Sijagusia hili pia kwenye Uzi wangu. Wala sifahamu yupi ni yupi. Yawezekana asiwepo au akawepo but lengo langu lilikua kuelezea Qnet ni E commerce system.
But navutiwa sana na nakuja sababu yako ya kupenda kujua mafanikio ya mjasiriamali fulani ni ipi! Usije ukawa kama walio wengi huafuata mkumbo kwenye kufanya maamuzi kwa sababu ya fulani kapata sana kwenye biashara fulani ngoja na mimi nifanye... hii sio dhana sahihi.. ipo siku nitaelezea hii kasumba na athari zake.
Thanks.
Mantiki ya uzi wako ni nini aswa?
 
Mleta mada umeandika maelezo marefuuu, lakini mantiki ni sifuri kabisa. Hauleweki kabisa.
Unasema Qnet in e-commerce platform, sasa ili iweje?
Ni uwendawazimu kujaribu kuilinganisha Ebay(ambayo karibu kila mtu anaijuia na anaweza kuitumia kufanya manunuzi) na Qnet (Pyramide scheme ya kutengeneza mnyororo wa kuvuna pesa za watu kwa ujanja wa maneno ya kushawishi)

Mleta mada nakushauri ufupishe maelezo yako na pia jikite kwenye mantiki.
Asante kwa ushauri. But nimejitahidi sana kufupisha ingawa bado kwako ni marefu. Kujua jambo linaanza taratibu. Kama ulikua hujui kwa qnet ni ecommerce kama ebay basi leo umejua. Na si kweli kiwa unapaswa kungunishana kama mnyororo ili kununua bidhaa. Leo nitakupa kazi moja tu uifanye sasa hivi ili uelewe zaidi.

Hiyo link otakupeleka moja kwa moja alibaba. Na utakutana na muuzaji akiuza saa ya qnet. Jaribu kufanya kama unanunua then uniambie unajikuta ukiwa kwwnye mnyororo upi uliounganishwa.
Qnet hukuwa unaijua vyema leo nimekusaidia. Uje kutoa mrejesho baada ya kuinhia kwenye hiyo link.
Screenshot_2019-11-09-23-28-23.jpeg
 
Mleta mada umeshindwa kuwa mkweli na muwazi hapa.

Sote tunajua zaidi ya 99% ya watu waliojiunga Qnet hawakuwa na lengo la kununua au kuuza bidhaa za Qnet(Maana ni ghali sana, luxurious na hazina jipya) bali wanawaza na kuota ndoto za kuwa mabilionea kwa muda mfupi na njia rahisi rahisi.

Sasa unaposema Qnet ni biashara ya mtu kumiliki duka mtandao lake, unakuwa hauna mantiki kabisa.
 
Mnajua sana kupamba kitu na kushawishi hii nguvu mnayotumia kumpata mtu mmoja ajiunge na qnet ungechukua matikiti ukapeleka pale kirumba sokoni ukatumia nusu ya hiyo nguvu tu kushawishi na uhakika ndani ya miaka miwili ungekuwa milionea ila kwa qnet utakoma miaka ata 40,, utakuwa masikini hivyo hivyo
Naona upo nje ya mada. Sielewi unazungumzia eneo lipi kwenye Uzi wangu kaka.
Samahani lakini.
 
Mleta mada umeshindwa kuwa mkweli na muwazi hapa.

Sote tunajua zaidi ya 99% ya watu waliojiunga Qnet hawakuwa na lengo la kununua au kuuza bidhaa za Qnet(Maana ni ghali sana, luxurious na hazina jipya) bali wanawaza na kuota ndoto za kuwa mabilionea kwa muda mfupi na njia rahisi rahisi.

Sasa unaposema Qnet ni biashara ya mtu kumiliki duka mtandao lake, unakuwa hauna mantiki kabisa.
Naamini hujaingia kwenye link niliyokupatia pale juu.. Punguza mwendo kidogo.. twende taratibu kaka mkubwa nia ni kueleweshana. Pia punguza kushambulia.. hoji kwa hoja.

Lete mrejesho juu ya hii link.

Nikupe na nyingine?
 
Hawa ni shenzi kabisa
Wanakutia ujinga then wanakufundisha namna ya kuwafool wengine(mainly ndugu au watu wa karibu).
Yaani hili no genge la wajinga wanaofundisha wengine ujinga na namna ya kuwapata wajinga wengi.

Nashukuru walinikosa nikawapa za uso nikawapa majibu ya shombo yamejaa puya la banana(mabaharia watanielewa hapa)
sipati picha hayo majibu ulowapa
 
Naamini hujaingia kwenye link niliyokupatia pale juu.. Punguza mwendo kidogo.. twende taratibu kaka mkubwa nia ni kueleweshana. Pia punguza kushambulia.. hoji kwa hoja.

Lete mrejesho juu ya hii link.

Nikupe na nyingine?
Niwe mkweli kabisa, sijaingia kwenye hiyo link kwa sababu maelezo yako ya kunishawishi kuifuata hiyo link hayana mantiki. Hujajibu hoja zangu.

Fupisha maelezo yako na jikite kwenye mantiki tukuelewe.

