungu kwa sauti nzito.

“We are almost there, I’ve initiated a plan to bring him closer to me, his curiosity will ensure our swift entry into the next phase”Aliongea akimaanisha kwamba anakaribia kumaliza , na ameanzisha mpango wa kumuweka karibu , anasema shauku yake itawafanya waingie hatua inayofuata kwa haraka”

“Elezea”Aliongea.

“Nimemfanya anifanyie Delivery ya Viungo vya akili kutoka Binamu , uhakika ni kwamba atauliza maswali juu ya malipo makubwa yanayolipwa kwa ajili ya chungu kimoja kama njia ya usafirishaji, kwa kile nilichoona amevutiwa”

“A risky move”

“Calculated Risky Sir”Aliongea Frida kwa kingereza na jibu lake lilimridhisha.

“Vipi kuhusu wale wengine , namaanisha wanaoangalia kutoka mafichoni?”

“We are keeping eye on them , once we have what we need, they ‘ll be nothing more than loose ends”

“Endelea na kazi kwa umakini , hatuwezi kuruhusu kosa lolote”

“Umeeleweka”

“Sinagogi wanataka hii misheni kumalizika kwa haraka , siku zijazo utashughulikia na zaidi ya mtu mmoja katika tafiti yako , mategemeo makubwa yamewekwa juu ya hii sayansi mpya Frida ,natumaini kila kitu kitaenda sawa,Hatuwezi kuruhusu washindani wetu kupiga hatua kabla yetu”

“Ili mradi malengo yanakuwa wazi , kila kitu kitaenda sawa , natumaini utakuwa vizuri kwenye kuwatoa wasiwasi”
“Kama ni hivyo tutaonana tena katika hatua inayofuata kujua maendeleo”Aliongea yule mwanaume na ilitokea kitu kama upepo tu kwani alipotea palepale na wala hali ile isimuogofye Frida ikionyesha ni jambo ambalo amezoea.


SEHEMU YA 01..
Ni saa moja dakika saba katika website maarufu ya JamiiForum linaonekana tangazo katika jukwaa la Connect , tangazo ambalo limetolewa na ID yenye jina la Ngwena.

Ajira: Boyfriend anatafutwa.

“Husika na kichwa cha tangazo, mimi ni msichana wa miaka ishirini na nne natafuta mwanaume ambae ataigiza kuwa boyfriend wangu kwa mkataba wa mwaka mmoja, vigezo ninavyovitaka ni mwanaume wa miaka 20 mpaka 30 awe ni mwenye kujiamini, dini yoyote, Mwonekano wowote lakini ukiwa mtanashati ni kigezo cha ziada, Elimu angalau ya chuo cha kati kuendelea, mshahara kwa mwezi si chini ya laki tano na maongezi yapo, kuhusu mimi zaidi utanifahamu baada ya kukidhi vigezo, Kama umevutiwa na kazi hii njoo PM jielezee kwa ufupi na weka mawasiliano yako”

Jukwaa la Connect mara nyingi hutumika kuunganisha watu ambao wanatafuta kuingia katika mahusiano ya aina mbali mbali aidha yale ya urafiki wa kawaida au yale ya kupelekea uchumba hadi ndoa, hivyo mwana jukwaaa mwenye ID ya Ngwena alitumia haki yake kuweka tangazo la namna hio , ijapokuwa tangazo limekaa kibiashara au kiajira lakini kwa namna moja ama nyingine lilikuwa likihusisha mahusiano.

********

Sifa yake kubwa ni mkimya lakini sio mpole, ni mtu mwenye kufikiria kila neno analolisikia na kulisoma mahali kwa kutumia akili nyingi, Hamza anaamini kuna zaidi ya maana katika kila neno analotamka binadamu na hii inampelekea kuwa kati ya watu ‘Overthinker’ sana , kwa mfano Hamza unaweza kumtania ila ule utani yeye akauchukulia siriasi , ijapokuwa hakukasirika lakini utani ataugeuza na kuanza kujitafakari kwa nini ametaniwa hivi na vile.

Hakuwa mchangiaji wa mada , lakini alipenda kusikiliza michango na maoni ya wengine , hakuwa mpenzi sana wa kuanzisha mada kwenye mitandao ya kijamii , lakini alipenda sana kusoma maoni ya wengine na mada za wengine , huku akiamini kwa kupitia maoni yao angeweza kufahamu tabia za watu mbalimbali kwa kuchanganua zaidi ya maana kwa kila maoni ya mtu mmoja mmoja , hayo ndio maisha ya Hamza na alipenda sana mtandao wa Twitter na JamiiForum.

Hakupenda kujichanganya na watu wengine, lakini alipenda sana mitandao ya kijamii kwa kiwango kikubwa sana huku akijiaminisha kwamba mitandao ya kijamii ndio sehemu ambayo watu wanaweza kuwakilisha uhalisia wao kwa urahisi kupitia maandishi kwani hawakuwa wakionekana kwani wengi wao walitumia utambubulisho feki,Kwa tabia yake hio unaweza kumuita Jasusi wa mtandaoni.

Licha ya hayo yote lakini Hamza ni moja wapo ya vijana ambao unaweza kusema ni wenye moto unaowaka ndani , moto wa upambanaji, moto wa kutodharau fursa iliopo mbele yake, ni kwamba tu kila fursa aliokutana nayo haikuwa kubwa ya kumtajirisha lakini ilimfanya kusongesha maisha yake.

Sasa Hamza ndio moja wapo ya watu walioweza kuona tangazo la ajira ya kuigiza kama boyfriend, ilikuwa ni majira ya usiku wa kwenda saa mbili na baada ya kusoma Tangazo hilo alivutiwa sana , akiamini lazima kutakuwa na Maoni ya kuchekesha na ndio alichokutana nacho.
Ni kweli Tangazo lilikuwa likijipambanua kwamba ‘Boyfried’ wa maigizo anahitajika kama ajira isio rasmi, lakini tangazo lilikaa sana kitapeli kwa watu wengi , nani anaweza kuamini mwanamke wa kitanzania kuajiri mwanaume kwa kumlipa malipo ya laki tano kwa mwezi kwa kuigiza kuwa boyfriend, ni jambo ambalo sio kawaida kabisa , hivyo maoni mengi ya wachangiaji ilikuwa ni matusi na dhihaka huku ID(jina la utambulisho) feki ya jina la Mnyoo ukiongoza kwa dhihaka lakini upande wa mtoa mada hakujibu chochote ni kama alitoa tangazo na kisha akapotea,watumiaji wa mtandao huo wanayo kauli ya kusema Uzi unatembea kwa kasi mno na hiko ndio kilichokuwa kikiendelea ,wachangiaji wengi wakiwa ni wale wenye ID za kiume.

Hamza aliendelea kusoma maoni huku mengine yakimchekesha sana, hakuwa na mpango wa kutoa maoni lakini watu walivyocharuka ilimfurahisha sana , baada ya kusoma karibia maoni yote alirudia upya kusoma tangazo lenyewe na kuanza kulitafakari kama ilivyokuwa tabia yake ya kutafuta zaidi ya maana kwa kila mtu anachoongea au anachokiandika kwenye mitandao, ndio tabia yake ambayo kwa umakini aliokuwa akitumia kuchambua mawazo na maandishi ya watu ungedhania analipwa alichokuwa akitafuta ni kujua kwanini mtoa mada alikuwa akidhihakiwa kwa kiasi kikubwa.

Hamza katika siku zote alizokutana na matangazo ya ndoa na kutafuta wenza hili kidogo lilikuwa na upekee , aligundua kulikuwa na zaidi ya maana , zilikuwa ni hisia ambazo hata yeye mwenyewe alishindwa kuzielewa , lakini ile tabia ya kufatilia maoni ya watu na mabandiko ilimwongezea utashi(Instinct) wa kuelewa hisia za watu kwa haraka zaidi kupitia kile wanachokiandika na wanachokitolea maoni na ndio alichokutana nacho , wakati akiendelea kusoma kwa kurudia rudia hilo Tangazo ujumbe wa meseji kwenye simu yake ya Tecno Spark 5 uliiingia , aliufungua haraka sana na kuona ni muamala wa pesa.

“Huyu Mzee leo kanikumbuka” Aliongea mwenyewe bila furaha huku akiangalia ile meseji, sababu moja ya kutokufurahia ule mwamala ni moja tu , hela iliotumwa haikuwa ikimtosha kwa matumizi kabisa achana na madeni ambayo alikuwa akidaiwa chuoni.
Kila ikifikia hio tarehe ndio siku ambayo alikuwa akipokea muamala kwa mwanaume anaemfahamu kwa jina la Mzee.

Miamala ambayo Mzee alikuwa akituma ni kwa kiasi anachojisikia yeye mwenyewe atume shilingi ngapi , mbaya zaidi ni kwamba Hamza hakuwa na uwezo wa kumpigia simu Mzee na kumwambia amwongezee kidogo.

Tusichokijua kuhusu Hamza ni kwamba alikuwa ni Yatima na kuna stori kubwa ya maisha yake iliomtokea mkoani Rukwa huko Sumbawanga ambayo ndio ilimfanya kuwa mtoto Yatima lakini pia kumkutanisha na mtu aliefahamika kwa jina la Mzee.
Maisha yake yote tokea kupatwa na janga la ajali huko Sumbawanga iliopelekea kupoteza ndugu zake na mzazi wake mtu ambaye alimsaidia mpaka kufikia katika umri huo ni huyo Mzee.

Mbaya zaidi kuhusu Mzee ni kwamba alimuona mara moja tu na ilikuwa ni usiku wa mvua kali na wakati huo alikuwa na miaka tisa akiwa darasa la nne na mpaka wakati huu akiwa na miaka ishirini na tisa hakuwahi kumuona tena, miaka ya mwanzoni aliwasiliana na mzee kwa barua , lakini mara baada ya ujio wa simu aliwasiliana nae kwa jumbe za meseji tu na siku zote Mzee angemtumia Hamza ujumbe kwa ‘Private number’(Namba ambayo huwezi kurudisha jibu) tena ikiwa ni nyakati za usiku pekee.

Kwa maneno marahisi ni kwamba Hamza alisaidiwa kimaisha na Mzee ambaye hakuwa akimfahamu kwa sura yake halisi na ndio maisha yake yalivyokuwa mpaka kufikia umri huo, Mzee alikuwa akimsaidia vitu vingi lakini hakuwahi kujionyesha kwake.
Hamza baada ya kupatwa na hasira kwa kiasi kile kidogo cha pesa alichopatiwa na Mzee alijikuta akirusha pembeni simu yake kwenye godoro ndani ya chumba chake alichopanga katika eneo la Gongo la mboto jijini Dar es salam.

Chumba chake hakikuwa na vitu vingi kabisa , kilikuwa na godoro dogo kama yale ya wanafunzi, mtungi wa gesi na baadhi ya vyombo vichache pamoja na chandarua. Alikuwa pia na mabegi mawili , moja kubwa kidogo la wastani na lingine ni la saizi ya kati ambalo hutumia kuwekea nguo zake, maisha yake yalikuwa ya chini sana huenda kuliko mwanafunzi yoyote anaesoma ndani ya chuo cha FEMU(Future Enterprise and Monetary University).

Baada ya kujilaza kwenye godoro lake alijikuta akipotelea usingizini na alikuja kushituka ni siku nyingine kabisa ya jumatatu , alijiandaa haraka haraka kwa ajili ya kwenda Chuo. Baada ya kutumia zaidi ya lisaa limoja na nusu kujiandaa kutokana na kusubiria zamu yake ya kuingia bafuni kufikia , hatimae aliweza kusogelea vituo vya daladala kwa ajili ya kupanda ambazo zingemwezesha kufika chuoni.

Njia ilikuwa na foleni na kwa bahati nzuri aliweza kupata siti ya kukaa , hivyo alitoa simu yake mfukoni na kuendelea kuperuzi peruzi mtandaoni huku Earphone zikiwa masikioni. Hamza ni aina ya watu ambao hawakupenda kabisa kusikiliza maongezi ya abiria kwenye daladala na miezi hio habari za uchaguzi zilikuwa zikijadiliwa sana kwenye magari kwani ilikuwa ndio mwaka wa uchaguzi na ilikuwa kama miezi mitatu tu hivi siku ya wananchi wa taifa la Tanzania kupiga kura.

Lakini kwa upande wake yeye hakuwa hata na mpango wa kupiga kura, kwanza hakuwa na chama na wagombea wote hakuna ambaye alikuwa akimvutia japo mmoja wapo ya wagombea aliweza kusikia akijinadi kwamba atakwenda kupambana na rushwa pamoja na Madawa ya kulevya nchini, kauli hio kidogo ilikuwa ni sera iliojitosheleza kulingana na hali ya taifa kwa ujumla lakini Hamza kwa mtazamo wake hakuwa na uhakika kama sera hio ingeweza kutekelezeka.

Katika kipindi cha miaka mitano iliopita madawa ya kulevya yalikuwa yameathiri sana vijana wa kitanzania , haikueleweka nini kinaendelea nchini kutokana na kuongezeka kwa wimbi la wagonjwa ambao wana uraibu wa madawa ya kulevya katika hospitali zenye vituo maalumu vya kusaidia wagonjwa hao.

Takwimu za kiserikali zilikuwa zikionyesha kwa wastani wa siku hospitali ya rufani ya Muhimbili hupokea zaidi ya wagonjwa wa tano wapya wanaofikishwa kwa ajili ya kutibiwa uraibu wa madawa ya kulevya.

Inawezekana ikawa idadi ndogo lakini kimahesabu ni idadi kubwa sana na hilo lilimaanisha kwamba kuna zaidi ya wagonjwa wenye uraibu huo uraiani ambao hawakufikishwa hospitalini.

Sasa Hamza kutokana na kuishi uswahilini alikuwa akikutana na watu wa aina hio wanaotumia madawa ya kulevya kwa kiwango kikubwa, ndio maana sera ya mgombea mmoja wa chama fulani cha kisiasa baada ya kutaja vipaumbele chake ni kupambana na dawa hizo aliona angalau ana mantiki lakini kwasababu anazozijua yeye aliona ni sera ambayo ni ngumu sana kutekelezeka.

Hamza akiwa kwenye gari kama hivyo huwa ni mwenye kuyafikiria mapito yake na asubuhi hio alipokuwa akielekea chuoni alijipa muda wa kufikiria nia ya mzee katika maisha yake.

Ukweli ni kwamba maisha yake yote ni kama yameshikiliwa na huyu mtu anaejiita mzee ndio maana alikuwa akiwaza na alijiambia huenda kama sio Mzee angetafuta uelekeo mwingine wa kimaisha na kuacha kuendelea kuishi maisha ya kimaskini yaliojaa maigizo ndani yake.

Tatizo moja tu kuhusu Mzee ni kwamba alikuwa anamtishia sana maisha yake pale tu asipotii maagizo yake, kwa upande wake huenda mtu ambaye anamuogopa katika maisha yake ni huyo Mzee.

Kilichomfanya kumuogopa zaidi ni kwamba ukiachana na kumsaidia kimaisha mpaka kufikia umri aliokuwa nao Mzee hakuwa akionekana na hata mawasiliano yake yalikuwa ni nyakati za usiku lakini kutokuonekana kwa Mzee mbele yake haikumaanisha hakuwa na nguvu, alikuwa na nguvu kubwa ambayo Hamza mwenyewe ameweza kuishuhudia kwa macho yake katika kila hatua aliopiga katika maisha yake akiwa chni ya uangalizi wa Mzee.

Kuhusu swala hilo lilikuwa likimfikirisha sana miaka na miaka na kujiuliza kuna siri gani ya huyu mtu anaefahamika kwa jila la Mzee kumtafuta tu usiku.

Hamza akiwa kwenye daladala ambayo ilikuwa kwenye msongamano wa magari , palepale alijipa muda wa kufikiria maisha yake ya nyuma namna alivyokutana na mzee.


SEHEMU YA 02.
MWAKA 2002-SUMBAWANGA.

Ni mwezi wa kwanza wa mwaka 2002 katika kijiji cha Kizwite mkoani Rukwa Wilayani Sumbawanga alifika mwanamke mmoja ambaye alijipatia umaarufu sana kwa watu wote wa kijiji hicho na vijiji vya pembeni , umaarufu wa mwanamke huyo ulitokana na kuwa na watoto wengi ambao walikuwa wamepishana kwa miaka michache sana kwa namna ambavyo walikuwa wakilingana kwa muonekano wa nje, lakini kubwa zaidi ni namna walivyokuwa na rangi zinazotofautiana ikidhihirisha baba zao kuwa tofauti tena wa makabila tofauti duniani.

Yaani kwa maneno marahisi kati ya watoto hao kuna waliokuwa na mchanganyiko wa Kiarabu , Kizungu , Kichina , kijapani na Kiafrika. Kwa maelezo ya awali ya wanakijiji wanasema mwanamke huyo tokea afike hapo haikuwahi kujulikana alitokea wapi na kuhusu watoto aliokuwa nao aliwapata pata vipi au baba yake alikuwa ni nani haikujulikana , kitu pekee ambacho wanakijiji wa Kizwite walijua kuhusu mwanamke huyo ni jina lake lake tu ambalo lilifahamika kama Chakwe.

Wanakijiji wanaelezea kwa kusema kwamba Chakwe alionekana kama mwanamke ambaye alikuwa hana akili nzuri sana na walikuwa na makisio hata watoto aliokuwa nao walitokana na kubakwa , hayo yalikuwa ni makisio tu ya wanakijiji hao lakini ukweli wote alikuwa nao Chakwe mwenyewe lakini kutokana na hali yake ilivyokuwa haikuweza kufahamika moja kwa moja maisha ya nyuma ya Chakwe yalikuwa kuwaje mpaka akawa katika hali kama hio na alipelekea stori nyingi kumuhusu zikitungwa ndani ya kijiji hicho.

Chakwe mara baada ya kufika katika kijiji cha Kizwite hakujali kushangawa na watu bali alifuatishana na watoto wake huku na huko kujipatia chakula ,alikuwa na mbinu za kipekee sana katika kujipatia chakula, mbinu yake ya kwanza ilikuwa ni kuamua kwenda kukaa na watoto wake nje ya nyumba ambayo ameichagua kwa siku na mwenye nyumba asipowapa chakula basi Chakwe na watoto wake hawawezi kuondoka.

Mbinu ya Chakwe kukaa nje ya nyumba ya watu ilikuwa ikimsaidia sana , kwani watu wengi kutokana na ile hali ya kumnyanyapaa yeye na watoto wake ilibidi tu kuwapa chakula ili kuwaondosha katika eneo lao. Mbinu yake nyingine ilikuwa ni ya kuiba , lakini mbinu hio haikumsaidia sana kukidhi mahitaji ya watoto wake wote kumi ambao alikuwa nao hivyo mbinu ambayo ilikuwa ikifanya kazi ni ile ya kupewa chakula.

Chakwe hakuwa na nyumba ya kuishi hivyo hakuweza kupika na mara nyingi sehemu ambayo waliishi ni sehemu ambayo alijenga yeye mwenyewe kama hema chini ya mti na kuishi na watoto wake.

Aliweza kujenga nyumba hio kwa kutumia turubai ambalo aliiba kwa mwanakijiji mmoja ambaye alikuwa akilitumia kufunikia matofali yake na hata mwanakijiji huyo alipokuja kugundua Chakwe ndio alieiba hakuwa na la kufanya zaidi ya kusamehe.

Baada ya wanakijiji kuona Chakwe alikuwa akiteseka na watoto wake ndipo wanakijiji hao wakiongozwa na mwenyekiti wao waliamua kumpatia Chakwe nyumba ambayo ilisemekana alikuwa akiishi mwanaume ambaye hakuwa na familia , lakini mwanaume huyo alifariki kwa kuwekewa sumu.

Nyumba ambayo Chakwe alipewa na wanakijiji hao ilikuwa mbali kidogo na makazi ya wanakijiji , yaani ilikuwa imejitenga kidogo lakini haikuwa mbali sana , ni nyumba ambayo ilikuwa karibu sana na barabara ikizungukwa na miti,baada ya Chakwe kupewa nyumba hio angalau sasa aliweza kupata sehemu ya kuwasitiri watoto wake.

