Hongera sana man u.
Ile trust iliyoyumba kipindi kile sasa imerudi.
Team spirit ya jana ilikua juu sana.

Ila bado tuna tatizo kwenye kukaba, tumewaruhusu tot kufika kwenye box mara nyingi sana.
Wachezaji wengi walikimbilia kukabia golini.

All in all points 3 zilikua muhimu sana.
Lets keep going, waliopo juu yetu wasiwasi tele!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mourinho ni Kocha mzuri sana kwa mbinu kuliko hata huyu OGS lkn tatizo ana ukoloni mwingi sn, kwani hapo unadhani OGS kuna anachofundisha kipya sana kuliko Wachezaji wenyewe kuwa na morali ya kujituma ili wapate matokeo mazuri?

Wachezaji walikuwa hawamtaki Mou tokana na mikwaruzano yake kila kukicha kati yake na Wachezaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa anayehoji uwezo wa Jose kama kocha, huwa siku zote ninamshangaa

Kwa anayehoji uwezo wa Jose kwenye Management, especially man management ninamuelewa vizuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila mashabiki sometimes hatupo fair kabisa linderlof huyu huyu ambaye mlikuwa mnamzodoa leo kawa lulu

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu mfano nimeupenda sana

Maana kuna watu (kama wewe) wanaamini mtu akitoa kauli huko nyuma kuhusu jambo flani basi hawezi kubadilika mbele ya safari kulingana na mazingira ya wakati huo

Kwa mtazamo huo huo watu waliokuwa pro Jose wana haki ya kubadilika kutokana na hali ya timu ilivyokuwa inaendelea kuzorota

Hapa nawaona watu flani waliokuwa wanamponda Matic (na ukimtetea wanakuita pro Jose) lakini sasa hivi wanamkubali hatari

Hivyo hivyo unaweza kushangaa ipo siku wanaomponda Fred sasa hivi wakaja kumfagilia mwaka mmoja baadae

Kati ya makocha walioanza vibaya pale United ni SAF, (obvious kuna watu walimponda kipindi hicho) lakini miaka 26 baadae akaitwa legend

Kuna United Fans Yutube Chanel moja inaitwa United Stand, operator wake anaitwa Mark, mwaka jana wakati VVD anaenda Liverpool alimuita Dutch Chris Smalling.

Lakini juzi amekiri kwamba VVD ni habari nyingine na ameibadili completely Liverpool defence na anatamani United asajili mtu kama Koulibally kufanya mapinduzi ya defence kama waliyoyafanya Liverpool bila kujali gharama. Kwahiyo jamaa akasema kwamba opinions change, na akasema opinions change with evidence.

Kwahiyo mambo ya kutoa povu kwa mtu eti kisa alikuwa ana mawazo flani na sasa amebadilika ni kutoelewa mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mashambulizi mengi yametokea kati na upande wa kushoto Shaw hakuwa vizuri na Pogba& Martial hawakuwa wanamsaidia kukaba while upande wa Young haukuwa na shida Sana na Herrera alikuwa anamsaidia Young kukaba.
De Gea amefanya 11 saves na 6 zilikuwa clear chance timu yenye clinical striker leo tungefungwa hata goli 4

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Kane ni clinical bhana

Halafu pamoja na ubovu wa Jones, jana amejitahidi kuwabana foward wa spurs akishirikiana na Lindelof

Kwenye mpira kuna mambo mengi, bahati pia ni sehemu ya mchezo

Lakini hata sisi tuliwakosakosa, wasijisahaulishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni kwamba Muna washabiki wengi kuliko nyuzi zote za Soccer humu JF na ndiyomana hata kipindi cha Mourinho plastic fans walipoukinbia uzi basi ulikuwa ukijaza page.

Kuhusu uzi kuwa Most Active si huu tu bali nyuzi zetu hazisogei sana kutokana na kuwa na Washabiki kidogo JF kiasi ya kwamba wanaocomment ni walewale tu.

Uzi uliokufa ni wa Arsenal Coz una Washabiki wengi JF kukaribia Man U lakini hausogei.
Still upo active

Imagine Mkuu kipindi kile hali mbaya lakini huu uzi bado ulikuwa unasogea japo sio kwa kasi hii ya sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mathematically Arsenal akishinda dhidi ya Chelsea itakuwa advantage kubwa kwetu. Mkuu unajua unahamu sana ya kutoka nafasi ya sita, ila fikiria, Chelsea katuzidi point sita, arsenal tuko naye sawa, just goal difference. So arsenal akishinda na sisi Tukishinda dhidi ya BHA Chelsea atadrop na kuwa only 3 points ahead. Hiyo ni advantage kwetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujataja kitu kimoja

Pia hata Arsenal akishinda, ni rahisi kuja kumkuta kuliko Chelsea japo wote hali ni tete

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa kubwa iliolifanya Man U ni kumfukuza The special one MOU.

Huu upepo mnapopitia nawaapia baada ya gane ya PSG tutarud hapa kuweka matanga upya na soon ile kampen yetu ya OLE-OUT itaanza rasmi.
Hongeren kwa ushindi mwembamba dhidi ya team nyepesi inayochipukia kama spurs, pia mshukurun sana De gea.
 
YOUNG....anakipiga mbele ya delle pale kisela mavi na undava undava manina anampa vikumbo na matusi ya chinichini kumtoa mchezoni...

JONES... kidogo nimeona leo akikaza ila bado mzito kwenye kumalizana na foward kwa wakati muafaka....

LINDERLOF... mmmhu huyu jamaa full mitatoo anakaba kama muuza kashata na pweza...manina yaani muuza pweza hata ule kwa siri namna gani ukimuuliza nimekula vingapi hakosei...

SHAW... ni stalet yenye speed 400 anatema mate kushoto anafukia kulia...

MATIC... Haha jitu kubwa la miraba 8 ***** ana mguu kama kwanja akishika mpira huchukui kama katengenez yeye...kama anapiga kumbe anafinya

HERRERA.. Hapa sasa ndo uelewe hakuna mwispania fala labda morata tu...jama kama hayupo anapiga pasi mbonyeo na buti za nyuma ya kisigino mbili tatu nje

LINGARD... the Mouse(panya) mjanja uwanjani sa hizi unamwona hapa baadae yupo kuleeeeee tayari kashatoroka ye kazi yake ni kuvuruga viungo wakabaji na mabeki kwa kudokoa mipira na kukimbia nayo....kiraka...

POGBA... jina kubwa duniani pasi za upinde wa mvua malamaaake...pasi inapigwa karikaoo hadi ubungo na inafika kwa mtu ukifata unategua nyonga...miguu kama buibui pasi za mauzi na chenga za kukera..

MARTIAL... hahah hajui kingereza hadi leo inajua chenga tu...***** akiwa na mpira anakufata kama mbwa wa polisi hakimbii mwizi.

RASHFORD... (boxer) yeye kazi yake moja tu kukimbia kama anarejeta kifuani *****...anafinya anapiga mashuti mbonyeo kipa huoni...miguu miembamba kama muwa wa kutengenezea sukari🤭

DE GEA... Malamamaaaaaake huyu sio binadam ni robot kama huamini nenda playstation utajione....msenge anaweza kudaka hata risasi,mabom,mbu,na rocket zote ziendazo kasi...jamaa ana mikona elfu kumi na kila mkono una kazi yake.....


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom