Belo, wanavyosema wenye timu yao humu ndani ni kwamba huu mfumo wa 4-2-3-1 ndio uliokuwa unatupa mafanikio kwenye mechi zetu za kujipima nguvu ikiwemo dhidi ya milan brothers, spurs na wengineo hivyo basi kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kutumika kwa mfumo huu. badala ya ule tuliouzoea wa 4-3-3 kwa takribani misimu mitatu iliopita.

unajua kwa kiasi kikubwa sana wengi wetu hatufahamu lolote linalotendeka ndani ya klabu kwa sababu hatuna uwezo wa kuaccess taarifa nyeti zinazoihusu klabu matokeo tumeishia kuwa watabiri kwa yale yanayo na yatakayotendeka mbeleni kwa kufuata zaidi mdundo wa vyombo vya habari.
  • kwa kutumia huu utabiri acha niamini ya kwamba bwana OGS alitegemea ingizo la kiungo mwengine mshambualiaji mfano wa eriksen, bruno fernandez au maddison atakayekuja kucheza namba 10 eneo ambalo tunamtumia jesse lingard kwa msimu huu baada ya kuswitch mfumo wa 4-2-3-1 tokea preseason, lakini ndio hivyo kama kawaida kwa mara nyengine tena ed woodward na rafiki yake matt judge walishindwa kufanikisha usajili wowote wa kiungo huku wakifahamu fika tumempoteza ander herrera na marouanne fellaini.
  • kwa kutumia utabiri huo huo acha pia niamini ya kwamba OGS huenda ndiye aliyefelisha baadhi ya sajili za wachezaji mfano wa bruno fernandez kwa hoja ya kukosa DNA zitakazomwezesha kuipigania klabu kwa jasho lake haijalishi kama atalipwa hela ndogo na kumuona jesse lingard ndiye kiungo sahihi zaidi kucheza namba 10 huku paul na scott wakicheza deep midfields eneo ambalo tumekwishazoea tukiwatumia herrera na nemanja matic.
kuna mwanadamu mmoja tu ambaye huenda akambadilisha fikra bwana ole ili arudishe tena mfumo wa 4-3-3 ambao unamwezesha paul pogba kucheza juu zaidi akitokea upande wa kushoto ambao ndio upande tunaoutegemea zaidi kupika mashambulizi na si mwengine isipokuwa ni fred the red.
kama fred atacheza vizuri pindi atakapopewa nafasi basi tutaswitch mfumo wa 4-3-3 kwa sababu OGS hana uwezo wa kumweka nje paul pogba ili apate kuendeleza mfumo wake wa 4-2-3-1.

pia tufahamu si nemanja matic, perreira wala fred atakeyekuwa na uthubutu wa kumfanya OGS abadilishe msimamo wa kifikra kwa kumweka nje scott mctominay kwenye eneo la kiungo mkabaji kwa sababu hao wote hawana DNA za kimanchester ukilingansha na scott hivyo basi wapenzi wa nemanja matic kwa msimu huu mujiandae kisaikolojia.
OGS na benchi lake wanamuona scott mctominay kama ndiye roy keane wetu mpya.​

  • fred ndiye aliyeshikilia ufunguo utakaomwezesha OGS abadili style ya kiuchezaji mara kwa mara msimu huu.
  • fred ndiye aliyeshikilia ufunguo wake mwenyewe utakaomwezesha kufungua au kufunga chumba chake cha kuhifadhia vifaa pale AON complex a.k.a carrington, kama atacheza vizuri basi msimu ujao ataendelea kuwepo klabuni ila kama ataendelea kucheza ovyo kwa ninavyomtazama solskajer na hii recruitment yake ya karne ya 20 aliyokuja nayo huenda nafasi yake rasmi akapewa gardner au yule mjinga anayetokea newcastle united anayeitwa sean longstaff
View attachment 1189467
Sijui kitu gani kikichofanya tushindwe kutumia nguvu zetu zote kumpata mmojawapo hapo kati ya Ericksen, Madison au BF. Pamoja na mapungufu yanayotajwa kuhusu Bruno siamini kama hiyo ni sababu ya Msingi, nadhani sababu he is not English

Naunga mkono hoja, Pogba style yake ya uchezaji ni ya ku risk kupoteza mipira hivyo anapaswa kupandishwa juu, ili hata akipoteza mpira iwe rahisi ku recover
 
Tangu Pre Season kumetokea waganga njaa wengi , wakiwemo mashabiki Wa United wakipiga ramli kuwa timu Yetu ingekula vipigo bandika bandua ...