Maisha ya Chakwe na watoto wake ambao hawakufahamika majina yaliendelea ndani ya kijiji cha Kizwite kwa miezi mitano kamili na baada ya hapo ndipo Chakwe na watoto wake walipokumbwa na janga la Asili ambalo lilimuua yeye mwenyewe na takribani watoto wake wote kasoro mmoja tu.

Ilikuwa ni mwezi wa masika yaani mwezi wa tano kwenda wa sita ndani ya kijiji hicho sasa usiku mmoja Chakwe akiwa amejisitiri na watoto wake ilipiga Radi ambayo haikuwa ya kawaida katika nyumba ambayo alikuwa akiishi Chakwe.

Kama ujuavyo Radi inavyotokea hupiga mara moja au mara mbili na kisha hupotea na kuacha madhara basi hicho ndio kilichotokea.
Sasa mara baada ya Radi ile kupiga , yaani zikiwa zimepita kama dakika mbili kilionekana kivuli kikifika katika maeneo ya nyumba ya Chakwe.

Alikuwa ni mtu lakini mtu huyo hakuonekana sura kutokana na mavazi yake ambayo alivaa yalikuwa ni mavazi flani kama ya kininja lakini hayakuwa ya kininja yalikuwa ni mithili ya mavazi ambayo kwa kingereza hufahamika kama Cloak, mavazi flani hivi kama majoho ya rangi nyeusi ambayo huunganishwa na kofia kama vile ni Sweta lakini Kofia flani hivi ambayo mtu akijifunika huwezi kuona sura yake.

Sasa kivuli cha mtu huyo kilionekana hivyo na kwa namna mtu huyo alivyoweza kutokezea katika eneo hilo haikujulikana ametokea upande upi lakini aliweza tu kuonekana akiwa amesimama pembeni ya nyumba ya Chakwe ambayo ilikuwa imeharibiwa na Radi.

Yule mtu mara baada ya kusimama kwa dakika kadhaa katika eneo hilo, akiwa anamulikwa na mwezi uliokuwa ukitoa mwanga hafifu alipiga hatua kusogea mbele na sasa hata kile alichovaa miguuni mwake kiliweza kuonekana , alikuwa amevalia aina flani ya buti ndefu za rangi nyeusi mithili ya zile za mvua lakini hizo zilikuwa ni za kubana miguu kiasi na kisigino kirefu.

Nyumba ile haikuwa imeharibika yote, upande mmoja ulikuwa umebomoka na mwingine ulikuwa umesimama na yule mtu aliingia upande ule uliosimama na ndani ya dakika chache tu baada ya kupotelea kwenye uharibifu ule wa nyumba aliweza tena kuonekana kutokana na mbalamwezi.

Katika mikono yake alionekana akiwa amebeba kitu na kwa maelezo ya shuhuda ambaye aliweza kuona kila kitu anasema kwamba mtu huyo alionekana kama amebeba mtoto, kwa mara ya kwanza hakuweza kujua kama ni mtoto lakini baada ya wanakijiji kuweza kufika katika nyumba hio ili kuangalia kama kuna aliebakia hai ndipo walipobaini Chakwe mwenyewe amekufa na maiti yake ilionekana pamoja na ya watoto tisa.

Shuhuda alieshuhudia kila kitu alikuwa ni mwanakijiji wa hapo hapo na anaendelea kusema kwamba baada ya yule mtu kutoka akiwa ameshikilia mtu palepale hakuweza kumuona tena, anasema ni kama vile alipotea mara baada ya yeye kupepesa macho.

Haikuwa mara ya kwanza kwa watu kufa kwa kupigwa na radi lakini tukio la Chakwe lilizua gumzo , moja ya sababu ambayo ilipelekea kuzua gumzo ni maelezo ya mzee Kabwela ambaye alishuhudia kila kitu, ukweli ni kwamba kwa stori yake hio alioelezea kuna ambao waliamini na kuna ambao hawakuamini ,walioamini waliamini kutokana na kutokuonekana kwa mwili wa kumi wa mtoto wa Chakwe mwenye asili ya kizungu na wale ambao hawakuamini ni kwasababu ya stori ya Kabwela ambayo ilikuwa ni ya kufikirika.

“Mimi siwezi kuamini kabisa, Mzee Kabwela ametupiga kamba labda alikuwa amelewa kama kawaida yake”

“Lakini hata kama hamumuamini kutokana na tabia yake, je vipi kuhusu kupotea kwa maiti nyingine?”

“Swali zuri Kizito, huenda mtoto hakulala na mama yake au alipona na kukimbia”

“Mimi naamini maneno yake , mambo mengi ya ajabu yalitokea ambayo yalikosa maelezo mpaka leo hii , naendelea kuamini kutokana na kwamba niliweza kuulizia katika kijiwe cha pombe ambacho Mzee Kabwela hupendelea kwenda na niliambiwa siku hio hakuweza kufika , hivyo moja kwa moja inaniaminisha kwamba siku hio hakulewa”

Yalikuwa ni malumbano ya vijana ambao walikuwa wakicheza Draft ndani ya kijiji hicho ambao walikuwa wakizungumzia tukio lililotokea juzi yake mara baada ya kukamilisha kumzika Chakwe na watoto wake.

Vifo vya watu kumi na moja wa kijiji hiko vilizua gumzo sio kwa wanakijiji tu lakini hadi kwa taifa mara baada ya kutangazwa katika vyombo vya habari, huku maelezo ya Shuhuda Mzee Kabwela yakiamsha msisimko wa hali ya juu.

Ukweli ni kwamba kila watu waliokuwa wakiongelea tukio hilo na hata baadhi ya waandishi wa habari waliweza kufika katika kijiji hicho na kujaribu kuwahoji wananchi na habari walizoambiwa zilikuwa zikichanganya kidogo lakini kutokana na kutumia usomi wao kuna wengine ambao waliondoka kwa kuona maelezo ya wanakijiji hao hayakuwa na mantiki na kuna wengine waliweza kuamini kutokana na sifa kuu ya vijiji vingi vya Sumbawanga kwa kusifika na uchawi.

Hata wanakijiji wengine walienda mbali na kusema kwamba huenda hata radi hio ilikuwa ni ile ya kutengenezwa na walozi wakubwa wa kijiji hicho lakini hata hicyo hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja, hivyo jalada la tukio hilo likafungwa rasmi na tukio likasahaulika.

******

Hamza ambaye alikuwa kwenye gari alikuwa akikumbuka kwa uchache sana maisha ya utoto wake, yaani yeye na mama yake na ndugu zake, alikuwa akikumbuka kabisa alikuwa na wadogo zake wengi na walikuwa na maisha magumu sana , maisha ya kutanga tanga huku na huko wakimfuata mama yake.

Hamza anakumbuka kabisa katika akili zake japo kwa uchache katika watoto wa mama yake yeye ndio aliekuwa mkubwa, ambaye kwa kiasi flani alikuwa akijitambua kutokana na kuwa wa kwanza , kumbukumbu zake nyingine ambazo alikuwa akikumbuka ni namna ambavyo aliweza kushuhudia namna wadogo zake walivyopoteza maisha mara baada ya kumulikwa na mwanga wa ajabu.

Hamza hakukumbuka kwa usahihi sana kuhusu maisha yake ya utoto lakini baadhi ya kumbukumbu ambazo zilikuwa ngumu aliweza kuzikumbuka, hakuwa akijua alikuwa na miaka mingapi katika kumbuukumbu zake za utoto akiwa na mama yake.
Baada ua janga la asili kumkumba Hamza na kusalimika maisha yake yaligeuka na kuwa msururu wa matukio ya kusisimua sana , huku mtu anaefahamika kwa jina la Mzee akichukua nafasi kubwa katika msururu wa matukio hayo.

******

Hamza hakuwa akishukia kituo cha karibu na chuoni kwake, ni utaratibu aliokuwa amejijengea, alipenda kuchangamsha mwili wake kwa kutembea umbali mrefu kidogo, sasa mara baada ya kushuka wakati akiwa anatembea kando ya barabara akipishana na watu wengi ambao walikuwa katika harakati za maisha palepale alijikuta akiitwa kwa nyuma na sauti ambayo alikuwa akiitambua.

Nyuma ya Hamza alionekana kijana wa rika lake aliekuwa amevalia suruali ya kitambaa nyeusi, shati la rangi ya mikono mirefu jeupe na moka ya rangi ya kahawia, alikuwa amependeza kwa namna ambavyo alikuwa amechomekea ukijumlisha na mwonekano wake kwa ujumla, alikuwa na kila sababu ya kuitwa mwanaume mtanashati au Handsome, kama utamfananisha na Hamza basi moja kwa moja kijana huyo angeshinda upande wa nanmna mavazi yake yalivyo lakini katika upande wa sura ilioumbwa vyema Hamza alikuwa akichukua nafasi kubwa.

Hamza alikuwa na mchanganyiko wa rangi na kwa kumuangalia tu kwa haraka haraka lazima ungejua ni mchanganyiki wa mzungu na mwafirka, kinachomfanya Hamza kutoonekana wa kuvutia ni namna ambavyo anajiweka , alikuwa akivaa kawaida sana pengine kuliko mwanafunzi yoyote wa chuo cha FEMU na hilo lilimfanya kuonekana wa kawaida sana macho ya watu wengi.

“Muuza vyungu mwenyewe nakuona kama kawaida yako”Aliongea Hamza huku akiuonyesha tabasamu kwa rafiki yake afahamikae kwa jina la Alex.

“Kwa namna ambavyo unataongea , ni kama kazi ninayofanya ni ya hali ya chini , lakiini ukawaida unaoniona nao leo ndio unatokana na kazi yangu”Aliongea na kumfanya Hamza kutoa tabasamu la uchungu na kuendelea kutembea.

“Imekuwaje leo hii ukatembea kwa miguu, nilitegemea muda kama huu upo njiani ukiwa umempa mtoto wa kike lift”

“Hahaha, sio kila siku nampa mwanamke lift siku nyingine ni washikaji kama nyie , gari imezingua kuwaka asubuhi ya leo, nimekuja kwa lift kutoka kwa jirani yangu na aliniacha kule upande wa chini ndio maana nikaamua kutembea tu”Aliongea Alex na kumfanya Hamza kutingisha kichwa.

Baada ya kukaribia getini Alex aliungana na watu wengine waliokuwa wakimfahamu na kuingia huku wakiongea kwa kucheka lakini kwa upande wa Hamza alionekana kuwa na mawazo yake kichwani kwani hakujichanganya katika stori za watu hao ambazo mara nyingi zilihusisha wanawake.

Hamza alikuwa na muda mrefu kidogo tokea aanze kusoma ndani ya chuo hicho lakini mpaka kipindi hicho hakuwa amezoeana na watu wengi, pengine ni kutokana na hulka yake ya ukimya.

Licha ya Hamza kufahamiana na Alex ukaribu wao huwezi kusema ni ule wa kirafiki, ukweli ni kwamba Alex alikuwa ni mcheshi mno kiasi cha kuongea na kila moja na kucheka nae , alikuwa amezoeana karibia na darasa zima.

Umaarufu wa Alex ndani ya chuo hicho hutokana na biashara yake ya uuzaji wa vyungu vya aina mbalimbali , Alex alikuwa akihusika katika uuzaji wa vyungu vya kupikia , vyungu vya kuwekewa maua ambavyo vina urembo wa aina yake na bidhaa nyingine za aina hio na hili ndio ambalo lilimpatia umarufu kwani biashara yake ilikuwa sio ya kawaida na imekaa vibaya lakini ukweli ni kwamba ndio biashara ambayo ilimfanya Alex kuonekana mtu mwenye pesa na alikuwa akimiliki kabisa gari aina ya IST gari ambayo ilimpatia umaarufu na kufanya ashobokewe na wanawake wengi chuoni.

“Alex mambo?”Sauti nyororo iliweza kusikika nyuma ya vijana wa kiume wa chuo hicho cha FEMU akiwemo Hamza ambaye muda wote alionekana kuwa kimya akiwa sio mwenye kusikiliza stori za wenzake.

“Anitha..!!!”

Alex aliitikia kwa kubabaika kiasi huku kundi la wenzake likikaa kimya kumwangalia mrembo Anitha.

Alikuwa ni mwanadada mrembo mno , huenda ndio ambaye alikuwa akishika namba moja kwa uzuri ndani ya chuo chote cha FEMU ni mwanadada huyo huyo ambaye alimfanya Hamza kuwa maarufu ndani ya chuo cha FEMU.

“Niambie mamii ,, uko poa?”Aliongea Alex kwa mbwembwe huku akianza kulamba midomo yake na kusugua sugua mikono kiswaga na kumfanya Anita kutabasamu kiasi cha kupelekea mashavu yake kutengeneza vishimo.

“Niko poa”Alijibu Anitha huku akiangalia kundi la watu hao na ilishangaza kwamba licha ya wanaume waliokuwa wametangulizan na Alex kuwa wanadarasa lakini hakujihangaisha kusalimiana nao , lakini hata hivyo ni jambo la kueleweka.

Hakuna ambaye hakuwa akijua tabia ya maringo aliokuwa nayo Anitha ndani ya chuo hicho na ni kupitia maringo hayo ndio yaliomfanya Hamza kudhalilika na kujipatia umaarufu wa aina yake baada ya kukataliwa waziwazi.

Anitha alionekana kuwa na maongezi na Alex hivyo wale wengine kila mmoja alijiongeza na kupiga hatua za kuelekea darasani , isitoshe ni muda mfupi uliobaki mpaka kipindi kuanza.

*******

Shauku ni msingi wa kitabia ambao ni muhimu kwa binadamu kuwa nao ili kumuwezesha kujifunza na kukua.
Tukiwa na shauku inatupelekea kupata motisha ya kujifunza vitu vipya jambo ambalo linaweza kutupelekea kupata gunduzi za vitu vingine vipya ambavyo hatujawahi kuvifikiria.

Shauku ya muda mfupi inaweza kukupeleka kupata shauku ya muda mrefu na mwisho wa siku kujibu maswali uliokuwa ukijiuliza kwa muda mrefu, kwa mfano unaweza ukawa na shauku ya kumjua mtu kwasababu mtandaoni kaandika jambo ambalo ni fikirishi mwisho wa siku shauku yako inakupa motisha ya kutaka kuonana na huyo mtu na anakuelezea kwanini aliandika vile na katika maneno yake unajikuta unapata kitu kipya ambacho hujawahi kufikiria na shauku nyingine kuanza.

Ni muhimu kuwa na shauku inayoendana na vipaumbele vyetu ili tuweze kukua na kujifunza zaidi na zaidi na mwisho wa siku kuyafikia mafanikio. Kumbuka kila kitu kilianza kama shauku na shauku ikaibua mawazo na hatimae ikaipelekea dunia kuwa kama inavyoonekana leo.

“Paaa.. Paaah”Wanafunzi walijikuta wakipiga makofi ya nguvu.

Alikuwa ni Profesa Issai Stephano a.k. a Mr Bonus point, alikuwa amepewa jina hilo la utani kutokana na mwishoni mwa kipindi chake lazima atoe ushauri nje ya somo lake kwa wanafunzi wake ambao mwenyewe anaita Bonus point na siku hio alikuwa akielezea kuhusu Shauku.

Ijapokuwa mara nyingi mwishoni mwa kipindi chake aliongea kama utani lakini maneno yake yalikuwa na maana kubwa kwa wale ambao walikuwa wakimchukulia siriasi.

Katika watu ambao walikuwa wakipenda kipindi chake kiishe na kuweza kusikiliza Bonus Point ni Hamza , alipenda sana kumsikiliza Profesa Stephano kwani maneno yake licha ya kuyaweka kimatani zaidi lakini alikuwa akifikisha ujumbe wenye maana nzito ambayo kwa mtu aliekuwa siriasi kwa kile anachoelezea basi pengine angepiga hatua kubwa katika ukuaji wa kifikra.

Hamza wakati wenzake wakitawanyika katika ukumbi kwa ajili ya kusubiria kipindi kingine , yeye alikuwa akifikiria neno Shauku , maneno ya Profesa Stephano ni kama yamegusa kile kinachoendelea katika maisha yake.

“Ili kutimiza shauku yako ya muda mrefu unapaswa kufanyia kazi shauku yako ya muda mfupi , pengine majibu utakayoyapata kwenye shauku yako ya muda mfupi ndio mlango wa kutimiza shauku yako ya muda mrefu”Maneno hayo yalijirudia rudia katika kichwa chake.

“Shauku yangu ya muda mfupi kwa sasa ni ipi?”Alijiuliza Hamza lakini alishindwa kujibu swali lake mara baada ya kuja kushituliwa na moja wapo ya rafiki yake wa karibu afahamikae kwa jina la Amiri au Pacha mdogo.

“Mzee unawaza nini tena , ushasahau mpango wetu wa jana?”Aliuliza Amiri mara baada ya kumsogelea Hamza.
“Hamna nilikuwa nayawazia maneno ya Profesa , yanaonekana kuwa na uhalisia”

“Hahaha… Profesa watu wanamchukulia kama mzee wa Komedi kwa aina yake ya ufundishaji lakini yule mzee ni mtu ambaye ana uzoefu wa mambo mengi, kuna tetesi ambazo nimesikia pia jamaa inasemekana ni jasusi mstaafu”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza kumwangalia kwa mshangao.

“Unasema kweli?”

“Nimesema ni tetesi tu mzee , kama swali lako ni kuthibitisha hizo tetesi basi naweza kukujibu ndio, ni tetesi ambazo zinazungumzwa na watu wengi”Aliongea na kumfanya Hamza kutoa tabasamu la uchungu na aliona ameuliza swali la kijinga.
“Oya halafu mwana unaonekana kuwa na mawazo mengi ujue , vipi tunaenda au hatuendi?”Aliuliza Amiri mara baada ya kuona utayari mdogo wa Hamza.

“Tunaenda ili mradi tu malipo yawe ya uhakika”

“Haha.. hilo ondoa shaka ili mradi tu ufanye kazi kama ulivyosema maana bado hata siamini kama unaweza tengeneza”
“Siwezi kusema naweza halafu nikashindwa, ongoza njia tuondoke”Aliongea na Amiri alitabasamu na kisha walianza kutoka kwenye Hall 5 hiio kupitia mlango wa nyuma na kutoka.

Dakika chache mbele walitokea katika maegesho ya chuo ya muda mfupi na kusogelea gari aina ya Ford.

Ilikuwa ni gari ambayo anatumia Amiri ambayo ni ya kwake kabisa , Amiri hakuonekana mnyonge, ijapokuwa alikuwa akisoma chuo cha kawaida kama hicho lakini maisha yake yalikuwa ni yale ya juu lakini licha ya hivyo hakua akibagua watu wa kufanya nao urafiki.

Pengine kutokana na maisha yake ya juu angechagua marafiki wenye pesa kama yeye lakini ajabu alimchagua Hamza kama moja wapo ya marafiki zake, kwa mara ya kwanza Hamza na Amiri kujenga urafiki wao ni siku ambayo Hamza alitokea kuweka wazi hisia zake mbele ya mrembo Anitha, Hamza anakumbuka siku kilichompelekea mpaka kuweka hisia zake wazi ni kutokana na kuamua kutumia Bonus Point zilizotolewa mwisho wa kipindi na Profesa Singano.

Pointi ambazo zilimpa ujasiri Hamza na kuomba kuongea na Anitha pembeni na kumweleza hisia zake kwamba anampenda na bla blah kibao lakini mwisho wa siku Hamza aliambulia kejeli na kusonywa tena mbele ya Kadamnasi ya wanafunzi wenzake, ilikuwa ni kama vile Anitha alimfanyia makusudi kwani licha ya kwamba alikuwa na uwezo wa kumjibu kistaarabu lakini mwisho wa siku akaamua kumjibu kwa sauti kubwa ili mradi tu kumdhalilisha huku akimwita Hamza mtu masikini ambaye hana hadhi kabisa ya kutoka na yeye kimapenzi na aende kutafuta wa hadhi yake.