Mimi nimesema haya...
1/Qnet kimsingi ni pyramide scheme
2/Sio sahihi kimantiki kuifananisha Qnet na platform zingine za kuuza na kununua bidhaa mtandaoni kama ebay, alibaba.
3/Mantiki ya kiujumla ya watu kujiunga Qnet ni ili kuvuna mabilioni kirahisi na wala sio kufanya biashara ya bidhaa za Qnet
 
Sasa ndugu yangu huna nia ya kuifunza utakuwa. Wewe unapewa utirio ujisomee unachana si utafeli? Hahahahaha
Any way kaka yangu leo sikuwa na nia ya kugusa huko kote ubao usingetosha. Ila nakuahidi next time nitakuja na mada zinazogusa hayo maeneo.
Kwa sasa emdelea kubaki na hiyo fikra hadi huo wakati utakapo fika nitaweka mada husika kwa Uzi.
Ila pitia zile link upate kuelewa kwa nini nakwambia Qnet ni Ecommerce. Next time nitagusa qnet kwenye angle nyingine
 
Niwe mkweli kabisa, sijaingia kwenye hiyo link kwa sababu maelezo yako ya kunishawishi kuifuata hiyo link hayana mantiki. Hujajibu hoja zangu.

Fupisha maelezo yako na jikite kwenye mantiki tukuelewe.

Mimi nimesema haya...
1/Qnet kimsingi ni pyramide scheme
2/Sio sahihi kimantiki kuifananisha Qnet na platform zingine za kuuza na kununua bidhaa mtandaoni kama ebay, alibaba.
3/Mantiki ya kiujumla ya watu kujiunga Qnet ni ili kuvuna mabilioni kirahisi na wala sio kufanya biashara ya bidhaa za Qnet
Hoja yako namba moja na namba tatu hazipo kwenye mada. Nitazizungumzia ziaidi siku zijazo. Vuta subra
Hoja yako namba mbili ipo kwenye mada.. nakushauri ingia kwenye link ya alibaba ili uahuhudie ukweli wa maelezo yangu. Fanya kama unanua ile bidhaa uone.
Nakushauri uwe mpole na uwe ready kupata elimu juu ya jambo jipya kabla ya kupinga. Au pinga kwa facts na sio kwa maoni yako tu kaka yangu.
 
Hahaah
umenikumbusha rafiki Qnet
Binafsi nimehudhuria kitu kinaitwa TRAINING
zaidi ya mara moja
Huwa wana ya kwanza na ya pili n.k

Salamu yao huwa ni Moja tu
GOOD MORNING
haijalishi ni Asubuhi, Mchana, Jioni ama Usiku.

Siku ya kwanza hahaah yale masharti yao ya salamu, mnazunguka duara, mara ushuhuda kwa watangulizi
Duh
Nikajisemea kimoyo moyo
wallah Leo nimeingia Freemason
nimeingia cha kike!

Hiyo nyumba yenyewe ili uingie humo utadhani unaingia Ikulu mizengwe kibao, huwezi kuingia ingia tu
HATA SIJUI WANACHOHOFIA.

Nikaoneshwa walioacha kazi zao za maana zenye mishahara mikubwa kisa kuingia Qnet
AKILI IKAGOMA
Wana maneno mazuri
utasikia HUYU NI MTU MUHIMU SANA NINAYEJIFUNZA VITU VINGI KWAKE, MTU NINAYEMHESHIMU MNO, ALIYENIONESHA HII FURSA, n.k

Nikaonesha bidhaa mara
saa za mkononi, vifurushi vya holidays, vya Elimu
AKILI IKAGOMA.

Nikaelekezwa kuhusu B-system inavyofanya kazi
AKILI IKAGOMA.

Saa za hadi $2000 kwa mtz wa kawaida?
Eti ni wadhamini wa F1
Hahah

KIFUPI SIKURUDI TENA
WALA SIFIKIRII KURUDI QNET
Hahah AMA
KWELI UKIITWA KUWA NJOO KUNA FURSA
BASI TAMBUA KUWA HAPO
HIYO FURSA NI WEWE MWENYEWE.
Sina hakika kama umesoma vyema Uzi wangu au umeon tu neno Qnet ukaaamua utirililike na wewe.. hahha
Sijaelewa upo eneo lipi kwenye Mada yangu. But
Kwa maelezo yako kuna kitu unapaswa kujifunza zaidi kinachohusu WAJASIRIAMALI ndani ya mfumo wa QNET. Hii ni mada nyingine ambayo itasaidia kwa kiasi fulani kutibu aina ya UGONJWA ulionao. But hii itakuwa next time.
Ila nikushauri tu Soma vyema UZI wangu na dadisi zaidi taarifa yangu then njoo ukiwa kwenye mstari wa mada husika. Ama la subiri next time twende sawa kwenye hayo maeneo.
Thanks
 
Qnet ni kituo cha mauzo ya bidhaa. Kutohitaji kwako kununua bidhaa fulani kwa umasikini wako kusipelekee kukashifu bidhaa au duka la watu. Yapo magari ya 5mil USD.. (10 billions tsh). Vipi unaweza sema hizo kampuni ni scamm kisa huna pesa?
Bei ya kawaida ni ipi? Au hujui kuwa kun biatu bya milion 100 tsh duniani. W unataka bei ya elfu 30 ya Sinza mori?
Any way ipo siku nitalezea pia hii taharuki kwa mapana yake.
Unaweza kujificha kwenye kichaka cha kutoa elimu, alafu ukakuta umeharibu zaidi katika kupendezesha mada. Ukiwa na muda, naamini unao wakutosha tafakari juu ya uwezekano wako binafsi wa kumiliki hilo duka la viatu vya 100m Tshs ili utuuzie watanzania.
haya mawazo ya ajabu sijui mnapata wapi. Bahati mbaya unakutana na jamaa waliobahatika kwenda shule, mpaka unapata hasira kuona ujinga unavyokua katika taifa kila siku.
 
Back
Top Bottom