Tulionyana humu hizo ni ramli chochezi ... Sasa naona ramli zinazidi kuendelezwa na mashabiki wa timu pinzani wakiungwa mkono na Genge Dogo la mabaki ya nduli morinho lililobaki kwenye viunga vya old Trafford ..

Hili Genge nalikumbusha kuwa tumecheza mechi mbili na tuna pointi 4 ...

Sasa endeleeni kuchoma ubani na kuvunja Nazi timu ifanye vibaya ..

Nawakumbusha Next point ni Crystal Palace pelekeni habari moto atakaoupata itakuwa ujumbe kwa wazandiki wote kuwa "Tumewashaaaa"

Nawatakia Weekend Njema..
Soka halina ubinadamu, cheki sasa ushaumbuka
 
Mkuu, tupo nyumbani, tunahitaji goli, then unaanzaje kumtoa Scot (mkabaji) halafu umuingize Matic (mkabaji mwingine)

Idea ilikuwa kuongeza nguvu kwenye mashambulizi na si kuimarisha ulinzi
I think vitu vyote vinatakiwa kuwa balanced la si hivyo ni kupanic

I think Unapotafuta goli boresha safu ya mashambulizi huku Defensive midfield ikiwa hai"face" overruns. Goli la Patrick van Anholt ukiangalia pale unaona kabisa kiungo cha MUFC kilikuwa overrun kama sio walichoka
 
Sitakuja kaa na kuangalia mechi ya man kamwe
mkuu mbona bado ni mapema sana kujipiga ban ya muda mrefu.​
kwa mtazamo wangu sidhani kama itakuwa ni sahihi kuzitumia hizi mechi tatu (chelsea, wolves, palace) tulizocheza kama ni samples za kufanyia maamuzi na utabiri kuhusiana na muelekeo mzima wa klabu kwenye ligi kuu na mashindano mengineo.

bado nina imani kubwa sana ya klabu kufanya vizuri msimu huu kama tutazifanyia kazi hizi warning signs tulizopewa na wapinzani wetu uchwara tena ligi ikiwa bado ndio kwanza imeanza.

ila kama tutazipuuzia hizi warning signs basi hata mimi pia nitafuata mkondo wako kwa kujipiga ban ya muda mrefu kama nilivyofanya nyakati za utawala wa louis van gaal na mdogo wake david moyes.

tusipokuwa makini huenda jose mourinho huyu tuliyekuwa tunamdhihaki kwa lugha mbali mbali akawa ndiye kocha pekee mwenye mafanikio ndani ya klabu tokea aondoke sir alex ferguson.

kumaliza nafasi ya pili nikiwa kama kocha wa manchester united ndio mafanikio yangu makubwa klabuni.
dah! wengi wetu tulimuona jamaa ni mwehu baada ya kutoa kauli hii.
 
Inaitwa Lingard all the way

Inaitwa Lingard all the day

Katika msimu uliopita uliochezwa ndani ya miezi kumi ya mwaka Jesse Lingard alifunga na kuassist mwezi wa December peke yake

August 2018 - no any goal no any Assist for Lingard

September 2018 -no any goal no any Assist for Lingard

October 2018 - no any goal no any Assist for Lingard

November 2018- no any goal no any Assist for Lingard

December 2018- four goals two assist for Lingard

Kituko sasa

Mwaka mzima wa kalenda wa 2019 Jesse Lingard hajafunga hata goli moja wala kutoa Assist hata moja
Dah! Kazi munayo Haki ya Mungu.