Amiri ambaye alikuwa ni sehemu ya wanafunzi hakuchulia swala la Hamza kama la aibu bali alichukua katika upande wa Chanya na kumuona Hamza kama mtu jasiri hususani pale alipoweza kumsikia Hamza na yeye kiropoka mara baada ya kukataliwa na kumwambia Anitha:

“Anitha unaweza usinipende leo , lakini mimi ni mbishi kufa na siku moja wewe mwenyewe ndio utanifuata na kutaka mahusiano na mimi , ndio itakuwa wakati wangu wa kukukataa”Aliongea Hamza bila ya aibu na kisha akapangua watu na kuondoka.

“Oya mzee sasa sikia , inshu niliokuambia jana ni complex kidogo lakini malipo yake ni ya kueleweka”

“Unamaanisha nini , si kufunga tu kwanini iwe Complex?”Aliuliza Hamza kwa mshangao kidogo.

“Ni kama nilivyokuambia Kamera ambazo unapaswa kufunga ni za siri sana na anaeishi hapaswi kujua”Aliongea na kumfanya sasa Hamza kuelewa anachotaka kumaanisha.

“Kwahio unamaanisha unataka nikusaidie kufunga spy Camera?”

“Ndio nilichokuwa nikimaanisha , najua tulikubaliana ni kufunga tu kamera lakini sijakuambia ni wapi na kwa ajili gani , ndio maana nikasema ni inshu Complex lakini ambayo ina malipo makubwa kama utafanikisha”

Kwa jinsi ambavyo Amiri alikuwa akiongea ilimfanya Hamza kuona pengine hamjui vizuri rafiki yake kwani ombi lake lilionekana kuwa na utata lakini ambalo limekaa kijasusi zaidi.

“Amiri kama ndio ulikuwa mpango wako najitoa , nina shida kweli ya pesa lakini vipi kuhusu usalama wangu , ninaweza kufanya kama unavyotaka lakini kama itagundulika ni mimi inaweza kuniletea matatizo”Aliongea Hamza.

Ukweli ni kwamba siku ya jana mchana Amiri alimuuliza Hamza kama alikuwa na ujuzi wowote wa kufunga CCTV Kamera amsaidie na Hamza alimjibu Amiri kwamba alikuwa na uwezo huo jibu ambalo lilimfurahisha sana Amiri na kumwambia kwamba kuna kazi anataka kumpatia na ina malipo mazuri kama tu atamsaidai katika jambo hilo.

Hamza alimwambia atamsaidia kwasababu ni rafiki yake lakini Amiri akagoma na kusema lazima amlipe na Hamza mara baada ya kuona Amiri analazimisha malipo hakutaka kukataa isitoshe alikuwa na shida ya pesa.

Sasa walikubaliana kesho yake ambayo ndio siku hio sasa , lakini ajabu ni kwamba Amiri anampatia Hamza maelezo tofauti na ya jana yake na kusema Kamera ambazo anapaswa kufunga ni Spy Camera , yaani sio kamera za ulinzi bali kamera za kiuchunguzi tena katika nyumba ya mtu, jambo hilo linamfanya Hamza kuona ni swala la hatari kwani inaweza ikabainika yeye ndio muhusika na kujiingiza matatizoni.

“Sikia Hamza najua ni kweli nimekuahidi malipo , lakini nimekuchagua kunisaidia hii kazi kwasababu wewe ni rafiki yangu , kuna kitu muhimu sana nataka kufatilia ili niweze kupata majibu ya wasiwasi wangu na shauku ya muda mrefu”
“Shauku gani na majibu gani?”Aliuliza.

“Ni stori ndefu rafiki yangu , lakini jua ni maswala ya kimapenzi ndio yananifanya niende mbali namna hii, nataka Kamera hizi zifungwe katika Apartment anayoishi demu wangu , kuna vitu ambavyo sivielewi kuhusu Mellisa ndio maana”Aliongea huku akianza kutia huruma kidogo.

“Kama nitakuwa sawa basi naweza kusema ni kwamba humuamini mpenzi wako , lakini sidhani kama kufunga Kamera sehemu anayoishi inaweza kukupa majibu ya kile unachokitaka , wenzako sehemu ambayo wanatakiwa kuweka umakini ni kwenye simu na sio mambo ya Kamera”

“Upo sahihi , lakini hayo unayoyasema ni kwamba nishayafanya tayari na ni mwaka sasa tokea nianze kumfatilia Mellisa kuhusu mawasiliano yake lakini sijawahi kuona kitu cha tofauti lakini bado hisia zangu zinaniambia Mellisa ananisaliti tena ananisaliti ndani ya nyumba ambayo nimempangishia mimi , Bro hebu nisaidie katika hili ni swala la dakika chache tu kulifanya na mimi lazima nikulipe” Aliongea na kumfanya Hamza kuanza kukuna kicha chake kwa namna flani alianza kumwelewa Amiri lakini bado kuna kitu hakipo sawa katika maelezo yake.

“Kama ni hivyo hisia zako zinakuambia nini na kwa nini ubahisi anakusaliti ndani ya nyumba uliompangishia , kuna viashiria vyovyote ambavyo umevipata?”

“Ni stori ndefu ambayo ina mlolongo wa matukio ambayo hata kama nitakuelezea hapa huwezi kunielewa bro , ila ninachojua ni kwamba Mellisa ananisaliti tena usaliti anaufanyia ndani ya Apartment niliompangia mimi , sina uhakika wa hisia zangu na hizo Kamera zitanipa majibu ya kile ninachotafuta , Bro nikipata ushahidi wa hisia zangu nitakuambia kila kitu kwasasa naomba unisaidie”

Amiri alimbembeleza Hamza kwa kila namna ili tu aweze kumsaidia na mwisho wa siku Hamza alikubali , isitoshe Amiri alikuwa amemsaidia katika mambo mengi sana ambayo yalihitaji pesa.

“Okey nitakusaidia katika hili lakini lazima tukubaliane jambo moja”

“Nipo tayari kukubaliana na chochote unachotaka , Hamza ili mradi tu unisaidie katika hili”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza kutoa tabasamu la uchungu.

“Sikia nitakusaidia lakini sihitaji malipo ya aina yoyote ile”Aliongea na kumfanya Amiri kushangaa kidogo lakini alijikuta akilipukwa na furaha isiokuwa ya kawaida haikuwa furaha kwamba hatolipa bali ni furaha kwamba ataweza kufungiwa hizo Kamera maana Amiri hakuwa na shida ndogo ndogo za pesa.
 
IBILISI RUDISHA AKILI ZETU(MIMI NA MKE WANGU).

MTUNZI:SINGANOJR

WATSAP:0687151346.
“Life is full of wonders, if you start wondering , you yourself might become a wanderer”
TULIPOISHIA
“Sikia Hamza najua ni kweli nimekuahidi malipo , lakini nimekuchagua kunisaidia hii kazi kwasababu wewe ni rafiki yangu , kuna kitu muhimu sana nataka kufatilia ili niweze kupata majibu ya wasiwasi wangu na shauku ya muda mrefu”
“Shauku gani na majibu gani?”Aliuliza.
“Ni stori ndefu rafiki yangu , lakini jua ni maswala ya kimapenzi ndio yananifanya niende mbali namna hii, nataka Kamera hizi zifungwe katika Apartment anayoishi demu wangu , kuna vitu ambavyo sivielewi kuhusu Mellisa ndio maana”Aliongea huku akianza kutia huruma kidogo.
“Kama nitakuwa sawa basi naweza kusema ni kwamba humuamini mpenzi wako , lakini sidhani kama kufunga Kamera sehemu anayoishi inaweza kukupa majibu ya kile unachokitaka , wenzako sehemu ambayo wanatakiwa kuweka umakini ni kwenye simu na sio mambo ya Kamera”
“Upo sahihi , lakini hayo unayoyasema ni kwamba nishayafanya tayari na ni mwaka sasa tokea nianze kumfatilia Mellisa kuhusu mawasiliano yake lakini sijawahi kuona kitu cha tofauti lakini bado hisia zangu zinaniambia Mellisa ananisaliti tena ananisaliti ndani ya nyumba ambayo nimempangishia mimi , Bro hebu nisaidie katika hili ni swala la dakika chache tu kulifanya na mimi lazima nikulipe” Aliongea na kumfanya Hamza kuanza kukuna kicha chake kwa namna flani alianza kumwelewa Amiri lakini bado kuna kitu hakipo sawa katika maelezo yake.
“Kama ni hivyo hisia zako zinakuambia nini na kwa nini ubahisi anakusaliti ndani ya nyumba uliompangishia , kuna viashiria vyovyote ambavyo umevipata?”
“Ni stori ndefu ambayo ina mlolongo wa matukio ambayo hata kama nitakuelezea hapa huwezi kunielewa bro , ila ninachojua ni kwamba Mellisa ananisaliti tena usaliti anaufanyia ndani ya Apartment niliompangia mimi , sina uhakika wa hisia zangu na hizo Kamera zitanipa majibu ya kile ninachotafuta , Bro nikipata ushahidi wa hisia zangu nitakuambia kila kitu kwasasa naomba unisaidie”
Amiri alimbembeleza Hamza kwa kila namna ili tu aweze kumsaidia na mwisho wa siku Hamza alikubali , isitoshe Amiri alikuwa amemsaidia katika mambo mengi sana ambayo yalihitaji pesa.
“Okey nitakusaidia katika hili lakini lazima tukubaliane jambo moja”
“Nipo tayari kukubaliana na chochote unachotaka , Hamza ili mradi tu unisaidie katika hili”Aliongea Amiri na kumfanya Hamza kutoa tabasamu la uchungu.
“Sikia nitakusaidia lakini sihitaji malipo ya aina yoyote ile”Aliongea na kumfanya Amiri kushangaa kidogo lakini alijikuta akilipukwa na furaha isiokuwa ya kawaida haikuwa furaha kwamba hatolipa bali ni furaha kwamba ataweza kufungiwa hizo Kamera maana Amiri hakuwa na shida ndogo ndogo za pesa.

