Sijui kitu gani kikichofanya tushindwe kutumia nguvu zetu zote kumpata mmojawapo hapo kati ya Ericksen, Madison au BF. Pamoja na mapungufu yanayotajwa kuhusu Bruno siamini kama hiyo ni sababu ya Msingi, nadhani sababu he is not English

Naunga mkono hoja, Pogba style yake ya uchezaji ni ya ku risk kupoteza mipira hivyo anapaswa kupandishwa juu, ili hata akipoteza mpira iwe rahisi ku recover

Nguvu ipi unaizungumzia wakat fred na matic wapo bench scott atafute namba huko wakat timu ina watu?
 
Kiungo hakikuwa overrun mkuu, goli tulilofungwa lilitokana na Kupoteza mpira wakati tunashambulia kwa maana kwamba hata angekuwepo Matic/Scot uwanjani nao wangekuwa mbele kushambulia kwa hiyo tungepigwa tu kwa goli la namna ile (counter attack)

Kutoa mzuiaji na kisha kuingiza mchezaji anayesaidia mashambulizi si kupaniki kama unavyosema, Lengo ni kuongeza nguvu kwenye kushambulia. SAF alikuwa anafanya, Jose huwa anafanya hivyo na Nimeona makocha wengi wanafanya hivyo

Hiyo ni sawa na timu inaongoza na inataka kulinda matokeo, inaamua kutoa mchezaji wa kushambulia na kuingiza mchezaji wa ukabaji. Sio kila sub lazima iwe like for like substution, yaani kwa kuwa ametoka Scot basi aingie Matic. No, it's like that. Circumstance ya game ndio huwa inaamua nani aingie na nani atoke

Siku nikiangalia game ya kocha wako kipenzi Pep, akifanya hivyo nitakukumbusha huu mjadala. Tuombe uzima.

Yule lindelof huwa namuangaliaga sana ni bek wa hovyo sana sijawah kumuona akipambana mipira ya juu huwa wengine tunakaaga kimya tu ule mpira unampitaje wakat chenyewe kilikuwa naye yule jamaa ile timu bila kusajili watu 7 daraja inaweza kushuka sababu hata southampton kiungo chao sio lelemama
 
Dah! Kazi munayo Haki ya Mungu.

Kuhusu Jesse nadhani OGS anapaswa kuwa dynamic, intensity ya Jesse haihitajiki tunapokutana na Cristal Palace au Southampton au Norwich. Tukikutana na hivi vitimu vidogo ambavyo kazi yao ni kukaa nyuma na kusubiri mfanye makosa ili wawaadhibu tunapaswa kuwatumia akina Angel Gomes na Mata

Tunapokutana na timu ambazo zipo tayari kucheza mpira sina tatizo na Jesse kuanza. Ila jana overall alikuwa na game mbovu sana
 
Toka sir alex asepe Jose Mourinho ndio kocha mwenye mafanikio makubwa sana hata uwiano wa kushinda mech ni mzur anakamata nafasi ya pili baada ya sir alex sema bodi na mashabiki uchwara hawakuona vile huyu mreno anavutwa shati

Mimi nilitambua mchango wake ila kuna baadhi humu walifikir ubovu wa timu ni kocha peke yake

Sijui kaka ya Garry Neville anasemaje sasa

Pia hii timu inazimishwa na class of 92 vimekuwa visemaji kila uchwao kila mchezaj wakigeni ni kuponda tu

Tujiulize Lingard ana ball contro nzur zaidi ya Lukaku? Nani amewah kumsikia scholes akimsema lingard au garry? Pogba ni mbovu zaidi ya lingard?

Class of 92 wanachangia kuua morali ya timu

Usijeshangaa kuwa hao the so called class of 92' wanasumbuliwa na Wivu hawataki Rekodi na Mafanikio yao Kuvunjwa ndiyomana wapo tayari Aondoke Mourinho aje Ole, Aondoke Herrera abaki Scot, Aondoke Lukaku abaki Lingard, Aondoke Pogba asajiliwe Muengereza yeyote ambae watakuwa na uhakika hataleta mafanikio kama yao.

Sometimes mafanikio binafsi ya Mtu yanakuwa shida sana kupinduliwa.
 
Nguvu ipi unaizungumzia wakat fred na matic wapo bench scott atafute namba huko wakat timu ina watu?
Kwa sasa Scot is better kuliko Matic, game za pre season zimethibisha hivyo, Matic amepungua sana uwezo

Nadhani hata mazoezini hali ni hiyo hiyo

Kwa Fred sijajua tatizo ni nini ila nahisi kwa kuwa hakushiriki pre season fully ndio maana OGS anataka awe na level of fitness ya wenzake ndio ampange

Na hata Fred akiwa fit sidhani kama atamkalisha Scot bench, labda Lingard, ili Pogba apande juu na huku chini abaki Fred na Scot
 
Kwamba huoni anavyo struggle?
Hivi kwanini aki struggle Lingard au Martial au Daniel James au Scot au Mata au yoyote hatusemi wanaangushwa na akina Pogba?