Tafadhali mkuu, usimseme mchezaji wetu "anaewika ulaya" na ujue kuwa ametoka academy bora Uingereza.
 
mkuu mbona bado ni mapema sana kujipiga ban ya muda mrefu.​
kwa mtazamo wangu sidhani kama itakuwa ni sahihi kuzitumia hizi mechi tatu (chelsea, wolves, palace) tulizocheza kama ni samples za kufanyia maamuzi na utabiri kuhusiana na muelekeo mzima wa klabu kwenye ligi kuu na mashindano mengineo.

bado nina imani kubwa sana ya klabu kufanya vizuri msimu huu kama tutazifanyia kazi hizi warning signs tulizopewa na wapinzani wetu uchwara tena ligi ikiwa bado ndio kwanza imeanza.

ila kama tutazipuuzia hizi warning signs basi hata mimi pia nitafuata mkondo wako kwa kujipiga ban ya muda mrefu kama nilivyofanya nyakati za utawala wa louis van gaal na mdogo wake david moyes.

tusipokuwa makini huenda jose mourinho huyu tuliyekuwa tunamdhihaki kwa lugha mbali mbali akawa ndiye kocha pekee mwenye mafanikio ndani ya klabu tokea aondoke sir alex ferguson.

kumaliza nafasi ya pili nikiwa kama kocha wa manchester united ndio mafanikio yangu makubwa klabuni.
dah! wengi wetu tulimuona jamaa ni mwehu baada ya kutoa kauli hii.

Toka sir alex asepe Jose Mourinho ndio kocha mwenye mafanikio makubwa sana hata uwiano wa kushinda mech ni mzur anakamata nafasi ya pili baada ya sir alex sema bodi na mashabiki uchwara hawakuona vile huyu mreno anavutwa shati

Mimi nilitambua mchango wake ila kuna baadhi humu walifikir ubovu wa timu ni kocha peke yake

Sijui kaka ya Garry Neville anasemaje sasa

Pia hii timu inazimishwa na class of 92 vimekuwa visemaji kila uchwao kila mchezaj wakigeni ni kuponda tu

Tujiulize Lingard ana ball contro nzur zaidi ya Lukaku? Nani amewah kumsikia scholes akimsema lingard au garry? Pogba ni mbovu zaidi ya lingard?

Class of 92 wanachangia kuua morali ya timu
 
I think vitu vyote vinatakiwa kuwa balanced la si hivyo ni kupanic

I think Unapotafuta goli boresha safu ya mashambulizi huku Defensive midfield ikiwa hai"face" overruns. Goli la Patrick van Anholt ukiangalia pale unaona kabisa kiungo cha MUFC kilikuwa overrun kama sio walichoka
Kiungo hakikuwa overrun mkuu, goli tulilofungwa lilitokana na Kupoteza mpira wakati tunashambulia kwa maana kwamba hata angekuwepo Matic/Scot uwanjani nao wangekuwa mbele kushambulia kwa hiyo tungepigwa tu kwa goli la namna ile (counter attack)

Kutoa mzuiaji na kisha kuingiza mchezaji anayesaidia mashambulizi si kupaniki kama unavyosema, Lengo ni kuongeza nguvu kwenye kushambulia. SAF alikuwa anafanya, Jose huwa anafanya hivyo na Nimeona makocha wengi wanafanya hivyo

Hiyo ni sawa na timu inaongoza na inataka kulinda matokeo, inaamua kutoa mchezaji wa kushambulia na kuingiza mchezaji wa ukabaji. Sio kila sub lazima iwe like for like substution, yaani kwa kuwa ametoka Scot basi aingie Matic. No, it's like that. Circumstance ya game ndio huwa inaamua nani aingie na nani atoke

Siku nikiangalia game ya kocha wako kipenzi Pep, akifanya hivyo nitakukumbusha huu mjadala. Tuombe uzima.
 
Back
Top Bottom