SEHEMU YA 03.
Iliwachukua muda mchache sana kwa Amiri na Hamza kufika mwisho wa safari yao , katika maikazi ambayo anaishi mpenzi wake Amiri afahamikae kwa jina la Mellisa.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Hamza kufika ndani ya hili eneo na lilikuwa likivutia mno kama sifa zake zilivyokuwa zikivuma kwa watu wengi ndani ya jiji la Dar es salaam.
Ni moja wapo ya Apartment ambazo zinamilikiwa na kampuni ya kimataifa ya Dosam Global.
Kwa machache ambayo alikuwa akijua Hamza kuhusu kampuni yaDosam ni kwamba ilikuwa ni kampuni namba moja Afrika ambayo inajihusisha na maswala ya mahoteli na Real estate ambayo makao makuu yake ni hapa nchini.
Dosam ni kampuni namba mbili kwa ukubwa ukiachana na kampuni ya Vexto group ambayo imeweza kuwa na biashara karibia kila kona ya Dunia, ndio kampuni ya Kitanzania ambayo imeorodheshwa katika Nasdaq.
“Bro hii sehemu ni nzuri sijapata ona”Aliongea Hamza mara baada ya kuruhusiwa kuingia na watu wa usalama wa eneo hilo.
“Ni sehemu ya hadhi ya juu hii broo, asilimia kubwa wanao ishi hapa ni aidha michepuko ya vigogo wakubwa serikalini au familia zinazojiweza kiuchumi”Aliongea Amiri huku akiweka tabasamu la kirafiki.
Hamza aliishia kutingisha kichwa huku akizungusha kichwa kulia na kushoto akijaribu kushangaa mazingira.
Ndani ya jiji la Dar es saalam kuna apartment nyingi tu ambazo zina mazingira ya juu lakini ukizungumzia Apartment hii ya Dosam’s Homes sio tu ukubwa wa jengo hilo bali ni uzuri wa jengo lenyewe , usanifu wake ulikuwa ni ule wa ulioendelea na pengine ndio jengo la makazi lenye mvuto mkubwa ndani ya Afrika nzima.
Hamza alijiambiaAmiri alikuwa na haki ya kuwa na wivu na mpenzi wake kama kweli amempangishia hili eneo.
“Bro hapa kwa mwezi malipo yake yakoje?”
“Kwa mwezi hapa ni doller elfu tano”Aliongea Amiri bila wasiwasi lakini bei yake ilimfanya Hamza kushindwa kupumua vizuri maana kwa haraka haraka pesa hio kama ikibadilishwa kwenda hela za kitanzania ni zaidi ya milioni kumi na mbili.
Pesa hio kwake ingeweza kumtosha kutatua changamoto zake zote hata kuanzisha biashara ambayo itaweza kumsaidia kwenye maisha yake ya hapo jijini Dar es salaam.
Dakika ambayo wanasubiria mlango wa lift kuweza kufunguka waliweza kukutana na harufu nzuri ya marashi na Hamza mara baada ya kuangalia mbele aliweza kukutanisha macho yake na mwanamke mmoja mwenye urembo wa ajabu mno ni aina flani ya wanawake ambao ni ngumu sana kuwaona mtaani , aliishia kujisemea Mungu anajua kuumba maana ni kama macho yake yanamdanganya na mwanamke huyo alikuwa akimuona ndotoni.
“Broo !!!, Oya Hamza!!”
“Eeh..!!”Hamza alijikuta akishikwa na mshangao na aliishia kujifikicha macho na kisha akatumbukia kwenye Lift huku yule mwanamke mrembo wa rangi ya chocolate akitoa tabasamu la dhihaka na kumpita Hamza kama kituko.
Alionekana ni wale wanawake ambao washazoea kushangawa na wanaume kutokana na urembo wao.
“Hahaha…. Bro naona mtoto kakuchanganya mpaka ukawa unaota?”Aliongea Amiri huku akishindwa kujizuia kucheka.
“Bro huyo manzi sio wa kawaida, nilidhani naangaliana na jini”
“Hahaha..huyo ni demu wa kawaida mbona , halafu mwanangu usihadaike na huo uzuri ni wa kutengeneza”
“Unamaanisha nini wa kutengeneza?”
“Namaanisha sio wa kuzaliwa nao , huyo manzi uliepishana nao nimemjua vizuri sana kupitia Mellisa, kwa habari za chini nasikia anafanya kazi Binamu Island”Aliongea Amiri kwa sauti ya chini kama vile jambo analoongea ni la usiri na usiriasi.
“Binamu Island !!?”Aliongea Hamza kwa mshangao kidogo na palepale macho yake yaliongezeka ukubwa.
Hamza alikuwa na taarifa chache sana kuhusu Kisiwa cha Binamu(Binamu Island) , taarifa chache alizokuwa nazo kuhusu kisiwa hicho ni kwamba kwanza kabisa ni cha kutengeneza ambacho kinapatikana bahari ya Hindi karibu kabisa na jiji la Dar es salaam.
Kwa fununu ambazo aliweza kusikia ni kwamba kisiwa hicho muda unafanya kazi tofauti na nje ya dunia(Timeless island), ni uzushi ambao kwenye maisha yake hajawahi kukubaliana nao hata mara mara moja.
Siku ambayo aliweza kusikia habari hizo kwanza alicheka na kujiambia waru wanadanganyika kirahisi sana ili tu kuweza kwenda kutembelea katika eneo hilo.
Ukiachana na fununu ambazo anasikia Hamza ukweli ni kwamba Kisiwa hicho kipo kabisa na kimejibebea jina kwa zaidi ya miongo kumi dunia nzima na kimekuwa chanzo cha kuendelea kwa mataifa ya Afrika mashariki kutokana na kutembelewa sana ,kimekuwa kivutio kikubwa sana kwa watalii.
Kwa maelezo machache ni kwamba sio watu wote ambao walikuwa na uwezo wa kufika katika kisiwa hicho kwani ni gharama kubwa sana.
“Nimesikia hivyo bro lakini bado siamini , mimi mwenyewe pamoja na kuwa na hela sijawahi kufika katika hiki kisiwa , lakini kwa upande mwingine naweza kumuamini Mellisa kwani maisha ya Tresha ambayo anayaishi hapa jijini sio ya kawaida”
“Tresha ndio nani?”Aliuliza Hamza muda huo mlango wa Lift ukifunguka na kuwaruhusu kutoka.
“Ni huyo mrembo uliekutana nae kule chini , anafahamika kwa jina la Tresha Noah ni maarufu sana mtandaoni”Aliongea na kumfanya Hamza kutingisha kichwa vhake kumwelewa.
Asilimia kubwa ya wakazi wa hili jengo kwa muda huo wanakuwa kazini na hata wale wachache wanaobaki majumbani ilikuwa ni ngumu sana kuonana nao nyakati za muda huo nadhani ndio maana Amiri akachagua kazi yake kufanyika katika wakati huo.
Baada ya kutembea umbali mfupi walisimama kwenye Apartment namba 103 na Amiri alitumia ‘pasword’ kufungua mlango huo na kisha wote wakaingia.
Hawakuwa wamesahau vifaa vya kazi kwani Amiri alikuwa amebeba begi kubwa wakati huo huku na Hamza mwenyewe akiwa na begi dogo.
Hamza mara baada ya kuingia ndani aliishia kutingicha kichwa na kujiambia kuna watu wanaishi pazuri , ijapokuwa watanzania wengi walikuwa wakidharau kuishi katika nyumba za kupanga aina ya Apartment lakini ufahari uliokuwemo humo ndani ulimpa msukumo na yeye siku moja kuweza kuishi katika mazingira kama hayo.
Hamza kama kawaida yake mara baada ya kuingia eneo la ndani alianza kukagua sebule hio na macho yake yalikuja kutua katika picha mbao yenye kuonyesha sura ya mwanamke mrembo ilioning’inizwa ukutani.
“Oya huyu ndio demu wako?”Aliuliza Hamza.
“Ndio huyo babu , unamuonaje?”
“Aisee ni kisu hata zaidi ya yule Tresha?”
“Hahaha,.. bro sipingani na wewe , Mellisa ni mzuri kuliko unavymuona kwenye hio picha , ukimuona laivu ndio utajua yule Tresha ni wa kawaida sana halafu Mellisa yeye uzuri wake ni wa asili sio wa kutengeneza”Aliongea Amiri kwa kujigamba.
“Ndio maana hujiamini?”
“Hehe ,, bro hata ni wewe ungekosa amani, nina pesa na namtimizia kila kitu lakini bado tu siamini kama ananipenda na hatonisaliti, isitoshe pia aina ya kazi yake inamkutanisha na vibopa zaidi yangu”
“Anafanya kazi gani?”
“Ni meneja wa benki ya Dosam Commercial Bank(DCB) tawi la Ubungo”Aliongea na kumfanya Hamza kushangaa kidogo.
“Anaonekana amepiga hatua katika maendeleo binafsi, naweza kusema haumhudumii kwa kila kitu, maana kwa ninavyojua wafanyakazi wa Dosam sio kama wafanyakazi wa mabenki mengine”
“Hicho ndio kinachonitia wasiwasi bro Mellisa hanitegemei kwa kila kitu hana njaa na mengine namfanyia kwasababu ni mapenzi, ukumbuke pesa ya mwanamke katika mahusiano pia haina thamani na wanajali sana wanachopewa kuliko wanachonunua”
“Haha uko sahihi”Aliongea Hamza huku akimuonea wivu Amiri kuwa na mwanamke mrembo mwenye mafanikio kama Mellisa,alijiambia yeye kama mwanamke wa kawaida kama Anitha amemshindwa ndio atafanikisha kwa Mellisa.
Ijapokuwa maelezo ya Amiri yalimwambia Mellisa ni mzuri zaidi kuliko anavyoonekena kwenye picha lakini kwa haraka haraka alimuona ni mzuri zaidi kuliko Anitha mwanamke ambaye alijaribishia bahati yake na akamdhalilisha mbele za watu kwa kejeli huku akimwambia ananuka umasikini.
Hamza mara baada ya kukumbuka matusi ya Anitha alijikuta akijichekea moyoni na kuachana na mwazo hayo na kisha alianza kufanya uchunguzi wa namna ya kufanya kazi yake.
“Bro unaonaje hapa , nataka picha kwanzia chumbani kwake mpaka hapa eneo la sebuleni , nataka kila kinachofanyika hapa niweze kukiona kupitia simu yangu”Aliongea na kumfanya Hamza sasa kuona kuna kitu hajakifikiri.
“Hizo ni Camera aina gani umenunua?”
“Ni IP Camera , vipi kuna tatizo?”
“Kama ni hizo hakuna tatizo, unachotaka kinawezekana”Aliongea huku akifungua mfuko wa vifaa na kuchunguza kamera hizo za kiuchunguzi na palepale Hamza alianza kufanya vipimo vyake kwa kutumia Angle ,ili kuweza kufunga Camera hizo kwa siri
Hamnza aliomba aonyeshwe na eneo la chumbani ili kuanza kazi yake na Amiri hakupimgas na waliingia wote chumbani na baada ya Hamza kuridhika alianza kazi yake ya ufundi, alifanya kazi kwa spidi kubwa mno huku akimuagiza Amiri kumpatia kila anachohitaji.
Amiri kwa upande wake alijikuta akimshangaa tu Hamza na kujiuliza ujuzi huo Hamza katolea wapi , ijapokuwa alikuwa akijua anaiweza kazi hakutegemea kama anaweza kuwa mtaalamu hivyo kwani ilikuwa ni kama anaangalia filamu za kijasusi, ndani ya dakika ishirini tu kila kitu kipo tayari na Hamza alirudisha mazingira sawa kama yalivyokuwa na kumwambia Amiri akague kama anaweza kugundua na mara baada ya Amrii kuangalia matokeo yake yalizidi matarajio aliokuwa ameyaweka kwa Hamza.
“Bro sijategemea kama kazi ingekuwa nyepesi kwako kiasi hichi , unaonekana ni mtaalamu wa hali ya juu”Aliongea Amiri huku akitoa mwanya wake nje lakini kwa wakati mmoja akimwangalia Hamza kwa wasiwasi na kujiambia pengine bwana huyo anajifanyisha kuishi maisha ya chini tu na ni mtu mwenye historia yake..
“Kaka sisi ambao maisha yetu ni ya chini tunajitahidi kujifunza aina mbalimbali za ujuzi ili tu tusiweze kupitwa na fursa , kwa wewe ambaye maisha yako yana msingi mzuri huwezi kunielewa”Aliongea Hamza na kumfanya Amiri kutoa tabasamu kwani maneno yake hayakuwa mbali na ukweli.
Yeye amezaliwa katika familia ambayo ilikuwa na kipato cha juu , hivyo ni rahisi kusema utajiri ameukuta na hata anachokisomea ni kwa ajili tu ya kuendeleza mali, kwake shida yake kubwa pengine ni maswala ya kimapenzi tu lakini likija swala la pesa alikuwa vizuri.
Baada ya kukamilisha kazi Hamza alimwambia kazi nyingine wanaweza kuifanyia mbali na eneo hilo kumsaidia kuseti kila kitu kuweza kuonekana kwa vifaa vya mbali na Amiri hakuwa na shida.
“Kwahio kwanzia hapa nitaweza kuona kila kitu?”
“Yeah zile ni aina ya Camera ambazo zinatuma teknolojia ya live streaming na zinatuma vidio kwako kwa njia ya internet, ni rahisi kuunganisha kupitia tarakishi kuliko hio simu yako ya Apple, unapaswa kuwa na Android tuweze ku install Apk maalumu ili kufanya configuration ya RTSP”Aliongea Hamza.
“Ninayo hapa hapa simu ya Android”Aliongea na palepale alifungua mkebe wa gari na kutoa simu janja kampuni ya Sumsung tole jipya na kumpatia Hamza.
Hamza alitumia dakika chache tu aliweza kumuunganishia Amiri kila kitu na kumpa aangalie na bwana huyo mara baada ya kuona mitambo imekaa vizuri alijikuta akishindwa kuzuia furaha yake.
“Mellisa japo nakuamini lakini kwa mapenzi yangu kwako nimeona niende mbali hivi , utanisamehe lakini naheshimu hisia zangu, naomba unithibitishie ninachowaza sio cha kweli”AluwazaAmiri huku akiangaalia mazingira ya eneo la Sebuleni kwa Mellisa na ndani chumbani wake.
“Hamza shukrani sana kwa msaada wako mzee , ukiachana na hisia zangu mbaya zidi ya Mellisa lakini kama ni kweli nina shauku ya kutaka kumuona mwanaume anaenisaliti nae”
“Nadhani unajitafutia maumivu ya moyo tu ndugu yangu?”
“Ni kweli unachosema , lakini nimewekeza hisia zangu nyingi kwa yule mtoto nampenda kuliko hata neno lenyewe , najua ninachofanya ni hatari lakini najua nini nitafanya hata kama nnikigundua ananisaliti , ila nikwambie tu Mellisa ni mwanamke ambaye siwezi kumuacha”
“Unaonekana kuwa jasiri , lakini usisahau ni vizuri kupenda na kupendwa pia”
“Haha..hata wewe mwenyewe ni mtu jasiri usisahau nilivutiwa na ujasiri wako ndio maana leo hii sisi ni marafiki , tuna tabia zinazofanana”
“Haha.. sidhani ule ulikuwa ujasiri , pengine wewe unaweza kuona ni ujasiri ila wengine wanaona ni ujinga na wananichukulia kama mwanaume dhaifu”
“Haijalishi wanafikiria nini ili mradi kama mwanaume umeweka wazi hisia zako bila ya kujali mazingira , mengine yapo nje ya uwezo wako”Aliongea na kumfanya Hamza kutabasamu.
*******
Ni masaa kadhaa baada ya Hamza kuachana na Amiri moja kwa moja alichukua daladala kuelekea mahali anapoishi.
Amiri alitaka kumpeleka lakini Hamza alimgomea na kumwambia atapanda daladala na Amiri hakutaka kwenda mbali kwenye kumbembeleza hivyo alikubali aondoke kinyonge.
Amiri alishangazwa na rafiki yake Hamza kwani alionekana kuwa na shida ya pesa lakini alikataa malipo kiasi cha kumfanya kukosa raha lakini kwasababu yalikuwa ni makubaliano hakutaka kulazimisha sana , aliona pengine Hamza amemsaidia kutokana na mara nyngi alikuwa akimsaidia.
Wakati Hamza akiwa kwenye daladala akiwa amepata siti yake kwa kuigombania, alitoa simu yake kwa ajili ya kuingia mtandaoni maana yalikuwa yamepita masaa bila kuingia huko kuona kinachoendelea.
Alikuwa akipenda sana mitandao ya kijamii na alikuwa ni radhi asile chakula ili mradi tu kuwa na bando hiyo yote ni kutokana na kwamba hakuwa na marafiki wengi na mitandao hio lilikuwa sehemu ya kupunguzia mawazo.
“Huu uzi bado tu una trend?”Aliongea Hamza huku akijaribu kuufungua tena na alishangaa kulikuwa na maoni mengi mno, alijaribu kutafuta maoni ya mtoa mada lakini hakuona chochote na kuishia kujawa na shauku zaidi juu ya mtoa mada aliona pengine anamaanisha alichokiandika.
“Kwanzia sasa hivi ngoja nifanyie kazi maneno ya Profesa Stephano nione kama yana uhalisia”Aiongea Hamza akikumbuka somo la Bonus point lililokuwa likizungumziwa na Profesa kuhusu Shauku.
Hamza alijikuta akipotezea makelele ya watu waliokuwa kwenye daladala kushabikia maswala ya uchaguzi na kwenda katika PM ya mtoa mada na kutuma ujumbe.
“Kwa kuzingatia tangazo lako , nipo tayari kwa ajili ya Ajira mawasiliano yangu ni 0656786***** naishi mkoani Dar es salaam”
Ni ujumbe mfupi ambao Hamza aliandika na alijikuta akijicheka mwenyewe , aliona ni kama anajiingiza kwenye mtego wa mtoa mada lakini aliona potelea pote , ngoja ajaribu bahati yake.
Baada ya kutuma ujumbe huo aliamua kuendelea na kutafuta mada nyingine ambazo zilikuwa zikimfurahisha na kupitia mada pamoja na maoni , lakini hata hivyo hakuna kizuri alichoona zaidi ya habari za uchaguzi tu, pengine habari ya ajira ya mahusiano ndio ambacyo ilikuwa ni habari mpya iliopata umaarufu na kutrend katika hizo siku kadhaa..
Usiku wakati Hamza akijiandaa kulala aliingia katika mtandao wa Watsapp na kutafuta jina la Anitha ambalo baada ya kulipata aliweza kuona mrembo huyo yupo Online , Hamza alitoa tabasamu na kisha akatuma ujumbe mfupi wa kumtakia mrembo Anitha usiku mwema huku akimsifia maneno ya hapa na pale kuusifia uzuri wake.
Aliangalia ujumbe huo kusomwa huku akiwa kama mtu mwenye matarajio ya kujibiwa ilihali alijua kwa asilimia tisini na nane Anitha hawezi kujibu ujumbe wake, mara baada ya kusubiria kwa dakika kadhaa alishuhudia tu ujumbe wake kusomwa na kisha palepale DP ya mrembo huyo ikipotea na kuweka kivuli cha sura ya mtu na kwa akili yake ya haraka haraka alishajua ashalambwa tofali.
“Hahaha… maringo ya huyu mwanamke inamfanya kutabirika”Aliongea Hamza huku akitoa kicheko cha uchungu na kujikuta akirusha simu pembeni, alijilaza kwenye gorodo lake la wanafunzi la nchi sita huku akiangalia darini kama kuna kitu anachokiwaza, aligeuza kichwa cheke upande wa kushoto lakini palepale alijikuta akikunja uso mara baada ya kuhisi harufu nziro iliokuwa ikitoka kwapani.
“Hizi ndio sababu ndogo ndogo ambazo zinampelekea Anitha kutonipenda , ngoja nikaoge kwanza”Aliongea Hamza na kisha alipiga teke dumu moja kivivu kuona kama lina maji na alitoa tabasamu mara baada ya kuhisi lilikuwa na maji japo kidogo.
Baada ya kuyamimina yote kwenye ndoo , licha ya kwamba haikujaa mpaka juu lakini hakujali, palepale alipunguza nguo na kisha akachukua taulo lake lililochakaa na kutoka nje kulitafuta bafu la pamoja(public) kuoga.
Ilikuwa usiku hivyo muda kama huo mara nyingi hakukuwa na bughuza upande wa bafuni na ilikuwa ratiba yake mara nyingi kuoga muda huo ili kuepuka kero za wapangaji wengine.
Hamza alitumia dakika chache kuoga pamoja na kukata gogo(Haja kubwa) huko huko na kisha alirudi na kujifuta maji na kisha akavaa bukta yake ya jezi ya Simba na kujitupa kitandani lakini usingizi ulikuwa mbali hivyo alichukua simu yake na kuzama tena JamiiForum.
“Hapa ngoja nitafute bandiko lolote la kizushi refu litanisaidia kupata usingizi”Aliongea huku akifungua mtandao wa JamiiForuma na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye jukwaa la Jamii Intelligence na kutafuta bandiko la kizushi.
‘Wajue Night Shadows , kikundi cha siri kinachotawala Dunia nyuma ya pazia”
Hamza mara baada ya kukutana na uzi huo alijikuta akivutiwa nao mara baada ya kuona una maoni ya watu wengi pamoja na Views , aliufungua kuona kuna kipi ambacho kimewavutia watu.
“Je unawajua Night Shadows ndio wamiliki wa kisiwa cha Binamu?”
Hamza mara baada ya kuona swali hilo ambalo mwandishi alionekana kuliweka makusudi ilimfanya kuvutiwa kwani ni mchana tu aliweza kukutana na mrembo Tresha Noah katika Apartment za Dosam Homes , alijiambia hapo ni mahali pake.
SEHEMU YA 04
Mwaka 2020 ni mwaka ambao ni wa kukumbukwa dunia nzima, ni mwaka ambao uliandika historia ya aina yake tokea binadamu kuanza kuishi maisha katika dunia akitegemea nishati ya joto na mwanga kutoka kwenye jua.
Kwanini mwaka 2022 ni mwaka wa kihistoria?
Ni kwasababu ya tukio la ajabu sana ambalo liliwahi kutokea , tukio ambalo mpaka leo hii halikutolewa ufumbuzi wa kueleweka kwa wakazi wote wa dunia hii.
Kwa maneno marahisi ni kwamba ni tukio ambalo tumefichwa ukweli wake na watu wanaojiita serikali.
Mwaka huu ndio mwaka ambao kwa mara ya kwanza ndani ya bara la Afrika kupata majira ya theluji(snow).
Linaweza kuwa jambo la kushangaza lakini ni kwa maeneo machache sana pengine hakuna kabisa ndani ya bara la Afrika kihistoria joto kushuka mpaka kufikia hatua ya unyevu nyevu uliopo angani kuganda na kupelekea Theluji.
Kushuka kwa baridi kwa kiwango cha kushangaza haikuwa kwa Afrika tu , tukio hilo linakumbukwa kutokana na kwamba maeneo ambayo yalikuwa yakipata Theluji katika vipindi vya majira, joto lake lilishuka sana kiasi kwamba kuyafanya mazingira hayo kutoweza kusapoti maisha ya binadamu, mimea na wanyama kiasi cha kukimbilia katika bara la Afrika ili kuweza kupata hifadhi ya muda kwa matarajio ya kipindi cha baridi kitakapo pita wangerejea katika makazi yao.
Hili ndio tukio la kwanza kuikumba dunia kiasi cha kufanya Afrika kuonekana mahali salama kwa makazi ya muda ndani ya dunia kwa ajili ya kujikinga na baridi iliokumba mabara mengi..
Ijapokuwa sio watu wote waliokimbia makazi yao na kuja kuishi katika bara la Afrika lakini idadi kubwa ya watu waliokuja kuomba makazi ya muda katika bara la Afrika ilikuwa kubwa mno.
Wanasayansi mbalimbali walishindwa kutolea maelezo mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa hio na kuishia kusema ni tukio la kustaajabisha.
Wapo waumini ambao waliweza kuamini ni siku za mwisho za dunia zilizotabiliwa zimewadia.
Ajabu ni kwamba tukio hilo halikudumu muda mrefu sana mpaka hali ya hewa kurudi katika hali yake ya kawaida na maisha kuendelea,
Baada ya tukio hilo ambalo lilikosa maelezo yakinifu, nadharia za kizushi za aina nyingi ziliibuka na kusema pengine ni onyo kutoka kwa Mungu kwa binadamu kwa matendo yao wanayoyafanya kutokana na anasa mbalimbali zilizokuwa zikifanyika , anasa ambazo zilikuwa zikienda kinyume na mapenzi ya Mungu.
Ukweli ni kwamba kila mtu aliibua kauli yake na wale watu wenye wafuasi wengi kwenye mitandao waliweza kuvumisha kila uzushi uliosemwa na watu wengi kuamini,.(Wakuu nyie ni mashahidi wa tukio hili)
Lakini watu wanasema sikio la kufa halisikii dawa , baada ya tukio hilo la ajabu kuikumba kupita kila mtu alisahau na maisha kuendelea na wale ambao ni watu wa dini walizidi kujikita zaidi na sala wengine wakisema wanaisubiria siku ya kiama na wengine walisema wanasubiria siku ya unyakuzi.
Mara baada ya tukio hilo kupita kulitokea Uzushi maarufu wa kinadharia(Consipiracy theory) iliohusisha uwepo wa watu vivuli(Night Shadows) ambao hutembea usiku.
Zimekuwepo shuhuda mbalimbali kuhusu matukio ya watu kadha wa kadha ambao wameweza kukutana na hawa watu wanaosemekama kuwa ni vivuli na kuwahusisha na viumbe kutoka sayari nyingine(Aliens).
Wakuu mnachokiona chini ni baadhi ya picha za ushahidi ambazo zimepigwa kuhusisha hawa watu wanaojiita Night Shadows.
Je hawa watu ni kweli ni Alien kama watu wanavyosema, je tukio la mwaka 2020 December lilikuwa na uhusiano na hawa watu vivuli , je ni kweli ujenzi wa kisiwa cha Binamu kuna uhusiano na hawa watu.
Kabla ya kuendelea wanabodi nataka kwanza mjiulize kwanini kisiwa cha Binamu kimekuwa maarufu?, kwanini kisiwa hichi ni ghali sana kutembelea lakini bado watu wanaenda.?
Itaendelea hivi punde
********

Down here in the rain fields
Outside of the Glow
My world is getting Smaller
Oh , oh , oh no
………………..

