severinembena
JF-Expert Member
- Jun 2, 2018
- 2,435
- 2,397
Daaa hao wahuni wana zali sanaMapacha wa Tatu wa Mr.Nice Guy.
Jose Moja ya kocha ambaye sjawahi kuwa muumini wa Soka lake(Soka la Uoga),Japo naheshimu Mafanikio yake dimbani.
Juzi alivyokuwa akihojiwa aliongea jambo la Msingi sana Ukiwa Ukiwa Mr nice guy sahau kapata mafaniko makubwa dimbani,kama ukiweza kuweka walau uwiano sawa Mr nice guy vs Ruthless(devil May care )itafaaa zaiidi.
A Ruthless SAF hakuwa na utani kidogo,siku Moja aliwahi kuulizwa na shabiki wa Man U,
Mbona sjawahi ona tabasamu lako Uwanjani..?
SAF akajibu sipo hapa kutoa tabasamu,Tabasamu utapewa na mkewe...nipo hapa kutoa burudani na kupata Ushindi.
Wakina Mr nice guy Giggs watapa wakati mgumu kupata mafanikio makubwa dimbani.
Mr nice guy Mwinyi,Bwana Mashirika a.k.a Nyerere alimwambia wewe bwana ni Mwema sana,Mtu safi lakini kama kiongozi wewe ni dhaifu.
(Uongozi na Hatima yetu by Nyerere ).
Sosha anauthubutu kuwaondoa wachezaji Mizigo,wavivu,Uwezo mdogo Uwanjani kama alivyowahi kutamba na kauli zake...?
Au ni bwana asiyeweza kusimamia maneno yake...?
Nani top six Epl aweza kutoa mkataba miaka Mitatu kwa Jones Plus £120K....? mechi tano yupo gereji... (Labda bodi ya Man u wanamijihela tele)
Sosha aweza kufanya mabadiliko makubwa na kutuvusha mbali au twajivika Upofu wa Imani..
Nyota njema itaonekana Majira ya joto,Pamoja na madhaifu ya Uendeshwaji wa club(Glazzer & Ed)kocha lazima uwajibike kwa kazi yako..Japo Jose Ni kocha asiyependa kuwajibika anahamisha lawama kama aina ya viongozi wengi wa Africa.
Karata kubwa ya sosha iliyobakia ni Ulenged wa Man United Fc (Uvumilivu wa Mashabiki).
Inasemekana Jose alitaka kuwaondoa mizigo na wavivu wote ndani ya timu msimu wa pili,ghafla akiitwa na bwana Mapesa (Bank teller)Ed Woodward,
Ed akasema wewe bwana shida yako nini..? si ni pesa..? chukua fedha hii hapa,Hao uwaitao mizigo ni asset,Mishahara tunagharamia sisi.
Mchezaji anaweza kukaaa man u miaka mitatu hachezi lakini kalidhika anakula posho,anajimwayamwaya katika Jacuzzi wala hana hata presha...mfano Darmian.
Sosha anamlima Mrefu sana,kama atatangulizi Ujasiri ,Umafia akiongozwa na falsafa yake ya soka (Hata sjui huyu bwana kama kweli anafalsafa ya soka) ndio vitamvusha,la sivyo kichwa chake kabla ya mwana wa adamu kuzaliwa huko Bethlehem kitatolewa sadaka ya Kuteketezwa.View attachment 1099767View attachment 1099769View attachment 1099771