Hivi Pogba ku struggle inasababishwa na wenzake? Kwanini wenzake wanapo struggle hatusemi Pogba na wengine ndio chanzo?

Hivi Pogba kupoteza mpira kisha timu pinzani ikatumia huo udhaifu na kuiadhibu United, hapo wenzake wanakuwa wamemuangushaje?
 
Usijeshangaa kuwa hao the so called class of 92' wanasumbuliwa na Wivu hawataki Rekodi na Mafanikio yao Kuvunjwa ndiyomana wapo tayari Aondoke Mourinho aje Ole, Aondoke Herrera abaki Scot, Aondoke Lukaku abaki Lingard, Aondoke Pogba asajiliwe Muengereza yeyote ambae watakuwa na uhakika hataleta mafanikio kama yao.

Sometimes mafanikio binafsi ya Mtu yanakuwa shida sana kupinduliwa.

Fact
 
Hivi kwanini aki struggle Lingard au Martial au Daniel James au Scot au Mata au yoyote hatusemi wanaangushwa na akina Pogba?

Hivi Pogba ku struggle inasababishwa na wenzake? Kwanini wenzake wanapo struggle hatusemi Pogba na wengine ndio chanzo?

Hivi Pogba kupoteza mpira kisha timu pinzani ikatumia huo udhaifu na kuiadhibu United, hapo wenzake wanakuwa wamemuangushaje?

Yani haya munayoyapitia humu kuhusu upangaji mbovu wa Kikosi kwa kiburi cha kocha nayakumbuka Vilivyo nilivyoyapitia kila siku kulialila na kujawa na Hasira mpaka nikayazoea.
Na Siku zote kwenye Uzi hakosi mtu wa kutetea ujinga wa Kocha
 
Hivi kwanini aki struggle Lingard au Martial au Daniel James au Scot au Mata au yoyote hatusemi wanaangushwa na akina Pogba?

Hivi Pogba ku struggle inasababishwa na wenzake? Kwanini wenzake wanapo struggle hatusemi Pogba na wengine ndio chanzo?

Hivi Pogba kupoteza mpira kisha timu pinzani ikatumia huo udhaifu na kuiadhibu United, hapo wenzake wanakuwa wamemuangushaje?

Pogba tayar kisha prove ni world class player huwez kumueweka daraja moja na kiungo yoyote pale united

Pogba anacheza timu yoyote duniani ila sio hao uliowataja

Mata tayar kafanya makubwa na kashinda vitu vingi ngaz ya club na timu ya taifa

Mata tayar umr umekwenda huwez kumtafutia watu wa kufanya nao kazi zaidi anatakiwa kustaafu

Lingard ana miaka 27 au 26 hamna cha maana alichofanya

Lingard yupo kwenye umr wa ukomavu wa mpira lakin anashindwa kufanya vitu sahihi

James kacheza mech tatu naona umeona madhara yake ila kwa kuwa ni mdogo tunampa muda

Pogba anahitaj timu ya kushinda makombe kwa kuwa tayar yupo kwenye ubora wake ndio maana tunalaumu kumuweka na watu wasio na tija

Ndio maana unasikia kocha anasema nataka kujenga timu ya kumzunguka pogba sio jeseey lingard kwa nini sio jesey lingard jibu ni useless player

Tunapolaumu kumharibia pogba kiwango unaangalia mambo aliyofanya juventus na national team kisha unaangalia uwiano uliopo kule na huku sasa jaribu kutazama kwa engle hiyo nani ana mpotezea muda mwenzie

Kumbuka pogba sio mkabaji ila sisi tunataka awe mkabaji
 
Mashabiki wa Manchester city, Liverpool,chelsea hamuwezi kukoment humu bila matusi?

Kama matusi ndo raha yenu basi jaribu kufikiri unatukana mtu sawa na babako?

MKUYENGE narudia jiheshimu.
Apo fans wa Chelsea tutoe ..sisi ni wastaarabu sana ..

Kila la kheri Chelsea
 
Sijui wenzangu mnaona kama mimi ninavyoona maana hadi muda huu sijui hii timu imekamilika eneo gani

Bado naona mapengo na mashimo makubwa sana usajili wa maguire na bissaka hauwez kuficha mashimo

Napata shida sana kama tunakocha ndani ya hii timu maana sina hiyo taaluma ila naona udhaifu mkubwa sana bado kocha kakubali tuenze ligi na mashimo ya maana

Dirisha la usajili lipo waz toka mwez wa 5 tunasajili kama vile sisi ndio manchester city
 
167 Reactions
Reply
Back
Top Bottom