Mwito wa simu wa wimbo wa Low Tides kutoka kwa msanii Tom Rhodes ndio uliomuamsha Hamza ambaye hakujua hata amelala saa ngapi na alichokumbuka tu ni kwamba alikuwa akisoma mada ya kizushi kwenye mtandao wa JamiiForums mpaka kupitiwa na usingizi , baada ya kufumbua macho kivivu akiwa bado na usingizi alianza kuitafuta simu yake kwa kupapasa godoro lake lakini hakuiona na iliita mpaka ikakatika na hapo hapo aliendelea kujilaza kivivu, asiangalie hata muda huo ni saa ngapi.
Wakati akibadilisha staili ya kulala palepale simu ilianza kuita tena na awamu hii ilimuamsha kwa kusogea kidogo mpaka kwenye kingo ya Godoro na kuichukua simu hio ikiwa imedondoka chini Sakafuni.
Hakushangaa kwani hata hivyo haikuwa mara yake ya kwanza kupotelea usingizi usiku akiwa anaitumia na kudondokea chini.
“Hello!!”
Hamza hakujisumbua kabisa hata kuangalia aliekuwa akipiga ni nani na yote hio ni kutokana na macho yake kuogopa mwanga wa simu kwani ndio kwanza alikuwa akiamka.
“”Naongea na Ndugu Hamza Mzee?”
Sauti ya kike nzuri iliweza kusikika kwenye ngoma za masikio yake na kumfanya Hamza kushituka na kutoa simu sikioni na kuangalia namba ambayo ameipokea bila ya kuangalia jina la mpigaji lakini alishangaa mara baada ya kugundua ni namba mpya.
“Hello.. Mbona kimya!!”Sauti upande wa pili iliweza kusikika mara ya pili mara baada ya kimya cha Hamza kuwa kirefu.
“Ndio mimi ni Hamza , naongea na nani tafadhari?”
“Unaongea na mwanachama wa JamiiForuma mwenye ID ya Ngwena”Sauti ilisikika na kumfanya Hamza akili yake kufanya kazi kwa haraka na mara baada ya kukumbuka alijikuta akijikalisha kwenye godoro lake.
“Oh! .. wewe ndio ulieotoa tangazo la Ajira la kutafuta boyfriend feki eh?”Aliongea Hamza akiwa sio mwenye kuamini.
“Upo sahihi , je utapenda tuchati kwa meseji au tuongee kwa simu?”Sauti ile nyororo ilianza kumsisimua Hamza.
Katika maisha yake hio ilikuwa ndio mara ya kwanza kuamshwa na simu asubuhi na sauti ya mwanamke mwenye sauti nyororo namna hio , ilikuwa ni kama anaota na muda wowote angeshituka kutoka usingizini.
Ukweli ni kwamba licha ya jana kujaribu kuingia katika PM ya mwanachama huyo wa mtandao wa Jamii Forum hakuwa na uhakika kama anaweza kutafutwa yote hayo ni kutokana na kwamba hakuchukulia swala lenyewe kuwa siriasi kutokana na maoni ya watu , lakini pia asili ya Tangazo lenyewe kwani halikukaa sawa.
Maisha ya watanzania wengi yalikuwa ni ya kimasikini sana na uchumi ulikuwa ni mgumu mno na hata waajiri hawakuajili tena zaidi ya kupunguza wafanyakazi.
Hali hii haikuwa ya kawaida kwa mtu kuweka tangazo mtandaoni la kutafuta mchumba wa maigizo halafu kumlipa , ilikuwa ni swala la kichekesho na ambalo haliwezekani.
“Kwahio unasema kwamba tangazo lile lilikuwa siriasi na umeridhishwa na mimi ndio maana ukanipigia?”Aliuliza Hamza akiwa bado haamini huku akiangalia saa ya simu yake na kulaani kimoyo moyo kwani alikuwa amechelewa kuamka sana, ilikuwa ikikaribia saa moja na nusu na muda huo pengine angetakiwa kuwa kwenye gari kuelekea chuoni.
“Ndio maana nimekupigia Hamza , lakini ili kujua kama unafaa lazima nikuulize maswali kadhaa ndio nikupe muongozo wa kinachofuata”
“Unaweza kuendelea tafadhari?”Aliongea.
“Una ishi mkoa gani Hamza?”
“Naishi hapahapa Dar es salaam kama nilivyoelezea kwenye ujumbe wangu”Alijibu Hamza huku akitoa tabasamu , alijiambia lazima mwanamke huyo atakuwa ni mrembo kutokana na sauti yake.
“Vizuri , je una miaka mingapi?”
“Nina miaka ishirini na saba?”
“Okey! Hamza asante kwa kujibu maswali yote , hatua ya pili inayofuatia kama upo siriasi kufanya kazi ya kuwa boyfriend feki unapaswa kufika katika Dosam V hotel muda ni kesho saa nne asubuhi kwa ajili ya Usaili na kama utafanikiwa kupita basi utasaini mkataba wa ajira”
“Usaili!!, ?Unamaanisha nini kuhusu Usaili , kuna haja juu ya hilo?””
“Hamza nadhani ni utaratibu wa kawaida kufanyiwa Usaili na kama utafaa kivigezo basi utaweza kupewa ajira rasmi kama ilivyotangazwa”
“Aaa..!”
“Kumbuka Hamza ni siku ya kesho saa nne kamili asubuhi heshimu muda”Baada ya mwanamke huyo kuongea maneno hayo palepale simu ilikatwa na kumfanya Hamza kushikwa na bumbuwazi akisahau kwamba anachelewa kwenda chuoni.
******
Maisha ya ajabu ni nini na tunawezaje kuyatumia kufanikiwa?
Maisha ya ajabu ni neno ambalo lina urejeo wa mambo mengi , lakini kwa ujumla linamaanisha mambo ya kuvutia na kushangaza ambayo tunakutana nayo maishani, mambo ya ajabu kama hayo ni kama vile kuangalia maporomoko ya maji ya umbali mrefu , uzuri wa mtoto anapotabasamu na mengine mengi.
Maisha ya ajabu yanaweza kutusaidia kufanikiwa kwa njia nyingi ikiwemo , kutupatia hali ya mshangao na udadisi , kutusaidia kuthamini mambo madogo madogo , kutuhamasisha kuwa wabunifu , kutuunganisha na wengine pamoja na kutupa matumaini mapya.
Zipo njia kadha wa kadha ambazo zinaweza kutusaidia kutumia maisha yetu ambayo yamejazwa na uajabu ili kufanikiwa ikiwemo: kutengeneza orodha ya mambo ya ajabu ambayo ni ya kukushangaza na kukuvutia , jaribu kutafuta uzoefu mpya nje na eneo la faraja(Comfort Zone),Kuwa na shukrani na shirikisha uzoefu wako kwa wengine.
“Haya ndio maneno yangu kwenu ambayo ni kama Bonus Point kwenu , niwatakie siku njema , Mono no aware.
“Paaa.. Paaah!!!
Ilikuwa kama kawaida Hamza aliguswa sana na maneno ya Profesa Singano ukiachana na namna maneno hayo yalivyomwingia na kuyaelewa lakini kwa wakati mmoja ni kama yaligusia kile ambacho amekutana nacho asubuhi ya leo.
Hamza tokea anatoka mahali anapoishi kuja chuoni alikuwa akiikumbka mara mbilimbili kauli ya kuhitajika kwenda kwenye usaili kwa ajili ya kupewa kazi ya kuwa Boyfriend feki.
“Hakika maisha na maajabu yake , lakini leo Profesa maneno yake yamenifanya nichukue maamuzi , lazima kesho niende kwenye huo usaili nikajionee mwenyewe”Aliwaza Hamza.
“Oya Mzee unawaza nini? , huna mpango wa kuondoka nini?”Sauti ilisikika nyuma ya Hamza na kumfanya ageuke na kukutana uso kwa uso na Alex muuza vyungu.
“Hamna ndio najiandaa kutoka hivyo”
“Haha,, Hamza una mawazo mengi sana , kila siku ambayo Profesa akimaliza kipindi chake wewe unaishia kushangaa”
“Mara nyingi namchukulia Profesa kama mchungaji pale anapokuhubiria juu ya jambo la Dhambi ambalo unalifanya, kwa urahisi ni kama Profesa anayagusa sana maisha yangu kwa ujumla”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Alex kuangua kicheko.
“Unajua nini braza ,Profesa Singano naona muda mwingi anapoteza muda wake tu lakini hakuna cha maana anachoongea na hilo sio kwangu tu nakuhakikishia ni wachache sana ambao wanaguswa na maneno yake , wengine wote wanapenda kumuona anavyoongea ili kucheka basi lakini sio ujumbe”Aliongea Alex na kumfanya Hamza asiweze kuongeza neno.
“Sio kawida yako kunitafuta wakati wa kumaliza kipindi kama huu kwa ninavyokujua sasa hivi ungekuwa na kundi la warembo kwenye gari yako mnaondoka”Aliongea Hamza.
“Upo vizuri mtu wangu , nimekufuata kwasababu nina mishe nataka msaada wako”
“Mishe gani?”
“Ni kazi nyepesi sana yenye malipo mazuri”
“Okey , nipe mchongo”
“Iko hivi leo nina oda za kupeleka vyungu sehemu mbalimbali na wafanyakazi niliokuwa nao ni wachache na hawawezi kumudu oda zote..”
“Nipo tayari, nishakuelewa unachomaanisha , wewe zungumzia kiasi cha pesa ambacho utanilipa “
“Elfu ishirini unaonaje kwa trip moja”Aliongea Alex na Hamza macho yalichanua , aliona ni dili zuri.
“Kama upo siriasi mimi nipo tayari kwa ajili ya kazi”
“Ndio maana nakukubali Mzee , huna tabia za kulemba lemba kwa kuchagua kazi , sasa sikia muda wa jioni jioni saa kumi ndio utaanza , kuna mfanyakazi wangu nitampa namba yako atakupigia na utafika maeneo ya uzalishaji na kisha utachukua mzigo na atakupa na Anuani wapi unapaswa kupeleka”Aliongea na Hamza hakuona tatizo , alikuwa na uhitaji wa pesa na kama kuna mtu alikuwa tayari kumlipa kiasi kidogo cha pesa kwa malipo ya kawaida aliona hana haja ya kukataa dili hilo.
Baada ya kuachana na Alex Hamza yeye hakuona haja ya kwenda nyumbani mapema hivyo , chuoni kulikuwa na Wife ya bure hivyo kutokana na mara nyingi kutokuwa na bando la kuosha aliona atumie muda huo kukaa chuoni hapo kupakua muvi na kwenda kuangalia getoni kwake.
 
SHETANI RUDISHA AKILI YA MKE WANGUMTUNZI: SINGANOJR.“The difference between ordinary and extraordinary is that little extra.”-Jimmy Johnson


TULIPOISHIA

“Oya Mzee unawaza nini? , huna mpango wa kuondoka nini?”Sauti ilisikika nyuma ya Hamza na kumfanya ageuke na kukutana uso kwa uso na Alex muuza vyungu.

“Hamna ndio najiandaa kutoka hivyo”

“Haha,, Hamza una mawazo mengi sana , kila siku ambayo Profesa akimaliza kipindi chake wewe unaishia kushangaa”

“Mara nyingi namchukulia Profesa kama mchungaji pale anapokuhubiria juu ya jambo la Dhambi ambalo unalifanya, kwa urahisi ni kama Profesa anayagusa sana maisha yangu kwa ujumla”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Alex kuangua kicheko.

“Unajua nini braza ,Profesa Singano naona muda mwingi anapoteza muda wake tu lakini hakuna cha maana anachoongea na hilo sio kwangu tu nakuhakikishia ni wachache sana ambao wanaguswa na maneno yake , wengine wote wanapenda kumuona anavyoongea ili kucheka basi lakini sio ujumbe”Aliongea Alex na kumfanya Hamza asiweze kuongeza neno.

“Sio kawida yako kunitafuta wakati wa kumaliza kipindi kama huu kwa ninavyokujua sasa hivi ungekuwa na kundi la warembo kwenye gari yako mnaondoka”Aliongea Hamza.

“Upo vizuri mtu wangu , nimekufuata kwasababu nina mishe nataka msaada wako”

“Mishe gani?”

“Ni kazi nyepesi sana yenye malipo mazuri”

“Okey , nipe mchongo”

“Iko hivi leo nina oda za kupeleka vyungu sehemu mbalimbali na wafanyakazi niliokuwa nao ni wachache na hawawezi kumudu oda zote..”

“Nipo tayari, nishakuelewa unachomaanisha , wewe zungumzia kiasi cha pesa ambacho utanilipa “

“Elfu ishirini unaonaje kwa trip moja”Aliongea Alex na Hamza macho yalichanua , aliona ni dili zuri.

“Kama upo siriasi mimi nipo tayari kwa ajili ya kazi”

“Ndio maana nakukubali Mzee , huna tabia za kulemba lemba kwa kuchagua kazi , sasa sikia muda wa jioni jioni saa kumi ndio utaanza , kuna mfanyakazi wangu nitampa namba yako atakupigia na utafika maeneo ya uzalishaji na kisha utachukua mzigo na atakupa na Anuani wapi unapaswa kupeleka”Aliongea na Hamza hakuona tatizo , alikuwa na uhitaji wa pesa na kama kuna mtu alikuwa tayari kumlipa kiasi kidogo cha pesa kwa malipo ya kawaida aliona hana haja ya kukataa dili hilo.

Baada ya kuachana na Alex Hamza yeye hakuona haja ya kwenda nyumbani mapema hivyo , chuoni kulikuwa na Wife ya bure hivyo kutokana na mara nyingi kutokuwa na bando la kuosha aliona atumie muda huo kukaa chuoni hapo kupakua muvi na kwenda kuangalia getoni kwake.
SEHEMU YA 05.

Muda wa jioni Hamza akiwa chuoni aliweza kupokea simu kutoka kwa mtu aliejitambulisha ni mfanyakazi wa Alex na Hamza mara baada ya kusikia utambulisho wake aliweza kumjua mara moja na palepale alipewa maagizo ambayo Hamza alionekana kuyaelewa na kisha simu ilikatwa.

Dakika chache tu alikuwa tayari ashapata daladala ambayo ilimpeleka moja kwa moja mpaka Mwenge mahali ambapo ndio alielekezwa kushuka.

Kutokana na kuwa mzoefu aliweza kutoka kituoni na kuchukua upande wa kulia kwake na kueleka moja kwa moja mpaka eneo husika.

Hamza alijikuta akishangaa mara baada ya kugundua kazi ya Alex haikuwa kazi ndogo , kwani ilikuwa ni kama Kiwanda.

Jambo hilo lilimshangaza , watu walikuwa wakimchukulia Alex wa kawaida kutokana na kazi yake , lakini Hamza mara baada ya kupita getini na kuingia ndani aligundua ilikuwa ni zaidi ya alivyofikiria , kwani kulikuwepo wafanyakazi wengi.

“Wewe ndio Hamza?”Aliuliza jamaa mmoja mwenye nywele ndeefu mara baada ya kumuona Hamza ana shangaa shangaa”

“Ndio Bro”

“Umefanya la maana kuja haraka maana kidogo tu usingenikuta hapa , nina oda ya kupeleka , njoo nikuonyeshe Mzigo chapu”Aliongea yule bwana huku wakipita wamama ambao walikuwa bize kutengeneza vyungu.

Kulikuwa na utengenezaji wa aina tofauti tofauti , kulikuwa na vyungu ambavyo vilikuwa maalumu kwa ajili ya kuwekea maua na urembo mwingine , kitu kingine ambacho Hamza alikuja kugundua ni kwamba kilichokuwa kikitengenezwa hapo sio vyungu tu.

“Bosi mzigo huu hapa utaupeleka kwenye hii Anuani”Aliongea yule bwana huku akimpatia Hamza boksi ambalo juu lilikuwa na Sticker ambayo mzigo ulipaswa kupelekwa.

“Malipo yanakuwaje baada ya hapa?”Aliuliza.

“Bosi hajakuambia?”

“Hamna tumekubaliana ni 20k ila hajaniambia utaratibu wa kunilipa upoje?”

“Samahani mkuu, iko hivi huu mzigo bado haujalipiwa ukishafikisha utakaguliwa na baada ya hapo utalipiwa bei yake ni laki moja na nusu na gharama ya usafirishaji utapewa hapo hapo”

“Laki moja na nusu!!?”Hamza alijikuta jicho likitoka na kujiuliza ni chungu cha aina gani ambacho kinauzwa laki moja na nusu

Yule bwana alijua mshangao wa Hamza lakini hakutaka kumtolea maelezo yoyote na alionekana kuwa na haraka kwani aliingia kwenye gari na kisha akaondoka.

Hamza alitaka kuuliza kuhusu nauli vipi , lakini alikuwa amechelewa na kuishia kuangalia boksi ambalo lipo chini limefungwa kwa namna ya kipekee..

Alikuwa na shauku ya kujua ni chungu cha aina gani ambayo kinaweza kuwa na bei ghali namna hio lakini asingeweza kufungua.

Baada ya kusoma Anuani ya mzigo unapopaswa kueleka aligundua ni Madale .

Hamza alijaribu kuchunguza mazingira yaliokuwepo hapo ndani na aliweza kugundua hakuna ambaye alikuwa akimwangalia , kulikuwa na vijana wengi pamoja na wamama waliokuwa bize kuteneneza vyungu lakini hawakumwangalia usoni , ni kama hawakujali uwepo wake.

Hamza alinyanyanyua lile boksi na aliona halikuwa zito sana , alitamani kutafuta mfuko kulifunga lakini ilikuwa ngumu kuingia kwenye mfuko wa kawaida labda kwenye kiroba lingefiti lakini kiroba chenyewe hakuwa nacho hivyo aliamua kubeba hivyohivyo na kutoka ndani ya eneo hilo na kwenda kusimama kituoni.

Kama kawaida watu wa jiji la Dar hawakuwa na habari na mtu kila mtu alikuwa bize na mambo yake na Hamza na yeye hakujali watu na kuendelea kusubiri usafiri.

Hamza wakati akiwa kituoni hapo aliona ndio maana Alex alimtajia pesa kubwa kwa ajili ya kusafirisha kwa awamu moja kumbe gharama ya chungu kimoja ilikuwa kubwa hivyo.

Dakika kadhaa tu akiwa amesimama kituoni gari iliweza kusimama na Hamza licha ya kuona gari hio ilikuwa imejaa sana aliingia moja kwa moja na kisha akaweka mzigo wake sehemu husika na kisha akasimama na safari ikaanza.

Muda wa saa kumi foleni ilikuwa kubwa mno kutokana na watu wengi ndio kwanza wanatoka kazini , hivyo ilimchukua dakika nyingi sana kusimama mpaka kufika eneo husika.

Jiji la Dar lilikuwa limeboresheka sana katika maswala ya anuani za nyumba , ilikuwa ukiingia mtandao kwenye ramani unaweza kuona kila nyumba hivyo haikumpa Hamza shida kutafuta nyumba ya mzigo unapopaswa kufikishiwa.

Baada ya kushuka katika kituo husika alianza kutembea kwa kufuatisha Ramani na alitembea kwa dakika kama kumi tu alikuja kusimama kwenye nyumba kubwa iliokuwa na geti rangi nyeusi ambalo lilikuwa limenakshiwa na madini ya shaba.

Hamza aliangalia kulia na kushoto katika maeneo hayo na alionyesha kuridhika , ijapokuwa kulikuwa na nyumba za kawaida ndani ya hilo eneo lakini nyumba nyingi zilionekana ni zile za kifahari na zenye bustani za kuvutia nje.

“Ngoo… ngooo , ngooo!!!”

Hamza aligonga mara tatu na kisha akasubiria kwa dakika nzima lakini hakukuwa na dalili yoyote ya kufunguliwa, na alijikuta akigonga tena kwa dakika nyingine lakini bado mlango haujafunguliwa na aliamua awamu hio kugonga kwa nguvu lakini kabla hata mkono wake haujagusana na geti kijimlango kidogo cha nyumba hio kilifunguliwa.

“Una shida gani?”

Sauti iliokuwa ya kibabe iliweza kusikika na Hamza kwa ufahamu wake wa haraka haraka alijua mtu huyo atakuwa mlinzi kwani hata rafudhi yake haikuwa ile ilionyooka katika kiswahili chake.

“Nimeleta Mzigo”Aliongea Hamza.

“Mzigo gani?”

“Chungu”

“Hapo pembeni yako unaona nini?”

“Pembeni wapi tena?”

“Kushoto kwako?”

“Sioni kitu?”Aliongea Hamza.

Ukweli ni kwamba wakati alipofika hapo aliweza kuona kitufe cha kengele lakini hakutaka kukigusa na aliamua kugonga geti na mlinzi huyo alivyokuwa akimuuliza alikuwa akijua alichokuwa akimaanisha.

“Acha ushamba basi , angalia pembeni yako hapo kuna kengele na Camera , bonyeza hiyo na kisha utasema shida yako”Aliongea kwa hasira na kisha alifunga kijidilisha na kumuacha Hamza kutoa tabasamu la uchungu

Hamza alijiamulia kubonyeza ile kengele mara mbili na palepale aliweza kusikia sauti kutoa ndani”

“Delivery!!”Aliongea

“Ok”

Sauti ya kike iliweza kusikika kutoka ndani na mara baada ya kusubiria kwa dakika kama mbili hivi mlango wa geti ulifunguliwa.

“Kijana unaweza kuingia”Aliongea Mlinzi na sasa Hamza aliweza kumuona yule mlinzi.

Ijapokuwa sauti yake haikuwa imekaa vizuri lakini kimuonekano alikuwa vizuri sana kuliko hata yeye kwa upande wa mavazi.

Hamza mara baada ya kuingia ndani alijikuta akishangazwa na mandhari nzuri pamoja na ufahari wa jengo ambalo lilikuwa mbele yake.

Mlinzi alimuonyeshea ishara Hamza kutembea kueleka upande wa kushoto na Hamza mara baada ya kuangalia upande ambao anaelekezwa ni kando ya bwana la kuogelea sehemu ambayo imejengwa kwa ajili ya mapumziko.

Hamza kila hatua aliokuwa akipiga kueleka hilo eneo mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda mno mpaka mwenyewe kujishangaa , ijapokuwa kiumbe alichokuwa akikiangalia mbele yake kilikuwa kimempa mgongo lakini utashi wake ulimwambia huyo mwanamke alikuwa mzuri sio kawaida.

Hamza alijiambia pengine anachanganyikiwa sana kila anapowaona wanawake warembo kwasababu ni muda mrefu hajakutana na mwanamke kimwili.

Ilikuwa ni kama akili yake ilivyomwambia kwani mara baada ya kufika katika hilo eneo aliweza kukutana na mwanamke ambaye alikuwa nusu uchi , ilionekana kabisa alikuwa akiogelea kwenye hilo bwawa na muda huo alikuwa amepumzika kwani hata mwili wake haukuwa umekauka maji.

Hamza kwa akili yae palepale alijua huyo sio mtu ambaye alimwitikia baada ya kubonyeza kitufe.

Hamza mara baada ya kufika mbele ya mwanamke yule akiwa ameshikilia boksi lake mapigo yake ya moyo yalionekana kudunda sana.

Alikuwa ni msichana mweupe mwembamba kiasi ambaye alikuwa na ngozi laini mno na nywele zake ndefu, alikuwa na macho madogo ambayo yaliendana na namna uso wake ulivyoumbwa.

Ijapokuwa mrembo huyo hakuwa akimfikia yule msichana aliefahamika kwa jina la Tresha Noah ambaye alikutana nae kule kwenye jengo la Apartment la Dosam Homes lakini itoshe kusema huyo alikuwa mrembo na wakuvutia zaidi.

Katika maisha ya Hamza alishakutana na wanawake wa aina nyingi , kuna wanawake ambao alikutana nao licha ya kwamba walikuwa na uzuri wa aina yake lakini hawakuwa wakivutia kingono , kuna wanawake wengine ambao alikutana nao licha ya kwamba hawakuwa na muonekanno wa kirembo lakini walikuwa wakivutia mno kingono(Sexy), hizo ni aina mbili ambazo alikutana nazo Hamza , ijapokuwa mrembo huyo hakuwa mzuri sana lakini alikuwa na umbo ambalo linavutia kingono sana, yaani ni aina ya wanawake ambao ukimuona tu unawaza kufanya mapenzi.

