Sijui kitu gani kikichofanya tushindwe kutumia nguvu zetu zote kumpata mmojawapo hapo kati ya Ericksen, Madison au BF. Pamoja na mapungufu yanayotajwa kuhusu Bruno siamini kama hiyo ni sababu ya Msingi, nadhani sababu he is not English

Naunga mkono hoja, Pogba style yake ya uchezaji ni ya ku risk kupoteza mipira hivyo anapaswa kupandishwa juu, ili hata akipoteza mpira iwe rahisi ku recover
ujio wa maguire, james na bissaka kwa kuziangalia hizi mechi tatu tulizocheza wameonyesha kiwango chenye kuleta matumaini makubwa sana pia wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuziba baadhi ya nyufa zetu zilizokuwa zinatishia kuiangusha nyumba yetu ya matofali.

eneo linalotufanya tuonekane kwa mara nyengine tena ni underdog mbele ya wapinzani wetu ni middle third, hii ndio sehemu nyengine tuliopaswa kuifanyia uwekezaji mkubwa sana kama zinavyofanya timu nyenginezo lakini kwa bahati mbaya au kwa makusudi tumeshindwa kufanya hivyo kana kwamba klabu ya manchester united wana umasikini wa fedha.

ukiziangalia hizi mechi zetu mbili za mwisho tunamiliki mpira kuliko hata wapinzani wetu lakini tunashindwa kupata matokeo ya ushindi kwa sababu ya kukosa ubunifu kwa wachezaji wetu tunapofika eneo la adui.
wolves na crystal palace kwa viwango walivyovionyesha kwenye mechi zetu laiti kama nafasi hii wangeliipata liverpool au man city basi wangelipata alama zote sita.

ndio maana nilisema humu ndani tokea mechi za pre season ya kwamba timu yetu bado ipo ovyo, haiwezekani tunamiliki mpira kwa asilimia 60 baadae tunapiga shots on target mbili kwa dakika takribani 70 then tujisifu tumeimarika kiuchezaji, kwangu mimi kumiliki mpira pamoja na kuwa na defence ngumu ya ulinzi bila ya kuwa na safu hatari ya viungo washambuliaji ni kazi bure kwa sababu mwisho wa siku utawafanya mabeki wachoke kwa kukimbia ovyo muda wote na hatimaye kuwafanya waonekane ni vilaza.

tusipobadilika kiuchezaji tutaendelea kupoteza pointi pindi tutakapokutana na timu zinazokaba chini kama walivyotuonyesha wolves na crystal palace na bahati mbaya sana timu nyingi za kiingereza ndio mfumo wao na hazichezi mpira wa pressing kama ule waliocheza chelsea dhidi yetu (wazee wa kuachia nafasi).

hivi tokea tufanye usajili wa henrikh mkhitaryan kuna kiungo mshambuliaji mwengine tuliemsajili?
dirisha lijalo tunapswa tuwekeze eneo la viungo washambuliaji kama tunataka turudishe zama zetu za kufunga wastani wa magoli matatu kwa mechi.
 
Baada ya kuondoka kwa Bissaka sisi Chelsea bila ya huruma tukawadondoshea CP beki bora kabisa upande wa kulia ivi.. Garry Cahill..

Sasa ameenda kuwa new Bissaka pale..

We are proudly of you Captain Legendary..

Kila la kheri Chelsea

#KTBFFH
 
Kwa sasa Scot is better kuliko Matic, game za pre season zimethibisha hivyo, Matic amepungua sana uwezo

Nadhani hata mazoezini hali ni hiyo hiyo

Kwa Fred sijajua tatizo ni nini ila nahisi kwa kuwa hakushiriki pre season fully ndio maana OGS anataka awe na level of fitness ya wenzake ndio ampange

Na hata Fred akiwa fit sidhani kama atamkalisha Scot bench, labda Lingard, ili Pogba apande juu na huku chini abaki Fred na Scot
mkuu hata kama fred atapewa nafasi basi si ajabu kumkuta OGS anampa nafasi lingard awe namba 7 huku daniel james akitokea benchi.
teh teh teh

nemanja matic uhusiano wake na man utd ndio unaelekea mwishoni kama OGS ataendelea kuwa mwalimu.
 
