Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

INEOS wasipofanya operesheni ya moyo hawatofika mbali.

  • Eriksen mwili wake hautaki tena kugombania mpira.
  • Tukubali makosa ya kusajiliwa wan bissaka, level yake ni crystal palace.
  • Varane bado ana kitu mguuni lakini mwili hautaki tena, majeruhi yasiokwisha huku akiramba mshahara mkubwa.
  • Kulipa millioni 60 paundi kwa casemiro mwenye miaka 30 kwenye dunia yenye ruben neves, palhinha ni kosa jengine la kutoipa umuhimu future.
  • Kwanini tulimsajili Onana ikiwa mfumo wetu wa uchezaji ni ule ule, tujiulize amekuja kuongeza nini, hapa kipara awajibike.
  • Tuache tabia ya kupapatikia wachezaji kwa hoja mfu, tuliwahi kukataa kumuuza lingard kwenda newcastle kwa hoja ya kumuimarisha adui, msimu huu klabu imekataa 30 millioni kwa scott mctominay, ni kichekesho.
  • Klabu ya mpira si hisani, luke shaw aonyeshwe mlango wa kutokea, amekosa mechi nyingi sana kwa hoja ya majeruhi na pia hana consistency.
  • Nguvu aliotumia kipara kumgombania amrabat hailingani na anachomfanyia, hapa tumelipa paundi millioni 10 kwa mkataba wa mwaka mmoja, kosa jengine la kipara.
  • Victor lindelof hawezi kuwa na miujiza na hatokuwa na miujiza.
Ni mchakato unaoweza kuchukua madirisha mawili makubwa ya usajili.
Ukiondoa Simba na Kaizer Chiefs Man United ndiyo timu inaendeshwa hovyo zaidi duniani kwa vilabu vikubwa.

Wachezaji walioko United hawawezi kuwa sehemu ya kikosi chochote cha vilabu vikubwa Uingereza,Spain au Bundesliga.

Tuna idadi kubwa ya wachezaji wanaopaswa kuhamia Serie A.
 
Sisi ni tofauti na chelsea linapokuja swala la kuuza wachezaji (hatuna mvuto)
Tupo ovyo sana eneo hilo ndio maana nimeweka madirisha mawili ya usajili.

Vile vile hatuna nguvu ya kureplace wachezaji 10 kwa mkupuo kwa sababu sisi hatufanani na Yanga au Simba.
Open heart surgery ya Ralf ilikuwa na maana kubwa sana kama ingezingatiwa tungekuwa tulishaondoa.
Lindelof, Shaw, Fred, Bissaka, Antony, Brandon, Eriksen, Varane, na Martial. Kwa dirisha moja tu.
 
Leo hio tuko na Nottingham Forest halafu ukuta wa Berlin Harry Maguire atakosekana uwanjani huku Bruno na Varane hakuna uhakika kama watakuwepo.
Hofu yangu ni Forest kuondoka na Clean sheet maana timu inaingia uwanjani bila ya uwepo wa goal scorers muhimu Hojlund na Maguire.
Kama vile nawaona kina Awoniyi, Elanga, Hudson-Odoi na Morgan Gibbs White wanavyochekelea
Halafu jumapili tuko na Man City yaani mpaka tuseme Baba ubaya pale Carrington hua anafundisha Rugby au rede.
1709107160167.jpg
 
Xavi Hernandez yupoje wadau,
Navutiwa na uthubutu wake wa kuwapa nafasi vijana, naamini muda huu alvaro fernandez, zidane iqbal, kobbie, gore, hannibal, forson, garnacho.

wote wangelikuwa na uhakika wa kuwepo klabuni.

Nafahamu erik ten hag anajitahidi kwenye eneo hilo.

Nafikiri Xavi ameangushwa na watu wabovu waliopo barcelona si kwamba ni layman kiasi hicho.

Anaweza kuwa mrithi mzuri wa alonso au de zerbi roberto kwa timu zao.
 
18-year-old Habeeb Ogunneye is in the #mufc squad to face Nottingham Forest in the FA Cup this evening. Ogunneye is a right-back.
[@AcademyScoop]
1709145253663.png
 
GettyImages-8516562111547206112908_large.jpg

Hapa Anderson na Forster wanashangilia wenyewe.
Hii timu kuna WAZZA, VAN DER SAR , J.S PARK, Hawapo ilikuwa na Ubora kila Mahali, Picha karibu wachezaji 8 ni "World Class"

Ukweli Mchungu ni kwamba Tumeshuka sana kuanzia kiutendaji mpaka kiuchezaji. Nyakati za Nyuma timu nyingi UTD ndo ilikuwa mfano wao ndo walikuwa wanachukua Viongozi toka UTD, Wachezaji na kuiga Mpaka Uendeshwaji.

Leo Hii timu Yetu Nahodha ni BRUNO, Jamaa anajilalamikia Mpaka yeye Mwenyewe! Tukimkosa Licha mfumo mzima unabadilika kiuchezaji.

Msimu ulopita tumecheza na kina Weghorst lakini una Uhakika na timu, ETH aliwaambia fans tukutane Wiki ijayo tunaitoa Barca, walianza pata goli ila kwa uchezaji wetu ulikuwa unajua tutawafunga tu na ndicho kilichotokea, FRED, WEGHORST wanaeza wasiwe Madaraja ya wachezaji wa UTD lakini walikuwa na ile Ari ya Wachezaji asili wa UTD.

Rashy anapiga Mpira nje anatupa mikono juu anarudi anafanya Jogging. WAZZA, TEVEZ walikuwa wanakuja kama MBOGO na kizuri wakiwa na Mpira wana Ubora, Rashy anaweza kokota Mpira akampelekea Beki mguuni!

Palace, Nottingham, W/ham, Everton, Luton, Sheffield, zinashindwa chukua Watu wao kwa sababu tumewafunga na Mikataba mikubwa.
 
Palace, Nottingham, W/ham, Everton, Luton, Sheffield, zinashindwa chukua Watu wao kwa sababu tumewafunga na Mikataba mikubwa.
😀😀😀 hapa nimepapenda zaidi.
Ni ukweli usiopingika tumeshuka sana kiubora katika nyanja mbalimbali ila kinachonipa hofu zaid ni kwamba tunaona tumeshuka lakini hatujali sana.
Tunajidanganya tunataka kocha na wachezaji wanaocheza the united way ila wakati tunasajili hatufanyi sajili za namna hiyo,tunafanya sajili ili kuuza jersey na kupata mikataba bora ya udhamini.
 
Back
Top Bottom