“You are Hamza right?”Aliuliza yule mwanamke na sauti yake ilimuacha Hamza hoi.

“Yes.,.. yess”Alijibu kwa kubabaika.

“Okey nimepewa taarifa zako na Alex ,unaweza kufungua nithibitishe mzigo”Aliongea yule mwanamke , hakuwa na sura ya dharau wala ya ukarimu yaani alikuwa katikati huku akionekana kumkagua Hamza.

Hamza hicho ndio kitu pekee ambacho alikuwa akitaka kufanya , alikuwa na shauku ya kutaka kujua kwanini chungu hicho kilikuwa kikiuzwa pesa nyingi sana kuliko uhalisia.

Ilimchukua dakika chache sana kwa Hamza kufungua ndani , ijapokuwa kwa mtu wa kawaida angehitaji kisu kukata hizo gundi lakini Hamza hakuhitaji kisu na namna ambavyo alifungua ilimshangaza kudogo yule mwanadada lakini hakuongea chochote zaidi ya kubakia kimya.

Hamza mara baada ya kufungua lile boksi macho yake ni kama yamesaliti matarajio yake , ukiachana na namna ufungashaji wa chungu hicho ulivyo lakini hakikuwa na muonekano ule wa kimaajabu , kilikuwa chungu kama chungu ambacho muonekano wake ulikuwa wa kawaida sana , vilikuwa vyungu kama vile vya kitamaduni ambavyo wamama wengi hupikia.

Jambo hili lilimfanya Hamza kushangaa na kujiuliza nini kinaendelea , alijaribu kuangalia ndani yake kwani mwanzo alijua pengine kuna madawa ya kulevya kwenye hilo boksi lakini hakukuwa na kitu chochote cha kushangaza zaidi ya chungu.

“Kaka , inaonekana hii ni mara yako ya kwanza kufanya Delivery”

“Kwanini?”

“Unashangaa sana”Aliongea yule msichana huku akisimama na kumpokea Hamza kile chungu na kuanza kukichunguza kwa dakika kadhaa na mara baada ya kuridhika alitoa tabasamu na kumpatia Hamza kukirudisha kwenye boksi.

“Wait here”

Aliongea huku akibeba kile chungu na kutembea kuelekea upande mbele wa jengo hilo sehemu ambayo kuna mlango wa kuingilia ndani.

Hamza macho yake yalikuwa yakiangalia mpwito wa makalio ya mrembo huyo ambaye hakuwa akijali kama amevalia kijichupi tu na kuingia hadi ndani.

“Kuna watu wanafaidi aisee”Alijiwazia Hamza mara baada ya mrembo yule kutokomea kwenye jumba hilo ambalo lilikuwa na ghorofa mbili kwenda juu.

Hamza alitumia dakika hio kujaribu kukagua mazingira kwa haraka haraka na ile anagueza sura yake macho yake yalikutana na mlinzi aliekuwa akimwangalia na baada ya kukutanisha nae macho alionekana kama mtu ambaye alikuwa akimwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida na Hamza alishindwa kuelewa lakini aliamua kupotezea na kugeuza macho yake sehemu nyingine.

Baada ya dakika kama sita hivi mwanamke yule alirudi huku awamu hio akiwa tofauti na alivyokuwa , alikuwa amejisitiri kwa kuvalia vazi refu la kitambaa cha hariri(Silk Duster) ambalo lilikuwa na vishikizo huku kichwani akiwa amevaa Bonnet.

Alikuwa hajalifunga vishikizo vyake na kumfanya bado nguo yake ya ndani kuonekana.

“Hesabu hizi?”Aliongea yule mwanamke huku awamu hii akiweka tabasamu na kumfanya Hamza kushangaa kidogo na kujiuliza mwanzoni hakuwa na mwonekano wa kusomeka lakini sasa hivi alikuwa akitabasamu.

Hamza alihesabu kwa haraka sana zile hela na baada ya kumaliza aligundua ni Shilingi laki moja na tisini.

“Hela iliozidi ni kama ofa Hamza , naamini utakuwa mwaminifu kuniletea mzigo wangu mwingine kila nitakapohitaji”Aliongea huku akiweka tabasamu na kuufanya uzuri wake kuzidi kuongezeka.

“Asante sana”Aliongea Hamza , ijapokua hakuelewa mwanamke huyo anamaanisha nini kumwambia anategemea kuletewa mzigo mwingine na yeye lakini hakutaka kuuliza.

Hamza mara baada ya kuaga aliweza kutoka nje ya geti huku bado akiwa na maswali mengi sana , swali lake kubwa ni kwanini chungu cha kawaida kama kile mwanamke huyo akakinunua kwa bei ghali,

Ilikuwa ni ajabu ambayo chungu cha kawaida ambacho kilikuwa kikiuzwa sokoni kwa shilingi elfu tatu kununuliwa kwa zaidi ya laki mbili.

Hamza alijiambia hata kama watu hao ni matajiri lakini bei hio ni kubwa sana kiasi kwamba haina uhalisia , akili yake palepale ilimwambia pengine kuna kitu cha ziada kwenye kile chungu lakini hakujua, kwani kila kitu hakikumwingia akilini.

Ijapokuwa alikuwa akijua madawa ya kulevya yalikuwa yakisafirishwa kwa mbinu nyingi lakini ilikuwa ngumu madawa kusafirishwa kwenye kile chungu, lakini hata hivyo hivyo hakutaka kufikiria zaidi.

Wakati akianza kutembea kukisogelea kituo cha daladala simu yake ilianza kuita na alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Alex na palepale alipokea.

“Hahaha.. Bro kazi nzuri”Sauti ya Alex ilisikika bila hata ya salamu.

“Nimeleta mzigo tu sehemu husika , ni swala ambalo mtu yoyote anaweza kufanya”

“Hapana Bro , ni kweli linaweza kuonekana swala la kawaida lakini sio la kawaida kama unavyoona wewe”

“Unamaanisha nini?”

“Tutaongea usijali , ila nikuambie mwanangu sijui niseme una bahati au kuna siri kuhusu inayoendelea ,ila kwanzia sasa hivi utahusika na kumpelekea huyo demu kila atakapohitaji mzigo , amenipigia simu na kusema lazima iwe wewe”Aliongea Alex na kumfanya Hamza kusimama kwanza.

“Alex unajua mambo mengi umeniacha hewani , nina maswali mengi sana , itoshe kusema leo ni siku ambayo imenifanya kushangaa sana”

“Najua bro lazima utakuwa na maswali ila utajua , kwasasa elewa kwamba utakuwa unampelekea huyo manzi mzigo wake na malipo yatakuwa mazuri”Aliongea Alex na kumfanya Hamza kufikiria kidogo.

“Tunakutana wapi nikupe hela ya mzigo”

“Haina haja mzee unaweza kwenda nayo, hio chukulia kama pesa ya kujikimu kwa mwanzo wa kazi yako”Aliongea na palepale simu ilikatwa na kumfanya Hamza kuzidi kuchanganyikiwa

Kitu kingine kilichomfanya kuchanganyikiwa ni kama Alex alikuwa akiongea kinafiki ila hakutaka kuwaza sana kuhusu Alex bali aliwazia vyungu.

“Kuna siri gani juu ya hivi vyungu..?”

Ndio swali ambalo liliibuka kwenye kichwa chake na hali ya kutaka kuanza udadisi ilimvaa palepale , Hamza alijikuta akitengeneza Scenerio mbalimbali kwenye kichwa chake kuhusu vyungu ambavyo anatengeneza Alex.

Ukweli ni kwamba hata yeye aliona kuna kitu ambacho sio cha kawaida tokea dakika ambayo aliingiza mguu katika kiwanda cha Alex cha utengenezaji vyungu.

Hamza alianza kufikiria mbali zaidi na kujiambia hili swala halikuwa la kawaida tokea siku ambayo anaisikia Alex alikuwa muuza vyungu , kulikuwa na wafanyabiashara wengi nchini ambao wanatengeneza vyungu iweje Alex biashara hio imtoe na kuwa na maisha mazuri namna hio.

Safari yake ya kupata majibu ni kama ndio imeanza rasmi , kwanza kabisa alishajua aina ya vyungu ambavyo vilikuwa vikitengenezwa lakini pia alijua uthamani wa vyungu vingine , kilichokuwa kimebakia ni kujua nini siri iliokuwemo kwenye vyungu hivyo.

Swali tu la kumshangaza Hamza ni kwamba kwanini maisha yake yamejaa mshangao tokea siku anajitambua.

******

Saa kumi na mbili kamili za jioni Hamza alikuwa eneo la Mwenge , ijapokuwa haikuwa mwisho wa safari yake lakini aliamua kushukia hapo huku akiwa na wazo moja akilini na hio yote ni kutokana na kuwa na pesa nyingi mfukoni.

Hamza mara baada ya kushuka kituoni alivuka barabara upande mwingine na kisha akaingia kwenye maduka ya nguo, alikuwa na wazo la kununua nguo kwa ajili ya kwenda kwenye usaili siku ya kesho.

Ijapokuwa kwake ilikuwa kichekesho kwenda kwenye usaili huo kutokana na aina ya kazi yenyewe lakini hakutaka kudharau hata kidogo , kitendo cha kupigiwa simu asubuhi kilimwaminisha yoyote ambaye alituma lile tangazo alikuwa siriasi , lakini shauku yake nyingine ni kwamba kama mtu huyo alikuwa siriasi na kuamua kumlipa mtu zaidi ya laki saba wa ajili ya magizo tu basi ilimaanisha kwamba ni mwanamke mwenye pesa , lakini vilevile huenda kuna sababu ya ziada.

Hamza moja kwa moja aliingia kwenye jengo la Dosam Shopping Mall . hili ni jengo ambalo alikuwa akitamani sana kuingia siku moja kwa ajili ya kununua nguo , lakini kutokana na kukosa pesa kila siku alikuwa akiliogopa kama ukoma,lakini siku hio alikuwa na zaidi ya laki na nusu mfukoni hivyo aliamua kuzitumia katika manunuzi ya nguo kadhaa na kisha baada ya hapo angeenda saluni kuweka muonekano wake vizuri.

Sifa kubwa ya maduka ya Dosam ambayo yametapakaa nchi nzima ni nguo zake kuwa bora lakini kwa bei nafuu kabisa , ilikuwa ni tofati kabisa na madumka ambayo yalikuuwa yakipantikana mlimani City na kwingineko.

Kwa mfano Mlimani unaweza kukuta nguo inauzwa bei lakini ubora wake ukafanana na nguo ambayo inauzwa katika maduka ya Dosam, na inasemekana tokea kampuni ya Dosam kufungua maduka ya nguo biashara nyingi zimefirisika sana kutokana na mauzo kupungua.

Sifa nyingine katika maduka haya ni huduma ya viwango vya juu sana , yaani hawakujali muonekano wa mteja ambaye alikuwa akifika kufanya manunuzi katika maduka yao, wao walimjali kila aina ya mteja na kuwakwa daraja sawa na muda wote walikuwa ni watu wenye tabasamu usoni na wangekusaidia katika machaguzi ya nguo mpaka pale utakaporidhika.

Jambo hili lilimfanya Hamza kukubali sana mmiliki wa kampuni ya Dosam Global,

Ukweli ni kwamba inasemekana kampuni ya Dosam mmiliki wake ni mwanamke tena pengine ni kosa kusema mwanamke bali ikawa sahihi kusema ni Msichana ndio mmiliki.

Mwanzoni kampuni hii ilimilikiwa na Mzee Lasuli Dosam mwenywe na mara baada ya kufariki inasemekana usimamizi na urithi wa makampuni yote ulienda kwa mjukuu wake kike.

Uzushi unaenda mbali zaidi na kusema kwamba msichana huyo ambaye ni mmiliki alikuwa ni mrembo haswa , pengine zaidi ya neno lenyewe la Urembo lakini pia kwa wakati mmoja alionekana kuwa ni mwenye akili nyingi , baadhi ya watu walikuwa wakimtaja kama kiumbe kutoka sayari nyingine.

Jina hilo liliibka kutokana na kwamba aliweza kufanya biashara nyingi katika mataifa mbalimbali kupata hasara kubwa kutokana na mbinu zake za kibiashara tokea kupewa uongozi wa kampuni , vyombo mbalimbali vya habari vishawahi kumwandika kuhusu mwanamke huyo.

Hamza yote hayo alikuwa akiyajua , isitoshe alikuwa ni mtu mpenda mitandao ya kijamii hivyo ilikuwa ni rahisi kwake kukutana na taarifa ambazo zinamzungumzia , ukweli ni kwamba kukutana na taarifa hizo kwenye mitandao sio jambo la bahati mbaya , ukweli ni kwamba kuna taarufa zake nyingi , kwa mfano tu katika mtandao wa kijamii wa JamiiForum umejaa mada zinazomzunguzia mmiliki wa kampuni ya Dosam Global mara mia nne tokea kupewa uongozi , sio hivyo tu majarida makubwa duniani na yenywe yamemzungumzia mara nyingi sana na kufanya mahojiano nae.

Ajabu ni kwamba katika kila mahojiano ambayo yalifanyika inasemekana mwanamke huyo alikataa kupigwa picha.

Kuna wengine wanasema mrembo huyo alikuwa mbaya wa sura ndio maana hakutaka kuonekana lakini wale ambao wameenda kumfanyia mahojiano walisema alikuwa mrembo wa sura na hata wale ambao walikuwa wakifanya kazi katika kampuni hio walikuwa wakisema ni mrembo wa sura.

Hamza alijikuta akiwaza kila aina ya mada ambazo alizisoma mtandaoni kuhusu mmiliki wa kampuni ya Dosam na kilichomfanya kukumbuka taarifa hizo ni siku hio mara baada ya kuingia kwenye duka hilo.

“Kaka hii itakufaa sana , kwanza kabisa inaendana na mwonekano wako wa mwili kwanzia rangi yako mpaka urefu na unene wako , kitu kimoja ambacho kitakufanya upendeze zaidi ni kunyoa nwele kwa mtindo huu”Aliongea mwanamke mrembo sana huku akimuonyesha Hamza vazi maalumu ambalo amechagua.

Hamza aliweza kushika kishikwambi huku akiangalia mtindo wa nywele ambao mfanyakazi wa eneo hilo amependekeza na aliishia kutoa tabasamu.

“Sijazoea kunyoa hivi dada”AliuongeaHamza.

Mtindo wa nywele ambao aliokuwa akiangalia kwake ni kama haukukaa kimaadili, pengine sio kwamba mtindo wenyewe haukukaa kimadili lakini kutokana na sheria zake au pengine aina ya maisha aliokulia ndio maana aliona ni mtindo ambao haukukaa kimaadili.

Ilikuwa ni kama vile wale wazee waliozaliwa miaka ya sitini na sabini uwaambie wanyoe kiduku ukweli ni kwamba hawatokuelewa, lakini sasa kidogo ilishangaza kwa Hamza kwani alionekana ni kijana kabisa ambaye hata miaka therathini hajafikisha.

Yule mfanyakazi wa kike mrembo aliishia kushangaa kidogo lakini aliubadilisha mshangao wake na tabasamu.

“Kaka niamini , huu ni mtindo ambao utamfanya mwanamke yoyote yule kukupenda , kwanza wewe ni handsome na kwa muonekano wako ni kama vile Justin Timberlake, hivyo staili yako ya nwele inakupasa kufanana…..”

Hamza kwa namna ambavyo mwanamke huyu alivyokuwa akiongea ungeweza kuamini na kujisikia vizuri lakini kilichomfanya kutokuamini maneno yake ni kwamba pembeni yake kulikuwa na bwana ambaye alikuwa ni mweusi sana na kichwa kama kibuyu aliekuwa pia akihudumiwa , ukweli katika maisha yake hakupenda kujifanananisha lakini alisema ijapokuwa yeye hakuwa akijiona Handsome lakini huyo bwana aliekuwa pembeni yake alikuwa na sura ngumu mno, ndio mwanaume hasifiwi kuwa na sura nzuri lakini kilichompa mshangao ni namna ambavyo mfanyakazi alivyokuwa akimpamba kwa kumwambia alikuwa na sura nzuri na kichwa kizuri, hivyo ilikuwa ni ‘redflag’ ya kuona hata yeye alikuwa akipambwa tu kinafiki nje ya uhalisia wa muonekano wake.

Iliimchukua kama nusu saa kuhudumiwa na kisha alipewa nguo zake na kutoka, alikuwa amenunua suruali mpya , Jeans pamoja na viatu na ajabu ni kwamba hakuwa amelipa pesa nyingi, kilichokuwa kimebakia ni kwenda Saluni na kuweka nywele zake sawa kwa ajili ya maandalizi ya kesho.

Hamza wakati akitoka kwenye Lift alijikuta akijichekea , yaani kwa namna ambavyo alikuwa akijiandaa ni kama vile anakwenda kukutana na mchumba au anaenda kwenye ‘Blind date’, alicheka kutokana na kwamba siku kadhaa zilizopita wakati wa kumtongoza mwanamke mrembo kama Anitha hakujali kabisa muonekano wake zaidi ya hisia zake, tena anakumbuka ile siku shati lake lilikuwa limechafuliwa na juisi ya matunda wakati akiwa kwenye daladala na kutengeneza doa..

Hamza alitamani kughairisha kwenda saluni lakini kuna roho ilikuwa ikimwambia ‘ingia saluni bro upendeze acha uchafu’, pengine mwanamke unaekwenda kukutana nae ni zaidi ya Anitha.

Hamza mwenyewe alishangaa na kujiuliza hio sauti inatoka wapi , lakini aliamua kuitii na kujiambia pengine ni roho mtakatifu , lakini mara baada ya kuingiwa na neno Roho mtakafitu alipotezea na kujiambia kwanza hakuelewa yeye ni dini gani hivyo aliamua kupotezea kile anachofikiria na kuamua kufuata utashi wake unakomwelekeza.

“Bro unanyoa staili gani?”Aliuliza kinyozi mara baada ya Hamza kukalishwa kwenye kiti na kinyozi kumaliza maandalizi yake.

Hamza alifikiria ni staili gani anyoe , au apige para..”Alijikuta akikosa majibu na palepale macho yake yalitua kwenye picha ambazo zilikuwa na vichwa ambavyo vimenyolewa kwa staili tofauti tofauti.

Baada ya kuangalia ni staili gani ingemfaaa palepale alijikuta akiishia kwenye staili ambayo alionyeshwa muda mchache uliopita na yule muuza nguo,.

“Bro hio staili ni nzuri na inaendana na nywele zako lakini kidogo itakugharimu, kwani ili upendeze utahitajika na kuosha pia na kupakwa dawa”Aliongea kinyozi akiwa na wasiwasi Hamza asingeweza kumdumu bei.

“Ni shilingi ngapi jumla?”

“Kwa kila kitu nilichokutajia jumla yake ni elfu kumi na tano tu?”Aliongea .

“Ni bei kubwa ndio ila nitalipia”Aliongea Hamza na yule bwana alimwangalia kidogo na kisha akaanza kupiga kazi,

Hamza hakuwa mwafrika orijinal bali alikuwa ni chotara , mchanganyiko wa Mwafrika na mzungu hivyo nywele zake zilikuwa zimekaa kizungu pia japo rangi yake ilikuwa imefubaa kidogo kupoteza ile hali ya uzungu yaani kwa maneno marahisi ni kwamba uzungu wake umeathiriwa na rangi ya kiafrika.

Zilipita dakika chache tu kama nusu saa hivi kinyozi alikuwa ashamaliza kumuweka Hamza sawa upande wa nwele na alitakiwa kuweka dawa pamoja na kuoshwa na kukaushwa na hakuwa na hiyana kufuata maelekezo kutokana na kwamba ndio mwenyewe aliamua kuyavulia maji nguo hivyo hakuwa na budi kuyaoga.

Baada ya lisaa lizima aliweza kusafishwa vizuri na alipewa na ofa ya kusafishewa uso na Scrub .

“Edmund naelekea nyumbani , bado hujamaliza tu?”Sauti ya kike iliweza kusikika katika Saluni ambayo Hamza anapunguza nywele.

