Xavi Hernandez yupoje wadau,
Navutiwa na uthubutu wake wa kuwapa nafasi vijana, naamini muda huu alvaro fernandez, zidane iqbal, kobbie, gore, hannibal, forson, garnacho.

wote wangelikuwa na uhakika wa kuwepo klabuni.

Nafahamu erik ten hag anajitahidi kwenye eneo hilo.

Nafikiri Xavi ameangushwa na watu wabovu waliopo barcelona si kwamba ni layman kiasi hicho.

Anaweza kuwa mrithi mzuri wa alonso au de zerbi roberto kwa timu zao.
 
18-year-old Habeeb Ogunneye is in the #mufc squad to face Nottingham Forest in the FA Cup this evening. Ogunneye is a right-back.
[@AcademyScoop]
1709145253663.png
 
GettyImages-8516562111547206112908_large.jpg

Hapa Anderson na Forster wanashangilia wenyewe.
Hii timu kuna WAZZA, VAN DER SAR , J.S PARK, Hawapo ilikuwa na Ubora kila Mahali, Picha karibu wachezaji 8 ni "World Class"

Ukweli Mchungu ni kwamba Tumeshuka sana kuanzia kiutendaji mpaka kiuchezaji. Nyakati za Nyuma timu nyingi UTD ndo ilikuwa mfano wao ndo walikuwa wanachukua Viongozi toka UTD, Wachezaji na kuiga Mpaka Uendeshwaji.

Leo Hii timu Yetu Nahodha ni BRUNO, Jamaa anajilalamikia Mpaka yeye Mwenyewe! Tukimkosa Licha mfumo mzima unabadilika kiuchezaji.

Msimu ulopita tumecheza na kina Weghorst lakini una Uhakika na timu, ETH aliwaambia fans tukutane Wiki ijayo tunaitoa Barca, walianza pata goli ila kwa uchezaji wetu ulikuwa unajua tutawafunga tu na ndicho kilichotokea, FRED, WEGHORST wanaeza wasiwe Madaraja ya wachezaji wa UTD lakini walikuwa na ile Ari ya Wachezaji asili wa UTD.

Rashy anapiga Mpira nje anatupa mikono juu anarudi anafanya Jogging. WAZZA, TEVEZ walikuwa wanakuja kama MBOGO na kizuri wakiwa na Mpira wana Ubora, Rashy anaweza kokota Mpira akampelekea Beki mguuni!

Palace, Nottingham, W/ham, Everton, Luton, Sheffield, zinashindwa chukua Watu wao kwa sababu tumewafunga na Mikataba mikubwa.
 
Palace, Nottingham, W/ham, Everton, Luton, Sheffield, zinashindwa chukua Watu wao kwa sababu tumewafunga na Mikataba mikubwa.
:D:D:D hapa nimepapenda zaidi.
Ni ukweli usiopingika tumeshuka sana kiubora katika nyanja mbalimbali ila kinachonipa hofu zaid ni kwamba tunaona tumeshuka lakini hatujali sana.
Tunajidanganya tunataka kocha na wachezaji wanaocheza the united way ila wakati tunasajili hatufanyi sajili za namna hiyo,tunafanya sajili ili kuuza jersey na kupata mikataba bora ya udhamini.
 
Back
Top Bottom