Pogba tayar kisha prove ni world class player huwez kumueweka daraja moja na kiungo yoyote pale united

Pogba anacheza timu yoyote duniani ila sio hao uliowataja

Mata tayar kafanya makubwa na kashinda vitu vingi ngaz ya club na timu ya taifa

Mata tayar umr umekwenda huwez kumtafutia watu wa kufanya nao kazi zaidi anatakiwa kustaafu

Lingard ana miaka 27 au 26 hamna cha maana alichofanya

Lingard yupo kwenye umr wa ukomavu wa mpira lakin anashindwa kufanya vitu sahihi

James kacheza mech tatu naona umeona madhara yake ila kwa kuwa ni mdogo tunampa muda

Pogba anahitaj timu ya kushinda makombe kwa kuwa tayar yupo kwenye ubora wake ndio maana tunalaumu kumuweka na watu wasio na tija

Ndio maana unasikia kocha anasema nataka kujenga timu ya kumzunguka pogba sio jeseey lingard kwa nini sio jesey lingard jibu ni useless player

Tunapolaumu kumharibia pogba kiwango unaangalia mambo aliyofanya juventus na national team kisha unaangalia uwiano uliopo kule na huku sasa jaribu kutazama kwa engle hiyo nani ana mpotezea muda mwenzie

Kumbuka pogba sio mkabaji ila sisi tunataka awe mkabaji
Mkuu Dimaria alii prove Dunia kwamba ni world class, je alipokuja United kina nani walimfanya ashuke kiwango, Falcao, Sanchez wakishushwa na akina nani n.k

Kwa mfano hapa unasema akina Lingard ndio wanamsababisha Pogba asicheze vizuri. Nikikuuliza Lingard na nani sidhani kama utataja hata wachezaji 4 ambao utawaingiza kwenye hiyo blame game

Swali linakuja, akina Degea, Wan Bissaka, Shaw, Maquire, Lindelof, Tony Martial, Rashy, James je wote wanamuangusha Pogba? Je Pogba pale Ufaransa ana world class players tu wanaomzunguka, Pavard, Giroud, namba 3 wao yule n.k

Je pale Juve alikuwa amezungukwa na wachezaji wote world class players? Je unapotaja mafanikio ya Juve kwa wakati ule, ulikuwa unamtaja kama Pogba ndio ameibeba timu au Pogba was just another Juventus player

Pogba kucheza timu yote duniani, sidhani. Ana hiyo potential, KWELI na pengine mpaka anastaafu atabaki kuwa na POTENTIAL tu, lakini sio timu yoyote duniani anaweza kucheza. City hawezi kupata namba, na Pep alimkataa, Madrid pamoja na Luka kuwa kikongwe sidhani kama anaweza kumvua namba. Barca ndio kabisaa.

Hapa nazungumzia uwezo wake uwanjani na influence yake kwenye timu, hivi vitu ukiviunganisha kuna viungo wengi duniani wanaweza kuwa mbele ya Pogba.

I would rather have Ericksen, Madson, BF, Milinkovic than Pogba in my team
 
❌ Crystal Palace
❌ Southampton
❌ PSG
❌ Arsenal
❌ Wolves
❌ Watford
❌ Wolves
❌ Barcelona
❌ West Ham
❌ Barcelona
❌ Everton
❌ Man City
❌ Chelsea
❌ Huddersfield
❌ Cardiff
✅ Chelsea
❌ Wolves
❌ Crystal Palace

Man Utd have kept ONE clean sheet in their last 18 games 😬
 
Naona umeanza kumkubali Bissaka taratibu

Kuna siku ulimponda sana humu
Bissaka sijawai kumponda mkuu nilimwesabia mechi ..lakini ameonesha kiwango kizuri ila tatizo timu ya Man united itamtumia tu bila mafanikio yeyote ..hii Man united ya sasa inaeza Ku struggle ata misimu kadhaa mpka kurudi kwenye uwezo wake tunaoujua. Hii timu itakuwa inapanda na kushuka hivi hivi hadi msimu unaisha. Hivyo Bissaka na Pogba naona kwa mtizamo wangu watafute timu za kwenda tu kama wanataka mafanikio ya makombe ..ila kama ni pesa basi wabaki wazichote tu
 
Kwa upande wa timu sina shida nayo tulikuwa na upungufu mdogo sana hata mwisho wa ligi tumeangushwa na foward ambapo soon wataenda kurekebisha kama wakiamua unajua timu ikiwa na ushambuliaji mkali hata mabek huwa imara hawachok sasa muda wote mpira upo kwetu mbele hakutish timu itakuwa mbovu tu hiv barcelona tunaamini wana bek bora pale? Mbele barcelona kunatisha

Hao wakina smalling na jones wamecheza chini ya sir alex lakin kuanzia namba 6 tulikuwa vizur had ushambuliz kiasi kwamba muunganiko wa timu unakuwepo pogba anajitahidi sana kutengeneza nafasi japo ana shida yake lakin umaliaziaji upoje?
Nakukumbusha mkuu radika kuhusu comment yako juu ya timu yetu.
 
mkuu hata kama fred atapewa nafasi basi si ajabu kumkuta OGS anampa nafasi lingard awe namba 7 huku daniel james akitokea benchi.
teh teh teh

nemanja matic uhusiano wake na man utd ndio unaelekea mwishoni kama OGS ataendelea kuwa mwalimu.
Hahahaa

Mimi kiukweli Lingard naona anaweza kutumiwa katika baadhi ya mechi kimkakati lakini si mechi zote

Lingard hana uwezo wa kumuweka DJ especially kwa nafasi za pembeni

Kinachonifurahisha, naona kama umeanza kumuelewa swala
 
Bissaka sijawai kumponda mkuu nilimwesabia mechi ..lakini ameonesha kiwango kizuri ila tatizo timu ya Man united itamtumia tu bila mafanikio yeyote ..hii Man united ya sasa inaeza Ku struggle ata misimu kadhaa mpka kurudi kwenye uwezo wake tunaoujua. Hii timu itakuwa inapanda na kushuka hivi hivi hadi msimu unaisha. Hivyo Bissaka na Pogba naona kwa mtizamo wangu watafute timu za kwenda tu kama wanataka mafanikio ya makombe ..ila kama ni pesa basi wabaki wazichote tu
Chelsea sijaona mchezaji wa kushauri aondoke maana wote ni wa level za Chelsea
 
Crystal Palace
Southampton
PSG
Arsenal
Wolves
Watford
Wolves
Barcelona
West Ham
Barcelona
Everton
Man City
Chelsea
Huddersfield
Cardiff
Chelsea
Wolves
Crystal Palace

Man Utd have kept ONE clean sheet in their last 18 games
Nikumbushe mara mwisho Liverpool kuwa na clean sheet, maana United mara ya mwisho ilikuwa ni Agost 2019
 
mkuu mbona bado ni mapema sana kujipiga ban ya muda mrefu.​
kwa mtazamo wangu sidhani kama itakuwa ni sahihi kuzitumia hizi mechi tatu (chelsea, wolves, palace) tulizocheza kama ni samples za kufanyia maamuzi na utabiri kuhusiana na muelekeo mzima wa klabu kwenye ligi kuu na mashindano mengineo.

bado nina imani kubwa sana ya klabu kufanya vizuri msimu huu kama tutazifanyia kazi hizi warning signs tulizopewa na wapinzani wetu uchwara tena ligi ikiwa bado ndio kwanza imeanza.

ila kama tutazipuuzia hizi warning signs basi hata mimi pia nitafuata mkondo wako kwa kujipiga ban ya muda mrefu kama nilivyofanya nyakati za utawala wa louis van gaal na mdogo wake david moyes.

tusipokuwa makini huenda jose mourinho huyu tuliyekuwa tunamdhihaki kwa lugha mbali mbali akawa ndiye kocha pekee mwenye mafanikio ndani ya klabu tokea aondoke sir alex ferguson.

kumaliza nafasi ya pili nikiwa kama kocha wa manchester united ndio mafanikio yangu makubwa klabuni.
dah! wengi wetu tulimuona jamaa ni mwehu baada ya kutoa kauli hii.
Mourinho anazingua Sana, aliulizwa juzi timu ambazo zinaweza chukua EPL mwaka huu jamaa akataja Manchester City, Liverpool, Tottenham na Manchester City "B" team...
Kwamba hata wachezaji waliopo benchi pale Manchester city wanaweza compete for tittle wakipewa nafac....
 
Hahahaa

Mimi kiukweli Lingard naona anaweza kutumiwa katika baadhi ya mechi kimkakati lakini si mechi zote

Lingard hana uwezo wa kumuweka DJ especially kwa nafasi za pembeni

Kinachonifurahisha, naona kama umeanza kumuelewa swala
yes, swala analeta matumaini lakini unakuta wachezaji kama wale wanaotoka timu ndogo baadae wanajikuta wanaingia first eleven kwenye timu kubwa wanachoka mapema sana au wanajisahau pindi wanapokosa upinzani.

jana alifunga goli zuri sana.
dogo anahitaji zaidi utulivu wa nafsi ndio maana sikutamani awe winga pekee aliyesajiliwa kwa kuhofia kumbebesha mzigo mzito wa majukumu haliyakuwa bado ni kijana mdogo.​
 
Bissaka sijawai kumponda mkuu nilimwesabia mechi ..lakini ameonesha kiwango kizuri ila tatizo timu ya Man united itamtumia tu bila mafanikio yeyote ..hii Man united ya sasa inaeza Ku struggle ata misimu kadhaa mpka kurudi kwenye uwezo wake tunaoujua. Hii timu itakuwa inapanda na kushuka hivi hivi hadi msimu unaisha. Hivyo Bissaka na Pogba naona kwa mtizamo wangu watafute timu za kwenda tu kama wanataka mafanikio ya makombe ..ila kama ni pesa basi wabaki wazichote tu
Utageuka tu maneno yako, Kuna siku nyingine ukasema Azpilikweta ni bora kuliko Bissaka
 
Mourinho anazingua Sana, aliulizwa juzi timu ambazo zinaweza chukua EPL mwaka huu jamaa akataja Manchester City, Liverpool, Tottenham na Manchester City "B" team...
Kwamba hata wachezaji waliopo benchi pale Manchester city wanaweza compete for tittle wakipewa nafac....
yes, alikuwa anajaribu kuonyesha jinsi gani majirani zetu walivyojaaliwa utajiri wa wachezaji wenye viwango visivyopishana sana.

baadhi ya nyakati ni bora uwe na wachezaji 18 wenye uwezo mkubwa kuliko kuwa na kundi la wachezaji 23 wenye uwezo wa kawaida.
 
Sijui kitu gani kikichofanya tushindwe kutumia nguvu zetu zote kumpata mmojawapo hapo kati ya Ericksen, Madison au BF. Pamoja na mapungufu yanayotajwa kuhusu Bruno siamini kama hiyo ni sababu ya Msingi, nadhani sababu he is not English

Naunga mkono hoja, Pogba style yake ya uchezaji ni ya ku risk kupoteza mipira hivyo anapaswa kupandishwa juu, ili hata akipoteza mpira iwe rahisi ku recover
Man united zamani ilikuwa ni dream ya wachezaji wengi kucheza. Ilikuwa ni heshima sana kukipiga ndani ya dimba la OT ..

Kama ilivyo Anfield ya sasa ..ndivyo ilivyokua OT, lakini kumekuwa shamba la bibi timu yeyote tu ata Yanga ikija inashinda tu ..unaona hata haina mvuto kwa wachezaji kuja kucheza apo..
 
Back
Top Bottom