“Leila nisuburi kuna bwana anamalizia kukaushwa nataka nione kama hana kasoro tuondoke”Aliongea kijana huyo na kumfanya Leila kuvuta pumzi na kisha kwenda kukaa kwenye sofa.

“Zamu yako ishaisha , leo mapema sana mpenzi”Aliongea Edmund.

“Bosi katoa maagizo kila mfanyakazi anaefikia malengo ya mauzo kwa siku anaweza kuondoka hata kama ni mchana”Alijibu na kumfanya Edmund kutingisha kichwa huku akichomoa simu yake chaji.

Dakika ileile mlango wa chumba cha wanaooshwa kwenye saluni hio kilifunguliwa na Hamza aliweza kutoka akiwa anawaka hatari na kumfanya yule mdada aliekuwa ameketi kwenye Sofa kupigwa na mshangao.

“Kaka nilikuambia hio staili ya nywele itakufaa , jamani hebu muone alivyopendeza”

Msichana Leila alikuwa ndio aliemhudumia Hamza katika kununua mavazi na aliweza kumtambua Hamza mara baada ya kumuona.

“Leila unamjua?”

“Yeah mimi ndio nilimuelekeza kuja hapa”Aliongea huku akimwangalia Hamza kwa macho ya kurembua na kumfanya Edmund kuona wivu.

Ukweli hata Hamza mara baada ya kujiangalia kwenye kioo alijiona kabisa amebadilika , ijapokuwa bado alikuwa na mavazi yake yaleyale lakini aliamini kama atavaa alionunua basi atakuwa ni mtu mwingine kabisa, aliishia kutoa tabasamu kwa kujikubali na kujiambia yeye kumbe ni Hamdsome aliekosea matunzo.

“Bro naona umekaa sawa sasa , unaweza kulipa sasa , nilikuwa nikikusubiria wewe tu”Aliongea Edmund huku akimkatisha Hamza ambaye alikuwa akijiangalia kwenye kioo pasipo ya kuridhika.

“Okey ngoja nilipe”Aliongea na palepale aliingiza mkono mfukoni na kutoa pesa nyekundu mbili na kisha kumpatia”

“Sister asante kwa kupendekeza hii staili ya kunyoa , chenchi inayobakia ni shukrani yangu kwako”Aliongea Hamza huku akitoa tabasamu na palepale alimkonyeza Leila na kuchukua mifuko yake na kutoka.

“Broo….!!”Edmund alitaka kuongea neno lakini palepale Leila aliekuwa akimwangalia Hamza kwa macho ya kurembua alimpa ishara ya kufunga mdomo wake.

Siku iliofuata Hamza hakuwa na ratiba za chuo kabisa mpaka jumatatu, yaani siku hio ilikuwa ni Ijumaa na kwa kozi aliokuwa akisomea ni kama wikiendi ndio imeanza rasmi.

Usiku hakuwa amelala kabisa , alikuwa na mawazo mengii, kwanza aliwaza sana kuhusu mtu anaefahamika kwa jina la Mzee mtu ambaye hakuwa akimjua licha ya kwamba amehusika katika maisha yake kwa kiasi kikubwa , aliwaza namna ya kumfahamu Mzee ni nani na kwanini alikuwa akimtafuta nyakati za usiku , aliwaza mambo mengi kuhusu mzee na kujijengea picha katika akili yake na kujiambia pengine Mzee ni mtu mzito serikalini .

Mawazo ya namna hio yalimjia kutokana na maisha ambayo amekulia kulingana na maagizo ambayo Mzee alitaka awe.

Yaani kwa maneno marahisi ni kwamba mpaka wakati huo Hamza hakuwa ameyaishi maisha yake , ni kama maisha aliokuwa akiishi ni kwa ajili ya Mzee kwani ndio aliekuwa akimwambia afanye hivi na vile na yeye kutii.

Alikumbuka siku ambayo hakutii maagizo ya Mzee na kilichomkuta mpaka siku hio na umri wake huo hajawahi kusahau , sasa kutokana na tukio hilo ambalo lilimtokea ilimfanya kuamini pengine mzee ni mtu mkubwa sana serikalini , ukweli ni kwamba alikuwa na mawazo mengi kuhusu Mzee.

“Kama mzee hataki kujitokeza kwangu mimi nitajitokeza mbele yake uwezo huo ninao”

Aliongea Hamza baada ya kuwaza , alionekana ameamua mwenyewe katika kichwa chake na kujiambia kama mtu huyo anaemtambua kwa jina moja tu la Mzee asipojitokeza kwake basi yeye atajitokeza kwake ,. Hakujua ni kwa namna gani ambavyo angemfahamu Mzee lakini alijiambia kutokana na uwezo wake basi lazima amfahamu mzee .

Hamza hakuwaza tu kuhusu Mzee pia aliwaza kazi ya Alex ya utengenezaji vyungu namna ambavyo ilionekana kumtajirisha nje ya uhalisia wa biashara wenyewe , alikuwa na shauku ya kutaka kujua kilichopo nyuma ya vyungu vile ni nini, kuna hali ilikuwa ikimwambia pengine ni njia nyingine ya usafirishaji madawa lakini alipingana na mawazo yake na akili yake ilimwambia kabisa pengine ni kitu kingine kabisa ambacho hajawahi kukifikiria kwenye maisha yake, kutokana na mawazo mengi alijiambia pia hilo ni swala ambalo atalitafutia ukweli.

Baada ya kuoga vizuri na kujiandaa kwa kuvaa mavazi yake mapya na viatu, licha ya kwamba hakuwa na kioo lakini aliamini alikuwa amependeza haswa.

Usaili kwa maelekezo ya mwanamke kwenye simu alimwambia ni saa nne asubuhi katika hoteli ya Dosam V

Hamza alikuwa akijua hoteli hio vizuri kwani ilikuwa ni hoteli maarufu na yenye jengo refu kwenda juu ndani ya jiji lote la Dar es salaam , pengine asilimia hamsini ya watanzania wote walikuwa wakiijua hoteli hio kwani matamasha mengi hufanyikia hapo, hata vikao vya waandishi wa habari hufanyikia ndani ya hoteli hio.

Siku hio pengine ndio inakuwa mara yake ya kwanza kuingia katika hio hoteli,lakini licha ya hivyo hakuonekana na wasiwasi kabisa.

Hakutaka hata kujihangaisha na maswala ya nchi asubuhi hio na alijiambia atajua mbele kwa mbele.

Mara baada ya kutoka nje ya eneo hilo la uswahilini wanawake na wanaume walikuwa wakimkodolea macho kwa mshangao mkubwa.

Ukweli ni kwamba muoenknao wa Hamza ulikuwa hauendani kabisa na maeneo hayo ya uswahilini , kitendo cha kuchanganya rangi ya mzungu na mwafrika ilikua ni kama sababu kubwa ya kumuona Hamza sio wa kawaida.

Hata asubuhi hio watu wengi sio kama walikuwa wakimwangalia kutokana na kupendeza kwake bali ni kwamba walikuwa wakimwangalia huku wakijiambia moyoni Hamza amerudi katika uhalisia wake na maisha ambayo alikuwa akiyaishi hapo na familia hizo ni ya magizo tu.

“Niliwaambia mimi , hakuna mtu mzungu akawa masikini hivi”Aliongea mmoja ya viijana walioamkia kucheza pooltable.

“Juma uko sahihi , hata mimi kwasasa nakuunga mkono , jamaa hakuwa mwenzetu kabisa, ule upole wake ulikuwa ukificha mambo mengi”Alichangia mwingine. Na stori juu ya Hamza hazikuishia kwa wacheza pooltable tu hata wanawake waliokuwa wakiuza vitafunwa nje ya vibaraza vya nyumba zao walikuwa wakimzungumzia Hamza.

Hamza kutokana na watu wengi kumshangaa kwake ilitosha kumwambia kwamba alikuwa amependeza.

Naam ni saa tatu na nusu Hamza aliweza kufika kandokando ya bahari ya Hindi nje ya geti la kuingilia katika hoteli ya Dosam.

Tofauti ya Hamza na wageni ambao walikuwa wakiingia ndani ya hoteli hio ni kwamba yeye alishuka na basi la mwendokasi lakini wageni wengine wote aidha walifika wakiwa kwenye gari binafsi au waliletwa hapo na Uber , Bolt na magari mengine yanayofanya huduma ya Taxing,

Licha ya hivyo swala hilo halikumpa unyonge sana Hamza , pengine kwa watu waliokuwa wakimwangalia wangesema labda Hamza alikuwa amejipa uzoefu mwingine wa kupanda magari ya abiria.

Mwonekano wake ulimbeba,alikuwa ni mtanashati mno, Hamza alikuwa ni mwanaume mrefu kwenda hewani , mwenye mwili ambao umejengeka kimazoezi akiwa na weupe wa kuchanganya rangi na macho yake ambayo yana kiini ambacho hakikuwa cheusi sana kama waafrika wengi , pengine uzungu wake ulionekana zaidi machoni kuliko sehemu yoyote ya mwili lakini hata hivyo ilikuwa kosa kumuita Mzungu.

Katika mavazi yake aliovaa kitu pekee alichokosa ilikuwa ni saa tu mkononi , pengine ingemfanya kuonekana Handsome zaidi lakini hata hivyo bado alionekana kupendeza.

Hamza alitembea kwa kujiamini kana kwamba alikuwa ni mzoefu kabisa wa eneo hilo.

“Ni muda mrefu sana nimejitenga na maeneo ya namna hii , nadhani ni mwanzo wa mimi kurudi kwenye maisha yangu”Alijiwazia Hamza huku akiongea kauli ambayo kidogo inachanganya.

“Hello!, nina miadi na mtu ndani ya hii hoteli?”Aliongea Hamza mara baada ya kufika katika Front desk.

“Karibu sana kaka , nitajie jina la mgeni unaetaka kukutana katika hoteli yetu tafadhari”Aliongea yule mwanadada na kumfanya Hamza kuwaza kidogo , ukweli ni kwamba hakuwa akijua jina lake kamili na aliambiwa tu kufika ndani ya hoteli hio muda wa saa nne.

Wakati akijiuliza ni jina gani anapaswa kutaja palepale simu yake ilianza kuita na aliitoa haraka haraka na kuangalia jina la mpigaji na alitoa tabasmau na kumwangalia yule mrembo wa mapokezi akimpa ishara kwamba anapiga.

Hamza aligeukia upande mwingine ili kuongea na simu lakini macho yake yalitua kwa mwanamke mrembo sana ambaye alikuwa akisogea katika dawati la eneo la mapokezi.

“Hello Mr , uko wapi unakumbuka miadi ni saa nne kamili?”Sauti ilisikika upande wa pili lakini wakati huo macho ya Hamza yalikuwa kwa mwanamke aliekuwa akitembea kimadaha kusogelea upande wake.

“Nipo eneo la mapokezi ndani ya hoteli ya Dosam”Aliongea Hamza na palepale yule mwanamke alisimama huku akitoa simu yake sikioni na kuangalia mbele yake na palepale alionekana kugundua kitu na haikuwa kwake tu hata kwa Hamza mwenyewe alionekana kugundua mtu aliekuwa akiongea nae kwa simu ni mwanamke aliekuwa mbele yake.

Sasa tofatui ni kwamba Hamza mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda mno kutokana na kushangaa urembo wa mwanamke ambaye alikuwa akimsogelea huku akiwa na uso uliopambwa tabasamu.

Hamza ni kama hakuamini kama huyo ndio mwanamke ambaye alikuwa akienda kuonana nae.

Kuhusu yule mwanamke hakuonyesha mshangao wowote wa Hamza , yaani ni kama Hamza alionekana wa kawaida sana na mara baada ya kumfikia alinyoosha mkono kwa ishara ya kusalimia.SEHEMU YA 06.

Wasichana wawili ambao walikuwa eneo la mapokezi kidogo walionyesha kukosa utulivu mara baada ya kumuona mwanamke alievalia suti akisogea upande wao na walijua pengine alikuwa akiwasogelea lakini walijikuta wakishangaa mara baada ya kumuona mwanamke yule akisimama mbele ya Hamza na kunyoosha mkono.

“I Suppose wewe ndio Hamza right!!?”Aliuliza yule mwanamke akiwa na tabasamu usoni.

“Yes ndio mimi Hamza Mzee”Aliongea Hamza huku akionyesha kukosa utulivu kiasi na kunyoosha mkono wake kusalimiana nae.

Wakati wa kushikana mkono na yule mwanamke alihisi ni kama kuna shoti za umeme zinampiga kwani zilianzia mkononi na kwenda kichwani kutoa mawasiliano kama ameshikana na kitu kisichokuwa cha kawaida na baada ya pale taarifa zilitumwa kwenye moyo kwa ajili ya kuongeza msukumo wa damu kuelekea kiwiliwili cha chini na ghafla tu kiungo cha uzazi cha Hamza kilianza kusisimka.

Muunganiko wa mwili ulikuwa ni wa ajabu sana na pengine Mungu katika kazi aliopatia ni kuumba kiumbe binadamu.

Mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa ni mweupe wa wastani, mrefu kiasi mwenye mwili uliojipanga huku ngozi yake ikiwa ni kama vile imetengenezwa , itoshe kusema katika wanawake ambao Hamza alishawaona tokea afike jijini Dar es salaam huyo ndio mwanamke wa kwanza kwa uzuri , Melissa mpenzi wake Amiri alijiambia tupilia kule , Tresha Noah msichana alieambiwa alikuwa ametengenezwa muonekano wake tupilia kule , Anitha hakutaka hata kuongea zaidi ya kutamani kusonya.

“Mr Hamza!, naitwa Prisila Singano Afisa mkuu wa idara ya Rasilimali watu kampuni ya Dosam, mimi ndio niliekupigia simu nadhani sauti yangu hujaisahau”Aliongea kwa mapozi na kumfanya Hamza kuzidi kupagawa , hakuamini huyu ndio mwanamke ambaye alikuwa akitafuta mchumba wa maigizo.

‘Nimefurahi kukufahamu mrembo Prisila Singano , lakini naomba kuuliza una undugu na Profesa Stephano Singano?”Alongea Hamza huku akiwa anajiamini kiasi kwamba kama unamjua ungesema hio hali ya kujiamini kaitolea wapi, maana Hamza tunaemjua sisi ni yule Mzembe aliepigwa cha mbavu na mrembo Anitha.

Wale wafanyakazi wa mapokezi walikuwa na maswali kibao , walikuwa wakimfahamu Prisila sio mtu wa mchezo mchezo ijapokuwa alikuwa mdogo ki umri lakini alikuwa ni mkali mno kazini na hakupenda uzembe lakini sio hivyo cheo chake kilikuwa kikubwa mno ndio aliekuwa ni CHRO wa kampuni ya Dosam Global.

Kila mwanadada ndani ya jiji la Dar es salaam ambaye alikuwa ni mtaaluma alikuwa akimchukulia Prisila kama ‘role model’ wao kutokana na mafanikio yake ya haraka haraka na kuongoza kampuni kubwa Afrika na duniani.

Yaani kwa maneno marahisi yeye ndio alikuwa mwajiri mkuu wa kampuni ya Dosam hivyo watu wengi wanaotafuta ajira walikuwa lazima wapitie kwa huyu mwanamke, kutokana na watu wengi kutaka kufanyia kazi katika kampuni ya Dosam wale ambao walipata nafasi hawakutaka kuzembea kazini na kutolewa , kwani kudumu ndani ya kampuni ya Dosam ilihitajika zaidi utendaji mzuri na ujuzi na sio maswala ya GPA au ufaulu mkubwa unaonekana katika cheti chako.

Hivyo ilimfanya Prisila kuogopeka sana kwani alikuwa ni mwanamke aliekuwa akienda na falsafa yake ya 4E katika eneo la kazi ambayo ilisimama kama mbadala wa Effort(juhudi), Excellence(Ubora), Embodiment(Mfano halisi) na Environment(Mazingira).

Yaani kama mfanyakazi akikosa vigezo katika hio falsafa ya 4E basi kama ni mfanyakazi atafukuzwa au kama ndio anaomba hawezi kupatiwa kazi, ukikidhi vigezo hivyo hata kama cheti chako hakina maksi kubwa basi jihesabie unafanya kazi katika kampuni kubwa Afrika ya Dosam Global.

Prisila alicheka kwanza , hakuamini Hamza angekuwa ni mwanaume wa kujiamini namna hio tena na kwenda mbali na kumtania kama mrembo , asilimia kubwa ya wanaume wa rika la Hamza aliokutana nao wengi walionekana ni wenye kukosa hali ya kujiamini.

“Mzee Stephano ni baba yangu, sijui umefahamiana nae vipi lakini sina muda wa kuukuliza sasa hivi kwani unapaswa kukutana na bosi mwenyewe ambaye anataka kukuajiri , naomba nifuate Hamza”Aliongea na kauli yake ilimfanya Hamza kutoa macho.

Inamaana huyu mwanamke sio ambaye alikuwa akihitaji mtu wa kufanya nae maigizo ya boyfriend, alijiuliza Hamza na aliona ilikuwa ikileta maana , mwanamke mrembo kama huyo anahitaji vipi boyfriend wa maigizo kwa mfano , ilikuwa kichekesho.

Hamza alijiambia alikuwa akijidanganya tu , pengine matumaini yake ya kukutana na mwanamke mrembo yalikuwa yakienda kusambaratikika kabisa..

“Kwanini isingekuwa ni wewe , pumbavu kabisa yaani nimejitutumua vyote hivi kupendeza na kuwa jasiri mbele yako…”

“Mr Hamza come on,.. muda unaenda?”Aliongea Prisila mara baada ya kumuona Hamza amesimama tu na kumfanya bwana huyo kushitika kutoka kwenye mawazo na kuanza kutembea.

Wale wafanyakazi wa mapokezi waliishia kuangaliana kwa ishara kama vile wanajiuliza huyo mtu ni nani , kwanini bosi Prisila ndio kaja mpaka hapo kumchuka.

Asilimia kubwa ya watu ambao aliweza kuwaona ndani ya jengo hilo ni wazungu na wahindi na waliochanganya rangi kama yeye , watu weusi walikuwa ni wa kuhesabu sana , pengine ni kutokana na eneo lenyewe kuwa ghali sana , hii ilimfanya Hamza kujiambia kwamba hata kama mtu anaekutana nae kuwa mbaya lakin angalau anaonekana kuwa na pesa na kama angepita katika usaili huo ilimaanisha kwamba moja kwa moja angepata Exposire ya maeneo ya watu wazito wazito.

“Hata kama ni mbaya nnitaenda nae hivyo hivyo kibishi, pengine inaweza kuniweka na watu wazito wazito na ikawa safari ya kumjua Mzee”Aliwaza Hamza wakati akiwa kwenye lift.

Ijapokuwa alikuwa katika hali ya mawazo lakini bado hakuchoka kutazama umbo la mwanamke mrembo Prisila, alitamani kuuliza swali lakini alishindwa mara baada ya lift kufunguka na kuruhusu mtu mwingine kuingia.

Dakika chache tu walienda kutokezea katika floor ya juu kabisa na mara baada ya Hamza kutoka kwenye lift hiyo alijikuta akishangaa baada ya kuona uzuri wake lakini macho yake yalichanua mara baada ya kugundua eneo hilo lilikuwa likihudumia watu wa hadhi ya juu yaani VVIP.

Ijapokuwa alikuwa akijiamini kama vile amekunywa kiroba lakini bado mapigo yake ya moyo hayakuacha kudunda kwa kasi na kujiuliza ni mtu gani ambaye anaenda kufanya nae usaili tena eneo la VVIP katika hoteli kubwa ya hadhi kama hio.

Prisila alionyesha kutembea kama vile anafanya makusudi , pengine amevutiwa na sura ya Hamza maana bwana huyo alikuwa amependeza kweli ukijumlisha na muonekano wake wa ngozi ilimfanya kuwa wa kuvutia kwa kila mwanamke yoyote yule , lakini licha ya hivyo hali ya kimasikini ya Hamza haikujificha kwenye uso wake.

