Man united zamani ilikuwa ni dream ya wachezaji wengi kucheza. Ilikuwa ni heshima sana kukipiga ndani ya dimba la OT ..

Kama ilivyo Anfield ya sasa ..ndivyo ilivyokua OT, lakini kumekuwa shamba la bibi timu yeyote tu ata Yanga ikija inashinda tu ..unaona hata haina mvuto kwa wachezaji kuja kucheza apo..
Kwamba Madson Man wakimtaka ana ubavu wa kuchoma, si kweli
 
Na wanacheza mpira mzuri mechi zote
Hata United wanacheza vizuri mbona!! Nani anawadharau Chelsea by the way? Watu mjifunze na kuvumilia tambo za fans wa mpira. Starehe ya ushabiki wa mpira imejikta zaidi kwenye tambo na hii ni kwa michezo yote so football tuu.

Watu mnapandwa sana hasira kuliko hata wenyeji.

Msiwe mnajipatia matumaini makuubwa kuliko practical reality.
 
OGS anarudia kufanya tactical mistake mechi ya tatu mfululizo na kibaya zaidi yeye bado hajaona kama ni tatizo

Mechi zote ametumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao unamfanya Pogba(creative player) anacheza nyuma na timu ina-struggle kutengeneza nafasi licha ya kumiliki mpira kwa sababu anakuwa anacheza kama DM .Game vs Chelsea tulikuwa na advantage alinza Pereira ambaye yeye kiungo so muda mwingi alikuwa anarudi kusaidia kukaba kukamfanya Pogba akawa free na kutengeneza nafasi nyingi ,mechi zilizofuatia badala ya Perreira ameanza James ambaye sio kiungo ni winga so harudi kusaidia kukaba na kuwapa mzigo mzito viungo (Pogba,McTominay) na tumecheza na timu zinazocheza mpira wa nguvu kwa sasa James anafaa awe anaingia second half.
Pia wakati mwingine anapaswa kuswich 4-3-3 ambayo aliicheza msimu uliopita na kujaribu kuwapa nafasi Fred na Matic
I like fans of your calibre and arguments. Watu wanashambulia as if nothing can be done. Kwanza as from the next game, Lingard hataanza. Danny ni muhimu kuanza. Mid aanze Paul, Tominay/Matic na Perreira/Fred
 
Yule lindelof huwa namuangaliaga sana ni bek wa hovyo sana sijawah kumuona akipambana mipira ya juu huwa wengine tunakaaga kimya tu ule mpira unampitaje wakat chenyewe kilikuwa naye yule jamaa ile timu bila kusajili watu 7 daraja inaweza kushuka sababu hata southampton kiungo chao sio lelemama
Horjberg na Romeo ni balaa
 
Pogba tayar kisha prove ni world class player huwez kumueweka daraja moja na kiungo yoyote pale united

Pogba anacheza timu yoyote duniani ila sio hao uliowataja

Mata tayar kafanya makubwa na kashinda vitu vingi ngaz ya club na timu ya taifa

Mata tayar umr umekwenda huwez kumtafutia watu wa kufanya nao kazi zaidi anatakiwa kustaafu

Lingard ana miaka 27 au 26 hamna cha maana alichofanya

Lingard yupo kwenye umr wa ukomavu wa mpira lakin anashindwa kufanya vitu sahihi

James kacheza mech tatu naona umeona madhara yake ila kwa kuwa ni mdogo tunampa muda

Pogba anahitaj timu ya kushinda makombe kwa kuwa tayar yupo kwenye ubora wake ndio maana tunalaumu kumuweka na watu wasio na tija

Ndio maana unasikia kocha anasema nataka kujenga timu ya kumzunguka pogba sio jeseey lingard kwa nini sio jesey lingard jibu ni useless player

Tunapolaumu kumharibia pogba kiwango unaangalia mambo aliyofanya juventus na national team kisha unaangalia uwiano uliopo kule na huku sasa jaribu kutazama kwa engle hiyo nani ana mpotezea muda mwenzie

Kumbuka pogba sio mkabaji ila sisi tunataka awe mkabaji
pogba hapati namba kwa shibubo
 
Mkuu Dimaria alii prove Dunia kwamba ni world class, je alipokuja United kina nani walimfanya ashuke kiwango, Falcao, Sanchez wakishushwa na akina nani n.k

Kwa mfano hapa unasema akina Lingard ndio wanamsababisha Pogba asicheze vizuri. Nikikuuliza Lingard na nani sidhani kama utataja hata wachezaji 4 ambao utawaingiza kwenye hiyo blame game

Swali linakuja, akina Degea, Wan Bissaka, Shaw, Maquire, Lindelof, Tony Martial, Rashy, James je wote wanamuangusha Pogba? Je Pogba pale Ufaransa ana world class players tu wanaomzunguka, Pavard, Giroud, namba 3 wao yule n.k

Je pale Juve alikuwa amezungukwa na wachezaji wote world class players? Je unapotaja mafanikio ya Juve kwa wakati ule, ulikuwa unamtaja kama Pogba ndio ameibeba timu au Pogba was just another Juventus player

Pogba kucheza timu yote duniani, sidhani. Ana hiyo potential, KWELI na pengine mpaka anastaafu atabaki kuwa na POTENTIAL tu, lakini sio timu yoyote duniani anaweza kucheza. City hawezi kupata namba, na Pep alimkataa, Madrid pamoja na Luka kuwa kikongwe sidhani kama anaweza kumvua namba. Barca ndio kabisaa.

Hapa nazungumzia uwezo wake uwanjani na influence yake kwenye timu, hivi vitu ukiviunganisha kuna viungo wengi duniani wanaweza kuwa mbele ya Pogba.

I would rather have Ericksen, Madson, BF, Milinkovic than Pogba in my team
wewe jamaa kila sikunakuambia unakaakili kuliko mashabiki wote wa Manchester United
 
Mourinho anazingua Sana, aliulizwa juzi timu ambazo zinaweza chukua EPL mwaka huu jamaa akataja Manchester City, Liverpool, Tottenham na Manchester City "B" team...
Kwamba hata wachezaji waliopo benchi pale Manchester city wanaweza compete for tittle wakipewa nafac....
sure kabisa morinho ni msema ukweli kama Paul makonda
 
Back
Top Bottom