Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,274
9,911
MIAKA sita iliyopita, Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo nchini Tanzania ulikuwa ukitajwa kama mmoja wa miradi ya kimkakati yenye fursa kubwa ya kuzimua uchumi wa taifa hilo. Midomoni kwa watumishi wa umma na viongozi wa serikali, neno bandari ya Bagamoyo halikutoka.

Hata hivyo, miaka miwili iliyopita, upepo ukaanza kubadilika. Aliyekuwa Rais waTanzania wakati huo, hayati John Magufuli, alizungumza hadharani kuhusu mradi huo na kusema ulikuwa na "masharti ya hovyo" ambayo serikali yake isingeweza kuyakubali.

Watanzania ni watu ambao kwa tabia wanapenda kuwaamini viongozi wao. Kauli hiyo kutoka kwa Kiongozi Mkuu wanchi ilizua mkanganyiko miongoni mwa wananchi; wengine wakiamini wale waliosema bandari hiyo ijengwe na wengine wakiamini mradi huo ni wa hovyo.

Hiyo ndiyo Tanzania ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameirithi linapokuja suala la ujenzi wa bandari hiyo. Kwenye kujibu swali kubwa la makala haya, ni muhimu kurudi nyuma kidogo kufahamu kuhusu mradi wenyewe.

Kuhusu mradi wa Bandari Bagamoyo
Kwa sadfa ya kijiografia, Tanzania imejikuta ikiwa nchi yenye bandari katika eneo ambalo wengi wa jirani zake hawana bandari. Miongoni mwa jirani zake nane; Malawi, Msumbiji, Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia, ni Kenya na Msumbiji pekee ndiyo wenye bahari.

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari.

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari, Hata hivyo, ingawa huduma za bandari hiyo zinahitajika sana, bandari ya Dar es Salaam- kwa sababu tofauti ikiwamo udogo wa eneo lake na ongezeko la mahitaji ya huduma na teknolojia za kisasa za meli, imeanza kuzidiwa.

Iliyokuwa Mamlaka ya Bandari wakati huo, iliona changamoto hiyo na ndiyo ikapendekeza kujengwa kwa bandari nyingine kubwa zaidi katika eneo la Bagamoyo - umbali wa takribani kilomita 75 tu kutoka Dar es Salaam ili kuendelea kuwa kitovu cha usafiri wa maji katika eneo la Afrika.

Katika kutimiza azma hiyo, Mamlaka ya Bandari ikaja na Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania - ambao, pamoja na mambo mengine, ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022.

Sadfa nyingine ya kijiografia ni kwamba eneo la Bagamoyo ni mojawapo ya maeneo ambayo China imeyatambua kama ya kimkakati katika Mpango wake Kabambe wa Belt and Road - ambao kimsingi unaunganisha dunia kupitia njia ya maji.

Tanzania iko katika eneo la kimkakati kwa sababu inazungukwa na nchi nyingi zisizo na bahari, tayari ina reli mbili zinazounganisha na nchi jirani; TAZARA kwa maana ya Zambia na ile ya Kati inayokwenda mpaka Kigoma ambako ni jirani na Congo, Rwanda na Burundi pia.

Kama ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) ukikamilika, Tanzania itakuwa na reli ya kisasa ya kusafirisha watu na mizigo kutoka Tanzania kwenda katika nchi jirani kwa haraka.

Kwa hiyo, wakati Tanzania ikipanga kuwa na Bandari ya Bagamoyo kubwa na imara, wawekezaji kutoka China na Oman waliona fursa ya Eneo la Uwekezaji wa Biashara (EPZ) katika mji huo kwa sababu ya urahisi wa kusafirisha bidhaa kutoka eneo la Maziwa Makuu kwenda kwingineko duniani.

Faida nyingine ya Bandari ya Bagamoyo ilikuwa kwamba kwa sababu ya ukubwa wake, itakuwa na uwezo wa kupokea mizigo zaidi ya mara 20 ya Bandari ya Dar es Salaam na pia kupokea meli kubwa za kisasa ambao kwa sababu ya ukubwa wake, haziwezi kuja Dar es Salaam.

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo imekuwa kama lango kuu la kupitishia bidhaa zinazokwenda katika nchi jirani zisizo na bahari.

Kupitia mradi wa EPZ, ilielezwa vitafunguliwa zaidi ya viwanda ya 700 na kuajiri takribani watu 250,000 - ukiwamo mradi wa masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka kwa wawekezaji kutoka Korea Kusini. Huu ulikuwa uwe mradi mkubwa zaidi katika historia ya Tanzania ambako wawekezaji hao kutoka China, Oman na Korea Kusini wangeingiza nchini mtaji wa zaidi ya dola bilioni 10 (zaidi ya shilingi trilioni 23).

Wawekezaji hao na nchi wanazotoka kwenye mabano ni China Merchants Ports Limited(China), Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), na Science and Technology Policy Institute(STEPI)Korea Kusini.

Hofu ya Mradi wa Bagamoyo
Maneno ya Magufuli yalikuja katika wakati ambao kulikuwa na taarifa nyingi kuhusu namna China inavyotwaa mali zisizohamishika za nchi zilizokopa fedha kutoka kwake na zikashindwa kurejesha kwa wakati. Mifano iliyokuwa ikitolewa sana ilihusu nchi kama Zambia na Sri Lanka.

Katika mkutano wake na wafanyabiashara wa Tanzania, Magufuli alizungumza waziwazi kwamba kwa namna makubaliano yale ya Tanzania na wawekezaji yalivyokuwa, mkataba ule ulikuwa hauna maslahi na Tanzania naye asingekubali kuona mradi huo ukiendelea kwa namna hiyo.

"Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha mikoa ya Kusini kupokea mafuta badala ya Dar es Salaam kisha yarudihuko, hatutakiwi kuiendeleza, barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge," alisema Rais Magufuli.

Spika Job Ndungai aliwahi kulalama kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa.

Rais huyo aliyefariki dunia Machi 17 mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu Rais wake, alisema masharti mengine ya kufanyika kwa mradi huo ni kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotakiwa kwenda kukusanya ushuru wala kodi katika eneo hilo, umiliki wa eneo hilo kwa miaka 33 na kufidiwa kwa gharama za uwekezaji wa ujenzi huo.

Spika wa Bunge, Job Ndugai, alizungumza katika nyakati hizo na kulalama kwamba serikali inafanya makosa kutoendelea na mradi huo kwa vile una faida kubwa na hizo ambazo zinaonekana kasoro zinaweza kuzungumzika.

Kuna ukweli kwenye madai ya "mkataba wa hovyo"?
Mmoja wa viongozi wa juu katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete ambao mradi huo ulikuwa unaelekea kukamilika, ameniambia mengi ya yanayoyosemwa kuhusu mradi huo hayana ukweli na kwamba kulikuwa na upotoshaji mkubwa.

Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yake, kiongozi huyo alisema gharama pekee kubwa ambayo serikali ingetakiwa kuingia katika mradi huo ni ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaohamishwa kupisha ujenzi wa bandari hiyo ambao kwa makisio ya mwaka 2016 yalikuwa kiasi cha dola takribani dola milioni 20.9 (shilingi bilioni 43).

" Gharama yetu ni hizo dola milioni 20 za kulipa wananchi lakini mengine yote ni siasa tu. Wanaokuja wanaleta shilingi trilioni 23 na ni uwekezaji wala si mkopo. Ni sawa na kampuni zinazokuja kuchimba madini hapa kwetu. Huwezi kusema wanakuja kutukopesha hela za kuchimba madini. Ni biashara yao.

" Jambo la muhimu kuliko yote ni kwamba huo mpango wa kuwa na Bandari ya Bagamoyo tulikuwa nao hata kabla wawekezaji hawajaja. Na wala hakuna masharti ya kutuzuia kujenga barabara wala miundombinu mingine. Hilo suala la miaka 33 ni la kawaida, yaani mtu aweke shilingi trilioni 23 na halafu asiweke muda wa kurudisha hela zake? Mwisho kabisa, baada ya miaka 33, bandari na hivyo viwanda havitahamishwa Tanzania na nina imani nchi yetu itakuwepo bado," alisema kiongozi huyo.

Huku Lamu, kule Bagamoyo
Kenya, kwa muda mrefu, ilikuwa ikitegemea Bandari ya Mombasa kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo kwa wateja wake wa ndani na katika eneo la maziwa makuu. Kwa sababu ya ongezeko la mahitaji, yenyewe pia ikaamua kujenga Bandari ya Lamu - kwa sababu zilezile ambazo zimeifanya Tanzania kuwa na mpango wa Bagamoyo.

Hadi sasa, nchi hizi mbili zinashindana katika kuhakikisha ipi inakuwa ya kwanza kufanikisha mradi huo ambao unatarajiwa kuleta picha mpya ya ukuaji wa uchumi wa mataifa haya mawili jirani.

Bandari ni mojawapo ya maeneo ambayo yana fursa kubwa katika ukuaji wa uchumi na majirani hawa wote sasa wanatafuta wawekezaji katika miradi ya bandari lakini kwa kuiunganisha na ile ya miundombinu ya reli za kisasa.

Hata hivyo, kwa maana ya ukubwa na umuhimu, mradi wa Bandari ya Bagamoyo una faida kubwa na muhimu zaidi kwa Tanzania kwa sababu ya faida kubwa za viwanda na kilimo zitakazosababishwa moja kwa moja na uwepo wa bandari hiyo.

Rais Samia atafanya nini?
Katika muda wote aliowahi kuwa Makamu wa Rais, Samia hajawahi kutoa kauli yake rasmi kuhusu mradi wa Bagamoyo. Hata hivyo, sasa akiwa Rais, ni wazi washauri wake wa uchumi na wenzake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), watampa ushauri unaofaa kuhusu nini hasa anatakiwa kufanya sasa.

Akiwa Rais, huenda washauri wake wa uchumi na wenzake ndani ya Serikali na CCM , watampa ushauri unaofaa kuhusu nini hasa anatakiwa kufanya sasa.

Dhana ya hofu dhidi ya Wachina ina mashiko miongoni mwa Watanzania wengi na ukweli kwamba hofu hiyo ilitangazwa na Rais Magufuli hadharani na katika namna ambayo ilikuwa rahisi kueleweka kwa Watanzania, inampa Rais Samia fursa ya kufanya upembuzi yakinifu wa kuondoa mambo ambayo yanaweza kuwa hayana maslahi kwa taifa lake.

Bahati nzuri ambayo Watanzania wanayo kwasasa ni kwamba Samia ana asili ya Zanzibar na anajua nini maana ya bandari - pengine kuliko viongozi waliozaliwa mbali na pwani.
Screenshot_20210414-142027.png
Screenshot_20210414-141542.png


Thread 'Mbowe ataka Bandari ya Bagamoyo ijengwe kwa masharti yoyote' Mbowe ataka Bandari ya Bagamoyo ijengwe kwa masharti yoyote

Maoni ya Wadau
MAONI YA ZITTO KABWE MWAKA 2019 BAADA YA KUFUTWA KWA MRADI WA BANDARI YA BAGAMOYO

Juzi Serikali imetangaza bungeni kuwa Mradi mkubwa wa Ukanda Maalumu wa Kiuchumi wa Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) wa thamani ya Dola za Marekani 10 Bilioni (sawa na TZS 23 Trilioni) umesitishwa na kuwa hautafanyika tena. Mradi huu mkubwa wa uwekezaji ambao thamani yake ni zaidi ya Bajeti ya Maendeleo ya Wizara nzima ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa miaka minne (TZS 18 Trilioni) haupaswi kufutwa tu bila mjadala wa kina. Ni lengo la makala haya kuibua mjadala huo.

Kwangu kufutwa kwa mradi wa Bagamoyo SEZ ni kielelezo cha uelewa mdogo wa Uchumi na Diplomasia uliotamalaki miongoni mwa watawala wa sasa wa nchi yetu Tanzania. Kwanza ni muhimu kuuelewa mradi wenyewe kabla ya kubomoa hoja za Serikali zilizotumika kufuta mradi huu. Watanzania wanapaswa kutambua kuwa mradi huu ni wa Uwekezaji kutoka nchi mbili ambazo tuna historia nazo kubwa, Oman na China, hivyo tutazama athari za maamuzi haya ya Serikali pia katika eneo hilo la mahusiano na nchi hizi mbili.

Kiujumla watanzania wengi wakisikia mradi wa Bagamoyo SEZ wanajua ni ujenzi wa bandari ya Bagamoyo tu, La si hivyo. Bandari ni sehemu tu ya mradi. Lakini Bagamoyo SEZ ni mradi wenye lengo la kuufanya mji wa Kihistoria wa Bagamoyo kuwa Kituo kikubwa Cha Usafirishaji Mizigo (Main Logistics Hub) Katika Bara zima la Afrika. Ni Uwekezaji wa Ubia (Joint Venture Investment) kati ya wawekezaji kutoka China na Oman, ambao walikuwa tayari kuutekeleza kama Special Economic Zone (Eneo la Ukanda Maalum wa Uchumi Bagamoyo). Ujenzi wa Bandari ni moja tu kati ya maeneo Manne ya Mradi huo mkubwa, maeneo mengine ya mradi ni pamoja na;

1. Ujenzi wa eneo la viwanda (industrial park) ambalo katika awamu ya kwanza litakuwa na viwanda 190 vitakavyozalisha ajira mpya za moja kwa moja 20,000 na awamu ya pili na tatu ikikamilika kutakuwa na viwanda 790 vitakavyozalisha ajira mpya 100,000.

2. Ujenzi wa Mji wa Kisasa wa makazi unaonendana na mahitaji ya karne ya 21. Ujenzi wa mji huu ulilenga kusaidia kupunguza msongamano wa jiji la Dar es saalaam kwani shughuli nyingi za uchumi zitakazotokana na Bagamoyo SEZ ungepelekea watu wengi kuhamia kwenye mji mpya kutoka Dar es Salaam.

3. Ujenzi wa Kituo Cha Usafirishaji (Logistics Park) ambacho kingeifanya bagamoyo kuwa kitovu cha usafirishaji wa mizigo na hivyo kuiimarisha Tanzania kama njia kuu ya usafirishaji mizigo ‘transit route’ inayotoka na kuingia kwenda nchi mbalimbali tunazopakana nazo. Hii ‘Logistics Park’ ndio ililenga kuhudumia Meli (handle transshipment) kutoka Afrika kwenda Ulaya na Marekani.

Mradi huu na maeneo yake hayo manne (4) ungekamilika, na haswa hilo eneo la nne (Logistics Hub), jumla ya Kontena 20 milioni zilitarajiwa kupita Bagamoyo kwa mwaka na kuifanya kuwa bandari kubwa kuliko ile ya Rotterdam ya Uholanzi ambayo ndio kubwa kuliko zote Bara la Ulaya. Kwa hakika ndani ya miaka 10 Bagamoyo ingekuwa Dubai ya Bara zima la Afrika.

Wazo la mradi huu linafanana na wazo la Mradi wa Shenzhen - Special Economic Zone, ambapo Kampuni inayotaka kuwekeza Bagamoyo ilikuwa mojawapo ya kampuni zilizowekeza huko. Ukanda Maalumu wa Uchumi wa Shenzhen ulikuwa Mpango Maalumu wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi ya China chini ya Kiongozi Deng Xiaoping.

Ulikuwa mji wa majaribio ya sera za Kiuchumi ambazo zimeibadilisha nchi ya China na kuwa inavyoonekana sasa. Bagamoyo ilikuwa inajengwa kuwa Shenzhen ya Afrika kupitia mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone ambayo wengi hupenda kuita Bagamoyo Port kiufupi na kwa hakika kwa makosa.

Hii Ndio bahati mbaya iliyotokea, watu wengi wanajikuta kuzungumzia bandari na huenda hata maamuzi ya kusitisha mradi yamefanyika kwa kuzingatia sehemu moja tu ya bandari na wameacha kufikiria manufaa makubwa ya ajira kutoka maeneo mengine matatu ya mradi, hasa kipindi hiki ambacho vijana wengi wa Tanzania wanamaliza shule bila matumaini ya kupata ajira rasmi au hata kujiajiri wenyewe.

Mradi huu mkubwa umekuwa gumzo sehemu mbalimbali ulimwenguni kutokana na ukubwa wake pamoja na athari zake kwa maslahi ya makundi mbalimbali ulimwenguni. Jambo moja muhimu sana kukumbukwa ni kuwa Biashara ni vita ya makundi yenye maslahi mbalimbali. Rais John Pombe Magufuli amekuwa akihubiri kuwa nchi yetu ipo kwenye vita vya kiuchumi, masikini kwenye ‘The Bagamoyo Battle’ ameshindwa vita kabla hata risasi ya kwanza kupigwa. Maslahi yapo kutoka maeneo kadhaa;

1. Kwa mataifa ya Ulaya Magharibi mradi huu ulikuwa tishio kwa hoja za kiushindani na ushawishi ndani ya ukanda wa Bahari ya Hindi ambao unabashiriwa kuwa kitovu muhimu katika bishara ya kimataifa katika miaka michache ijayo. Wazungu waliuona mradi huo kuwa utaipa China nguvu kubwa zaidi ya kiuchumi. Ilikuwa ni muhimu sana kwa wao kuhakikisha mradi huu hautekelezwi kwa namna yeyote ile ili kuzuia nguvu ya China Katika ukanda huu.

2. Kwa mataifa mengine ya Afrika, mfano kwa SADC nchi kama Afrika ya Kusini - mradi huu ulikuwa tishio kwa maslahi yao ya kiuchumi kwa kuwa ungepelekea ushindani mkubwa kwa Biashara ya Bandari ya Durban ambao hivi sasa ndio kuna bandari pekee zenye uwezo wa kuhudumia meli kubwa kabisa za mizigo (4th generation ships). Inawezekana kabisa Afrika Kusini haikufanya kitu kuhujumu Mradi huu lakini kutofanyika kwake ni faida kubwa wa Durban kwani Bagamoyo ilikuwa inakwenda kuwa mshindani wake Mkuu. Hali ni hiyo hiyo kwa Angola ambayo inataka kujenga reli ya kuiunganisha DRC Kongo ili mizigo ya nchi hiyo ipitie bandari yao ya Luanda.

3. Kwa Afrika Mashariki, hasa Kenya, mradi wa Bagamoyo ulikuwa ni tishio kubwa kwa mradi wa Bandari mpya wanayopanga kuijenga huko Lamu, ambayo nayo itakuwa na uwezo wa kuhudumia meli kubwa (4th generation ships) na pia itakuwa na kitovu cha usafirishaji wa mafuta barani Afrika. Siamini kuwa Kenya imefanya chochote kuhujumu mradi huu wa Bagamoyo SEZ, lakini maamuzi ya Tanzania kusitisha mradi huo yametoa ushindi wa bure bure kwa Kenya, kwani sasa Meli kubwa zitahudumiwa Lamu na kuipa Kenya nafasi kubwa sana Katika Biashara ya Usafirishaji Katika eneo la Afrika Mashariki na Kati (The Great Lakes Region).

4. Taasisi nyingine za kimataifa zimeingia katika vita hii kusaidia nchi zenye nguvu Duniani. Benki ya Dunia (WB) kwa Mfano haikuupenda mradi huu, na ni dhahiri kuwa imetumia ushawishi wake Serikalini kuupiga vita Mradi wa Bagamoyo SEZ. Ushawishi huo uliwezekana kutokana na misaada na mikopo ambayo Benki ya Dunia inaipatia Tanzania na hivyo kupenyeza ushawishi wa kuupinga mradi. Hoja kubwa iliyotumika kupinga mradi wa Bagamoyo ni kwamba kwakuwa wao WB wameipa Serikali mkopo wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, hivyo mradi wa Bagamoyo hauna tija, na endapo ungefanyika utaleta ushindani kwa Bandari ya Dar es salaam na hivyo kushindwa kulipa mkopo. Hoja hii ni muflisi, lakini Serikali yetu ikaingia kingi na kupoteza Uwekezaji wa Fedha za Kigeni (FDI) wenye thamani ya USD 10 Bilioni (TZS 23 Trilioni) kwa tishio la mkopo wa USD 400 milioni (TZS 920 Bilioni). Inasikitisha sana!

Makundi hayo yote yalikuwa na maslahi yanayofanana ya kuhakikisha|kuombea kwamba Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone usitekelezwe. Maamuzi ya Serikali yetu yamewezeshwa matakwa ya Makundi hayo, kwa kujua ama kutokujua. Najua kuwa imetumika nguvu kubwa ya ushawishi kwa kutumia; Propaganda za vyombo vya habari, Ujasusi wa kiuchumi (economic intelligence) na hata Ushawishi wa kisiasa (political influence and scaremongering).

Mfano ni kugonganisha utawala wa Awamu ya 5 na Uongozi uliopita wa Awamu ya 4 (kwa kuonyesha kwa kuwa Rais aliyepitisha mradi huu anatoka Mkoa wa Pwani, na hivyo amepeleka mradi huu kwao Bagamoyo kwa kujipendelea). Ndio maana Kikao Cha Baraza la Mawaziri, vikao vya mwanzo mwanzo tu vya utawala wa awamu ya tano, viliufuta mradi huu bila hata mjadala wa kina unaozingatia faida pana za mradi, na wala mahusiano ya kidiplomasia kati yetu na nchi za Oman na China.

Sasa tutazame hoja zinazotolewa dhidi ya mradi wa Bagamoyo SEZ ili kuona kama kuna mantiki.

1. Hofu ya Serikali kupoteza mapato kutokana na ushindani wa Bandari ya Bagamoyo

Serikali imejengewa hofu kuwa Bandari ya Bagamoyo itafanya mapato ya Bandari ya Dar kupungua na hivyo Serikali kukosa Mapato yake. Ukiangalia kwa juu juu hoja hiyo ina mantiki. Kwamba kutakuwa na ushindani na Dar es salaam itapoteza mapato. Lakini yapo mambo matatu yanayothibitisha kwamba hoja hiyo sio sahihi.

Mosi: Bandari ya Bagamoyo itahudumua meli kubwa (4th generation ships) ambazo hivi sasa haziwezi kuingia katika bandari ya Dar es salaam. Katika biashara ya kimataifa hivi sasa, usafirishaji kwa kutumia meli kubwa ndio wenye tija, unafuu na faida. Kwa mfano leo hii kusafirisha zao la korosho kutoka Tanzania hadi China au Marekani kwa kutumia meli ndogo inagharimu mara mbili ya gharama ya usafirishaji kwa meli kubwa.

Kutokuwa na uwezo wa kuhudumia meli kubwa kumefanya gharama za usafirishaji wa bidhaa kutoka Nchi zetu kwenda kwenye masoko mengineyo kuwa kubwa na ghali mno (uncompetitive). Ndio maana leo hii nchi za Latin America ambazo zipo mbali kabisa na China, zinauza bidhaa zake nyingi katika soko la China kuliko nchi za Afrika ambazo zipo karibu na China kijiografia.

Mfano halisi umetokea karibuni tu, Marekani ilipoanza vita ya biashara na China kwa kuongeza kodi katika bidhaa za China, ili kujibu mapigo China nao waliongeza kodi kwa maharage ya soya kutoka nchini Marekani. Ikumbukwe kwamba biashara ya maharage ya soya ni kubwa sana kwa Marekani, kila mwaka wanauza soya ya thamani ya USD 35 Billioni na zaidi kwa nchi mbalimbali, China ikinunua 60% ya soya yote.

Hivyo basi, kitendo cha China kuongeza kodi, gharama za soya zikapanda na hivyo wanunuzi wa soya kutoka China walitafuta soko mbadala la kununua soya (altenative source). Lakini badala ya kuja kununua Afrika, ambako ni karibu zaidi, waliamua kwenda kwa nchi za Amerika ya Kusini (Latin Amerika), hasa Brazili. Moja ya sababu ya kwenda kununua Soya huko ni pamoja na uwepo wa bandari zenye uwezo wa kuhudumia meli kubwa (4th Generation Ships) ambazo ni nafuu katika usafirishaji. Afrika imekosa fursa ya biashara kubwa sababu hiyo.

Pili: Uwepo wa bandari kubwa katika eneo moja unasaidia kuongeza wingi wa shughuli za usafirishaji wa mzigo kutoka kwenye bandari kubwa kwenda kwenye bandari ndogo, na hivyo kuongeza mnyororo wa thamani wa sekta ya usafirishaji. Mizigo mikubwa mkubwa ambao ungeshushwa katika bandari ya Bagamoyo ungetengeneza fursa ya biashara kwa meli ndogo na za kati kuuchukua Bagamoyo na kuupeleka kwenye bandari za jirani za Dar, Tanga, Mombasa, na Beira. Mapato yangeongezeka badala ya kupotea.

Tatu: Ajira zitakuwa nyingi kwenye Bagamoyo SEZ kuliko kwenye upanuzi wa bandari ya Dar es salaam. Ni vizuri pia kujiuliza kuwa upanuzi wa Bandari ya Dar manufaa yake ni zaidi ya manufaa tutakayopata katika Mradi wote wa Bagamoyo SEZ? Hivi sasa Bandari ya Dar es salaam inaajiri watu wangapi? Baada ya upanuzi utakaofanywa ni ajira ngapi mpya zitaongezeka?

Ukweli ni kwamba kwa teknolojia za karne ya 21 shughuli za bandari nyingi ziko kidijitali (digitalized) sana kiasi kwamba ile asili ya kuzalisha ajira nyingi haipo tena. Hivyo kwa vyovyote vile ajira mpya zitakazozalishwa baada ya kumalizika upanuzi hazitozidi 1000. Kwa upande mwingine, ajira zitakazozalishwa kwenye mradi wa Bagamoyo SEZ katika awamu ya kwanza tu ni 20,000. Je faida ipo wapi? Mapato ya Kodi za Wafanyakazi hao 20,000 tu yatazidi mara 10 Mapato yote ya Serikali kutoka Bandari ya Dar Es Salaam.

Nne: Kwa upande wa mapato (direct revenues) kwa Bandari ya Dar es salaam- serikali inapata kiasi gani? Kwa vyovyote vile mapato ya jumla ambayo serikali itakayapata katika mradi wa Bagamoyo SEZ yatakuwa ni makubwa zaidi, kwani mbali na mapato itakayopata katika component ya bandari kwa njia ya Wharfage charges; Imports Duties kwa bidhaa nyingi zitakazopitia katika bandari hiyo, serikali pia itapata kodi za aina mbalimbali katika viwanda 190 na baadaye viwanda 790 vitakavyojengwa.

Watumishi 20,000 PAYE yao itakuwa ni kiasi kikubwa cha uhakika kwa serikali. Achilia mbali multiplier effects zitokanazo na shughuli za viwanda. Katika mji mpya utakaojengwa Serikali itapata kodi za majengo na kodi nyingine zitokanazo na ardhi na pango, achilia mbali kodi za shughuli nyingine za biashara zitakazofanyika Bagamoyo. Hoja ya Mapato kupotea ni hoja dhaifu na haina mashiko kabisa.

2. Hofu ya Mgeni Kuendesha Bandari

Hoja nyingine inayotolewa ni kwamba kumpa mwekezaji mgeni aendeshe bandari ni hatari kwa usalama wa nchi. Hapa cha kujiuliza ni kuwa ndani ya Bandari ya Dar es salaam kuna kampuni ya Uwekezaji ya Kigeni - TICTS, ambayo imeendesha shughuli zake ndani ya bandari kwa miaka 20 na zaidi sasa, je ni usalama upi wa nchi umeathirika?

Inapokuja hoja za kiusalama ni nchi ya China yenye mahusiano ya karibu sana ya kijeshi na Tanzania. Kila leo tumeona vikifunguliwa vyuo (Chuo cha Ulinzi cha Jeshi Kunduchi), viwanja vya ndege (Uwanja wa Ndege wa Kijeshi wa Ngerengere, Morogoro) nk kwa msaada wa China. Wanajeshi wengi wa Tanzania wamepata mafunzo China, na vifaa vingi vya kivita vimetoka China. Ni jambo la kawaida kukuta gari yenye namba za usajili za JWTZ ndani yake kuna askari wa Tanzania na China.

Sasa kwa ukaribu huo wa kihistoria tangu JWTZ ilipoanzishwa baada ya kuvunja jeshi lenye asili ya kikoloni lililojaribu kufanya mapinduzi miaka ya 60, leo hii sisi ndio watu wa kuhofia usalama dhidi ya Wachina? Hata hivyo, kama hoja hii ni ya kweli, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama haviwezi kuweka mkakati mbadala wa kudhibiti masuala ya Usalama katika eneo la mradi la Bagamoyo SEZ?