Kuonekana tajiri ni tofauti na uvaaji wa mavazi , unaweza kuwa tajiri lakini ukaamua kuishi maisha ya kawaida lakini siku zote huwezi kuonekana masikini , masikini siku zote ataonekana kwa umasikini wake na tajiri ataonekana kwa utajiri wake, kuna vitu vingi sana vya kumtofautisha tajiri na masikini au mtu aliefanikiwa na ambaye hajafanikiwa na hio inaenda kabisa kwanzia katika namna mtu unavyoongea ,wajihi , namna unavyotembea na ujengaji wa hoja wakati wa kuchangia mambo.

Tajiri anaweza akajificha katika kundi la watu masikini lakini siku zote hawezi kufanana na masikini.

Masikini na tajiri wote wanaweza kuwa na njaa kutokana na kutokula lakini kama utaamua kuwatofautisha na njaa zao utagundua masikini ndio anaeteseka zaidi na njaa kuliko yule tajiri, maana njaa ya tajiri ni ya kuchelewa kula wakati njaa ya masikini ni ya kukosa chakula.

Kwa upande wa Hamza ukweli ni kwamba ilikuwa ngumu kumtofautisha na masikini , kwa haraka haraka unaweza kusema kwamba Hamza ni mtoto wa tajiri ambaye ameamua kuishi maisha ya kimasikini.

Prisila alienda kusimama katika mlango namba 402 na kisha aligonga mlango kwa dakika kadhaa na palepale mlango ulifunguliwa na mwanadada mwenye sura iliokakamaa alievalia suti kama vile ni afisa usalama au bodigadi.

Mwanamke yule alimruhusu Prisila kuingia lakini alimwashiria Hamza kusimama nje kabla ya kuingia.

“Kijaji mruhusu, ndio mgeni anaepaswa kuonana na bosi”Aliongea Prisila lakini mtu alieitwa Kijaji bado alimwangalia Hamza kwa macho ya tahadhari na palepale alimsogelea na kuanza kumpapasa kama hana siraha ya aina yoyote na aliporidhika alimpiga jicho kali la tahadhari na kisha akamruhusu kuingia.

Hamza alijiambia huyu mwanamke ni mrembo sana lakini tabia yake ya ukakamavu inamfanya kuwa na sura ngumu.

Hata hivyo hakutaka kumfikiria sana , yeye hofu yake ni mtu ambaye anakwenda kuonana nae.

Hamza alikaribishwa na mandhari ya kuvutia ya chumba cha hadhi ya raisi(Presidential suite), haikuwa chumba cha kawaida kwa mtu wa kawaida kuingia na ilimfanya Hamza macho yake kuangalia vitu vilivyokuwemo pamoja na uzuri wake kwa haraka haraka.

Mbele yake kabisa upande wa dirisha kubwa ambalo linaangaliana na bahari ya Hindi kulikuwa na eneo la sebuleni na sofa kubwa ambalo lilikuwa imekaliwa na mtu alievalia kofia ya hat kichwani.,

“Huyo ndio bosi , nadhani mawazo yangu yapo sahihi nakwenda kukutana na mtu mbaya ambaye amekataliwa na wanaume mpaka kuamua kutafuta boyfriend feki , aisee hata hivyo maji nimeyavulia nguo sharti ni yaoge”Alijiongelesha katika mawazo yake akimwangalia yule mwanamke aliempa mgongo akisubiria surprise ya kuona sura ya mwanamke mbaya,

“Bosi , Mr Hamza kashafika kwa ajili ya usaili?”Aliongea Prisila huku akionyesha hali ya heshima.

“Okey mnaweza kuondoka , nitawaita baada ya usaili”

“Boss!!’Aliongea Kijaji kwa tahadhari.

“Hakuna kibaya kinachoweza kunitokea , mnaweza kuondoka”Aliongea bila ya kugeuka .

Upande wa Hamza sauti hio ilimsababishia mshituko wa aina yake , ilikuwa ni sauti nyororo lakini yenye madaraka ndani yake, ilikuwa ni kama wimbo wa kubembeleza unaozigonga ngoma za masikio yake.

Ilikuwa ni sauti nzuri mno na Hamza alijiuliza au mawazo yake ni tofauti na uhalisia , kwanini mwanamke anaemdhania kuwa ni mbaya wa sura kuwa na sauti nyororo hivyo , alijiambia pengine sio mbaya kila kitu , isitoshe kuna msemo wa kwamba Mungu hakupi vyote , anaweza akakupa sauti nzuri lakini akakupa sura mbovu, anaweza akakupa mguu ila akakupa Komwe kubwa.

Licha ya Prisila Singano kusita sita pamoja na mlinzi wa bosi huyo lakini waliishia kutii maagizo yake.

“Ukifanya chochote kibaya kitakachomdhuru bosi basi jua ndio kifo chako”Aliongea Kijaji kwa tahadhari na kumfanya Hamza kutoa tabasamu na kuzidi kumkera mlinzi wa watu,

Baada ya kila mtu kuondoka ndani ya hiko chumba yule mwanamke palepale aliinua mkono wake na kuitoa ile Hat.

Ilikuwa ni hat aina ya Beekeeping Veil, yaani hat ambazo huunganishwa na kitambaa cheusi ili kuzuia sura ya mtu kutokuoenekana

Hamza mara baada ya kuona mkono wa yule mwanamke ukiondoa ile hat taratibu mapigo yake yalianza kuongezeka spidi spidi , ilikuwa ni hisia ambazo kwenye maisha yake hakuwahi kuzisikia hata siku moja, kadri ile Veil ilivyokuwa ikiiacha sura wazi alizidi kujawa na hofu pamoja na mshituko wa aina yake,

Mwanamke yule baada ya kuivua alisimama na sasa namna ambavyo alikuwa akisimama ni kama vile yupo kwenye mwendo wa slow motion , ni kama vile malaika anaibukia kutoka ardhini.

Yalikuwa ni matarajio tofauti kabisa na kile alichokuwa akikiwazia Hamza , mwanamke aliekuwa mbele yake akili yake ilimwambia kabisa ni mwanamke ambaye anapaswa kusujudiwa kwa kupaza sauti.

******

MIEZI KADHAA ILIOPITA.

Ni miezi kadhaa iliopita ndani ya eneo la maegesho ya magari katika hospitali ya chuo ya Mayaya Clinic iliingia gari ya kifahari aina ya Porsche Gayenne G Coupe .

Baada ya gari hii kusimama palepale mlango wa dereva ulifunguliwa na mwanaume mtanashati alievalia suti na kwa haraka haraka alizunguka upande wa kushoto na kisha akafungua mlango wa abiria.

Mwanamke mrembo sana alievalia gauni lenye mkanda kiunoni na Blazer ya rangi ya ugoro alishuka kwenye gari lile huku yule mwanaume akionyesha heshima mbele yake.

Kwa haraka haraka anaeangalia tukio lile angeelewa kwamba yule mwanaume ni dereva wa yule mwanamke.

“Utanisubiria hapa mpaka nitakapomaliza”.

“Sawa madam”

Alijibu yule bwana kwa heshima kubwa tu mbele ya yule mwanamke , alikuwa ni msichana mrembo haswa pengine zaidi ya neno urembo , alikuwa ni msichana mdogo pia kimuonekano makadirio ya miaka kama ishirini na nne hivi , alikuwa ni mweupe wa wastani mrefu na aliejaaliwa umbo zuri.

Kitu kimoja tu ambacho pengine ambacho kinapunguza asilimia mbili ya uzuri wake ni muonekano wa yule mrembo , alikuwa ni kauzu mnno lakini hata hivo bado alikuwa amependeza.

Aliweza mkoba wake kwapani vizuri na kisha alizipiga hatua kuingia ndani ya hospitali hio kubwa.

Mayaya Clinic ni moja ya hospitali kubwa sana ndani ya ukanda wa Afrika mashariki na kati yote , ilikuwa ni hospitali ya binafsi ambayo ipo chini ya kampuni ya Vexto Group kampuni namba moja kwa ukubwa Afrika na namba kumi kwa Dunia nzima.

Yule mwanamke mrembo alitembea kwa mwendo wa kujiamini mpaka kwenye lift huku akionyesha sio mwenye kujali macho ya wanaume na wanawake wanaomwangalia.

Ukweli ni kwamba ilionekana ni kawaida kwake kuangaliwa hivyo kutokana na yeye mwenyewe alivyo , alikuwa mzuri hivyo ilileta maana kuangaliwa na kila mtu , wengine walimwangalia kwa matamanio na wengine walimwangalia kwa maswali kwa Mungu kwa kuweza kuumba mwanamke wa aina hio.

Wahenga wanasema Mungu hakupi vyote na kauli hii ilithibitishika kwa mrembo huyu ndio maana siku hio ya asubuhi alikuwa ndani ya hospitali hio

Dakika chache mbele mwanamke yule alikuja kutokezea katika floor namba saba ambayo ni idara ya Saikolojia(Psychiatric Department).

Idara ya saikolojia mara nyingi huhusiika na tiba ya magonjwa mbalimbali ya yanahusiana na akili.

“Miss Regina karibu sana , Dr Shukuru anakusubiria”Aliongea mwanadada wa mapokezi.

Kwa haraka haraka ilionekana mrembo huyu ambaye sasa anafamamika kwa jina la Regina alikuwa ni mgonjwa wa mara kwa mara kufika ndani ya hospitali hio kutokana na nesi wa mapokezi alivyompokea.

Mrembo Regina aliishia kutingisha kichwa na kisha alitembea kuelekea upande wa kulia akipita mapokezi na alisimama mbele ya mlango uliokuwa na kibao juu ofisi ya daktari au chumba cha daktari namba 01.

Mazingira ya hospitali katika idara hio ya magonjwa ya akili ilikuwa tulivu mno, pengine unaweza kusema wagonjwa wanaofika katika hospitali hio ni wachache lakini huo sio ukweli hospitali hio ina floor mbili ambazo zote hutumika kama idara ya magonjwa ya akili lakini floor ya sita ni yale magonjwa ya akili ambayo ni very comnon yaani yanayoeleweka na floor namba sita ni ya magonjwa ya akili ambayo ni special zaidi.

Unaweza ukashangaa mgawanyo huu lakini ukweli ni kwamba zama za miaka ilipita na zama za wakati huo zilikuwa zimebadilika sana tena sana , ni miaka ya hivi karibuni kulibuka wimbi la magonywa ya akili ya kipekee ambayo yamekuwa ni magumu sana kueleweka wa wataaluma na mpaka wakati huo chanzo cha magonjwa hayo hakijafahamika bado na wanasayansi wanapambana kujua chanzo chake.

Hii yote inasemekana ni mara baada ya tukio la mwaka 2020 , tukio la mwaka 2020 halikuwa na athari moja tu bali lilikuwa ni tukio ambalo lilibeba athari nyingi na moja ambazo ya athari ambazo zinahusishwa ni kuibuka kwa magonjwa ya akili ambayo sio ya kawaida.

Sasa ukiona mtu ambaye sio mfanyakazi wa hospitali ya Mayaya anaingia floor namba saba basi jua ni mwasilika wa tukio la mwaka 2020.

“Miss Regina karibu sana”

Mwanaume mmoja mtanashati wa makamo alievalia koti la udaktari alisimama mara baada ya mango kufunguliwa na mrembo Leilani.

Kwa muonekano wa daktari huyo ilionekana Regina ukiachana na uzuri wake ambao sio wa kawaida lakini kuna sababu nyingine ambayo inambeba kwani daktari aliefahamika kwa jina la Shukuru alionyesha unyenyekevu mkubwa.

“Thanks , I can see that you’re still a little nervous around me , please relax , I am regular patient remember”Aliongea yule mwanamke akitoa tabasamu hafifu kidogo akimwambia yule daktari kuacha wasiwasi akiwa nae na atulie kwani yeye ni mgonjwa wa mara kwa mara.

“Bila shaka .. ni kwamba tu wewe ni mgonjwa wangu muhimu”Aliongea Dr Shukuru huku akikaa kwenye kiti chake”

“Najua lakini mimi ni kama wagonjwa wengine tu na isitoshe bado natakiwa kuonana na daktari wakati kwa wakati”

“Ni kweli kabisa Ms Regina , umuhimu wako katika jamii unanifanya niwe makini na kutotaka kufanya makosa”

“Oh.. nashukuru naamini utafanya vizuri , isitoshe wewe ndio daktari bingwa ninaekuamini na tatizo langu , ni miaka mingi sana tokea nianze kupata matibabu kutoka kwako, ni mwaka wa tatu huu unaingia kama sikosei”

“Upo sahihi na imekuwa heshima kwangu muda wote kukusaidia kwa kila namna kuweza kupona ..”Aliongea na kisha palepale aliwasha tarakishi yake na kuandika jina la Regina kutafuta taarifa zake.

Kwa haraka haraka ilionekana mrembo huyo anaefahamika kwa jina la Regina sio mara yake ya kwanza kufika ndani ya hospitali hio.

“Awamu hii umechukua muda mfupi sana tokea appointment ya mwisho , nilikutegemea mwezi ujao , vipi kuna mabadiliko yoyote?”Aliuliza Dokta na kumfanya Regina uso wake kidogo kukosa utulivu.

“Siwezi kusema kuna mabadiliko makubwa na leo nilitaka kuonana na wewe kwa ajili ya ushauri zaidi”

“Ushauri , unaweza kuendelea nipo tayari kukupatia ushauri wowote kama ni swala linalogusa shida yako maana ndio taaluma yangu”

“Dr kwa miezi kadhaa mpaka sasa familia yangu wanalazimisha niolewe na mwanaume ambaye wamemchagua , nilikataa pendekezo lao lakini wameenda mbali na kuanza kufanya vikao kushawishi Shareholders wa kampuni ili kunilazimisha , wanasema nisipokidhi vigezo basi natakuwa kuachia nafasi yangu kwenye kampuni kama CEO na mwenyekiti wa bodi”Aliongea na kumfanya Dr kuwaza kidogo.

“Nadhani nimekuelewa unachotaka kumaanisha .. lakini ili niwe more specific kwenye ushauri wangu , hebu elezea unachukuliaje swala hili?”

“Dokta ninachofuata ni ushauri wako wa kitabibu kuhusiana na ugonjwa wangu wa ukichaa…”

“Miss Leilani naomba nikurekebishe, wewe huna tatizo la ukichaa bali una shida ya ugonjwa wa DID, nadhani nimekuambia ili matibabu yako kufanya kazi vizuri lazima utambue ugonjwa wako kwa jina hilo na sio ukichaa”

“Nimezoea kwa muda kuiita ugonjwa wa ukichaa, tukiachana na hilo nadhani katika ushauri wako wa kitabibu ulisema ugonjwa wangu unaweza kumalizwa na mapenzi?”

“Ndio nilimaanisha kutokana na shida yako kuwa ya kisaikolojia zaidi itakuhitaji kuwa na high self willing ya kuchagua ni namna gani unataka kuishi na kuishinda nafsi yako nyingine na hili litawezekana ukiwa na msaada wa nje wa kisaikolojia , kama vile kushare hisia zinazofanana na mtu mwingine , hii ni moja wapi ya njia ambazo nilipendekeza lakini haikuwa lazima sana lakini kwa wagonjwa wengi ambao nimekutana nao njia hio imeonyesha mafanikio , njia ya pili ni kuzipatanisha nafsi zako zote mbili tofauti na kuzikataa na njia hii ili kuweza kufanikiwa nilikuelezea kwamba unatakiwa ujue chanzo cha kila nafsi na pengine kujua kumbukumbu za maisha ya nyuma ambazo umepoteza”Alielezea Dokta Shukuru kwa kirefu.

DID ni kifupi cha neno la Kingereza yaani Dissociative identity Disorder ni ugonjwa wa akili ambao ulikuwa ukifahamika kwa jina la Multiple personality disorder , ugonjwa ambao unamfanya mtu kuwa na Utu wa aina mbili au nafsi mbili ambapo humvaa mtu kwa nyakati tofauti tofauti na kudhibiti tabia.

Yaani kwa mfano unaweza ukajitambbua kama John na watu pia wakakutambua kama John na tabia zako lakini muda mwingine unabadilika na kuwa Ayubu na tabia zako zinakuwa ni kama Ayubu bila ya kufanana kabisa na John.

Huo ndio ugonjwa ambao mrembo Regina alikuwa nao , yaani anatawaliwa na ugonjwa wa akili ambao unamfanya kuwa na nafsi mbili zenye tabia tofauti tofauti.

Ni ugonjwa ambao huwapa changamoto sana madaktari kuutibu lakini unatibika kupitia njia za kiushauri zaidi.

“Kwahio kulingana na tatizo langu na mipango ya familia yangu , unanipa ushauri gani?”

“Njia ambayo ni rahisi zaidi ambayo tokea mwanzo nilisisitiza ni kuishirkisha familia yako juu ya tatizo uliokuwa nalo ,lakini sio wewe tu ambaye ulikataa juu ya hili lakini babu yako pia alikataa swala ambalo naelewa kulingana na haki za mgonjwa wangu, nasema hivi kwasababu pengine kama mama yako wa kambo anajua una tatizo la namna hii asingefanya maamuzi ya kutaka kukutafutia mume wa kuolewa nae kwani haitokusaidia kupona tatizo lako , nikizingatia msingi wa matibabu nikiri kwamba familia yako maamuzi ambayo imeamua ni hatari kwa maendeleo ya shida yako, lakini naelewa pengine ni kutokana na kutokuwa na uelewa, pia najua kwa upande wako unachukua tahadhari”

“Asante Dokta kwa kuwa muwazi , ukweli tokea nafike hapa nishafanya maamuzi na nilitaka kusikia maoni yako juu ya hili”

“Ndio nipo tayari kusikia maamuzi yako”

“Napanga kuajiri mwanaume yoyote aigize kuwa boyfriend wangu ili kuzuia mpango wa wazazi wangu zidi ya kampuni”Aliongea na kumfanya Dokta Shukuru kushangaa kidogo lakini alipotezea mshangao wake.

“Kuna haja ya kwenda mbali hivyo , Ms Regina najua unalichukulia tatizo lako kwa ukubwa lakini ni tatizo la kawaida na kwa muonekano wako na mafanikio yako sidhani kama kuna haja ya kuwa na mwanaume wa maigizo , wapo wanaume wengi ambao wanaweza kukupenda na wewe kuwapenda ni swala la kutoa nafasi tu”

“Dokta kwa maelezo yako unahisi ni rahisi kupata mtu kunipenda , ushasema kwa muonekano wangu na mafanikio hivyo sidhani kuna mwanaume ambaye anaweza kunipenda kwa dhati tofauti na kutanguliza nilichokuwa nacho , nimeona wakati nikiendelea kumtafauta huyo mwanaume nitakaempenda na ambaye atanipenda kwa dhati nitafute mbadala maana mapenzi pia ni swala la mchakato na kama hili swala likishindikana nitaenda na plan B kupatanisha nafsi zangu”

“Unafikiri unaweza kupata mwanaume ambaye anaweza kukubali kuajiriwa kuigiza kuwa mchumba?”

“Naamini nguvu ya pesa ndio itafanya kazi, itakuwa ni kama ajira tu na ni swala ambalo nataka kulifanya ili kujipatia muda nikiendelea kufuatlia namna ya kumaliza tatizo langu , huenda pengine ni kapata mwanaume ninaempenda na ikawa rahisi tatizo langu kumalizika”Aliongea na kumfanya Dokra Shukuru kuwaza kwa muda.

“Nadhani sio wazo baya kulingana na hali yako , umesema pengine unaweza kupata mwanaume unaempenda wakati ukiwa na mchumba wa maigizo , hoja yangu ni kwamba pengine mchumba wa maigizo akawa ndio mtu uliepangiwa kuwa nae na mkapendana hivyo nipo tayari pia kubeti , nilisha fikiria kwa kina nitakuja kufanya chochote kwa ajili ya kuhakikisha hali ya mgonjwa wangu inaisha , kwasasa tujaribu na hiki ulichoamua” Aliongea Dr Shukuru na kumfanya Regina kutoa tabasamu.

Ugonjwa wa DID ulikuwa mgumu kudili nao ndio maana inashauriwa na daktari kuwa flexible wakati wa kushughulika na mgonjwa na hicho ndio ambacho alikifanya Dr Shukuru.

Dr Shukuru Omari ni daktari mbobezi ambaye amepitia mafunzo makubwa ya kudili na wagonjwa wa akili na haikuwa mara yake ya kwanza kudili na mgonjwa mwenye nafsi mbili.
ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom