tumepumzika miezi mitatu, tunacheza na jose anatukumbushia adhabu tulioipata dhidi ya crystal palace pale old trafford...
  1. bado tunaendelea kuteswaa na team zinazojilinda mara mbili( breaking the lowblock imekuwa tatizo), na sielewi tatizo hili linasababishwa na nani (either kocha na mbinu zake au wachezaji tulionao pale mbele ni kikwazo).......
  2. ukikaa chini sana pindi unapocheza na united basi una asilimia kubwa sana ya kupata suluhu kwa sababu ya wachezaji tulionao pale mbele
  3. martial, james na hata rashford ni jamii ya wachezaji ambao hawapendi kushughulishwa na wapinzani hivyo basi muda wote hupendelea wawe huru (wawe na space itakayowawezesha kutembea watakapo, kumiliki mpira wapendavyo)
  4. mfano daniel james ni mchezaji ambaye ukimruhusu awe huru kwa umbali wa meter 5 tu anakuadhibu ila nje ya hapo hana miujiza yeyote hata kama utamkutanisha na masihi wa mpira
  5. ukiangalia mechi ya jana muda wote walinzi wa pembeni wa Spurs walikuwa chini (man to man) kukabiliana na winga zetu huku wakijua fika walinzi wetu wa pembeni hawana athari yeyote wanapofika kwenye eneo la adui (waliwapa free sana)
  6. pia namba 10 wao naye muda mwingi sana alikuwa anarudi chini kuongeza ulinzi kwa kutengeneza ukuta(block) dhidi ya midfield wetu (scott na fred ambao hupenda sana kutembea mbele), bila ya kumsahau sissoko pamoja na winks nao walizidi kuongeza ulinzi (spurs muda mwingi walicheza 4-2-2-1-1)
  7. mbinu yao ilipelekea team yetu ikose mipango yoyote itakayotuwezesha kuimiliki mechi (hatukuweza kupita pembeni na vile vile hatukuweza kutengeneza space, pace itakayopelekea defence yao ivunjike, si ajabu martial alikuwa haonekani akifanya cha maana
  8. hatuna mshambuliaji wa uhakika mwenye uwezo wa kuwafanya walinzi wa team pinzani wavunje defence line yao pindi wanapoamua kujilinda zaidi hivyo basi hata kama tungelianza na ighalo sidhani kama angelitupa maajabu yeyote, hapo ndipo unapowakumbuka washambuliaji mfano wa ronaldo delima, thierry henry, kun aguero, wayne rooney na wakati huo huo ukiendelea kuomba dua mason greenwood asije kuharibiwa ukubwani na vijana wakorofi
  9. mukimaliza kuombea corona iondoke, waombaji munapaswa pia muombee AS Roma amuondoe Sevilla michuano ya europe league......sevilla ndiye adui yetu mkubwa kuliko roma, milan brother na wengineo
  10. hatuhitaji kiungo wa ulinzi dirisha lijalo, tetesi za ndidi zipuuzwe na benchi la ufundi
 
OLE na vijana wake wakaze aise,
Tofauti na hapo hata top 5 ni mtihani.

Kesho Sheffield akishinda anatushusha.

Wolves nao hao hapo, tunalingana points(na wana fictures nzuri mezani).

GGMU
 
Back
Top Bottom