3. Hofu ya China kuchukua Mali za Taifa kama Zambia na Sri Lanka

Hoja nyingine inayozungushwa ni kwamba eti Wachina watanyang’anya mali za taifa endapo mradi huo utapata hasara kama ilivyokuwa kwa mradi wa Bandari wa Sri Lanka. Ukweli ni kwamba mradi wa Bagamoyo sio sawa na mradi wa Sri Lanka au mradi wa ujenzi wa Reli ya Kenya. Tofauti na miradi hiyo miwili ya Kenya na Sri Lanka, mradi wa Bagamoyo unatekelezwa kwa njia ya uwekezaji (FDI) kwa asilimia 100, wakati ile miradi ya Kenya na Sri Lanka inatekelezwa kwa mikopo ambayo nchi inawajibu wa kuweka dhamana (sovereign guarantee).

Hii maana yake Maana yake nini? Hata kama mradi wa Bagamoyo utendeshwa kwa hasara, atakayeumia ni mwekezaji na sio nchi yetu. Lakini kwa uzoefu wa kampuni ya China Merchant katika uwekezaji wa miradi mikubwa ya aina hii, haiwezekani wakafanya uamuzi wa kuwekeza mradi wa kupata hasara kirahisi namna hiyo. Ikumbukwe kwamba kampuni ya China Merchant ina uwezo wake kimtaji unaofikia mara 20 ya GDP ya Tanzania. Yaani Mapato ya Kampuni hiyo kwa mwaka ni USD 1,200 Bilioni, wakati GDP ya Tanzania ni USD 55 Bilioni.

4. Masharti Magumu

Hoja nyingine inayosemwa ni kuwa masharti ya kuendesha mradi wa bagamoyo ni magumu. Inawezekana kuwa hoja hii ina mashiko na ndio maana ni hoja pekee ambayo Serikali inaitaja. Hata Bungeni ndio hoja Waziri wa Uchukuzi ameizungumza katika hotuba yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka 2019/2020.

Lakini tuulizane, hivi mahala ambapo watu wanazungumza, kila upande una wajibu wa kuja na mapendekezo yake (proposal) na upande wa pili una haki ya kuja na counter proposal. Kuweka mpira kwapani sio njia sahihi hata kidogo, ni udhaifu uliopitiliza.

Kama serikali iliweza kwenda hatua ya ziada kuvutia mradi wa Bomba la Mafuta la Uganda kwa kutoa vivutio maalum vilivyopelekea hadi kufanyika mabadiliko ya sheria Bungeni iweje ishindwe kufanya hivyo kwa Mradi wa Bagamoyo? Kwa faida za ajira na kodi zinazokuja na mradi wa Bagamoyo kwa hakika zinazidi faida za mradi wa bomba la mafuta ambalo sehemu kubwa ya ajira zake zitatokea wakati wa ujenzi wa bomba lenyewe na likishakamilika ajira zitapungua kwa 80%.

Ukiachilia faida za moja kwa moja zilizotajwa kuhusu mradi wa Bagamoyo, ni wazi kwamba ujenzi wa mradi huo pia utasaidia kuufanya mradi wa reli ya Kati ya Standard Gauge kupata idadi kubwa ya mizigo ya kusafirisha ili uweze kurejesha mikopo iliyochukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo. Serikali yetu inashindwa kuona fungamanisho hili kati ya Mradi wa Reli ya Kisasa na Mradi wa Bagamoyo SEZ? Kwa ujumla na vyovyote iwavyo, faida za mradi wa Bagamoyo SEZ ni kubwa kuliko madhara tunayodhani tunayaepuka.

Athari za Maamuzi Haya Kiuchumi na Kidplomasia

Inawezekana kuwa sababu zinazotajwa hadharani sio sababu haswa zilizopelekea Mradi wa Bagamoyo SEZ kusitishwa. Sababu zisizotajwa zinatamanisha kuzifahamu. Tuna wajibu wa kuzitafuta hizi sababu zisizotajwa. Kama zinazotajwa ndio sababu basi si sababu maana hazina mashiko kulinganisha na faida kubwa za mradi huu kwa Taifa, na hasa Ajira na kwenye kukuza nafasi ya nchi Katika dunia ya Usafirishaji.

Nimalize kwa hoja ambayo sasa kama Tanzania tunapaswa kuwa nayo makini sana. Kwa miaka ya Hivi karibuni nchi yetu imeanza kupoteza heshima yake kimataifa na hata kuelekea kupoteza marafiki wa kudumu (all weather friends). China na Oman, nchi ambazo zilikuwa zishirikiane na Tanzania kwenye mradi wa Ukanda Maalumu wa Kiuchumi wa Bagamoyo (Bagamoyo SEZ) ni nchi muhimu sana kwa historia ya Tanzania.

China ilipoanzisha mikutano na Afrika (FOCAC) mwaka 2000 ni nchi 4 tu za Afrika zilihudhuria ikiwemo Tanzania. Hivi sasa FOCAC inahudhuriwa na marais wengi zaidi kuliko Mkutano wa AU wa kila nusu mwaka. Rais Magufuli hajahudhuria mkutano hata mmoja wa FOCAC tangu aingie madarakani na hivyo kutoonana na Rais wa China kuzungumzia masuala ya Maendeleo ya nchi zetu hizi. Mradi wa Bagamoyo ulikuwa mradi muhimu mno kwa wazo la Rais wa China la ‘Belt and Road Initiative’. Kutofanikiwa kwa mradi huu ni udhaifu wa kidiplomasia wa nchi yetu na udhaifu huu una gharama kubwa kwa Maendeleo ya nchi yetu.

Mshirika mwengine wa mradi huu ni nchi ya Oman. Oman Ina historia kubwa kwa Tanzania na hususan Zanzibar. Katika raia takribani milioni 5 wanaoishi Oman, takribani nusu yake wanaongea kiswahili. Kama kuna nchi ambayo Tanzania inapaswa kuwa na mahusiano nayo ya karibu zaidi nje ya Afrika ni Oman. Hivi karibuni Oman imekuwa ikijitahidi kuimarisha mahusiano yake na Afrika Mashariki na Mradi wa Bagamoyo ilikuwa ni moja ya Miradi ya kuonyesha nia na dhamira ya dhati ya Serikali ya Oman kuboresha mahusiano na Tanzania.

Oman inaagiza takribani vyakula vyote kutoka nje, na Tanzania ingeweza kufaidika sana na soko la Oman kwa Bidhaa za kilimo na mifugo. Hivi sasa nchi zinazofaidika ni India na Sri Lanka. Mradi wa Bagamoyo ulikuwa mradi muhimu sana kuifungua Oman kwa Tanzania. Kutofanikiwa kwa mradi huu ni udhaifu wa kidiplomasia wa nchi yetu na udhaifu huu una gharama kubwa kwa Maendeleo ya nchi yetu kiuchumi, hasa kwa wakulima na wafugaji.

Jambo linalonishangaza kwa Serikali hii ya Awamu ya Tano ni uwezo wake wa kukumbatia miradi inayotoa Fedha nje (outflows) na kuua miradi yote iliyoikuta ya kuleta fedha nchini (inflows). Mradi wa kinu Cha kuchakata Gesi Asilia cha Lindi (LNG) wenye thamani ya USD 30 bilioni (TZS 69 Trilioni) umecheleweshwa, Mradi wa Uwekezaji kwenye Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Liganga wenye thamani ya USD 3.5 Bilioni (TZS 8.05 Trilioni) nao pia umecheleweshwa, na sasa Mradi wa Ujenzi wa Ukanda Maalumu wa Kiuchumi wa Bagamoyo kuifanya Tanzania kuwa Kituo Kikuu Cha Usafirishaji Afrika nzima, wenye thamani ya USD 10 Bilioni nao umesitishwa.

Utekelezaji wa miradi hii mitatu ungerahisisha sana utekelezaji wa miradi ambayo Serikali inafanya sasa. Mradi wa LNG ya Lindi ungeipa nchi mabilioni ya fedha za Kigeni kutekeleza mradi wake pendwa wa Stiegler’s Gorge kama ingekuwa kuna haja kuendelea nao. Mradi wa Mchuchuma na Liganga ungewezesha kuzalisha Mataruma ya Reli hapa hapa nchini kujengea Reli ya SGR na kuokoa mabilioni ya Fedha za Kigeni tunayotumia kununulia mataruma nje ya Nchi. Mradi wa Bagamoyo ungeleta mizigo yote ya Afrika hapa Tanzania na Reli mpya kupata Biashara na hivyo kupata faida ya Uwekezaji.

Iweje sasa maamuzi yawe kuchelewesha na kufyeka miradi muhimu kama hii? Hakika Sina majibu ya maamuzi ya namna hii, ila najua ni maamuzi ya hovyo yasiyo na faida kwa Taifa letu.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Mbunge, Kigoma Mjini
Mei 12, 2019

NILIAMINI NIKO SAHIHI, LEO MAMA UMETUSHINDIA.

Na Yericko Nyerere

Hureeeeee vita vyetu kwa maslahi ya Taifa tumeshinda! Asante Rais Mama Samia suluhu Hassan, nilimpinga Magufuli alipositisha mradi huu kwa hoja dhaifudhaifu na za uongo wa kiwango cha rami. Nikampinga baada ya kufariki baada ya wapambe wake kuendelea kukomaza shingo.

Now naweza kusema Mama umetuheshimisha sisi wataalamu tuliofanya kazi kubwa kujenga hoja na kushauri umuhimu wa mradi huu kwa maslahi ya Taifa kwa uchumi wa Reli ya SGR.

Naomba niwarejeshe nyuma miaka miwili iliyopita 22 December 2019 nilipoandika Makala nikipinga hotuba ya Rais Magufuli akikataa kuendelea na ujenzi wa Mradi ya Bandari ya Bagamoyo, nilipinga hoja alizozijenga Rais ili kuhalalisha katazo lake juu ya mradi husika.

Nilieleza wazi kwamba, Kuna mambo katika nchi yanahitaji uchunguzi kubaini pengine kuna hujuma katika taifa, hii inatokana na michakato mingi muhimu ya kichumi na kijamii imekuwa ikiishia njiani na kuliacha taifa katika hasara kubwa. Hii ni hujuma inahitaji mwarobaini kulitibu.

Mifano ya michakato ambayo kwamiaka mingi imeikuwa ikiishia njiani ni kama vile sekta ya nishati ambapo uzalishaji wa umeme limekuwa jambo linalotumiwa kama mchakato wakuzuka na kufa kwa miaka mingi sana tangu mwaka 1994 ilipokuja kitu kinaitwa umeme wa dharula kuokoa taifa (IPTL), ikafata michakato mingi yenye kuumiza taifa na haikufanikiwa hadi tukafika kuchimba Gesi mtwara tukapoteza mabilioni, gesi hadi Kinyerezi, kufumba na kufumbua mradi umetelekezwa sasa tunaimba mradi wa Bonde la Rufiji. Twende tuendelee..

Serikali ya awamu ya nne ilianzisha mradi wa kimkakati kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara duniani, mradi huu ilikuwa ni kujenga bandari ya Bagamoyo kwa ubia kati ya China na Omani wenye thamani ya dola bilioni 10, Serikali ya Tanzania katika mradi huu ilikuwa haiweki pesa yoyote isipokuwa ardhi na raslimali zingine, huku Uchina na Omani wakiweka mtaji na utaalamu.

Kwamjibu wa mapendekezo ya mkataba wa awali wa mradi huo, ni kwamba kungeundwa chombo maalumu cha nchi zote tatu ambacho kingekusanya mapato ya mradi huu na kusimamia gawio la pande zote, hii inamaana kwamba TRA ya Tanzania isingekuwa na haki ya kukusanya mapato moja kwa moja kutoka katika mradi badala yake ingekusanya gawio toka kwa chombo cha wabia kinachokusanya mapato ya mradi wa nchi zote tatu.

Huu ni moja ya mradi ambo kimsingi ulikuwa umeitangazia dunia vita vya kiuchumi toka kwa washindani wetu ambao ni nchi jirani na zinazotuzunguka. Kwakuwa Afrika yote ingepokelea bidhaa zake toka ulimwenguni hadi Bagamoyo, sawa na ilivyo Dubai ambayo ndio mlango wa Afrika kupokelea bidhaa zake.

Afrika inaingiza bidhaa toka Uchina kwa 88.8% na kiwango cha 98% ya bidhaa hizo zinapita Dubai. Hivyo kujengwa kwa Bandari ya Bagamoyo kungefunga nyia ya Dubai na bidhaa zote za Afrika kutoka China kupita Bagamoyo. Hii inamaana kwamba uchumi wa Dubai na Marekani ambayo ndio mdau mkuu ungemegwa. Mradi huu ulikuwa ndio msingi halisi wa kuanzisha mradi wa reli ya kisasa ya SGR, bila Bandari itakayozalisha mizigo kwa wingi SGR itakuwa ni kwakubeba abiria tu badala ya mizigo.

Serikali ya awamu ya tano katika hali ya kustaajabisha imeutupilia mbali mradi huo kwakutoa sababu ambazo hazina nguvu na zingine za kushangaza sana, mimi naitafsiri kama ni hujuma kwa taifa, izingatiwe kuwa tayari taifa lilishaingia gharama kubwa kuanzia kwenye upembuzi yakinifu, na kusaini mikataba ya awali. Kitendo cha kusitisha katika hatua hii ni kulitia hasara taifa. Moja ya hoja zilizotolewa na rais kama sababu ni kwamba masharti ya wabia nikuwa TRA hairuhusiwi kukusanya mapato, hoja hii ya Rais alikuwa sahihi lakini bahati mbaya alishindwa kufafanua wazi sababu za TRA kutokuwa miusanya mapato ya ubia. Pengine hili Rais alidanganywa.

Pili rais alisema kuwa masharti ya wabia nikuwa Tanzania hairuhusiwi kuendeleza bandari zake zingine. Hoja hii nayo inautata mwingi sana, Bandari zingine zote ziko kwaajili ya ndani, na mradi huu ulikuwa kwa shughuli za kimataifa. Sasa hoja ya kuwa tusikarabati bandari zetu zilizopo ni hoja isiyo na mashiko, Hili inawezekana kabisa Rais hakuambiwa ukweli.

