Ujenzi wa Barabara tutumie Makampuni yenye teknolojia sahihi lakini ihusishe Technology Transfer

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Watanzania kwa kiasi kikubwa inaingizwa hasara kubwa na makampuni ya China.

Kwa asilimia kubwa barabara nyingi zimejengwa na makampuni ya Kichina. Barabara hizi hazieleweki kama ujenzi wake haujakamilika au ulikwishakamilika, maana huku zinaendelea kujengwa, walikoanzia tayari zinakuwa kwenye matengenezo. Barabara hizi zinajengwa kwa viwango duni kabisa vya ubora.

Wapo watakaosema kuwa tunayatumia makampuni ya Kichina kwa sababu ni cheap, lakini kiuhalisia makampuni ya China na bidhaa za China ni aghali maradufu ya bidhaa hizo hizo zinazotoka mataifa mengine. Fikiria barabara inayojengwa na kampuni ya China kwa shilingi bilioni 300 halafu inadumu miaka 3, linganisha na zile zilizojengwa na makampuni kama ya Japan, Italy au Dernmark kwa shilingi bilioni 500 halafu inadumu kwa miaka 20 bila kuhitaji kuifumua.

Hii ya mchina ni sawa na kutumia shilingi bilioni 100 kila mwaka (bilioni 300 ÷ miaka 3), wakati hizo nyingine zilizojengwa na makampuni yenye tekinolojia bora ni sawa na shilingi bilioni 25 kwa mwaka (bilioni 500 ÷ miaka 20). Kwa mfano fikiria barabara iliyojengwa na kampuni ya Italy toka Dar mpaka Mbeya mwaka 1975, imeanza kufumuliwa miaka 10 tu iliyopita, na maeneo mengine hasa kule Mbeya bado haijafumuliwa mpaka leo, linganisha na barabara nyingi zilizojengwa na makampuni ya China miaka mitatu iliyopita ambazo kila sehemu ya nchi zinabomolewa.

NINI KIFANYIKE

Tutumie makampuni yenye utaalam bora wa ujenzi wa barabara kutoka mataifa kama Japan, Italy, Dernmark, Sweden, Germany, UK, au mataifa mengine yoyote ambayo yanaheshimu ubora wa kazi. Lakini tunapoyapa kazi makampuni hayo, kwenye package ya mkataba kuwepo na lazimisho la technology transfer. Technology transfer ifanyike kwa hiyo kampuni ya kigeni kulazimishwa kumtafuta subcontractor ambayo ni local company kutoka kwenye orodha ya makampuni ambayo Serikali imejiridhisha angalao yamefikia kiwango fulani cha tekinolojia ya ujenzi wa barabara. Makampuni hayo ndani ya mkataba huo huo, kuwepo na asilimia ndogo ya urefu wa barabara itakayojengwa na kampuni ya Kitanzania chini ya usimamizi wa kampuni ya kigeni iliyopewa contract. Kisha kampuni hiyo ipewe mradi mdogo kwa kujitegemea kupima kama imefuzu au hakuna ilichoambulia. Ikionekana haijajifunza chochote ifutwe.

UKIFUNDISHWA NA MWALIMU MBAYA, NAWE UWEZEKANO MKUBWA UTAKUWA MTAALAM MBAYA.

Mpango huu hauwezi kuhusisha makampuni ya China kwa sababu yenyewe tayari yana tekinolojia hafifu. Tukijifunza kutoka kwa walio hafifu, sisi tutakuwa hafifu zaidi.

CHINA MPAKA LEO BADO INAJIFUNZA

Wanaofuatilia maendeleo ya China inavyoendelea kupata tekinolojia mbalimbali kutoka mataifa ya Magharibi, wanafahamu jinsi China inavyohangaika kuingia kwenye tekinolojia ya nchi za Magharibi:

1) Mradi wa ujenzi treni ya mwendokasi nchini mwao ulijengwa na kampuni ya Kijerumani. Mkataba ulihusisha pamoja na technology transfer. Leo China inajenga reli na kutengeneza treni za mwendokasi, japo kuna maeneo bado inayategemea makampuni ya Ulaya. Tukitaka kuwa wajenzi wazuri, tujifunze kutoka kwa hao walimu wabobezi na siyo kutoka kwa mwalimu mwanafunzi. Miaka ya nyuma tulinunua mitambo ya kutengenezea tairi za magari, nguo, transformer, baiskeli, n.k, kutoka mataifa ya Magharibi. Mikataba ilihusisha mafunzo kwa wafanyakazi. Hakika, bidhaa zote zilizotoka kwenye viwanda hivyo zilikuwa bora maradufu kuzidi zilizotoka China au India.

How did China build high-speed rail so fast?

China initially relied on high-speed technology imported from Europe and Japan to establish its network. Global rail engineering giants such as Bombardier, Alstom and Mitsubishi were understandably keen to co-operate, given the potential size of the new market and China's ambitious plans.9 Feb 2022

2) Miaka 10 iliyopita China ilikuwa na migodi yenye tekinolojia duni kabisa iliyoifanya migodi ya China kuongoza kwa ajali, na kuifanya China isiwemo hata kwenye top 20 ya wazalishaji wa dhahabu Duniani. Wakaamua kuuza sehemu ya migodi yao kwa makampuni ya Australia, Canada na US. Sasa zaidi ya miaka 6, China inaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu Duniani. Cha ajabu sana, hawa ambao wameshindwa kuchimba madini nchini mwao, sisi tumewapa mradi mkubwa wa Liganga iron ore na Mchuchuma coal project, tukainyima kampuni ya Rio Tinto ya Uingereza, kampuni namba 1 Duniani kwa tekinolojia ya uchimbaji chuma. Sasa ni zaidi ya miaka 10, mchina hajafanya chochote cha maana, na hata tukimlazimisha aanze kuchimba haraka, kwa vyovyote mradi huu mkubwa hautakuja kuwa na tija kwa Taifa kutokana na utaalam duni wa Wachina. Kiutaalam kwenye sekta ya madini, Watanzania ni bora zaidi maradufu ya wachina. Labda Wachina wanachowazidi ni wao kuwa na pesa wanayopewa na Serikali yao.

3) Kwaajili ya kuhuisha uchumi wa China na tekinolojia, nchi ya China ameyashawishi makampuni mengi ya nchi za Magharibi kwenda kuwekeza China baada ya wao Wachina kushindwa kutengeneza bidhaa zenye ubora zinazoweza kupenya soko la nchi za Magharibi. Wachina kila siku wapo nchi za Magharibi kutafuta wawekezaji wapya, halafu sisi tunaamini kuwa uchumi wetu unaweza kuboreka kwa kuwapata wawekezaji wa Kichina. Twende tukatafute wawekezaji huko huko ambako China inawatafuta, waje kuwekeza kwetu ili wakizalisha huku, wakauzie nchini kwao. Tutengeneze tu mazingira rahisi ili waone kuwa kwa kuja kuzalishia huku watapata faida zaidi kuliko wakizalishia kwako. Na ndicho China inachokifanya.

MAENEO MENGINE YA TEKINOLOGY TRANSFER

1) Utengenezaji pikipiki. Serikali inaweza kuingia mkataba na kampuni kama Honda wanaotengeneza pikipiki bora. Kwa mfano Serikali inaweza kuingia mkataba wa kununua pikipiki zenye thamani ya shilingi bilioni 500 katika kipindi cha miaka 5 kwaajili ya watumishi wake waliopo vijijini. Halafu mkataba uhusishe utengenezaji wa vipuli vyote vya pikipiki hizo hizo nchini, vipuli vyenye ubora kama ilivyo nchini kwao. Kama tukiweza kutengeneza vipuli vyenye ubora, na baadaye tukaweza kutengeneza pikipiki, vijana wetu watapata ajira, lakini pia tutapora soko la wachina la pikipiki za ubora duni kwenye mataifa yanayotuzunguka.

2) Magari. Kama ilivyo kwa kampuni ya pikipiki tunaweza kufanya hivyo hivyo kwa kampuni ya magari ya Toyota.

3) Matrekta. Tunaweza kufanya hivyo hivyo na kampuni ya Massey au Newholland.

Tusipofanya haya, tukaendelea tu kushindana na kuulizs nani amenunua gari zuri zaidi, pikipiki nzuri zaidi, na kuorodhesha matoleo mapya yaliyotoka, hakika tutabakia duni milele.

Kumbukeni ndani ya China kuna makampuni zaidi ya milioni 1 ya nje yaliyowekeza nchini China.

How many foreign manufacturers are in China?

By the end of 2020, a total of 1,040,480 foreign companies were registered in Mainland China, the Official data was provided by the Ministry of Commerce (MOFCOM).2 Nov 2021
 
Technology transfer ifanyike kwa hiyo kampuni ya kigeni kulazimishwa kumtafuta subcontractor ambayo ni local company kutoka kwenye orodha ya makampuni ambayo Serikali imejiridhisha angalao yamefikia kiwango fulani cha tekinolojia ya ujenzi wa barabara.
Naunga mkono hoja.....wachina wakijenga barabara kubwa hujenga sehemu muhimu kama madaraja au vivuko vikubwa usiku, tena peke yao na vibarua wachache ili walinde teknolojia yao waendelee kupiga hela kutoka miradi yetu..........hili lifike mwisho Sasa.
 
Kule juu wamejaa form four failure na Wana arts , mawazo kama haya inatakiwa vipanga hasa , na hata hvyo kupora technology sio kazi rahs kama unavyofkria inahtaji umafia wa Hali ya juu ....kama watu wenyewe ndo akina mwigulu , sahau
 
Yes, wachina ni cheap sana in short run ila kwa long run ni gharama kubwa sana hawa watu kuwaendekeza.

1. Hawatrain watu wetu.
2. Hawalipi vizuri watu wetu.
3. Hawazingatii usalama kazini.
4. Watoa rushwa wazuri sana.
5. Wakitoa rushwa ni mwendo wa substd.
6. hawana social interference.
7. nk nk.
 
Hongera mkuu article yako imeshiba vizuri kama academic conference paper
 
angalao yamefikia kiwango fulani cha tekinolojia ya ujenzi wa barabara.

Wajenge za zege maana cement ya Tanzania, mchango wa hapa hapa, nondo za Tanzania ni suala la utashi tu kuwapa wakandarasi wajenge barabara ambazo hazihitaji fedha za kigeni.

Huko The Philippines 🇵🇭 , Mexico, Ecuador n.k barabara zote za kuunganisha mikoa na kanda ni za zege. Je wahandisi wetu hawawezi ?

Matumizi ya cement yatapanua viwanda na kuongeza ajira nchini, matumizi madogo ya fedha za kigeni, uchumi wa ndani utakuwa pia mzunguko wa fedha ndani ya nchi kugusa wananchi ktk mnyororo huo kwa asilimia kubwa.
 
Kule juu wamejaa form four failure na Wana arts , mawazo kama haya inatakiwa vipanga hasa , na hata hvyo kupora technology sio kazi rahs kama unavyofkria inahtaji umafia wa Hali ya juu ....kama watu wenyewe ndo akina mwigulu , sahau
Kwa hiyo Dr Mwigulu mchemba,PhD holder ni form four failure?
 
Back
Top Bottom