Hoja ya Tatu aliyoitumia Rais Magufuli kukataa mradi ule, ilikuwa kwamba, wabia wanataka wapewe umiliki wa ardhi kwa miaka 99. Hili si la mwekezaji bali la sheria zetu ambazo zinatoa uwekezaji katika ardhi kwa miaka 33 hadi 99. Sasa hoja hii haiwezi kuwa kwa wabia wawili tu kati ya watatu ikiwemo Tanzania yenyewe. Hili nalo kuna uwezekano watu waliamua kumpotosha rais wetu.

Chakusikitisha kwa nchi yangu, Katikati ya mvutano wetu na wabia hadi Rais Magufuli kusitisha mradi, Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kwakutumia majasusi wake waliotanda kila pembe ya Afrika na kwingineko, amefanya mageuzi makubwa, amechukua wazo lilelile ambalo limekataliwa Dar es Salaam na wajuvi, amekwenda kulisimika katika Bandari ya Nacala kwakuingia ubia na Wachina kwa Dola bilioni 5 za Kimarekani, hii ni Bandari inayotarajiwa kuwa lango kuu la kiuchumi Afrika.

Wakati hili halijapoa, Mwaka 2017 tu juzi Tanzania tulipowazuia wazungu wasisafirishe madini ghafi na makinikia yao, tuliimba nyimbo kwamba Tanzania itajenga vinu vya kuchenjulia madini hapahapa, na nyimbo ziliimbwa kisiasa zikaitikiwa kishabiki kwa beti za kinafiki kwelikweli. Leo nyimbo haziimbwi, hakuna anayejua kama viwanda vimeshajengwa au laa na hakuna anayehoji hilo kwakuwa ukihojihoji tu basi ukinusurika sana utaenda mochwari au Ubelgiji, tulishazoe vimbunga kwamba vitavuma na kutulia.

Lakini huku sisi tukiwa tumebadili nyimbo sasa tunaimba nyimbo za Standard Gauge nk, Rwanda kwakutumia majasusi wao waliotanda kila pembe ya Dunia, imelichukua wazo lilelile la Tanzania imejenga vinu vya kuchenjulia madini na inatarajiwa kwamba hadi 2024 Rwanda iwe ndio nchi ya kwanza barani Afrika inayosafirisha madini kwa wingi nje ya Afrika. Kumbuka na elewa Rwanda sio mzalishaji wa Dhabu, Almasi wala chochote kiitwacho madini isipokuwa kwenye kilimo cha chai na kahawa huko. Hivyo anategemea viwanda vyake vipokee madini ghafi toka Tanzania, Kongo, Zambia akusanye kodi yake na kugonga muhuri wa madini unaotambulisha kuwa ni madini toka Rwanda nk. Sisi tumelala. Siasa inanguvu bana.

Kwa maoni yangu ninafiki kuna tatizo kubwa kwenye eneo la Ujasusi katika nchi yetu, hasa ujasusi wa Kiuchumi, na hili ndilo lilikuwa msingi wa mimi kuandika Kitabu changu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi. Michakato mingi ya kiuchumi katika nchi hii imekuwa haina mafaa ama inaliacha taifa katika makovu makubwa yasiyozibika. Hii inazaa uhalali wa kuhitaji mageuzi makubwa katika Idara ya Ujasusi nchini kuanzia kwenye ideology, sheria, misingi, kanuni, na mambo anuai ndani ya idara ya ujasusi nchini.

Ujasusi kwa nchi zilizoendelea kama China, Israel, Urusi na Marekani, unafanywa na watu ambao ni smart na wanajengwa kuwa smart ili kuweza kumudu ugumu wa kazi hiyo na kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa. Majasusi katika nchi hizo hawapewi kazi kwasababu ya ujomba ujomba na kujuana.
Ni kweli asilimia kubwa ya information's zenye thamani katika kazi ya ujasusi huwa zinaletwa na "human intelligence" badala ya magazeti, TV na source nyingine za habari.

Kwa maana hiyo basi ni lazima kuwe na watu competent ambao wana uwezo wa kukusanya habari za kijasusi ili tuweze kupata information's za maana na kujenga uwezo wa kuzifanyia kazi informations hizo. Imagine wakati ule wa vita baridi jinsi Directorate 16 ya KGB ilivyoweza kufanya kazi ya kununua sensitive navy information za USA na kuweza kutengeneza balance ya navy fleet bila USA kugundua kwa miaka 17 kupitia kwa Johny Walker junior!

Tanzania kwenye balozi zetu kuna majasusi. Lakini ni majasusi wa aina gani? Wale wa kujua kuongea kifaransa na kireno na lugha nyingine za mataifa ya nje bila upeo wowote wa Technologia? Kama kuna sehemu tunakosea basi ndio hapo. Majasusi wengi wa Tanzania au tunaoambiwa kuwa ni watu wa system wengi katika tafsiri ya kijasusi ni "informers". Ujasusu kama ujasusi hapa Tanzania ni kama hakuna. Usalama wa Taifa au TISS/UWT msingi wao uliounda chombo hiki ni "power defensive", yaani wajibu mkubwa unaelekezwa kwenye kumonitor mwelekeo wa kisiasa Tanzania hasa kuwadhibiti oppositions na elements zote za upinzani na assasinations za elements zozote zinazoonekana kuwa against na himaya ya CCM.

Idara ya Usalama wa Taifa hii tuliyonayo leo ilianzishwa na CCM 1997 kutoka katika muundo wa kijamaa wa chama kimoja, hii ni baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo bado unaiserve CCM kwanza kisha Taifa linatafsiriwa salama kupitia matokeo ya uimara wa ccm, kama yakifanyika mageuzi ya kimuundo, kisheria, kikanuni na kisera, uimara wa Taifa hautatafsiriwa kupitia uimara wa ccm madarakani, na mambo mengi tunayolalamikia sasa juu ya taifa hayatakuwepo tena. In simple words, taswira kubwa inayoonekana yauhakika ni kazi yao ya kulinda viongozi, kusafiri na viongozi na kuilinda CCM.

Nje ya mambo ya Ujasusi wa Kiuchumi ambao mimi ndio ninaoupigania siku zote uongoze nchi, Naweza kusema Tanzania tuko vizuri katika Ujasusi wa kidola kuliko nchi yoyote pengine Afrika nzima, Hili limefanya kuimeza idara na kuonekana siasa ambazo ndio zinabeba taswira kubwa ya ubora ama udhaifu wa ujasusi Tanzania, Eneo la Ujasusi wa Kidola Tanzania kuna vitengo vya wachapakazi hasa kiko jeshini.., kitengo cha ujasusi ambacho kilikuwa kiko free from politics party ni CMI (central military intelligence). Lakini bahati mbaya muundo na aina ya uongozi wa Magufuli ulikiingiza katika siasa pale kilipofanywa kuwa decision maker wa nchi, lakini upande wa foreign assets ndio wazuri sana wako bize kukusanya taarifa hatarishi dhidi ya nchi...

Kwahatua hii naomba niseme wazi, Mradi wa Bagamoyo ulitakiwa uanze kabla ya Bwawa la Nyerere kule Rufiji ama ungeanza kabla ya SGR, Now sasa nasema taifa linakwenda kushinda vita vya kiuchumi afrika mashariki na kati.

Kuanzia sasa atakayempinga mama nitamloga nitamloga
 

Attachments

  • VID-20210627-WA0003.mp4
    2.2 MB
  • VID-20211118-WA0015.mp4
    15.5 MB
  • VID-20211118-WA0038.mp4
    11.2 MB
Kwamba Bagamoyo itakuwa ni centre ya kupokea meli kubwa na kisha kupakua mizigo na kupakia kwenye meli ndogo kuzimbaza barani Afrika na Mashariki ya mbali.

Kwamba hata mizigo ya Tanzania itahudumiwa na bandari ya bagamoyo kisha mizigo kupakiwa kwenye malori kwenda mikoa ya Pwani na Bara.

Sasa bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara zitafanya kazi gani kwa sababu hata Malawi, Zambia Uganda Rwanda, Burundi na Congo watahudiwa na Bandari ya Bagamoyo!

Ramadhan Kareem.
 
According to prof assad, profitability ya ndege hutegemea loading capacity na masaa mangapi ndege iko hewani.

Je, loading capacity ya meli kubwa kubwa (refer zitto) itatoka wapi wakati nchi yetu na majirani zake ni maskini? Nani ataleta meli? na Meli hizo zitabeba nini kutoka wapi na kwenda wapi?
 
Bandari ijengwe maana itafungua fursa zaidi kuliko iligyo sasa

Hofu yangu ni je wawekezaji wale bado wako tayari kuwekeza au ndio wameshasepa maana tayari Lamu inafanya Kazi na bandari yenye ukubwa karibu na huo inajengwa Msumbiji kwa hiyo ile potential huenda kwa sasa ikawa haipo na wawekezaji wakasita kuleta pesa zao.

Mwisho Serikali ya mama ifanye tathmnini ya mradi na kuona kama wanaweza kuendelea nao na huu ndio utakuwa legacy yako mama itakahoishi miaka na miaka,kizazi na kizazi.

Hata hiyo sgr yenu Ili iwe na tija ni lazima kupatikane bandari kubwa itakayoweza kuifanya iwe operational vinginevyo maskini wa nchi hii hakuna siku watakuja kuona unafuu wa maisha
 
according to prof assad, profitability ya ndege hutegemea loading capacity na masaa mangapi ndege iko hewani
Je loading capacity ya meli kubwa kubwa (refer zitto) itatoka wapi wakati nchi yetu na majirani zake ni maskini? Nani ataleta meli? na Meli hizo zitabeba nini kutoka wapi na kwenda wapi?
Ni muhimu sana kusoma kabla ya kukurupuka,bandari kubwa ukanda wote wa Afrika unauliza nani ataleta meli? Kwani zinazotua dar kea sasa au mombasa serikali inazileta?

Afu uelewe maana ya kuwa lango na mfano wake ni ule wa port ya Dubai ambako 80% ya bidhaa zinazokuja Afrika zinapitia ,so kwa kuwepo Bagamoyo means kuchukua japo 20% ya share yake tayari ku lisha Afrika.

Tuulizane sgr ya tani zote hizo inajengwa itabeba mzigo gani wakati kabandari hakaruhusu mzigo mkubwa?

Afu tunavyodelay ndivyo Lamu na nakala ports zitakavyotake advantage .Nchi za kijamaa ni tatizo Sana maana watu ni waoga wa kutake risks as if Dunia inakusubiria.

Hii ni sawa na kusema eti tusivune madini tusubirie vizazi ,hii ni nonsense yeknology inabadilika huenda yakawa useless huko baadae lazima tuyavune sasa Ili tujenge msingi wa uchumi imara na kuandaa kizazi kijacho
 
1) Bandari ijengwe ila.masharti magumu katika huo.mkataba pia yaangaliwe

2) Bandari ijengwe kwa pesa za ndani..hata kama itachukua miaka 23 Ili kuhakikisha faida yote inaingia Serikali.

3) Bandari ijengwe kwa kushirikiana na hizo nchi Kama Ilivyo..Kisha kuundwe kampuni ya pamoja Kama Ilivyo swala kwenye Mambo ya gesi na madini, kampuni hio iwe na wajumbe sawa kutoka kila nchi na pia zipokezane kwenye nafasi ya CEO wa hio Bandari kwa kipindi cha miaka miwili miwili...

faida inaweza kugawanywa kwa kuzingatia nani kawekeza kiasi Gani,..ama faida kila nchi ipokezane kwenye kuchukua faida..mfn.mwaka huu ni tz, mwakani ni China, mwaka ujao keshokitwa ni oman mpaka hao wakorea.

4) Bandari isijengwe mpaka.pale Taifa litakapokuwa na uwezo wa kuijenga yenyewe bila kuhitaji msaada kutoka nnje..

5) Badala ya kuhangaika na hio Bandari ya bagamoyo Tanzania iwashawahishi hao wawekezaji..wajoin kwe mpango wa kuiboresha na kuipanua Bandari ya sasa ya Dar..ikiwemo kuongeza ukubwa wake wa eneo..kwa kuchimba kina bahati I..na kuvunja baadhi ya majengo ikiwemo feri na soko lake..na ofisi zingine pale Ili kupata eneo kubwa sawa na la bagamoyo Ili kuufanya eneo hilo lifanane na eneo la bagamoyo
 
Kama tumeweza kujenga S. G. R na kununua ndege kwa kutumia trillions zetu wenyewe, kwanini tushindwe kwenye bandari.

Tanzania tujipange kuimarisha vyanzo vyefu vya fedha tujenge bandari kwa hela zetu, ikishindikana kabisa tukope hela kwenye mabenki makubwa duniani tukamilishe huo mpango maana hawa wawekezaji ni wazi wana agenda yao chafu
 
Kama tumeweza kujenga S. G. R na kununua ndege kwa kutumia trillions zetu wenyewe, kwanini tushindwe kwenye bandari.

Tanzania tujipange kuimarisha vyanzo vyefu vya fedha tujenge bandari kwa hela zetu, ikishindikana kabisa tukope hela kwenye mabenki makubwa duniani tukamilishe huo mpango maana hawa wawekezaji ni wazi wana agenda yao chafu

Sawa ujenzi wa Bwala la umeme ni 7trn, SGR ni 7trn, tukiamua tunaweza huo mradi ni 23trn tu.
 
According to prof assad, profitability ya ndege hutegemea loading capacity na masaa mangapi ndege iko hewani.

Je, loading capacity ya meli kubwa kubwa (refer zitto) itatoka wapi wakati nchi yetu na majirani zake ni maskini? Nani ataleta meli? na Meli hizo zitabeba nini kutoka wapi na kwenda wapi?
hujui kuwa hujui, pole.
 
Kama tumeweza kujenga S. G. R na kununua ndege kwa kutumia trillions zetu wenyewe, kwanini tushindwe kwenye bandari.

Tanzania tujipange kuimarisha vyanzo vyefu vya fedha tujenge bandari kwa hela zetu, ikishindikana kabisa tukope hela kwenye mabenki makubwa duniani tukamilishe huo mpango maana hawa wawekezaji ni wazi wana agenda yao chafu
Dah! bado unaamini uliyoyaandika hapo?
Tukipata 30% ya Watanzania wenye fikra kama yako tuiombe UN utuletee Mkoloni.
Tuwe Watumwa tu.

Ni aibu na kichefuchefu unachosema.
.
Kwani humu mtandaoni unafanya nini mkuu?
Inaelekea huna unachoelimika nacho.
 
Back
Top Bottom